Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva ametangazwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Oktoba akiifungia timu yake magoli manne na kutoa pasi 5 za mwisho na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya alama 14 katika mechi sita ilizocheza. Kwa kuchaguliwa huko, Msuva atazawadiwa Tshs milioni moja na mdhamini wa ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Msuva alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wachezaji wengine wawili ambao ni Shiza Kichuya na Muzamiru Yasin wote kutoka klabu ya Simba.