Simon Msuva mchezaji bora mwezi Oktoba, awapiku Kichuya na Muzamiru kutoka Simba

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970

Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Oktoba akiifungia timu yake magoli manne na kutoa pasi 5 za mwisho na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya alama 14 katika mechi sita ilizocheza. Kwa kuchaguliwa huko, Msuva atazawadiwa Tshs milioni moja na mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya Vodacom

Msuva alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine wawili ambao ni Shiza Kichuya na Muzamiru Yasin wote kutoka klabu ya Simba.
 
ujinga mtupu, liCHURA lake limefungwa alafu yeye anapewaje mchezaji bora???
 
Reactions: PNC
uwe unasoma na kuelewa ww chura msaidizi!

timu yake imefungwa amepewaje hiyo tuzo???
Wewe ndo mbumbumbu kama lilivyo timu lenu.

Mchezaji bora anapatikana kwa vigezo vingi si timu yake kushinda tu.
 
TFF mmeanza hujuma kwa wanyama
haya ni maajabu, huyu MSUBA ameisaidia timu yake kufungwa na chama la wana na mbeya city alafu alinganishwe na mh kichuya aliyeisaidia timu yake kutokupoteza mechi hata moja, na bado ni top scorer!
 
haya ni maajabu, huyu MSUBA ameisaidia timu yake kufungwa na chama la wana na mbeya city alafu alinganishwe na mh kichuya aliyeisaidia timu yake kutokupoteza mechi hata moja, na bado ni top scorer!
Huyo Kichura imesaidia timu yake kufungwa na watoto wa mjini African Lyon!
 
haya ni maajabu, huyu MSUBA ameisaidia timu yake kufungwa na chama la wana na mbeya city alafu alinganishwe na mh kichuya aliyeisaidia timu yake kutokupoteza mechi hata moja, na bado ni top scorer!
Ukiwa na roho mbaya ni shida sana..elewa basi umeambiwa mchezaji bora kulingana na vigezo vilivyotumika na sio timu bora acha wivu wewe
 
uwe unasoma na kuelewa ww chura msaidizi!

timu yake imefungwa amepewaje hiyo tuzo???
aki ya nani tena mi nilijua hukuisoma hiyo habari...ila kama umeisoma na ukapost hayo mashudu basi kichwa chako hakipo sawa.
 
Msuva ni mchezaji bora wa wakati wote,hawa wa upepo ukipita hawapo watasubiri sana tuzo.
 
Naomba kuuliza, hivi Tanzania kuna mpira kweli na wachezaji wazuri au tunadanganyana tu? Juzi juzi hapa tulidanganywa kuwa Ngassa ni bonge la mchezaji kumbe hata danadana hajuwi ila baada ya kwenda kwa babu na kulishwa kizizi cha kufunga Simba wabongo wakampa chati ya mchezaji mzuri kumbe hana lolote mpaka katimuliwa South kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha mpira ila huku Bongo (kwa Babu) anaonekana bab kubwa. Ombi...wachezaji wa kibongo wacheni kula vizizi toka kwa babu, haviwasaidii hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…