SIMIYU: Samwel Makeja afikishwa mahakamani kwa uhujumu uchumi. Tumpongeze RC Kafulila kwa hili

Kumbe kesi yenyewe ni ya milioni 2? rubbish nikadhani ni kesi ya maana sn, gharama za kesi ni mara 10 ya hiyo milioni 2
 
Hiki ni kipindi ukiwa mwizi wa kuku lazima unyooke..., ila wale kina Symbion et al huu ndio wakati wao....

Tunadeal na vidagaa, wale wachelewesha kupatikana kwa Crane kule Bwawa la Nyerere.., tuwape muda....
Wale wanatafuna nchi taratibu
 
Huyu jamaa Kama vile nimesoma naye tabora boys halafu alikuwa msabato muimba kwaya
 
Hiki ni kipindi ukiwa mwizi wa kuku lazima unyooke..., ila wale kina Symbion et al huu ndio wakati wao....

Tunadeal na vidagaa, wale wachelewesha kupatikana kwa Crane kule Bwawa la Nyerere.., tuwape muda....
Kwani akina Symbioni wanekuja kipindi hiki tu? mbona walikuwepo vipindi vyote?
 
KATIBU WA AMCOS WILAYANI MASWA KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imemfikisha Katibu Wa Chama Cha Msingi cha Ushirika (Amcos)cha Mbaragane katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu,Samwel Makeja katika mahakama ya wilaya hiyo kwa makosa mawili ya Uhujumu Uchumi.

Katibu huyo alisomewa leo mashitaka yake yanayomkabili mahakamani hapo ambayo ni Ubadhirifu wa fedha na kuchepusha fedha.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru Albertina Mwigilwa ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Chirstian Rugumila kuwa Mshtakiwa alitenda makosa hayo Oktoba 4 mwaka 2021 katika Wilaya ya Maswa.

Mwendesha Mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa kosa la kwanza ni kwamba mshitakiwa akiwa Katibu wa Amcos ya Mbaragane alifanya ubadhilifu Sh 2,000,000/-ambazo alipaswa kulipia ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU) katika musimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.

Amesema kosa hilo ni kinyume ya kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2019.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa katka kosa la pili mshtakiwa alichepusha fedha hizo kwa madhumuni yake binafsi kinyume na kifungu cha 29 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2019.

Mshitakiwa mara baada ya kusomewa mashitaka hayo aliyakana na hivyo kesi kupangwa tena Juni 24,mwaka huu ambapo atasomewa hoja za awali kwani upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.

pia soma USHIRIKA SIMIYU MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

Hakuna kesi hapo
 
Msimu wa wezi wa kuku kupelekwa mahakamani huku wasafirisha Twiga wakipeta na V8.
 
Hali ya Watumishi wa Umma wilayani Maswa ni mbaya sana kwani Watumishi wa kada za elimu na afya wanalazimishwa kukopeshwa fedha nakwa kupitia Saccos bubu iliyopo ndani ya Halmashauri(Inayo milikiwa na Mkurugenzi pamoja na baadhi ya Maafisa utumishi) kwa riba ya asimilia 20 kwa mwezi.

Ndani ya Halmashauri ya Maswa Dc Viongozi wa Halmashauri husika wamekuwa na Tabia ya kujichukulia sheria mkononi kama vile wao ni mahakama.Hii imepelekea watumishi kuwa waoga hata kudai haki zao za msingi,kwa kuhofia mkono wa chuma wa viongozi wa Halmashauri Maswa Dc.

Ajabu ni kwamba watumishi wa umma waliopo ndani ya Halmashauri hii hasa kada ya Elimu na Afya hawana Furaha ya kutumika ndani ya Halmashauri hii,Walimu na wahudumu wa afya wamelazimishwa kuchangia Shilingi 5,000/=kila mmoja toka kwenye mshahara wake(makato ya Moja kwa moja?ili kuchangia shughuli za mbio za Mwenge.

Je,ni kwamba Serikali haina bajeti husika kuhusu mwenge?Kwanini tuwapokonye hata hiki kidogo walichonacho hawa watu ambacho wanajipatia kwa taabu.

Waziri wa Tamisemi na Mkuu wa mkoa wa Simiyu mnapaswa kujua hili na kama mnalijua basi mlichukulie hatua haraka iwezekanavyo,huu ni unyanyasaji wa kiwango cha hali ya juu zaidi kwa watumishi hawa ambao baada ya miaka mitano tunawaomba watuchague tena tukiwachukulia kama kundi muhimu sana.

Jambo lingine mpaka sasa tangu Waajiriwa wapya wa kada za afya na elimu waripoti kazini 28/07/2022 Mapaka leo hawajaingiziwa hata shilingi kumi kwenye akaunti zao hata pesa ya kujikimu,Je bado tutarajie uzalendo na huduma bora toka kwa Watumishi hawa?

Mtu aliyepelekwa eneo kama Ikungulyankhoma anaishije ilihali hana hata pa kuanzia na ni mwezi sasa umepita.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu ameanzisha Saccos bubu ndani ya Halmashauri ambapo wanawakopesha Watumishi wapya fedha za kujikimu kwa riba ya Asilimia 20 kwa mwezi.

Je hii SIMIYU (Maswa) ni nje ya Tanzania?
 
Wacha kazi iendelee kwa kasi,
 
Kafulila anasemaje

Ova
 
Back
Top Bottom