Simshauri mtu yeyote kuweka fedha benki kwa Tanzania ya sasa, ni hasara sana!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wana JF,

Kumekuwa na ushauri mbalimbali unaotolewa kwamba watu waweke fedha zao benki. Ukweli ni kwamba kwa hali ilivyo Tanzania, nisingemshauri mtu yoyote kuweka fedha zake benki kwa sasa. Kuweka fedha benki kwa sasa ni kukubali kupata hasara juu ya fedha yako kwa mambo mawili ya msingi; kuporomoka kwa kila siku kwa shilingi ya Tanzania, na pia gharama za kupita kiasi zinazotozwa na benki.

Hali ilikuwa tofauti wakati wa enzi za Nyerere ambapo Benki ya Taifa ya Biashara ilikuwa inatoa riba ya juu kwa wateja wake, bila kuwatoza gharama zozote kwa kuweka fedha zao benki. Wakati huo, hakukuwa na gharama za kila mwezi au zakila wakati unapochukua au kuweka fedha benki. Na pia thamani ya shilingi ilikuwa haiporomoki kila siku kama siku hizi.

Siku hizi ukiweka fedha benki kwanza inabidi ulipie gharama za benki za kila mwezi,hata kama huchafanya chochote benki, na pia kila unapochukua au kuweka fedha unatozwa bank charges. Cha ajabu ni kwamba benki hizo zinatumie fedha zako kuwakopesha watu na makampuni na kuwatoza riba kubwa! Ukikopa wanakutoza riba hadi 20%, wakati wewe ukiweka fedha benki wanakupa riba kiduchu ya2%.

Napia kwa hali ya mfumuko wa bei Tanzania, kila siku hela yako iliyo benki inapoteza thamani. Kama uliweka Tshs 1M mwaka jana tarehe kama ya leo, thamaniyake leo hii itakuwa kama Tshs 700,000/-, ukitoa gharama za benki na mfumuko wa bei. Kwa hiyo kwa kila Tshs 1m unayoiweka benki kwa mwaka, unapoteza kama Tshs300,000.

Hata hivyo sikushauri utunze fedha zako nyumbani, hakuna usalama. Ni vema sana ikiwa badala ya kuweka fedha benki ukaziingiza kwenye vitu vyenye risk ya chini kama kununua dhahabu, Tanzanite na kuhifadhi vitu hivi sehemu zenye usalama. Unaweza pia kujenga au kununua nyumba, kiwanja au shamba, vitu ambavyo ni rahisi kuviuza baadaye vikiwa vimeongezeka sana thamani.
 
Samahani wana JF. Nimeweka post hapo juu lakini nikashindwa kubadilisha font size, nadhani kuna tatizo.
 
Huu ni ukweli mtupu, nami siku hizi ndo natumia formula hiyo. Ukiona nina salio kubwa Benki basi jua nadunduliza ili ninunue kitu cha maana au nifanye investment. Hata kama makato ni sh 1,000/= kwa mwezi na kutoa pesa ni sh 1,000/= pia hapa tu inatosha kukufilisi laki mbili (200,000/=) kwa mwaka bila wao kukuongezea chochote
 
Unaongelea Fixed Deposit au Current Account mdau?
Mbona naona faida ipo tena kubwa tu au unaongelea aina fulani ya bank? Hebu niweke wazi.
 
vipi kuhusu kuwekeza katika soko la hisa??kwa kampuni kama google,facebook ,apple etc?
 
Hili swala ni kweli tupu, hela yetu ya tz inaporomoka sana thaman.... Ukiweka kwny saving akaunt ni kuzidi kupoteza
 
Wana JF,

Kumekuwa na ushauri mbalimbali unaotolewa kwamba watu waweke fedha zao benki. Ukweli ni kwamba kwa hali ilivyo Tanzania, nisingemshauri mtu yoyote kuweka fedha zake benki kwa sasa. Kuweka fedha benki kwa sasa ni kukubali kupata hasara juu ya fedha yako kwa mambo mawili ya msingi; kuporomoka kwa kila siku kwa shilingi ya Tanzania, na pia gharama za kupita kiasi zinazotozwa na benki.

Hali ilikuwa tofauti wakati wa enzi za Nyerere ambapo Benki ya Taifa ya Biashara ilikuwa inatoa riba ya juu kwa wateja wake, bila kuwatoza gharama zozote kwa kuweka fedha zao benki. Wakati huo, hakukuwa na gharama za kila mwezi au zakila wakati unapochukua au kuweka fedha benki. Na pia thamani ya shilingi ilikuwa haiporomoki kila siku kama siku hizi.

Siku hizi ukiweka fedha benki kwanza inabidi ulipie gharama za benki za kila mwezi,hata kama huchafanya chochote benki, na pia kila unapochukua au kuweka fedha unatozwa bank charges. Cha ajabu ni kwamba benki hizo zinatumie fedha zako kuwakopesha watu na makampuni na kuwatoza riba kubwa! Ukikopa wanakutoza riba hadi 20%, wakati wewe ukiweka fedha benki wanakupa riba kiduchu ya2%.

