Simu ya aina gani umeshawahi kuitumia na ukaikubali sana?

Simu ya aina gani umeshawahi kuitumia na ukaikubali sana?

Simu zinakuja na kuondoka. Binafsi nimetumia simu nyingi sana. Simu yangu ya kwanza ilikuwa Motorola, mwaka 1996, service provider wangu alikuwa Tritel.
Lakini katika simu zote ambayo nilizama nayo penzini kwa dhati ilikuwa Nokia Lumia 1020, hiyo ilikuwa 2012.
Hadi leo sijaona mwamba wa kulitikisa jabali lile.
Let's share the experience
Iphone 12, hana mbadala japo Mkorea anajaribu kuiga na Samsung lakini original ni original tu no matter what
 
Nokia jeneza ndio sim yang ya kwanza kumilik na ndio bola kuliko zote nilizowai kutumia nilipewa na b mkubwa 2011 nilipo maliza darasa la 7
 
Acha kabisa, mimi mwenye Iphone akiwa anajishebedua namwangalia tu najisemea hiiiiiiiiii!
Huu mzigo jamaa angu mmoja alinunua ikawa inamshinda baadhi setting ivo akaniambia nikaichek kwenda nakutana na huyu mnyama.

Nikamwambia niuzie akagoma[emoji16].

Mnyama hatari sanaa iphone hapa ni mbulura tu.
 
SAMSUNG WAMETOA SIMU KIBAO ILA KATIKA A-SERIES USIGUSE A-7 (2018) NI SMOOTHLY HUNITOI HAPA WATAPITA KOTE ILA HII BABA LA A-SERIES
 
Mwaka 2011 ndio mwaka hasa nilianza tumia simu, si kwamba sikuwahi tumia simu la hasha kipindi kabla ya hapo nilikuwa natumia tu vyombo vya mawasiliano, nikikumbuka kidogo mwaka 2004 rasmi nikiwa form one ndio nilianza miliki simu nakumbuka ilikuwa tarehe 14 oktoba 2004 siku ya kwanza kupewa simu siemens a35, niliendelea tumia siemens series nyingi mpaka 2007 nilikuwa namiliki siemens yenye kamera na kioo cha rangi, 2007 rasmi niliachana na kampuni ya siemens na kuhamia Sony Erickson, huyu mbabe wa kipindi hicho alikuwa vizuri na kamera, bluetooth, infrared kasoro tu memory card hakunifurahisha nikahamia kwa wazee wa hello moto, motorola L6, 2008 januari hiyo, ile kitu ilinipa heshima kwanza ilikuwa na internal memory mb10, kubwa sana kipindi kile pili ilikuwa inahifadhi na kucheza Mp3 songs mpaka zenye quality ya 128bits per sec, bluetooth, spika yake sasa ilikuwa inachuja safi sana kubwa kuliko lote ilikuwa naweza chomeka kwenye PC yangu na ku convert nyimbo zangu kadhaa na kuanza tumia bila shida ili mradi nisimalize zile mb10. Potelea pote ile simu kidogo inipe jimama pale mbeya wakati nasoma, niliishia kumuuzia huyo mama na kupewa malipo ya kuunga unga na ofa ya kwenye kula wali kila siku na kulipapasa... Baada ya hapo wachina walianza niteka na simu zao za tachi za kutumia kijiti, memory card plus chaji kuisha haraka hiyo 2009.

