Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Makini, Simon Ngilisho, ameendelea na kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiahidi kuboresha miundombinu ya biashara na usafiri ndani ya jiji la Arusha.
Akizungumza leo Oktoba 22, 2025, katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Arusha, Ngilisho amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, atajenga masoko ya kisasa yatakayokidhi mahitaji ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Aidha, ameahidi kujenga stendi ya kisasa ya mabasi na magari ya mizigo yenye lengo la kuboresha huduma za usafiri na kuongeza ufanisi wa shughuli za kiuchumi ndani ya jiji hilo.