Simulizi - change (badiliko)

CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

TANGAZO: Nimebadili namba ya WhatsApp, sitapatikana kwenye ile ya mwanzo tena, bali sasa nitapatikana kwenye hii +255 678 017 280. Karibuni.

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Efraim Donald akashangazwa na jambo hilo na kumshika Namouih mabegani, aliyekuwa ameachama huku pumzi zake zikiongezeka kasi zaidi.

"Nini Namouih?" Efraim akamuuliza.

"Ahh... a... aahaaaaah!" Namouih akaanza kulia kwa sauti ya juu sana.

Efraim Donald akamwahi kumshikilia kwa kuwa mwili wake ulishuka chini kwa njia iliyoonyesha ameishiwa nguvu. Mwanamke huyu akaendelea tu kulia kwa uchungu, na Efraim akiwa haelewi sababu, ikabidi aivute simu yake hapo chini na kuangalia kama aliyepiga bado alikuwepo, naye akaiweka sikioni baada ya kuona bado Blandina alikuwa hewani. Akamuuliza tatizo lilikuwa nini, naye Blandina akasema ndiyo alikuwa amepata taarifa za mauaji ya rafiki yao wa karibu sana, yule mpelelezi aliyeitwa Felix Haule. Efraim Donald alimfahamu pia, na alijua Felix alikuwa mtu muhimu
sana kwa mke wake kama ilivyo Blandina tu, naye akampa Blandina pole na kusema angehitaji kumtuliza mke wake kwanza maana alikuwa ameishiwa nguvu kwa sababu ya taarifa hiyo.

Jambo jipya likawa limezuka. Felix Haule alikuwa ameuawa, na zilikuwa ni taarifa zilizomshtua sana Namouih hasa ukitegemea na ukweli kwamba walikuwa wametoka tu kuonana siku hiyo hiyo iliyopita, maana hii tayari ilikuwa ni siku mpya. Efraim Donald akamkumbatia mke wake wakiwa hapo chini, akimbembeleza kwa upendo na kumwambia aendelee tu kulia ili autoe uchungu wake wote, na ndipo hodi ikasikika nje kwenye mlango wa chumba chao. Efraim tayari akiwa anajua ni Esma, akamwambia aingie tu, na mwanadada huyo akaingia na kuwasogelea huku akiwa na sura
iliyoonyesha kujali sana. Efraim Donald akamwambia kwamba Namouih amefiwa na rafiki yake wa
karibu sana, naye Esma akashuka hapo chini na kumshika Namouih begani kwa huruma.

Baada ya dakika chache Efraim akajitahidi kumnyanyua mke wake na kumpeleka kitandani, akiwa
anamtia moyo na kumbembeleza, na Namouih alikuwa analia bado huku amemlalia Efraim kifuani. Esma akawa ameondoka baada ya Efraim kumwambia akapumzike tu ili asubuhi waanze kufanya mipango ya kwenda kukutana na familia ya Felix. Namouih akawa analia kwa sauti ya chini kadiri muda ulivyoendelea kusonga, mume wake akiwa amemkumbatia kitandani na kumpa faraja kwa kutembeza kiganja chake kwenye nywele zake taratibu mpaka Namouih alipobebwa na usingizi
ilipofika saa kumi usiku. Yaani mwanamke huyu alikuwa amelia kwa masaa mawili mfululizo, kwa sababu jambo lililokuwa limetokea lilimtia huzuni kuu moyoni kwa kuwa tayari alikuwa ameshapigia picha ni nini kilichomsibu Felix ingawa hakuwa na taarifa kamili. Ingetakiwa kusubiri kukuche ili kujua mwanaume yule alipatwa na masaibu gani, na baada sasa ya Namouih kusinzia, Efraim Donald
akautafuta usingizi pia.


★★★


Siku ikakucha zaidi. Hii ikiwa ni Jumapili, Efraim Donald na Namouih waliamka na kuanza kujiandaa ili kwenda nyumbani kwa Felix pamoja na Esma pia. Namouih alikuwa ameamka saa mbili tu, na kwa sababu ya huzuni alishindwa kuhisi lepe lingine la usingizi ingawa alilala kwa masaa machache. Efraim akawa amemtia moyo tena kwa kuwa alifahamu jinsi mambo haya yalivyomtikisa sana mke wake, na Namouih kiukweli alikuwa ameishiwa raha kabisa. Efraim
Donald akawa amewasiliana na Blandina, ambaye alimjulisha kwamba yeye pia alikuwa anaelekea
kule, hivyo wangeona jinsi mambo yalivyokuwa mpaka kupelekea kifo cha rafiki yao. Safari nzima ya kuelekea huko Namouih hakusema lolote lile ingawa Efraim alijaribu kumsemesha. Suleiman ndiye aliyewaendesha wote kwa gari la Efraim Donald na kuwafikisha mpaka upande wa mji ambako familia ya Felix iliishi kwenye mida ya saa sita mchana.

Walikuta watu wengi wakiwa wamekusanyika hapo nyumbani kwake na kufanya mambo kama jinsi taratibu za msiba zinavyokwenda, na baadhi ya marafiki na ndugu zao waliowafahamu Efraim na Namouih
waliwappkea na kuanza kufarijiana. Namouih akaelekea ndani ya nyumba pamoja na Esma, na huko alimkuta Blandina akiwa pembeni ya mke wake Felix, aliyeitwa Oprah.
Mwanamke huyo alikuwa analia tu kwa sauti ya chini huku akiwa ameketi kwa kuishiwa nguvu, na
binti zake wawili walikuwa karibu wakimpa faraja kwa kulia pamoja naye. Alikuwa na watoto watatu pamoja na mume wake marehemu; wa kiume mwenye miaka 14, na hao wasichana wawili mapacha wenye miaka 10. Mama yake mzazi na ndugu wa kiukoo walikuwepo hapo pia, na baada ya Namouih kumfikia akamkumbatia na kumfanya Oprah aanze kulia kwa uchungu zaidi. Walikuwa wanafahamiana na kupendana sana, naye Namouih akawa anamwambia maneno yenye kufariji huku naye akidondosha machozi, kisha akawakumbatia na binti zake Oprah. Mwana wake alikuwa mkoa wa mbali kimasomo na ndiyo alikuwa safarini wakati huu pamoja na mjomba wake kuja huku baada ya kupata taarifa za kifo cha baba yake, kwa hiyo alikuwa akisubiriwa pia.

Muda mfupi baadaye, Mwantum, yule mwanamke ambaye mume wake na mwana wake waliokoka ajali ya barabarani, akawa amefika hapo pia kutoa faraja kwa Oprah. Efraim Donald, Namouih na Blandina wakawa wametoka nje ili kuzungumza kidogo, kwa sababu Namouih alitaka kujua undani
wa kifo cha Felix kutokana na Blandina kusema kwamba "aliuawa." Taarifa alizokuwa amezipata ni
kwamba Felix aliuliwa usiku wa kuamkia leo, na mwili wake ulikuwa umepatikana ndani ya choo cha kulipia ambapo ulikuwa umekatwa tumboni na kunyofolewa ulimi. Namouih na Blandina walielewa wazi kwamba huo ndiyo mtindo ambao muuaji au wauaji wa wasichana wale wadogo walitumia, na Namouih akawaza kuwa kwa sababu Felix alikuwa anapeleleza jambo hilo
inawezekana alikuwa amekaribia sana kupata ukweli ndiyo maana akauawa namna hiyo.

Blandina alikuwa anaongea kwa huzuni sana, akisema anahisi hii kuwa ni ndoto kwa maana walikuwa wametoka kumwona tu saa chache walipokutana naye kwenye kumbi moja ya starehe kisha ndiyo akaja kupewa taarifa hizo baadaye usiku zilizomshtua sana. Namouih akamuuliza alikuwa na nani wakati alipomwona Felix, naye Blandina akajibu ni Draxton. Namouih akakunja ngumi kwa nguvu sana, akiwa ameingiwa na hasira nyingi kwa sababu alielewa kabisa kitu hicho kilihusiana moja kwa moja na kifo cha rafiki yake. Yaani, alijua na alijua kwamba ni Draxton ndiye
aliyemuua rafiki yake, na kutambua jambo hilo kukamfanya aanze kulia tena, lakini zamu hii kwa hasira. Efraim akajaribu kumbembeleza na kumwambia atulize hisia, lakini Namouih akaondoka tu hapo walipokuwa na kwenda kujifungia ndani ya gari lao.

Aliwaza mengi sana mwanamke huyu. Aliendelea kulia kwa uchungu mwingi sana kwa sababu ya kuhisi kwamba ni yeye ndiye aliyemsababishia Felix maafa hayo ambayo yalikuwa na athari mbaya
sana kwa familia yake aliyoiacha. Lakini kwa jambo hili asingekaa tu na kuendelea kulia, alitaka afanye yote kuhakikisha muuaji wa Felix analipia kwa ubaya huu alioufanya. Jinsi alivyowaona wengine wakiwa bila wazo lolote kumhusu mtu aliyehusika kulimuumiza sana, hasa Blandina, ambaye alimwona kuwa kipofu kwa kumwamini mwanaume yule mwenye roho ya kikatili. Hivyo
ndivyo Namouih alivyohisi, na sasa akawa amejiamulia kuwa ni lazima tu haki ingetendeka wakati huu tofauti na ilivyokuwa kwa Agnes.

Shughuli za msiba ziliendelea siku hii, na Namouih pamoja na wapendwa wake waliendelea kuwa
hapo mpaka usiku, kisha Efraim Donald akarudi nyumbani pamoja na Namouih. Mwili wa Felix ulikuwa mochwari, na ulifanyiwa uchunguzi na wengi wa wapelelezi waliofahamiana naye kubaini kile kilichompata, yaani muuaji alikuwa nani, lakini hakukuwa na jambo lolote lililowaongoza kwa muuaji huyo. Walijaribu kuchunguza eneo lile la choo cha kulipia, wakamuuliza aliyefanya kazi pale kuhusu watu walioingia na kutoka wakati ambao mwanaume huyo aliingia ndani ya choo hicho, lakini haingekuwa rahisi kwa mhudumu huyo kujua na kukumbuka watu walioingia na kutoka, kwa kusema kwa usiku ule watu walikuwa wengi, labda kama angewaona tena.

Hakukuwa na viambishi vyovyote kumhusu muuaji vilivyopatikana mwilini mwake Felix, lakini ilieleweka kwamba muuaji wake ndiyo yule yule aliyemuua Agnes pia, kwa kupenda kuwakata watu ulimi na tumbo. Ilikuwa inashangaza sana kwamba matukio haya yaliendelea kwa muda huu wote bila kubaini mhusika ni nani, kwa hivyo bidii ingehitajika zaidi ili kuzuia maafa hayo, na Namouih alikuwa ameazimia kuukomesha mchezo huu kwa sababu yeye tayari alimjua mlengwa wake.


★★★


Jumatatu ikafika. Namouih na Blandina wasingekwenda kazini siku hii, hata Efraim Donald pia. Walikwenda msibani tena, na wakati huu watu waliokwenda kutoa pole zao walikuwa ni wengi sana, kwa sababu Felix alijulikana kwa idadi kubwa ya watu. Mwanaye wa kiume alikuwa amekwishafika pia, na tayari matayarisho ya mwili wa marehemu yalikuwa yamemalizika kufikia muda wa saa tisa alasiri kule hospitalini, ukiwekwa ndani ya jeneza maridadi, kisha ungepelekwa hapo nyumbani, halafu ungelala ili kesho ndiyo usafirishwe kupelekwa mkoa aliozaliwa Felix ili kuzika. Familia yake ingekwenda huko, na walikuwa wameamua tu kumzika Felix mapema na kuendelea kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kifo chake.

Mwili ulipofikishwa nyumbani tena vilio vya huzuni vilitawala kutoka kwa familia ya mwanaume huyo, na ilimchoma sana Namouih kwa sababu ya hatia aliyohisi moyoni mwake. Aliona ni kama hakustahili kabisa kuwa hapo kwa sababu ya kuchangia kifo cha Felix, lakini hakuwa na namna ila kuwepo na kutoa mchango wake wa faraja kwa familia hii ya rafiki yake. Inafika saa kumi hivi jioni baada ya mwili kuingia nyumbani hapo ndiyo Namouih akapata kuliona gari lisilokuwa geni sana machoni mwake likifika maeneo hayo ya nje. Hisia kali zilianza kumwingia mwanamke huyu baada ya kumwona Draxton akitoka ndani ya gari hilo na kusimama karibu nalo, naye Namouih akasimama huku akimtazama kwa mkazo mkali.

Blandina alikuwa ameshamwona Draxton kule alikosimama, hivyo akamfata haraka na kumkumbatia huku baadhi ya watu wakiwatazama sana. Wawili hao wakaonekana wakiongea, naye Namouih akaanza kuelekea hapo walipokuwa akiwa anatembea kama mtu anayehisi baridi kali. Efraim Donald alikuwa anamwangalia mke wake na kuona jinsi alivyotembea, na kwa haraka
akawa ametambua kwamba kuna jambo halikuwa sawa. Akatoka sehemu aliyokuwa na kuanza kumfata pia. Namouih akawa amefika mbele ya Blandina na Draxton, naye Blandina akamgeukia
na kumwangalia kwa njia ya kirafiki usoni, lakini Namouih akawa anamtazama Draxton kwa mkazo
sana mpaka Blandina na Draxton wakatazamana kama kuulizana 'vipi?'

Blandina akamwangalia tena rafiki yake na kumuuliza, "Vipi Nam?"

Draxton akawa anamwangalia Namouih kwa umakini.

Kuna kitu fulani kuhusu namna Draxton alivyomwangalia Namouih kilichomtia hasira sana mwanamke huyu na kumfanya amsogelee karibu na kumwasha kofi zito usoni!

"Namouih!"

Blandina akaita hivyo akiwa ameshtushwa sana na kitendo hicho cha rafiki yake, na ni hapo ndiyo
Efraim Donald akawa amewahi na kumvuta mke wake nyuma kidogo. Blandina akamwangalia Draxton na kumwona akiwa ameinamisha uso wake kidogo tu, akitazama chini kwa njia ya kawaida, naye akamwangalia Namouih tena.

"Unafanya nini Namouih?" Blandina akauliza.

"Muuaji mkubwa wewe!" Namouih akamwambia Draxton kwa hisia.

Watu walioona jambo hilo wakaanza kusogea upande huu waliokuwepo.

Draxton akamtazama tena Namouih kwa umakini.

"Yaani wewe ni mfano halisi wa Shetani! Imekupa faida gani kumuua?" Namouih akasema huku
akijitahidi kujitoa kwenye mikono ya Efraim.

"Namouih... unatengeneza scene hapa... naomba tuondoke," Efraim Donald akamwambia hivyo
mke wake kwa kung'ata meno.

"Halafu unakuja kabisa hapa ili kuthibitisha nini? Kwamba hauhusiki au?" Namouih akasema kwa
hasira.

"Namouih..."

Akawa amefika mama yake Oprah hapo na kumwita hivyo, naye Namouih akamtazama.

"Nini kinaendelea hapa?" mama yake Oprah akauliza.

"Aa, samahani mama. Namouih hajisikii vizuri... Namouih, naomba tuondoke," Efraim Donald akaongea.

Namouih akajitoa mikononi mwa Efraim kwa nguvu na kusema,

"Mama, unamwona huyu
mwanaume? Usimwamini... yaani hapaswi kuaminiwa... ni huyu ndiyo amemuu...."

Kabla Namouih hajamaliza maneno yake, akashikwa mkono na Blandina kwa kugeuzwa, na alipomwangalia tu, Blandina akamtandika kofi usoni pia!

"Blandina..." Efraim akaita hivyo na kumshika tena Namouih.

Draxton akamsogelea Blandina na kumshikilia mikono pia kutokea nyuma.

Namouih akamwangalia rafiki yake kwa mkazo huku akiwa amejishika shavuni, naye Blandina alikuwa anadondosha machozi huku akipumua kwa hasira, na akimtazama Namouih kwa hisia kali
sana. Watu walikuwa wameanza kukusanyika zaidi hapo wasielewe kilichokuwa kinaendelea, naye
Efraim Donald akamtoa Namouih hapo kwa nguvu na kumpeleka garini kwao. Mama yake Oprah alikuwa anamtazama sana Draxton, na wakati huu mwanaume huyu alikuwa anamfuta machozi Blandina, kisha kwa kumkumbatia akaanza kuondoka naye kuelekea mpaka kwenye gari lake Blandina, akamsisitiza aingie tu na kuliwasha, halafu yeye Draxton angerudi kwenye lake ili waondoke hapo wakifuatana.
Baada ya Efraim Donald kumwingiza Namouih kwenye gari akampigia simu Esma, ambaye alikuwa ndani kule kwenye nyumba ya Felix, na kumwambia arejee kwenye gari ili waondoke. Efraim akawa amejishika kichwani huku amefumba macho yake kutokana na kutoamini kioja kilichokuwa kimetokea, kisha akamtazama mke wake na kumwona ameangalia upande wa kioo cha mlango wa gari huku analia kwa kwikwi. Alikuwa ameshindwa kuzizuia hisia zake pale na kusababisha picha mbaya sehemu ya msiba, lakini kiukweli roho ilikuwa inamuuma sana. Alikuwa amechoshwa na unafiki mwingi uliomzunguka, na tena na hapo alijua mwisho wa siku ni yeye ndiyo angeonekana mbaya. Blandina kumpiga kofi ilithibitisha hilo.

Safari ya kuanza kurejea makwao ikaanza baada ya Esma kufika ndani ya gari. Efraim Donald akamtazama mke wake kwa hisia, kisha akakishika kiganja chake kwa ustaarabu, naye Namouih akamwangalia. Mwanamke huyu alikuwa anamtazama mume wake kwa huzuni sana, naye Efraim
akamvuta kwake, akimlaza kifuani na kuanza kumbembeleza taratibu. Akawa anamwambia kwamba ingawa kitendo kile hakikuwa sahihi lakini alimwelewa vizuri, na zile zilikuwa ni hisia tu zilizopaswa kuongozwa vizuri kwa sababu zikizidi sana matokeo yake ndiyo yanakuwa hayo. Akamwambia aache kumlaumu Draxton hata kama alihisi vipi kwamba ni yeye ndiyo msababishi wa haya yote, kwa sababu hakuwa na ushahidi wa kuonyesha madai yake kuwa kweli. Hicho tu.

Wakaendelea tu na safari yao huku bibie akiendelea kubembelezwa mpaka walipofika nyumbani, naye Esma akaanza kuandaa masuala ya chakula kwa kuwa hawakula kule walikotoka. Lakini Namouih yeye akaamua kwenda kulala tu kwa kukosa hamu ya kula, na mume wake akamsindikiza chumbani mpaka mwanamke alipojilaza na kuanza kuutafuta usingizi ili ayakimbie kwa kitambo kifupi mambo yaliyotokea awali nyumbani kwa Felix.

★★

Blandina na Draxton walielekea mpaka pale alipoishi mwanamke huyu baada ya kuondoka kule
msibani kwa mtindo wa ukweli! Blandina alikuwa na huzuni sana, akihisi kama vile kilichotokea
pale msibani ilikuwa ni ndoto, kwa sababu hakufikiri kwamba Namouih angeweza kufanya jambo ile lililosababisha na yeye Blandina afanye jambo ambalo hakutaka kufanya. Draxton akaenda pamoja naye ndani, na alipotaka waingie sebuleni, Blandina akasema angependelea zaidi kulala chumbani, hivyo wakaenda wote, naye Draxton akajilaza kwa njia iliyomruhusu Blandina amlalie kifuani, na mwanaume huyu akawa anapitisha kiganja chake mkononi kwa mpenzi wake taratibu.

"Utakuwa sawa?" Draxton akavunja ukimya.

"Ndiyo... nafikiri nitakuwa sawa," Blandina akajibu kwa sauti ya chini.

"Samahani Blandina..."

"Samahani ya nini?"

"Kwa kilichotokea. Labda ingekuwa bora kama nisingekwenda pale."

"Hivi, Namouih ana tatizo gani na wewe? Jana... umeondoka, ukasema... mlivyoonana si yalikuwa
maongezi mazuri? Hayo anayoyasema yametoka wapi? Yaani me simwelewi Draxton kwa kweli.
Amenifanya nimefikia yaani...."

"Usiwaze sana Blandina... ni huzuni yake tu ndiyo...."

"Kwani sisi wengine hatuna huzuni Draxton? Lakini umeona mimi namfata mume wake na kusema
ndiyo amemuua Felix? Yaani yeye... anachofikiri ndiyo ukweli ndiyo hicho hicho, anataka sikuzote judgement yake ndiyo iwe sahihi tu... si vinginevyo. Isingekuwa ya wewe yule Japheth tungemfunga wakati hakuwa na hatia, na hapo Namouih bado angejiona kuwa sahihi kabisa. Ndiyo anachotaka kufanya na sasa hivi... kila kitu Draxton, kila kitu Draxton, sijui huwa anataka nini...."

"Basi, Blandina please... usi... anaumia tu. Unajua huzuni ya kufiwa huwa ina-impact watu kwa njia tofauti..."

