Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #21
Umezidisha sana chumvi, ili millioni moja iwe sawa na 700,000 ndani ya mwaka mmoja inflation inabidi iwe kama 30% kitu ambachoi sio kweli kwa TZ inflation ni kama 7% pia savings account inakupa 7-10% percent kutegemea na benki na kiasi unachoweka hivyo kuweka benki unakuwa kama umetoa droo na inflation au umepata fida kidogo.
Kuweka benki hela ni kwa ajili ya usalama wa hela yako, usitegemee kupata faida ya ajabu lakini pia sio rahisi kupoteza hela yako kama kwenye biashara au hisa.
Risks Vs Rewards.
Mkuu, unadhani natia chumvi? Fanya hesabu kidogo. Nenda mbali zaidi ya inflation. Fikiria mwaka jana ulikuwa na Tshs 1,000, 000 ukataka kuzibadili kuwa dola uende shopping Marekani. Ukaamua ngoja uziweke benki ili ziongezeke ukafanye shopping ya nguvu zaidi mwakani.
Sasa kama ungebadili Tshs 1000 000/= kuwa dola mwaka jana ungepata USD 625 kwa exchage rate ya 1USD = Tshs 1600.
Lakini uliamua kuweka benki hela yako upate interest ya 10% unayoisema. Gharama utakazokuwa unatozwa na benk kila mwezi, ni wastani wa shs 15,000, ambayo kwa mwaka ni Tshs180,000. Sasa pia kuna inflation ya7% ni Tshs 70,000 kwa mwaka unapoteza.
Baada ya mwaka benki wanakupa interest yako ya 10% sawa na Tshs 100,000/=
Sasa unachukua hela yako yote toka benki, 1,000,000 + 100,000 - 180,000 = 920,000/=, pungufu kwa Ths 80,000 toka hela yako uliyoweka benki.
Na kama utaitumia hapa Tanzania, kimsingi hii Tshs 920,000 unayopewa sasa ni Tshs 855,600/= ukiweka inflaton ya 7%sawa na Tsh 70,000.
Sasa kwa kuwa lengo lako lilikuwa kwenda shopping Marekani, utaenda Bureau kubadili hii shs 920,000 kwa exchange rate ya leo 1SD:Tshs 210,000/= na utapata dola $438.
Tofauti ya dola kama ungebadili hela yako mwaka jana bila kuweka benki ni $623 - $438 = $ 186
Hiyo ni hasara ya $186 ni sawa na Tshs 392,500.
Kwa hiyo kwa kuweka hela yako benki upate interest rate ya 10% unapata hasara ya Tsh392,5000/
Je unaona sasa kwamba hasara unayopata kwa kuweka hela yako benki Tsh 1M kwa mwaka ni kubwa kuliko ile niliyokadiria ya Tshs 300,000?