Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA 31 YA 50
Maneno ya Babu yalimpatia faraja Akwelina kwa kiasi kikubwa. Usiku ulizidi kukomaa siku hiyo Kakinga alichelewa sana kurudi nyumbani, Babu alipoona usiku unazidi kukomaa alimwambia Akwelina aingie ndani akalale lakini Akwelina alikataa kwa sababu alikuwa hajamuona Baba yake, Babu alijaribu kumshawishi Akwelina ili aingie ndani kutokana na baridi kuwa kali bado haikusaidia kitu. Baada ya masaa mawili kupita Kakinga alifika nyumbani akiwa amechoka sana siku hiyo , Akwelina alipomuona Kakinga alimkimbilia akamkumbatia , Kakinga akamuuliza Akwelina : Umekula binti yangu ?
Akwelina alijibu : Mama yangu yupo wapi Baba niruhusu kidogo tu nikamuone tafadhali nakuomba .
Kakinga alichukia sana akamjibu Akwelina kwa jazba na kwa sauti ya juu : Mimi ndio MAMA na BABA yako hakuna mwingine sihitaji uniulize tena hilo swali umenielewa ? Nenda ndani haraka ukalale kila mda Mama , Mama sasa kama hayupo Mimi nifanyaje ? Nenda ndaniii ??
Akwelina alilia sana baada kuona Baba yake anamkaripia, Kakinga alimuonea huruma Akwelina akambembeleza na kusema : Usijali mtoto wangu Mama yako atakuja siku moja sawa , Nisamehe kwa kukuogopesha mtoto wangu acha kulia Mama angu futa machozi .
Akwelina alimsikiliza baba yake akaacha kulia wakaingia ndani pamoja na Babu. Asubuhi na mapema palipo pambazuka Monna alikuwa katika Chumba alichofungiwa , Chumba hicho kilikuwa na mateso makali sana , Monna akiwa amechoka walikuja wanajeshi watatu wakamfunga kitambaa Monna kwenye macho alafu wakaondoka nae, baada ya hatua kadhaa walimfungua kitambaa kile Monna alijikuta yupo katikati ya watu wengi sana mfano wa Gereza, Monna akiwa bado anashangaa mazingira hayo alishikwa mkono alipogeuka alimuona Mama wa Akwelina , Mama huyo alimvuta Monna pembeni kisha akasema : Samahani mdogo wangu mtoto wangu niliyekupatia yupo hai na kama yupo hai ni mzima ? Daah masikini mtoto wangu ??
Monna alijibu : Yupo hai mtoto wako na anaitwa AKWELINA .
Mama alitokwa na machozi ya furaha akasema : Daah ahsante Mungu kumbe mtoto wangu mzima jamani ??
MONNA : Acha kulia mwanao ni mzima kabisa naomba nikuulize kwani ilikuaje na kwanini nilikukuta msituni na ukaamua kunipatia mtoto wako na hapa ni wapi ?
Mama alifuta machozi kisha akasema : Daah ni stori ndefu sana nakumbuka miaka kumi iliyopita nilikuwa ......
MAMA ?? Daah ni stori ndefu sana nakumbuka miaka 10 ( kumi ) iliyopita nilikuwa naishi na mume wangu #Steven maisha yetu yalikuwa yenye furaha na amani mume wangu alikuwa anapesa sana japo sikutambua anafanya kazi gani inayompatia pesa nyingi kama alizokuwa nazo, sikuhitaji sikuhitaji kumfatilia sana kwakua nilimuamini sana mume wangu. Siku moja mume wangu alikuja na Julius huyu ambaye ndio mmiliki wa eneo hili kwa sasa, Julius alikuwa mdogo wa mume wangu siku hiyo nilikuwa chumbani nikasikia wanatupiana maneno makali , baada ya muda mfupi nilisikia mlango unafungwa kwa nguvu nikatoka nje nikamkuta mume wangu peke yake akiwa na mawazo sana nilipomuuliza alinijibu “” Amechoka kufanya unyama kwa watu wasio na hatia “” ukweli sikuelewa anamanisha nini ikabidi nimuulize akasimama akaniambia
“” Leo mke wangu nahitaji utambue ukweli kuhusu Mimi lakini naomba usinichukie kwa ukweli wangu “”
Mume wangu alisimama akavua shati lake akanionesha alama iliyokuwa kwenye bega lake alikuwa ameandikwa neno #AKWELINA sikutambua neno lile lilikuwa na maana gani na kwanini alinionesha ile alama , Baada ya kunionesha aliniambia nikae chini kisha akasema
“” Mke wangu hili neno ni jina la…
“””” Nani monna hapa “” Monna na mama wa akwelina Walistuka baada ya askari mmoja aliyekuja akauliza jina la monna .
“” Ni Mimi hapa “” Monna alimjibu yule askari , yule askari alimchukua monna akaondoka nae. Monna alikasirika sana kwa sababu alitamani kujua mengi toka kwa mama wa Akwelina. Monna aliondoka na yule askari hadi ndani ya Chumba kimoja katika eneo hilo, Monna alipofika aliwakuta watu wengi sana wakiwa busy na computer ( kompyuta ) wakati anatazama huku na huko alimuona Patrick mbele yake hakutambua amekujaje mbele yake , Patrick akasema :
PATRICK ?? Oooh mrembo kipenzi changu wa zamani najua hujui kwanini upo hapa sio ?
MONNA ?? Ndio sijui hilo alafu samahani Mimi sio mpenzi wako bora kifo kuliko kuniita hivyo nakuchukia sana wewe mshenzi .
PATRICK ?? Hahaha tuliza hasira binti nimekuita hapa kuna kitu nahitaji kukuonesha muda huu upo tayari hebu tazama hapa katika computer hii unaona nini ?
Moyo wa monna ulipatwa na mshituko wa ajabu sana baada ya kumuona Kakinga akiwa anacheza na binti mdogo bila shaka monna alitambua yule ni akwelina monna alianza kutetemeka na kujiuliza maswali mengi kakinga yupo wapi hapo na wamewezaje kumuona. Kipindi monna anajiuliza maswali