Simulizi: Anguko La Aibu

Simulizi: Anguko La Aibu

Stavros Myles

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2020
Posts
350
Reaction score
390
ANGUKO LA AIBU
Mwandishi: Duarte
Simulizi Fupi.






"Nina imani na wewe. Nategemea mrejesho mzuri" aliongea Mr.Deus na kukata simu. Mr.Deus alirejea chumbani kwake ambako hawali alimwacha mkewe ambaye kwa muda huu alikuwa amelala.


"Mke wangu, mke wangu!" Mr.Deus alijaribu kumuita mkewe ambaye alikuwa amejisokomeza kwenye blanketi zito.


Baada ya kuona mkewe alikuwa na usingizi mzito, Mr.Deus alisogelea kabati kubwa la nguo lililokuwa chumbani humo. Dakika tano zilimtosha kuchagua koti zito la baridi ambalo alivaa na kuotoka chumbani.



"Akiamka mama utamwambia nimetoka, sawa?" Aliongea Mr.Deus alipokutana na dada wa kazi aliyekuwa anatazama runinga majira yale ya mchana.
Hali ya ubaridi ilifanya mwezi huu wa sita kuwa mwezi wakujijazia mwilini, yaani bila kuvaa nguo nzito isingewezekana kutembea kabisa.



New Corner Hotel

Gari nyeusi aina ya Klugger V ya Mr.Deus ilifunga breki katika maeneo ya kupaki magari. Baada ya kushuka garini Mr.Deus alivaa miwani na kuanza kupiga hatua kusogelea sehemu ya mapokezi.

Ukubwa wa hoteli hii iliyokuwa ikipatikana maeneo ya Forest mpya jijini Mbeya iliwafanya watu wengi wapende kufika mahali hapo.

"Ni chumba namba 507, fungui zako hizi hapa.Panda lift hiyo then utabo....." Kabla hata dada wa mapokezi hajamaliza kutoa maelekezo Mr.Deus alianza kuzipiga hatua zake taratibu akiwa anaisogelea lift ile.



"Halo! nakuhitaji nyumbani.Kuna jambo la msingi tujadiliane....., hela hipo mzee" Docho alikata simu na kuisogelea sigara yake ambayo muda huu ilikuwa imeanza kuisha baada ya kuachwa bila kuvutwa kwa kitambo kidogo.


Nyumba ya Docho ilipambwa na picha za wanawake wakizungu waliopiga picha za utupu. Hali ya kutokuwa na mpangilio ndabi ya sebule ilikuwa inasawili hali yake ya kutokujipenda. Hata kama angetaka angeanzia wapi kufanya usafi?, Labda ingemchukua hata wiki kutoa taka alizokuwa akiziswaga chini ya Uvungu.





Chumba 507

Mr.Deus alikuwa uchi wa mnyama akimtazama binti mbichi wa miaka 23, mwanafunzi wa chuo cha uhasibu. Tamaa ya kuburungushana kwenye shuka za kitanda imara cha mninga zilikuwa zinapanda kila dakika.

"Njoo sasa kwani unatoa nguo mwaka mzima" binti aliongea kwa mapozi akiwa anamtazama Mr.Deus.




Nyumbani kwa Docho

"Sasa hii kazi nataka unilipe mapema kabisa, sio unaanza kuniruka mwishoni" Hassan aliongea akiwa anamtazama Docho kwa jicho la aisee-tutatifuana-hapa.

"Sasa wewe umefika muda mchache tu unaanza kukoroma kuhusu pesa, vipi umeambiwa utatapeliwa?" Docho aliongea kwa jazba.

"Chukua kwanza 'advance' " Docho aliongea baada ya kumtupia bunda dogo la hela alilolitoa kwenye kabati. "Tukimaliza nitakuongezea, kazi yenyewe rahisi mno" .







'Piii Piiii" Hii ilikuwa ni sauti ya honi aliyokuwa akiipiga Mr.Deus nje ya geti la Nyumba yake, mlinzi alisogelea geti na kutazama kwenye kadirisha kadogo kujua nani alikuwa akipiga hodi.


Ndani ya gari Mr.Deus alichomoa laini kutoka kwenye simu yake kubwa na kuiweka kwenye soksi ya mguu wa kushoto.


"Vipi nyumbani mko salama kabisa?" Aliongea Mr.Deus akiwa anakaribia mlango wa sebuleni alipotazama na mlinzi wake. Kwakuwa yalikuwa majira ya saa 4 usiku Mr.Deus alikuta chakula kikiwa mezani alikifuata na kula vijiko vichache na kutokomea bafuni.




"Kulikoni mwenzetu?, mbona ghafla tu umekimbilia bafuni, leo ndo umechoka sana au?" Mke wa Mr.Deus aliongea akiwa ameuegamia mto wa kitanda.


