Simu yako ya gharama ulinunua bei gani na siku ulipopoteza au kuibiwa ulijisikiaje?

Simu yako ya gharama ulinunua bei gani na siku ulipopoteza au kuibiwa ulijisikiaje?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Nilijitahidi sana na kufanikiwa kununua iPhone 7 Plus nikiwa mwaka wa kwanza chuoni mwaka 2019, kipindi hicho simu hiyo bado ilikuwa maarufu sana. Nilikuwa naipenda sana kwa sababu ilikuwa inapiga picha nzuri na pia niliweza kuhifadhi mambo yangu mengi.

Siku moja nikiwa njiani kuelekea Mwenge, wahuni wakanisachi kwenye daladala wakaondoka nayo. Niliumia sana, kiasi kwamba sikuhudhuria darasani kwa wiki nzima, mwili ulikosa nguvu. Simu hiyo niliinunua kwa laki tano, nikawa nawaza hiyo hela bora ningeifanya mtaji wa biashara ya viatu na pochi.

Sio kwamba ilikuwa ndo simu ya gharama nimewahi miliki ila ile simu niilikuwa attached nayo.

Wewe mdau simu yako ya gharama kuimiliki ni ipi na bado unayo?
 
Smart kitoch ya 45 elfu nilichomolewa Las Vegas kwa wahuni
 
Mil 3+ nikaipoteza kizembe tu nilihisi kuhara, nashukuru niliipata kwa msaada wa mzee flani humu namuombea baraka zote
 
Back
Top Bottom