Used from dubai imekuwa ni msemo kuvutia biashara, na kwasababu watu tunaamini kitu kilichotumika kutoka nje kinakuwa bora kama vile tunavonunua used magari kutoka japani kwasababu wenzetu hatumii bitu kwa mda mrefu.
Hizi simu used zinauzwa kwetu zinzkuwa zimetumika mahali popote pale hata hapa hapa kwetu Tz, mtu karudisha kafanya top-up wanrepair then inauzwa kama used, vivo hivyo na kutoka nje pia. (Inaweza kuwa ilivunjika kioo, ilichubuka rangi, ilimba betri ilipiga shrort, software problem n.k)
NB:- ukiwa hujui hizi cm utauziwa kama mpya ikiwa package kwenye box.
Kwa Samsung kuanazia s22 na mote 22 ndio simu mpya na iPhone ni kuanzia iphone14 kuendelea ndio mpya. Chini ya matoleo hayo zote ni used, usiuziwe na ukaambiwa kuwa ni mpya.