Simulizi : Any solution

Simulizi : Any solution

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Simulizi hii inaletwa kwako kwa hisani ya binti wa kiroho wa pastor Anni Kaleb.

Shuka nayo kama binti anavyomsimulia mamaye wa kiroho......

Pastor Anni acha Leo nikupe story ya Ndoa yangu ucheke maana unaomba sana Mama yangu leo ufurahi kidogo.

Pastor Bwana Mimi kiufupi sijasoma, niliishia darasa la saba ile ya kijijini na shule yetu hakuna aliyeenda secondary wazazi walikuwa hawana uwezo, kiufupi kingereza nilikuwa sijui kabisaaa zaidi ya "What my name, Yes, No, ok, yaaah hapo ndio nimemaliza. Nikawa najishughulisha na kilimo basi.

Sasa siku moja akaja Mkaka kutoka Dar anaitwa Hillary, yeye ni muuza mitumba hapo Ilala, na anajua kuvaa haswa. Akaanza kunitongoza kwa kingereza jamani nilichanganyikiwa aisee, Basi utakuta ananiambia I love you Baby, Mimi nacheka tu mara anasema ukiwa na SOLUTION yoyote wewe niambie tu, nikamuuliza SOLUTION ni nini akasema tatizo au shida kwa kizungu, nikasema sawa. Kwahiyo akinipigia simu ananiuliza ANY SOLUTION namwambia NO, ananiambia usiogope any solution niambie tu fresh. Tukaanza mahusiano akasema anataka kunioa.
Basi nikaenda kwa wazazi kuwaambia nimepata mchumba katoka Dar wakasema sawa aje. Basi siku mchumba anakuja kaulamba hatari na ananukia huyo, na kingereza chake kama kawaida. Basi Baba akamuuliza umempendea nini mwanangu huko Dar hujaona wanawake? Bwana weeh si akajibu nimempenda kwasababu YUKO TAKE CARE SANA, YANI YUKO MAKINI 🤣🤣. Wazazi nao kingereza hawajui wajashika tu hiyo YUKO TAKE CARE SANA, basi akatoa mahari akasema atanitumia nauli nimfwate Dar.

Basi baadae akatuma nauli nikaja Dar, Pastor nimekuja mshamba sijui kusoma sijui chochote niponipo tu. Jamaa akipokea simu anaongea kingereza tu sasa Mimi sielewi. Akaanza tabia ya kurudi usiku sana huku kalewa, na siku zote akipigiwa simu anaongea kingereza Mimi sielewi kitu. Siku moja nikasikia anasema neno Dear Dear, nikamuuliza Dear ni nani akasema Dear kwa kiswahili ni mfanyabiashara mwenzangu, ndio tunaitana Dear nikasema sawa. Lakini nikasema hapana mbona huyu Dear kama mwanamke, nikahisi kunakitu.

Basi siku nikasubiri usiku kalala nikachukua simu yake weeeh nakuta message za kizungu tu jamani sielewi ila nilihisi kuna kitu. Sisi tulikuwa tunakaa na mjumbe alikuwa jirani yetu na Mke wa mjumbe tulizoeana, nikafwata Mke wa mjumbe nikamwambia Mume wangu anarudi usiku kalewa na akirudi anachat sana kingereza Mimi sielewi, akasema usijali mjumbe ni msomi na ashapitia mpaka Jeshi chukua karatasi andika hayo maneno halafu tutampa atutafsirie. Nikasema sawa maana Mke wa mjumbe na Yeye hajasoma kabisaaa haelewi kitu hata kuandika hawezi bora Mimi.

Basi usiku kama kawaida yule Bwana alirudi kalewa akaanza kupiga simu zake sijui Dear nini nini huko nikasema sawa leo ndio mwisho wako. Nikamsubiri alale nikaamka nikachukua simu na peni na katatasi nikaanza kuandika yale maneno ya kwenye message nimpelekee mjumbe msomi mwanajeshi mstaafu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣


Basi Bwana Mimi nikacopy maneno yote na mbaya zaidi walikuwa watu kama wawili tofauti anachat nao kingereza. Nikacopy nikalala, asubuhi kama kawaida anaongea na simu Yes Dear mara My heart Mimi nasikiliza tu my Heart tena. Alivyoondoka tu Mimi mbio kwa mjumbe, kufika kule nikamuonyeaha mke wa mjumbe akaniambia ngoja nimuamshe Mzee aje. Basi kidogo mjumbe akaja nikamuelezea hali halisi nikampa katatasi asome, kasoma weeeh, akaniambia unajua Sisi tumesoma Elimu ya Muingereza kingereza chetu ni cha Muingereza ila hawa wanatumia kingereza ya Mmarekani ni tofauti. Vingereza vimetofautiana sana, cha kimarekani na kingereza tofauti kabisa, kwahiyo hapa Mimi kingereza cha kimarekani sielewi ila cha Muingereza aaahh faster. Nikaona shughuli ishakuwa ngumu nikaondoka.

