MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Nakumbuka KEROZENE nilipochangia Uzi wakati Chama alipouzwa nilisema hapa hapa kuwa ile ilikuwa ni Gia tu, ila muda mchache atarudi Tanzania na Kutua Yanga SC.
Kuna sababu Kuu Nne ambazo niliziona wakati nachangia huo Uzi kuwa Chama atatua Yanga SC moja ikiwa ni ukaribu wake na Ridhiwani Kikwete, Haji Manara Mwenyewe, Familia ya Rais Mstaafu Kikwete na Kutoelewana Kwake na Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Mo Dewji.
Sijui ni kwanini wana Simba SC wenzangu leo tunakubali Kudanganywa na Uongozi wetu kuwa Chama ana Vipengele vinavyomzuia Kutua Yanga SC wakati kwa Ushahidi uliopo CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez aliweka wazi juu ya hilo kwa Mchezaji Luis Jose Miquissone tu na siyo kwa Clatous Chota Chama.
Achilia mbali yote haya ila kama ukiwa Mfuasi ( Follower ) wa Mchezaji Clatous Chota Chama ( hasa Instagram ) kwa jinsi ambavyo huwa 'anakomenti' hasa kwa 'Kejeli' na 'Dharau' pindi Simba SC ilipofungwa na Yanga SC Ngao ya Hisani, ilipofungwa na Jwaneng Galaxy katika Kombe la Klabu Bingwa Afrika na ilivyotoka Sare katika Mechi zake za mwanzo katika NBC Premier League huwezi si tu Kuamini bali hata Kukubali kuwa anarejea / atarejea Simba SC yetu.
KEROZENE nauheshimu sana Uongozi wangu wa Simba SC na naipenda mno Klabu yangu ya Simba SC ila kwa hili la Chama kurejea Simba SC au ana Vipengele vya Kumzuia kutua Yanga SC nalikataa na nasema ni Uwongo wa Mchana kweupe na sijui kwanini Wametudanganya na kwamba ikitokea kweli akatua Yanga SC watatueleza nini.
Counter pekee ambayo Simba SC wanaweza Kuifanya kwa haraka ili Kujiweka salama ni wao pia kufanya 'Umafia' wa Kumsajili Kiungo Khalid Aucho ( ambaye ndiyo Roho ya Yanga SC ) kwa sasa au Kusajili Wachezaji Mahiri zaidi ya Aucho na Bangala na siyo hizi 'porojo' zao wanazotupa na bahati mbaya Mashabiki wengi wa Simba SC wanaamini / wanawaamini.
Kwa Chama kuja tena Simba SC tusahau.