Blandina akanyanyua uso wake na kumwangalia machoni. "Kwa hiyo unataka kusema alichofanya
ni sawa kabisa?"

"Si hivyo..."

"Ila nini sasa? Acha kujifanya una huruma sana Draxton, amekuaibisha mbele ya wengi wasiotufahamu. Siku moja ukipita mbele za watu wanaanza kukunyooshea vidole, yule pale alifanya hivi, yule pale alifanya hivi, kwa sababu tu ya mtu kusema vitu asivyokuwa na uhakika navyo kukuhusu wewe... na vya uwongo," Blandina akaongea kwa mkazo.

Draxton akajiketisha vizuri na kumshika Blandina kiunoni taratibu ili amnyanyue na kumfanya aketi
pia, nao wakawa wanatazama kwa ukaribu sana.

"Kuna mambo mengi yanayomchanganya yule mwanamke... anajikuta katikati ya eneo ambalo kila mara akitazama upande fulani na kufikiri ndiyo barabara sahihi ya kuondoka, barabara zingine zinatokea... na hivyo anashindwa kujua ipi ndiyo sahihi zaidi. Anapopita kwenye ile anayodhani ni sahihi, anapotea, lakini anaona kurudi nyuma ni ngumu mno... kwa hiyo anakazana kuipita hiyo hiyo tu akijiaminisha kwamba bado yuko njia sahihi. Wewe Blandina... unaijuia njia sahihi, unaujua ukweli, Namouih haujui. Unajua kwamba usiku huo wote mimi na wewe tulikuwa pamoja, tukalala pamoja, tukaamka pamoja... Namouih halijui hilo. Anadhani yuko sahihi kuona mambo namna
yoyote anayoyaona, lakini wewe unatakiwa kumfanya auone ukweli ili... asipotee," Draxton
akamwambia kwa hisia.

"Lakini tayari ameshapotea Draxton...."

"La... hajapotea. Kama navyokwambia, anakazana kupita huko anakodhani ni sahihi, ila wewe ndiyo wa kumshika mkono na kumvuta atoke huko. Nachojaribu kusema ni kwamba... anakuhitaji. Jaribu tu kumwelewa. Wewe kuliko mtu yeyote unajua kwamba Namouih amepitia mengi, ndiyo maana
yuko kama alivyo..."

"Nakuelewa Draxton. Lakini amevuka mipaka. Mtu unafika tu, anaanza kukurushia maneno, tena hadi anataka kumwambia mama ya mfiwa kwamba wewe ndiyo umemuua mume wa mtoto wake
kweli? Ah-ah..." Blandina akaongea kwa kuudhika.

Draxton akaushika uso wake na kumwangalia machoni kwa upendo. "Zile zilikuwa ni hisia Blandina. Anaumia. Nimefurahi tu kujua kwamba unaniamini ingawa... mambo mengi kuhusu
mimi... ni fumbo. Lakini maneno ya watu yasikusumbue. Wewe na Namouih ni kama dada, najua
unampenda sana. Mfanye auone ukweli hata kama akisisitiza vipi kwamba tayari anaujua... you are
good at that. Kwa hiyo nakuomba uniahidi kwamba utajaribu kuyanyoosha mambo kati yako na
yeye kesho... tafadhali. Hiyo haitamsaidia Namouih na wewe pekee kuwa na amani... bali na Felix
pia."

Blandina alijawa na faraja yenye simanzi sana kwa sababu ya maneno hayo yenye kugusa moyo
kutoka kwa Draxton, naye akaulaza uso wake kwenye shingo ya mpenzi wake huyo. Draxton akawa anatembeza kiganja chake taratibu kwenye kiuno cha Blandina, na kwa kadiri kubwa hii ikafanya mwanamke apandwe na hisia za kimahaba. Akaunyanyua uso wake na kuigusisha midomo yake sikioni kwa Draxton, halafu akabusu sehemu ya chini ya sikio hilo kwa hisia sana. Draxton akaushika ubavu wake, akiwa na lengo la kumvuta kidogo ili amkumbushe kwamba hawangepaswa kupitiliza, lakini alimshika na kumbinya kwa njia iliyofanya Blandina asisimke sana,
na mwanamke huyu akaanza kumbusu shingoni, shavuni, na kumfata midomoni akidhani Draxton
alikuwa anamwamshia hisia zake pia.

Kutokana na uzito wa hisia aliokuwa nao, Blandina akaendelea kumbusu Draxton kimahaba sana mdomoni mwake, naye Draxton akawa anambusu kwa upendo pia. Blandina alipoanza kuongeza kasi, Draxton akajitoa mdomoni mwake na kumwangalia machoni. Mwanamke alikuwa anamwangalia kwa hamu sana, na hii ikamfanya Draxton aone kweli alihitaji kujaribu tena kwa
wakati huu kumpa kile alichohitaji.

"Taratibu..."

Draxton akamwambia hivyo kwa sauti ya chini, naye Blandina akatikisa kichwa kuonyesha
ameelewa. Wakarudia tena penzi lao la mdomo, huku sasa mambo yakienda taratibu kweli, naye
Blandina akapitisha miguu yake pande za mapaja ya Draxton ili awe kama amemkalia katikati, huku akiendelea kumpiga busu. Wakati huu ilionekana kweli Draxton alitaka sana kumpa penzi mwanamke huyu, na tayari Blandina alikuwa anafurahia mno hatua hii waliyofikia. Wakiwa wanaendelea kupiga busu Blandina akaanza kuufungua mkanda wa suruali ya Draxton kwa
kupitisha mikono yake kwa chini, huku mwanaume akiwa amekishikilia kiuno cha mrembo na
kulichezea kalio lake kubwa kwa viganja vyake. Blandina akawa amefanikiwa kuingiza kiganja
chake ndani ya suruali ya Draxton na kuishika sehemu yake ya siri, lakini hapo hapo akautoa mkono
wake upesi.

Draxton alikuwa ameanza kuchemka tena, na hapa ndiyo wakaivunja busu yao, Blandina akimwangalia usoni kwa kujali, na Draxton akitazama chini huku akipumua na kukaza macho kama vile kuonyesha anaumia. Blandina alimtazama kwa huruma sana asielewe ni kwa nini jambo hili lilikuwa linampata mpenzi wake kila mara walipojaribu kuonyeshana upendo, na alipokuwa
anataka tu kusema kitu, Draxton akajivuta nyuma na kufanya Blandina ajitoe hapo alipokuwa
amemkalia na kujiweka pembeni. Draxton akawa amefumba macho yake huku akipumua kwa nguvu kiasi, naye Blandina akamsogelea mgongoni na kupitisha mikono yake kiunoni kwa jamaa.

"Samahani Blandina.... nahitaji kwenda..."

Draxton akasema hivyo kwa sauti tetemeshi kiasi, na kiukweli Blandina alikosa hata cha kusema na kuitoa mikono yake kiunoni kwa mpenzi wake huyo. Mwanaume akajitoa kitandani hapo na kusimama kwa ufupi, akiwa amempa mgongo Blandina kama anafikiria jambo fulani, na mwanamke huyu akawa anataka kusikia atakachosema.

"Nitakupigia."

Draxton akaongea tu hivyo bila kumwangalia na kuondoka ndani ya chumba hicho.

Blandina akainamisha uso wake kidogo, kisha akajitupia kitandani hapo na kutazama juu akiwa
anatafakari vitu vingi. Kuwa na mtu kama Draxton kulimridhisha sana kihisia kwa kuwa alionekana kuwa na moyo mzuri mno, lakini tena kila mara alipotaka kufurahia zaidi upendo wake kwake kwa njia hii jambo hilo lingezuka, na mwanaume mwenyewe alionyesha kutotaka kutafuta suluhisho. Hali hii ingeendelea hivi mpaka lini? Blandina akajiahidi kufanya yote yaliyokuwa ndani ya uwezo wake kujua na kusaidia kusuluhisha kile kilichomtatiza mpenzi wake, lakini kwa sasa, angehitaji kujitahidi kurudisha hali ya amani baina yake na Namouih kama tu Draxton alivyokuwa amemshauri.

★★

Namouih anafumbua macho yake na kujikuta akiwa ndani ya kitu kilichoonekana kama sanduku la
chuma, akiwa amelala chali na mwili wake ukihisi baridi sana. Yaani alikuwa amenyooka, na alipojaribu kunyanyuka akatambua kwamba ilikuwa ni ndani ya chumba kidogo sana sehemu hiyo aliyolala iliyoubana mno mwili wake, naye asingeweza kunyanyuka hata kidogo. Alihisi ni kama vile amelala ndani ya jeneza, na jambo hilo likamfanya aingiwe na hofu kubwa. Akaanza kupiga kelele na kilio cha kuomba msaada, ndipo akahisi kifaa hicho kinavutwa kwa nyuma, na mwili wake ukarudi nyuma pia.

Kifaa hicho kiliposimama, yeye akiwa amelala vile vile chali, akaanza kuona namna ambavyo sehemu hiyo ilikuwa na umaridadi wa kiasi fulani, na kwa haraka akajinyanyua kwa kujivuta nyuma ili apatazame vizuri zaidi. Kwa macho ya haraka akawa ametambua kwamba alikuwa ndani ya chumba cha kutunzia maiti, yaani mochwari, na alipoangalia sehemu aliyokuwa akatambua ilikuwa
ni kwenye masanduku ya kutunzia miili ya maiti yaliyokuwa kama majokofu ili miili isiharibike, naye
akajitoa hapo haraka na kuanguka chini. Kweli kulikuwa na sehemu zenye meza za matairi ambazo
angeweza kuona miili mibichi ya watu waliokufa ikiwa imelazwa hapo, mingine ikiwa imekatika
katika viungo na hata mifupa ya viunzi, naye akaanza kutembea kuelekea pale alipouona mlango
huku akijitahidi kutoangalia mambo yote hayo yaliyohofisha.

Alipoufikia mlango akaufungua upesi na kutoka nje ili aondoke ndani ya mochwari hiyo, lakini akajikuta anakanyaga sehemu yenye majani kwenye eneo lenye giza sana, naye alipogeuka nyuma akashangaa sana baada ya kukuta chumba kile cha mochwari kimetoweka kabisa; kana kwamba hakuwa ametoka huko muda mfupi tu. Akaingiwa na hofu zaidi, lakini akajiimarisha kwa kutoa sala kimoyomoyo, kisha akaanza kujipapasa mwilini ili kuona kama alikuwa na simu yake hapo, awashe
tochi, lakini hakuwa nayo. Ni katika kujipapasa huko ndiyo akawa ametambua kwamba mwili wake
haukuwa na nguo hata moja, naye akaanza kuwaza kwamba huenda na hapa alikuwa akiota.

Eneo hilo lilikuwa na giza zito na kimya kikali sana, naye akaanza kupiga hatua kwenda mbele huku
akiyashika manyasi marefu kujipa mhimili mzuri, akijiambia moyoni mwake kwamba alikuwa anaota na asingechukua muda mrefu kuamka, lakini ni hapa ndiyo akaanza kusikia sauti ya popo ikilia kuzungukia sehemu alipokuwepo. Akasimama kwanza na kutulia. Sauti hii ikaendelea kusikika kwa njia fulani kama vile inasema "njoo," "njoo," "njoo," naye Namouih akageuka huku na kule kuangaza chochote kile, na ndipo akaona kitu kama mwangaza wa mbali ukitembea hewani taratibu. Hofu kuu ilikuwa imemtawala mwanamke huyu, lakini hakujua ni nini tu ambacho kilimsukuma aanze kuufata mwangaza huo, ingawa alijua uwezekano wa yeye kujipeleka kwenye mwisho wake ulikuwa huko.

Akaendelea kuufata mwangaza huo huku akiwa ndani ya hali yake ya utupu, na ingawa majani yalimchoma hapa na kule lakini hakukata tamaa kuendelea kuufata. Sauti ile ya mlio wa popo ikaacha kusikika, na mwangaza huo ukakatika ghafla kama umeme. Hali hiyo ya utulivu uliorudi baada ya Namouih kusimama ikamfanya aanze kusikia sauti fulani hivi kama za kitu kikitafunwa, au kunyonywa, hakuwa na uhakika. Zilitokea mbele yake kidogo, naye akaamua kupiga hatua
chache kwa sababu ni sehemu hiyo hiyo ndiyo mwangaza ule uliishia. Alijitahidi kutembea kwa tahadhari sana mpaka alipofikia usawa wenye manyasi mengi marefu yaliyobanana sana, naye aakayatenganisha ili aweze kuona kilichokuwa huko mbele.

Macho ya mwanamke huyu yalitanuka kwa kushtushwa na jambo aliloona mbele yake. Kulikuwa na giza ndiyo, lakini aliweza kuona kwa usahihi sehemu hiyo yenye mti, ikiwa imetundikiwa kitu kama kamba iliyoning'iniza mwili wa mtu ukiwa uchi kabisa, ukiwa bila ulimi mdomoni, na utumbo wake
ukininginia kutoka tumboni! Pembeni ya mwili huo kilisimama kitu fulani cheusi, kama mtu lakini mwenye mwili mkubwa sana, na alikuwa amekinga kama kopo la kisado sehemu hiyo ya tumbo iliyokatwa kwenye mwili ulioning'inizwa, akionekana kuziweka damu zilizomwagikia ndani humo. Namouih alikuwa anataka kugeuka na kukimbia, lakini ikawa kama vile analazimishwa kuendelea
kuangalia.

Akaanza kumwona kiumbe huyo akinyanyua kopo hilo juu, taratibu, kisha akalirudisha chini usawa
wa mdomo wake na kuanza kunywa damu hizo! Alikuwa anazinywa taratibu, lakini sauti ya jinsi
alivyozimeza ilikuwa inasikika vyema kwa Namouih. Aliona kero na kinyaa sana, na wazo la kwamba yeye pia alikuwa uchi sehemu hiyo isiyoeleweka ni wapi, mbele yake kukiwa na mwili uliokatwa namna hiyo, na jitu hilo likinywa damu kukazidisha hofu yake hata zaidi, naye akapata nguvu ya kugeuka na kuanza kukimbia. Alikimbia sana na kuanguka mara kwa mara, lakini
angenyanyuka na kuendelea kujitahidi kukimbia kwa nguvu zake zote. Alikuwa anajiuliza hii ni ndoto gani isiyoisha, yaani alitaka ikatike lakini ndiyo kwanza ikazidi kumpeleka mbali zaidi.

Akafika sehemu na kuanguka kwa nguvu sana, kitu kilichofanya abamize tumbo lake vibaya na
kuhisi maumivu makali mno. Alipojishika tumboni, mkono wake ukaingia ndani kabisa, kuonyesha
kwamba lilikuwa limechanika, na maumivu aliyohisi yalifanya jambo hili liache kuonekana kuwa ndoto bali kitu halisi kabisa. Akawa anapumua kwa shida sana, na ile aliponyanyua macho yake mbele akakutana na macho makubwa na mekundu sana yakiwa yanamtazama kwa ukaribu! Akapiga kelele lakini sauti yake haikutoka, na ndipo akahisi miguu yake ikianza kuburuzwa kwa nyuma, kitu kilichofanya maumivu yake tumboni yaongezeke! Alilia sana, akipiga kelele zisizotoa sauti yoyote ile, na ndipo.....

"Aaaaaaaaah!"

Namouih akaamka na mayowe hayo ya hali ya juu, akijikuta kitandani chumbani kwake. Alikuwa anapumua kwa kasi sana, naye akajishika tumboni kwake kuangalia kama alikuwa sawa. Akafumba macho na kuanza kulia kwa sauti ya juu, akiwa ameumizwa sana na ndoto hiyo mbaya mno, naye akaanza kumwita mume wake ili aje kumpa faraja angalau.

"Efraim... hhh... Efraiiim...."

Namouih akaendelea kuita tu, lakini hakupata jibu lolote lile. Akapunguza kasi ya upumuaji wake na kuanza kukitathmini chumba chake kwanza.
Palikuwa kimya, na ingetakiwa kuwa jioni au usiku kwa kuwa alikumbuka kwamba waliporejea nyumbani kutoka msibani ilikuwa ni saa kumi na moja, hivyo hata giza lingekuwa limeshaanza kuingia. Lakini mwangaza uliokuwa chumbani hapo ulikaribiana na rangi ya weupe-weusi,
iliyofanya kila kitu kionekane kama hakina rangi. Akatazama mlangoni, palionekana kuwa mbali sana kutoka kitandani hapo kiasi kwamba alihisi asingeweza kuufikia haraka na kutoka, naye akaita tena jina la mume wake lakini akaambulia kunyamaziwa.

Nini kilikuwa kinaendelea? Bega lake likaguswa kutokea nyuma ya mgongo wake, na mishipa ya
shingo ya Namouih ikakaza kutokana na kuhisi woga wa hali ya juu sana. Akageuka taratibu na
kumtazama aliyemgusa, na macho yake yakatanuka kwa mshangao huku akitetemeka sana baada
ya kumwona Felix akiwa amekaa karibu na uso wake huku akitabasamu!


★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumatatu, Jumanne, na Jumatano. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

TANGAZO: Nimebadili namba ya WhatsApp, sitapatikana kwenye ile ya mwanzo tena, bali sasa nitapatikana kwenye hii +255 678 017 280. Karibuni.

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SITA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Namouih akashtuka na kujinyanyua kwa nguvu sana kutoka kitandani, yaani akiketi, huku akipumua kwa nguvu sana kutokana na hofu kubwa iliyokuwa ndani yake. Akatazama huku na huko na kutambua kwamba alikuwa chumbani kwake, taa zikiwa zimewashwa na ikiwa wazi kwamba usiku umeshaingia. Akapaangalia kitandani hapo na kukumbuka jinsi alivyonwona Felix ndotoni akiwa anatabasamu, naye akainamisha uso wake kwa kufadhaishwa sana na ndoto hiyo iliyojirudia mara mbili, ikiwa kama ni kitu halisi kabisa kilikuwa kinaendelea alipokuwa akiiota.

"Jamani... jamani... f(.....)!"

Namouih akaongea hivyo kwa hasira sana na kuanza kuirusha mito chini, akiwa amechoshwa sana na ndoto hizi, na ni hapo ndiyo Efraim Donald akaingia kutokea bafuni huku akimwangalia mke wake kwa mshangao. Akamfata kitandani hapo, na sasa Namouih alikuwa ameikunja miguu yake na kuikanyagisha kitandani huku uso wake akiuinamishia kwenye magoti yake, na mikono yake ikiibana kwa nguvu miguu yake kuonyesha mfadhaiko. Efraim Donald akakaa kitandani na kumshika Namouih kwenye nywele zake, na mwanamke huyu akashtuka na kujisogeza nyuma, akimwangalia Efraim kwa hofu sana.

"Namouih tulia... ni mimi. Vipi tena?"

Efraim Donald akamsemesha mke wake kwa kujali, naye Namouih akaangalia chini huku machozi
yakionekana kumtoka.

"Mbona unapiga kelele? Umepatwa na nini?" Efraim akauliza kwa kujali.

"Hhh... Efraim me nachoka jamani... hizi ndoto... kwa nini lakini?" Namouih akaongea kwa huzuni.

"Umeota ndoto mbaya tena?" Efraim akauliza.

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Umeota nini?"

"Ahh... yaani sitaki hata...."

"No, Namouih, naomba uniambie. Hili jambo linaweza likageuka kuwa tatizo kubwa. Jikaze uniambie..." Efraim akamsihi huku akimfuta machozi.

Kweli Namouih akajitahidi kutafuta utulivu kiasi na kuanza kumwelezea mume wake mambo aliyokuwa anaona kwenye ndoto hizo zenye kutisha. Alieleza namna ambavyo zilimfanya ahisi ni kama vile yuko sehemu halisi kila mara zilipompata, na hakujua kwa nini ila ilikuwa ni kama zimebeba ujumbe fulani wenye maana kwake ambao ulikuwa mgumu kuelezeka. Yeye hakutaka
hata kujua maana ya ujumbe huo lakini ilionekana kwamba ziliendelea kumpata kwa sababu ALITAKIWA kuelewa maana ya hizo jumbe. Efraim Donald alimsikiliza mke wake kwa umakini sana, akitambua kuwa kweli hiki kitu kingekuwa tatizo kubwa kama asingefanya jambo fulani kumsaidia mke wake; kama tu jinsi yule rafiki yake, Godwin Shigela alivyokuwa amemwambia.

Mume akamfariji tu mke wake na kumwambia labda angehitaji kujipumzisha zaidi, hasa akili yake.
Namouih alikuwa ameweka wazi kwamba mambo yote haya yalimfanya hadi awe anaogopa giza
kabisa wakati hicho ni kitu ambacho hakuwa nacho. Kwa kuwa sasa Efraim alikuwa amemwelewa zaidi akasema wangekuwa wanalala na taa zikiwa zimewaka ili kumpa ahueni zaidi, na baada ya hapo akamwambia mke wake waelekee chini kupata chakula kwa sababu ndiyo ilikuwa imefika saa mbili tu usiku.