Napia kwa hali ya mfumuko wa bei Tanzania, kila siku hela yako iliyo benki inapoteza thamani. Kama uliweka Tshs 1M mwaka jana tarehe kama ya leo, thamaniyake leo hii itakuwa kama Tshs 700,000/-, ukitoa gharama za benki na mfumuko wa bei. Kwa hiyo kwa kila Tshs 1m unayoiweka benki kwa mwaka, unapoteza kama Tshs300,000.

Hata hivyo sikushauri utunze fedha zako nyumbani, hakuna usalama. Ni vema sana ikiwa badala ya kuweka fedha benki ukaziingiza kwenye vitu vyenye risk ya chini kama kununua dhahabu, Tanzanite na kuhifadhi vitu hivi sehemu zenye usalama. Unaweza pia kujenga au kununua nyumba, kiwanja au shamba, vitu ambavyo ni rahisi kuviuza baadaye vikiwa vimeongezeka sana thamani.

Nimekusaidia kurekebisha font na size isomeke.
 
Unaongelea Fixed Deposit au Current Account mdau?
Mbona naona faida ipo tena kubwa tu au unaongelea aina fulani ya bank? Hebu niweke wazi.

Iwe fixed deposit au savings au current account zote hasara tupu. Ili fixed deposit iwe na faida lazima interest wanayokupa iwe zaidi ya inflation rate. Lakini mara nyingi benki wanachofanya ni kukupa interest just below inflation rate kwa fixed deposit, halafu wanakuambia umefaidika, kumbe hakuna lolote ulilopata.
 
hujui? benki siku zote haimjali anayesave manake hana faida kwao, benki inamjali mkopaji! Nashangaaga mtu ana 20~50M ziko benki zimekaa tu mpaka mwaka unakatika!
 
vipi kuhusu kuwekeza katika soko la hisa??kwa kampuni kama google,facebook ,apple etc?

Mkuu soko la hisa la kweli unaweza kupata sana au kukosa sana! Ila unapata sana ikiwa mtaji wako ni mkubwa sana, kitu mbcho knawezafanya uose sna! Kwa Tanzania hapa sahau kuwa tajiri kupitia soko la hisa, halipo ni maigizo tu ya soko la hisa. Utamu wa ngoma ya la soko la hisa ni kwamba thamani ya hisa za kampuni iwe inabadilka kutokana na current affairs. Mfano, leo ukisikia Tanzania Oxygen (TOL) wamechemsha kitu utegemee bei ya hisa za TOL kushuka, na kama wakifanya kitu kizuri bei ya hisa ipande. Lakini Tanania hii unaweza kulipua makao makuu ya TOL wala bei ya hasa zao isibadike! Sasa kweli hilo soko la hisa au danganya mtoto alale!
 
Umezidisha sana chumvi, ili millioni moja iwe sawa na 700,000 ndani ya mwaka mmoja inflation inabidi iwe kama 30% kitu ambachoi sio kweli kwa TZ inflation ni kama 7% pia savings account inakupa 7-10% percent kutegemea na benki na kiasi unachoweka hivyo kuweka benki unakuwa kama umetoa droo na inflation au umepata fida kidogo.

Kuweka benki hela ni kwa ajili ya usalama wa hela yako, usitegemee kupata faida ya ajabu lakini pia sio rahisi kupoteza hela yako kama kwenye biashara au hisa.

Risks Vs Rewards.
 
Unaongelea Fixed Deposit au Current Account mdau?
Mbona naona faida ipo tena kubwa tu au unaongelea aina fulani ya bank? Hebu niweke wazi.

Hebu tuoneshe hiyo faida kupitia hizo account.
Halafu linganisha na riba ya 20% wanayokutoza ukienda kukopa kwao.
 
Umezidisha sana chumvi, ili millioni moja iwe sawa na 700,000 ndani ya mwaka mmoja inflation inabidi iwe kama 30% kitu ambachoi sio kweli kwa TZ inflation ni kama 7% pia savings account inakupa 7-10% percent kutegemea na benki na kiasi unachoweka hivyo kuweka benki unakuwa kama umetoa droo na inflation au umepata fida kidogo.

Kuweka benki hela ni kwa ajili ya usalama wa hela yako, usitegemee kupata faida ya ajabu lakini pia sio rahisi kupoteza hela yako kama kwenye biashara au hisa.

Risks Vs Rewards.

Lakini kiuhalisia benki ilitakiwa isikukate hela yeyote unapoweka hela yako kwenye current account.
Kwasababu unawapa mtaji wa kufanyia biashara.
 
Kuweka hela nyumbani nako ni challenge kubwa hasa kwa hawa wajomba wenye pikipiki aina ya Boxer, afadhali wanasiasa wenzetu wanaenda kuweka pesa za Swiss tena wanapoenda kuzihifadhi gharamq zote za safari zinalipwa na serikali
 
Back
Top Bottom