Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,559
- 12,518
Lipia Tangazo
Kuna rafiki yangu mmoja hivi hajatulia kivile kwa wanawake, sasa akawa anahisi mke wake ana cheat na huyo mke wake ni kutoka nchi jirani sema ni mjanja mjanja sana. Basi sijui nani alimpa ushauri wa kwamba afanye kila njia a hack simu ya mke wake ili kujua njema inayo toka naye.
Jamaa ana vijipesa akajaribu kucheki na jamaa wa kampuni moja ya mawasiliano kama wanaweza msaidia ikashidikana, sasa wazo likawa ni kutafuta app za phone spy, akapata moja kwa USD 80 akalipia kwa Mastercard, akatumiwa link ya kupakua appl na ilikuwa ni ya kuisntall kwenye device mbili, au simu mbili.
Mpango wa kuinstall kwenye simu ya mke wake ukaanza make lazima upate simu ya mtu unaye taka ku mspay na uinstall, jamaa katumia trick ya kwamba simu yake imekufa na kuna email muhimu ya kazini so akapewa simu ili asome email kumbe ndio kufanya instalation.Baada ya hapo sasa ni kuanza kufuatilia, ila jamaa ni mtu wasafari sana sasa akampatia mshikaji wake mmoja laptop na jukumu la kufuatilia kila kinacho toka kwenye simu ya mke wake, make app ilikuwa ina track call, picha, sms, whatsapp, facebook mesenger, Insta na hata twiter. Rafiki yake ile siku ya kwanza tu alicho kuiona, akakataa kyendelea na zoezi akazuga amepata dharura, ikibidi sasa jamaa arudi safari aje mwenyewe asome na kufuatilia simu.
Jamaa amerudi ile amelog in na kuanza kuangalia, jamaa kidogo azimie kwa alicho kiona, jamaa anakuambia yeye mwenyewe anapenda wanawake ila alicho kishuhudia kilimtisha sana, sema jamaa alijipa ujasiri akaendelea kufuatilia kwa mwezi mzima make app ilikuwa ni ya mwezi mzima.
Kwenye device ya pili nayo akainstall kwenye simu ya mchepuko wake mwingine ili aangalie kama anaweza replace mke wake,huko kwenye mchepuko nako akukatana na yale yale kama ya kwa mke wake,mshikaji anakuambia wanawake wanatongozwa sana facebook huko ndiko wanako gawa number,yaani Instagram na facebook huko sio salama kabisa, make mshikaji alikutana na jam ya watu wanaomba number na wanatumiwa, wengine wanapotezewa.
Ninavyo andika jamaa walisha gawana mbao na huyo mke wake kitambo sasa, jamaa aligoma kuvumilia akaamua kila mtu afuate mambo yake.
Mshikaji ila anajutiaga sana anasema bora asingefuatilia,make anasema anaona kama wanawake wote wako sawa sawa tu kwa tabia.Sema kavuta mwingine ila amekoma kufuatilia mawasiliano ya simu ya mke wake.
Njia pekee ya kumdhibiti Mke ni TEGO la kichawi tu! akichepuka atakiona cha Moto kudaadeki.Nimuamua kushare na nyie huu ujumbe nimekutana nao sehemu ili uwe na Amani ya moyo fanya hivi;
=======
Kwa wanandoa na wenye wapenzi waaminifu, uaminifu limekuwa ni jambo la msingi sana ili udumu na huyo uliyeingia naye kwenye ndoa, mjengee imani kuwa wewe ni wake na haitatokea siku ukamsaliti.
Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, kwenye baadhi ya ndoa kuna sarakasi nyingi sana. Katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na tatizo kubwa la baadhi ya wanandoa kutibuana kila siku kisa kikiwa ni kutokuaminiana kupitia simu zao.
Kwa hili niseme tu kwamba, ni wanandoa wachache sana ambao wanaamini simu za wenza wao hazina madhambi, wengi wanahisi wanasalitiwa kupitia simu na ndiyo maana unaweza kukuta mke akishika simu ya mumewe tu inakuwa shida.
Si hivyo tu, wapo wake za watu nao hawataki kabisa simu zao zishikwe na waume zao, unajiuliza kwa nini iwe hivyo kama kila mtu anajiamini? Lakini sasa, leo naomba niwashauri kitu wale walioingia kwenye ndoa.
Kuna mambo ambayo unatakiwa kuyapuuza laa sivyo huwezi kuwa na amani katika maisha yako. Kama kweli unampenda huyo uliyenaye, usimfikirie vibaya! Jenga imani kuwa, hawezi kukusaliti.
Hii tabia kwamba simu ya mwenza wako ikiita tu unachungulia kujua nani kapiga, SMS ikiingia unafungua, ya nini kujipa presha? Hivi unadhani kweli unaweza kumzuia huyo mwenza wako asikusaliti kwa kutompa uhuru wa simu yake? Hili ni gumu hivyo unachotakiwa kufanya ni kumuacha na simu yake. Usijipe presha zisizo na msingi.
Unaweza kukurupuka, ukapokea simu ya mumeo, mara unakutana na sauti nyororo ya msichana, presha inakupanda bila kujua aliyepiga ni nani. Na yeye kwa kuwa aliyepokea siye aliyempigia, anakata.