★★★


Siku iliyofuata, hali ikaonekana kuwa shwari baada ya Namouih kuamka asubuhi bila kuwa amesumbuliwa na ndoto nyingine wala vioja vya usiku, naye akaanza kujiandaa kwa ajili ya kazi. Efraim Donald alikuwa anataka kuhakikisha kwamba mke wake yuko sawa kiakili na kihisia ili kumruhusu aende kazini, lakini Namouih akamwambia alikuwa vizuri, bila shaka kadiri ambavyo muda ungekwenda ndivyo ambavyo angezoea hali, nao wangetafuta wakati mzuri wa kutafuta utatuzi wa suala lake la ndoto mbaya. Baada ya kumaliza kujiandaa na kupata kiamsha kinywa pamoja, wanandoa hawa wakaondoka nyumbani hapo; Efraim akiendeshwa na Suleiman ndani ya Range Rover yake nyeusi na Namouih akiondoka kwa Premo yake ya silver.

Lakini mwanamke huyu hakuelekea moja kwa moja mpaka kazini, bali alikwenda kukutana na wakuu wa wapelelezi waliohusika na uchunguzi wa kifo cha mpelelezi mwenzao, Felix. Alipokutana nao akaanza kuwaambia kuhusiana na mambo aliyofikiria yalipelekea kifo cha rafiki yake,, naye akawaomba wafanye yote wawezayo kumchunguza Draxton; kwa kuwa aliamini kabisa kwamba mwanaume yule alihusika moja kwa moja na mauaji ya rafiki
yake baada ya yeye Namouih kumwambia Felix amfatilie Draxton.
Wakuu hao wakawa wamwelewa na kumwambia kwamba wangemtafuta huyo jamaa na kumpiga uchunguzi wa ndani ili kuona kama kweli alihusika, naye Namouih akaridhia hilo na kuagana nao. Uzuri wa Namouih ni kwamba alikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi kwenye maneno yake, kwa hiyo aliondoka akijua kabisa kwamba suala hilo lisingepuuziwa hata kidogo.

Alifika kwenye kampuni yao na kuanza kuelekea juu kwenye ofisi yake, na ile tu alipokuwa ameikaribia, akakutana uso kwa uso na Blandina, ambaye alikuwa amesimama na mwanamke mwingine aliyefanyia kazi hapo. Wawili hawa wakatazamana kwa ufupi machoni, kwa njia ya kawaida tu, kisha Namouih akatazama mbele na kuwapita bila kusema lolote mpaka alipoingia ofisini kwake. Blandina alielewa wazi kwamba kofi alilomtandika rafiki yake jana bado lilikuwa linamwasha, na kwa kumjua Namouih vizuri alielewa pia kwamba kufanya amani naye isingekuwa rahisi sana hasa kwa sababu alijiona kuwa sahihi, lakini kwa wakati huu kulikuwa na jambo lingine alilohitaji
kumwambia, hivyo akamfata huko huko ofisini kwake na kuingia bila hata kupiga hodi. Blandina hakujali kwamba eti Namouih alikuwa kama "boss" kwake, yeye aliendelea kumwona kama rafiki yake tu haijalishi walikuwa wanapitia nini, hivyo akamsogelea mpaka mezani kwake na kusimama.

Namouih akafanya kama vile hajamwona kabisa, akiendelea kutazama kompyuta yake tu, na Blandina akatabasamu kwa kejeli huku akitazama pembeni, kisha akaona ni vyema aseme
kilichompeleka na kuondoka.
Akaanza kumwelezea kuhusiana na kazi fulani iliyohitajika kufanywa, ambayo ingempasa yeye Blandina kwenda nje ya jiji ili kuikamilisha leo leo kisha ndiyo angerudi kesho, halafu akamwekea kablasha mezani lenye orodha ya kesi ambazo angetakiwa kupitia ili achague zile alizotaka kufanyia kazi. Namouih aliigiza kama vile hayupo hiyo sehemu, yaani hakumsemesha wala
kumtazama, hivyo Blandina akashusha pumzi na kusema yeye angeondoka muda si mrefu, kwa
hiyo Namouih akijisikia kukiweka kisirani pembeni basi angemtafuta wakati wowote aliomhitaji. Blandina akajiondokea tu hapo baada ya kumaliza kuongea hayo, na Namouih akatazama pale rafiki yake alipoishia mlangoni na kutoka.

Roho ilikuwa ikimuuma sana Namouih kumtendea mwenzake namna hiyo lakini bado na yeye pia
aliumizwa na kitendo cha Blandina kumpiga kofi kisa mwanaume ambaye alimwona kuwa mbaya,
kwa hiyo hakuona faida yoyote ya kuwaza sana juu ya hilo. Aliona kwamba ni Blandina ndiye aliyetakiwa kuomba samahani, na kwa sababu hakufanya hivyo basi ndiyo angemnunia mpaka
kieleweke. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wawili hawa walipendana sana, basi tu. Kukomoana huku
kusingechukua muda mrefu sana na kila mmoja alijua hilo, lakini bado hili suala lililosababisha utofauti wao lilikuwa zito mno na hivyo bila shaka muda ungepita. Namouih akalichukua kablasha lile na kuanza tu kupitia kazi ambazo Blandina alikuwa amemletea.

Imefika mida ya saa nane mchana, Namouih akawa amemaliza kupata chakula na kutumia muda mwingi kwenye masuala ya kazi ambazo hazikumhitaji aende mahakamani wala wapi. Mwenye hiyo kampuni, yaani Mr. Edward, alikuwa amemwambia kwamba alitakiwa kwenda nyumbani kupumzika tu, lakini Namouih akasema alikuwa vizuri kuendelea na kazi. Mkuu wake huyo akamsisitizia sana kwenda nyumbani kwa kusema alijua namna ambavyo siku hizi chache zimekuwa ngumu sana kwake, na moja kwa moja Namouih akawa ametambua kwamba Efraim alikuwa ameongea naye ili afanye jambo hili. Hakuona haja ya kubishana na mwajiri wake, kwa sababu hii ingempatia fursa ya kwenda tena kufuatilia ishu ya Draxton kwa wale wapelelezi, kwa
hiyo akatii ombi la Mr. Edward na kuondoka.

Alikwenda moja kwa moja tena kuonana na mkuu wa wapelelezi wale, naye akapewa taarifa ambazo hazikuwa nzuri kwake. Walikuwa wamefanya uchunguzi kumhusu Draxton na kugundua kwamba usiku ule Felix alipouawa mwanaume huyo alikuwa pamoja na mpenzi wake kwa muda wote wa usiku ule mpaka kukucha, yaani walilala pamoja pale pale alipoishi Draxton. Walikuwa
wamemhoji Draxton asubuhi hii na hata kuongea na majirani zake ambao walisema ni kweli usiku
huo wawili hao walikuwa pale, yaani Blandina na Draxton, na asubuhi wakaondoka pamoja. Draxton yeye alisema kwamba usiku huo alipokuwa na mpenzi wake walikutana na Felix na kutambulishana kwa mara ya kwanza, hivyo hakuwa akimjua mwanaume huyo hata kidogo
isipokuwa tu kuwa rafiki ya Blandina.
Namouih akawa anasisitiza kwa kusema kwamba inawezekana mwanaume huyo alimwambia mtu
fulani amuue Felix kwa niaba yake, kwa sababu huenda baada ya kumwona alitambua kwamba
alikuwa anampeleleza, lakini Namouih akaambiwa kwamba kwa jambo hilo ingehitajika kuwa na
uthibitisho zaidi; kitu ambacho hakikuwepo kabisa. Draxton alikuwa msafi kuhusiana na jambo hilo. Ingawa hivyo, Namouih akaambiwa kwamba angetakiwa kusubiri ili wapelelezi waendelee na uchunguzi wao kwa sababu muuaji angeweza kuwa yeyote na wangehitaji kumkamata haraka sana, lakini Namouih aliziona hizo kuwa ahadi bandia tu. Akawashukuru kwa jitihada zao, kisha akawaacha na kwenda zake nyumbani.

★★★

Muda ulitembea sana siku hii, mpaka inafika jioni baada ya Namouih kuondoka kazini alikuwa zake
nyumbani tu akiendelea kufikiria njia za kumfichua Draxton. Mume wake alirejea kwenye saa nne usiku, nao wakapata mlo wa pamoja na kuzungumza kidogo mpaka walipokwenda kulala. Namouih alijitahidi kuonyesha kwamba sasa alikuwa sawa zaidi, lakini hiyo ilikuwa ni ili amridhishe tu mume wake. Aliendelea kuwaza sana kuhusu kifo cha Felix na nini afanye ili haki itekelezwe kwa mauaji yake, na jambo hili likamnyima hata usingizi.

Imefika saa saba usiku, mwanamke huyu akamwacha mume wake kitandani na kwenda kule chini
kwenye ofisi yao ya hapo nyumbani ili ajaribu tena kuunganisha vipisi vya hapa na pale kubaini ukweli. Alitaka kuhakikisha ana vigezo muhimu vya kujua namna ya kumnasa mwanaume yule vizuri, naye akajikuta anaendelea kuumiza tu kichwa kwa muda mrefu zaidi ndani hapo. Akawa ameketi kwenye kiti chake ndani ya ofisi hiyo baada ya kuwa amejaribu kuunganisha mambo mbalimbali yenye kumhusisha Draxton na mauaji ya Felix bila kupata mafanikio yoyote chanya.

Efraim Donald, akiwa chumbani bado, akawa ameamka muda huu na kukuta mke wake hayupo kitandani, naye akajaribu kumwita akidhani yuko bafuni, lakini hakupata jibu. Akashuka kutoka kitandani na kuangalia saa. Ilikuwa ni saa nane usiku sasa, naye akaenda kuchungulia huko bafuni na kukuta kweli pakiwa tupu. Akatoka chumbani na kuzielekea ngazi, na alipofika kwenye kingo yake akaona chumba cha ofisi kule chini kikitoa mwanga, naye anajua bila shaka mke wake alikuwa humo. Akashuka na kuelekea mpaka huko, na baada ya kuingia ndani ya chumba hicho
akamkuta Namouih akiwa ameinamisha kichwa chake mezani huku amekifunika kwa mikono yake,
kama vile kuonyesha amechanganywa na jambo fulani.

Efraim akasogea mpaka hapo na kuona makaratasi kadhaa yaliyoandikiwa vitu vingi kwa njia ya
mahesabu, michoro, na viunganishi, naye akatambua haraka kwamba hayo yote yalihusiana na suala la mke wake la kukazana kuthibitisha kwamba Draxton alihusika katika mambo mengi mabaya. Akamwangalia kwa umakini, kisha akamgusa taratibu kwenye mkono wake. Namouih bila shaka hakuwa ametambua uwepo wa mume wake ndani hapo kwa kuwa alinyanyua kichwa chake kwa njia ya kushtuka, ila baada ya kuona ni Efraim akatulia na kuendelea kumwangalia tu.

"Unafanya nini huku? Umeota ndoto mbaya tena?" Efraim Donald akauliza.

Namouih akatikisa kichwa kukanusha, na macho yake yalionyesha uchovu sana.

"Sasa mbona uko hapa? Tatizo nini?"

"Nilikuwa nimekuja tu... kusoma kidogo," Namouih akasema.

Efraim Donald akaichukua karatasi moja na kuanza kuisoma. "His car on sight when Agnes died...
the tattoo... the same tattoo on his back... how he lowers his chin and tilts his head whenever.... ahh... kusoma? Namouih haya ndiyo unayoamka usiku wa manane kusoma?" akamuuliza.

Namouih akatazama tu mezani na kubaki kimya.

"Kwa nini unaacha kupumzika na kuja kukaa huku kufanya mambo yasiyo na faida yoyote? Draxton,
Draxton, Draxton, mke wangu kwa nini hutaki kuachana naye? Amekukosea nini?"

"Vitu anavyofanya ndiyo vinanikosesha usingizi, na hakuna mtu anayetaka kuamini kwamba huyo mwanaume ni hatari mpaka atakuja kusababisha maafa zaidi," Namouih akaongea kwa hisia.

"Una uhakika gani ni yeye ndiyo anafanya hayo... Namouih mbona unakuwa hivi?"

"Sijapata tu ushahidi mzuri lakini najua ni yeye ndiye aliyemuua Agnes na Felix," Namouih akasema kwa uhakika.

"Okay. Kwa hiyo kama ni yeye ndiyo amewaua, wewe unataka nini?"

Nataka nini?!" Namouih akauliza kimshangao na kusimama. "Unauliza nataka nini? Mtu amewaua watu naowafahamu, halafu unaniuliza nataka nini? Nikae nisubiri amuue Blandina next, au wewe si ndiyo?"

"Namouih acha utoto. Angekuwa muuaji kweli mpaka sasa hivi rafiki yako angekuwepo?"

"Ni utoto kwako ndiyo kwa sababu hujapoteza mtu yeyote muhimu. Angekuwa ameniua mimi je?
Usingefatilia chochote kwa sababu ungeuona kuwa utoto, si ndiyo?"

Efraim akanyanyua kidole juu kumwelekea huku akimtazama kiukali, na Namouih akatulia.

"Nimechoshwa na hii tabia Namouih. Unapotea. Watu wanaofanya mauaji wako macho, na wewe ukikaa kujiingiza huko unaweza ukasababisha nikupoteze kweli. Sijali kingine chochote zaidi ya usalama wako, kwa hiyo nakukanya... achana na haya mambo," Efraim akamwambia.

"Kwa hiyo haujali jinsi navyohisi kwa sababu ya kumpoteza rafiki yangu?"
"Nimesema hivi... sijali chochote kile zaidi ya usalama wako. Ikiwa hizo hisia zako zitapelekea uumie zitakuwa na faida gani kwangu? Acha kuwa mpuuzi Namouih, hata ukifanya nini huyo Agnes na Felix hawatarudi. Sitaki tena kusikia habari hizi. Iwe mwanzo na mwisho," Efraim Donald akaongea kwa ukali kiasi.

Namouih akawa anamwangalia mume wake huku akidondosha machozi kwa huzuni.

"Zima taa, twende tukalale," Efraim akasema kwa uthabiti na kuondoka hapo.

Namouih akaketi tena kwenye kiti taratibu, akiwa amehisi kuumizwa sana na maneno ya mume wake. Alilia bila kutoa sauti, na wakati huu alikuwa akilia kwa hasira. Aliuona ukweli kwenye maneno ya mume wake, kwamba hata kama angepata ushahidi dhidi ya mtu aliyehusika na mauaji, wale waliokufa wasingerudi kuwa hai tena. Kwa hiyo hasira aliyokuwa nayo sasa ilitokana na
utambuzi wa kuwa njia ya haki katika kisa hiki ilikuwa ni kwa malipo ya damu, yaani uhai kwa uhai.
Alikuwa amejihakikishia moyoni mwake kabisa kwamba ni Draxton ndiye aliyewaua rafiki zake, hivyo kutokana na jinsi ambavyo wengine walipuuzia kile alichokiona kuwa uhalisia, sasa akawa ameamua kurudisha malipo hayo kwa mikono yake mwenyewe, na hangejali chochote kile ambacho kingejaribu kusimama mbele ya njia yake. Draxton angelipia kwa kifo cha Felix.


★★★


Asubuhi na mapema kulipokucha, Efraim Donald aliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kazi, huku akimwacha Namouih amejilaza kitandani. Mpaka inafika saa 3 bado tu Namouih alikuwa amelala, siyo kusinzia, bali hakutaka tu kunyanyuka kutoka kitandani. Kufikia muda huu sasa Efraim ndiyo alikuwa amemaliza kila kitu na kutaka kuondoka, hivyo akamfata mke wake ili amuage. Mwanamke alikuwa amelala kwa ubavu, mikono akiikunjia kwa pamoja kuelekea mpaka kwenye upande wa uso wake alioulaza kwenye viganja vyake; akiwa macho tu, na akiwa kimya tu. Efraim Donald akachuchumaa karibu na uso wake na kumtazama kwa upole, kisha akamshika shavuni na kupitisha mkono wake mpaka nyweleni, lakini Namouih hata kumwangalia hakumwangalia. Efraim akamwambia 'mimi ninaenda sasa honey, tutaonana baadaye,' lakini ukimya ndiyo jibu pekee alilopewa. Kwa hiyo mwanaume akambusu tu mke wake kwenye paji la uso, kisha akamwambia angempigia baadaye, halafu akanyanyuka na kuanza kuondoka huku akimwangalia mara mbili-mbili kuonyesha namna alivyomjali sana. Namouih akaendelea tu kujilaza namna hiyo hiyo mpaka mume wake alipoondoka kabisa nyumbani, kisha akajinyanyua taratibu na kuketi.

Alikuwa ameweka uso makini sana, yaani hakuwa ameamka na hisi ya uchangamfu wala utani hata kidogo. Akaenda bafuni kujisafisha na kutoka kujiandaa, na haikuwa kujiandaa kwa ajili ya kazi. Akavalia T-shirt nyeusi yenye mikono mirefu iliyobana, suruali laini ya kijivu, na viatu vyeupe vya mazoezi. Akavaa na sweta jepesi lenye kofia ya kufunika kichwa, kisha akaingia kwenye vifaa
vya mume wake na kuitoa bastola yake kwa mara nyingine tena wakati huu. Akahakikisha kuna risasi za kutosha, kisha akaiweka nyuma ya kiuno chake na kutoka chumbani hatimaye.

Ikiwa ni saa 4 sasa ndiyo Namouih anatoka ndani ya chumba chake, Esma alishangaa kiasi baada ya kuona jinsi alivyovaa na kujiuliza ikiwa alikuwa anaenda kazini au gym. Akamsalimia, lakini Namouih hata hakumwitikia. Akaelekea nje tu bila kusema lolote na kuchukua gari lake la Premo, kisha naye akaondoka hapo. Esma kwa kufikiri labda mwajiri wake huyo alikuwa amekorofishana na mume wake, akaamua tu kuendelea na shughuli zingine kama ilivyo kawaida.

★★

Inafika mida ya saa saba mchana, Efraim Donald akaanza kumtafuta Namouih kwa simu, lakini
hakumpata mara zote alizojaribu. Akaamua kuacha mpaka ilipofika saa tisa, akampigia tena, lakini
hakumpata. Ikabidi ajaribu kupiga ofisini kwake Namouih, naye ndiyo akataarifiwa kwamba leo mke wake hakukanyaga huko. Kwa kufikiri labda alikuwa amebaki nyumbani, akapiga namba ya Esma, na mwanadada huyo akapokea na kuweka wazi sasa kwamba dada mkubwa aliondoka nyumbani pia muda fulani baada ya yeye Efraim kuondoka, na hakusema lolote kabisa. Akamweleza namna mwonekano wa Namouih ulivyokuwa, naye Efraim akaingiwa na wasiwasi zaidi sasa.

Ikabidi mwanaume ampigie na Blandina pia, ambaye ndiyo alikuwa anarejea kutoka upande mwingine wa jiji alikokwenda jana kikazi, naye akasema kwamba hakuwa na utambuzi wowote wa ni wapi rafiki yake angekuwa maana hata yeye pia alijaribu kumtafuta leo bila mafanikio na kuchukulia labda bado alikuwa na kisirani naye. Kila mtu ambaye Efraim aliulizia kama amemwona
mke wake, jibu lilikuwa hapana. Hivyo akaamua kuacha mambo mengine ili kwenda maeneo
mbalimbali kumtafuta. Alielewa kwamba kilichotokea usiku wa kuamkia sasa ndiyo kilichokuwa chanzo cha maigizo haya kuanza, na kama mke wake huyo alipuuzia maonyo yake ya wazi, basi huko alikokuwa amekwenda ilikuwa ni kutafuta matatizo. Ikabidi ampigie na Draxton, akimuuliza ikiwa alikutana na mke wake leo, lakini mwanaume huyo akakanusha. Efraim hakutaka Draxton ahisi labda kuna shida fulani, kwa hiyo akasema tu kwamba hakuweza kumpata kwa simu yake na hivyo akadhani yeye Draxton
akiwa mwanasheria mwenzake na mtu wa karibu wa rafiki ya mke wake angekuwa amemwona labda kimikutano na kadhalika.

Efraim Donald alihisi kuchanganyikiwa baada ya kufanya jitihada nyingi na kukosa matokeo
mazuri. Alizunguka hapa, huku, kule na huko akiwa na swali moja tu kichwani: Namouih angekuwa
amekwenda wapi?


★★★


Siku hii, Namouih alikuwa ameondoka nyumbani kwake, akibeba bastola ya mume wake, na ni sehemu moja tu aliyokuwa amekwenda; msituni/porini kule ambako alimfuatilia Draxton siku
chache nyuma na kumshurutisha amwambie ukweli kuhusu matendo yake. Tokea alipoondoka nyumbani na kufika huko, mwanamke huyu hakuwa na nia ya kufanya lolote lile zaidi ya kuusaka ukweli mwenyewe na kupata haki kwa ajili ya kifo cha Felix, na kwa kusema haki ilimaanisha ayaondoe maisha ya yule aliyeyaondoa ya rafiki yake. Hata ingawa jambo hilo lilionekana kuwa sahihi kwake, bado kilikuwa ni kitu ambacho hakuwahi kufanya kabla katika maisha yake, na hivyo
hakujua uzito wa kile alichotaka kufanya tofauti na jinsi alivyotazamia.

