Simpendi Dada Yangu!

Simpendi Dada Yangu!

Asante kwa ushauri Ashadii. Tupo wanne na huyo dada kanizidi miaka kumi.



Katavi that explains it all... tafakari chukua hatua... she is more of a mlezi than dada...
 
Heshima Katavi,

Nakushauri mwite Dada yako mweleza haya uliyoandika hapa jamvini pengine tatizo likamalizwa na mhusika mkuu kwa njia rahisi kuliko ulivyofikiri.
 
1. inaonekana dada yako ana tabia ambazo wewe kama wewe huzipendi na hazikuvutii
2.kutokana age gape yenu kuwa kubwa unajikuta hauko huru ktk baadhi ya mambo
 
Mimi ilitokea kumchukia baba yangu mzazi kama wewe unavyomchukia dada yako! na mimi sikuwa na amani kabisa akiwepo. Lakini yalishapita sa ivi ni marafiki sana tu. Labda niseme tu wewe time will tell utajikuta unampenda dada yako
 
Ni kawaida fisrt born na last born kuto pendana

wazazi wanakuwaga very strict na first born
halafu wanawadekeza sana last born....

Sasa yaweza kuwa dada yako alikuwa hapendi hiyo na alikuwa strict na wewe
sasa wewe waweza kuwa ulichukulia kama ana chuki na wewe

halafu tofauti ya miaka ina maana ile bond hamkuweza kuijenga,bond ya kindugu
ukichukulia ni jinsia tofauti......

Ushirikina waweza ku play kama kwenye ukoo kuna imani hizo
 
Ni kawaida fisrt born na last born kuto pendana

wazazi wanakuwaga very strict na first born
halafu wanawadekeza sana last born....

Sasa yaweza kuwa dada yako alikuwa hapendi hiyo na alikuwa strict na wewe
sasa wewe waweza kuwa ulichukulia kama ana chuki na wewe

halafu tofauti ya miaka ina maana ile bond hamkuweza kuijenga,bond ya kindugu
ukichukulia ni jinsia tofauti......

Ushirikina waweza ku play kama kwenye ukoo kuna imani hizo
Mkuu Heshima Mbele,
The Boss Amezungumza mambo ya msingi sana, Labda kwa kuongezea ni kwamba wewe kama mtoto pekee wa Kiume unaona kuwa nafasi yako ya kuwa Kiongozi katika Familia imemezwa na Dada yako hivyo mara zote unajikuta kuwa Unataka kufanya mambo yako lakini unakuta kuwa yeye anataka ufanye katika namna ambayo yeye anafikiri, au unapotoa mawazo yako yeye anayakosoa, hivyo mnaingia katika mgongano wa mawazo na nafasi katika familia, Ki-msingi familia inakuwa na wazaliwa wa kwanza wawili!!! Kitu ambacho ni kigumu wewe kukikubali na hasa ukizingatia kuwa Dunia imeumbwa na kutawaliwa na Mfumo Dume.
 
kuna uwezekano mkubwa saaana kua wazazi wanakupenda wewe most (ni last born na the only boy) to the extent kua wanakudekeza kupita maelezo. Hilo suala husababisha dada yako kua mlezi mzuri kwako kuliko hata wazazi, Yawezekana yeye ndie uhakikisha uko katika mstari, kukujenga na kukuelekeza mienendo ya maisha, kukukemea ukikosea n.k - Kwa ufupi Yaani yeye ndie kachukua nafasi ya malezi bora - yoote yale ambayo mzazi anafanyia wanawe (na ndio maaana watoto wengi huchukia wazazi maana huona kama wanaonewa ama kukabwa - mpaka awe mkubwa na akili timamu ndio anajua kua ah! kumbe wazazi had best interest in me) Hivo hiyo chuki ambayo ingelenga wazazi ipo kwa dada ambae anafanya mambo dhidi yako out of LOVE.

Msome vyema AshaDii kuna point za maana sana hapo .kazi n kwako

Nakubaliana nawe mdau.
Inawezekana kabisa wazazi wanakulea kiaina ambayo dada mkubwa inabidi ashikilie ukanda ili usiharibikiwe. Kwa yeye kufanya hivyo labda ndio hapo unapoanza kumchukia na kuona anakubania, ili hali yeye ana nia njema tu. Labda ungekuwa muwazi zaidi kuwa kwa nini unamchukia?
 
