Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Waliofariki ni Maleki Legi (16), Isaka Njile (14) na Wille Njile ambao ni watoto wa familia moja huku watoto wawili wakinusurika.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo, amefika katika eneo hilo na kujumuika na wananchi ambapo pamoja na kuwapa pole wafiwa amewaasa wazazi juu ya umuhimu wa kuzingatia malezi ya watoto hasa kipindi hiki cha mvua kubwa.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Inspector Faustine Mtitu, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wavukapo mito na madimbwi kwani kumekuwa na maji mengi ambayo yanaweza kuleta maafa.
Wananchi wa Kijiji cha Pugu wameiomba Serikali kujenga kivuka cha daraja ili kuwa suluhisho kwa wananchi wa maeneo hayo kwani mto huo umekuwa ni hatari kwa maisha ya watoto wao kutokana na wanafunzi kutumia mto huo katika kuvuka kwenda shuleni.