Ingawa hivyo, tayari akili yake ilikuwa imeazimia kabisa kulitimiza jambo hili ambalo kwa maneno mengine lingeitwa kulipa kisasi. Alikwenda mpaka sehemu ile ambayo Draxton aliishia siku ile, kisha yeye akaliingiza gari sehemu za ndani zaidi za msitu huo ili kutafuta vitu vyovyote ambavyo vingethibitisha ubaya wa mwanaume yule, na alikuwa akiwaza kwamba kama angemkuta huko basi angehakikisha anamwacha akiwa maiti. Alifanya uchunguzi wa hapa na pale bila kuchoka, kula, bila kunywa, na bila kukata tamaa. Hakujua ingemchukua muda mrefu kadiri gani kuuzunguka msitu huo wote, lakini hakutambua kwamba kadiri alivyoendelea kuzunguka huko ndivyo alivyozidi kupotea. Ili kutosumbuliwa na yeyote yule alikuwa ameiweka simu yake katika mfumo wa kutopokea mawasiliano kama mtu akiwa kwenye ndege (Airplane mode), na muda ukazidi kwenda na kwenda hadi inafika saa kumi jioni, ndipo akapata kuona jambo fulani.

Katika eneo la ndani zaidi la msitu huo, aliweza kuona kitu kama nyumba, iliyokuwa imekinzwa na
miti mingi sana. Kwa eneo hili ilikuwa wazi kwamba hakukuwa na umeme, hivyo endapo kama giza
lingepiga basi pasingeonekana kabisa. Ikambidi aliache gari na kwenda karibu zaidi ili aitazame
vizuri, naye akaona namna ilivyokuwa ndogo kiasi, ikiwa imejengwa kwa mbao na magogo juu
mpaka chini, lakini sehemu za madirisha zikiwa ni vioo. Hakukuonekana kuwa na mtu hapo, na ni sauti za ndege mitini na upepo uliopuliza matawi ya miti ndizo pekee zilisikika.

Eneo hilo, kwa jinsi tu lilivyokuwa, ingekuwa rahisi kwa yeyote kuogopa kwa sababu kulikuwa na hali fulani yenye kutisha, kama vile kujua hauko peke yako sehemu kama hiyo ingawa hakuna uwepo wa watu wengine. Lakini Namouih alijitahidi sana kuwa jasiri na shupavu, bastola ikiwa
mikononi mwake alijiona kuwa na nguvu ya ziada iliyomsaidia kuzizima hofu zake kwa kadiri kubwa. Alikuwa akiwaza kwamba ni lazima Draxton alihusika moja kwa moja na sehemu hiyo, na alipotazama sehemu ambayo alijua ndiyo mwingilio wa nyumba hiyo ndogo, akaona pakiwa
pamefungwa kwa kufuri kubwa na zito sana. Kwa hiyo akaamua kurudi kwenye gari lake ili aende sehemu nyingine kwanza, ikiwezekana amsubirie mwanaume huyo afike huku ili yeye Namouih aitekeleze nia yake ya kuukomesha mchezo wake mchafu. Kila kitu kingetakiwa kufanyika kwa mikono yake kwa sababu hakuna mtu aliyetaka kumwamini, kwa hiyo angejivika roho ya kikatili pia ili kumwondoa mkatili.

Alianza kuendesha gari lake ili arudi kule alikotokea, na njaa aliihisi vyema ingawa alipuuzia hilo, lakini njia za kumrudisha alikotoka zikampiga chenga. Hakukuwa na barabara ya moja kwa moja
iliyomfikisha huku alipofika isipokuwa tu kwa sababu ya jitihada zake za kutokata tamaa. Kurudi
kule, angetegemea kifaa cha ramani cha kwenye gari, yaani GPS, lakini katika mzunguko wake NDANI ya msitu huo hakutumia njia hususa, hivyo akakosa kujua apite wapi. Akajaribu hata kutumia maarifa; aangalie uelekeo mmoja kwenye kifaa chake ambao ungempeleka moja kwa moja mpaka kwenye barabara kuu, lakini shida ikawa kwamba miti, mabonde, na miinuko
iliyoingiliana na uelekeo huo ingemzuia kwenda moja kwa moja, na kila mara ambayo angejaribu
kugeuza mkondo, basi angetakiwa abadilishe uelekeo, yaani kwa maneno mengine aanze upya kila
mara ambayo angekutana na vizuizi vya namna hiyo.

Mwanzoni hii ilionekana kama shida ndogo tu lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda ndiyo ikawa wazi kwamba alikuwa amejipoteza sana, na msitu huo ulikuwa mkubwa kuliko alivyodhani. Inafika saa kumi na mbili jioni ndiyo wazo la kutafuta msaada kwa simu likamjia. Alipojaribu kutafuta mawasiliano, mtandao ukazingua. Piga, piga, piga, wapi. Pole kwa pole giza likaanza kuingia, na wakati huu alikuwa akihisi njaa SANA, ila alichowaza zaidi ilikuwa ni njia ya kutoka huko haraka mno, kwa hali na mali yoyote. Akaendelea na jitihada zake za bila kuchoka kutafuta njia ya kutokea
mpaka akawa anahisi kutaka kulia kwa sababu ya hali hii yenye kuvunja moyo sana. Hapa ni yeye ndiyo alikuwa anajaribu kutafuta haki kwa sababu aliona mambo yaliyotokea kutokuwa sawa kihaki, lakini bado tena ni yeye ndiyo akawa anaadhibika.

Akafika sehemu fulani ya wazi kiasi na kulisimamisha gari lake, na alipotazama saa akakuta ni saa
mbili usiku tayari. Sasa alihisi kuchoka. Akatulia tu hapo na kuanza kulia kwa sauti ya chini, akikumbukia maneno ya mume wake alipomuonya kuhusu kufanya mambo ambayo
yangemwingiza kwenye shida tu, na sasa alikuwa akiipitia. Akainamisha kichwa chake kwenye usukani huku akipumua kwa nguvu, naye akaukaza usukani kwa viganja vyake akihisi kufadhaika sana. Lakini Namouih kama Namouih hakuwa mtu wa kupoteza matumaini kabisa, naye
akanyanyua uso wake na kujifuta machozi, kisha akaanza kulitia gari mwendoni ili aendelee na jitihada zake. Halikuwa hata limemaliza mita mbili pale alipolisimamisha ghafla na kutazama mbele yake.

Hapo mbele, aliweza kuona gari lingine likija upande wake, taratibu, lakini kama vile linataka kuja
kumgonga. Taa za mbele za gari hilo zilimulika sana hivyo Namouih hakuweza kutambua ni la nani hasa; katika maana ya ikiwa ni gari la mtu mwenye urafiki, au adui. Akaichukua bastola yake na kuishikilia kiganjani kwa utayari, na gari hilo likasimama mbele yake kwa umbali mfupi sana
kutokea kwenye la kwake, kisha taa zake zikazimwa. Namouih sasa akawa amejihakikishia kwamba hilo lilikuwa ni gari la Draxton. Kama waswahili wasemavyo, usiyempenda kaja. Namouih akaendelea kutazama tu huko nje, akiona jinsi mlango wa gari hilo ulivyofunguliwa, Draxton
akishuka na kusogea mbele kidogo, kisha akasimama kama anamsubiria.

Namouih alikuwa anawaza atoke tu na kumpasua kichwa kwa kuwa jamaa alichagua muda mzuri sana wa kumfikia, usiku, hivyo angelimaliza tatizo hilo upesi na kuendelea na safari zake. Alikuwa
ameshautia moyo wake ugumu namna hiyo, naye akaendelea kukaa tu ndani ya gari akisubiri kuona mtu huyo angefanya nini. Draxton akaonekana kupindisha shingo kidogo kama vile anachungulia, kisha akanyanyua kiganja chake na kutoa ishara kama kuuliza 'vipi?' naye Namouih akawa anamwangalia kwa hisia kali. Taa za gari la Namouih bado zilimulika mbele hivyo Draxton alionekana vizuri sana. Alivalia shati la jeans lenye rangi ya samawati, ambalo hakulifungia vifungo kuonyesha T-shirt nyepesi nyeupe kwa ndani, suruali nyeusi pia na viatu vyeupe; mwonekano wake
wa kawaida tu.

Namouih alikuwa akimtazama kwa chuki kuu moyoni, huku mapigo yake ya moyo yakidunda kwa nguvu sana kutokana na msisimko wa hisia nyingi kuvurugikana ndani yake. Akajivika ujasiri zaidi na kuufungua mlango, naye akatoka na kuanza kupiga hatua mbele huku mkono ulioshika bastola akiuweka kwa nyuma. Alikuwa anataka kusikia lolote lile kutoka kwa mtu huyo kabla hajamfumua risasi, ikiwa ni kitu alichodhamiria kufanya kwa asilimia zote. Akasimama mbele ya gari lake
akiiziba taa moja kwa mwili wake, na akimwangalia Draxton kwa hisia kali. Draxton alikuwa anamtazama kwa umakini tu, na ikawa wazi kwamba wote walisubiri mmoja wao ndiyo aanze kusema kitu.

Draxton akavuta pumzi ndefu na kuishusha akiwa anaangalia pembeni, kisha akamtazama tena
machoni. "Unafanya nini huku?" akauliza kistaarabu.

"Nikuulize na wewe," Namouih akasema.

"Namouih ingia kwenye gari... nifate."

"Unipeleke wapi? Kuzimu?"

"Kuna watu wanaokupenda, wanaowaza juu yako, wanaokutafuta sana kwa sababu hawajui ulipo..."

"Kwani me ni mtoto?"

"Huu unaofanya ni utoto Namouih! Kwa nini uko hapa? Bado una hii... crazy theory kwamba mimi ndiyo nimemuua rafiki yako, siyo? Watu uliowatuma jana wanipeleleze hawakukwambia vitu
vilivyokuridhisha eh? Unafikiri kwamba utapata kitu fulani huku?"

"Sijaja kutafuta chochote ili kuthibitisha nachojua kuwa kweli. Nimekuja kuliondoa tatizo
linalosababisha hayo yote."

"Namouih...."

Kabla Draxton hajaendelea, Namouih akamnyooshea bastola kwa uhakika kabisa na kuishika na mikono yote sasa. Draxton akaacha kuzungumza na kubaki amemwangalia kwa ufupi, kisha akatazama chini kwa njia ya kusikitika.

"Usifikiri leo nimekuja kimasihara. Huu ndiyo mwisho wako Shetwani wewe!" Namouih akamwambia kwa mkazo.

"Namouih ni hatari sana kwako kuwa huku, hujui hilo."

"Acha kujifanya mwema mpuuzi wewe. Unaniongelesha namna hiyo kwa sababu unajua nitakuua, siyo? Unafikiri unaweza kuitumia hiyo njia kunirubuni ili na mimi unimalize, si ndiyo?"

"Mambo hayako kama unavyofikiria. Sijaua mtu yeyote mimi..."

"Nadhani ulikuwa unaiambia hivyo hivyo maiti ya Felix baada ya kuikata ulimi na tumbo..."

"Kwa nini nimuue Felix, Namouih? Hata nilikuwa simjui!"

"Wapi imeandikwa kwamba ni lazima kumjua mtu ili kumuua? Logic mpya za ma-serial killer au? Ulijua nilimweka akufatilie, na kwa kuwa angekuvuruga na yeye ukaona umuue."

"Ulimweka anifatilie?"

"Funga mdomo wako. Mwanzoni ulinifanya niogope, lakini sasa hivi hapana. Ni mimi ndiyo nilimweka Felix kwenye njia hiyo iliyomsababishia kifo... kifo kwa mikono yako. Ni bora hata
nisingemwambia akufatilie... hhh... umemuua kwa sababu yangu. Na sasa nitahakikisha unalipia kifo chake," Namouih akaongea kwa hisia huku akilia.

"Ninajua Felix alikuwa muhimu kwako lakini unachofanya now si sahihi. Sijamuua. Kila jambo liko wazi kabisa kwamba sikumuua, umepofushwa tu na chuki yako kunielekea ndiyo maana hutaki
kukubali ukweli. Namouih nakuomba ushushe bastola tuongee vizuri," Draxton akamwambia kwa upole.

Namouih hakutii hilo. Akaendelea kumnyooshea bastola huku akipumua kwa hasira.

"Ni vitu vingi vinakuumiza, hilo najua. Lakini unapaswa utambue kuwa hata kama ukiniua mimi, mambo unayodhani mimi ndiyo nasababisha hayatakwisha. Na itakuja kukuumiza zaidi ukigundua kwamba uliondoa maisha ya mtu asiye na hatia, na tayari itakuwa kuchelewa. Namouih wewe siyo muuaji, na wala usifikiri kuniua mimi itakupa amani... ni jambo baya sana litakalokuandama kwa maisha yako yote. Utanawa mikono yako lakini utakachobaki kuona itakuwa ni damu tu
uliyomwaga. Felix ameuawa kikatili, itakuwa jambo la busara tukishirikiana kujua ni nani amemuua ili apate malipo kwa ubaya huo..."

Draxton alipokuwa anasema maneno hayo alikuwa anapiga hatua chache kumwelekea Namouih mpaka alipofikia bastola yake, ambayo sasa ikagusa kifua chake kabisa. Namouih alikuwa anajitahidi kuonyesha kwamba amekaza bado, hataki kabisa masihara, hivyo akaendelea kumwelekezea namna hiyo hiyo huku akimtazama kwa ukali.

"Wewe ni mtu mzuri Namouih, usichukue hatua hii. Najua kuna mambo kuhusu mimi ambayo ni
fumbo kwako, na haitakuwa rahisi kuelewa jinsi maisha yangu yalivyo lakini sijafanya ubaya huo
unauosema juu yangu. Niruhusu nikusaidie, tusaidiane. Nina imani tutapata suluhisho kwa mambo haya lakini hili siyo suluhisho unalohitaji Namouih," Draxton akaongea kwa ushawishi.

Namouih hakutaka kabisa kumwamini, kwa sababu aliona maneno yote hayo ya jamaa kuwa njia ya kumrubuni ili aweze kumdhuru. Lakini tena kuna kitu ambacho kilikuwa kinamvuta nyuma
kutofyatua risasi, kwa kuwa kwa ukaribu huu alianza kuona jinsi jambo hili lilivyokuwa zito kuliko namna alivyodhani. Draxton akashika viganja vya mwanamke huyu, na taratibu akaanza kuvishusha chini ili Namouih aache kumwelekezea bastola. Vilishuka ndiyo, lakini Namouih
akavipandisha tena na kumwelekezea silaha hiyo upya kifuani.

"Namouih tafadhali... tafadhali nipe hii silaha... hiki siyo kitu unachotaka kufanya..."

"Usiniongeleshe hivyo. Haunijui. Haujui ninachokitaka na nisichokitaka..."

"Najua hautaki kuwa mnyama, na ukifanya hivi utakuwa mnyama."

"Kama nani... kama wewe?"

"Ningekuwa nataka kukudhuru ningekuwa nimeshafanya hivyo, hata sasa. Lakini kwa nini hauoni kwamba ninakupatia nafasi ya kutambua mwenyewe aina ya mtu ambaye ni wewe?"

"Unanipa nafasi wewe kama Mungu au?"

"Namouih acha tafadhali... nipe hii silaha..."

Draxton akajaribu kuvishika viganja vya Namouih tena, lakini mwanamke huyu akagoma na kurudi nyuma kidogo. Ikabidi atumie nguvu kiasi ili aweze kumnyang'anya, naye Namouih akaweka upinzani zaidi na kuivuta kwa nguvu.

"Namouih acha... please... utajiumiza!"

"Niachie... nimesema niachie..."

Draxton akaivuta kwa nguvu, kitu kilichofanya Namouih avutwe kwake pia kutokana na kuingang'ania bado, na miili yao ikakutana karibu zaidi. Mikono yao ilikuwa kwa chini sasa katika vuta nikuvute hiyo, na ni hapo hapo mlio wa risasi ukasikika kwa nguvu sana! Namouih akaachama
huku ametoa macho kwa sababu ya mshtuko wa ghafla uliomwingia, huku akimwangalia Draxton
ambaye bado alikuwa karibu yake sana. Draxton akaibana midomo yake na kufumba macho, kisha
akainamisha uso wake kama mtu anayetaka kulia. Pumzi za Namouih zikaanza kutetemeka, naye akarudi nyuma kidogo na kutazama tumboni kwake. Damu zilionekana kulowanisha sweta alilokuwa amevaa, lakini hazikuwa zake. Alipomwangalia Draxton, akaona akiwa amejishika ubavuni huku damu nyekundu sana ikivia kwenye T-shirt yake nyeupe kama wino.

Namouih akaidondosha bastola kwa kuhisi ni kama nguvu imemtoka, naye akamwangalia Draxton, ambaye sasa alikuwa ameishika sehemu hiyo iliyopigwa kwa risasi kwa mikono yake yote huku akimwangalia Namouih kwa uso ulioonyesha alijitahidi kukaza maumivu. Akarudi nyuma kilegevu na kuliegamia gari lake kwa mbele, akiwa amekandamiza mkono mmoja hapo huku mwingine ukishikilia tumbo. Namouih alihisi kuchanganyikiwa. Midomo yake ilitetema sana, pumzi zikishuka na kupanda bila utaratibu. Aliogopa sana. Alivyokuwa ametazamia jambo hilo kwenda ikawa tofauti na uhalisia alioupata. Akamwangalia Draxton na kuona jinsi alivyojitahidi kukaza maumivu, akipumua kwa nguvu sana na jasho likimtoka kwa wingi. Akashindwa kujua la kufanya, lakini ilikuwa ni kama akili yake ya kawaida ilimrudia baada ya jambo hili kutokea. Kweli alikuwa ni kama amepotea kabisa mpaka kufikiria kuua mtu, na uzito wa jambo hilo ukakolezwa zaidi baada ya kuona mwanadamu
mwenzake akiteseka namna hiyo, tena kwa sababu yake. Kilichoingia akilini mwake sasa hivi ilikuwa ni kumsaidia Draxton kwa njia yoyote ile ambayo angeweza.

Akiwa bado anaogopa, akamsogelea karibu zaidi na kuanza kusema, "Draxton... Ddrax... am so
sorry... am... a... sikuwa... siku..."

Akawa anaongea kwa sauti tetemeshi iliyoonyesha woga wake mwingi. Badiliko hili la moyo kutoka kwa mwanamke huyu halikuvuta umakini wowote kutoka kwa Draxton kwa sababu alionekana kupambana zaidi na maumivu aliyokuwa akihisi.

"Tuna... tunahitaji uende... hospitali... twende hospitali... oh Allah... nimefanya nini? Draxton... twende kwenye gari... nikupeleke..."

Namouih alikuwa anaongea hayo huku akikumbuka vizuri kabisa kwamba njia ya kutoka huku
hakuifahamu, lakini ilikuwa ni jitihada ya kuhakikisha angefanya lolote ili kumtoa mwanaume huyo
kwenye maumivu. Akamshika upande wa juu wa mkono wake, akijaribu kuupitishia begani kwake,
lakini Draxton akagoma kuutoa.

"Draxton tafadhali.... unahitaji tiba..." Namouih akasema.

Draxton alikuwa akipumua kwa nguvu sana. Alionekana kupata shida mno, na hilo likamwongezea
simanzi mwanamke huyo. Akakishika kiganja cha Draxton ili aanze kumsisitizia kuhusu kwenda
hospitalini kupata tiba, lakini akakiachia ghafla na kwa kasi sana. Kilikuwa cha moto kupita kiasi.
Yaani aliungua mkononi kama vile amegusa maji au pasi ya moto. Akamtazama tena mwanaume
huyo na kuona jinsi alivyopumua kwa uzito mwingi sana, naye akashindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kikimpata zaidi.

"Draxton..." Namouih akaita.

Draxton akapiga ngumi juu ya buti la kufunikia sehemu ya mbele ya gari lake, nayo ikakunjika. Namouih akabaki kumwangalia kimshangao.

"Nam... Nnamoouih..." Draxton akaita hivyo kwa sauti... mbili.

Namouih akabaki kumtazama kwa butwaa.

"Na... Namouih... nakuomba ukimbie... kimbia!"

Eh! Aliongea kwa sauti nzito iliyobadilika kutoka kwenye ile yake ya kawaida. Namouih hakuweza
kuelewa ni kwa nini hiyo ilikuwa ikitokea, lakini akahisi kwamba bado angeweza kumsaidia.

Akamsogelea tena na kusema, "Draxton... nini shida? Risasi... una... unahitaji..."

"Nahitaji ukimbie Namouih... kimbia!" Draxton akasema hivyo huku ameinamisha uso wake kwenye
gari.

"Lakini Draxton...."

Kabla Namouih hajamaliza maneno yake, Draxton akamgeukia ghafla na kumwangalia. Namouih alishtuka sana na kurudi nyuma kidogo, kwa sababu macho ya mwanaume huyo yalikuwa yanang'aa rangi ya blue kutokea kwenye lenzi zake. Yalikuwa yale macho makali sana kwa jinsi
alivyomtazama Namouih, na jambo hilo lilimtia hofu sana. Mwanaume huyo akatoa sauti ya muungurumo na kuinamisha tena uso wake kwenye gari, na Namouih akaanza kuona ngozi ya Draxton ikibadilika na kuwa nyeupe kama ya mzungu, huku kichwani kwake nywele nyeupe kabisa zikianza kuota; yaani zikiota na kuongezeka. Zilikuwa ndefu na laini, zikikua na kukua mpaka
zilipofunika sehemu yote ya juu ya kichwa chake kufikia mgongoni, naye Draxton akapiga goti chini huku bado akiendelea kuhangaika. Mkono wake uliokuwa umeshikilia gari ukaanza kuota nywele hivyo hivyo sambamba na mkono wake mwingine, na makucha marefu yakaanza kuonekana yakikua vidoleni mwake!

