Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Acha ukichaa

Kama unasapotiwa yanini uanze kutishia wananchi wasi discuss anything kuhusu corona?..
Hapo ndio upumbavu wenu ulipo mkuu!

Hataki kwa sababu wengi wenu ni wajinga mnataka kutengeneza taharuki ili watu wawe na hofu washindwe kujifanyia shughuli zao za kuwaingizia kipato, na yuko sahihi hata mimi naunga mkono ukipatikana hata risasi upigwe tu.

Hao wajinga wachache wanaopiga kelele mitandaoni ni kakikundi ka watu wachache tu wanaofanya hivyo kwa maslahi yao.

Naona sasa hivi mmeacha hata kuingelea kesi zenu mlizopeleka ICC sasa mmejikita kuamisha dunia kwamba kuna maelfu hapa tz wanakufa kwa corona. Na mtafeli tu kama mlivyofeli tangu corona inaanza.
 
Korona haina tiba wala haina kinga. Njia zote zinazoshauriwa ili kujikinga na korona ni za dhahania na nadharia tu. Ndiyo maana hakuna mahala popote walipofanikiwa kuiondoa na kuimaliza korona. Hizo chanjo zimekaa kisiasa na kibiashara tu. Mafua yana karne nzima mpaka leo hakuna kinga, ukimwi una nusu karne mpaka leo hakuna chanjo, halafu leo miezi 9 tunaambiwa Kuna chanjo ya korona! Rubbish!...
Kina mbowe ni wakala wa mabeberu wasaka fulsa ya biashara au wizi kwenye mazingira yoyote. Popote duniani ukiacha uchina dili za kulisha watu kwenye karantini ni uhuni tu wanapeleka hapa na hapa halafu invoice wanajidai wamelisha kila mtu serikali inalipa ni wizi mtupu. Yaani ukisikia ushetani ni huu. Watu wateseke ili wao waibe hela za umma.

Hapo ni mfano mdogo tu. Kimataifa ni biashara za kinyang'anyi tu. Hii homa ya mafua tutaenda nayo tu na tutatoka sio mafedhuli duniani kuona ni fulsa ya kuzikamua nchi changa kufisha matumaini yao ya maendeleo.
 
Kama hakuna Corona tunavaa Barakoa za nini? Kwanini hataki mamlaka zitangaze tu kuwa Corona ipo ili watu wachukue tahadhari?
Mkuu!kusoma mtu hujui ina maana hata picha inayochorwa huioni?
Kuna mambo lazima tujiongeze mzee mm ccm siukaligi lkn kwenye hii issue ya corona jpm ame play vizuri
Kila siku watu wanambiwa mvae barakoa mnawe mikono,muepuke misongamano isiyo kuwa ya lazima ....mnataka nn tena
Au mnataka mpigwe lockdown na mkipigwa lockdwn msitegeme kma serikali itawaletea mahitaji

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Korona haina tiba wala haina kinga. Njia zote zinazoshauriwa ili kujikinga na korona ni za dhahania na nadharia tu. Ndiyo maana hakuna mahala popote walipofanikiwa kuiondoa na kuimaliza korona. Hizo chanjo zimekaa kisiasa na kibiashara tu. Mafua yana karne nzima mpaka leo hakuna kinga, ukimwi una nusu karne mpaka leo hakuna chanjo, halafu leo miezi 9 tunaambiwa Kuna chanjo ya korona! Rubbish!!

Njia na mbinu zinazopendekezwa kuchukuliwa kuepuka korona hazitekelezeki na zinaongeza tatizo. Tumeona maandamano na mabishano hata katika mataifa makubwa kama Marekani, Brazil, Ujerumani na kwingineko wananchi wanapinga makatazo na masharti mbalimbali ya kujikinga na korona yanayowekwa na viongozi wao.

Sasa watanzania wenzangu mnaoshinikiza na kumtaka JPM atoe tamko kuhusu korona naombeni mnijibu. Mnatakaje? Alishasema tumuachie Mungu. Sasa kelele za nini?

Hivi mnataka JPM atangaze kitu gani kifanyike hapa nchini ili kuizuia korona zaidi ya kumwachia Mungu?

Awafungie watanzania ndani? Hawa hawa watanzania wanaokula kwa kufanya umachinga na uchuuzi? Hawa hawa wanaolima na kuvuna ndipo wapate mlo? Hawa hawa wanaochunga mifugo yao kwa kuzunguka nayo maporini? Ulaya kuna zero grazing. Hapa Tanzania na nchi zote za Afrika tutauwa watu na mifugo kwa njaa.

Na ndiyo maana South Africa hali ilikuwa tete, na pale Kenya ulifanyika usanii tu wa kuzuia watu kutoka usiku, halafu mchana kutwa wako majiani. Usanii mtupu. Uganda wamejikanyaga wakashindwa. Usiitolee mfano Rwanda. Kale kanchi ni kadogo sawa na kisiwa cha Unguja ndiyo maana wanagawana gunia kumi za unga kwa siku na zinawatosha.

Halafu hii kunawa nawa, nayo pia ni ujinga tu. Unanawa halafu unaingia kwenye daladala kubanana? Mnashea kikombe cha maji ya kunywa nyumba nzima? Mnashea kete za bao, kopo la mbege, komoni na wanzuki? Acheni zenu bhana! BTW, kirusi kinauawa kwa kunawa? Sanitizer inauwa kirusi? Unazijua tabia za kirusi?

Virus is immortal. Why? This is because Virus is the RNA/DNA particle. Na ndiyo maana mpaka leo ukitaka DNA/RNA ya dinosaurs walioishi miaka milioni150 iliyopita utapata.

