Simulizi -2 Hours of Memories (Espionage and Science)

SEHEMU YA 26
Rania alichukua funguo haraka haraka na kisha aliingia na kuja kusaidiana na Mama Rania ambae hata kuvaa alisahau kwani wakati huo alikuwa amevaa kanga tu alio jifunga .
“Mama kavae nguo utaenda hivyo” Aliongea Rania baada ya kumuona mama yake akiwa hata hajavaa nguo , Mama Rania aliingia ndani haraka haraka na kisha alivaa dela na kuchomoka huku akifunga ile laptop na kisha akatoka na alipotoka Rania alikuwa tayari ashaukalia usukani na hapo hapo gari iliwashwa na kuingia barabarani na ndani ya nusu saa tu walikuwa washafka kwenye hospitali ya Ocean Road na kisha samiri alichukuliwa na machela kisha wakampeleka kwenye chumba cha wagonjwa wa dharula .
Rania alijikuta akikaa chini kwenye mabenchi na kuanza kulia na kumfanya mama yake kumwangalia mwanae huyo na kisha aliinuka alipo kaa na kumfata kisha akamkumbatia . huku wakifarijiana , baada ya kama nusu saa hivi dokta alitoka na hapo wakwanza kuamka alikuwa ni Rania .
“Baba yangu anaendeleaje Dokta” Aliuliza Rania na Mama Rania na yeye aliinuka na kumsogelea Dokta na Dokta aliwaambia wamfuate .
“Hali ya mgojwa inaendelea vizuri japo bado hajarudiwa na fahamu , lakini kiufupi ni kwamba kapata mshituko wa moyo na muda si mrefu atakuwa sawa”
“ Kwa hio tunaweza kumuona?”
“Sio kwa sasa , sasa hivi nawashauri kwanza mrudi nyumbani na mtarudi hapa siku ya kesho , kwani saivi yupo kwenye uangalizi maalumu kwani tunataka kuujihakikisha kabisa kuwa hana shida nyingine” .
“Dokta Mosesi habari”Aliongea mwanaume mmoja akiwa mlangoni alieonekana kuwa mtanashati sana na akichangiwa na uhandsome .
“Dokta Singano “ Rania alinyanyuka na kwenda kumkumbatia mwanaume yule kwa muda ndipo walipo achiana.
“Mimi ni dokta wa familia , nipo hapa kwa ajili ya kumuangalia mgonjwa wangu”Aliongea Dokta Singano na hapo Dokta Moses akatingisha kichwa kukubaliana na Dokta Singano huku wote wakitoka nje .
“Madam nadhani mnaweza kwenda tu kwa sasa , nitakaa hapa kuangalia hali ya mgonjwa” Aliongea Dokta Singano na Mama Rania alie kuwa yupo kimya muda wote akionekana kwenye mawazo aliitika kwa kichwa kukubaliana nae
“Mimi nitabaki mpaka nimuone baba akiamka “ Aliongea Rania na mama yake alimwangalia kisha akakubaliana nae na akaondoka eneo hilo .
“Jamani Singano umerudi lini kutoka masomoni, na umezidi kupendeza na kunawili”
“Nina wiki sasa”Aliongea Singano kwa mapozi akimuangalia Rania kwani walionekana kulingana kiumri japo Singano alionekana kuwa mkubwa kidogo.
Basi baada ya masaa kama mawili hivi Samir alirudiwa na fahamu na wakati huo alikuwa tayari ashatolewa kwenye chumba cha dharula na kupelekwa katika wodi ya VIP ,Rania alikuwa mpaka wakati huo hajandoka bado na muda ulikuwa ni kama saa moja inaenda na nusu na alikuwepo katika chumba hicho cha ward .
“Dady!!“ Aliongea Rania baada ya kupapaswa mkono na baba yake kwani alikuwa amepitiwa na usingizi.
“Mama yako yuko wapi ?” Aliongea Samir kwa wasiwasi kweli .
“Kaenda nyumbni alikuwa hapa muda si mrefu” Alijibu na Samir kufumba macho na wakati huo Dokta Singano aliingia na kumfanyia vipimo.
“Hali yake ipo sawa inabidi turudi nae nyumbani kwa sasa ,nitamhudumia akiwa nyumbani” Aliongea Dokta Singano na kisha Rania alitoka na kwenda mpaka mapokezi na kupewa karatasi ya kumruhusu mgonjwa na baada ya taratibu zote Samir alitolewa huku akiwa mzima japo alikuwa akionesha hayuko sawa kimawazo .
*****
Peter alishangaa uwepo wa mrembo alie kutana nae kule fukwe ya kawe kwani alikuwa akimkumbuka sana na hajawahi kuisahau sura yake .
“Kumbe mnaishi wote?”Aliongea Nasma na kasauti kake kakitoto lakini mwili mkubwa na kumfanya Peter atabasamu .
“Ndio sisi ni ndugu” Aliongea Peter huku akimwangalia Masumbuko na kurudisha uso wake kwa Nasma na kisha akasogea mpaka kwenye sofa na kukaa .
“Vipi Steve mgeni wetu mshamkaribisha vizuri?”
“Yeah , ndio kama unavyo ona kaja kwa ajili ya Masumbuko”
“Sijaja kwa ajili ya Masumbuko tu , ila nimekuja kwa wewe pia “ Aliongea Nasma kwa hali ya aibu huku akimwangalia Peter na kushusha macho chini jambo ambalo lilimvutia sana Peter.
“Halafu isitoshe mimi ni jirani yenu “ Aliongezea .
“Mhmh tangu lini?”
“Muda mrefu tu , halafu nilikuwa nikiwatafuta kila siku niwashukuru kwa siku ile , ila juzi nilikutana na Masumbuko kaa..”
“Kafanyaje ?”Aliuliza Peter na kumfanya Masumbuko amwangalie Nasma kwa sura ngumu kama askari anaemrushia adui risasi , alitamani hata ambadilishe mawazo kwani hakutaka kuumbuka.
“Nilikutana nae hapo nje ya geti” Alibadilisha na kumfanya Masumbuko ashushe pumzi na kutabasamu na Nasma na yeye alitabasamu na kitendo hicho Peter alikishuhudia na hata Steve .
“Kwa hio wewe unakaa wapi?”
“Nakaa nyumba hio hapo yenye geti lililoonakshiwa kwa rangi ya silver”
“Kumbe una kaa hapo jirani tu hapo, inaonekana familia yenu iko vizuri sana” Aliongea Peter maana hakujua kuwa mtu anae ongea nae alikuwa ni mtoto wa adui yake yaani tajiri Samir na pia ni mtoto wa mchepuko wake yaani Mama Rania Au Shani The Boss ,lakini pia hakujua kama anaongea na mdogo wake wa damu.
“Hapana nakaa mwenyewe tu ni nyumba yangu baba na mama wako nje ya nchi kwa sasa” Aliongea Nasma huku akidanganya maana hakutaka wajue kuwa yeye ni mtoto wa tajiri mkubwa nchini tajiri Samir .
Basi Peter alienda kubadilisha nguo zake na kisha akarudi sebleni ambako Nasma na Masumbuko walikuwa wakipiga stori kana kwamba wamekutana miaka mingi iliopita kumbe ndio mara ya tatu walikuwa wanakutana , aliwaangalia na kisha akamgeukia Steve aliekuwa akiwashangaa na muda wote alikuwa akimshangaa Nasma tu na alikuwa akitamani bahati ya Masumbuko iwe ya kwake,Peter alitabasamu na kisha akamkonyeza Steve na kumuita chumbani kwake .
“Hivi hawa unawaelewa kweli?” Aliuliza Peter .
“Mimi hata sielewi maana mtot kaja Masumbuko kamvuta kwenye kona ya jiko ile na si nikaenda kupiga chabo nilikuta mtoto ananong`onezwa na Masumbuko.
“Hili jamaa na ndio maana nakwambia huyu muhuni sana huyu, unajua mambo ambayo anayofanya namuona kama kiumbe kutoka sayari nyingine”
“Mimi natamani niwe kama yeye halafu yule mwanamke ni mzuri ile mbaya , halafu wanaonekana wamekutana mara nyingi hawa”
“Hahaha..Steve wewe huwezi cheza na nyota ya Masumbuko ushasahau kuwa alikula mtoto mkaliiii.. wewe ambaae huwezi mla . sasa huyo Nasma inaonekana tayari keshajaa kwenye kumi na nane za Masumbuko , sijui walikutana wakapeana kumbukumbu hata sijui” Aliongea Peter huku kuna karoho ka wivu kakimsumbua maana alikuwa akimkumbuka sana Nasma sema mambo yake ya kisasi yalikuwa ndio yamemsahaulisha kwa muda . “Kaka eti Masumbuko hajui kusoma?” Aliuliza Nasma baada tu ya wao kutoka kwenye chumba ambacho walikuwa wa wakipiga umbea na mwenzake Steve.
“Ndio , kwani kakuambia?”
“Ndio , nitamfundisha mimi na atajua kusoma”
“Wewe huwezi kunifanya nijue kusoma mimi ni Zaidi ya kilaza nimesoma mpaka darasa la saba najua kuandika baba , mama , na kaka tu” .
“Utajua mimi nakwambia mimi wewe kubali ni kufundishe , kubali basi “ Aliongea Nasma kwa kumlazimisha Masumbuko na ubishi wake alikubali maana hata yeye alikuwa keshavutiwa na Nasma na muda mchache walio kuwa wamekaa pamoja alijikuta Masumbuko akifurahi sana .

******
Hii nchi ni nzuri sana , kwa mara yangu ya kwanza najisikia kuwa huru na mwenye furaha kama hivi” Aliongea mrembo aliekuwa amezungukwa na walinzi kibao na huyu sio mwingine ni Queen mrembo na mwanamitindo ambae wana habari hawakuwa nae mbali, kila mahali alipo kuwa anaenda walikuwa wakirusha habali zake kwa kila kitu alicho kuwa akifanya kwani watu wengi walionesha kuvutiwa na mwandada huyo .
“Ndio Madam , hi inchi imebarikiwa sana ina vivutio vingi”
“Kweli”
“Ndio , na kwasababu wewe ushakuwa mmoja ya mabalozi wetu basi tutahakikisha kwa muda utakao kuwa hapa nchini unatembelea kila kivutio “
“Nitafurahi sana “
“Dadii” ilisikika sauti ya mtoto ikiita na kumfanya waziri wa utalii aliekuwa akionge na mrembo Queen kugeuka na kuangalia sauti iliko tokea kwani alikuwa akiifahamu sauti ya mwanae kuliko sauti zote .
“My daughter huyoo .. huku wakikimbiliana na kukumbatiana na kisha akahamia kwa mama yake alie kuwa na mtoto huyo .
“Queen kutana na familia yangu , huyu ni Paskalina mke wangu “ Aliongea waziri na kumfanya Queen kuvutiwa na kila kitu kuhusu familia .
“Na huyu ni malikia wangu ajulikane kwa jina la Patricia “
“Dadii .. nilimuona kwenye tv “ Aliongea Patricia na kumfanya Queen ajiulize mtoto huyo kasema nini.
“She says has seen you on Tv “
“Wow! so beutifull you are so cute”
Basi Queen siku hio alijikuta akifurahi sana siku hio , na kilicho mpa furaha na kujihisi wa tofauti katika maisha yake ni uwepo wa familia ya waziri, kwake ni kituambacho hakuwahi kupitia hapo kabla.
Kwa siku hio walikuwa katika moja ya vivutio vilivyopo Ngorongoro Crater , Paskalina au Mama P kama wengi walivyozoeakumuita na Queen urafiki wao ulianzia hapo kwani ucheshi na ujuaji wa lugha ya kingereza kwa paskalina vilimfanya waendane sana katika mazungumzo na mwanadada Queen.
Na ni moja ya kitu ambacho kwa namna moja kilimfanya ajihisi wa tofauti katika siku zake za kuishi kwani hakuwahi kuishi kwa furaha kiasi hicho , hii ni kutokana tokea azaliwe katika ‘tube’ aliotengenezewa hakuwahi kukutana na mwanafamilia wa Profesa Snart , licha ya kwamba tajiri huyo alikuwa akimwaminisha Queen kuwa yeye ni baba yake na hana ndugu wengine Zaidi yake .
***
Maisha ya Stella na Sebastiani pamoja na rafiki yake Lea ambae alikuwa akimwamini sana yaliendelea , huku ukaribu wa Sebastiani na stella ukizidi kukomaa , licha ya ukaribu huo kukomaa, Sebastiani hakuwahi kumwambia Stella alikuwa akimpenda sana ,alikuwa ni kama hajiamini na alikuwa akikosa ujasiri wa kumwambia Stella kuwa anampenda.
Na mara nyingi sana walikuwa wakikutana chuoni na kuongea na Stella kama ni kwenda kula walikuwa wakienda pamoja na kufanya mambo mengi pamoja , lakini pia kila mmoja alikuwa bize sana na masomo kwani muda wakuingia kwenye mitihani yao ya mwisho ili waweze kupewa vyeti vyao vya shahada ukikribia
Stella aliendelea kumchekea na kumuamini rafiki yake Lea usoni na kumbe upande mwingine ndie aliekuwa injinia mkuu kabisa wa kutengana kwao na James mwanaume alietokea kumpemnda sana na kudumu nae katika mahusiano. .
Mapenzi kati ya James na Lea yaliendelea huku Lea akiamini kabisa kuwa James alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati kabisa .
Stella japo alikuwa yuko bize na mitihani na pamoja kuwa karibu na Sebastiani lakini hakuna siku ambayo alikuwa ashawahi kumsahau hata maramoja James , kwani alimkumbuka kila siku na kuna siku alitamani hata ampigie aongee nae au kumtumia ujumbe wa maandishi , lakini haikuwezekana kwani kwa muda huo alikuwa ashablokiwa muda mrefu na hakukuwa na njia zozote za kumpata kimawasiliano.
Siku hio alijikuta kumkumbuka sana James wake hata akajikuta akikosa kabisa Amani ndani ya moyo wake na kutamani sana kuiskia sauti ya James , kwani kile alicho kuwa akiamini katika moyo wake ni kwamba james alikuwa akimpenda na ndio maana wamedumu katika mapenzi kwa muda mrefui kwa kiasi hicho.
Pasipo kujua kuwa katika mapenzi muda hautafsiri mtu kukupenda , kwani unaweza ukakutana na mtu ambae ndio Mungu amekupangia kuwa nae ukaona kwa vitu mlivyofanya kwa muda mfupi basi ni zadi ya muda wa miaka mitano au kumi ulivyofanya na mtu ambae si sahihi kwako..
Siku hio alijikuta akipanda juu kabisa ya nyumba(Apartment) ambayo alikuwa kapanga gorofa ya juu kwani chini yake alikuwa amepanga mtu mwingine na uzuri wa nyumba ile ni kwamba kila gorofa kwa juu ilikuwa na sehemu ya kupumzikia na sehemu ya kuogelea pia kama tu utataka yaani ‘swimming pool’ (Infinity pool) ni moja ya Apartment ghali sana ndani ya jiji la Dar ,lakini gharama yake iliendana na mazingira na ubora wa Apartment hizo kwa haraka haraka unaweza ukasema ni ‘Penthhouse’.
Wakati akiwa anaangalia mbele juu kabisa ya nyumba hio huku mawazo juu ya James yakimwendesha ndipo alipo jikuta akishusha macho yake chini na kumuona mwanume mwenye mwili kama wa James wake akiwa akiogelea kwenye swimming pool ilio kuwa kwa chini ya nyumba hio .
Mwanaume yule alionyesha ujuzi mkubwa sana katika kuogelea na alionekana mtu ambae alikuwa akipenda sana kuogelea , kwani ufundi alio kuwa akionyesha ulikuwa wa hali ya juu sana . kwani alikuwa akiogelea kama vile alikuwa akishindana jambo hilo lilimfanya Stella hata yale mawazo yake juu ya James kupotea kwa muda na kujikuta akimshangaa mwanaume huyo aliekuwa na uwezo kwa kuogelea kwa ujuzi mkubwa sana , japo hakumjua mwanaume yule ila mawazo yake yualimwambia labda ndio mpangaji alio kuwa akiambiwa na mtu alie mpangisha hio nyumba .
Alijikuta mapigo yake yakipiga kwanguvu baada ya mwanaume huyo kuibukia juu ya maji na kuonyesha sura yake , na mwanume yule aliangalia juu na kumuona Stella, alimwangalia jambo ambalo lilisababisha kwa wao kugongana kwa macho (Puzzled look)
****
“Madam naweza kuongea na wewe” Ni Dokta Singano aliekuwa akiongea na hio ni baada tu ya kuingia ndani ya nyumba hio ya tajiri Samir na jambo ambalo lilimsukuma kufanya hivyo ni kuona kuwa kuna hali ambayo sio ya kawaida inayoendelea ndani ya nyumba hio na yeye kama daktari ambae alikuwa akihakikisha kuwa kila kitu katika nyumba hio kinakuwa sawa ili afya za wateja wake kuwa sawa pia , aliona ni vyema sana kama ataongea na Madam ili kupata kufahamu tatizo ni nini , kwani alikuwa akimjua sana Samir alikuwa mtu mwenye afya yake na hakuwahi kupatwa na tatizo la moyo hapo kabla .
“Sawa tunaweza kuongea “ Alijibu Mama Rania baada ya kumfunika Samir vizuri na kisha akatoka na wakaongozana katika ofisi moja iliokuwa imejaa vitabu katika nyumba hio na ilionekana kama ni kijimaktaba kidogo cha kusomea maana kilikuwa na vitabu(Home library)
“Nipo hapa kwa ajili ya kujua shida ni nini haswa mpka kikapelekea hali ya afya ya boss wangu kubadilika ghafla” .
“Ni maswala ya ndoa tu Singano na nipo tayari kukuambia kwani najua wewe ni Daktari na pia mnajua jinsi ya kumsahuri mtu”
“Ni kweli kabisa unaweza kuniambia”
Mama Rania alianza kumwambia kila kitu na hapo ndipo Dokta Singano alipo kuja kujua ni nin kilitokea mpaka kikapeleka hali ya Samir kuwa katika hali ile maana alikuwa akimjua sana mteja wake huyo na alikuwa akiifatilia afya yake na mara ya mwisho kuangalia afya yake ni mara tu alipo tua nchini .
“Najua ni jambo ambalo linauma sana na mimi kama mshauri siwezi kulizingumzia hili katika njia ya kukwambia unacho takiwa kufanya , lakini jambo ambalo ninataka kukushauri ambalo litakusaidia wewe mwenyewe kufikia hatua ya kulitatua tatizo hili bila kuathiri muunganiko wa familia ni kuangalia ni faida gani na hasara kwa maamuzi utakayo chukua , jaribu kuweka hisia zako pembeni na jaribu kufikira juu ya hilo . pia napenda ni kushauri kabla ya hayo maamuzi utakayo yafikia kaeni chini muongee ila msishtukizane hali ambayo inaweza kuleta madhara ya kiafya , Angalieni chanzo cha kuanza kwa matatizo yenu ni nini na kama mnaweza kurekebisha kaeni chini muongee na muangalie ni namna gani mnaweza kufanya kuokoa hali inayo endelea katika familia” .
Aliongea Dokta Singano na kisha akatoka hapo na kwenda chini ambako alikutana na Rania .
“Singano naweza kuongea na wewe kabla haujaondoka?”
“Ndio “
“Unajua sielewei hali ya baba imekuwaje mpaka akiwa vile na najua mama hawezi kuniambia chochote , kwahio mimi najua ushamuuliza na kakwambia kila kitu sasa nataka namimi uniambie ni nini kinaendelea kati ya baba na mama please” Aliongea Rania kwa hali ya kuomba kabisa.
“Sikia Rania mimi ni daktari na daktari ili kuilinda heshima yangu lazima nilinde na kutii sheria zote nilizo wekewa kuzifata na moja ya sheria kubwa ni kutotoa taarifa zozote za mgonjwa pasipo ridhaa yake mwenyewe nafikiri wewe ni msomi unaelewa hilo, najua unawasiwasi lakini ni swala dogo sana litaisha”Aliongea Dokta Singano na hapo hapo akachukua kijibegi chake na kisha kutoka huku akipisha na Najma ambae alikuwa akiingia ndani hapo bila kujua ni kipi kilicho kuwa kinaendelea .
****
Mke wangu naomba unisamehe sana , najua ni kosa ambalo litahitaji muda na ujasiri wa kunisamehe ila niko chini ya miguu yako naomba unisamehe tafadhari mke wangu nakupenda sana na sipo tyari ya kukupoteza “ Hayo ni maneno yalio kuwa yakimtoka Samir .
Mama Rania alimwangalia Samir kwa hasira huku akionekana aking`ata meno na alionekana kufanya maamuzi tayari na yupo tayari kutoa hukumu yake kwa mume wake .
Mama Rania alitoa simu yake na kupiga simu kwa Peter na mume wake akiwa anamuangalia na haikujulikana hata dhumuni la kupiga simu hio kwa Peter mcheouko wake mbele ya mme wake ilikua ni nini .
“Hellow!”
“Naulizia lile jambo tuliloongea mchana kama upo tayari naomba unijibu sasa hivi ni muhimu sana” hayo ndio maneno ya Mama Rania yalio sikika na Samir vizuri na kumfaya mwanume aliepiga goti chini kuonesha kujutia kwa kitendo chake cha kutoka nje ya ndoa .
laiti angejua kuwa hapo ni ngoma droo kwani kila mtu alikuwa na mchepuko wake nadhani asingepiga magoti hayo chini kwani kitendo hicho kilionekana kumpa ushindi Mama Rania .

SEHEMU YA 27
Mama rania alikuwa ni mwenye kuhitaji kutoka kwa Peter ili aweze kiutoa maazu juu ya mme wake , alishusha simu yake chini na kumwangalia samir kwa hasira , na kisha alipanda kitandani na kuchukua shuka na kulala akiangalia upande wa ukutani , Samir alijikuta akikosa cha kufanya na kunyanyuka zake na kutoka kwenye chumba hicho na kwenda kwenye chumba cha kujisomea na kisha alikaa huko mpaka akapitiwa na usingizi , na kwa jinsi alivyo kuwa amelala alikuwa akitia sana huruma kwani ungeambiwa masaa mawili alikuwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharula usingeamini.
Rania alikuwa akiingia ndani ya chumba hiko cha kujisomea ndipo alipojikuta akishangaa sana kwa kuwepo wa baba yake katika chumba hicho , alijikuta akijuliza alifikaje fikaje hapo kwani alikuwa akijua kuwa baba yake alikuwa kapumzika na muda huo ulikuwa ni usiku yapata saa nne za usiku , alijikuta akidondosha chozi la huruma kumhurumia baba yake , kwani alikuwa akimpenda sana baba yake na alikuwa hayupo tayari kumuona akiwa katika hali kama hio , alijikuta akimgusa baba yake kwenye bega na kumuamsha na Samir aliejiinamia kwenye meza akuwa amelala alishtuka .
“Rania nimepitiwa na usingizi”
“Baba jamani mbona uko hapa daktari si alikuambia kuwa unahitaji kupumzika”
“Nilikuwa nimepumzika nikawa sijisikii kulala na ndipo nilipo kuja kusoma kidogo sasa nilipitiwa na usingizi” Aliongea Samir huku akijiamsha kivivu na kisha akatoka na kumuacha Rania akiwa kwenye huzuni sana kwani alijua yote baba yake alio yasema sio ya kweli na kuna jambo kubwa ambalo lilikuwa likiuendelea yeye na mama yake , na hakuwa na jinsi ya kulitatua .
“Yakiendelea hivi nitampigia bibi na babu simu” Aliongea rania huku akikaa kwenye kijimeza na kuanza kusoma kitabu chake alicho kuwa ameshikilia , lakini kadiri alivyo kuwa akisoma kitabu hicho alijikuta akizama kwenye mawazo ya kumfikiria Peter .
“Daah .. Peter nimekupenda kwanini unaamua kunifanya nisubiri kiasi hichi , moyo wangu umechoka nakuona kama haunipendi kama ninavyo kupenda na unanisubiilisha kwakuwa una mwanamke mwingine” Aliongea mwenyewe na kujikuta hata machozi yakimtoka bila hata ya kujielewa .
Alijikuta akitamani sana kusikia sauti ya Peter , lakini alijizuia kwani alitaka ampigie simu.
****
Peter baada ya Nasma kuondoka huku akimwahidi Masumbuko kuwa atakuwa anamuita kwenye nyumba yao ka ajili ya kumfundisha jinsi ya kusoma na kuandika basi aliona apumzike na alikuwa amechoka kwani mchana alikuwa kwenye shoo ya kumridhisha Mama Rania , alijikuta akipitiwa na usingizi na kilicho kuja kumshitusha ni simu aliangalia nani anapiga ndipo alipoona kuwa ni mama rania ama boss wake .
Alipokea simu hio kivivu lakini swali alilo ulizwa na mama huyo lilimfanya ainuke na kukaa vizuri .
“Lakini si nilikuambia kuwa naomba muda wa kufikiria juu ya hili Shani , siwezi kujibi swala kama hili kwani ni muhimu sana na linagusa maisha yangu , kwa hio naomba nifikirie”
Aliongea Peter na kuona kama mwanamama huyu alikuwa akimpelekesha maana hapo hapo alipo sema maneneo hayo alikata simu, alijikuta akivuta shuka lake jepesi na kuendelea kulala kwani hakutaka kufikiria chochote
“Mwanangu mambo unayo yafanya hayanifurahishi kabisa mimi mama yako , ushasahau kuwa mimi nimekufa kwa kuonewa , nimekufa kifo chakusababishiwa na watu ambao wanayafurahia maisha , kwanini unasahau ni kwa jinsi gani mimi mama yako nilivyo kufa , mwangu nataka uwatafute walio nisababishia mimi kufa , mwanangu anza sasa kuwatafuta ili mama yako nipumzike kwa Amani , anza sasa , anza sasa mwanangu , inuka anza sasa”
“Mamaaa” Ilisikika sauti ya Peter akipiga makele na kumfanya masumbuko aliekuwa akiota anafanya mapenzi na mwanmke mrembo kushituka na yeye na kukimbilia kwenye chumba cha ndugu yake Peter na aliingia kwani mlango ulikuwa haujafungwa.. na kumkuta Peter akitokwa na jasho jingi sana alijikuta akimkumbatia Masumbuko kwa woga sana , masumbuko alijikuta akikosa cha kufanya kwani kufariji alikuwa hajui alimwnagalia Peter aliekuwa akitetemeka kwa hofu.
“Peter” Aliita Masumbuko na Peter kwa wasiwasi alimwangalia Masumbuko na Masumbuko hakuchelewa alimchezeshea na kumpa faili la masaamawili ya kumbukumbu na Peter alijikuta akiwa sawa kabisa na kuchukuwa shuka na kulala zake .
Masumbuko alitabasamu na kisha akamfunika kaka yake huyo na kisha kisha na yeye aliondoka zake kulala maana ilikuwa ni usiku sana . .
Peter aliamka zake asubuhi na wala hakuna kitu alicho kuwa akikumbuka kabisa zaidi ya kujiandaa kwa jili ya kuelekea chuoni kwani kwani hata yeye alikuwa yupo mbioni kumaliza chuo .
Basi hio ndio ikawa maisha ya Peter kila siku alikuwa akiota ndoto ambayo mimi msimuliaji nimeamua kuita kwa neno la ‘Anza Sasa’kwani kila siku Peter alikuwa akiota ndoto hio na kubweka usiku na Masumbuko alikuwa akiamka na kumpa faili la kumbukumbu na akiamka subuhi ashasahau kabisa kuhusu ndoto.
****
Stella alijikuta akiona aibu baada ya kukutanisha macho kwa macho na mwanaume yule . na kujikuta akitoka hapo na kuelekea ndani kwake na kukaa , huko huku akichukua laptop yake na kuanza kujisomea ,kwaajili ya mtihani hakutaka kujiuliza zaidi yule mwanaume ni nani kwa muda huo lakini jambo hilo lilishindikana.
Lakini ilikuwa kama ni starehe ya mwanume yule kwani kila siku alikuwa akimuona akiogelea na Stella ule muda alikuwa akipanda juu kwa jili ya kumuona mwanume yule na ni kweli kila siku alikuwa akimkuta akiogelea , yaani ni kama wanaume yule asie mfahamu jina hio ndio ilikuwa ratiba yake au na yeye alifanya makusudi kumuona Stella , kwani kila siku alikuwa on time alikua akiogelea ,lakini mwanume yule hakuwa hata na habari na Stella kwani alionekana hata alikuwa hajali kabisa , lakini kwa Stella ilikuwa na yeye ratiba yake imebadilika kwani kila akirudi chuo alikuwa akipanda juu kabisa ya nyumba hio na kungalia chini kumuona mwanume yule akiogelea , kila siku alijikuta akipenda sana kumuona mwanaume yule akiogelea katika swimming pool na kilichomfurahisha mwanume yule ni jinsi mbavyo mwanaume yule alikua akiogelea .
****
Ukaribu wa Nasma na Masumbuko ulikomaa zaiidi na zaidi na walikuwa wamezoeana sana kiasi kwamba ilifikia kipindi Masumbuko alikuwa akienda nyumbani kwa Nasma , na alipo kuwa Nasma anasoma na Masumbuko alikuwa yupo anasoma na nasma ndio alikuwa mwalimu wa masumbuko , alijitahidi kila siku kumfundisha masumbuko kusoma lakini masumbuko akili yake ilikuwa ni kusahau tu kwani anvyofundishwa leo kesho alikuwa tayari amekwisha sahau kabisa na Nasma hakukata tamaa kabisa katika kumfundisha kwani kwanza alikuwa kifurahia kwa jinsi Masumbuko alivyokuwa akimchekesha na kumfanya afurahi kiufupi alifurahia uwepo wa Masumbuko.
Kuna muda alikuwa akimuomba Masumbuko alale mahali hapo , lakini masumbuko aligoma kwani alikuwa anajua anakazi moja usiku ya kufanya , ya kumpa Peter dozi ya kumbukumbu ili asisumbuliwe na ndoto zake za kila siku zilizo kuwa zikimsumbua , kwani Peter kila anapo ota , alikuwa akimpa dozi ya kumbukumbu za masaa mawili na kisha Peter analala na akiamka asubuhi amesahau kama usiku alikuwa ameota ndoto ya ‘Anza sasa’.
Hayo ndio maisha ya Peter , lakini kiufupi ni kama Masumbuko alikuwa anamsaidia sana Peter kwani kipindi hicho Peter ilikuwa ndio wakati wake wa kuuthibitisha uwezo wake katika masomo yake ambayo alikuwa ndio kwanza anamalizia na zilikuwa zimebaki siku chache sana mpaka kufikia siku ya mtihani , na hata kwa upande wa Rania ilikua ni hivyo hivyo hakumsumbua sana Peter kuhusu mapenzi kwani wote walikua katika mitihani yao ya mwisho na kila mtu alikuwa na ndoto za kupata GPA za juu kabisa.
***
Mama Rania hakumsamehe kabisa Samir na hakutaka kusikia kabisa mume wake akimuomba msamaha , kwa upande wa Samir alikuwa amebadilika sana na kilicho msaidia kumbadilisha ni kwamba Amanda alikuwa tayari amekwisha ondoka na kurudi .
Na kutokana Samir hakuwa na mtu ambae alikuwa akimchelewasha kurudi , basi hakuchelewa kazini na hata Mama Rania nae hakuchelewa kazini , aliwahi kurudi lakini hakuna kupeana dudu kwani Mama Rania alikuwa hataki hata kuguswa na Samir alichojua ni kwamba mke wake huyo ana hasira bado ila kuna siku atamsamehe na ndio maana alikuwa kila siku akirudi kutoka kazini na zawadi kwa ajili ya mke wake , lakini zawadi hizo wala hazikuleta athari au kumbadilisha mawazo kabisa Mama Rania kwani wakati huo alikuwa kafa kaoza kwa dudu ya Peter, kwani vitu ambavyo walikuwa wakipeana na Peter vilikuwa ni vitu ambavyoo vilimfanya asimtamani kabisa mume wake .
Lakini kutokana na kuomba msamaha na kuonesha kujutia sana kwa Samir hatimae Mama Rania alimsamehe mumewe bila kinyongo jambo ambalo Samir hakulitarajia siku hio na hata Najma na Rania walivyo ona wazazi wao wamemaliza tofauti zao , jambo hilo liliwafurahisha sana .
“Mom , dady jumamosi ijayo ni graduation yangu”Aliongea Rania siku hio walipo kuwa wapo mezani familia nzima wakiwa wanapata chakula cha usiku .
“Dada yaani ndo siku hio na mimi napanga kufungua kampuni yangu usiku huo rasmi” Aliongea Najma
Ungejiuliza ni kwanini Najma yeye kamaliza chuo na dada yake bado lakini jibu ni kwamba Rania yeye alikuwa anachukua masters ya uchumi na kwa Najma yeye alipita moja kwa moja kwenda chuo baada ya kumaliza ‘high school’ kwa mtaala wa Cambridge kwani ulikuwa unachukua miaka kumi na moja tu .
“haitakuwa mbaya tutaweza kuzifanya sherehe zote kwa wakati mmoja , kwakuwa wewe ufunguzi wa kampuni yako itakuwa ni usiku , basi tutaanza na Rania huku watu wengine wakiweka sawa kila kitu kwa ajili ya usiku na sisi familia tutakuwa kwenye sherehe,pindi sherehe itakapofika tamati tutajiandaa kwa jili ya ufunguzi wa kampuni yako .
“Ni sawa dady itakuwa vizuri”Aliongea Rania na Najma na yeye alikubali
Mama Rania aliangalia watoto wake hao na kujikuta akitamani na Nasma angekuwepoo ila ndio hivyo Nasma alikuwa akipenda kuishi mwenyewe na alikuwa hapendi kujulikana kama mtoto wa kitajiri na alikuwa amekosana na baba yake nyuma kabisa kisa ni kwa Nasma kwenda kusomea nje ya nchi lakini Nasma alikataa kabisa ndipo ugomvi ulio sababisha Nasma kuhama nyumbni ukatokea kwani Samiri aliweka walinzi wakumfatilia Nasma kila anapo enda jambo ambalo lilimkasirisha mwanadada huyo baada ya kugundua na mama yake kumpa nyumba akaishi baada ya kutaka kuhama, na kwa Samiri hakuwa na shida maana alikuwa amechoka kugombana nae
. ****
“Boss unampango gani na Rania kwa sasa?“ Aliuliza Ramso .
“Kwa sasa nadhani kama unavyojua kuwa yupo mbioni kumaliza chuo , na kama baba yake alivyoniahidi ni kwamba akishamaliza tu basi nitapeleka barua ya posa na nitawafanya wazazi wake wakubali na mimi mwenyuewe ninayo njia ya kumfanya binti yao akubaliane na mimi kwa namna yoyote ile” Aliongea Hemedi huku akitabasamu kifedhuli.
“Boss ukimpata yule utakuwa umepata chombo maana kila siku nikimwangalia nasisimka”
“Pumbavu wewe na nikishampata wewe nakuhamisha kikazi maana ushaanza kumtamani mke wangu mtarajiwa”
“Sio hivyo boss”
“Ramso wewe ni kijana wangu ila kwa Rania atakae mgusa tu hata unywele napiga risasi”
“Sawa boss , ila haujaniambia ni udhaifu gani utamshawoshi mama yake kukubalia na umuoe bint yake”
“Hivi Ramso unanifanya mimi kama mtoto mdogo , mimi najua kila kitu kinacho muhusu Mama Rania na lazima akubaliene na mimi kwa namna yoyote il” .
“ kwanza siku yake ya mahafali nataka ukamnunulie gari ambalo hakuna mwanke anae litumia hapa Dar, gari hilo litakuwa nizawadi yangu kwake”
“Sawa boss”
****
Ilikuwa ni siku ambayo ilisubiliwa na kila mmoja , siku ambayo ilikuwa ndio siku maalumu kwa wanachuo walio kuwa wakimaliza masomo yao katika ngazi tofauti tofauti , kuna waliokuwa wakimaliza katika level ya shahada ,kuna waliokuwa wakimaliza katika ngazi ya udhamiri (Masters) kuna waliokuwa wakimaliza katika ngazi ya PhD graduation hii ilifanyika kabla ya mtihani wa mwisho jambo ambalo halikuzoeleka lakini lililokubalika kwa wahitimu na hawakupewa vyeti halisi .
“Naona mzee leo umetoka chicha ile mbaya” Aliongea Steve siku hio alio kuja asubuhi kwa jili ya kumpitia rafiki yake kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe hio .
“Hata wewe umetoka sana na hiko kitai chako”
Siku hio Peter alikuwa na furaha sana kwa kile kilicho kuwa kinakwenda kutokea , alijikuta akiisogelea picha ya mama yake na , kisha kuingalia kwa huzuni sana.
“Mama natamani siku hii ungekuwepo unione mwanao katika sherehe hii” Aliongea Peter kwa huzuni sana kwani alionekana alikuwa amemkumbuka mama yake sana.
“Tuondoke muda tayari , Masumbuko yeye si kasema anakuja na Nasma ,sisi tutangulie”
“Okey , halafu najihisi siku hizi kuna kitu hakipo vizuri ,. Nahisi kuna kitu nimesahau “ aliongea Peter wakati wakitoka nje ya nyumba hio na kuliendea gari .
“Kwanini ?“
“Hamna tu yaani hata sielewi kuna kitu nahisi nakisahau ila hata sielewi nahisi moyo wangu kuwa mzito kila ninapoamka asubuhi”
“Itakuwa mawazo tu ndio maana usiliweke sana akilini hilo”
“Daah! poa .. ngoja tukasherehekee hivyo muda si mrefu tunamalizana na chuo na tunrudi mtaani”
Waliendesha gari mpaka chuoni na kuungana na wenzao kwani sherehe hio ilikuwa ikifanyika mapema,
Baada kama masaa mawili ya wao kuwasili chuoni hatimae walivaa majoho yao na kuingia kwenye ukumbi mkubwa wa Nkurumah Hall , ili kuanza sherehe hio .
Huku kwenye geti la kuingialia alionekana Mama Rania na mumewe wakiingia ndani ya chuo na haikupita hata muda mrefu alionekana Masumbuko akiwa na mwanadada mrembo Nasma na yeye akishuka kwenye gari moja nzuri , huku Masumbuko nae akiwa amependeza kweli kweli na kama ungemuona usingejua ni Masumbuko maana kwanza likuwa amevalia miwani moja ya jua huku akiwa amevalia suti fulani ilioshonwa kwa mtindo wa kipekee sana ya rangi ya bluu.
Waliongozana na Nasma na kuingia ndani ya chuo hicho huku watu wengi wakiwaangalia walivyopendezana , na walio kuwa wakimshangaa Zaidi ni Masumbuko kwani umaarufu aliokuwa nao Nasma wa kuwa mzuri na bila ya kuonekana na mwanaume wa aina yoyote tokea aanze masomo halafu siku hio kuongozana na mwanaume , ni jambo ambalo wengi walihitaji kumjua huyo mwanume ni wa aina gani, anapesa kiasi gani na kipi spesho hata aweze kumpata mrembo Nasma hukuwatu wengi wakishindwa kumpata mrembo huyo. .
Basi sherehe hio ilienda vizuri,mheshimiwa rais ambae alikuwa mgeni rasmi siku hio , alitoa hotuba yake na hapo wanafunzi ambao walifanya vizuri wakizawadiwa,akiwemo Peter ,Stella , Rania na Steve hao ndio moja ya wanfunzi ambao walipata zawadi katika maswala ya taaluma.
Ratiba ilienda haraka haraka sana na baada ya saa saba mchana sherehe hio iliisha na watu walianza kupeana zawaidi , huku wengine wakipiga picha .
Wakati huo Peter akiwa anapiga picha na Masumbuko , ndio wakati ambao na familia nzima ya Samir ilifika katika eneo hilo ,mwanzoni hakuna alie muona Peter kwani alikuwa amezungukwa na watu wengi na alikuwa haonekani mpaka pale Samir na familia yake walivyofika katika eneno hilo .
Hapo ndipo Peter alivyo geuka na kukutanisha macho na ya Samiri akiwa na familia yake. .

SEHEMU YA 28

Peter alimwangalia tajiri Samir na tajir Samir alimwangalia Peter na wote walijikuta wakiangaliana kwa macho ya hasira sana , na alie kuja kukatiza ni Rania kwani alimfuata Peter na kumkumbatia huku na Mama Rania na yeye akimkubatia Peter na kumpa hongera zake , kwa Samir aliwaangalia tu mke wake na Rania alijikuta hasira na chuki za waziwazi zikimpanda na kwa Mama Rania kuna kitu alikigundua juu ya Peter na Samir lakini alimezea mate.
“Hongera sana Peter kwa kuwa mwanafunzi bora katika sayansi am so proud of you “Aliongea Mama Rania .
“Asante sana” Huku wakiweka maigizo mbele ya Rania na Samir na haikujulikana wakati huo Masumbuko ,Nasma na Najma walikuwa upande gani kwani wao hawakuwepo eneo hilo.
“Vipi wazazi wako wamekuja tusalimiane nao?” Aliuliza Rania na kumfanya Peter awe mnyonge huku akifikiria jibu la kuwapa na Rania siku zote hakufahamu kama Peter alikuwa yatima.
“Tupo hapa” Ilisikika sauti ya kike na kuwafanya wote wageuke na kuangalia sauti ilikotokea .
“Haa! Aunt Grace, baba mdogo Gift” Aliongea Rania huku akiwakumbatia .
“ Kaka za siku !” Alisalimia Gift akimsalimia Samir .
“Salama Tu” Alijibu huku akiondoka eneo hilo na hata haikueleweka kwanini aliondoka maana walio kuwa mbele yake walikuwa ni ndugu zake tena wadamu , kwani Grace , Gift , Samir ,Profesa Gladness walikuwa wanazaliwa na baba mmoja japo mama tofauti tofauti(Soma: My dream my favourite).
“Peter my boy njoo unikumbatie” Aliongea Gift na Peter alimsogelea Gift na kisha kumkumbatia , huku akihamia kwa Grace, Rania alikuwa akimwangalia Peter na kuna jambo aliliwaza kwa wakati huo .
“Shemeji sisi tumekuja kwa ajili ya Peter leo kumwakilisha Profesa kwani kabanwa na majukumu na kasema hatoweza kuhudhuria , ila pia tumembebea Rania zawadi uncle wangu ”Aliongea Grace.
Basi familia ile ilijumuika kwa kupiga picha za hapa na pale huku Mama Rania akipiga picha na Peter naMama Rania kila alipo kuwa akimwangalia Peter usoni alikuwa akipata hisia za kufanya mapenzi.
“Peter hii ni kadi yako naomba uongozane na mimi leo kwenye tukio la ufunguzi wa kampuni ya mdogo wangu nataka uwe my plus one”Aliongea Rania wakati wakiagana na Peter.
Peter aliingalia ile kadi baada ya kuichukua katika mikono ya Rania na kisha aliitikia kwa kichwa kuwa atahudhuria katika tukio hilo .
Basi hatimae sherehe iliisha na watu walitawanyika na kurudi majumbani , wengine wakibakia chuo hapo kwa wale walio kuwa wakiishi hosteli za chuo .
****
Ndani ya ukumbi ulio kuwepo ndani ya hoteli ya Serena kulionekana kukiwa na mapambo ya hapa na pale yaliokuwa yakiandaliwa kwa kupambwa kwa ustadi mkubwa ndani ya ukumbi huo , huku akionekana mwanadada Najma akisimimia shughuli hio yeye mwenyewe kwani hakutaka kitu kiharibike kwani alikuwa amealika watu wa kubwa wakiwemo wanamuziki na wasanii mbalimbali wakubwa ndani ya tukio hilo la uzinduzi rasmi wa kampuni yake.
“Vipi kuhusu ile picha ulio kuwa unasemea? “ Aliuliza Rehema rafiki yake.
“Rey ile ni muhimu kwangu na lazima katika tukio hili niiweke kwani nina amini kwa kutumia picha ile nitampata mwanaume ninae mtafuta , kwani najua kesho atakuwa kwenye magazeti na mitando ya kijamii pamoja na picha yangu na lazima atakuja kunitafuta” Aliongea Najma huku akiendelea na kazi alio kuwa akiifanya na yalikuwa yamebaki masaa machache tu kwa muda wa wageni kuwasili kwa ajili ya sherehe hio
****
“Boss kuna dharula”Ni sauti ya Kadabra iliekuwa ikisikika katika simu ya Samir wakati huo Samir akiwa nyumbni kwake baada ya kurudi kutoka kwenye mahafali .
“Dharula gani hio ?”
“Peter atahuduhuria kwenye tukio la leo kwani keshapewa kadi na mtoto wako Rania na kamuomba kuwa mtu wake wa pembeni siku hio”
“Whaat! Kadabra hakikisha huyo mwana haramu hafiki kwenye hio sherehe kwa namna yoyote ile , kwani Najma atakuwa pale”
Aliongea Samir kwa kupanick kwani taarifa hii ilikuwa ni ya kushitua kweli na ni kweli kama Najma angemuona Peter kupitia sherehe hio sijui ingekuwaje .
“Sawa boss , ila sijui cha kufanya kwani muda umeenda sana bado masaa machache sana sijui namna yua kumzuia”
“Wewe mpumbavu nini? , mimi sitaki maneno ya aina hiyo,nasema hivi hakikisha huyo mwanaharamu hafiki kwenye sherehe kwa namna yoyote ile “ Aliongea Samir kwa msisitizo huku akijikuta akitetemeka kwa hofu na hasira kwani alijua kile ikinacho enda kutokea,alijikuta akikaa kitandani huku akipumua kwa nguvu , alijifikiria kwa muda na alijikuta akiinua simu yake na kuanza kutafuta jina katika majina na alipo lipata , alipiga na haikupita muda mrefu simu ilipokelewa
“Hemedi habari za saa hizi!?”
“Salama mkwe habari yako ,siku hizi hatuonani”
“ Hakuna habari nzuri wakati huu, nafikiri unafahamu kuwa Najma leo anatukio lake linaendelea hapo Serena “
“Ndio kwanini nisijue bwana Samir na wakati nina surprise kwa Rania”
“Sasa kuna tatizo , Rania kampa mwaliko Peter kufika katika shughuli hio na nafikiri unajua kuwa mwanangu kafa kaoza kwa huyo mwanaharamu”
“Hahaha.. , Samir hii ndio kwanza faida ya kuwa karibu na mimi, kwani shida kama hizi naweza kuzitatua mara moja na najua kwanini umenipigia simu hii”
“Mimi sijui faida nina chotaka huyo mpuuzi asifike kwenye hio sherehe kwa namna yoyote ile”
“limeisha hilo kuwa na Amani kabisa nishalimaliza” Aliongea Hemedi kwenye simu na kumfanya Samir ashushe pumzi kwani swala hilo aliogopa sana , alichukua simu yake na kumpigia Kadabra .
“Usijisumbe kuhusu huyo mshenzi kazi hio nimememkabizi mtu mwingine”
“Boss una uhakika?”
“Nimesema kazi hio nimempa mtu mwingine , achana nayo kwa sasa na maswali sitaki”
“Sawa boss”
*****
Peter alifika nyumbani kwake aliko kuwa nakaa na Masumbuko , maana japo alikuwa amepewa nyumba na Mama Rania lakini hakuwahi hata mara moja kwenda kulala katika nyumba ile.
“Daah ! mzee sherehe ilikuwa nzuri ile sijapata ona” Aliongea Masumbuko .
“Yeah zile ndio mahafali ya vyuo , yanakuwa makubwa kama vile”
“Kumbee!”
“Ndio”
“ Sasa mimi najiandaaa kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe nyingine usiku huu ila nimepewa kadi moja tu tungeenda wote”
“Na mimi nina enda na Nasma kuna sherehe kaniambia kuwa anakwenda na kasema niende nae”
“Kumbe mshapanga mambo yenu na Nasma tayari ?”
“Ndio” Aliongea Masumbuko huku akilisogelea sofa na kujibwaga kwani muda huo alikuwa amesimama wakati akiongea na Peter.
“Hivi Masumbuko unajua yule Nasma ni mzuri sana na nikimwanglia anavutia kweli kweli na anaonyesha dalili kabisa za kukupenda , kwanini usimtongoze?”Aliongea Peter kwani ni kweli kila alipo kuwa akimwangalia Masumbuko wakiwa na Najma kuna kitu alikuwa akikiona kwa Nasma na alionekana kumpenda sana Masumbuko .
“Wewe Peter unafikiri atanipenda yule na kunikubalia wakati nikimtognoza?”
“Ndio kwanini asikubali na wakati anaonyesha kabisa kukupenda”
“Basi nitajaribu ila sio leo wala kesho namuacha acha tu maana sijui kama atakubali kuwa na mwanaume kama mimi ambae sina akili na sijasoma”
“Wewe mwanaume ni kujiamini, nani kakwambia mapenzi yana angalia elimu , wewe ukimfata usiangalie maisha yake angalia moyo kwake na huo ndio unatakiwa kuushawishi sawa”
“Poa nitajaribu”
“Sio ujaribu fanya , sema shida kubwa inaweza ikawa kwa wazazi lakini wewe hilo usilizingatie kwanza kasema wako nje ya nchi huko”
Masumbuko alijkuta akimkubalia Peter kwa kichwa na kisha akatoka hapo na kwenda kwenye chumba chake na alivyo fika alitoa suruali yake na kuanza kuangalia kijidudu chake kilicho kuwa kama cha mtoto , alikigusa gusa kutafuta hisia za kimapenzi ila hakuna kitu , alijikuta akivaa na kutoka zake hadi sebuleni na kisha alikaa hapo na kuanza kuangalia Tv muda huo
*****
“Mom and dad huyu ni Sebastiani ni rafiki yangu” Alongea Stella siku hio alipo kuwa amejumuika katika hoteli wakipata chakula na Stella alimualika Sebastiani , na wazazi wake Stella siku hio walikuwa wamekuja kwa ajili ya mahafali ya mtoto wao.
“Shikamooni !” Alisalimia Sebastiani kwa heshima kubwa na mzee Elvice aliitikia salamu huku akimwangalia Sebastiani , huku akimsaminisha .
“Nafurahi sana kukufahamu , nilikuwa na wasi wasi na mwanngu Stela ila nadhani uwepo wako kidogo unamfanya awe anatabasamu kama anavyotabasamu leo” Aliongea mama yake Stella na kumfanya Stella amwangalie Sebastiani usoni na kisha katabasamu.
Basi walichafua meza siku hio ndani ya hoteli hio ilio kuwepo Ubungo ilio kuwa ikijulikana kwa jina la Landmark hotel , walikunywa kwa furaha sana huku wakimpatia Stella zawadi walizo zindaa kwa siku hio .
Sebastiani alijikuta akifurahi sana kwani aliona hio ilikuwa ni hatua muhimu katika harakati zake za kumpata mrembo Stella .
Wakati wanendelea kula na kunywa kwa furaha ,huku stella akionekana kuwa katika furaha sana , mara alimuona mtu ambae ni kama wanzoni alimfananisha ila alipo angalia kwa umakini alimfahamu na kufanya mapigo yake ya moyo kupiga kwa nguvu na kujikuta akiangalia sehemu ile , na kuwafanya hata wazazi wake walio kuwa wakitaniana kuangalia upande ambao Stella alikuwa akiangalia , Stella alijikuta haaminin kwani alimuona James mwanume anae mpenda akiwa na rafiki yake Lea na wala wao wakiwa hawana habarikwani hawakutambua uwepo wao hapo hotelini .
“Yule si James yule , na yule msichana ni nani? “ Aliongea mam yake Stella na kabla hajajibiwa Stellla alinyanyuka na kufata upande walio kuwepo Lea , lakini kabla hajafika aliwaona wakitoka eneo hilo na kuingia kwenye lift .
