Simu zinazodaiwa ni Used kutokea Dubai na Korea ni nzima au tunapigwa?

Simu zinazodaiwa ni Used kutokea Dubai na Korea ni nzima au tunapigwa?

Mpaka sasa natumia Samsung s8 ni mwaka sasa haijawahi sumbua, ni kama mpya tu. Zingatia duka la kununua tu hizi used, usije unganishwa na madalali ukapewa used from bongo
 
Jambo ninalokumbuka sina hakika lina ukweli kiasi gani.

Wanasema ni Used lakini sio Used ni Simu mpya hizo ambazo ni copy ya matoleo halisi na zinatengenezwa South Korea na China.

Simu hizo huja baada ya mwaka au miaka miwili ikishatoka toleo original. Hivyo zinashushwa bei na ili usishtuke wanaziita ni Used clean au Refurbished.

Niliwahi kuchukua mzigo wa simu za Samsung wa biashara nikiamini Samsung ni simu bora kilichonitokea ni balaaa.
Swali la msingi ni je zinafanya kazi kama zile na camera zinakiwa quality au ni za kubumbabimba tu
 
Used from dubai imekuwa ni msemo kuvutia biashara, na kwasababu watu tunaamini kitu kilichotumika kutoka nje kinakuwa bora kama vile tunavonunua used magari kutoka japani kwasababu wenzetu hatumii bitu kwa mda mrefu.

Hizi simu used zinauzwa kwetu zinzkuwa zimetumika mahali popote pale hata hapa hapa kwetu Tz, mtu karudisha kafanya top-up wanrepair then inauzwa kama used, vivo hivyo na kutoka nje pia. (Inaweza kuwa ilivunjika kioo, ilichubuka rangi, ilimba betri ilipiga shrort, software problem n.k)

NB:- ukiwa hujui hizi cm utauziwa kama mpya ikiwa package kwenye box.
Kwa Samsung kuanazia s22 na mote 22 ndio simu mpya na iPhone ni kuanzia iphone14 kuendelea ndio mpya. Chini ya matoleo hayo zote ni used, usiuziwe na ukaambiwa kuwa ni mpya.
 
Back
Top Bottom