Namouih alichoka. Yaani ikiwa na hii ilikuwa ni ndoto nyingine, basi alijua asingeamka kamwe, kwa sababu ilikuwa kwenye ulimwengu halisi.

"RUN!!!"

Sauti hiyo nzito kutoka kwa Draxton ikamwondolea mwanamke huyu bumbuazi la woga uliokuwa
umepanda maradufu, naye akalifata gari lake upesi ili aondoke haraka sana. Akaingia na kuliwasha huku vidole vyake vikitetemeka haswa, na ile alipotaka kulirudiaha nyuma kishindo kikubwa kutokea mbele kikamfanya apige kelele kwa hofu. Alitazama huko mbele na kuona kwamba, Draxton, au kiumbe huyo, alikuwa amepiga sehemu ya mbele vya gari na kusababiaha
pajikandamize vibaya sana, hivyo kuna mifumo iliyoharibika na kufanya gari lisiweze kutembea
tena. Akamwangalia tu na kumwona akiendelea kuhangaika na kugaagaa chini huko nje, naye Namouih akafungua mlango na kuamua kukimbia tu kwa miguu.

Moja ikageuka mbili ikageuka tatu ikageuka nne. Mambo yalizidi kubadilika na kubadilika. Yaani kila mara Namouih alipodhani amefikia ukomo wa jambo moja, lingine lingejitokeza tu, tena katika njia zisizofikirika kabisa. Aliendelea kukimbia msituni hapo huku akilia sana. Aliogopa. Palikuwa na giza, na mara kwa mara alianguka na kujigonga kwenye miti na vichaka, lakini akaendelea tu kusonga huko huko kusikojulikana. Alikuwa amechoka SANA. Kihisia, kimwili, kifikira, yaani alikuwa tupu kabisa isipokuwa ya hii nguvu ndogo ambayo hakujua ilitokea wapi ambayo iliendelea kumsukuma ajitahidi kuikimbia shida ile.

Akafika sehemu moja na kusimama, akihisi kuishiwa pumzi, naye akawa anakohoa huku akilia kwa sauti ya chini. Akachuchumaa na kupiga magoti chini huku bado akilia, na kwa hapa akawa anayahisi vyema maumivu aliyopata mwilini kutokana na kujigonga na kuanguka mara kwa mara. Alielewa fika kwamba huenda jitu lile kwa jina la Draxton lingekuwa linamfatilia, hivyo kukaa hapo
kusingekuwa na matokeo mazuri kwake. Kwa kuwa alikuwa amechoka mno, akafikiria apande mtini na kutulia huko juu, hivyo akasimama na kuvua viatu vyake vyeupe, kisha akavirusha mbali, naye akaufata mti mmoja na kuanza kujaribu kuupanda.

Jitihada zake zikakoma na kumfanya atulie baada ya kusikia sauti fulani. Haikuwa sauti ya muungurumo kama aliotoa Draxton, bali ilikuwa sauti ya kicheko. Hakutaka hata kugeuka nyuma, naye akaendelea kujaribu kupanda mti bila mafanikio huku akitetemeka sana. Sauti hiyo ya kicheko ikasikika tena, lakini hakikuwa kicheko cha kawaida kabisa. Alipoweka umakini wake vizuri, sauti hiyo ya kicheko ikatambilulika kwake, naye akaelewa sasa kwamba ilikuwa ni kicheko cha fisi. Upande kilipotokea, ilionekana kwamba fisi huyo alikuwa karibu sana, hivyo Namouih akaanza
kuelekea upande mwingine tena, na wakati huu alikuwa mzito sana kutokana na miguu yake isiyokuwa na viatu kuumia kila alipokanyaga chini. Kila hatua aliyopiga sauti ile ya kicheko ilikuwa naye, nayo ikaongezeka idadi na kuwa ni kama fisi wengi ndiyo wanamfata huku wakicheka. Aliumia sana miguuni mpaka akashindwa kusonga mbele zaidi na kuanguka tu chini.

Akageukia nyuma yake huku akiwa amekaa, akizisikia sauti hizo bado, na zilikuwa zinamchanganya sana kwa kusikika huku na kule na hivyo yeye kushindwa kujua fisi hao walikuwa wapi kihalisi. Haya majanga aliyokuwa amejiingiza ndani yake yalizidi kuwa mabaya tu, na sasa hakukuwa na njia tena ya kutoka hapo akiwa salama. Upande wake wa kushoto, akatokea fisi
mmoja aliyekuwa akionekana zaidi macho lakini mwili ukifichwa zaidi na giza, naye Namouih akajitahidi kusimama na kubaki amemwangalia tu. Wazo la kwamba huenda huyo fisi alikuwa ndiyo Draxton aliyegeuka na kuwa fisi-mla-watu likamwingia, na hakuonekana kutaka kumsogelea
Namouih kwa sababu aliendelea kusimama tu huko huko.

"Toka... toka!"

Namouih akajaribu kumtisha ili amwache, lakini mnyama huyo akaganda hapo hapo tu. Hajatulia
vizuri, upande wa kulia wakatokea fisi wengine wawili kutoka vichakani, nao wakawa kama wamemzingira. Akajitia ujasiri tena masikini, akijaribu kuwafokea, lakini wakaanza kujongea taratibu kumwelekea. Aliogopa mno. Alipomshtua wa upande huu, wa upande mwingine
angemsogelea karibu zaidi, na walimfanyia kama mchezo wa kumfanya atambue kwamba hakuwa
na sehemu ya kukimbilia. Namouih akawa analia sana, akihisi kuchoka, yaani kuchoka kuupambania uhai wake ambao alielewa haukuwa na thamani yoyote mbele ya viumbe hao
isipokuwa yeye kuwa kama chakula tu. Hapa sasa ndiyo akawa amepoteza matumaini kabisa. Hivi hata alijikutaje kwenye hali hii?"

Mwanamke huyu akiwa anaelewa wazi kwamba huu ulikuwa ni mwisho wake, na fisi hawa wakiwa karibu yake zaidi, sauti ya muungurumo wa chini ikasikika sehemu hiyo. Namouih alitambua kuwa
sauti hiyo haikutokea kwa yeyote kati ya fisi wale, kwa kuwa hata baada ya wao kuisikia wakaacha kumfata na kusimama huku wakionekana kuangaza pande tofauti-tofauti; bila shaka kutafuta chanzo. Namouih sasa alikuwa akipumua kwa hofu bila kulia, akitetemeka, na akiwaangalia fisi hao, pale muungurumo huo uliposikika kwa mara nyingine tena. Zamu hii, muungurumo huu uliendelea tu bila kukata, kwa sauti isiyo ya juu sana, na wale fisi wakaanza kutangatanga sasa. Muungurumo huo uliposikika karibu hata zaidi, Namouih akatambua kwamba ulikuwa unatokea nyuma yake, naye akageuka taratibu huku akihisi ni kama vile hana miguu kutokana na kuishiwa nguvu.

Kutokea kwenye kichaka kikubwa upande huo aliogeukia, akatoka mnyama MKUBWA akitembea
taratibu sana, meno yake makali mdomoni yakiumana, na sauti hiyo ya kuunguruma ikiendelea.
Namouih alimeza mate kwa shida kutokana na hofu iliyopanda zaidi ndani yake. Mnyama huyo alikuwa mweupe, mwenye macho makali yaliyozungukwa na giza fulani hivi na lenzi zenye rangi ya blue, meno marefu, na mwili wake ulionekana kuwa na nguvu nyingi. Alikuwa wa jamii za mbwa mwitu (wolves), lakini wale hasa wanaopatikana kwenye milima ya mabarafu nchi za nje, kwa
sababu kwa nchi hii hakukuwa na wanyama wa jamii hii. Lakini mwili wake ulizidi hata ule wa simba dume mkubwa, akionekana kuwa mara tatu zaidi ya hapo kwa sababu ingawa Namouih alikuwa mrefu kwa kusimama, bado aliangaliana naye machoni kwa usawa. Ni hapa ndiyo Namouih akadondoka kwa mara nyingine tena, akijua habari yake ni kwisha.

Mnyama huyo akaendelea kumfata na kumkaribia zaidi huku akiendelea kuunguruma, na hata wale fisi wakawa wanajirudisha nyuma lakini hawakuondoka hapo kabisa. Jinsi manyoya ya mnyama huyo yalivyokuwa meupe sana ilimfanya aonekane vizuri mno gizani hapo, naye Namouih akavilaza viwiko vya mikono yake chini na kukilaza kichwa chake chini pia baada ya huyu mnyama kumfikia karibu kabisa na uso wake. Ingawa alikuwa anaogopa, Namouih aliweza kuendelea kumwangalia, akitazamana macho kwa macho na kiumbe huyo hatari sana. Mnyama huyu alikuwa akimtazama Namouih huku ameng'ata meno yake kwa hasira, kisha akafungua kinywa chake na kuanza kuunguruma huku akirudisha kichwa chake nyuma kidogo.

Namouih akijua fika kwamba hapo alikuwa anajivuta ili aanze kumtafuna, akafumba macho yake
na kugeuzia shingo pembeni, akiwa hataki kuona jinsi ambavyo kinywa hicho kingerudi usoni mwake. Mnyama huyo akaachama mdomo wake na kukielekea kichwa cha Namouih, naye akapiga kelele nzito ya muungurumo, kitu kilichofanya ionekane ni kama anataka kukimeza kichwa chote cha mwanamke huyo kutokana na upana wa mdomo wake. Ilimuumiza Namouih sana sikioni, naye akabaki tu kuyafumba macho yake kwa nguvu sana.

Lakini baada ya mnyama huyo kumaliza kupiga kelele hizo, akaelekeza umakini wake kwa wale fisi watatu, naye akawaungurumia pia kwa hasira. Fisi walionekana kuogopa lakini bado wakajitia ujasiri wa kuendelea kubaki hapo, hivyo mnyama huyo akamvuka Namouih na kuwafata. Namouih aliweza kuhisi uwepo wa mnyama huyo ukiondoka karibu yake, naye akafumbua macho na hapo hapo kusikia kilio cha maumivu kutoka kwa fisi mmoja. Akajigeuza na kutazama kule ambako fisi walikuwa na kumwona mnyama huyo mkubwa akiwa amemkamata fisi mmoja mdomoni mwake na kumrusha huku na huko kwa nguvu sana, na wale fisi wawili wakakimbia kutoka hapo. Fisi
aliyekuwa amekamatwa kwa mdomo akararuliwa vipande viwili na vyote kurushwa juu, kisha mnyama huyo mkubwa akaunguruma na kutoka kwa kasi sana hapo, akiwafukuzia fisi wale wengine.

Namouih alikuwa amebaki chini hapo akipumua kwa mtetemo, kisha akaanza kujitahidi kunyanyuka tena. Akili yake ilikuwa kama imekufa ganzi, hakuwaza wala kujiuliza chochote tena, ilikuwa ni yeye kunyanyuka na kuondoka. Akawa anainuka kilegevu na kuweweseka, jasho likimtoka sana, kifua kikiwa kimekaza, miguu ikitetemeka, na baada ya kujaribu kupiga hatua
chache, akadondoka na kupoteza fahamu.


★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumatatu, Jumanne, na Jumatano. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA SABA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Siku ikakucha hatimaye. Mpaka inafika mida ya saa tano asubuhi, Efraim Donald hakuwa amepata
lepe hata moja la usingizi kutokana na kumuwaza sana mke wake. Siku nzima iliyopita mpaka kunakucha alikuwa anakwenda huku na huko akiongea na watu wengi kwa simu na kutafuta baadhi ya watu ambazo wangemtafuta mke wake maeneo mbalimbali jijini hapo. Alikuwa
ameshatafuta karibia hospitali zote na kutumiwa majibu kwamba hakukuwa na mwanamke wa jina
la Namouih aliyeendana na jinsi aliyomwelezea, na sasa akawa amekwenda kutoa taarifa polisi ili
msako kwa ajili ya kumpata mke wake ufanywe. Hakuzungumza na maaskari-uchwara, bali wenye
mafunzo na walio makini na kazi ili kuhakikisha matokeo yanakuja vizuri; hata kama ingehitajika awalipe pesa nyingi angefanya hivyo.

Blandina pia alikuwa akimtafuta rafiki yake kipenzi kwa bidii sana, ingawa mara ya mwisho hawakuwa wameachana kimtazamo mzuri. Alikuwa amemuulizia kwa wengi kati ya marafiki zake, na jibu lilikuwa ni lile lile tu lenye kuvunja moyo. Hata yule mwajiri wao kwenye kampuni
waliyofanyia kazi, yaani Mr. Edward Thomas, alifanya jitihada za kutafuta mahali ambako mwanasheria wake mkuu angekuwa amepotelea, na msako huo ulifanywa kwa umakini sana kuonyesha kwamba Namouih alikuwa mtu wa muhimu na pekee kwa wengi. Blandina alikuwa
amejaribu sana kumtafuta Draxton pia lakini simu ya mwanaume huyo haikupatikana. Akaamua hadi kwenda na kwake pale alipopanga ili kuona ikiwa alikuwepo ila akaambulia patupu. Alikuwa
amechanganyikiwa sana kwa sababu sasa ilionekana ni kama alikuwa amewapoteza watu wawili
muhimu kwake.

Efraim Donald aliahirisha mipango na majukumu yote ya kikazi kwa muda huu ili kukazia fikira suala la kumpata mke wake kwanza. Alikaa nyumbani akipokea na kupiga simu huku na kule bila kuacha, na Esma pamoja na Suleiman walikuwa karibu wakitaka kujua jambo lolote jipya lenye uchanya kumhusu bibie lakini bado hawakupata taarifa nzuri, wala mbaya. Esma akawa ameshauri
kwamba wampigie mama yake Namouih, labda hata angekuwa amempa taarifa za alikokuwa,
lakini Efraim Donald akasema Zakia hakujua lolote, na ingetakiwa kubaki kuwa namna hiyo hadi ahakikishe Namouih anarudi nyumbani akiwa salama salimini ili kutompa mama yake mawazo yasiyofaa.

Muda ukazidi kusonga mbele bila ya taarifa zozote juu ya mwanamke yule kusikika, na hiyo hasa ilitokana na yeye kutafutwa sehemu nyingi ndani ya jiji na siyo sehemu za mapori ambako isingefikirika kwa yeyote kwamba mwanamke yule alikuwa amekwenda kwenye moja ya sehemu
za namna hiyo, na kilichokuwa kimemkuta usiku wa kuamkia sasa kilikuwa kitu cha kutisha sana.
Namouih angekuwa wapi baada mambo yale yote kumpata?


★★★


Sauti za ndege wakiimba zilisikika vyema, na kitu fulani kama msuguano wa msasa na mbao
ukawa ukipiga kona za masikio ya Namouih. Haikuwa rahisi kutambua zilitokea wapi lakini kuna jambo lililokuwa linamvuta nyuma kumfanya asijue. Akapambana vya kutosha kuliondoa na taratibu akafumbua macho yake. Alikuwa ndiyo anarejesha fahamu sasa, na polepole akawa anajaribu kuichora vizuri taswira ya sehemu aliyokuwepo kwa wakati huu.

Hapa alikuwa amelala kitandani, ndani ya chumba fulani. Kilikuwa chumba kidogo tu chenye giza kiasi, lakini vitu vilionekana vyema. Alikuwa amelala chali, hivyo kwa kugeuza shingo yake kidogo
akaweza kuona viti viwili vya mbao upande wa pembeni, kitu kama kabati ndogo lenye droo kadhaa, boksi kubwa kwa chini lililojaa vitu fulani, kuta za mbao zilizokuwa na vitu fulani virefu kama vile mabomba lakini ya vioo vyembamba, yaani taa, na mlango kwa mbele zaidi. Hakukuwa hata na dirisha, lakini hewa haikuwa nzito na hata kulikuwa na hali fulani ya ubaridi wa chini kama vile panapulizwa kwa feni. Akiwa ameanza kuingiwa na wasiwasi hasa baada ya kukumbukia
alipokuwa mara ya mwisho, akajivuta na kuketi kitandani hapo. Kilikuwa ni kitanda kidogo tu, cha mtu mmoja lakini kingetoshea wawili kama wangelala vizuri, na kilibananizwa kwenye kona ya ukuta wa chumba hicho.

Akajishangaa sana. Alifikaje hapo? Siyo kwamba alitakiwa kuwa amekufa? Au labda alikuwa
ameshakufa? Kama hii ilikuwa ni mbingu basi alikuwa amewekwa kwenye kona ya mwishoni kabisa! Kulikuwa na shuka hapo ambalo ndiyo alikuta limeifunika miguu yake kufikia kiunoni, naye akaliondoa miguuni kwake na kujiangalia vizuri. Angetarajia hata kukuta michubuko au kuhisi maumivu miguuni na mwilini, lakini haikuwa hivyo. Yaani alikuwa bila mkwaruzo wala doa lolote sehemu alizojua aliumia usiku ule. Akajiuliza ni muda mrefu kadiri gani ungekuwa umepita tokea usiku huo, lakini asingeendelea kukaa hapo akiumiza kichwa. Sweta alilokuwa amevaa usiku ule halikuwepo tena mwilini mwake, akiwa amebaki na T-shirt yake nyeusi na suruali yake laini ya kijivu, naye akaamua kushuka kitandani ili aangalie uwezekano wa kuitoroka sehemu hiyo.

Alikuwa ndiyo ameiweka tu miguu yake chini na kuanza kujitoa kitandani hapo kwa uangalifu pale
mlango ule ulipofunguliwa na kuanza kusogea kwa ndani. Alishtuka sana na kurudi kitandani upesi, akijibananiza kwenye kona ya ukuta huku akijishikilia miguuni kwa hofu. Aliona mkono ulioshikilia mlango huo ukiendelea kuingia, na mwenye nao akaingia ndani pia hatimaye. Pumzi za Namouih ziliongezeka kasi kwa kupandwa na woga baada ya kumwona Draxton hapo, na wakati huu akiwa kama Draxton. Alikuwa amevalia T-shirt nyeupe na bukta ya rangi ya kijani-nyeusi, mwili wake imara ukionekana vyema. Alikuwa amesimama mlangoni akimwangalia Namouih kwa njia fulani ya huruma, na kuingia kwake hapo kulifanya chumba kiangazwe zaidi, jambo lililoonyesha kwamba haikuwa usiku.

Draxton akapiga hatua tatu mbele, taratibu, naye Namouih akajibana zaidi huku akionekana kutaka kuanza kulia. Draxton akasitisha kupiga hatua na kusimama tuli, akinyanyua mikono yake juu
kumwonyesha Namouih kwamba hakuwa na lengo la kumuumiza, lakini hicho ni kitu ambacho
mwanamke huyu hangeamini kabisa baada ya mambo yote aliyojionea.

"Namouih..." Draxton akaita kwa sauti ya upole.

Namouih akaendelea tu kumwangalia kwa hofu.

"Naelewa unaogopa... na una kila sababu ya kuogopa... lakini sina nia ya kukuumiza... sitakuumiza..." Draxton akasema kwa upole.

Namouih akawa anatikisa kichwa kwa njia ya kukataa, akipinga fikira yoyote ile ya kuamini jambo lolote ambalo mtu huyo wa ajabu angesema.

"Okay... look... usiniamini, alright? Unaweza kuniona mimi kuwa mbaya... sikulaumu. Unaweza ku...
kufanya kama precaution ya kujilinda. Hapo hivi... pembeni ya kitanda... ipo pistol yako. Ichukue
ujilinde," Draxton akamwambia.

Namouih alimtazama sana kama vile hakuwa amesikia kile alichoambiwa. Alishindwa kumwelewa mwanaume huyo kabisa. Hivi kweli, bado, pamoja na mambo yote aliyokuwa amejionea, huyu mtu alikuwa anataka kuthibitisha kwamba yeye siyo mbaya? Alikuwa na lengo gani hasa? Draxton akarudi nyuma kidogo huku akimwambia Namouih aichukue bastola yake. Akakaa chini
kabisa, hivyo Namouih akajivuta mpaka upande huo wa kitanda na kuichukua bastola, kisha akamwelekezea jamaa akijipa ujasiri ndani ya hofu yake nzito. Draxton akanyanyua viganja vyake vyote kumwonyesha kwamba hana ujanja, hivyo na yeye Namouih asifyatue risasi. Bado mwanamke huyu alikuwa amechanganyikiwa sana, maswali rundo kichwani, njaa kali mwilini, na hofu kubwa moyoni. Akawa tu amemwelekezea Draxton bastola akisubiri aseme alichotaka
kusema.

"Samahani sana Namouih. Samahani sana kwa kukufanya upitie wakati mgumu," Draxton akamwambia.