Wewe huko uliko unachanganyikiwa, unafikiri aliyepiga ni mchepuko. Kumbe aliyepiga labda ni mfanyakazi mwenzake au rafiki yake wa kawaida tu. Wewe unakuja juu na kumwambia mumeo anakusaliti, kumbe hamna kitu kama hicho.
Au wewe mwanaume unaweza kuchukua simu ya mkeo, ukaenda kwenye sehemu ya meseji ukitaka kujua ni nani huwa anachati nao. Bahati mbaya unakutana na meseji ya kimahaba iliyotumwa na mwanaume ambaye alikosea namba. Wewe bila kuwa na uhakika na kile ulichoona unakimbilia kuhitimisha kuwa, mke si muaminifu.
Hili ni tatizo kubwa ndiyo maana leo hii nimeona niwakumbushe tu kwamba, simu ya mwenza wako achana nayo ili kujihakikishia amani ya moyo wako.
Kujua mwenendo WA mwenzi wako ni MUHIMU SANA tena Sana kwa sababu hiyo itasaidia kuwekana Sawa kabla ya matatizo kutokeaSio kuwashwa bana saa nyingine yanakuwa Mahaba hayo
Jina la ile nimesahau sijui ni my spy, sijui ilikuwa inaitwaje..Huwa nahitaji ila nashidwa
Uko sawa mkuuKujua mwenendo WA mwenzi wako ni MUHIMU SANA tena Sana kwa sababu hiyo itasaidia kuwekana Sawa kabla ya matatizo kutokea
Kumbuka mke au mume wako NDIYE msiri wako wa kwanza na huyo NDIYE mtakae Kula wote janga lolote litakalo mkuta yeyote miongoni mwenu, Uhuru usizidi kiasi kufuatililiana mienendo kwa wanandoa na kuonyana MAPEMA NI MUHIMU zaidi kuliko kuungana na wanao halalisha umalaya na ufuska kwa kwa hoja nyepesi eti usishike Simu ya mwenzi wako, labda kama sio mumeo ambaye lako lake na lake lako.
Sababu tatizo lolote lile ndani ya ndoa litawahusisha wanandoa wenyewe nankuna wakati linaweza sababisha matatizo Hadi kwa watoto wenu
Mke au mume akiwa na hofu juu ya upekuzi WA mke au mume kwenye mienendo yake itasaidia Sana kupunguza traffic zisizo na tija ,pia kuambiana na kukumbushana mara kwa mara juu ya uaminifu lakin kila MTU kutimiza majukumu yake ya kindoa kwa mwenzie kikamilifu kwa upendo kama wanandoa,
Hakuna privacy kati ya wanandoa halisi wanao ishi kindoa kabisa , labda kama mnaigiza kwenye hiyo ndoa au mnaishi kwa kuviziana , kujifanya kuleta usasa kwenye ndoa ndiko kuliko Fanya ndoa kwa SASA isiheshimike kabisa watu wanachukulia ndoa kama mchezo wa kuigiza.
Nina kisa kimoja
Ndugu mmoja anaishi na mke wake, mke akamtambulisha rafiki yake kwa mume wake rafiki ambae wanatoka kijiji kimoja ila wote wapo mwanza kwa SASA wanafanya kazi ,
Baadae mke akabaini ukaribu wa kiasi kwa mumewe na yule rafiki, kikubwa kilicho saidia NI ujumbe kupitia SMS ambao mke aliuona kwenye simu ya mumewe wakichat kimahaba na rafiki yake , baada ya mke kuona hivyo haraka sana bila kuchelewa pamoja na kughafirika Sana lakini alimwabia mumewe kuwa unataka kunipa adhabu ya kubugia ARV maisha yangu yote huyu bint ni mgonjwa tangu Tupo Advance na ni carrier mzuri Sana punguza Tamaa mume wangu utasababisha maisha yasiyo na Nuru katika familia yetu napenda mungu taupe uzima tuufikie uzee tukiwa Salama tufurahi na wajukuu zetu mungu akijalia.
Ni kweli usemalo Mkuu.Kujua mwenendo WA mwenzi wako ni MUHIMU SANA tena Sana kwa sababu hiyo itasaidia kuwekana Sawa kabla ya matatizo kutokea

Nafanana na nani tena huyo bwana yaweza ikawa ndiye 😂😂Ni kweli usemalo Mkuu.
Japo aina yako ya uandishi umefanya nitabasamu tu kwani mnafanana na mtu mmoja hivi. Koh koh
Kama ni wewe basi nakusalimia Mkuu. 😜
😂Depal huna utani kabisaSimu yake simu yangu, yangu ni yake 😂
Hahahaaaa. Lol.Nafanana na nani tena huyo bwana yaweza ikawa ndiye 😂😂
Kabisa Polo..🤣 nakaba mpaka penatly😂Depal huna utani kabisa
Kiazi weweHater wangu namuachia vyote sense Sim Wtf 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
nakutafuta sehem uje dom kwanzaKiazi wewe
Hahahah sidanganyiki ng’oonakutafuta sehem uje dom kwanza
Aikooh acha uoga we keyboard warrior 🤣 🤣 🤣Hahahah sidanganyiki ng’oo