Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wana JF,
Kumekuwa na ushauri mbalimbali unaotolewa kwamba watu waweke fedha zao benki. Ukweli ni kwamba kwa hali ilivyo Tanzania, nisingemshauri mtu yoyote kuweka fedha zake benki kwa sasa. Kuweka fedha benki kwa sasa ni kukubali kupata hasara juu ya fedha yako kwa mambo mawili ya msingi; kuporomoka kwa kila siku kwa shilingi ya Tanzania, na pia gharama za kupita kiasi zinazotozwa na benki.
Hali ilikuwa tofauti wakati wa enzi za Nyerere ambapo Benki ya Taifa ya Biashara ilikuwa inatoa riba ya juu kwa wateja wake, bila kuwatoza gharama zozote kwa kuweka fedha zao benki. Wakati huo, hakukuwa na gharama za kila mwezi au zakila wakati unapochukua au kuweka fedha benki. Na pia thamani ya shilingi ilikuwa haiporomoki kila siku kama siku hizi.
Siku hizi ukiweka fedha benki kwanza inabidi ulipie gharama za benki za kila mwezi,hata kama huchafanya chochote benki, na pia kila unapochukua au kuweka fedha unatozwa bank charges. Cha ajabu ni kwamba benki hizo zinatumie fedha zako kuwakopesha watu na makampuni na kuwatoza riba kubwa! Ukikopa wanakutoza riba hadi 20%, wakati wewe ukiweka fedha benki wanakupa riba kiduchu ya2%.
Napia kwa hali ya mfumuko wa bei Tanzania, kila siku hela yako iliyo benki inapoteza thamani. Kama uliweka Tshs 1M mwaka jana tarehe kama ya leo, thamaniyake leo hii itakuwa kama Tshs 700,000/-, ukitoa gharama za benki na mfumuko wa bei. Kwa hiyo kwa kila Tshs 1m unayoiweka benki kwa mwaka, unapoteza kama Tshs300,000.
Hata hivyo sikushauri utunze fedha zako nyumbani, hakuna usalama. Ni vema sana ikiwa badala ya kuweka fedha benki ukaziingiza kwenye vitu vyenye risk ya chini kama kununua dhahabu, Tanzanite na kuhifadhi vitu hivi sehemu zenye usalama. Unaweza pia kujenga au kununua nyumba, kiwanja au shamba, vitu ambavyo ni rahisi kuviuza baadaye vikiwa vimeongezeka sana thamani.