Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Tano 13
Roda akabaki mdomo wazi,, akainamisha uso wake akalitazama tumbo lake,, akajisemea moyoni,, “Mungu wangu inamaana Tobi ni jini? Pia alikuwa akiniingilia kimwili miaka yote hiyo? Sasa nimepata jibu la swali nililokuwa najiuliza kila siku, kwa nini kila nikiamka usingizini nakuta sehemu zakungu za siri zimelowana,kumbe ni Tobi,
Nini hatma yangu? Roda alijisewmea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu…,kumbe tarehe za kujifungua zilikuwa zimetimia,,, punde si punde akaanza kuhisi maumivu makali chini ya kiuno, pamoja na mgongoni!! Maumivu hayo yalikuwa makali kupita kiasi,, yakahamia tumboni Roda akajikuta anashindwa hata kusimama,
Wakati huohuo,,upande mwingine, lilionekana gari likiendeshwa kwa mwendo wa taratibu,, ndani ya gari hilo walikuwemo watu wawili,, mke na mume! Watu hao walikuwa wamepotea njia,, kwa sababu ni wageni maeneo hayo,, walikuwa wanamtafuta ndugu yao aliyekuwa anaumwa kwa kipindi kirefu,, punde si punde Tobi akajitokeza kimiujiza ndani ya gari hilo! Akabadilisha mawazo ya dereva huyo pasipo yeye mwenyewe kujionyesha,
Tobi aliamua kufanya hivyo ili dereva huyo akamsaidie Roda,, kumpeleka hospitali,,kisha akatoweka kimiujiza,,, punde si punde dereva wa gari hilo akaamua kukatisha kona na kuifuata barabara ya vumbi!!
Kwa mbali akaona nyumba,,,akaamua kuifuata nyumba hiyo,, alipofika akashuka na kugonga hodi,,
Wakati huo Roda alikuwa anatambaa utadhani mtoto mdogo,, huku akihisi maumivu makali kupita kiasi, (uchungu wa mimba) Roda akasikia mlango unagongwa, akaingiwa na matumaini ya kupata msaada wa kupelekwa hospitali.. akajaribu kulaza sauti huku akisema,, “FUNGUA MLANGO UPO WAZI, yule dereva akastushwa na sauti hiyo!
Akajisemea moyoni bila shaka mtu huyu ni mgonjwa,,
Dereva huyo hakujali,, akafungua mlango alipoingia upande wa ndani ya nyumba akashtuka kumuona Roda akiwa anatambaa huku machozi yakimtoka,,
Roda akasema naomba msaada nipeleke hospitali tafadhali nahisi uchungu wa mimba!
Dereva huyo akamnyanyua Roda na kutoka nae nje ya nyumba,, akamuingiza ndani ya gari,, mke wa dereva huyo akaingiwa na roho ya huruma akasema,,”najua unapata maumivu kupita kiasi kwa sababu hata miminpia nina watoto.. uchungubwa mimba unatesa kupita kiasi.. jikaze.. wakati anaongea maneno hayo,, dereva alikuwa tayari ameshaliondosha gari,,
Wakiwa njiani Tobi akajitokeza ndani ya gari,, Roda akamuona Tobi kaketi kando yake,, lakini dereva pamoja na mkewe hawakuweza kumuona Tobi, Roda akasema,, “haya yote umeyasababisha wewe,,, tazama ninavyoteseka! Kwa nini umenitenda hivi?
Yule dereva pamoja na mkewe wakastaajabu,, kila mmoja akabaki anajiuliza anaongea na nani?
