Simu ilipokelewa lakini hakusema chochote baadaye nilisikia miguno ya watu wakifanya mapenzi

Simu ilipokelewa lakini hakusema chochote baadaye nilisikia miguno ya watu wakifanya mapenzi

Tajiri wa matajiri

Senior Member
Joined
Apr 17, 2024
Posts
166
Reaction score
649
MY STORY; Simu ilipokelewa lakini hakusema chochote, badala yake nilisikia miguno ya watu wakifanya mapenzi.

Siku tatu baada ya ndoa mke wangu kuniambia kuwa anataka kwenda kwao kumsalimia mama yake kwani anaumwa, nilimpigia simu mama yake na akaniambia kuwa hali yake si nzuri. Nilimruhusu kwenda na akakaa huko kwa wiki mbili. Niliona aibu hata kuwaambia nyumbani kuwa mke wangu hayupo, hivyo ndugu zangu walipotaka kuja kunisalimia kama ndoa mpya, niliwaambia tumesafiri kidogo ingawa sikutaka kuwaambia tuko wapi.

Siku mbili kabla ya mke wangu kurudi, nilimpigia simu usiku, ilikuwa kama saa nane usiku hivi. Sababu ya kumpigia ni kwamba nilikuwa sijisikii vizuri, pumzi zilikuwa kama zinanibana, nilitaka tu kuongea naye kwani nilimkumbuka sana. Simu ilipokelewa lakini hakusema chochote, badala yake nilisikia miguno ya watu wakifanya mapenzi. Kwa zaidi ya nusu saa, nilimsikia mke wangu akipiga kelele akiwa na mwanaume mwingine. Niliumizwa sana kiasi kwamba nilishindwa kuvumilia, mwisho niliamua kukata simu.

Asubuhi nilimpigia simu tena nikiwa na imani kwamba labda angeomba msamaha, lakini aliIkea kwa bashasha kama vile hakuna kitu kilichotokea. Nilimuuliza mama yake hali yake ikoje, akanijibu anaendelea vizuri nikamuambia nipe simu ili niongee naye, kweli nikapewa simu na tukazungumza. Aliniambia kuwa yuko vizuri na anarudi nyumbani kesho.

Nilichanganyikiwa kabisa. Aliporudi, aliendelea na maisha kama kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea. Nilishindwa kuvumilia na nikamuuliza kwa nini nilimsikia usiku ule akifanya mapenzi na mwanaume mwingine. Alianza kucheka sana na akaniambia, "Si mwanaume bana, ningefanyaje mapenzi na mwanaume nyumbani kwa mama? Nilikuwa naangalia video za ngono na najichua, ni tabia yangu tangu chuo lakini nitakuja kuacha."

Ingawa nilikasirika, nilijipa faraja kidogo kwa kudhani kuwa alichokuwa anakifanya ni kujichua tu, hivyo nilisamehe na maisha yakaendelea kama kawaida. Miaka mitatu baadaye, alipokuwa na ujauzito wa mtoto wetu wa pili, aliniambia kuwa anataka kujifungulia kwao. Nikamruhusu kwa sababu mama yake alikuwa anaomba sana kumsaidia uzazi.

Baada ya kuondoka, simu zake hazikupatikana, na mama yake ukimpigia simu anaseama yuko bize na masuala ya uzazi. Nilivumilia niakshindwa kwani sikuwa nimepata taarifa yoyote kuhusu hali ya mke wangu, hivyo nikahisi labda kajifungua na hali si nzuri.

Siku moja niliwasha gari usiku saa mbili, hadi inafika saa sita usiku nilikuwa tayari nimefika Morogoro kwao. Nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwao. Sikumuambia mtu yeyote kuwa nakuja lakini kwa kuwa nilikuwa najua nyumbani kwake, nilienda. Chumba cha mke wangu ni sehemu ambayo tunalala tunapoenda kwao. Nyumba yao ina madirisha yanayoangalia nje ya ua, haipo ndani ya geti. Nilifika mpaka chumbani kwa mke wangu, nikaanza kumpigia simu, iliita lakini haikupokelewa. Nilitaka kugonga lakini nikasikia watu wanaongea kwa ndani.