Namouih akamkazia tu macho yake.

"Kile ulichokiona jana... ni kitu ambacho sikutaka mtu yeyote aje kukiona tena," Draxton akasema
kwa huzuni.

Sasa Namouih akawa ametambua kwamba ni usiku mmoja tu ndiyo ulikuwa umepita, naye akaendelea kumsikiliza.

"Ninajua una maswali mengi... na wakati huu sitakuwa na budi ila kukupa majibu yote unayohitaji.
Niulize chochote kile... nami nitakwambia ukweli," Draxton akamwambia.

Namouih hakujisi nguvu sana mikononi mwake, lakini akajitahidi kuendelea kuielekeza bastola yake kwa jamaa. Wakaendelea kutazamana kwa sekunde chache, na Namouih akameza mate kwa shida kiasi na kumwangalia tena.

"Unahisi kiu... wacha... ngoja nikufatie maji, ngoja... nikuletee maji."

Draxton aliongea kwa upole sana, na Namouih akabaki kimya akihisi kwamba bado jamaa alikuwa
anaigiza. Mwanaume akanyanyuka taratibu na kutoka ndani ya chumba hicho, huku bado Namouih akiwa ameielekeza bastola upande huo wa mlangoni, kisha Draxton akarudi akiwa ameshika chupa ndogo ya maji safi. Akamrushia kitandani hapo na kukaa tena chini sehemu ile ya mlangoni, wakati huu akiwa hajanyanyua viganja vyake. Namouih hakuyachukua maji hayo, bali akakaa akimtazama tu.

"Usijali, ni maji salama. Mapya kabisa. Kunywa," Draxton akamwambia.

Namouih akaendelea tu kumwangalia kama vile hajamsikia.

"Ninajua mwili wako ni dhaifu... utahitaji kunywa maji na...."

"Nipe sababu moja ni kwa nini sitakiwi kukipasua kichwa chako sasa hivi," Namouih akamkatisha.

Alisema maneno hayo kwa sauti kuu ingawa ni kweli alihisi udhaifu mwingi mwilini mwake.

Draxton akatulia kidogo, kisha akasema, "Ni kwa sababu sitakufa."

Kauli hiyo ikamwacha Namouih akimtazama Draxton kama vile ni mtu aliyerukwa na akili.

"Utanipiga risasi nyingi utakazo... lakini upande wangu wa pili... uliojionea jana... utazitoa zote," Draxton akamwambia.

Namouih akazidi kuchanganywa na jambo hili. "Upande wako wa pili? Wewe ni... wewe ni kama nini... Hulk?"

Draxton akainamisha uso wake.

"Jana... jana... uligeuka na kuwa.... mnyama?" Namouih akauliza.

Draxton akatikisa kichwa kukubali.

"No. Yule hakuwa mnyama. Wewe... siyo binadamu wa kawaida... inawezekanaje?" Namouih akaongea kwa hisia nzito.

"Nilizaliwa hivi, Namouih," Draxton akamwambia.

"Nini?!" Namouih akashangaa.

"Ndiyo. Baba yangu... alikuwa daktari msomi na mtaalamu wa masuala ya binadamu na wanyama, na kipindi fulani alikuwa akijaribu sana kuthibitisha kwamba kuna uwezekano wa binadamu na
mnyama... kutengeneza kiumbe hai kwa pamoja. Neno wanalotumia ni... hybrid," Draxton akaanza kueleza.

Namouih sasa alikuwa ameiegamiza mikono kwenye magoti yake aliyoyabana kwa pamoja, bastola bado akiielekeza kwa Draxton, na akimsikiliza kwa umakini.

Draxton akaendelea, "Yeye na wataalamu wengine wa masuala hayo walijitahidi kufanya majaribio
mengi bila mafanikio, kwa kuwa ni kitu ambacho hakikuwezekana. Ilikuwa imefikia hatua uchunguzi huo ukapigwa marufuku, lakini baba akawa ameipata hiyo njia na... ikapelekea mimi kuzaliwa."

Namouih akamtazama kimaswali sana, kisha akauliza, "Unataka kusema kwamba baba yako
alijamiiana na wolf ndiyo wewe ukazaliwa?"

"La. Kuna mambo mengi aliyofanya ambayo sijui kwa undani, lakini nilizaliwa naturally na mwanamke. Ilikuwa kama muujiza tu kwamba alichokifanyia utafiti na kutaka kuthibitisha kwamba kingewezekana kiliwezekana, lakini baada ya muda alitambua ingekuwa hatari sana kwangu endapo ningejulikana kwa watu wengi. Ningeonwa kama kifaa fulani kwa ajili ya majaribio, na mama yangu pia hakutaka maisha yangu yawekwe hatarini. Baba... alituficha... mimi na mama. Watu ambao tayari walijua kuhusu mimi walimkamata baba yangu wakimlazimisha aseme nilikokuwa... na inaonekana ndiyo jambo lililopelekea kifo chake kwa sababu alikataa kuwaambia," Draxton akaelezea.

Namouih akaendelea tu kusikiliza.

"Mama yangu ndiyo alikuja kuniambia hayo. Sikuelewa vitu vingi kuhusu baba mbali na kujua kwamba alijitoa badala ya uhai wangu, ili niwe salama. Lakini ilikuwa ngumu kuishi nikiwa hivi. Kuna mara ambazo nilimuumiza mama alipokuwa anajitahidi... kama kuufuga upande huu wa pili... na sikuwahi kuweza kuji-control kila mara ambapo ningegeuka kuwa... namna ambavyo uliniona. Kwa hiyo, ilikuwa lazima mimi kukaa mbali na watu, nijitahidi kwa uwezo wangu wote ili hiki kitu
kisitoke nje ingawa haikuwa rahisi. Kila mara ambapo haikuwa rahisi na kunizidi nguvu... niliumiza mtu. Na kwa miaka yote ambayo niliendelea kuishi nilielewa kwamba hali hii isingekwisha kamwe... kwa sababu hata nilijaribu kujiua... lakini ikashindikana," Draxton akaongea kwa huzuni.

Mikono ya Namouih ikalegea zaidi, akiacha kumwelekezea bastola sasa, na akiwa amevutwa sana kihisia kutokana na mambo ambayo mwanaume huyo alimwambia.

"Nimehamia sehemu nyingi kwa muda wote ambao nimeishi, lakini kwenye nchi hii ndiyo nimekaa kwa muda mrefu zaidi. Nilijitahidi kuelewa namna mwili wangu unavyofanya kazi bila kuhusisha mtu yeyote yule, na hata ningepitisha muda mrefu bila kubadilika lakini bado sijaweza kuji-control kwa asilimia zote. Ninajitahidi kukaa mbali na watu ili nisije kuwaumiza, na sikuzote ni lazima tu tatizo litatokea nikianza kumjali sana mtu..." Draxton akaongea hivyo huku akimtazama kwa hisia.

Namouih akatulia kidogo, kisha akauliza, "Ni nani unayemjali namna hiyo?"

Draxton akainamisha uso na kusema, "Blandina."

Namouih akamwangalia kwa uelewa, kisha akatazama pembeni.

"Mwanzoni... nilijaribu kumwepuka kwa sababu ni kweli nilihofia kwamba ningemuumiza. Lakini
kadiri tulivyoendelea kukutana na kukutana... nikaanza kumzoea... nikavutiwa na utu wake, lakini bado nisingeweza kujiruhusu kuwa karibu naye zaidi kwa sababu nikikosea kidogo tu.... nisingejisamehe kama angeumia. Kuna mambo mengi Namouih, mambo mengi kuhusu mimi ambayo siyo mazuri. Lakini ninasema ukweli napokwambia hivi... sikumuua Felix," Draxton akasema.

Namouih akaanza kulengwa na machozi.

"Najua ni ngumu kuamini lakini ni kweli. Sijamuua Felix, wala Agnes, wala hao wasichana wengine,"
Draxton akamwambia.

"Unajuaje? Ikiwa unapoteza control ukibadilika... unajuaje kwamba hukuwaua?" Namouih akauliza.

"Kwa sababu kusingekuwa na miili ya kuzika ikiwa mimi ndiyo ningekuwa nimewaua," Draxton akasema.

Namouih akafumba macho na kutikisa kichwa chake kwa kusikitika.

"Namouih... mimi... sitoendelea kukaa kuwa ndoto mbaya kwako. Kila mara mtu anapojua kuhusu
hili, upande wangu mwingine humwondoa, lakini nashukuru sana kwamba haikuwa hivyo kwako.
Sitaki wewe au yeyote aumie, na kwangu mimi ni ngumu sana kuishi maisha ya kawaida ijapokuwa
nimejitahidi mara nyingi mno kufanya hivyo. Najua haitakuwa rahisi kwako kusahau ulichokiona, na
mimi sitaendelea kujichanganya kwenye maisha yako tena. Nitaondoka huku. Hautaingiwa na hofu tena kwa kuwaza labda niko karibu yako... nahitaji tu ujitahidi kujifikirisha kwamba mimi... hukuwahi kunijua. Ningesema usimwambie yeyote kuhusu hili lakini hilo ni juu yako. Nataka tu kuhakikisha kwamba unarudi nyumbani salama... Efraim anawaza sana juu yako," Draxton akamwambia kwa upole.

Namouih akaendelea tu kumtazama, akijitahidi kumeza kila kitu alichosikia kwa uelewa ndani ya akili yake.

"Umepoteza fahamu kwa masaa mengi. Utahitaji kula. Ngoja nikuletee kitu ule... halafu nikupeleke nyumbani," Draxton akasema.

Mwanaume huyu aliyekuwa fumbo kubwa sana akanyanyuka kutoka chini, akamtazama Namouih kwa hisia machoni, kisha akatoka hapo tena. Namouih kiukweli alishindwa kujua hata ikiwa ingewezekana kuamini lolote kati ya mambo ambayo Draxton alisema. Njia yake ya kuzungumza, jinsi alivyomtendea kwa upole, na yeye Namouih kuwa hai mpaka sasa ni kati ya mambo yaliyoonyesha aina fulani ya ukweli ndani ya mwanaume huyo, ingawa isingekuwa jambo rahisi kumwamini kwa asilimia zote. Draxton akarejea tena, na mikononi mwake alishika boksi pana la mraba lisilo kubwa, kisha akaanza kuelekea upande wa Namouih. Mwanamke akainyanyua bastola tena polepole kama tahadhari, naye Draxton akaliweka tu boksi hilo kitandani hapo na kurudi nyuma tena. Namouih alipoliangalia akatambua kulikuwa na chakula aina ya pizza ndani yake, naye akamtazama tena machoni.

"Karibu. Niliinunua jana... bado ni nzuri," Draxton akamwambia.

Namouih akabaki kumwangalia tu, kama vile anawaza alikuwa akiambiwa hayo ili iweje sasa.
Ikabidi Draxton ampishe tu na kutoka ndani hapo, lakini akarudi tena sekunde hiyo hiyo aliyotoka.

"Aa... niko nje. Ukiwa tayari kutoka utanikuta. Unaweza kunawa tu hapo chini... nitapasafisha baadaye. Tafadhali kula Namouih," Draxton akaongea kwa upole.

Kisha akaondoka tena. Namouih akalitazama boksi lenye chakula hicho, akifikiria pia labda halikuwa wazo zuri kula chochote anachopewa na mwanaume huyo, lakini kiukweli alihisi njaa sana, tena ile njaa inayofanya mpaka unahisi kichefuchefu kwa sababu ya damu kukimbia mno. Hakungekuwa na sababu ya kudhani labda kimetiwa sumu, maana kama ni kufa basi Draxton angekuwa amemuua mapema au kumwacha afe kule kule msituni, hivyo angetakiwa kula kweli ili mwili urejeshe nguvu.

Akalivuta boksi la Pizza na kulifunua, akiona namna chakula hicho kilivyozivutia pua zake kwa harufu nzuri, naye akachukua chupa ile yenye maji na kuifungua. Akanawa mkono wake chini, maji yakimwagikia kwenye sakafu la mbao hapo, kisha akasali na kuchukua kipande kimoja na kuonja.
Koo lake lilikuwa kavu sana hata kumeza akahisi ni mateso, hivyo akayachukua yale maji na kunywa kidogo. Akaendelea kula taratibu chakula hicho, huku kichwani bado akiwa na mawazo mengi sana, hadi kuna wakati akawa anadondosha machozi kwa huzuni huku akiendelea kula, lakini akajitahidi kukaza moyo. Alijitahidi sana kula mpaka akafikisha vipande vitatu, kisha akatulia kidogo. Alihisi ni kama mwili wake umechoka zaidi, mapigo ya moyo yakikimbia kwa kasi mno, na
hiyo ni kwa sababu mwili ulikuwa ukiitikia chakula alichokula sasa hivi kwa sababu hakuwa amekula chochote siku nzima iliyopita. Hadi kichefuchefu kile kikaongezeka zaidi na hata kichwa kuanza kuuma.

Akiwa bado anajisikilizia, Draxton akagonga kidogo mlango wa hapo na kuingia, naye Namouih
akamtazama. Mwanaume akanyoosha kitunzio cha dawa aina ya Panadol, akimwonyeshea kwamba alikuwa amemletea. Namouih akiwa amebaki kumwangalia tu, jamaa akasogea mpaka karibu yake, akatoa vidonge viwili, kisha akampatia. Namouih akavipokea kiganjani taratibu, huku
macho yake yakiganda tu usoni kwa Draxton, naye Draxton akitikisa kichwa mara moja kama kusema 'kunywa,' kisha akaondoka tena. Namouih akafumba macho na kutikisa kichwa kwa kutoamini kabisa kama haya yaliyokuwa yakiendelea yalikuwa halisi. Ila msaada huo kutoka kwa mtu mwenye kuogopesha ukamfanya ajipe tu ujasiri wa kuchukua maji na kuzinywa dawa, kwa sababu muda si mrefu angeachana naye kabisa.

★★

Muda mfupi baada ya hapo, Namouih akaichukua bastola yake na kujitoa kwenye kitanda hicho kisha kuelekea mlangoni ili atoke baada ya kichwa kutulia na mwili kuwa sawa zaidi. Hakuwa na viatu miguuni, hivyo alitembea kama vile ananyata taratibu na kufikia kwenye kingo ya mlango huo, halafu akachungulia nje. Mbele yake aliweza kuona chumba kingine kipana kiasi kuzidi hiki chenye
kitanda, kikiwa ndiyo sebule bila shaka.

Kulikuwa na masofa mawili madogo ya rangi nyeusi hapo yaliyopangiliwa kuizunguka meza ndogo ya mbao, shehena ndogo ya kutunzia vyombo vichache na vyakula, jiko dogo la gesi, na vifaa vingine vichache vya matumizi ya nyumbani. Ingawa hakukuwa na mambo mengi lakini palipendeza sana kwa jinsi palivyopangiliwa, naye Namouih akatoka kabisa chumbani na kuingia hapo sebuleni. Mwangaza ulioingia chumbani kule ulitokea kwenye mlango wa kwenda mpaka nje kabisa, ambao ulikuwa wazi, na baada ya Namouih kutazama pembezoni kwenye kuta za nyumba
hiyo akaona madirisha mawili yaliyowekewa vioo vizito vyeusi, kitu kilichofanya atambue kuwa nyumba hii bila shaka ndiyo ilikuwa ile aliyoiona jana wakati amekuja huku kutafuta ukweli kuhusu mwanaume huyo.

Akiwa anaangalia sehemu hiyo bado, Draxton akaingia ndani hapo kutokea nje na kusimama ghafla baada ya kukutana na Namouih sehemu hiyo. Hakuwa ametarajia bila shaka, na Namouih akawa anamwangalia machoni kwa umakini. Mikononi, Draxton alishikilia viatu vya wazi vya
kutembelea vya masai, na Namouih akaviangalia pia.

"Namouih... unahitaji kitu fulani?" Draxton akamuuliza.

Namouih akamtazama usoni mwake tu.

"Aa... nimekuletea viatu vya..." Draxton akaishia hapo na kumnyooshea hivyo viatu.

Namouih hakutoa itikio lolote isipokuwa kuendelea kumwangalia tu, huku bastola yake ikiwa kiganjani.
Draxton akatulia kidogo, kisha akaanza kupiga hatua chache kumwelekea, taratibu, na wakati huu
Namouih akaendelea tu kusimama badala ya kukimbia au kujihami na bastola yake. Mwanaume alipofika karibu zaidi, akachuchumaa na kuviweka viatu hivyo chini mbele ya miguu yake mrembo, halafu akasimama na kumtazama usoni.

"Umekula?" Draxton akauliza kwa upole.

Namouih akaendelea tu kumtazama.

"Ikiwa unahitaji jambo fulani labda, basi...."

"Nataka kwenda nyumbani," Namouih akamkatisha.

Draxton akatazama chini na kutikisa kichwa chake kuonyesha ameelewa, kisha akasema, "Sawa. Gari lako liliharibika kwa hiyo nililitoa kule na kulivuta mpaka huku. Nitakuendesha kurudi jijini huku nalivuta pia, lakini itabidi nikuache sehemu salama ili... uchukue usafiri uende nyumbani."

"Kwa nini? Kwa nini usinipeleke nyumbani kabisa?" Namouih akauliza.

"Singekuwa na tatizo kukupeleka nyumbani Namouih. Ila sidhani kama italeta picha nzuri mbele ya mume wako ikiwa atajua ulikuwa na mimi... I mean, ulikuwa mbali na nyumbani pamoja na mtu mwingine bila yeye kujua."

"Kwa hiyo unasema kwamba natakiwa nimdanganye?"

"Utakachoamua kumwambia itakuwa ni juu yako. Ila najua itakuwa ngumu kwake kuamini ukweli hata kama ukimwambia, na mimi singependa akuchukulie vibaya..."

Namouih akaangalia chini kwa uelewa. Alichosema Draxton kilikuwa kweli kabisa.

"Vaa... tafadhali... twende," Draxton akamwambia.

Kisha akaanza kugeuka ili atoke nje, lakini Namouih akasema, "Subiri."

Draxton akamgeukia na kumtazama tena.

"Ulisema ukibadilika unapoteza control. Inakuwa siyo wewe ila ni mnyama, si ndiyo? Kwa nini basi huyo mnyama hakuniua jana?" Namouih akauliza kwa umakini.

Draxton akatikisa kichwa kuonyesha hajui na kusema, "Sijajua Namouih. Ilikuwa kama bahati tu. Siwezi kukumbuka chochote nikishabadilika kuwa hivyo. Nimejikuta tu asubuhi nimelala pembeni yako."

Namouih akakunja uso wake kimaswali.

Draxton akatikisa kichwa kidogo na kusema, "Nitakusubiri kwenye gari."

Mwanaume huyo akatoka na kumwacha Namouih amesimama tu huku akiwa na maswali mengi
kichwani. Hali hii ilishangaza na kukera sana kwa wakati mmoja kwa sababu ya yeye kutoielewa hata kidogo. Alikumbuka vyema kwamba Draxton akiwa amegeuka kama mnyama alitoka sehemu ile ya msitu
walipokuwa jana na kuwafukuza wale fisi. Sasa hayo ya kuamka pembeni yake yakitoka wapi? Ikiwa hakukumbuka chochote akiwa namna ile hiyo inamaanisha yule mnyama alirudi kwa Namouih tena na kukaa pembeni yake bila kumuumiza mpaka alipokuja kuamka akiwa kama Draxton; kitu ambacho hakingewezekana. Maswali yaliyopita kichwani kwake yalikuwa mengi sana, lakini kwa sasa alihitaji kuondoka sehemu hii haraka mno maana alikuwa ameshachoka akili.

Akavaa viatu hivyo na kuiweka bastola nyuma ya kiuno chake, naye akaelekea nje. Macho yake yaliumia kiasi kutokana na mwangaza mkali wa nje lakini kwa sekunde chache, naye akayaona magari mawili kule mbele zaidi yakiwa yamesimama kwa kupangana. Gari lake lilikuwa nyuma ya gari la Draxton, kukiwa na kamba ngumu iliyoyaunganisha kwa chini ili gari la Draxton likitembea, la
Namouih livutwe, na mwanamke huyu akaanza kuyafata. Alipofikia usawa wa gari lake, akaliangalia na kuona kweli bado sehemu ile ya mbele ilikuwa imeharibika sana, kitu kilichofanya akumbuke namna ambavyo Draxton alivyokuwa anatenda jana baada ya yeye Namouih kumpiga kwa risasi.

Hapo hapo mlango wa gari la Draxton ukafunguka, naye Namouih akamwona mwanaume huyo
akishuka na kuanza kumfata. Akamwangalia tu mpaka alipofikia karibu yake zaidi kisha akampatia
simu yake, yaani simu ya Namouih, na mwanamke huyu akaipokea na kumtazama usoni kwa umakini. Draxton akamwambia alikuwa anaitengeneza kidogo kwa sababu ilipatwa na shida baada ya kudondoka chini vibaya wakati Namouih alipoanza kukimbia bila shaka, na sasa ilikuwa vizuri.
Akamwambia akipenda angeweza tu kukaa ndani ya gari lake ili yeye Draxton ampeleke kwa kumvuta, au kama angeona hiyo inasumbua basi angeweza kuingia ndani ya gari la mwanaume.