Wakati huo Tobi alikuwa anatabasamu,, huku kashika viganja vya mikono ya Roda,
Tobi akasema,, “usiogope,, mimi ndiye mwanaume ninayekupenda na wewe ndiye mama wa mtoto wangu,, Roda akajibu,, lakini wewe ni jini,
Mke wa dereva akamwambia mume wake,, huyu anaongea peke yake,,ni mimba ndiyo imemchanganya,, huwa inatokea kwa mama mjamzito,
Safari iliendelea,, hakuna aliyetambua Roda anaongea na nani,, walihisi ni uchungu wa mimba tu inamchanganya! /
Baada ya dakika kumi kupita wakafika hospitali.. Roda akapokelewa haraka akaingizwa kenye wodi maalumu ya wazazi,,,
Roda akaandaliwa kwa ajili ya kusukuma mtoto atoke tumboni…
Alisukuma kwa muda mrefu lakini ikashindikana,,
Punde si punde Tobi akajitokeza ndani ya wodi hiyo,,Roda akashtuka kumuona Tobi.. alipojaribu kuongea na Tobi,, sauiti haikutoka Roda akawa kama bubu!
Tobi akafumba macho yake,, ishara ya kuwasiliana na mama yake,(Malkia wa bahari)
Ili apewe maelekezo jinsi ya kumchukua mtoto,,, malkia wa bahari akasema,, usichelewe ndani ya sekunde tatu.. mtoto atakapotoka tumboni… endapo utachelewa basi mtoto huyo atakuwa binadamu wa kawaida,, hatoweza tena kuwa jini! Hivyo tutakuwa tumepoteza aseti,, na mtoto huyo ni muhimu kwetu..
Tobi akafumbua macho baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Malkia wa Bahari.
Wakati huo huo zikasikika sauti za manesi wakimuhimiza Roda asukume bila kubana miguu ili mtoto atoke akiwa hai.
Punde si punde akaingia nesi mwingine.. nesi huyo alikuwa na uwezo wa kuona majini pasipo kudhurika na chochote,, pia majini walikuwa wanamuogopa sana mtu wa aina hiyo! Nesi huyo alikuwa na pete maalumu aliyoachiwa na marehemu bibi yake,, pete hiyo ni adui mkubwa wa majini.. Tobi akashtuka kumuona nesi huyo!
Punde si punde,, ikasikika sauti ya mtu,, akimuita nesi,, aliyekuwa anaingia ndani ya wodi hiyo ya wamama wajawazito. Nesi huyo akaamua kufunga mlango na kurudi upande wa nje! Kumba daktari ndiye alimuita nesi huyo,, ampe maagizo juu ya jambo fulani.
Kule ndani ya wodi,, Tobi akaanza kuwa na wasiwasi kupita kiasi! Akajisemea moyoni,, “huyu nesi anakitu ambacho ni adui wa majini,, na kama akirudi humu basi mpango wangu utavurugika,, na sijui kama mama(Malikia wa majini )atanielewa!
Wakati huo Roda alikuwa anafanya jitihada za kusukuma mtoto huku manesi wakimuhiziza,, asukume bila kukata tamaa,, endapo ataacha kusukuma atambana mtoto hivyo mtoto huyo atakufa! Roda alijitahidi kusukuma,,
Manesi waliokuwemo ndani ya wodi hiyo,, hawakuwa na uwezo wa kumuona Tobi,, pia sasahivi Tobi hakutaka kujionyesha machoni mwa Roda,, Tobi akajisemea moyoni,, “wacha nifanye jambo fulani,, ili mpango wangu ukamilike.,,,,baada ya kuwaza hivyo akatoweka kimiujiza! Akajitokeza kwenye korido inayokwenda kwenye wodi!! Akuona yule daktari aliyempa maagizo yule nesi mwenye uwezo wa kuona majini!
Tobi akamfuata daktari huyo,, alipomuongelesha tu,, akili ya daktari hiyo ikabadilika,, akazipiga harakaharaka kutoka kwenye kordo hiyo na kuezlekea nje kabisa,,, kwa mbali akamuona yule nesi anarudi,, ni baada ya kumuagiza akalete taarifa ya maendeleo ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi nyingine,, tofauti na wodi ya wamama wajawazito…. Daktari huyo akaendelea kuzipiga hatua mpaka akamkaribia nesi huyo,, kisha akamuagiza kuwa aende kwenye maabara akalete test tube.
Nesi huyo akaondoka zake kuelekea maabara.
itaendelea