Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanasema usiusemee moyo wa Mwingine, huwezi jua akiona hali ngumu anayoipitia Mwenzake akaingiwa huruma akampa hata mtaji ajiajiri.Hapo kwenye mambo safi na kupigwa tough ndiyo sijapaelewa yaani upigwe tafu na pesa za mwaume mwezio anayehudumia mke wake? Kuna tukio unalitazamia wewe eeh shauri tabia za kimarioo hizo.
Sjasahau ndo maana nikaimajin kwa upande wanguUsisahau kuna Watu wamejaliwa kusamehe na kusahau.....ni Wachache lakini wapo.
Duh, ni noma...ila inategemea na Mtu na tabia yake.Mkuu wanawake wana visasi vizito hasa kwenye suala la kuumizwa ki hisia
Nilishawai muumiza mdada hivy hivy yaani kilichotokea ni hatari nilijutaaaaa
Na aliniambia bado maisha yangu nitajutia labda niwe mbali sna nae au nife
WIvuGold digger wa kiume,, hata aibu huna mxeeeeeeuw
Duh, ni noma...ila inategemea na Mtu na tabia yake.
HujaulizwaUnitende afu tena ujirudishe ayayayayayayaa ntahakikisha umetoweka kwenye ulimwengu wa wanadamu wa kawaida
Ila kapisi😂😂😂Gold digger wa kiume,, hata aibu huna mxeeeeeeuw
Kwaivo ukaona hilo ni jibuHujaulizwa
Kwenye komenti yangu moja katika mada mojawapo .Ananisimulia jamaa yangu:-
Miaka kama tisa iliyopita nilikuwa kwenye mahusiano na Mwanadada mmoja tuliyekuwa tunafanya nae kazi kwenye kampuni moja.
Ndani ya miaka mitatu mapenzi yetu yalikuwa motomoto kabla ya Mimi kuamua kujitoa ghafla bila ya hata sababu za msingi. Hali iliyomuumiza sana Mwanadada huyu mpaka kupelekea kuhitaji msaada wa kisaikolojia (niliambiwa na watu wake wa karibu).
Siku zikapita kila Mtu akiendelea na maisha yake....baadae Dada alipata Mtu mwingine na sasa ana maisha yake na wana Watoto wawili.
Baada ya kupoteana kwa muda niliamua kumtafuta kisirisiri kujua yuko wapi na anaendeleaje kwani Mimi niliacha kazi kwenye ile kampuni nae nikasikia baadae aliacha.
Baada ya sakasaka ya muda karibia miaka miwili hatimae nilimpata kwenye facebook akitumia jina tofauti kabisa...na nilimshtukia kupitia comment yake kwenye ukurasa wa Mtu.
Nilianza kwa kucomment na ku like kwenye post zake mwishowe aligundua ni mimi...kinyume na matarajio yangu Dada akaonesha amefurahi sana na tukaanza kuwasiliana. Kutoka hapo tumekuwa tunawasiliana mara kwa mara huku mimi nikiwa muoga kumtonesha kidonda cha yaliyopita kwani ni dhahiri ya kuwa nilimuumiza sana mpaka nikikumbuka najiona sifai....nakumbuka neno la mwisho alinitumia kwenye meseji wakati huo "wewe ni shetani...wewe ni muuaji"
Kwa sasa huwa tunafuatana facebook ku comment na ku like, na mara moja moja huwa anakuja inbox...mimi kama mimi sijawahi kuanza kwenda inbox ila kuna siku niki comment kwenye post yake yeye anakuja inbox na tunachati hili na lile.
Kuna wakati atapost yupo kwenye bata na Wanae au Rafiki yake/zake, niki comment tu yeye ata comment "njoo".....mimi naishia tu kusema "nipo mbali ningekuja".
Kwa sasa mambo yake ni safi kwani ni boss kwenye kampuni anayoifanyia kazi na ameanzisha kampuni yake ya utalii.
Bado sijaelewa kama ananikaribisha ki roho safi pamoja na nilichomfanyia miaka kadhaa nyuma. Ingawa nimeshawahi kumuuliza kama alishanisamehe akaniambia yaliyopita yamepita tuachane nayo.....Huo moyo ndio bado nimeuogopa.
Ningekuwa sijamtenda ningekuwa huru hata kumwambia anipige tafu maana mambo yake safi huku mimi nachechemea.
SweetiKwaivo ukaona hilo ni jibu