Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Simu za mkopo zimezuiwa features nyingi mno za muhimu ambapo kibongo bongo ni ngumu mtu kutumia simu bila kuzigusa. Njia kuu wanayotumia wakiona mtu analazimisha kufikia features hizo ni kuzuia kabisa simu yenyewe isitumike
Kinachotokea ni kwamba mtu anatumia simu siku chache akiivuruga inakuwa kopo anaweka kapuni. Baada ya hapo anakwenda kusajili nyingine na kuendelea. Sijui hii ina madhara gani kwa kampuni maana kwa mteja ni kianzio chake tu!
Kinachoonekana ni hofu ya makampuni kuibiwa ndiyo maana wanafanya wafanyayo. Hii hali ukiangalia kwa pande zote tatu (kampuni/mteja/taifa) inaleta athari nyingi kiuchumi, kijamii na kadhalika.
Ushauri; wataalamu wa tehama hizi zilikuwa ndiyo sehemu zenu za kuapply mlichosomea. Badala ya kuzalisha simu za kuja kutupwa ovyo ni bora mkaangalia namna ya kuboresha simu zenu zifanane na za kawaida bila kuathiri mifumo yenu ya malipo