Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Naunga mkono hoja kwa 100%. Tusisumbuane, kwanza hili neno kwangu ni kero, kila MTU achukue tahadhari ki vyake, kweli watu wazima wanataka rais asema korona ipo basi! Hilo tu? Chukua hatua.
 
Kwanza punguza jazba, halafu toa ushauri nini kifanyika kwa waafrika.
Ni kweli nakasirika eti watu wanasubiri Rais aseme ndio wachukue tahadhari.. yaani Lawama zimezidi.
Ugonjwa huu umejulikana dunia nzima, ni jukumu la kila familia kuchukua hatua.. sababu akifa mtu kwenye familia yako ni hasara kwenu sio kwa rais... suala la afya linaanza na mtu binafsi.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Utafiti wa kutokuwa na mafanikio umefanyia maabara ipi
Hivi matokeo ya huu ugonjwa unahitaji uwe na maabara?

Kwani utafiti kwamba watu wanakufa kwa corona umefanyia maabara ipi?
 

“...kinatucost roho za watu...”?

Tupe dondoo ya mikakati ya Rais wa kupigiwa mfano ambayo imeokoa roho za watu wote!
 
Hivi matokeo ya huu ugonjwa unahitaji uwe na maabara?

Kwani utafiti kwamba watu wanakufa kwa corona umefanyia maabara ipi?
Dunia ingeenda kienyeji kama unavyotaka iwe,huenda ingeshaangamia,tena kwa kukosa maarifa
 
China ilipoanzia umesikia wanalia lia na corona? Je walibweteka tu wakisubiri mungu awasaidie.
 
Hatua za awali zipi mkuu ambazo zina tija?

Na unapogusia fungu kutengwa, hili fungu litafanya kazi ipi yenye kufifisha ama kuondoa korona?

Kwa mawazo yangu itakuwa ni kupoteza muda na fedha.
KUTANGAZA KORONA IPO KUNASAIDIA KUONGEZA TAHADHARI SEHEMU ZA MIKUSANYIKO, MAHOSPITALI SASA HIVI HATA ISOLATION HAKUNA WAGONJWA WANALAZWA WARD MCHANGANYIKO NA WENGINE, HUONI KAMA HILI NI TATIZO? TUSISUBIRI IFIKE HATUA HALI IMEKUWA MBAYA.

HII ITAKUWA BALAA ZAIDI YA ILIVYO SASA.
 
WAGONJWA WANALAZWA WARD MCHANGANYIKO NA WENGINE,
Hakuna tatizo. Mbona wagonjwa wa malaria wanachanganyikana na wa ukimwi, wa TB na kaswende,wa kifaduro na wa ajali. Kwann korona? Vifo vya korona vina kelele isiyokuwa na maana
 
Leo alipokua anazindua miti amesema corona haikuwepo tz karbia mwaka mzima ulopita ila umeletwa tena kwa sasa na waliosafiri kwenda kufata chanjo sasa sijui kina nani. But Mm nipo na JPM kwenye hili. Tutamuomba Mungu tutafanya mazoezi ya kutembea juani mpk kieleweke
 
Unajua tatizo linapoanzia ni kwamba huku nje ya Serikali tupo watu wengi sana wanye hekima, maarifa na busara zaidi kuliko viongozi wote wa Serikali yetu. Sisi tuliopo nje ya Serikali inaonekana tunajua zaidi kuliko viongozi wetu, hilo ndiyo tatizo
 
Covid 19 ilishindwa kuwaangamiza waafrika kama ilivyotarajiwa na baadhi ya wenye agenda za siri. Sasa bara la Africa limekumbwa na aina nyingine ya Covid 501-2v ambayo imetengenezwa na kuongezwa makali ili waafrika tupungue duniani.
Tanzania imevamiwa na strain mpya ya Covid 501-2v ambayo inauwa watu wengi nchini Zimbabwe na South Africa.
 
For my first time leo nimeona Sexless umeongea kitu chenye mashiko na si siasa. Wanasiasa wa Tanzania wangefikiri kama ulivyofikiri leo basi tungekuwa mbali lakini kinyume chake chake ni kuwa wao wanafikiri kwa ajili ya interest zao. Sio kila kitu kinachofanywa na serikali ni cha kupinga na si kila ushauri wa upinzani ni wa kupinga. Baya lisemwe na zuri lipongezwe. Kwenye ishu ya covid Magu yuko sahihi. Tujiulize jizo nchi walizojifungia wamefikia wapi na sisi tuliomwachia Mungu tumefikia wapi
 
Nina mhudumu wa afya ninayefahamiana naye yupo Uswisi, huwa ananipa taarifa kwamba kazi sometimes zinamuelemea kutokana na kufurika kwa wagonjwa wa covid ICU.
 
Nina mhudumu wa afya ninayefahamiana naye yupo Uswisi, huwa ananipa taarifa kwamba kazi sometimes zinamuelemea kutokana na kufurika kwa wagonjwa wa covid ICU.
Unataka kusema nn mkuu? Hebu funguka kidogo.
 
Unataka kusema nn mkuu? Hebu funguka kidogo.
nilikuwa nakazia kwa Mkazamoyo kwamba hata huko ambako tunaamini hizo taratibu za kuzingatia kuhusu corona hali si hali, mambo bado moto, so ni vema tu kujichaguliwa namna ya kupambana na korona maisha yaendeleee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…