Namouih akiwa bado ni mzito kutoa jibu, Draxton akarudi tu ndani ya gari lake na kumwacha hapo nje. Mwanamke akawasha simu yake na kukuta ni saa nane mchana tayari, na hii ikamfanya atambue kwamba ni kweli alipoteza fahamu kwa masaa mengi sana. Akashusha pumzi kujipa
utulivu, kisha akaanza kwenda mpaka kwenye gari la Draxton. Akaingia siti za nyuma na kukaa
huku akiwa ameangalia mbele tu, na macho ya Draxton yalionekana kumwangalia kupitia kioo cha juu kutokea alipoketi kwenye usukani. Namouih alipokitazama kioo, Draxton akaacha kumwangalia na kuwasha gari lake, kisha akaanza kulitia mwendoni.

Wakiwa wanaelekea nje ya msitu huo, Draxton alikuwa akimsemesha Namouih kwa kumweleza namna ambavyo alifanya ili kufika kwenye nyumba ile ya msituni. Namouih akawa anamsikiliza tu, jinsi mwanaume huyo alivyotoa maelekezo ya namna ya kufika huko bila kupotea kwa sababu alikuwa anafata viashiria fulani vilivyomsaidia, na Namouih akawa anavikariri viashiria hivyo haraka. Alikuwa anamwambia kwamba alikaa sehemu hiyo kwa muda mrefu na kuna pindi ambazo baadhi ya watu walifikia sehemu ile lakini alihakikisha hawamharibii mazingira aliyokuwa amejitengenezea hasa kwa kuwa wachache waliopaona walipaogopa, na ulikuwa umepita muda mrefu sana bila ya mtu kukanyaga pale tofauti na yeye. Namouih hakuchangia maongezi hata kidogo ingawa Draxton alijitahidi kumwonyesha urafiki, hivyo ikafikia hatua mwanaume huyo
akaona anyamaze tu.

Mwishowe wakawa wameondoka kutoka msituni hapo na kuingia barabara kuu ambayo ingewapeleka jijini hatimaye. Namouih akashusha kioo cha nyuma ili upepo uingie ndani vyema, naye akawa amefumba macho yake tu kwa kuhisi ni kama alikuwa ametoka kuamka kwenye ndoto mbaya tena, na sasa alikuwa salama zaidi. Mara kwa mara angemwangalia Draxton pale mbele ya gari na kuona namna alivyokuwa makini kuendesha gari lake huku nyuma akilivuta la Namouih, na
mwanamke huyu bado alikuwa akijiuliza vitu vingi sana kumhusu hasa kwa sababu ya akili yake ya
kisheria kuwa na udadisi mwingi.

Wakafika sehemu za ndani za jiji, naye Draxton akawapeleka eneo lililokuwa na magari mengi
yaliyohitaji kutengenezwa ili kuliacha gari la Namouih hapo lifanyiwe ukarabati. Baada ya kufanya makabidhiano na kuliacha kwa mafundi, wakaondoka na kuelekea upande wa jiji ambako Namouih
aliishi, na wakati huu simu yake ilikuwa ikiita sana kutoka kwa mume wake. Namouih hakupokea hata moja na kuendelea tu kuiangalia kila mara ilipoita, naye Draxton akawafikisha eneo lililokuwa na taxi kadhaa na kumwambia Namouih kwamba hapo ndiyo angepaswa kushuka. Akampatia na fedha, kiasi cha shilingi elfu thelathini, akisema achukue taxi ili impeleke mpaka nyumbani, na yeye angemfata kwa nyuma kuhakikisha kwamba anafika nyumbani salama.

Namouih alimwangalia sana mwanaume huyo, kisha akafungua tu mlango wa gari hilo na kuondoka. Draxton akaachia tu tabasamu hafifu na kuendelea kumwangalia mpaka alipomwona anaingia ndani ya taxi na kuanza kuondoka, naye kweli akaanza kuifatilia mpaka ilipokaribia kufika nyumbani kwake Namouih, halafu ndiyo akarudisha gari lake barabarani ili arudi pale kwenye ile
nyumba aliyopanga chumba. Muda ule Namouih alipokuwa ameingia ndani ya taxi, aliamua kupokea simu ya Efraim Donald kwa sababu mume wake huyo hakuacha kumpigia toka alipoona simu ya mke wake imerudi hewani. Alikuwa anauliza yuko wapi, alipatwa na nini, na kwa nini
hakupatikana, na ndiyo Namouih akamwambia kwamba yuko njiani kuelekea nyumbani kwa hiyo wangekutana huko ili waongee vizuri. Efraim Donald bado alikuwa nyumbani kwa kusubiri taarifa
kuhusu mke wake kwa hiyo akasema angemsubiri kwa hamu kubwa sana kwa sababu aliwaza mno juu yake.

Kwa hiyo sasa Namouih akawa amefika nyumbani, naye akamlipa dereva wa taxi na kuelekea getini. Tayari Efraim Donald alikuwa amesimama nje akisubiri, nje ya geti kabisa, na baada ya kumwona mke wake akamfata upesi na kumkumbatia kwa nguvu kiasi. Namouih alikuwa kama ameganda tu asiweze kulirudisha kumbatio la mume wake, huku Efraim akimwambia ni jinsi gani alivyotaabika sana baada ya malkia wake kupotea ghafla. Akamwachia na kumtazama hapa na pale akiuliza kama alikuwa sawa, na Namouih akamwomba waende ndani ili waongee maana hakuwa sehemu nzuri siku iliyopita. Efraim akamkubalia, naye akaelekea ndani pamoja naye.

Yule msaidizi wao wa kazi, Esma, alikuwa amesimama nje ya mlango wa kuingilia ndani ya nyumba, na baada ya kumwona Namouih akamkimbikia na kumkumbatia kwa furaha sana. Akawa anamwambia jinsi alivyowaza kuhusu hali yake pia, naye Namouih akamtuliza kwa kusema alikuwa sawa. Wote wakaelekea ndani huku wameshikana kwa ukaribu mpaka bibie alipokalishwa chini kwenye sofa, naye Esma akamletea maji ya kunywa. Namouih akanywa maji kidogo huku Efraim akimtazama kwa umakini sana, kisha mwanamke huyu akamwangalia mume wake.

"Ulikuwa wapi Namouih? Nini kilitokea?" Efraim Donald akauliza.

"Nilikwenda mbali Efraim. Mbali sana. Nilitaka tu kusafisha kichwa changu lakini... ikapita kiasi," Namouih akaongea kwa huzuni.

Kabla Efraim hajauliza swali lingine, Namouih akaitoa bastola kutoka nyuma ya kiuno chake na kumpa, naye Efraim akaipokea huku akishangaa kiasi, na Esma pia alishangaa.

"Namouih... kama kuna jambo baya limetokea naomba unieleze. Umetoweka siku nzima... unajua
nilikuwa mpaka nimeshatoa taarifa polisi ili wakutafute... niambie honey ni sehemu gani hiyo uliyokwenda? Gari liko wapi? Kwa nini ulichukua hii... nini kilitokea?" Efraim Donald akauliza kwa kujali.

Namouih akakumbuka mambo yote yaliyotokea jana kufikia siku hii kwa ufupi, kisha akasema, "Nilipatwa na ajali Efraim."

"Ajali?!" Efraim Donald akashangaa.

"Jamani... ajali dada? Haujaumia?" Esma akauliza kwa kujali pia.

"Sijaumia. Nili... nilipoteza mwelekeo nikagonga mti tu... ndiyo..."

"Namouih naomba twende hospitali... twende hospitali sasa hivi!" Efraim akasema huku akisimama.

"Niko sawa Efraim, please... sijaumia..."

"Unajuaje hujaumia?"

"Si unaniona niko sawa? Sikuligonga kwa nguvu... ni... gari tu ndiyo... liliumia kidogo..." Namouih akawa anaongea kwa kubabaika.

"Unaweza ukawa umeumia kwa ndani dada..." Esma akasema.

"Hiyo ajali imetokea saa ngapi?" Efraim akamuuliza.

"Jana usiku... nilipokuwa narudi," Namouih akadanganya.

"Kwa hiyo unataka niamini kwamba umepatwa na ajali kusikojulikana halafu umerudi nyumbani ukiwa sawa tu... tena na bastola mkononi?" Efraim Donald akauliza kwa ukali kiasi.

"Kwa hiyo unataka niseme nini ambacho utaamini? Nini... nimeua mtu, au nilikuwa nimeenda kudanga?!" Namouih akauliza kwa sauti kali pia.

Esma akarudi nyuma kwa kuingiwa na hofu.

"Siyo hivyo Namouih...."

"Unataka niseme nini sasa? Hata kama nikikwambia nini hutaki kuamini! Nimekaa kutafuta
suluhisho mwenyewe kwa matatizo mengi mpaka najikuta ndani ya hali mbaya kwa sababu tu hakuna mtu anayetaka kuniamini! Nikikwambia nimekutana na Captain America ndiyo utaamini au? Nikisema nimekutana na mwanadamu anayebadilika kuwa mnyama utaniamini Efraim?!" Namouih akaongea kwa hasira sana huku sasa akiwa amesimama.

Efraim Donald pamoja na Esma walishangazwa sana na jambo hilo, na sasa Namouih akaanza
kuonekana kulengwa na machozi.

"Hutaki kuamini hilo basi chunguza. Ukiupata ukweli utakaokuridhisha niulize zaidi," Namouih akasema.

"Namouih mbona unakuwa hivi? Shida ni mimi kukuuliza tu kwamba...."

Efraim Donald akaishia hapo na kuangalia upande wa nyuma yake Namouih; Esma akaangalia huko pia. Namouih akageuka nyuma na kumwona rafiki yake kipenzi akiwa amesimama kwenye mwingilio wa nyumba hii, Blandina mwenyewe. Alikuwa ndiyo amefika hapo tu na kukuta Namouih anaongea kwa hasira sana, naye akawa ametulia tu akimwangalia rafiki yake kwa hisia. Ni wakati ule Efraim Donald alipopata mawasiliano na mke wake kwamba anakuja nyumbani ndiyo mwanaume huyo alikuwa amempigia na Blandina pia kumjulisha kwamba rafiki yake alikuwa amepatikana, na
Blandina akawa amesema angefika hapo nyumbani upesi. Sasa ndiyo akawa amefika, na baada ya
kuangaliana na Namouih kwa sekunde chache, Blandina akaanza kuelekea hapo alipokuwa amesimama na kumfikia karibu, kisha akamkumbatia.

Namouih akaanza kulia bila kutoa sauti yoyote, machozi yakimwagika tu, naye akazungusha mikono yake mgongoni kwa Blandina kurudisha kumbatio lake. Blandina akawa anambembeleza kwa kusugua-sugua mgongo wake taratibu, halafu akamwangalia Efraim na kumtikisia kichwa mara moja; ishara ya kumwambia kwamba amwache yeye na rafiki yake ili waongee vizuri. Esma akaondoka hapo kwanza, naye Efraim Donald akazifata ngazi na kuanza kuelekea juu. Blandina
akamwachia rafiki yake na kuanza kumfuta machozi kwa vidole vyake, na Namouih akawa anajituliza kulia. Rafiki yake akamketisha tena kwenye sofa huku akiwa ameshikana naye viganja.

"Nam... yaani nakosa hata cha kusema... unaendeleaje?" Blandina akaongea kwa kujali.

"Najihisi ovyo tu Blandina... hata sielewi kwa nini maisha yangu yanakuwa hivi," Namouih
akamwambia.

"Jamani Nam... ulikuwa wapi? Tulikutafuta sana, yaani... kila mtu..."

"Yaani sijui hata nianzie wapi.... Kiufupi tu ni kwamba nimekutana na ajali ndogo jana... kuna... mtu fulani aka... akanisaidia... ndiyo nimerudi sasa," Namouih akasema.

"Ajali ya nini?" Blandina akauliza.

"Gari. Niligonga mti mdogo..."

"Ikawaje?"

"Nilipoteza fahamu ila... kuna mtu alinisaidia, akanipeleka... sehemu salama... akanipa dawa ndiyo baadaye akanisaidia kutafuta njia ya kurudi nyumbani..."

"Pole sana Nam. Sisi wote tuliwaza sana juu yako. Niliogopa sana yaani..."

"Niko sawa Blandina. Sikuumia sana."

"Lakini naona ni muhimu kwenda angalau kufanya checkup hospitali Namouih... just to be sure," Blandina akamwambia.

Namouih akatafakari kwa ufupi, kisha akatikisa kichwa kukubali.

"Huyo mtu aliyekusaidia ni nani, yuko wapi?" Blandina akauliza.

Namouih akamtazama rafiki yake usoni na kubaki amemwangalia tu baada ya kushindwa kujua jibu la kumpa. Kufikia hapo alikuwa amedanganya vya kutosha na hakuwa akifurahia kufanya hivyo
ila ni hali tu ndiyo iliyomlazimu. Alikumbuka vyema maneno ya Draxton, kwamba ikiwa angesema
ukweli basi maswali mengi zaidi yangezuka, na kwa sababu watu hawakuamini mengi kati ya madai yake ingekuwa ni kama anajiweka mtegoni ndani ya kitu ambacho ni yeye pekee na Mungu wake ndiyo walijua kuwa ukweli. Sasa akawa anajiuliza amwambie nini rafiki yake ambacho kingekuwa na faida kwao wote. Amwambie ukweli, au amdanganye?


★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumatatu, Jumanne, na Jumatano. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

TANGAZO: Nimebadili namba ya WhatsApp, sitapatikana kwenye ile ya mwanzo tena, bali sasa nitapatikana kwenye hii +255 678 017 280. Karibuni.

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★


"Nam?" Blandina akamwita baada ya kuona amezubaa kiasi.

"Bee..." Namouih akaitika kwa sauti ya chini, akionekana kuwa mbali kimawazo.

Blandina akalishika paji la uso wake kuangalia joto, na kiukweli Namouih alikuwa amechemka.

"Namouih nahisi unaweza kushikwa na homa. Itabidi twende hospitali. Hivi hata umekula?"

"Namouih akatikisa kichwa kidogo kukubali.

Blandina akafumba macho na kushusha pumzi, kisha akamwangalia na kusema, " Nam... nahitaji kuomba samahani kwa kilichotokea msibani. Nilitenda kwa hasira na kukupiga kofi rafiki yangu...
sikujisikia vizuri baada ya hapo. Kwa njia moja au nyingine ikiwa jambo hilo limechangia haya yote kutokea naomba sana unisamehe."

Blandina aliongea hayo kwa hisia sana, naye Namouih akaangalia chini kwa huzuni.

"Draxton ndiyo alinisaidia kuona mambo vizuri ingawa ni yeye ndiye aliyepigwa kofi. Ahah... huwa ana tumaneno tuzuri... na yeye mpaka sa'hivi simpati labda simu yake itakuwa imezima," Blandina akasema.

Namouih sasa alikuwa anamtazama rafiki yake usoni, akiwa anafikiria jinsi ambavyo Blandina alikuwa amewekwa gizani kuhusiana na mambo mengi sana.

"Anyway... tuyaache mengine yote. La muhimu ni kwamba uko nasi sasa. Niahidi tena kwamba hautaenda mbali namna hiyo na kusababisha uingie matatizoni. Niahidi Namouih," Blandina akamwambia.

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

Basi, baada ya hapo Blandina akampigia simu Efraim ili ashuke kutoka juu kwa kuwa angalau
Namouih alikuwa sawa kihisia wakati huu. Efraim Donald akatoka chumbani na kufika hapo walipokuwa wanawake, naye Namouih akasimama na kumwangalia mume wake kwa hisia sana. Efraim akamshika mabegani na kumuuliza ikiwa alikuwa sawa, na mke wake huyu akamwambia
alikuwa sawa na kumwomba samahani kwa sababu ya kuongea maneno makali muda mfupi nyuma. Efraim akamkumbatia tu kwa kujali, naye Blandina akamwambia mwanaume huyo kwamba Namouih angehitaji kwenda hospitalini maana alihisi angeweza kushikwa na homa.
Watatu hawa wakaondoka hapo kwa pamoja baada ya kumuaga Esma, Suleiman akiwaendesha Efraim na Namouih kuelekea hospitalini, na Blandina akiwafata kwa gari lake ambalo alikuwa ameacha nje ya nyumba hiyo. Namouih akawa amemwambia mume wake kwamba lile gari lake la Premo lilipelekwa kwa mafundi na yule mtu aliyemsaidia, akiwa hajaweka wazi kwamba mtu huyo alikuwa Draxton.

Wakafika hospitalini na kumfanyia vipimo, nao wakapata kujua kwamba kiwango cha kuchemka cha damu ya Namouih kilikuwa kimeongezeka lakini bila kuona sehemu yoyote mwilini ambayo angeweza kuwa na jeraha labda. Namouih mwenyewe alishangazwa na jambo hilo hasa kwa sababu alikumbuka namna alivyoumia usiku wa jana halafu leo akajikuta bila doa, ikimaanisha ni
Draxton ndiye aliyekuwa amefanya kitu fulani kwenye mwili wake kilichosababisha jambo hilo.
Pamoja na yote hayo, mwanamke huyu hakusema ukweli wenyewe wa kilichompata, hasa kwa kuwa daktari alisema hakuwa na shida yoyote mwilini na ambacho angehitaji ni kunywa dawa fulani na maji mengi, bila kusahau chakula kwa wingi.

Baada ya hapo wapendwa hao wakaondoka kwa pamoja, na Blandina alikuwa anamwambia rafiki
yake kipenzi kuwa kuna masuala ya kikazi alikuwa anampangia hivyo yeye angepita ofisini halafu
angekwenda nyumbani kwake Namouih baadaye kuwa pamoja naye. Namouih aliridhia hilo, nao
wakaagana na kuachana. Efraim Donald akamwambia mke wake wapite kupata chakula kizuri sana sehemu ya kipekee ili Namouih apate mlo aliofurahia zaidi kisha ndiyo wangeelekea nyumbani baada ya hapo.

★★

Blandina akiwa anaelekea upande wa kampuni yao, akaamua kujaribu kumpigia Draxton kwa mara nyingine tena bila kuwa na matumaini yoyote, na hatimaye simu ya mwanaume huyo ikaita. Akaingiwa na msisimko mzuri kwa kuhisi furaha, nayo simu ikapokelewa hatimaye. Akaanza
kumuuliza Draxton alikuwa wapi, nini kilikuwa kimetokea jana na kwa nini alizima simu wakati haikuonekana kama umeme ulikatika, naye Draxton akamwambia samahani na kusema kwamba angependa waonane ili wazungumze vizuri kama ingemfaa. Blandina akaridhia hilo na kumwambia anapita ofisini kwake mara moja kisha angemfata mwanaume huyo huko kwake, lakini Draxton akamwambia wangekutana kwake Blandina ili asisumbuke kumfata; yeye ndiyo amfate.

Blandina akajitahidi kuendesha gari upesi na kufanikiwa kufika ofisini, naye akawa amewapa watu wengi hapo taarifa kuhusu kupatikana kwa Namouih akiwa mzima kabisa, na baada ya kumaliza kufanya kazi alizohitaji kupangilia akaondoka tena na kuelekea kwake. Alifika kwa kuchelewa kiasi kutokana na msongamano wa magari barabarani lakini alikuwa anawasiliana na mpenzi wake kumjulisha kwamba anakaribia, mpaka akawa amefika sasa. Alilikuta gari la Draxton pale nje ya nyumba yake, lakini kuna jambo fulani likawa limevuta umakini wake kwa njia iliyomkasirisha kiasi.

Lilipokuwa limeegeshwa gari la Draxton, alimwona mpenzi wake huyo akiwa amesimama kwa
kueligamia, na karibu yake alisimama yule msaidizi wake wa kazi, yaani Hamida. Alikuwa ndiyo
amelifikisha gari eneo hilo na kumwona Hamida alivyokuwa anazungumza huku akijichekesha
sana na hata kumpiga-piga Draxton begani kwa kiganja chake kwa njia iliyoonekana kuwa ya utongozi kwake, na hali hiyo ilimtia hasira Blandina kwa sababu ya kuingiwa na wivu. Huyo mjinga alikuwa anafanya nini hapo nje? Blandina aliwaza. Kilichomkera hata zaidi ilikuwa ni baada ya Hamida kuona gari la Blandina, akatoka sehemu hiyo na kuharakisha kurudi ndani, naye Blandina akatikisa kichwa kwa kuudhika na kushuka.

Draxton alikuwa amesimama tu kwa utulivu, akimtazama Blandina kwa upendo mwingi sana, naye Blandina akamfata mpaka karibu akiwa ameweka uso makini. Draxton akamkumbatia kwa wororo na kumbusu shingoni mara mbili, kisha akatoa kumbatio na kuendelea kuweka mwili wake karibu naye huku akitabasamu kwa mbali.

"Nini maana yake Draxton?" Blandina akauliza.

"Kuhusu mimi kutopatikana au kuongea na Hamida?" Draxton akauliza pia.

"We' unahisi namaanisha nini?"

"We' unahisi nilikuwa namwongelesha kuhusu nini?"

"Kilichofanya akimbie ni nini?"

Draxton akatabasamu na kuangalia chini.