Nikakumbuka Nina mjomba wangu yuko hapa Dar anafanya shughuli za ulinzi, aliniambia ameanza masomo ya Form one mpaka form four kwa miaka miwili. Nikamwambia akasema sawa niandikie hiyo message fupi nisome. Mjomba nae hajui kitu ndio kumpelekea Mkewe, Mke wa mjomba akanipigia mwanangu achana na mjomba wako kwanza masomo yale kafeli hajui kitu, uje basi tuonane unionyeshe.
Nilihangaika wiki nzima na karatasi langu sijapata msaada.

Mke wa mjomba Yeye kasoma kidogo mpaka Form Four, anauelewa kuliko mjomba. Nikamuonyesha akaniambia huyu ni mchepuko wake haswa huyu ni mwanamke wake, aisee nikaumia sana. Akasema leta namba tumchambe hapa. Basi akachukua namba tukatumia message

HABARI, UNAMJUA HILLARY?
"AKAJIBU I DON'T UNDERSTAND SWAHILI"

TUKAMJIBU HILARY AND YOU WHAT WRONG

"NOTHING NOTHING WHO ARE YOU"

NIKAMWAMBIA MY WIFE OF HILARY, PLEASE STOP CALL HILARY NO MESSAGE NO PHONE I WILL KUKUROGA
HAKUJIBU TENA

Jioni yule Bwana karudi kakasirika kwanini unasumbua watu wangu, nani kakufundisha kuandika, nikamwambia najua kuandika Mimi sio mshamba kiasi hicho. Weeeeh akaanza kunipiga, alinipigia usiku kucha akaniumiza asubuhi nikatoka nikaenda kwa mjumbe, mjumbe akasema tumpeleke kwa mtendaji hii ni kesi maana aliniumiza usoni. Mtendaji akasema aitwe akaitwa kuja Mimi nikaanza kuelezea ndio kutoa lile karatasi kumbe mtendaji kasoma bwana na kingereza kinapanda, weeeh si akaanza kutafsiri neno moja moja. Jamaa Alikuwa mdogo balaa.

Mtendaji Akasema Huyu mwanamke wako na ni Mke wa Mtu, na umemwambia Mkeo ni mshamba hajui kingereza kwahiyo tuwasiliane kingereza. Pili huyu mwanamke mwingine ni mzazi mwenzio umezaa nae, mnaulizana habari za maendeleo ya Mtoto na kutuma matumizi. Mimi ndio kushangaa waaaah ana Mtoto?

Mtendaji kwani hujamwambia mwenzio kuwa una Mtoto? Akamuuliza Kwanini umpige Mtoto wawatu wakati unajua kabisa wewe ndio umekosea. Basi nikaanza kulia nikapigia wazazi wangu, wazazi wakasema Binti yetu arudi, basi yule bwana ndio kuanza kuomba msamaha, nisamehe Mke sitarudi tena.
Akakiri pale ni kweli nina mwanamke nimezaa nae lakini simpendi ndio maana sikumuoa. Nikamuuliza mbona hujaniambia kama unamtoto, ulisema huna Mke huna Mtoto ndio maana nilikukubalia. Akaomba msamaha pale, akalipa fine na hela ya matibabu.
Mtendaji akasema nendeni ila ukikuta ujumbe wowote wa kingereza ulete nikutafsirie.

Pastor nikasema hapana huu ujinga siutaki, unaweza kuuzwa huku unajiona. Nikatafuta darasa la kingereza nikaanza kusoma sasa hivi angalau naelewa na ananikoma aisee hakuna kitu sielewi. Ndio nimejua hata yeye kingereza hajui ni broken tu hamna kitu mshamba tu, niliingia kichwa kichwa.

HAYA JAMANI MCHEKE KIDOGO, NDOA HIZI ZINA MENGI SANA.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Ubarikiwe
 
Huu ni uchoko tu kubwa zima hovyo huna akili tena ukute una watoto waliokuzidi hekima na stara.

Kunywa bia ulale stupid 🚮
 
Back
Top Bottom