<br />
<br />
Nakubaliana nawe mdau.<br />
Inawezekana kabisa wazazi wanakulea kiaina ambayo dada mkubwa inabidi ashikilie ukanda ili usiharibikiwe. Kwa yeye kufanya hivyo labda ndio hapo unapoanza kumchukia na kuona anakubania, ili hali yeye ana nia njema tu. Labda ungekuwa muwazi zaidi kuwa kwa nini unamchukia?
Ishu ya kwa nini namchukia sijui na ndio maana nauliza hii ishu ni kawaida?
 
watu wengine wanapenda kuropoka pasina sababu, mtu kaomba ushauri watu wengine wanaanza kufikia mambo mengine
 
Ishu ya kwa nini namchukia sijui na ndio maana nauliza hii ishu ni kawaida?
Maybe unamchukia sababu she has things you dont have, kama self confidence au wazazi wanamthamini zaidi yako kwa vile yeye ni mkubwa.
We mwenyewe unahisije kuhusu dada? ni mtu anajiweza kimaisha kuliko unavo jiweza wewe? au uhusuano wake na wazazi ni ule ungependa uwe nao? ao maisha yake na familia yake unaya tamani? Hivyo ni baadhi ya vitu vinaweza kukufanya ujihisi unapoteza confidence anapokua karibu.
Pia jaribu kukumbuka uhusiano wenu mlivo kua wadogo. Maybe alikua anapendelewa na wazazi au alikua anakuonea kwa vile ni mkubwa na ikaacha kovu.
 
inawezekana alikutesa ukiwa mdogo maybe,au ni mshirikina, sioni kwa nn unakuwa hivo, au hujiamini maybe
 
Katavi sijui mko wangapi katika familia... lakini ni dhahiri kitendo chakua ni last born tena Mvulana ni kitu ambacho wazazi wako walifurahia mno ulipopatikana/zaliwa maana ukute walisha kata tamaa ya kua na mtoto wa kiume... Sijajua umepishana umri gani na dadako (hio ingetoa picha kamili ya hali halisi ) Ila kitu ambacho nimekisoma mimi ni kua kuna uwezekano mkubwa saaana kua wazazi wanakupenda wewe most (ni last born na the only boy) to the extent kua wanakudekeza kupita maelezo. Hilo suala husababisha dada yako kua mlezi mzuri kwako kuliko hata wazazi, Yawezekana yeye ndie uhakikisha uko katika mstari, kukujenga na kukuelekeza mienendo ya maisha, kukukemea ukikosea n.k - Kwa ufupi Yaani yeye ndie kachukua nafasi ya malezi bora - yoote yale ambayo mzazi anafanyia wanawe (na ndio maaana watoto wengi huchukia wazazi maana huona kama wanaonewa ama kukabwa - mpaka awe mkubwa na akili timamu ndio anajua kua ah! kumbe wazazi had best interest in me) Hivo hiyo chuki ambayo ingelenga wazazi ipo kwa dada ambae anafanya mambo dhidi yako out of LOVE.

What to do Ni vizuri saaana kua umetambua kua wamchukia.... pamoja na kusema haipendezi. Hivo hio ni first stage, stage inayo fuata hapo ni wewe kujiuliza (free of emotions - yaani logicaly) ni vitu gani hasa akifanya dadako ndio huongeza chuki! Ukipata jibu hapo utajua kua je una haki ama una haki... na ni muhimu kua uliangalie hili suala vizuri saaana. Na toka maelezo yako ni dhahiri dada akutesi wala kukunyanyasa - maana lazima katika maelezo ungegusia kua anafanya hivo. Hivo Katavi, tumia busara urudi katika mstari na utafakari upya chuki yako.

N:B Nimekutana sana nawe jamvin, you are one of the most peaciful JF member ninae mfahamu.... nimeshangaa saana kukuta una hii issue hivo kunifanya nijue kua kweli hili suala liko critical kwako. BEST OF LUCK.... katika Ku resolve.

Pamoja Saaaana.

ADI

Hapa mkuu umegonga IKULU. case closed.
 
Lakin thread haijaeleza sababu za kumchukia, je jambo gani amefanya mpaka ukawa humpendi. Umedai una mfadhaiko, neno mfadhaiko ni pana sana! Nahisi kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Lakin thread haijaeleza sababu za kumchukia, je jambo gani amefanya mpaka ukawa humpendi. Umedai una mfadhaiko, neno mfadhaiko ni pana sana! Nahisi kuna kitu nyuma ya pazia.
Kuna sehemu nimesema napata mfadhaiko?
 
Pole kaka inwezekana huyo dada yako alikuwa na katabia ka kukurekebisha tabia ulipokuwa unapinda ndio maana unamuogopa sio kumchukia humchukii kaka
 
Kuna sehemu nimesema napata mfadhaiko?

kukosa amani na ile hali ya kujiamini kupotea kabisa unapomuona dada yako si umesema hivyo au?! huo ndio mfadhaiko wenyewe
 
Back
Top Bottom