Mnataka atangaze watanzania wavae barakoa? Hawa hawa wanaokosa hata leso ya kufutia kamasi? Hawa hawa wanao omba mia tano ya kununua kipande cha muhogo?? Hapa tutasababisha mlipuko wa magonjwa mengine. Maana watu wanaweza kuvaa kitambaa mwezi mzima bila kukifua.

Tumuunge mkono JPM (simtaji kama mheshimiwa Rais kwa kuwa ushindi wake katika uchaguzi wa 2020 mpaka siku nakufa sitaukubali), lakini kwenye suala la korona namuunga mkono 100%.

Tuweke pembeni chuki na tofauti zetu zote za kila aina tuangalie uhalisia. Msimamo wa JPM katika suala la korona unaendana na uhalisia na ndiyo njia bora ya kuifuata. Hayo mataifa yanayojitia kuwafungia na kupiga sanitizer watu wake wamefanikiwa kiasi gani kujikinga na korona?

Halafu hivyo vifo Cha mmoja mmoja vinavyotokea mbona ni kidogo sana kuliko vile vya magonjwa kama malaria, TB, ajali, ukimwi, n.k?? Kwann hivi havihesabiwi??

Wewe mwenye unafuu wa maisha kaa ndani tuache walala hoi tuendelee kuzurura na kupengeana makamasi ili miili yetu ijenge kinga asili dhidi ya korona. (Kajisomee types of immunity, kuna natural na artificial).

Nimemaliza.
Lockdown ingeleta mazara makubwa sana, hilo hata mimi namuunga mkono, Wasaidizi wake waendelee kuhamasisha watu kuchukua zile tahazari, Kunawa mikono, kuepuka misongamano isyo na łazima, watu watumie dawa za kienyeji na nyungu pia.
 
Nchi hii ina watu wanaodeka kupita maelezo, yaani Rais atangaze korona ipo ndio uchukue hatua? Kila nikisoma comments za watu huwa napata ukakasi sana.

Ugonjwa huu utaendelea kuwepo hata lockdown ya mwaka ikiwepo!! Hakuna maisha bila kukutana kati ya binadamu na binadamu... Hizo za lockdown sijui carfew ni upumbavu mtupu...

Shida ipo kwa waafrika kufikiria walichosema Wazungu

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Yani kweli watanzania ndio tumefika hukukweli kuilinda afya yako mpaka ikwambie serikali afya nimaliyako ilinde mwenyewe au ndio unasubili uambiwe shusha nety usiku umeingia
 
Waeleze watu ukweli ili kila mtu achukue tahadhari na sio kutangaza kuwa hakuna Corona.
Watu wenyewe wa kuchukua tahadhari ndio hawa mkuu?
download.jpg
 
Kukiri Corona ipo ndio njia ya kwanza kukabiliana nayo, siku zote huwezi pigana na adui usiemjua.

Rais lazima atoe kauli ili kila mmoja wetu ajue Corona ipo na achukue hatua za kujilinda kwa umakini.

Kauli ya Rais sio sawa na kauli yangu au yako, hiyo itachujuliwa kwa uzito unaostahili na wengi wataanza kuwa serious na huu ugonjwa.

Lakini Rais kuendelea kukaa kimya au kusema Tanzania hakuna Corona ndio kunapelekea watu kudharau kuchukua hatua za kujilinda.

Huko vijijini wengi hawana access ya internet kujua hali halisi tofauti na sisi tuliopo mijini, wao wakisikia Magifuli kasema hakuna Corona wanaamini hivyo, wanaendelea kuchapa kazi.

Hili halihusiani na lockdown au vyovyote, muhimu watu wajue Corona ipo seriously na wajilinde badala ya kuamini haipo wakati wengine wanaugua na hata kufa.
Nduguyangu kilamtu ajilinde mwenyewe na watuwake wakalibu lakini ukisubili serikali ikwambiye utasubilisana kwa utalahuu huyo unaemsubili akwambie amekimbia bila yakumwambia mtu
 
Kina mbowe ni wakala wa mabeberu
Siyo kusudio la mada hii kuwatukana viongozi mahili wa kisiasa kama kamanda Freeman Mbowe.

Tujenge hoja tu za kutafuta suluhisho la tatizo la korona.
 
Hii ni sawa na baba aliyeketi barazani jioni na familia yake kisha wote wakamuona nyoka akiingia ndani lakini kwa mshangao baba kwakuwaondolea hofu familia yake, kawaambia yule nyoka kazunguka nyumba na kutokomea zake. Watoto na mama yao wameingia ndani kwa hofu kubwa. Kwa hali isiyo ya kawaida baba yule kawaaga na kuwaambia anakwenda kutembelea mifugo yake hivyo hatakuwepo pale usiku ule. Kijijini hakuna umeme na baba kaondoka na tochi.

Hapo familia itaacha kumlaumu baba??
Je ni sahihi baba kuidanganya familia yake??
Hahahahahahahhaaha Asante nimeipenda hii
 
Lazima sasa tubadili mfumo wa maisha
Mambo ya kukaa kwenye makundi etc tuache
Mpaka gonjwa lenyewe litokomee lenyewe

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Mkuu kukaa kwenye vikundi ndiyo kunakotupatia riziki wengine. Watu tuna vibanda umiza, ni ma-MC, ni madalali wa samaki ferry DSM na mwaloni Mwanza, Sasa tutaishije?
 
Mkuu kukaa kwenye vikundi ndiyo kunakotupatia riziki wengine. Watu tuna vibanda umiza, ni ma-MC, ni madalali wa samaki ferry DSM na mwaloni Mwanza, Sasa tutaishije?
Watu wakae kwa style [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tutajifunza tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom