SEHEMU YA 28
Peter alimwangalia tajiri Samir na tajir Samir alimwangalia Peter na wote walijikuta wakiangaliana kwa macho ya hasira sana , na alie kuja kukatiza ni Rania kwani alimfuata Peter na kumkumbatia huku na Mama Rania na yeye akimkubatia Peter na kumpa hongera zake , kwa Samir aliwaangalia tu mke wake na Rania alijikuta hasira na chuki za waziwazi zikimpanda na kwa Mama Rania kuna kitu alikigundua juu ya Peter na Samir lakini alimezea mate.
“Hongera sana Peter kwa kuwa mwanafunzi bora katika sayansi am so proud of you “Aliongea Mama Rania .
“Asante sana” Huku wakiweka maigizo mbele ya Rania na Samir na haikujulikana wakati huo Masumbuko ,Nasma na Najma walikuwa upande gani kwani wao hawakuwepo eneo hilo.
“Vipi wazazi wako wamekuja tusalimiane nao?” Aliuliza Rania na kumfanya Peter awe mnyonge huku akifikiria jibu la kuwapa na Rania siku zote hakufahamu kama Peter alikuwa yatima.
“Tupo hapa” Ilisikika sauti ya kike na kuwafanya wote wageuke na kuangalia sauti ilikotokea .
“Haa! Aunt Grace, baba mdogo Gift” Aliongea Rania huku akiwakumbatia .
“ Kaka za siku !” Alisalimia Gift akimsalimia Samir .
“Salama Tu” Alijibu huku akiondoka eneo hilo na hata haikueleweka kwanini aliondoka maana walio kuwa mbele yake walikuwa ni ndugu zake tena wadamu , kwani Grace , Gift , Samir ,Profesa Gladness walikuwa wanazaliwa na baba mmoja japo mama tofauti tofauti(Soma: My dream my favourite).
“Peter my boy njoo unikumbatie” Aliongea Gift na Peter alimsogelea Gift na kisha kumkumbatia , huku akihamia kwa Grace, Rania alikuwa akimwangalia Peter na kuna jambo aliliwaza kwa wakati huo .
“Shemeji sisi tumekuja kwa ajili ya Peter leo kumwakilisha Profesa kwani kabanwa na majukumu na kasema hatoweza kuhudhuria , ila pia tumembebea Rania zawadi uncle wangu ”Aliongea Grace.
Basi familia ile ilijumuika kwa kupiga picha za hapa na pale huku Mama Rania akipiga picha na Peter naMama Rania kila alipo kuwa akimwangalia Peter usoni alikuwa akipata hisia za kufanya mapenzi.
“Peter hii ni kadi yako naomba uongozane na mimi leo kwenye tukio la ufunguzi wa kampuni ya mdogo wangu nataka uwe my plus one”Aliongea Rania wakati wakiagana na Peter.
Peter aliingalia ile kadi baada ya kuichukua katika mikono ya Rania na kisha aliitikia kwa kichwa kuwa atahudhuria katika tukio hilo .
Basi hatimae sherehe iliisha na watu walitawanyika na kurudi majumbani , wengine wakibakia chuo hapo kwa wale walio kuwa wakiishi hosteli za chuo .
****
Ndani ya ukumbi ulio kuwepo ndani ya hoteli ya Serena kulionekana kukiwa na mapambo ya hapa na pale yaliokuwa yakiandaliwa kwa kupambwa kwa ustadi mkubwa ndani ya ukumbi huo , huku akionekana mwanadada Najma akisimimia shughuli hio yeye mwenyewe kwani hakutaka kitu kiharibike kwani alikuwa amealika watu wa kubwa wakiwemo wanamuziki na wasanii mbalimbali wakubwa ndani ya tukio hilo la uzinduzi rasmi wa kampuni yake.
“Vipi kuhusu ile picha ulio kuwa unasemea? “ Aliuliza Rehema rafiki yake.
“Rey ile ni muhimu kwangu na lazima katika tukio hili niiweke kwani nina amini kwa kutumia picha ile nitampata mwanaume ninae mtafuta , kwani najua kesho atakuwa kwenye magazeti na mitando ya kijamii pamoja na picha yangu na lazima atakuja kunitafuta” Aliongea Najma huku akiendelea na kazi alio kuwa akiifanya na yalikuwa yamebaki masaa machache tu kwa muda wa wageni kuwasili kwa ajili ya sherehe hio
****
“Boss kuna dharula”Ni sauti ya Kadabra iliekuwa ikisikika katika simu ya Samir wakati huo Samir akiwa nyumbni kwake baada ya kurudi kutoka kwenye mahafali .
“Dharula gani hio ?”
“Peter atahuduhuria kwenye tukio la leo kwani keshapewa kadi na mtoto wako Rania na kamuomba kuwa mtu wake wa pembeni siku hio”
“Whaat! Kadabra hakikisha huyo mwana haramu hafiki kwenye hio sherehe kwa namna yoyote ile , kwani Najma atakuwa pale”
Aliongea Samir kwa kupanick kwani taarifa hii ilikuwa ni ya kushitua kweli na ni kweli kama Najma angemuona Peter kupitia sherehe hio sijui ingekuwaje .
“Sawa boss , ila sijui cha kufanya kwani muda umeenda sana bado masaa machache sana sijui namna yua kumzuia”
“Wewe mpumbavu nini? , mimi sitaki maneno ya aina hiyo,nasema hivi hakikisha huyo mwanaharamu hafiki kwenye sherehe kwa namna yoyote ile “ Aliongea Samir kwa msisitizo huku akijikuta akitetemeka kwa hofu na hasira kwani alijua kile ikinacho enda kutokea,alijikuta akikaa kitandani huku akipumua kwa nguvu , alijifikiria kwa muda na alijikuta akiinua simu yake na kuanza kutafuta jina katika majina na alipo lipata , alipiga na haikupita muda mrefu simu ilipokelewa
“Hemedi habari za saa hizi!?”
“Salama mkwe habari yako ,siku hizi hatuonani”
“ Hakuna habari nzuri wakati huu, nafikiri unafahamu kuwa Najma leo anatukio lake linaendelea hapo Serena “
“Ndio kwanini nisijue bwana Samir na wakati nina surprise kwa Rania”
“Sasa kuna tatizo , Rania kampa mwaliko Peter kufika katika shughuli hio na nafikiri unajua kuwa mwanangu kafa kaoza kwa huyo mwanaharamu”
“Hahaha.. , Samir hii ndio kwanza faida ya kuwa karibu na mimi, kwani shida kama hizi naweza kuzitatua mara moja na najua kwanini umenipigia simu hii”
“Mimi sijui faida nina chotaka huyo mpuuzi asifike kwenye hio sherehe kwa namna yoyote ile”
“limeisha hilo kuwa na Amani kabisa nishalimaliza” Aliongea Hemedi kwenye simu na kumfanya Samir ashushe pumzi kwani swala hilo aliogopa sana , alichukua simu yake na kumpigia Kadabra .
“Usijisumbe kuhusu huyo mshenzi kazi hio nimememkabizi mtu mwingine”
“Boss una uhakika?”
“Nimesema kazi hio nimempa mtu mwingine , achana nayo kwa sasa na maswali sitaki”
“Sawa boss”
*****
Peter alifika nyumbani kwake aliko kuwa nakaa na Masumbuko , maana japo alikuwa amepewa nyumba na Mama Rania lakini hakuwahi hata mara moja kwenda kulala katika nyumba ile.
“Daah ! mzee sherehe ilikuwa nzuri ile sijapata ona” Aliongea Masumbuko .
“Yeah zile ndio mahafali ya vyuo , yanakuwa makubwa kama vile”
“Kumbee!”
“Ndio”
“ Sasa mimi najiandaaa kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe nyingine usiku huu ila nimepewa kadi moja tu tungeenda wote”
“Na mimi nina enda na Nasma kuna sherehe kaniambia kuwa anakwenda na kasema niende nae”
“Kumbe mshapanga mambo yenu na Nasma tayari ?”
“Ndio” Aliongea Masumbuko huku akilisogelea sofa na kujibwaga kwani muda huo alikuwa amesimama wakati akiongea na Peter.
“Hivi Masumbuko unajua yule Nasma ni mzuri sana na nikimwanglia anavutia kweli kweli na anaonyesha dalili kabisa za kukupenda , kwanini usimtongoze?”Aliongea Peter kwani ni kweli kila alipo kuwa akimwangalia Masumbuko wakiwa na Najma kuna kitu alikuwa akikiona kwa Nasma na alionekana kumpenda sana Masumbuko .
“Wewe Peter unafikiri atanipenda yule na kunikubalia wakati nikimtognoza?”
“Ndio kwanini asikubali na wakati anaonyesha kabisa kukupenda”
“Basi nitajaribu ila sio leo wala kesho namuacha acha tu maana sijui kama atakubali kuwa na mwanaume kama mimi ambae sina akili na sijasoma”
“Wewe mwanaume ni kujiamini, nani kakwambia mapenzi yana angalia elimu , wewe ukimfata usiangalie maisha yake angalia moyo kwake na huo ndio unatakiwa kuushawishi sawa”
“Poa nitajaribu”
“Sio ujaribu fanya , sema shida kubwa inaweza ikawa kwa wazazi lakini wewe hilo usilizingatie kwanza kasema wako nje ya nchi huko”
Masumbuko alijkuta akimkubalia Peter kwa kichwa na kisha akatoka hapo na kwenda kwenye chumba chake na alivyo fika alitoa suruali yake na kuanza kuangalia kijidudu chake kilicho kuwa kama cha mtoto , alikigusa gusa kutafuta hisia za kimapenzi ila hakuna kitu , alijikuta akivaa na kutoka zake hadi sebuleni na kisha alikaa hapo na kuanza kuangalia Tv muda huo
*****
“Mom and dad huyu ni Sebastiani ni rafiki yangu” Alongea Stella siku hio alipo kuwa amejumuika katika hoteli wakipata chakula na Stella alimualika Sebastiani , na wazazi wake Stella siku hio walikuwa wamekuja kwa ajili ya mahafali ya mtoto wao.
“Shikamooni !” Alisalimia Sebastiani kwa heshima kubwa na mzee Elvice aliitikia salamu huku akimwangalia Sebastiani , huku akimsaminisha .
“Nafurahi sana kukufahamu , nilikuwa na wasi wasi na mwanngu Stela ila nadhani uwepo wako kidogo unamfanya awe anatabasamu kama anavyotabasamu leo” Aliongea mama yake Stella na kumfanya Stella amwangalie Sebastiani usoni na kisha katabasamu.
Basi walichafua meza siku hio ndani ya hoteli hio ilio kuwepo Ubungo ilio kuwa ikijulikana kwa jina la Landmark hotel , walikunywa kwa furaha sana huku wakimpatia Stella zawadi walizo zindaa kwa siku hio .
Sebastiani alijikuta akifurahi sana kwani aliona hio ilikuwa ni hatua muhimu katika harakati zake za kumpata mrembo Stella .
Wakati wanendelea kula na kunywa kwa furaha ,huku stella akionekana kuwa katika furaha sana , mara alimuona mtu ambae ni kama wanzoni alimfananisha ila alipo angalia kwa umakini alimfahamu na kufanya mapigo yake ya moyo kupiga kwa nguvu na kujikuta akiangalia sehemu ile , na kuwafanya hata wazazi wake walio kuwa wakitaniana kuangalia upande ambao Stella alikuwa akiangalia , Stella alijikuta haaminin kwani alimuona James mwanume anae mpenda akiwa na rafiki yake Lea na wala wao wakiwa hawana habarikwani hawakutambua uwepo wao hapo hotelini .
“Yule si James yule , na yule msichana ni nani? “ Aliongea mam yake Stella na kabla hajajibiwa Stellla alinyanyuka na kufata upande walio kuwepo Lea , lakini kabla hajafika aliwaona wakitoka eneo hilo na kuingia kwenye lift .
Sebastian alijikuta akiona sasa mambo yanakwenda kubumbuliuka kwa upande wa Lea na alijua kabisa kuwa siku hio urafiki wa wawili hao unakwenda kuisha siku hio , ila alicho kumbuka ni ahadi yake Lea kwake kwamba endapo Stella atamfuma mmoja wapo basi hakuna kutajana , lakini kwa Sebastiani bado hakuwa na uhakika na ndio maana hata yeye roho yake ilikuwa juu juu .
Stella hakutaka kushindwa na uzuri wa hoteli ile ulikuwa na lift , mbili kulia na kushoto , Stella alikimbilia lift za upande wa kushoto na bahati ni kwamba haikuwa na mtu mana alipo binya tu ilifunguka, na akaingia huku akisahau kabisa floor alio kua anaenda maana hakujua kuwa James na Lea walikuwa wanaelekea lift gani . .
“Naomba kisiwe kweli ninachokifikiria”
ITAENDELEA
SEHEMU YA 29
Mama na baba yake Stella walijikuta kwenye mshangao kwani walikuwa hawaelewi kinacho endelea,walikua wakijua kuwa mtoto wao huyo alikuwa ashaachana na James na alikuwa akiendelea na maisha yake .
Lakini kitendo cha kumuona Stella akinyanyuka na kumfuata James wao kama watu wazima walijua kuwa sio kama Stella alikuwa ameachana na James ila ni kwamba mtoto wao alikuwa akimsubira james kurudi kwenye maisha yake .
Hawakutaka kuliamini jambo hilo moja kwa moja na walitaka walione kabisa na wajue ni kwasababu gani Stella kamfuata James , walitaka kujua kama bado mtoto huyo alikuwa akiendelea kumpenda James na alikuwa akiweka tabasamu la uongo mbele yao wakati ndani anaumia, walikuwa washasau nguvu ya mapenzi.
Sebastiani alijikuta akiwa hajui cha kufanya na aliangalia wazazi wake Stella wakinyanyuka na kutoka eneo hilo wakifuata uelekeo wa Stella .
Stella alijikuta mwenye hasira , kwanza roho yake ilikuwa ikimuambia kuwa Lea na James ni wapenzi na walikuwa wakimzunguka , wakati akiwa kwenye lift hio , kuna muda alitamani hata isiwe kweli, kuwa rafiki yake alikuwa akimzunguka kwani alikuwa akimuamini sana Lea na alikuwa akimchukulia zaidi ya rafiki ..
Alijikuta akiwa juu kabisa floou namba nane ya hoteli hio na kiufupi ni kwamba alipo ingia ndani ya floor hio aliotea tu namba ya kwenda na alibonyeza .
Alijikuta akijiona mjinga kwani floor hio ilikuwa kimya kabisa , alijikuta akiingia kwenye lift tena na kushuka hadi chini na moja kwa moja elienda mapokezi.
“Dada samahani kuna ndugu zangu wameingia sasa hivi naomba kujua wameingia chumba gani ?”
“Samahani unazungumziwa watu gani hao ?“
“Wamengia sasa hivi nataka kujua wameingia chumba gani ni mdada na mkaka mrefu hivi maji ya kunde , angali jina anaitwa James na Lea “ Aliongea Stella huku akihema kama alikuwa akikimbizwa .
Muhudumu yule alimwangalia usoni na kisha kurudisha macho katika tarakishi yake .
“Siwezi kutoa taarifa za wateja wetu labda nipate kibali kutoka kwao nitajie jina lako niwailize na kama watakuruhusu ndipo na mimi nitakuruhusu kuonana nao”Aliongea muhudumu yule wa kike alievalia kinadhifu kabisa huku akimwagalia Stella .
“Stella kuna nini ?”Ilisikika sauti ya baba yake Stella ikiuliza swali hilo .
“James baba” aliongea Stella huku machozi yakiwa yashaanza kumtoka kwani alijihisi maumivu makali na wakti huo na Sebastiani alifika eneo hilo .
“James kafanyaje na anakuhusu nini mwanangu si msha achana na kila mtu ana maish yake kwa sasa “ aliongea baba yake stell na wakti huo , wakiwa wamesimama katika eneo hilo , alikuja mwanaume akiwa amevalia suti
“Dada za saa hizi naenda chumba namba 201 nina miadi na Lea Edward “ Aliongea mwanaume huyo kwa sauti kiasi kwamba utadhani alikuwa akitaka asikike na kumfanya stela aliekuwa ameinamisha kichwam chini kunyanyua uso wake na kumwanglia mwanaume huyo ambae aliruhusiwa na dada yule wa mapokezi baada ya kupiga simu na hapo ndipo Stella kama alikuwa kichaa vile alimfuata mwanume yule kwa nyuma na aliopo ingia na kubonyeza namba na Stella na yeye alikuwa ameshazama ndani ya lift hio na wala mwanaume yule aliekuwa amevaa miwani hakumwongelesha huku akionekana yuko siriasi kabisa na alikuwa akitafuna bublish.
Huku wazazi wa Stella walijikuta wakishangaa uchizi wa mapenzi ya mwana wao . Na sebastiani alikuwa ni kama ana angalia filamu kwani hakusema chochote Zaidi ya kuangalia kinacho endelea.
Stella alimfatisha mwanaume yule mpaka alipo simama kwenye chumba cha namba 201 .
“Dada kumbe tunaelekea chumba kimoja “” Aliongea mwanume yule huku akimwangalia Stella .
“Ndio nina shida na mtu wa chumba hiki “ Aliongea Stella na hapo jamaa yule wala hakutaka maneno mengi maana aligonga mlango na hapo ndipo Lea alipo fungua mlango ule .
“Mpenzi wangu kizibo haaa..! shost”Aliongea Lea huku Stella wala hakutaka kuongea mengi aliingia moja kwa moja mpka ndani na kuanza kutafuta .
“Lea! , James yuko wapi?” Aliuliza Stela
“James ?. atakuwa kwenye chumba chake niliachana nae kwenye lift” Aliongea Lea kwa kujiamini kabisa.
“Namba ngapi yupo natak kuonana nae?”
“Shost punguza hizo hasira kwanza unanifanya hata naogopa kukuambia”
“Lea tutaongea vizuri baadae naomba uniambie kwanza yupo chumba namba ngapi ?”
“Namba 320 floour ya nane”
Stella hakusubiri maelezo mengine alitoka nje ya chumba hicho na kisha kukimbilia kwenye lift , huku akikutana na wazazi wake na Sebastiani na walivyo muona akiingia kwenye lift hio na ilibidi wamshike Stella lakini ni kama mbogo vile , alibonyeza namba nane na kisha lift haikuchukua muda mrefu ikafunguka na wakwanza kutoka alikuwa Stella aliefuata alikuwa ni mama yake Stella akifuatiwa na baba yake na Sebastiani .
Stella aligonga mlango na hapo ndipo mwanamke mmoja mrembo alievalia khanga moja alitoka .
“Niwasaidie nini ?”
****
Peter ndani ya muda mfupi alikuwa tayari amesha maliza kujiandaa na alicho kuwa akingojea ni simu ya Rania tu kuita ili aianze safari ya kwenda kukutana nae kwa jili ya kuelekea ukumbini .
Alikaa na wakati huo na Masumbuko alitokea sebleni hapo akiwa amependeza kweli na kiufupi siku hizi chache ambazo masumbuko alikuwa amekaa dara , alikuwa akijua sana kuujali mwili wake kwani alikua anajua kujihudumia kweli , kwani suti alio kuwa mevaa masumbuko alikuwa imempendeza kweli .
“Wewe jamaaa hio suti mbona kama sikumbuki kama nilikupa mimi na sina suti kama hio kwenye kabati langu” Aliongea Peter kwani suti alio kuwa amevaa Masumbuko ilikuwa imkemkaa vyema lakini kingine ni kwamba ilionekana kuwa ya thamani kweli .
“ Nasma huyo broo” Aliongea Masumbuko na kumfanya Peter atingishe kichwa na kuona kweli Masumbuko alikuwa ni bonge la handsome kwani muonekano wake ulikuwa wakipekee sana.
“ Kweli mzee baba una bahati sana si kwa kupendezeshwa huko” Aliongea Peter na wakati huo simu yake ilitoa mlio kuwa ilikuwa ikiita na alipo angali jina aliona ni la Rania alipokea simu hio na kuweka sikioni na kisha akaitoa .
“Masumbuko tutaonana baadae mimi nelekea kwenye sherehe wasalimie huko”
“Poa Peter hata mimi nelekea kwenye sherehe wasalimie huko” Aliongea Masumbuko huku akimwigilizia peter na nikwamba hawakujua kuwa wanaenda sehemu moja .
Masumbuko na yeye hakukaa sana alienda kufungua mlango kwani kulikuwa kuna mtu alikuwa akigonga.
Ukisikia kuna wanawake ambao Mungu kawaajalia uzuri basi siku hio ungesema kuwa mrembo Nasma alikuwa ni moja ya kundi hilo la wanawake ambao wamejaliwa uzuri , japo kila mwanamke anakuwa na uzuri wake ambao unamfanya mwanume kumpenda , lakini kuna uzuri mwingine unakuwa ktika macho ya watu wote namaanish ule uzuri wa kuvutia sana pale tu unapo mwangalia mwanamke .
Nasma siku hio alikuwa amependeza kiasi kwamba hata Masumbuko ambae alikuwa hajui sana maswala ya wanawake aljikuta akitamka maneno ya kupendeza mbele ya mrembo Nasma .
“Umependeza kama malaika” Aliongea Masumbuko baada ya kumfungulia Nasma
“Asante Masu” Aliongea huku akifupisha maneno ya jina la Masumbuko na akiachia tabasamu ambalo kwa mwanume rijali lingempa presha ya ghafla sio Masumbuko ambae hana hata uwezo wa kusoma channeli .
“Hata wewe umepemndeza hakika ,nilijua kukupatia katika hio suti” Aliongea Nasma huku akimsogelea Masumbuko na kumuweka sawa masumbuko suti yake .
“Mimi napendeza sana nilikuwa nakosa matunzo tu”
“Hahahaha… Masumbuko huishiwi vituko na ndio maana kila siku nazidi kukupenda”
“Unasema !”
“Masumbuko twende buana tunachelewa ujue”
“PSoa twende “ Aliognea Masumbuko huku akipotezea lile neno ambalo aliliskia likitoka kabisa kwenye mdomo wa Nasma .
Basi walitoka huku wakiwa wamependezana na hata Lucy alipo waona alijikuta akitingisha kichwa na kukubali kuwa Masumbuko alikuwa ni bonge la HB.
Basi Lucy aliwafungulia mlango mabosi zake hao kwani hata Masumbuko wakti huo alikuwa akimuona kama boss.
****.
Ukumbi ulikuwa umependeza sana kiasi kwamba kwa ambae angeuona angejua kuwa siku hio kumetumika hela nyingi sana katika upambaji wa ukumbi huo.
Watu wengi wakiwemo wasanii wakubwa walionekan wakiwa wamependeza kisawaswa sawa huku wengine wakiwa na wenza wao .
Na kila anae kuwa akiiingia ndani ya ukumbi huo alikuwa ni lazima kupitia kwenye Red Carpert kwanza ,kufotolewa mapicha picha .
Moja ya wana mitindo walio hudhuria katika tukio hilo alikuwa ni mwanamitindo maarfu sana ajulikanae kwa jina la Queena , mwana mitindo kutoka Marekani na siku hio alikuwa amealikwa katika tukio hilo kama mgeni maalumu katika siku hio , kwani mwandada huyo alikuwa na heshima kubwa ndani ya taifa la Tanzania .
Siku hio alikuwa kapendeza kweli na waandishi wahabari walionekana kumuulizamaswali mengi ndani ya Red Carpet .
SEHEMU YA 30
“Ni wasadie nini” Hilo ni sauti ilio toka kwa bidada huyo aliekuwa amesimama hapo mlangoni , akiuliza swali ambalo lilimfanya Stela kumsukuma na kuingia ndani na alijikuta haamini kwani alimkuta James akiwa kifua tupu huku akiwa amevalia bukta tu akiwa amekaa kitandani huku akiwa maeshikilia glass ilio kuwa imejaa wine .
“James!” Aliita Stella huku machozi yakiwa yana mtoka mfululizo kwani moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kiasi kwamba alikuwa hana hata uwezo wa kuzuia machozi yale yasimtoke .
“Stella , umekuja kufanya nini hapa ?”
“James kwanini hivi lakini James , huoni ni kwa jinsi gani nakupenda James , kwanini unanifanyia hivi James kwanini unaufanya moyo wangu kuuma kiasi hiki eh , kwanini James” Aliongea Stella huku akiwa amekaa kabisa kwenye sakafu akilia .
“James niambie kwanini hutaki kunisikiliza , ni kosa gani hilo ambalo halisameheki James mpaka unaniacha kwenye machungu namna hii James why James”
“Stella sina sababu ya kukusikiliza , naomaba nikwambie tu ukweli sikukupenda Stella nimedumu na wewe kimazoea sio kihisia naomba unisamehe juu ya hilo , kwani nililkuwa natafuta njia ya kukuacha Stella , lakioni hata kama sikukupenda Stella nilikuwa nakuheshimu lakini kwa lile ulilofanya sitokusamehe na sitoweza kuishi na mwanmke mchafu kama wewe” Maneno hayo makali yalimtoka James bila hata woga na yakaenda kutua katika masikio ya Stella .
“James naomba unisikilize James nakuomba usinihukumu kabla haujaujua ukweli James , nakupenda James kwanini hivi lakini”
Ilikuwa nihali ya kuhuzunisha sana aliokuwa nayo Stella , hata Sebastiani alie kuwa moja ya mkandarasi ,alijikuta akimuonea sana huruma Stella kwani hakudhania kuwa Stella alikuwa na mapenzi makubwa kwa Jamesnamnaya kumlilia kiasi hicho .
Wazazi wake walijikuta wakijizuia kutotoa machozi kiutu uzima ila mioyo yao ilikuwa ikiungua , kwani hawakutarajia kuwa mwana wao huyo alikuwa akiishi na maumivu ndani ya moyo wake kwa kiasi hiko , mama yake Stella alijikuta chozi likimtoka , kwa jinsi alivyo kuwa akimuona Stella analia alijua nikwakiasi gani mwanae alikuwa akiumia..
Baba yake na Stella aliishia kumuangalia James kwa hasira na kisha alimsogelea Stella na kumkokota nje .
“James utakuja kunikumbuka James , utakuja kujutia siku hii ya leo na kuikumbuka katika maish yako yote James” Aliongea Stella na James wala hakuwa hata na habari Zaidi ya kuchukua glass yake ilio kuwa na wine kidogo na kuinywa mpaka ikamalizika na hapo hapo alitupa chupa ukutani kwa hasira.
*****
Tukirudi nyuma Sebastiani baada ya kumuona Stella akiingia kwenye lift na wazazi wake walivyo fuatia , alitoa simu yake haraka haraka na kish alipiga namba ya Lea na bahati nzuri ni kwamba ilipokelewa hapo hapo na alimwambia kuwa Stella kawaona kwa hio aangalie cha kufanya .
Ndani ya chumba cha Lea ambae alikuwa ameshikiliwa kiuno na James alipo maliza kuongea na simu alimgeukia haraka James na kumwambia kuwa Stella anakuja na katuona .
James alijikuta akipatwa nakiwewe na pia kwa lea hivyo hivyo na hapo hapo akili ya Lea ilifanya kazi haraka haraka na kumwambia james wanatakiwa kufanya jambo , na James alitingisha kichwa ila hakuona ni kwa jinsi gani wanatakiwa kukamiliaha jambo hilo .
Ndipo Lea alipo pata wazo na James na yeye aliona wazo hilo ni bora na ndipo alipo piga simu na kisha alitoka haraka haraka kwenye chumba hicho akimuacha Lea na wakati huo ndio alipo ikimbilia ;lift m na aliona kabisa kuna watu walikuwa wakipanda na lift hio na ndipo alipo pita kwa njia ya ngazi mpaka chumba cha bodigadi wake ambaco alikuwa amechukua yeye na mpenzi wake na bodigadi wake alimpigia simu na kumwambia jinsi ya kufanya na ndie alie kuwa pale mapokezi na kutaja jina la Lea kwa nguvu na kumfanya Stella ajue mwanaume huyo alikuwa akielekea kwenye chumba chao na pale ndipo alipo mfata kwa nyuma.
Huo ndio mchezo alio kuwa ameucheza Lea ili kutokamatwa na Stella , kwani mwanume yule aliemwita kizibo hata hakuwa akiitwa kizibo ila ni jina alilo kija nalo Lea ili tu kujikomboa katika kufumaniwa kwani hakutaka kumpa maumivu mara mbili Stela , japo alijua siku moja Stella atakuja kuujua ukweli , lakini aliona huo haukuwa wakati sahihi kwa stella kufahamu kia kitu
*****
“Kijana hebu njooo mara moja tuongee” Baba yake Stella aliongea akimwambia Sebastiani baada ya kumpandisha Stella kwenye gari .
“Ndio mzee wangu”
“Hivi unajua kinacho endelea hata kidogo tu nipate kujua”
“yeah mzee ni kwamba...” Alijifikiria huku akijiuliza amwambie .
“Ni kwamba nini hebu niambie ni nini kinaendelea , kwanini Stella anasema anataka kusikilizwa”
“Mzee kiukweli ni kwamba Stella siku ile alifanyiwa kama kupewa kumbukumbu”
“kumbukumbu!?”
“Ndio kumbukumbu za masaa mawili”
“Unanichanganya hebu niambie vizuri”
“Mzee sijui nikuelezeje, ila huo ndio ukweli ni kwamba Stella hakufanya kitendo kile makusudi chakumsaliti James ila ni kwamba alibadilishwa akili yake , kama uchawi”
“Kijana hebu weka mambo yanyooke , unamaanisha kuwa stella alirogwa?”
“Ndio mzee alirogwa kwa masaa mawili” Aliongea Sebastian huku akionekana kutojiamini kabisa kwani alionekana kutetemeka .
“Kwa hio ni kama kabakwa si ndio ?”
“Ndio baba”
“Unamjua alie mbaka?”
“Hapana...,ndio mzee”
“Jibu swali moja unamjua alie mbaka mwanangu nakuuliza wewe mpuuzi” Mzee alibadalika ghafla na kuwafanya hata walio kuwa kwenye gari watoke .
“Mume wangu kuna nini tena mbona mko hivyo”
“Hakuna kitu mke wangu” Aliongea huku akitoka eneo hilo na gari kuwasha moto huku Sebastiani akiingiza mkono wake kwenye shati lake huku akihema kwa nguvu na kutoa kikadi hicho alichopewa na mzee Elvice .
Alijikuta akipumua kwa nguvu na kushika magoti .
*****
Peter wakati akitoka ndani ya nyumba yao aliendesha gari kuelekea Mwenge kwa spidi ya kawaida , huku akiwasiliana na rania sehemu ya kukutania kwani walikuwa wakihitajika kuingia wote ndani ya hoteli hio .
Peter hakuwa na habari aliendesha gari yake huku akiongeza spidi kila baada ya dakika kwani muda ni kama ulikuwa umeenda sana .
Lakini wakati anendesha gari yake alikuwa akihisi kitu sio cha kawaida katika gari yake na wakati huo ndio wakati alikuwa akipita ITV na alikuwa kikaribia kituo kinachoitwa sanyansi nyuma kidogo na jingo lefu la LAPF.
Hapo ndipo alipojikuta akisikia mtikisiko wa gari lake na kujikuta akiyumba na kwakuwa alikuwa mjanja alijitahidi na kuliegesha pembeni kidogo na kituo hicho katika eneo hilo kukiwa na maua na miti miti ilionekana kama bustani.
Peter alishuka kwenye gari yake na kuzunguka upande wa kulia ambako ndiko gari yake ilikuwa imelemea na wakati akizunguka ndipo simu yake ilianza kuita na aliipokea huku akiliinamia gari na kujikuta akishangaa kwani tairi ya mbele ilikuwa haina upepo kabisa na aliangalia chini kwa umakini aliona kitu kama kijimsumari kikiwa kimeichoma taili hio .
Wakti akiendelea kushangaa taili yake ya gari huku akiongea na Rania na hapo hapo sijui kibaka alitokea wapi kwani simu yake ilikwapuliwa na kijana mmoja aliekuwa amevaa helmeti akiwa kwenye pikipiki .
Sasa wakti akinyanyuka huku akijikuta akipanua mdomo na kuangalia pikipiki ile ikitokomea , hapo ndipo alipo jikuta akilia kama mtoto kwani , ghafla kulipita gari kama ya zima moto na kutoa maji kama mvua na kumwagikia pita na hapo ndipo Peter alijikuta akiwashwa balaa na gari ile nayo ilikuwa ikipotea katika eneo hilo.
Baadhi ya watu walijikuta wakimuangalia huku wakiendelea na mishe zao , na bahati nzuri ni kwamba katika eneo hilo hakukuwa na watu wengi .
Lakini ghafra gari ilisimama pembeni yake na kufunga breki .
*****
Kwa hio biss unasema tutawazuia vipi” Aliongea Ramso baada ya Hemedi kupokea simu kutoka kwa Samir ..
“Ramso hebu fikiria kidogo bhana kwanini tushindwe kumzuia , tumefanya kazi nyingi za kimagendo na kupitisha madawa ya kulevya tushindwe na hili dogo”
“Ni kweli boss lakini muda , limebaki lisaa tu kwa wao kukutana na Rania”
“Una maanisha nini kukutana na Rania , Ramso utaniboa sasa hivi , usimtaje Rania ukimuhusiha na huyo boya maana roho yangu hapa naona kama itanipasuka kwa maumivu ya huyu boya kuwa namazoea na Rania”
“ sawa biss samahani “
“Mwite mzee wa mipango aje haraka hapa najua hashindwi kitu” Alikuja kijana mmoja alie kuwa akionekana mwembamba sana huku akiwa mrefu na alikuwa na miwani akiwa amevalia tisheti yake ya Levi.
“Derick una lisaa limoja tu la kumzuia mtu asifike Serena hoteli , nataka ndani ya hilo lisaa ufikirie ni kwa nammna gani tunaweza kumzuia “ Aliongea Hemedi kwamsisitizo na kumfanya Derick kushangaa kwani hizo ni dakika chache sana kwa yeye kufikiria wazo na kulifanyia kazi .
SEHEMU YA 31
“ Boss jambo hili siwezi kulifanya mwenyewe lazima wote tulifanyie kazi “
“ Kivipi derick mimi nataka kuondoka sasa hivi “
“Najua”
“Sasa kama wajua”
“Nina hitaji koneksheni na mtu wa gari la kutuliza ghasia la maji ya washawasha”
Unasemaje Derick , hayo maji yanahusika vipi Derick ,wewe nipe mpango wa kumuzia huyo mwanaharamu , na mimi ilikumpata Rania lazima swala hili lifanikiwe .
“Huo ndio mpango wenyewe sasa” Aliongea Derick na kumfanya Hemedi amwangalie Derick na kurudi kukaa katika kiti chake na Ramso mwenyewe akakaa kusikiliza mpango wa derick unakwendaje .
“Nimeshakuwa na idea tayari ambayo itamzuia yeye kufika katika tukio hilo na kukamilisha hilo tunahitaji vitu viwili vya haraka sana gari la maji ya washawasha na Tranguilizer gun ( hii ni bunduki ambayo hutumika kwa wanyama pori katika kuwapiga sindano na kuwafanya walale kama pale wanapo hitajika kufanyiwa matibabu ) na Hemedi alikuwa nayo kwani alikuwa pia na biashara za meno ya tembo na pia alikuwa akikamata wanyama kisiri siri na kuwasafirisha
“Hio bunduki tunayo ila hilo gari la maji ya washawasha hatuwezi pata”
“Boss umesahau kuwa hapa tupo na ghala la Police ?”
“Una akili sana Derick na ndio maana nakuaminia una maanisha kituo cha Police cha Osterbay “
“Ndio”
“Hilo gari lishapatikana ngoja nimpigie Sajenti Nuru pale Satatupatia”
Na hapo hapo Hemedi alitoa simu yake na kumpigia Sajent Nuru na alijikuta akitabasamu baada ya kushusha simu yake
“Anasema lipo , pesa inaongea bwana , ila nasema kama ni kwa njia ya uhalifu hatotoa”
“Hio sio njia ya uhalifu”Aliongea Derick “Haya tupe huo mpango wako”
“Kwaharaka haraka ni kwamba huyu Peter anakaa Mbezi Beach na hana ujanja wa kupitia njia nyingine kwenda Serena zaidi ya Mwenge , hatopitia kawe kwasababu ni kinyume ,na hilo lazima tufanye apitie njia ya Mwenge ,ila nina uhakika asilimia tisini , sasa inabidi tumtengezee pancha ya tairi la kulia na lazima ataegesha gari pembeni baada ya gari kupata pancha “
“Sasa pancha tutamtengenezeaje ?”
“tutatumia trangulizer gun na kazi hio ataifanya Ramso kwani najua ana shabaha sana na anacho takiwa ni kuilenga taili ya mbele na zoezi hilo anatakiwa kulifanyia pale kwenye kampuni ya Shelys mbele kidogo na ITV upande wa kulia na hilo atajua mwenyewe jinsi ya kufanya na najua kafanya kazi nyingi kama hizi .
“Na baada ya hapo nini tena “
“ lazima atasimamisha gari katika kituo cha sayansi kwani hana chaguo lingine au karibu na hapo kwani tairi itakuwa imeisha upepo na hapo inatakiwa asipige simu kuomba msaada na kwa maana hio lazima tumuweke mtaalamu wa kukwapua.
“Una maanisha Lenard afanye hio kazi ?”
“Ndio boss”
“Watu wawili wanatakiwa kwenda kuchukua maji ya washawasha na kisha wahakikishe wanalitega bomba la maji ya mvua litoe maji kumwagia , na kama linafanya makosa mara moja tu wakishamuona Peter sehemu alio egesha gari na wahakikishe gari isisimame na ionekane ni kama makosa tu.
“ Na hapo ndipo tutamaliza mchezo “
“Hahaha .. kazi na ianze nimeukubali huo mpango “
“Ila Derick na wewe hjujasema kazi yako utafanya nin ?”
“Mimi ndio nitamalizia kila kitu “
*****
Rania alijikuta akiwa kwenye hali wasiwasi kwani simu ya Peter haikupatikana kila alipokuwa akipiga jambo ambalo lilimpa wasiwasi mwingi sana na wakati huo watu walikuwa wakiendelea kuingia na muda ulikuwa umeenda sana.
Wakati akiwa amesimama nje ya hoteli hio akiangalia kama atamuona Peter ndipo wakati wa gari iliowabeba Masumbuko na Nasma likifka ndani ya hoteli hio ndani kabisa na kwenda kuegeshwa na hapo ndipo Msasumbuko na nasma walivyo toka katika gari hilo kila mmoja upanmde wake ,walikuwa wamependeza sana sio Masumbiuko Saio nasma .
“ Lucy sitaki kupitia katika Red Carpet na kuhojiwa” Aliongea Nasma baada ya kusoge ambele kabisa na mlango wa kuingilia .
Masumbuko yeye alikuwa akishangaa maana hio ndio mara yake ya kwanza katika maisha yake kuhudhuria matukio makubwa kama hayo , tena matukio ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa na kiingilio kikubwa sana na hata wahudhuriaji wake wakiwa watu maarufu na watu ambao walikuwa na pesa zao ..
“Hakuna shida Nasma tunaweza kupita kuna uwezekanao wa kuingia bila kuhojiwa na waandishi ama kupigwa picha” Aliongea Lucy na Nasma alitingisha kichwa na Masumbuko alishikiliwa na Nasma na kisha waliingia ndani ya ukumbi huo huku wakionekana kupendeza sana . .
Hapo ndipo Masumbuko alivyo jikuta akishangaa zaidi kwani kila kitu kilikuwa kigeni kwake , kwanzia vinywaji na kila kitu kilicho kuwa kipo katika eneo hilo alikuwa hajawahi kukiona , alijikuta akifurahi na uzuri ni kwamba Nasma hakutoka pembeni ya Masumbuko .
Huku nje Rania aliwaona Nasma wakiingia lakini hata akili yake haikuwajali kabisa kwani alicho kuwa akijali wakati huo ni Peter tu,alikuwa kwenye wasiwasi mkubwa hasa pale alipo mwambia kuwa gari yake imepata hitilafu na hapo hapo kabla hawajaelewana ndipo mawasiliano yakakatika , jambo hilo lilimfanya kuwa katika wakati mgumu na kujawa na wasiwasi mwingi sana
“Rania!”
Aliita Samir akiwa yupo nje ya kabisa akiwa katika maegesho ya magari na alionekan kuna simu muhimu aliokuwa akipokea .
“Mbona umesimama hapa na wakati tukio limeanza mtoto wangu twende ndani au kuna mtu unamsubiria ?”
“Aaa.. ndio dadi kuna mtu niliahidiana nae atakuwa my plus one lakini mpaka sasa hajafika na mara ya mwisho aliniambia gari yake imepata hitilafu na mawasiliano yake yamepotea
“Atakuwa salama my daughter hauna haja ya kumsubiria kwani kama gari yake itakuwa imepata hitilafu nadhani anaweza asifike kabisa na ,muda kama unavyo ona umeenda sana twende ndani”
Rania alikubali kinyonge sana na kisha akaungana na baba yake a wakaingia ndani .
Ndani ya ukumbi tukio lilikuwa likiendelea na waburudishaji walioalikwa kutoa burudani siku hio walikuwa stejini, msanii aliekuwa amealikuwa katika tukio hilo na wakati hio alikuwa akitoa burudani alikuwa ni Ommy dimpoz. ******
“Kaka pole sana ingia kwenye gari nikupeleke kweenye hoteli ya karibu ukaoge na kuvua hizo nguo” Huyu alikuwa ni Derick aliepanga mpango mzima wa kumzuia Peter asiende katika tukio la ufunguzi wa kampuni ya Najma.
“Nashukuru lakini siwezi kuacha gari hapa” Alizungumza Peter huku akiwa anajikuna .na hata zile nguo ambazo zilikuwa zimempendeza zilikuwa zimekwisha kupoteza mvuto.
“Funga gari hio bro hayo maji yalio kuwamgikia ni hatari sana hayawezi kuisha makali yake mpaka uoge”
Peter alijkuta akimwangalia yule mshikaji na kisha akalisogelea gari lake haraka haraka huku mwili ukiwa unamuwasha na alitamani hata avue nguo , kijana Derick alikuwa akitabasamu moyoni kuona mpango wake umefanikiwa kwa asilimia mia moja alijikuta akijihisi mtu mmoja mtata sana na mwenye akili sana tena katika upangaji wa mawazo kwani alitumia muda mchache sana katika kupanga mpango wake na kuja kufanikiwa bila tatizo lolote .
