Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Aweza kuwa usajili mpya wa covid19
 
Corona aina miujz
 
Wewe mwenye unafuu wa maisha kaa ndani tuache walala hoi tuendelee kuzurura na kupengeana makamasi ili miili yetu ijenge kinga asili dhidi ya korona. (Kajisomee types of immunity, kuna natural na artificial).

Thank you Sexless
 
swali lako la kizembe, google mkakati wa Norway kupambana na Covid

Kuwa mpole; aliyefanya uzembe ni wewe uliyetuletea habari za kijiweni. Ungekuwa umefanya utafiti usingetoa mfano wa Norway ambayo imepoteza roho karibu 600!
 
Kuwa mpole; aliyefanya uzembe ni wewe uliyetuletea habari za kijiweni. Ungekuwa umefanya utafiti usingetoa mfano wa Norway ambayo imepoteza roho karibu 600!
wacha wee, 560 wengi kweli, hasa kwa nchi iliyopo bara la ulaya ambako kuna baridi sana na hata mafua yanaua watu. Haijalishi kwamba wenye maambukizi walikua karibu elfu sabini (70000) na waliopona ni karibuni elfu sitini (60000). Ukiachia kwamba wazee 23 waliopewa chanjo ya mmarekani na wakaongeza idadi kufikia hiyo 564. Mkakati wa Norway ni failure kabisa, unavuta bangi?
 

Inaonekana ulidandia train kwa mbele!
 
Lazima sasa tubadili mfumo wa maisha
Mambo ya kukaa kwenye makundi etc tuache
Mpaka gonjwa lenyewe litokomee lenyewe

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kukaa kwenye makundi ni muhimu Mkuu. Kinga ya mwili inakuwa developed kupitia kukutana na si kujificha. Mwenye kunielewa anajua namaanisha nini.
 
wenye tiketi hua hawadandii, wewe si ndo ulieanza kunijbu? shule za kata bado hazisaidii aisee

Unasema do-nothing strategy ya Magufuli inatucost roho halafu unaambiwa utoe mfano wa mikakati ambayo haicost roho unasema Norway, hapo unakuwa umeelewa swali au mradi umetoa jibu? Hiki ndicho ulichojifunza kwenye prestigious schools zako? Mbaya zaidi Norway yenyewe imepoteza mamia ya roho!
 
Sexless unamatatizo ya akili, siku nyingine umpondee, tabu tupu vijana, kuleni ndizi nyingi kutunza kumbukumbu
 
Kuwa mpole; aliyefanya uzembe ni wewe uliyetuletea habari za kijiweni. Ungekuwa umefanya utafiti usingetoa mfano wa Norway ambayo imepoteza roho karibu 600!
Mkuu wewe ni great thinker ila nikisoma huu Uzi I'm seriously doubting that, kwamba Tanzania haikuwahi poteza maisha kisa COVID 19?

Hao tuliowakejeli mbona Leo hii wanadunda tu no mask anymore na maambukizi yameisha. Tuliyemsifia weee ndio corona imemsomba pamoja na Nkuruzinza wake!!

Medics isichanganywe na siasa and conspiracy theories.
 
Wewe umevaa mask?
 
Wewe umevaa mask?
Huyo jamaa kasema Tz hakuna aliyekufa kwa corona ila Norway walikufa 600 plus. Ndio najiuliza Tz hakuna mtu aliyekufa kwa covid 19? Like serious?

Hii nchi JPM aliharibu sana. Yaani Dunia nzima wafe ila Tanzania tu? Kwamba we are special? Mbona Ukimwi na Malaria vipo au Mungu anachagua ugonjwa wa kuponya siku hizi?
 
Uko sahihi Mkuu, nimekuelewa vema kwenye hoja hii,

Lakini, njia alizotumia huyu usiyempenda zilikuwa sawia kabisa kulingana na mazingira pia maisha ya wengi walala hoi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…