Sebastian alijikuta akiona sasa mambo yanakwenda kubumbuliuka kwa upande wa Lea na alijua kabisa kuwa siku hio urafiki wa wawili hao unakwenda kuisha siku hio , ila alicho kumbuka ni ahadi yake Lea kwake kwamba endapo Stella atamfuma mmoja wapo basi hakuna kutajana , lakini kwa Sebastiani bado hakuwa na uhakika na ndio maana hata yeye roho yake ilikuwa juu juu .
Stella hakutaka kushindwa na uzuri wa hoteli ile ulikuwa na lift , mbili kulia na kushoto , Stella alikimbilia lift za upande wa kushoto na bahati ni kwamba haikuwa na mtu mana alipo binya tu ilifunguka, na akaingia huku akisahau kabisa floor alio kua anaenda maana hakujua kuwa James na Lea walikuwa wanaelekea lift gani . .
“Naomba kisiwe kweli ninachokifikiria”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 29
Mama na baba yake Stella walijikuta kwenye mshangao kwani walikuwa hawaelewi kinacho endelea,walikua wakijua kuwa mtoto wao huyo alikuwa ashaachana na James na alikuwa akiendelea na maisha yake .
Lakini kitendo cha kumuona Stella akinyanyuka na kumfuata James wao kama watu wazima walijua kuwa sio kama Stella alikuwa ameachana na James ila ni kwamba mtoto wao alikuwa akimsubira james kurudi kwenye maisha yake .
Hawakutaka kuliamini jambo hilo moja kwa moja na walitaka walione kabisa na wajue ni kwasababu gani Stella kamfuata James , walitaka kujua kama bado mtoto huyo alikuwa akiendelea kumpenda James na alikuwa akiweka tabasamu la uongo mbele yao wakati ndani anaumia, walikuwa washasau nguvu ya mapenzi.
Sebastiani alijikuta akiwa hajui cha kufanya na aliangalia wazazi wake Stella wakinyanyuka na kutoka eneo hilo wakifuata uelekeo wa Stella .
Stella alijikuta mwenye hasira , kwanza roho yake ilikuwa ikimuambia kuwa Lea na James ni wapenzi na walikuwa wakimzunguka , wakati akiwa kwenye lift hio , kuna muda alitamani hata isiwe kweli, kuwa rafiki yake alikuwa akimzunguka kwani alikuwa akimuamini sana Lea na alikuwa akimchukulia zaidi ya rafiki ..
Alijikuta akiwa juu kabisa floou namba nane ya hoteli hio na kiufupi ni kwamba alipo ingia ndani ya floor hio aliotea tu namba ya kwenda na alibonyeza .
Alijikuta akijiona mjinga kwani floor hio ilikuwa kimya kabisa , alijikuta akiingia kwenye lift tena na kushuka hadi chini na moja kwa moja elienda mapokezi.
“Dada samahani kuna ndugu zangu wameingia sasa hivi naomba kujua wameingia chumba gani ?”
“Samahani unazungumziwa watu gani hao ?“
“Wamengia sasa hivi nataka kujua wameingia chumba gani ni mdada na mkaka mrefu hivi maji ya kunde , angali jina anaitwa James na Lea “ Aliongea Stella huku akihema kama alikuwa akikimbizwa .
Muhudumu yule alimwangalia usoni na kisha kurudisha macho katika tarakishi yake .
“Siwezi kutoa taarifa za wateja wetu labda nipate kibali kutoka kwao nitajie jina lako niwailize na kama watakuruhusu ndipo na mimi nitakuruhusu kuonana nao”Aliongea muhudumu yule wa kike alievalia kinadhifu kabisa huku akimwagalia Stella .
“Stella kuna nini ?”Ilisikika sauti ya baba yake Stella ikiuliza swali hilo .
“James baba” aliongea Stella huku machozi yakiwa yashaanza kumtoka kwani alijihisi maumivu makali na wakti huo na Sebastiani alifika eneo hilo .
“James kafanyaje na anakuhusu nini mwanangu si msha achana na kila mtu ana maish yake kwa sasa “ aliongea baba yake stell na wakti huo , wakiwa wamesimama katika eneo hilo , alikuja mwanaume akiwa amevalia suti
“Dada za saa hizi naenda chumba namba 201 nina miadi na Lea Edward “ Aliongea mwanaume huyo kwa sauti kiasi kwamba utadhani alikuwa akitaka asikike na kumfanya stela aliekuwa ameinamisha kichwam chini kunyanyua uso wake na kumwanglia mwanaume huyo ambae aliruhusiwa na dada yule wa mapokezi baada ya kupiga simu na hapo ndipo Stella kama alikuwa kichaa vile alimfuata mwanume yule kwa nyuma na aliopo ingia na kubonyeza namba na Stella na yeye alikuwa ameshazama ndani ya lift hio na wala mwanaume yule aliekuwa amevaa miwani hakumwongelesha huku akionekana yuko siriasi kabisa na alikuwa akitafuna bublish.
Huku wazazi wa Stella walijikuta wakishangaa uchizi wa mapenzi ya mwana wao . Na sebastiani alikuwa ni kama ana angalia filamu kwani hakusema chochote Zaidi ya kuangalia kinacho endelea.
Stella alimfatisha mwanaume yule mpaka alipo simama kwenye chumba cha namba 201 .
“Dada kumbe tunaelekea chumba kimoja “” Aliongea mwanume yule huku akimwangalia Stella .
“Ndio nina shida na mtu wa chumba hiki “ Aliongea Stella na hapo jamaa yule wala hakutaka maneno mengi maana aligonga mlango na hapo ndipo Lea alipo fungua mlango ule .
“Mpenzi wangu kizibo haaa..! shost”Aliongea Lea huku Stella wala hakutaka kuongea mengi aliingia moja kwa moja mpka ndani na kuanza kutafuta .
“Lea! , James yuko wapi?” Aliuliza Stela
“James ?. atakuwa kwenye chumba chake niliachana nae kwenye lift” Aliongea Lea kwa kujiamini kabisa.
“Namba ngapi yupo natak kuonana nae?”
“Shost punguza hizo hasira kwanza unanifanya hata naogopa kukuambia”
“Lea tutaongea vizuri baadae naomba uniambie kwanza yupo chumba namba ngapi ?”
“Namba 320 floour ya nane”
Stella hakusubiri maelezo mengine alitoka nje ya chumba hicho na kisha kukimbilia kwenye lift , huku akikutana na wazazi wake na Sebastiani na walivyo muona akiingia kwenye lift hio na ilibidi wamshike Stella lakini ni kama mbogo vile , alibonyeza namba nane na kisha lift haikuchukua muda mrefu ikafunguka na wakwanza kutoka alikuwa Stella aliefuata alikuwa ni mama yake Stella akifuatiwa na baba yake na Sebastiani .
Stella aligonga mlango na hapo ndipo mwanamke mmoja mrembo alievalia khanga moja alitoka .
“Niwasaidie nini ?”
****
Peter ndani ya muda mfupi alikuwa tayari amesha maliza kujiandaa na alicho kuwa akingojea ni simu ya Rania tu kuita ili aianze safari ya kwenda kukutana nae kwa jili ya kuelekea ukumbini .
Alikaa na wakati huo na Masumbuko alitokea sebleni hapo akiwa amependeza kweli na kiufupi siku hizi chache ambazo masumbuko alikuwa amekaa dara , alikuwa akijua sana kuujali mwili wake kwani alikua anajua kujihudumia kweli , kwani suti alio kuwa mevaa masumbuko alikuwa imempendeza kweli .
“Wewe jamaaa hio suti mbona kama sikumbuki kama nilikupa mimi na sina suti kama hio kwenye kabati langu” Aliongea Peter kwani suti alio kuwa amevaa Masumbuko ilikuwa imkemkaa vyema lakini kingine ni kwamba ilionekana kuwa ya thamani kweli .
“ Nasma huyo broo” Aliongea Masumbuko na kumfanya Peter atingishe kichwa na kuona kweli Masumbuko alikuwa ni bonge la handsome kwani muonekano wake ulikuwa wakipekee sana.
“ Kweli mzee baba una bahati sana si kwa kupendezeshwa huko” Aliongea Peter na wakati huo simu yake ilitoa mlio kuwa ilikuwa ikiita na alipo angali jina aliona ni la Rania alipokea simu hio na kuweka sikioni na kisha akaitoa .
“Masumbuko tutaonana baadae mimi nelekea kwenye sherehe wasalimie huko”
“Poa Peter hata mimi nelekea kwenye sherehe wasalimie huko” Aliongea Masumbuko huku akimwigilizia peter na nikwamba hawakujua kuwa wanaenda sehemu moja .
Masumbuko na yeye hakukaa sana alienda kufungua mlango kwani kulikuwa kuna mtu alikuwa akigonga.
Ukisikia kuna wanawake ambao Mungu kawaajalia uzuri basi siku hio ungesema kuwa mrembo Nasma alikuwa ni moja ya kundi hilo la wanawake ambao wamejaliwa uzuri , japo kila mwanamke anakuwa na uzuri wake ambao unamfanya mwanume kumpenda , lakini kuna uzuri mwingine unakuwa ktika macho ya watu wote namaanish ule uzuri wa kuvutia sana pale tu unapo mwangalia mwanamke .
Nasma siku hio alikuwa amependeza kiasi kwamba hata Masumbuko ambae alikuwa hajui sana maswala ya wanawake aljikuta akitamka maneno ya kupendeza mbele ya mrembo Nasma .
“Umependeza kama malaika” Aliongea Masumbuko baada ya kumfungulia Nasma
“Asante Masu” Aliongea huku akifupisha maneno ya jina la Masumbuko na akiachia tabasamu ambalo kwa mwanume rijali lingempa presha ya ghafla sio Masumbuko ambae hana hata uwezo wa kusoma channeli .
“Hata wewe umepemndeza hakika ,nilijua kukupatia katika hio suti” Aliongea Nasma huku akimsogelea Masumbuko na kumuweka sawa masumbuko suti yake .
“Mimi napendeza sana nilikuwa nakosa matunzo tu”
“Hahahaha… Masumbuko huishiwi vituko na ndio maana kila siku nazidi kukupenda”
“Unasema !”
“Masumbuko twende buana tunachelewa ujue”
“PSoa twende “ Aliognea Masumbuko huku akipotezea lile neno ambalo aliliskia likitoka kabisa kwenye mdomo wa Nasma .
Basi walitoka huku wakiwa wamependezana na hata Lucy alipo waona alijikuta akitingisha kichwa na kukubali kuwa Masumbuko alikuwa ni bonge la HB.
Basi Lucy aliwafungulia mlango mabosi zake hao kwani hata Masumbuko wakti huo alikuwa akimuona kama boss.
****.
Ukumbi ulikuwa umependeza sana kiasi kwamba kwa ambae angeuona angejua kuwa siku hio kumetumika hela nyingi sana katika upambaji wa ukumbi huo.
Watu wengi wakiwemo wasanii wakubwa walionekan wakiwa wamependeza kisawaswa sawa huku wengine wakiwa na wenza wao .
Na kila anae kuwa akiiingia ndani ya ukumbi huo alikuwa ni lazima kupitia kwenye Red Carpert kwanza ,kufotolewa mapicha picha .
Moja ya wana mitindo walio hudhuria katika tukio hilo alikuwa ni mwanamitindo maarfu sana ajulikanae kwa jina la Queena , mwana mitindo kutoka Marekani na siku hio alikuwa amealikwa katika tukio hilo kama mgeni maalumu katika siku hio , kwani mwandada huyo alikuwa na heshima kubwa ndani ya taifa la Tanzania .
Siku hio alikuwa kapendeza kweli na waandishi wahabari walionekana kumuulizamaswali mengi ndani ya Red Carpet .

