Simu ya aina gani umeshawahi kuitumia na ukaikubali sana?

Mimi lumia 1520 ilikua ni hatari mashine ile, gps yake noma sana, ilikua inakusomea incoming message alaf inakuuliza should i read it ukijibu yes inatiririka meseji yote.
Nokia Lumia 1520 nadhani ndio simu bora kabisa kutengenezwa duniani katika kipindi cha miaka ya 2010 - 2020. Japokua simu hii ilitoka mwaka 2013, lakini ilikua mbele ya wakati wake na mpaka leo hii simu zinazotoka zinapambana kufikia ubora wa ile mashine bila mafanikio. Kuthibitisha hili, hii simu mpaka leo ukibahatika kuipata mpya kabisa itakutoka sio chini ya Tsh 800,000 na ushee ili uweze kuimiliki!
 
HAWA JAMAA SIMU ZAO HAZISHUKAGI BEI HATA UPITE MUDA GANI...ALAFU NI NGUMU..
 
Mimi nipo nje ya mada please. Simu yangu sumsung A50 ina camera mbaya inatoa picha mbaya. Plz advice me nidownload camera gani kwenye playstore
Ndio maana ya midrange products
 
Tecno canon CX , mwaka wa NNE huu bila usumbufu! Nainjoi!

Oppo A, uwiii mwaka wa tatu bila usumbufu.
 
Cm ya kwanza kuitumia ni nokia 3210 tuliletewa zawadi home na mzee sasa m ndio nilikuwa baba wa nyumba nikawa natamba nayo aiseee nilikuwa ni raha sanaaa maana wenye Nokia walikuwa na mabosi tu, baadae tukaletewa Nokia Fulani nimeisahau jina lake lkn ina mwanga mweupeeeeeeee nayo hii nilikuwa habari ya mjini maana niliambia tu inauzwa zaid ya laki 2, , hahaaaa ,hiyo nilikuwa mwaka 2000. Mm mwenyewe naingia dukani kununua cm nilikuwa Nokia 6070 baadae nikaamia kwenye samsang D 900 , na kuendeleea hukoooo

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nipo nje ya mada please. Simu yangu sumsung A50 ina camera mbaya inatoa picha mbaya. Plz advice me nidownload camera gani kwenye playstore
Ulinunua lini? Pengne umeuziwa kopi, umeupdate Os? Ndo natumia a50 hapa. Nijibu tuendelee na mazungumzo.
 
Panasonic GD 55.
 
ngoja nikaitafute ya mtumba hii simu kule Aliexpress ili nije kuuzia sura huku kitaa.
 

yaani mkuu roho huwa inaniuma nikiziona lumia,maana camera ilikuwa msala.

halafu mtu anakuja kusema iphone inatunza thamani.
 
Mimi nipo nje ya mada please. Simu yangu sumsung A50 ina camera mbaya inatoa picha mbaya. Plz advice me nidownload camera gani kwenye playstore
Iweke sokoni tu hyo simu alafu nunua nyingne ambayo itakuwa na kamera nzuri maana kwa huu wakati tulionao. Kamera na storage ni muhimu sna kwnye simu ,huwezi. Kuwa na samsung alafu unatiwa gap kwenye kamera na akina tekno na ndugu yake infinix ni jau sana
 

Nokia 6030

Kulikuwa na type a, b na c
Hizi simu nilitokea kuzipenda sana. ulikuwa ni ukombozi wa maisha yangu enzi hizo ni mwaka 2006 nikiwa naanza masomo ya sekondari.


Motola L7

Bwana bwana hii ikikuwa simu first Class Duniani

Hii L7 ilikuwa na mdogo wake L6 ambayo ioikuwa haina Memory card na ilikuwa ndogo kidogo kwa L7

Ni simu tamu sana kuwahi kutokea. Button zilikuwa laini sana kwa kuchat acha kabisa.



SAMSUNG CORBY

Baadae nikaja kuwa na huyu mnyama. kazimu kazuri sana ka Java OS , Apps zinarun vizuri kitukizuri Zaidi ilikuwa na camera poa na Fonts za kulala

naikumbuka sana hii corby yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…