Simu kujipiga yafichua siri

du una maneno!
 
jamani niliahidi nitarudi na majibu,baada ya kazi ngumu ya ushawishi na kufuatia na mistari ya biblia na nikisaidiwa na mwenye kutenda kosa kwapande wake alikuwa mpole sana ila ukweli alisema hajawahi kumpa penzi,na alisema swala la kumuita mume ni huyo jamaa kuwa king'ang'anizi kuwa ipo siku atampata tu,hivyo akawa anamwita mke wangu,tangu waanze hayo mawasiliano ni miezi sita imepita,na walishawahi kuonana mara mbili tu mlimanicity na engen petrolstation mbezi beach ambayo ndo siku alikuta jamaa yupo na gari ya kumuhonga akaikataa, na sikunyingine ndo hiyo ya jmosi walikuwa waonane mwenge lakini ndo simu ikajipiga kwa mume mtu mambo yakatibuka,alijuta na alisema hatakaa arudie tena katika maisha yake ameumbuka vya kutosha,na jamaa amemwambia akirudia hukumu ndogo sana ni kifo,hivyo wamesameheana sijui sasa kama litaibuka lingine ila jamaa anampenda sana mke wake,asanteni sana kwa ushauri wenu
 
mmh?hapo ngumu kumeza na pia ngumu kutema,hii kitu isikie tu kwa mwenzako,ampe kwanza likizo mke kupisha uchunguzi kabla ya kutengana,hata ivyo jamaa ana moyo wa chuma,lol?

akimrudisha kijiji kwa likizo fupi ndo mambo ya kwenda kukumbushia na wachumba zake wote,hapo ngoja kwanza asimpe likizo...
 

akirudia kifo hakitoshi
 
Huyo Mwanamke sio mwaminifu... Kwa sababu akimegwa, haachi alama, Huyo mama hafai ni wa kuachwa haraka!
 
Jibu lipo straight tu wambie jamaa amuambie afungashe vilago arudi nyumbani kwao
 
kwa hiyo ina maana jamaa alichoamua hakina maana? maana kaamua kumsamehe mke wake,sasa sijui tufanyeje jamani
 
kuna watu wengine wapo kuvunja ndoa za watu. mwanamke keshakuambia ana mume, tayari unataka kumpa gari, ili iweje. Hivi kwa nini wanaume hamuogopi wake za watu jamani...!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…