UNAWEZA PATA SOFTCOPY YA SIMULIZI HII SEASON 1 YOTE KWA MALIPO YA 1500 TU
LIPA : AIRTEL MONEY -0687151346 ISSAI SINGANO

SIMULZI ZANGU NYINGINE NI
-UMOJA NAMBA TISINI NA SABA
-NDOTO ZA KIKANUNI
-BOOK OF ALL NAMES (UMOJA NAMBA TISINI NA SABA )
-MY DREAM MY FAVOURITES)

mawasiliano 0687151346 WATSAPP
 
SEHEMU YA 30
“Ni wasadie nini” Hilo ni sauti ilio toka kwa bidada huyo aliekuwa amesimama hapo mlangoni , akiuliza swali ambalo lilimfanya Stela kumsukuma na kuingia ndani na alijikuta haamini kwani alimkuta James akiwa kifua tupu huku akiwa amevalia bukta tu akiwa amekaa kitandani huku akiwa maeshikilia glass ilio kuwa imejaa wine .
“James!” Aliita Stella huku machozi yakiwa yana mtoka mfululizo kwani moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kiasi kwamba alikuwa hana hata uwezo wa kuzuia machozi yale yasimtoke .
“Stella , umekuja kufanya nini hapa ?”
“James kwanini hivi lakini James , huoni ni kwa jinsi gani nakupenda James , kwanini unanifanyia hivi James kwanini unaufanya moyo wangu kuuma kiasi hiki eh , kwanini James” Aliongea Stella huku akiwa amekaa kabisa kwenye sakafu akilia .
“James niambie kwanini hutaki kunisikiliza , ni kosa gani hilo ambalo halisameheki James mpaka unaniacha kwenye machungu namna hii James why James”
“Stella sina sababu ya kukusikiliza , naomaba nikwambie tu ukweli sikukupenda Stella nimedumu na wewe kimazoea sio kihisia naomba unisamehe juu ya hilo , kwani nililkuwa natafuta njia ya kukuacha Stella , lakioni hata kama sikukupenda Stella nilikuwa nakuheshimu lakini kwa lile ulilofanya sitokusamehe na sitoweza kuishi na mwanmke mchafu kama wewe” Maneno hayo makali yalimtoka James bila hata woga na yakaenda kutua katika masikio ya Stella .
“James naomba unisikilize James nakuomba usinihukumu kabla haujaujua ukweli James , nakupenda James kwanini hivi lakini”
Ilikuwa nihali ya kuhuzunisha sana aliokuwa nayo Stella , hata Sebastiani alie kuwa moja ya mkandarasi ,alijikuta akimuonea sana huruma Stella kwani hakudhania kuwa Stella alikuwa na mapenzi makubwa kwa Jamesnamnaya kumlilia kiasi hicho .
Wazazi wake walijikuta wakijizuia kutotoa machozi kiutu uzima ila mioyo yao ilikuwa ikiungua , kwani hawakutarajia kuwa mwana wao huyo alikuwa akiishi na maumivu ndani ya moyo wake kwa kiasi hiko , mama yake Stella alijikuta chozi likimtoka , kwa jinsi alivyo kuwa akimuona Stella analia alijua nikwakiasi gani mwanae alikuwa akiumia..
Baba yake na Stella aliishia kumuangalia James kwa hasira na kisha alimsogelea Stella na kumkokota nje .
“James utakuja kunikumbuka James , utakuja kujutia siku hii ya leo na kuikumbuka katika maish yako yote James” Aliongea Stella na James wala hakuwa hata na habari Zaidi ya kuchukua glass yake ilio kuwa na wine kidogo na kuinywa mpaka ikamalizika na hapo hapo alitupa chupa ukutani kwa hasira.
*****
Tukirudi nyuma Sebastiani baada ya kumuona Stella akiingia kwenye lift na wazazi wake walivyo fuatia , alitoa simu yake haraka haraka na kish alipiga namba ya Lea na bahati nzuri ni kwamba ilipokelewa hapo hapo na alimwambia kuwa Stella kawaona kwa hio aangalie cha kufanya .
Ndani ya chumba cha Lea ambae alikuwa ameshikiliwa kiuno na James alipo maliza kuongea na simu alimgeukia haraka James na kumwambia kuwa Stella anakuja na katuona .
James alijikuta akipatwa nakiwewe na pia kwa lea hivyo hivyo na hapo hapo akili ya Lea ilifanya kazi haraka haraka na kumwambia james wanatakiwa kufanya jambo , na James alitingisha kichwa ila hakuona ni kwa jinsi gani wanatakiwa kukamiliaha jambo hilo .
Ndipo Lea alipo pata wazo na James na yeye aliona wazo hilo ni bora na ndipo alipo piga simu na kisha alitoka haraka haraka kwenye chumba hicho akimuacha Lea na wakati huo ndio alipo ikimbilia ;lift m na aliona kabisa kuna watu walikuwa wakipanda na lift hio na ndipo alipo pita kwa njia ya ngazi mpaka chumba cha bodigadi wake ambaco alikuwa amechukua yeye na mpenzi wake na bodigadi wake alimpigia simu na kumwambia jinsi ya kufanya na ndie alie kuwa pale mapokezi na kutaja jina la Lea kwa nguvu na kumfanya Stella ajue mwanaume huyo alikuwa akielekea kwenye chumba chao na pale ndipo alipo mfata kwa nyuma.
Huo ndio mchezo alio kuwa ameucheza Lea ili kutokamatwa na Stella , kwani mwanume yule aliemwita kizibo hata hakuwa akiitwa kizibo ila ni jina alilo kija nalo Lea ili tu kujikomboa katika kufumaniwa kwani hakutaka kumpa maumivu mara mbili Stela , japo alijua siku moja Stella atakuja kuujua ukweli , lakini aliona huo haukuwa wakati sahihi kwa stella kufahamu kia kitu
*****
“Kijana hebu njooo mara moja tuongee” Baba yake Stella aliongea akimwambia Sebastiani baada ya kumpandisha Stella kwenye gari .
“Ndio mzee wangu”
“Hivi unajua kinacho endelea hata kidogo tu nipate kujua”
“yeah mzee ni kwamba...” Alijifikiria huku akijiuliza amwambie .
“Ni kwamba nini hebu niambie ni nini kinaendelea , kwanini Stella anasema anataka kusikilizwa”
“Mzee kiukweli ni kwamba Stella siku ile alifanyiwa kama kupewa kumbukumbu”
“kumbukumbu!?”
“Ndio kumbukumbu za masaa mawili”
“Unanichanganya hebu niambie vizuri”
“Mzee sijui nikuelezeje, ila huo ndio ukweli ni kwamba Stella hakufanya kitendo kile makusudi chakumsaliti James ila ni kwamba alibadilishwa akili yake , kama uchawi”
“Kijana hebu weka mambo yanyooke , unamaanisha kuwa stella alirogwa?”
“Ndio mzee alirogwa kwa masaa mawili” Aliongea Sebastian huku akionekana kutojiamini kabisa kwani alionekana kutetemeka .
“Kwa hio ni kama kabakwa si ndio ?”
“Ndio baba”
“Unamjua alie mbaka?”
“Hapana...,ndio mzee”
“Jibu swali moja unamjua alie mbaka mwanangu nakuuliza wewe mpuuzi” Mzee alibadalika ghafla na kuwafanya hata walio kuwa kwenye gari watoke .
“Mume wangu kuna nini tena mbona mko hivyo”
“Hakuna kitu mke wangu” Aliongea huku akitoka eneo hilo na gari kuwasha moto huku Sebastiani akiingiza mkono wake kwenye shati lake huku akihema kwa nguvu na kutoa kikadi hicho alichopewa na mzee Elvice .
Alijikuta akipumua kwa nguvu na kushika magoti .
*****
Peter wakati akitoka ndani ya nyumba yao aliendesha gari kuelekea Mwenge kwa spidi ya kawaida , huku akiwasiliana na rania sehemu ya kukutania kwani walikuwa wakihitajika kuingia wote ndani ya hoteli hio .
Peter hakuwa na habari aliendesha gari yake huku akiongeza spidi kila baada ya dakika kwani muda ni kama ulikuwa umeenda sana .
Lakini wakati anendesha gari yake alikuwa akihisi kitu sio cha kawaida katika gari yake na wakati huo ndio wakati alikuwa akipita ITV na alikuwa kikaribia kituo kinachoitwa sanyansi nyuma kidogo na jingo lefu la LAPF.
Hapo ndipo alipojikuta akisikia mtikisiko wa gari lake na kujikuta akiyumba na kwakuwa alikuwa mjanja alijitahidi na kuliegesha pembeni kidogo na kituo hicho katika eneo hilo kukiwa na maua na miti miti ilionekana kama bustani.
Peter alishuka kwenye gari yake na kuzunguka upande wa kulia ambako ndiko gari yake ilikuwa imelemea na wakati akizunguka ndipo simu yake ilianza kuita na aliipokea huku akiliinamia gari na kujikuta akishangaa kwani tairi ya mbele ilikuwa haina upepo kabisa na aliangalia chini kwa umakini aliona kitu kama kijimsumari kikiwa kimeichoma taili hio .
Wakti akiendelea kushangaa taili yake ya gari huku akiongea na Rania na hapo hapo sijui kibaka alitokea wapi kwani simu yake ilikwapuliwa na kijana mmoja aliekuwa amevaa helmeti akiwa kwenye pikipiki .
Sasa wakti akinyanyuka huku akijikuta akipanua mdomo na kuangalia pikipiki ile ikitokomea , hapo ndipo alipo jikuta akilia kama mtoto kwani , ghafla kulipita gari kama ya zima moto na kutoa maji kama mvua na kumwagikia pita na hapo ndipo Peter alijikuta akiwashwa balaa na gari ile nayo ilikuwa ikipotea katika eneo hilo.
Baadhi ya watu walijikuta wakimuangalia huku wakiendelea na mishe zao , na bahati nzuri ni kwamba katika eneo hilo hakukuwa na watu wengi .
Lakini ghafra gari ilisimama pembeni yake na kufunga breki .
*****
Kwa hio biss unasema tutawazuia vipi” Aliongea Ramso baada ya Hemedi kupokea simu kutoka kwa Samir ..
“Ramso hebu fikiria kidogo bhana kwanini tushindwe kumzuia , tumefanya kazi nyingi za kimagendo na kupitisha madawa ya kulevya tushindwe na hili dogo”
“Ni kweli boss lakini muda , limebaki lisaa tu kwa wao kukutana na Rania”
“Una maanisha nini kukutana na Rania , Ramso utaniboa sasa hivi , usimtaje Rania ukimuhusiha na huyo boya maana roho yangu hapa naona kama itanipasuka kwa maumivu ya huyu boya kuwa namazoea na Rania”
“ sawa biss samahani “
“Mwite mzee wa mipango aje haraka hapa najua hashindwi kitu” Alikuja kijana mmoja alie kuwa akionekana mwembamba sana huku akiwa mrefu na alikuwa na miwani akiwa amevalia tisheti yake ya Levi.
“Derick una lisaa limoja tu la kumzuia mtu asifike Serena hoteli , nataka ndani ya hilo lisaa ufikirie ni kwa nammna gani tunaweza kumzuia “ Aliongea Hemedi kwamsisitizo na kumfanya Derick kushangaa kwani hizo ni dakika chache sana kwa yeye kufikiria wazo na kulifanyia kazi .