"Hapana mke wangu, ila nimeona tu niwahi kuoga ili nilale mapema nimechoka sana aisee" Mr.Deus aliongea na baada ya kumaliza kuvaa pajama alisogelea kitanda na kulala.Mbilinge mbilienge alizozipata kutoka kwa bibti mbichi wa chuo zilimfanya achoke vilivyo, mifupa yake ya uzee ilifanya kazi nzito.

"Sasa sijui ingekuwaje kama nisingepaka vumbi la kongo" alijisemea kichwani mwake na kisha kutabasamu.


Margaret ambaye ndiye aliyekuwa mke wa Mr.Deus aliwahi kuamka siku iliyofuata, kwakuwa ilikuwa ni siku ya Jumapili alijiandaa kuenda ibadabi. Baada ya kupata kifungua kinywa Margaret aliisogelea gari yake na kuwahi kanisani.


Mr.Deus yeye alivyoamka alielekea bafuni akaoga na kupata kifungua kinywa pamoja na wanawe wawili wakike, Joan na Jackline ambao walikuwa ni mapacha.


Akiwa njianiMaragaret aliamua kuegesha gari kando ya barabara kuu ya kuelekea Kabwe akitokea ilipokuwa nyumba yake na mumewe maeneo ya Iwambi.

"Binti mwenyewe huyu hapa bosi.Video zake akiwa na mumeo hizi hapa nimezituma"

Ujumbe huu uliingia kwenye WhatsApp, Margaret alijikuta anaishiwa nguvu baada ya kuziona picha za utupu za mumewe na binti mdogo zilizorekodiwa hotelini kwa kamera iliyotegeshwa.

"Halo!, hizo video nitumie zote.Na usiitume hata video moja mtandaoni nitajua jinsi ya ku 'deal' na mume wangu. Halafu huyo binti uniletee nyumbani kwangu majira ya saa 10" aliongea Margaret na kisha akaendelea na safari ya kuelekea ibadani.


Mr.Deus naye alielekea ibadani kwenye misa ya mchana akiwa na wanae wawili.


"Mume wangu wapeleke watoto kwa ba' mdogo wao wakamsalimie. Jana aliniomba waende"
ujumbe huu ulisomeka kwenye simu ya Mr.Deus akiwa anatoka ibadani na wanawe.



"Hapana shemeji mi' nawahi mahali.Nitakula siku nyingine mbona hapa nyumbani kabisa" aliongea Mr.Deus akiwa anaaga na kutoka nje ya nyumba ya mdogo wake.


Safari yake ya taratibu ilimfanya apitie kwenye Pub moja maarufu.

"Nipo hapa Katrina Pub. Upande wa nyuma" Mr.Deus alikata simu baada ya kumaliza kuongea na Docho.


Muda mchache mbeleni Docho aliwasili mahali hapo akiwa peke yake "Kama tukivyokubaliana.Mhusika yupo kwenye gari" aliongea Docho kwa bashasha.


"Tulia hivyo hivyo kijana!" Aliongea Hassan aliyekuwa kwenye gari ya Docho akimlinda kijana mdogo wa miaka 25 au 27.


"We unatafuna mali za wakubwa, hauoni wanaojiuza huko mitaani?" Hassan aliongea kwa jazba na kumtuliza kijana yule kwa kofi zito lililomtoa mawenge.



Docho akiwa na Mr.Deus na kijana yule walipanda gari kwa pamoja kurejea nyumbani kwa Mr.Deus. Hassan yeye alibaki Pub akiendelea kugida Bia na nyama choma.


Ilikuwa majira ya saa kumi na moja Mr.Deus alivyokuwa analifikia geti la nyumba yake. Mapigo ya moyo yalikuwa yanamuenda mbio lakini aliona ni bora aongee ukweli mbele ya mkewe kwanini anamsaliti na vijana wa hovyo kiasi kile.


Mr.Deus alikuwa wa kwanza kuusukuma mlango wa sebuleni.Macho yake yalipotazamana na binti aliyekuwa naye hotelini aliishiwa nguvu, kwa taratibu aliifuata sofa na kukaa. Mahtuko sasa ukaamia kwa Margaret alimuona James, kijana ambaye alikuwa akitumbua naye raha kwenye mahoteli ya jiji la Mbeya. Hata ile mvinyo aliyokuwa anainywa ilimpalia kwa ghafla tu.


MWISHO
 
Mr.Deus alikuwa wa kwanza kuusukuma mlango wa sebuleni.Macho yake yalipotazamana na binti aliyekuwa naye hotelini aliishiwa nguvu, kwa taratibu aliifuata sofa na kukaa. Mahtuko sasa ukaamia kwa Margaret alimuona James, kijana ambaye alikuwa akitumbua naye raha kwenye mahoteli ya jiji la Mbeya. Hata ile mvinyo aliyokuwa anainywa ilimpalia kwa ghafla tu.
Kwahio ngoma droo!
 
Back
Top Bottom