Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure



Upumbavu wake sio wa kila mtu, mimi nakagua, mimi nafuatilia kila kitu.
 
Njia pekee ya kumdhibiti Mke ni TEGO la kichawi tu! akichepuka atakiona cha Moto kudaadeki.
 
Sio kuwashwa bana saa nyingine yanakuwa Mahaba hayo
Kujua mwenendo WA mwenzi wako ni MUHIMU SANA tena Sana kwa sababu hiyo itasaidia kuwekana Sawa kabla ya matatizo kutokea

Kumbuka mke au mume wako NDIYE msiri wako wa kwanza na huyo NDIYE mtakae Kula wote janga lolote litakalo mkuta yeyote miongoni mwenu, Uhuru usizidi kiasi kufuatililiana mienendo kwa wanandoa na kuonyana MAPEMA NI MUHIMU zaidi kuliko kuungana na wanao halalisha umalaya na ufuska kwa kwa hoja nyepesi eti usishike Simu ya mwenzi wako, labda kama sio mumeo ambaye lako lake na lake lako.

Sababu tatizo lolote lile ndani ya ndoa litawahusisha wanandoa wenyewe nankuna wakati linaweza sababisha matatizo Hadi kwa watoto wenu

Mke au mume akiwa na hofu juu ya upekuzi WA mke au mume kwenye mienendo yake itasaidia Sana kupunguza traffic zisizo na tija ,pia kuambiana na kukumbushana mara kwa mara juu ya uaminifu lakin kila MTU kutimiza majukumu yake ya kindoa kwa mwenzie kikamilifu kwa upendo kama wanandoa,

Hakuna privacy kati ya wanandoa halisi wanao ishi kindoa kabisa , labda kama mnaigiza kwenye hiyo ndoa au mnaishi kwa kuviziana , kujifanya kuleta usasa kwenye ndoa ndiko kuliko Fanya ndoa kwa SASA isiheshimike kabisa watu wanachukulia ndoa kama mchezo wa kuigiza.

Nina kisa kimoja

Ndugu mmoja anaishi na mke wake, mke akamtambulisha rafiki yake kwa mume wake rafiki ambae wanatoka kijiji kimoja ila wote wapo mwanza kwa SASA wanafanya kazi ,

Baadae mke akabaini ukaribu wa kiasi kwa mumewe na yule rafiki, kikubwa kilicho saidia NI ujumbe kupitia SMS ambao mke aliuona kwenye simu ya mumewe wakichat kimahaba na rafiki yake , baada ya mke kuona hivyo haraka sana bila kuchelewa pamoja na kughafirika Sana lakini alimwabia mumewe kuwa unataka kunipa adhabu ya kubugia ARV maisha yangu yote huyu bint ni mgonjwa tangu Tupo Advance na ni carrier mzuri Sana punguza Tamaa mume wangu utasababisha maisha yasiyo na Nuru katika familia yetu napenda mungu taupe uzima tuufikie uzee tukiwa Salama tufurahi na wajukuu zetu mungu akijalia.
 
Huwa nahitaji ila nashidwa
Jina la ile nimesahau sijui ni my spy, sijui ilikuwa inaitwaje..
Ulikuwa una download, unaiweka kwenye simu ya mwenzio, we unakuwa una log in kwenye website yao, unapata utamu woote..

Ila uwe na moyo, niliiweka kwa mtu wa kwanza nikaona makorokocho, nikajiweka kando, kwa huyu wa pili nikaona usalama mwingi, nilimfuatilia kama miezi mi3 hivi, nikaona yanitosha nikaacha kumfatilia, kwa nilichokiona, sina haja ya kumfatilia tena, nikawa nimejiridhisha.
 
Uko sawa mkuu
 
Ni kweli usemalo Mkuu.

Japo aina yako ya uandishi umefanya nitabasamu tu kwani mnafanana na mtu mmoja hivi. Koh koh

Kama ni wewe basi nakusalimia Mkuu. 😜
 
Ni kweli usemalo Mkuu.

Japo aina yako ya uandishi umefanya nitabasamu tu kwani mnafanana na mtu mmoja hivi. Koh koh

Kama ni wewe basi nakusalimia Mkuu. 😜
Nafanana na nani tena huyo bwana yaweza ikawa ndiye 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…