SEHEMU YA 31

“ Boss jambo hili siwezi kulifanya mwenyewe lazima wote tulifanyie kazi “
“ Kivipi derick mimi nataka kuondoka sasa hivi “
“Najua”
“Sasa kama wajua”
“Nina hitaji koneksheni na mtu wa gari la kutuliza ghasia la maji ya washawasha”
Unasemaje Derick , hayo maji yanahusika vipi Derick ,wewe nipe mpango wa kumuzia huyo mwanaharamu , na mimi ilikumpata Rania lazima swala hili lifanikiwe .
“Huo ndio mpango wenyewe sasa” Aliongea Derick na kumfanya Hemedi amwangalie Derick na kurudi kukaa katika kiti chake na Ramso mwenyewe akakaa kusikiliza mpango wa derick unakwendaje .
“Nimeshakuwa na idea tayari ambayo itamzuia yeye kufika katika tukio hilo na kukamilisha hilo tunahitaji vitu viwili vya haraka sana gari la maji ya washawasha na Tranguilizer gun ( hii ni bunduki ambayo hutumika kwa wanyama pori katika kuwapiga sindano na kuwafanya walale kama pale wanapo hitajika kufanyiwa matibabu ) na Hemedi alikuwa nayo kwani alikuwa pia na biashara za meno ya tembo na pia alikuwa akikamata wanyama kisiri siri na kuwasafirisha
“Hio bunduki tunayo ila hilo gari la maji ya washawasha hatuwezi pata”
“Boss umesahau kuwa hapa tupo na ghala la Police ?”
“Una akili sana Derick na ndio maana nakuaminia una maanisha kituo cha Police cha Osterbay “
“Ndio”
“Hilo gari lishapatikana ngoja nimpigie Sajenti Nuru pale Satatupatia”
Na hapo hapo Hemedi alitoa simu yake na kumpigia Sajent Nuru na alijikuta akitabasamu baada ya kushusha simu yake
“Anasema lipo , pesa inaongea bwana , ila nasema kama ni kwa njia ya uhalifu hatotoa”
“Hio sio njia ya uhalifu”Aliongea Derick “Haya tupe huo mpango wako”
“Kwaharaka haraka ni kwamba huyu Peter anakaa Mbezi Beach na hana ujanja wa kupitia njia nyingine kwenda Serena zaidi ya Mwenge , hatopitia kawe kwasababu ni kinyume ,na hilo lazima tufanye apitie njia ya Mwenge ,ila nina uhakika asilimia tisini , sasa inabidi tumtengezee pancha ya tairi la kulia na lazima ataegesha gari pembeni baada ya gari kupata pancha “
“Sasa pancha tutamtengenezeaje ?”
“tutatumia trangulizer gun na kazi hio ataifanya Ramso kwani najua ana shabaha sana na anacho takiwa ni kuilenga taili ya mbele na zoezi hilo anatakiwa kulifanyia pale kwenye kampuni ya Shelys mbele kidogo na ITV upande wa kulia na hilo atajua mwenyewe jinsi ya kufanya na najua kafanya kazi nyingi kama hizi .
“Na baada ya hapo nini tena “
“ lazima atasimamisha gari katika kituo cha sayansi kwani hana chaguo lingine au karibu na hapo kwani tairi itakuwa imeisha upepo na hapo inatakiwa asipige simu kuomba msaada na kwa maana hio lazima tumuweke mtaalamu wa kukwapua.
“Una maanisha Lenard afanye hio kazi ?”
“Ndio boss”
“Watu wawili wanatakiwa kwenda kuchukua maji ya washawasha na kisha wahakikishe wanalitega bomba la maji ya mvua litoe maji kumwagia , na kama linafanya makosa mara moja tu wakishamuona Peter sehemu alio egesha gari na wahakikishe gari isisimame na ionekane ni kama makosa tu.
“ Na hapo ndipo tutamaliza mchezo “
“Hahaha .. kazi na ianze nimeukubali huo mpango “
“Ila Derick na wewe hjujasema kazi yako utafanya nin ?”
“Mimi ndio nitamalizia kila kitu “
*****
Rania alijikuta akiwa kwenye hali wasiwasi kwani simu ya Peter haikupatikana kila alipokuwa akipiga jambo ambalo lilimpa wasiwasi mwingi sana na wakati huo watu walikuwa wakiendelea kuingia na muda ulikuwa umeenda sana.
Wakati akiwa amesimama nje ya hoteli hio akiangalia kama atamuona Peter ndipo wakati wa gari iliowabeba Masumbuko na Nasma likifka ndani ya hoteli hio ndani kabisa na kwenda kuegeshwa na hapo ndipo Msasumbuko na nasma walivyo toka katika gari hilo kila mmoja upanmde wake ,walikuwa wamependeza sana sio Masumbiuko Saio nasma .
“ Lucy sitaki kupitia katika Red Carpet na kuhojiwa” Aliongea Nasma baada ya kusoge ambele kabisa na mlango wa kuingilia .
Masumbuko yeye alikuwa akishangaa maana hio ndio mara yake ya kwanza katika maisha yake kuhudhuria matukio makubwa kama hayo , tena matukio ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa na kiingilio kikubwa sana na hata wahudhuriaji wake wakiwa watu maarufu na watu ambao walikuwa na pesa zao ..
“Hakuna shida Nasma tunaweza kupita kuna uwezekanao wa kuingia bila kuhojiwa na waandishi ama kupigwa picha” Aliongea Lucy na Nasma alitingisha kichwa na Masumbuko alishikiliwa na Nasma na kisha waliingia ndani ya ukumbi huo huku wakionekana kupendeza sana . .
Hapo ndipo Masumbuko alivyo jikuta akishangaa zaidi kwani kila kitu kilikuwa kigeni kwake , kwanzia vinywaji na kila kitu kilicho kuwa kipo katika eneo hilo alikuwa hajawahi kukiona , alijikuta akifurahi na uzuri ni kwamba Nasma hakutoka pembeni ya Masumbuko .
Huku nje Rania aliwaona Nasma wakiingia lakini hata akili yake haikuwajali kabisa kwani alicho kuwa akijali wakati huo ni Peter tu,alikuwa kwenye wasiwasi mkubwa hasa pale alipo mwambia kuwa gari yake imepata hitilafu na hapo hapo kabla hawajaelewana ndipo mawasiliano yakakatika , jambo hilo lilimfanya kuwa katika wakati mgumu na kujawa na wasiwasi mwingi sana
“Rania!”
Aliita Samir akiwa yupo nje ya kabisa akiwa katika maegesho ya magari na alionekan kuna simu muhimu aliokuwa akipokea .
“Mbona umesimama hapa na wakati tukio limeanza mtoto wangu twende ndani au kuna mtu unamsubiria ?”
“Aaa.. ndio dadi kuna mtu niliahidiana nae atakuwa my plus one lakini mpaka sasa hajafika na mara ya mwisho aliniambia gari yake imepata hitilafu na mawasiliano yake yamepotea
“Atakuwa salama my daughter hauna haja ya kumsubiria kwani kama gari yake itakuwa imepata hitilafu nadhani anaweza asifike kabisa na ,muda kama unavyo ona umeenda sana twende ndani”
Rania alikubali kinyonge sana na kisha akaungana na baba yake a wakaingia ndani .
Ndani ya ukumbi tukio lilikuwa likiendelea na waburudishaji walioalikwa kutoa burudani siku hio walikuwa stejini, msanii aliekuwa amealikuwa katika tukio hilo na wakati hio alikuwa akitoa burudani alikuwa ni Ommy dimpoz. ******
“Kaka pole sana ingia kwenye gari nikupeleke kweenye hoteli ya karibu ukaoge na kuvua hizo nguo” Huyu alikuwa ni Derick aliepanga mpango mzima wa kumzuia Peter asiende katika tukio la ufunguzi wa kampuni ya Najma.
“Nashukuru lakini siwezi kuacha gari hapa” Alizungumza Peter huku akiwa anajikuna .na hata zile nguo ambazo zilikuwa zimempendeza zilikuwa zimekwisha kupoteza mvuto.
“Funga gari hio bro hayo maji yalio kuwamgikia ni hatari sana hayawezi kuisha makali yake mpaka uoge”
Peter alijkuta akimwangalia yule mshikaji na kisha akalisogelea gari lake haraka haraka huku mwili ukiwa unamuwasha na alitamani hata avue nguo , kijana Derick alikuwa akitabasamu moyoni kuona mpango wake umefanikiwa kwa asilimia mia moja alijikuta akijihisi mtu mmoja mtata sana na mwenye akili sana tena katika upangaji wa mawazo kwani alitumia muda mchache sana katika kupanga mpango wake na kuja kufanikiwa bila tatizo lolote .
Peter alipelekwa mpaka kwenye hoteli ilioko upande wa kulia nyuma kidogo na ITV hoteli ifahamikayo kwa jina la Kebbys, Derick alionekana kabisa alikuwa na chumba ndani ya hio hoteli kwani ile anaingia tu alichukua kadi yake na kisha akaongozana na Peter.
“Pole sana broo” Aliongea Derick baada ya Peter kutoka bafuni huku akijihisi mwili wake kuwa sawa na hakuhisi muwasho tena.
“Daah! Asante”
“Niliona wakati gari la police lilipo kumwagikiamaji nilikuwa pale pale nikiwa na nunua miche ya maua “
“Daah! wale wajinga sana , yaani hata sielewi ni bahati mbaya au ilikuwa makusudi wameniharibia kabisa mipango yangu ya leo ya kuhudhuria tukio maana saivi nimechelewa kabisa na siwezi kwenda tena na isitoshe simu yangu imeibiwa pia “ Aliongea Peter .
Basi Peter hakuwa na jinsi tena alikubali kuwa siku hio hawezi kutimiza miadi ya kukutana na Rania kwa ajili ya kuhudhuria tukio ambalo alimuahidi kuwa atahudhuria.
****
Baba yake Stella hawakutaka kumuacha mtoto wao katika hali alio kuwa nayo , walimuonea sana huruma kwa mambo yote alio kuwa akiyapitaia kwani walikuwa wakielewa kabisa mapenzi yalivyo kuwa yanauma na waliielewa hali alio kuwa nayo Stella kwa wakati huo .
Waliendesha gari mpaka katika nyumba ambayo Stella alikuwa amepanga waliingiza gari na kisha kwenda kuliegesha na kutoka.
“Nyumba hii ni nzuri sana, ina mazingira ya kuvutia kweli” Aliongea baba yake Stella ama mzee Elvice .
Huku wakiongozwa na Stella na kuingia ndani ya nyumba hio yenye ghorofa mbili kwenda juu lakini ile wanaingia ndipo uso kwa uso walijikuta wakikutana na mwanume alie kuwa akiishi ndani ya nyumba hio .
“Dokta singano!” Aliita mzee Elvice kwa mshangao. .
“Shikamoo mzee” Alisalimia Dokta Singano kwa heshima na wakati huo Stella na mama yake walikuwa washapita eneo hilo na mzee Elivice alie kuwa nyuma ndie aliemuona Singano peke yake .
“Kumbe unaishi hapa dokta ni siku nyingi sana tokea ulipotoka mwanza”
“Ndio naishi hapa japo nilikuwa nimesafiri kimasomo ila ndio nimerudi”
“Ndoo maana umeongezeaka kidogo , vipi tunaweza kuongea kidogo”
Singano na mzee alvice walikuwa wakifahamiana sana hii ni kipindi ambacho kijana singano alikuwa katika mafunzo kwa vitendo(intern) katika hospitali ya Bugando Mwanza , ndipo alipottokea bahati ya kutana na mzzee Elvice katika harakati za matibabu na Mzee Elvice alitokea sana kumpenda sana Singano hata kutamani moja ya watoto wake aolewe na Singano ,kwani kwa miaka kadhaa aliokuwa amefahamiana na Sngano ,alimfahamu kama kijana mchapa kazi mwenye heshima na Utu ndani yake , hata siku ambayo Singano alimwaga Mzee Elvice baada ya kumaliza elimu yake ya vitendo ,kwa mzee huyo ilikuwa ni huzuni kwani alikuwa akimpenda sana kijana Singano
“Unaishi sehemu nzuri sana , na wewe umepanga hapa?”
“Hapana hii ni nyumba yangu”
“Umejitahidi sana kijana ni nyumba kubwa sana hongera sana bwana Singano”
“Asante sana”
“ Sasa nilitaka niongeee mambo mawili matatu na wewe”
“Ndio mzee”
“Kwanza nadhani hujafahamu kuwa alieko juu ni mwanangu wa mwisho anaitwa Stella ni mwanfunzi anaemaliza chuo katika sheria”
“Kumbe!”
“Ndio lakini sasa hivi yuko kwenye hali mbaya sana na mitihani yake ipo karibu sasa ninacho taka unisaidie kupitia taaluma yako ya udaktari kumuweka sawa ili asije akaharibu katika mtihani wake ambao unafanyika hivi karibuni . aliongea Mzee Elvice na kumfanya Dokta Singano amwangalie na kufikiria kwa wakati mmoja .
“Sawa mzee wangu kwakuwa ni wewe nitakusadia katika hilo kwani kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya kwani nimepata uhadhiri katika chuo cha muhimbili”.
“Kumbe! hongera sana ni moja ya nafasi Nnzuri sana kufundisha vijana wenzio”
“Ndio ni nafasi nzuri na ndio inayo nifanya niwe bize sana na ratiba zangu kuibanana sana , lakini huhusu swala la binti yako nadhani lipo ndani uwezo yangu na uzuri ni kwamba yupo hapa hapa”
Basi mzee Elvice aliagana na Singano kwa kupeana mikono na kisha kila mtu akielekea kwenye sherehe ya ufunguzi wa kampuni ya Najma , lakini akiweka ahadi kwa mzee Elvice kumsadia Stella kurudi katika hali yake ya kawaida.
ITAENDELEA KESHO
SIMULIZI UNAWEZA KUIPATA KWA 2500 TU
******
✓PATA SIMULIZI YA KIJASUSI YA BOOK OF ALL NAMES KWA 5000/= SOFTCOPY

✓PATA SIMULIZI YA KIJASUSI YA UMOJA NAMBA TISINI NA SABA KWA 2500/= TU

✓PATA SIMULIZI YA MAPENZI MY DREAM MY FAVOURITE KWA 2500/=

NAMBA ZA MALIPO NI: 0687151346 AIRTEL MONEY AU 0657195492 TIGOPESA AU 0623367345 HALOPESA –JINA ISSAI SINGANO
UKISHALIPA NITAFUTE KWA NAMBA 0687151346 WATSAPP

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…