2011 nikiwa chuo ni mara ya kwanza kwenye nunua simu pale mlimani city duka la Samsung, hapo ndio first Android phone Galaxy S imezinduliwa bei yake ilikuwa laki 7 na ushee.... Ahh laki 7 kwa usawa ule hapana... Muda si punde ikazinguliwa galaxy mini...ebwana ee budget phone ya kwanza toka familia ya galaxy... Ila haikuwa cheap mazee 360,000 ilinitoka hapo nishagoogle dunia nzima ilikuwa ishaanza elewa maana ya Android phone [emoji336] ni nini, nilijua hii ndiyo platform ya kibabe duniani ukiachana na wave os ya samsung ambayo nayo ilikuwa sokoni kipindi hicho, Galaxy mini ilikuwa tamu wazee imagine for the first time naweza download kila kitu nikipendacho kwenye Market siku hizi playstore... Mara simu niitumie kama remote, naweka apps nizitakazo na kuzifuta, kalikuwa smooth na camera tamu sana kwa simu za kipindi hicho, watoto walinikoma maana ulikuwa ukiingia gallery yangu ina video kibao za kuchekesha nimepata whatsapp (nakumbuka whatsapp nimejiunga 2011 kipindi kile hata groups hakuna nilikuwa nachat na mtoto wa kiarabu classmate alikuwa na htc katoka nayo Dubai, basi nilikuwa femous balaa).

Kwangu mimi hii simu ilinifungulia dunia.
samsung-galaxy-mini-s5570-1.jpg
 
Simu zinakuja na kuondoka. Binafsi nimetumia simu nyingi sana. Simu yangu ya kwanza ilikuwa Motorola, mwaka 1996, service provider wangu alikuwa Tritel.
Lakini katika simu zote ambayo nilizama nayo penzini kwa dhati ilikuwa Nokia Lumia 1020, hiyo ilikuwa 2012.
Hadi leo sijaona mwamba wa kulitikisa jabali lile.
Let's share the experience
Ebanaeeeeee kwangu Sony hana mpinzani
 
Galaxy j7 pro daa nzito chuma tupu camera msako betri ya kutosha,Galaxy s8 ilikuwa na kaumbile fulani hv kadogo camera yake sio mchezo,usiku inatoa picha kama nikon,S9 ndo nagala gala nayo hapa nayo ni balaa zito
 
Simu yangu ya kwanza ilikua Motorola bapa, nilipewa zawadi ya simu pamoja na mpira kutoka kwa beberu mmoja hivi kwa kipindi hicho kijiji kizima mwenye simu kali ni mimi hapo nipo darasa la saba...walimu, wanafunzi wao, Afisa Elimu Kata, Wauguzi katika kituo cha Afya wote walipata habari za simu hii. I was a celebrity...
View attachment 1631960

NB: Mabeberu walishatuzoesha na misaada toka tupo underground. Hii ni vita ya kiuchumi ndugu zangu katika kuelekea dona kantri.
Hv bado zipo?
 
Kuna siku ya Google, nimeiona mwaka 2011. Sijui exactly ilikuwa model gn, lkn ile simu nadhani ilikuwa mbele ya wakati.
 
Simu yangu ya kwanza ilikuwa
1. Ericson nilinunua kwa Dada Mmoja alikuwa mfanyakazi wa Mobitel (Tigo) Enzi hizo kwa 60,000 mwaka1998

2. Siemens m35 nilinunua pale magomeni kwa bei 110,000 mwaka

3. Sony Ericson T100 hii niifurahia Sana kalikuwa kana milio mingi pia mwanga mzuri mwaka 2001.

4. Siemens L42 hii nilipewa na Boss wangu ilikuwa kali Sana enzi hizo ilikuuwa Ina tumia memory card kubwa ilikuwa 2003

5. Motorola Flat ilikuwa amazing hivi 2005

6. Vodafone

7. Samsung Dual sim

8. Tecno ya tochi

9. Coolpad one hii imevunjika kioo nimekiagiza simu nzuri naipenda Sana

Vísimu vya tochi 2 majina sikumbuki

10. Infinix hot 8 siipend nakutumia kwa dharura nasubiri kioo cha Coolpad one
 

Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    16.2 KB · Views: 18
  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    32.5 KB · Views: 9
  • images.jpeg
    images.jpeg
    8.9 KB · Views: 18
  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    6.9 KB · Views: 12
Back
Top Bottom