Peter alipelekwa mpaka kwenye hoteli ilioko upande wa kulia nyuma kidogo na ITV hoteli ifahamikayo kwa jina la Kebbys, Derick alionekana kabisa alikuwa na chumba ndani ya hio hoteli kwani ile anaingia tu alichukua kadi yake na kisha akaongozana na Peter.
“Pole sana broo” Aliongea Derick baada ya Peter kutoka bafuni huku akijihisi mwili wake kuwa sawa na hakuhisi muwasho tena.
“Daah! Asante”
“Niliona wakati gari la police lilipo kumwagikiamaji nilikuwa pale pale nikiwa na nunua miche ya maua “
“Daah! wale wajinga sana , yaani hata sielewi ni bahati mbaya au ilikuwa makusudi wameniharibia kabisa mipango yangu ya leo ya kuhudhuria tukio maana saivi nimechelewa kabisa na siwezi kwenda tena na isitoshe simu yangu imeibiwa pia “ Aliongea Peter .
Basi Peter hakuwa na jinsi tena alikubali kuwa siku hio hawezi kutimiza miadi ya kukutana na Rania kwa ajili ya kuhudhuria tukio ambalo alimuahidi kuwa atahudhuria.
****
Baba yake Stella hawakutaka kumuacha mtoto wao katika hali alio kuwa nayo , walimuonea sana huruma kwa mambo yote alio kuwa akiyapitaia kwani walikuwa wakielewa kabisa mapenzi yalivyo kuwa yanauma na waliielewa hali alio kuwa nayo Stella kwa wakati huo .
Waliendesha gari mpaka katika nyumba ambayo Stella alikuwa amepanga waliingiza gari na kisha kwenda kuliegesha na kutoka.
“Nyumba hii ni nzuri sana, ina mazingira ya kuvutia kweli” Aliongea baba yake Stella ama mzee Elvice .
Huku wakiongozwa na Stella na kuingia ndani ya nyumba hio yenye ghorofa mbili kwenda juu lakini ile wanaingia ndipo uso kwa uso walijikuta wakikutana na mwanume alie kuwa akiishi ndani ya nyumba hio .
“Dokta singano!” Aliita mzee Elvice kwa mshangao. .
“Shikamoo mzee” Alisalimia Dokta Singano kwa heshima na wakati huo Stella na mama yake walikuwa washapita eneo hilo na mzee Elivice alie kuwa nyuma ndie aliemuona Singano peke yake .
“Kumbe unaishi hapa dokta ni siku nyingi sana tokea ulipotoka mwanza”
“Ndio naishi hapa japo nilikuwa nimesafiri kimasomo ila ndio nimerudi”
“Ndoo maana umeongezeaka kidogo , vipi tunaweza kuongea kidogo”
Singano na mzee alvice walikuwa wakifahamiana sana hii ni kipindi ambacho kijana singano alikuwa katika mafunzo kwa vitendo(intern) katika hospitali ya Bugando Mwanza , ndipo alipottokea bahati ya kutana na mzzee Elvice katika harakati za matibabu na Mzee Elvice alitokea sana kumpenda sana Singano hata kutamani moja ya watoto wake aolewe na Singano ,kwani kwa miaka kadhaa aliokuwa amefahamiana na Sngano ,alimfahamu kama kijana mchapa kazi mwenye heshima na Utu ndani yake , hata siku ambayo Singano alimwaga Mzee Elvice baada ya kumaliza elimu yake ya vitendo ,kwa mzee huyo ilikuwa ni huzuni kwani alikuwa akimpenda sana kijana Singano
“Unaishi sehemu nzuri sana , na wewe umepanga hapa?”
“Hapana hii ni nyumba yangu”
“Umejitahidi sana kijana ni nyumba kubwa sana hongera sana bwana Singano”
“Asante sana”
“ Sasa nilitaka niongeee mambo mawili matatu na wewe”
“Ndio mzee”
“Kwanza nadhani hujafahamu kuwa alieko juu ni mwanangu wa mwisho anaitwa Stella ni mwanfunzi anaemaliza chuo katika sheria”
“Kumbe!”
“Ndio lakini sasa hivi yuko kwenye hali mbaya sana na mitihani yake ipo karibu sasa ninacho taka unisaidie kupitia taaluma yako ya udaktari kumuweka sawa ili asije akaharibu katika mtihani wake ambao unafanyika hivi karibuni . aliongea Mzee Elvice na kumfanya Dokta Singano amwangalie na kufikiria kwa wakati mmoja .
“Sawa mzee wangu kwakuwa ni wewe nitakusadia katika hilo kwani kwa sasa nina mambo mengi ya kufanya kwani nimepata uhadhiri katika chuo cha muhimbili”.
“Kumbe! hongera sana ni moja ya nafasi Nnzuri sana kufundisha vijana wenzio”
“Ndio ni nafasi nzuri na ndio inayo nifanya niwe bize sana na ratiba zangu kuibanana sana , lakini huhusu swala la binti yako nadhani lipo ndani uwezo yangu na uzuri ni kwamba yupo hapa hapa”
Basi mzee Elvice aliagana na Singano kwa kupeana mikono na kisha kila mtu akielekea kwenye sherehe ya ufunguzi wa kampuni ya Najma , lakini akiweka ahadi kwa mzee Elvice kumsadia Stella kurudi katika hali yake ya kawaida.
ITAENDELEA KESHO
SIMULIZI UNAWEZA KUIPATA KWA 2500 TU
******
✓PATA SIMULIZI YA KIJASUSI YA BOOK OF ALL NAMES KWA 5000/= SOFTCOPY
✓PATA SIMULIZI YA KIJASUSI YA UMOJA NAMBA TISINI NA SABA KWA 2500/= TU
✓PATA SIMULIZI YA MAPENZI MY DREAM MY FAVOURITE KWA 2500/=
NAMBA ZA MALIPO NI: 0687151346 AIRTEL MONEY AU 0657195492 TIGOPESA AU 0623367345 HALOPESA –JINA ISSAI SINGANO
UKISHALIPA NITAFUTE KWA NAMBA 0687151346 WATSAPP
Sent from my TECNO KA7 using
JamiiForums mobile app