Simpendi Dada Yangu!

kukosa amani na ile hali ya kujiamini kupotea kabisa unapomuona dada yako si umesema hivyo au?! huo ndio mfadhaiko wenyewe
Sawa lakini si zaidi ya unavyofikiria, nikiwa nae nakuwa na uoga fulani.

Katavi msome ashadii pamoja na hawa wengine hapa chini lazima tatizo lako katika haya waliyozungumza

Pole kaka inwezekana huyo dada yako alikuwa na katabia ka kukurekebisha tabia ulipokuwa unapinda ndio maana unamuogopa sio kumchukia humchukii kaka
Ni kweli namuogopa, nashangaa kwa nini namuogopa yeye zaidi kuliko mama au baba...

Katavi msome ashadii pamoja na hawa wengine hapa chini lazima tatizo lako katika haya waliyozungumza

Nimewasoma!

Asante kwa ushauri Ashadii. Tupo wanne na huyo dada kanizidi miaka kumi.

Unamchukia kwa sababu wewe ni mtoto wa mwisho tena wa kiume ,yaonekana wazazi wanakulea kama yai,ila dada yako ndio aliyeweza kukukemea na kukukanyahasa ulipokuwa mdogo,kwa miaka mliyopishana yeye ndie alikuwa mlezi wako mkubwa yaani kukulisha na hata kukuogesha.

Inawezekana......

Pole

Mimi nahisi lazima ulipokuwa mdogo alikuwa anakupelekesha na brain yako inaweza kuwa kwa mbali bado hiyo kitu ipo ila wewe huwezi kukumbuka vizuri.

Hii inaweza kuwa ndio imekuaffect kiaina fulani.

Mie sijui upo wapi ila ingekuwa vizuri ungeonana na wajuzi wa kukusaidia kuondokana na hii fear ulionayo wazungu huwa option yao kubwa ni hypnosis na inasaidia kukurudisha huko nyuma na utaona tatizo lipo wapi.

Pole sana anaweza kuwa alikuwa anakuonea wivu wa attention uliyokuwa unapewa na wazee au kuna maneno wazee walikuwa wanasema na wewe kama a son unakuwa na mamlaka mengi kifamilia kuliko yeye alie wa kike so kuna mengi hapo

Au ongea na wazazi wako au mmoja wao utakavyojisikia uone kama wanaweza kukusaidia.

N.B. Katika familia duniani siblings wengine wanakuwa na tabia za ajabu utazani wengine sio damu moja

Pia dada ameolewa? Ana urafiki na mtu? Anaishi bado kwa wazazi?

Kaolewa na ana mtoto mmoja...

Bro Katavi...Pole sana..

Lakini pia hongera kwa kutambua hilo na naamini michango ya wadau itasukuma moyo na akili yako kukubali mabadiliko..’Let bygone be bygone’ . Please note there is limited room in a person’s mental, emotional, and relational capacities. When you fill that capacity with hurtful stuff from your past or disappointment over things that could have been, you leave little room to explore present moments.

Vizuri ukasoma tena na tena posts zifuatavyo...

Katavi sijui mko wangapi katika familia.. et cetera......

…..Ralph Marston alisema 'WORRY is your own creation...and FEAR is nothing more than a response you have chosen'...et cetera...

Compilation ya Maty..
.. Katavi msome ashadii pamoja na hawa wengine hapa chini lazima tatizo lako katika haya waliyozungumza..et cetera

All the best!

Mengi yameshasemwa, my fifty cents:

a. Siyo jambo la ajabu kwa ndugu kuwa na hisia hasi baina yao. Katika baadhi ya famiila hizi hisia hasi huenda kiasi cha kuzaa uadui wa wazi. Uadui huo kwenye familia nyingine huenda mbali zaidi kiasi cha kudumu maisha yote na nimewahi kuona hadi watoto wa wanandugu wanachukiana kisa ni wazazi wao kutopatana na ukiwauliza sababu - tangu utoto walikuwa hawapatini! Kwa hiyo kwamba umelitambua na umesema hajakufanya kitu chochote basi ni wazi kwamba uamuzi wa kuendeleza hisia hizo au la unabakia mikononi mwako.

b. Kwamba ulipokuwa na miaka 10 dadako alikuwa na miaka 20 ni wazi kwamba kati yenu hakukuwa na ule uhusiano wa ndugu wawili wanaofuatana. Zaidi ni uhusiano wa 'dada mkubwa' na yawezekana dadako yuko karibu na mdogo wake wa tatu kuliko wanayefuatana naye. Yote haya ni katika kuonesha kilichosemwa hapo juu kwamba ili uweze kuhusiana naye vizuri mtazamo wako kuhusu wewe ni muhimu kuubadilisha - kwamba badala ya kumuona kama dadayako - umuona kama mama mdogo - utaona wanaume au vijana wa kiume wanaweza kuwa karibu zaidi na mama zao wadogo kuliko mama zao. Sijui ni kwanini. Mpe heshima yake kama hivyo na usimwogope kihivyo.

c. Kiri hisia zako za woga kwake na umwambie unavyojisikia - usimwambie kuwa humpendi. Mwambie tu kuwa sijui kwanini unamuogopa sana na umsikilize.

d. Go and do something nice for her. Not once but in more than ways. Utamuonesha kuwa sasa umekomaa na kuwa mtu mzima u can handle urself na kwamba asiwe na wasiwasi. Utamrelax.

NB: Kama una issues nyingine ambazo amekutaka mara nyingi uzishughulikie - as a big sister would do - na unapuuzia hamtafika popote hadi utengeneze kitu kicho.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…