"Kwanini anakupigia usiku?" Ilikuwa ni sauti ya kiume. Mke wangu alimjibu, "Tangu asubuhi sijapokea simu zake, nimechoka na huyu, sasa usiku huu anapiga nini tena." Huyo mwanaume akamuuliza, "Anajua kuwa mtoto si wake?" Mke wangu akajibu, "Hapana, hata yule mwingine analea tu lakini hajui kuwa si wake, na sijui itakuwaje, siku akijua!"

Wakacheka na baadaye nikasikia wakianza kutomasana kimahaba, miguno ilianza. Niliondoka kurudi kwenye gari. Nilikaa kwenye gari nalia mpaka asubuhi. Mtu wa kwanza kufungua mlango alikuwa mama wa mkwe wangu. Alipoliona gari langu nje alikuja kunigongea. "Mke wako yuko hospitalini, umefika saa ngapi?" Nilimwambia, "Nimekuja tangu saa sita usiku."

Nilitaka kuingia ndani mama yake akakataa na kuniambia niende hospitalini yeye anafunga nyumba yake. Niligoma na kumwambia kuwa najua kila kitu na nataka tu nimuone huyo mwanaume. Mama mkwe wangu aliona aibu, akaniambia kuwa hakuna mwanaume hapa. Hata hivyo, nililazimisha na kuingia ndani. Nilipoingia, nilikuta mwanaume aliyekuwa na mke wangu ni yule aliyenitambulishwa kama baba yake mdogo. Yeye ndiye alikuwa kwenye harusi yangu na hata wakati wa kutoa mahari alikuwa pale akisimamia kila kitu.

Ni mume wa mtu na kumbe walianza na mke wangu wakati tukiwa chuo. Walikuwa wanaendelea na mahusiano naye kwa siri. Huyo mwanaume alimwambia kuwa akipata mwanaume wa kumuoa, aolewe lakini hawawezi kuachana. Kilichoniumiza ni kwamba mke wangu hakuniomba msamaha. Badala yake alisema, "Umeshajua, niandikie talaka yangu."

Niliondoka bila kumuandikia talaka, kwa maumivu makubwa niliyokuwa nayo niliamua kurudi nyumbani bila kumwambia mtu yeyote kilichotokea. Kwa miaka minne, watu walijua nimeachana na mke wangu lakini hawakujua sababu ya kimya changu. Aliamua kuchukua watoto wake na kuhamia moja kwa moja kwa huyo mwanaume, kwani naye aligombana na mke wake na kumfukuza.

Mwaka jana, mwanaume huyo alifariki dunia, na ndugu wa mwanaume wakaja kuchukua kila kitu. Walimtafuta mke halali wa huyo mwanaume, walimuambai mke wangu hawamtambui kwa sababu hana ndoa halali. Kwenye mgawanyo wa mali, hakupewa chochote kwa sababu mali nyingi zilikuwa zimeandikwa kwa majina ya watoto aliozaa na mke mkubwa na si ya mwanaume.

Baada ya hali hiyo, alinifuata na kuniomba msamaha, akisema, "Wewe bado ni mume wangu, hujanipa talaka." Nilicheka na kumwambia aende kufuatilia mahakamani, maana hukumu tayari ilishatoka. Ndiyo, baada ya kutengana naye, kuna mtu alinishauri kuwa ni bora kutoa talaka ili asije kunisumbua baadaye.

Nilifuata taratibu za talaka mahakamani, na niliamua tu kumkomoa bila kumwambia chochote. Kesi ilisi9kilizwa upande mmoja kwani ilionekana kapokea samasi akasaini lakini hajatoke amahakamani ila ukweli nilikua namsainia mimi Nikapewa talaka ya upande mmoja. Alipokwenda kufuatilia mahakamani, alijikuta ameshaachika. Hivyo, talaka tayari ilikuwa imeshatolewa. Sasa hivi nina ndoa yangu mpya na nina amani hata sijui yuko wapi, kweli niliumia kwani nilimpenda sana.

😭😭😭😭
 
anhaa apo sawa nilijua umekuja kutuomba ushauri Mkuu, wanaume tunakutana na visanga sana mpaka tunakuwa sugu. hiyo ng"ombe bado iko Moro? nna lu teni hapa lunazagaa zagaa.
 
Back
Top Bottom