"Sijakuona kwa masaa mengi halafu unafika kwangu na hii crap... huyo msichana mazoea yameanza lini Draxton?"

"Kaniona hapa ndiyo akaja kunisalimu..."

"Salamu gani hiyo? Na kwa nini akimbie? Mlikuwa mnaongea nini?"

"Ahahah... unapendeza sana ukiwa na wivu..."

Blandina akamkazia macho kuonyesha hatanii.

"Kweli hakukuwa na jambo lolote baya. Hamida ni mwenye urafiki tu. Tafadhali usichukulie vibaya..." Draxton akasema kwa njia ya kumbembeleza.

Blandina akaendelea kumwangalia tu.

"Nimeku-miss Blandina," Draxton akasema kwa upendo.

"Ulikuwa wapi Draxton? Nimeku-miss sana yaani," Blandina akasema kwa hisia pia.

"Usijali, la muhimu nimerudi. Mara kwa mara naenda location ya mbali kushughulika na mambo mengi... kwa jana simu ilikata mawasiliano ila... tuko wote Blandina," Draxton akamwambia.

"Kulikuwa na kesi sehemu?"

"La... kuna mtu tu nilikuwa namsaidia na jambo fulani zito kiasi," Draxton akasema.

Blandina akakunja uso kimaswali kiasi.

"Vipi wewe, za huku?" Draxton akauliza.

"Mambo mengi. Yaani nyie sijui tu... mara Namouih apotee, mara na we' utoweke... imekuwa bonge moja la drama hii siku iliyopita, na sasa hivi tena Hamida anataka kuanzisha nyingine," Blandina akasema.

"Ahah... nimekwambia usishikilie hilo, hajafanya lolote baya. Nakujua vizuri. Usije ukamkaripia, umenielewa?"

"Utajuaje nikimkaripia? Mmeshaachiana na namba?"

"Ahahah... Blandina..."

"Hata hujaniuliza ikiwa Namouih ameshapatikana, yaani Draxton!"

"Okay, usiwe hivyo. Naelewa mambo ni mengi, na pole kwa sababu... yanakuchanganya. Namouih najua amesharudi kwa hiyo... usiwe na wazo juu ya hilo. Ninahitaji tuzungumze jambo moja muhimu Blandina," Draxton akamwambia kwa umakini.

"Mbona serious hivyo? Unanituliza halafu tena unaonyesha kama kuna jambo baya linaendelea...
unaniogopesha Draxton," Blandina akasema.

Draxton akatazama chini.

"Twende basi ndani..." Blandina akasema.

"La, nachotaka kusema haki-require kwenda ndani... ni... suala zito," Draxton akamwambia.

"Kama ni suala zito si ndiyo twende ndani tukaongee vizuri, sasa hapa nje kweli...."

"Ninaondoka Blandina," Draxton akamkatisha.

"Nini?"

"Ninaondoka."

"Unaenda wapi?"

"Itakuwa sehemu ya mbali..."

"Wapi? Draxton hebu tuache masihara basi, unaondoka unaenda wapi? Kwa nini?"

Draxton akabaki kimya.

"Hivi Draxton kwa nini lakini? Nini kinakusumbua mbona uko hivi? Kosa langu ni nini, em' niambie..."

"Haujakosea lolote..."

"Sasa nini maana yake? Mapenzi gani haya jamani? Unataka nifanye nini ili kuona... ili uone navyo... ah jamani..."

"Sijamaanisha naondoka leo, au kesho, ila... baada ya muda... Blandina...."

"Kosa langu ni kukupenda Draxton?"

"Si hivyo...."

"Kwa hiyo unaondoka tu, unaenda mbali, na mimi natakiwa nifanyeje, niseme safari njema? Sijui unaenda wapi, unatoka wapi, haunipi sababu za... niambie unataka kwenda huko mbali kufanya nini. Niambie nielewe..."

Draxton akabaki kumtazama tu.

"Kimya. Ni kimya... kimya... kimya," Blandina akasema.

"Sitaki kuendelea kuwa mwiba kwako Blandina, ninahitaji kusafisha maisha yangu kwanza ili... kama ikiwezekana... tuwe wote kwa njia ambayo...."

"Unataka tuwe wote kwa njia gani itakayokuridhisha Draxton? Ni nini unachotaka? Au... unapenda yale mambo ya kwa mpalange? Kama unataka hivyo basi nitakupa... sema tu," Blandina akamwambia huku machozi yakianza kumtoka.

Draxton akataka kumshika usoni, lakini Blandina akaitoa mikono yake kwa nguvu.

"Umekuja, unaniambia umenimiss, halafu tena unataka kuondoka? Ndiyo nini? Unatafuta tu sababu ili tuachane... yaani toka mwanzo imekuwa ni kama najipendekeza tu kwako, hunitaki kabisa Draxton. Si ungeniambia? Nikajipa matumaini kwamba labda muda ukipita mambo yatakaa sawa kwa sababu nilikuwa nimejipa uhakika wa asilimia zote kwamba nataka kutulia na wewe... lakini umeuchezea tu moyo wangu namna hii na sasa unautupa kweli? Nimekukosea nini?" Blandina akasema kwa huzuni.

"Blandina... najua ni ngumu kuelewa, ila naomba tu utambue kwamba nafanya hivi kwa ajili yako... una... unastahili...."

"Acha kuniambia kile nachostahili na nisichostahili. Hakuna cha maana ambacho mimi na wewe tumefanya zaidi ya kuambiana maneno yasiyokuwa na faida yoyote kama vumbi chafu tu... kama... kama ilikufanya ufurahie... kunitendea namna hiyo basi haina shida. Si unataka kuondoka? Ondoka. Tena ondoka sasa hivi! Nenda... kaendelee na maisha yako na mimi uniache niendelee kuteseka na moyo wangu!"

Blandina aliongea hayo huku akilia kwa hisia sana, naye Draxton akalengwa na machozi kwa
kuingiwa na simanzi sana.

Draxton akajaribu kumshika na kusema, "Blandina..."

"Usinishike! Ondoka... ondoka nimesema!" Blandina akaongea kwa hasira huku akimponda kwa pochi yake.

Draxton aliumia sana moyoni, ingawa tayari alikuwa ametegemea itikio la namna hiyo kutoka kwa
mwanamke huyu. Hakuwa na namna ya kumweleza sababu iliyofanya afikie uamuzi huu lakini alijua ilikuwa kwa faida ya mpenzi wake huyo ingawa Blandina asingeweza kujua jinsi gani. Mwanamke huyu alikuwa ameumizwa sana, kwa sababu alikuwa anampenda mno Draxton ila
akahisi labda kiwango chake cha upendo kumwelekea mwanaume huyo hakikumtosha Ijapokuwa
alitaka sana kutulia naye. Hivi siyo alivyotazamia mambo yaende leo baada ya mpenzi wake kurudi, kwa hiyo aliingiwa na mkazo mkali sana moyoni.

Draxton akainamisha uso wake kwa sekunde chache, kisha akafungua mlango wa gari lake na kuingia ndani huku Blandina akibaki kumtazama pale nje. Mwanamke huyo akaanza kulia zaidi na kuchuchumaa chini kabisa, na jambo hilo likamfanya Draxton adondoshe machozi huku
anamwangalia kwa huruma. Lakini alijua kurudi hapo kungemaanisha kuendelea kumpa matumaini bandia mwanamke huyo kwa sababu asingeweza kumpa mapenzi ambayo aliyastahili, hasa kutokana na kuishi maisha ya aina mbili ambayo yangemweka Blandina hatarini kama yeye Draxton angepoteza mwelekeo na kusababisha mnyama wake wa ndani atoke.

Kwa hiyo mwanaume akaliondoa tu gari hapo na kuondoka kabisa, akimwacha Blandina analia kwa uchungu wa kupoteza penzi lake alilotia imani kwamba lingefika mbali. Alilia sana. Yeye aliona kwamba Draxton alitafuta tu kisingizio ili amwache bila shaka, mawazo ya haraka kuwa labda
alipata mwanamke mwingine, na hivyo akawa anahisi hasira nyingi kwa kujiona mjinga sana kuendelea kuchezewa kihisia namna hiyo. Ingawa ni kwa muda mfupi tu toka alipoanza uhusiano na mwanaume yule, alikuwa amempenda sana, na ndiyo maana alivumilia mengi ambayo yangechosha mwanamke yeyote ndani ya uhusiano lakini alikomaa naye kwa kuwa alionyesha utu mzuri.

Ila sasa mwanamke huyu akawa amenyoosha mikono yake kabisa, mwanaume huyo aende anakotaka kwenda, na yeye Blandina angejitahidi kusonga mbele na mambo yake ingawa roho ilimuuma sana. Akajifuta machozi baada ya kuona watu kadhaa waliopita barabarani wakimwangalia sana, naye akajikaza na kuiokota pochi yake, halafu akaelekea ndani mpaka
chumbani na kujifungia kabisa; akijitupia kitandani na kuendelea kulia kwa huzuni sana.

★★

Baada ya wanandoa Efraim Donald na Namouih kumaliza kupata mlo wa wapendanao nje, walikuwa wamerejea nyumbani masaa kadhaa nyuma ili Namouih aliyehitaji zaidi kupumzika atulie. Mwanamke huyu alilala na kusinzia kabisa jioni hiyo mpaka alipokuja kuamka saa mbili
usiku, naye alikuta mume wake akiwa ameondoka, na alikuwa amemwachia ujumbe kwa kusema
amekwenda kuangalia mambo fulani kwenye kampuni yake hivyo angerudi baadaye kidogo.

Namouih alikuwa amepigiwa simu na baadhi ya watu aliofahamiana nao waliomjulia hali baada ya kusikia kuhusu "ajali" iliyompata, naye akawashukuru wengi kwa kuonyesha kwamba walimjali. Yule boss wake, Mr. Edward Thomas, alikuwa ameongea naye pia na kumpa pole, akisema kwamba mwanamke huyu akitaka kupumzika nyumbani kwa wiki nzima basi afanye hivyo ili awe sawa zaidi kimwili. Namouih alishukuru kwa hilo, lakini akamwambia asingekawia kurudi kazini kwa hiyo ndani ya hizi siku chache za mbele angeanza kwenda tena. Baada ya hapo akawasiliana na watu wa familia yake kuwasalimu, yaani mama yake na wadogo zake. Zakia alimwambia
kwamba wakati huu waliishi na binti ya mjomba wake pale nyumbani, aliyeitwa Manka, ambaye alikuwa huko kimasomo, naye Namouih akamwambia amsalimu pia.

Imefika mida ya saa tatu usiku Namouih akiwa ameendelea kutulia, Esma akamwambia kwamba chakula kilikuwa tayari, lakini Namouih akasema yeye angemsubiri mume wake ili waje kula pamoja kwa hiyo Esma aende tu kula na kumpelekea mlinzi. Akabaki akitafakari kuhusu mambo
yaliyompata kabla ya kurudi kwake nyumbani, na kiukweli ilikuwa ni kama usiku wa kuamkia siku hii ulikuwa ni ndoto ndefu na mbaya sana ambayo hakuwahi kuiota kabla. Akawa hata anajiuliza ikiwa Draxton alihusiana na zile ndoto mbaya zilizokuwa zinampata mara kwa mara, na ili kupata uthibitisho wa baadhi ya mambo mengi yaliyokuwa na utata, akaamua afanye utafiti.

Akachukua laptop yake na kuingia "Google" akitafuta habari au taarifa zilizohusiana na masuala ya
uzalishaji wa viumbe hai baina ya wanyama wa aina mbili tofauti. Mwanadamu ni mnyama pia, na
katika kundi la wanyama ni jamii za nyani ndiyo hukaribiana kidogo sana na chembe za urithi za mwanadamu, au chromosome, lakini hata kama wangekutanishwa, uwezekano wa kiumbe hai kutengenezwa ulikuwa finyu. Aliona kwamba kuna baadhi ya watafiti na wataalamu zamani
waliojaribu kuthibitisha mambo kama hayo lakini wakashindwa, hivyo akawa anajiuliza ingewezekana vipi mwanadamu na mbwa-mwitu kutokeza kiumbe kama Draxton wakati aina za wanyama hawa zilitofautiana sana, sembuse chromosome!

Akasoma na kusoma habari nyingi akijaribu kupata kitu ambacho kingehusiana na Draxton, naye
akapata jambo fulani lililoshangaza. Kuna daktari aliyefahamika kwa jina la Obadiah Pugsley Draxton, mtaalamu wa masuala hayo hayo ya wanyama, ambaye alitaka kuthibitisha kwamba jambo lile lingewezekana lakini utafiti wake ukawa bila mafanikio. Iliandikwa kwamba alikufa kwa kujiua kwa sababu alipoteza familia yake kusikojulikana, na utafiti wake na wa timu yake haukupata matokeo chanya kama tu wengine waliomtangulia na kufata. Kilichomvuta Namouih kukazia fikira kuhusu mwanaume huyo ni kwamba alikuwa na jina kama la Draxton huyu, lakini kilichomshangaza ni kipindi alichoishi. Daktari huyo aliishi enzi za vita vya kwanza vya dunia mpaka alipokufa mwaka 1928. Ikiwa huyu kimahusino labda ndiyo alikuwa baba wa Draxton, mwanaume huyu angekuwa na miaka mingapi?

Haikuonekana kwamba inawezekana hata kidogo, na huenda Namouih aliunganisha mambo vibaya; huenda majina yao yalifanana tu lakini haimaanishi kwamba walikuwa na uhusiano wowote. Ingawa hivyo, sasa akawa anataka kujua mambo mengi kumhusu mwanaume yule, kwa hiyo ingebidi atafute njia ya kupata ukweli zaidi wa maisha yake ili kuondoa utata mwingi
uliomzunguka.


★★★


Asubuhi ya siku iliyofuata, Efraim Donald aliondoka nyumbani kuelekea kazini akiwa amemwacha mke wake amepumzika. Hakukuwa na mpango wowote kwa Namouih kutoka leo hasa kwa sababu alionwa kama "mgonjwa" baada ya kilichompata, kwa hiyo akatulia tu nyumbani na paka wake pamoja na Esma, ambaye alimpa ushirika mzuri kwa maongezi yenye kufurahisha sana.

Mwanadada huyo alikuwa anamwambia Namouih kuhusu mambo mengi ya maisha yake, akisema pia kwamba alikuwa na mpenzi lakini ni muda mrefu ulikuwa umepita bila ya wao kuonana wala
kuwasiliana. Namouih akamuuliza ikiwa alijihisi vibaya kuwa mbali na mpenzi wake na ikiwa angehitaji kuwa anaonana na mwanaume ili mahitahi yake ya kimahaba yatimizwe, na jambo hilo likamfanya Esma acheke sana. Lakini akasema tu kwamba vitu kama hivyo vipo na siyo rahisi kukaa muda mrefu hivyo kwa njia fulani ya upweke, ila kwa kuwa wakati huu alikuwa anajitahidi
kufanya kazi kwa bidii ili aje kujenga maisha anayotaka, vitu hivyo aliviweka pembeni kwanza ili
visisababishe akakengeuka kutoka kazini na kuanza kufanya vitu vya kipuuzi. Namouih alipendezwa sana na unyoofu wa Esma, naye akamwambia kwamba angekuja kufanikiwa sana maishani kwa sababu ya jicho lake pevu.

Basi, imefika mida ya saa tano hivi asubuhi, Namouih akapigiwa simu na mmoja kati ya washiriki wa kampuni yao aliyetaka kuzungumza naye kuhusiana na jambo fulani la kisheria; kama kuomba msaada wa ushauri. Namouih akamwambia kwamba angetakiwa kuongea na mwanasheria wake msaidizi, yaani Blandina, kwa sababu yeye Namouih hakuwepo ofisini na jambo hilo
halingetatuliwa kwa simu. Lakini ndiyo mshiriki huyo akamwambia kwamba Blandina hakuwepo ofisini siku hii, na alikuwa ametafutwa sana bila kupatikana ndiyo maana wakaona wamsumbue tu Namouih. Mwanamke huyu akaona isiwe na shida; akaandaa laptop yake kwa kuweka programu ya mawasiliano kwa njia mubashara, kama mkutano, kisha akafikisha ujumbe huko kwa njia iliyoeleweka vizuri sana, na waliohusika wakampongeza na kumshukuru kwa hilo, halafu mkutano huo ukakatwa.

Sasa Namouih akawa anajiuliza ni wapi Blandina angekuwa bila kutoa taarifa kazini ya sababu iliyofanya asiende; haikuwa kawaida yake. Ikaingia akilini mwake kuwa hata jana rafiki yake huyo alisema angekuja hapo nyumbani jioni lakini hakufika kabisa. Akawaza sijui labda alikuwa na Draxton ndiyo maana, au alikuwa amepatwa na tatizo? Akaamua kumpigia, lakini simu ya Blandina iliita mara kadhaa bila kupokelewa mpaka mara ya tisa, ndiyo hatimaye akapokea. Namouih
akamuuliza rafiki yake alikuwa amepatwa na nini, mbona anatafutwa hajibu, na kwa nini hakuja hapa nyumbani jana, lakini Blandina akasema tu kwamba hakuwa akijihisi vizuri kwa hiyo
alipumzika kwake. Namouih aliweza kutambua kwamba njia ya Blandina ya kuongea ilikuwa ya uchovu kama siyo huzuni, naye akaelewa kulikuwa na tatizo. Blandina hakusema lolote lile zaidi ya kwamba alihitaji kupumzika, kisha akakata simu kabla hata Namouih hajaendelea kuzungumza naye kwa kina.

Namouih aliwaza sana kuhusu hali ya rafiki yake, na kwa kutambua kuwa bila shaka tatizo lililomsumbua lingekuwa la kihisia, akaamua
kwamba angekwenda kuonana naye huko huko kwake. Akapanda kwenda chumbani na kuanza kujiandaa, naye akavaa nguo rangi ya njano yenye blauzi na suruali pana iliyompendezea sana, akizibana nywele zake kwa nyuma kama mkia, na viatu virefu kwa chini. Akatoka na kumuaga Esma akisema anakwenda kwa rafiki yake, naye akaenda kuchukua gari lingine ili aondoke.

Wanandoa hawa walikuwa na magari matano; ile Range Rover Vogue nyeusi aliyotumia zaidi Efraim Donald, V8 VX nyeusi ambayo Efraim aliitumia pia mara kwa mara, Premo ile ya silver ya Namouih ambayo ndiyo iliharibika na kuachwa kwa mafundi, Toyota Fortuner nyeusi na Toyota Vanguard lenye rangi ya maroon-nyeusi. Magari hayo mengine mawili yalitumiwa mara moja moja sana au kukaa tu hapo kwa muda mrefu bila kutumiwa, kwa hiyo Namouih akaichukua Toyota
Vanguard na kuingia mwendoni.

★★

Alifika kwa Blandina mida ya saa sita mchana, jua likiwa kali hatari, naye akaegesha gari lake nje ya
nyumba aliyoishi rafiki yake huyo. Akaelekea getini na kugonga mara chache, na baada dakika mbili hivi mlango mdogo wa geti hilo ukafunguliwa, ikiwa ni Blandina mwenyewe ndiye aliyefungua.
Namouih alitulia na kumwangalia kwa umakini. Blandina alikuwa amejifunga khanga moja kutokea
kifuani, mwili wake mnono ukionekana vyema, na usoni alionekana kuwa kama mtu aliyetoka
kulala kwa jinsi macho yake yalivyoonyesha kuchoka. Alikuwa anamwangalia Namouih kama vile
hajafurahi kumwona, kisha akasema tu "karibu" kwa sauti ya chini na kuuachia mlango wa geti, naye akaelekea ndani ya nyumba hiyo.

Namouih akajua kwamba leo ilikuwa ni zamu yake kwenda kutoa kitia moyo huko ndani maana kumwona tu Blandina hivyo kulimaanisha ishu iliyomsumbua ilikuwa nzito. Akaingia na kurudishia mlango wa geti vizuri, kisha akaelekea ndani kule mpaka sehemu ya sebule na kusimama kwanza. Vitu hapo vilikuwa vimekaa shaghalabaaghala tu na chupa za wine na pombe zikiwa zimezagaa
chini pamoja na glasi, kuonyesha kwamba rafiki yake alikuwa amekunywa sana. Blandina alikuwa
ameelekea jikoni, na sasa akarudi kwa Namouih na kumpa tabasamu la kivivu tu, kisha akamwambia asikazie fikira namna ambavyo sehemu hiyo ilikuwa imeharibika mpangilio na aingie kuketi kwenye sofa.

"Blandina nini kinaendelea?" Namouih akauliza.

"Sijaamka vizuri tu leo... nahisi kuchoka that's all," Blandina akasema huku akikaa chini kabisa.

Alionekana kuyumba kwa mbali na kama mtu mwenye usingizi sana.

Namouih akasogea karibu yake kidogo na kuuliza, "Haya yote maana yake nini? Umekuwaje? Niambie tatizo nini tusaidiane rafiki yangu... please..."

"Hamna tatizo Nam. Nimerudi tu jana na kuchukua hivi vinywaji nikapiga wee ahahahah... mpaka usingizi ukanipitia yaani... halafu nimeamkia kutapika... wa supu naye kazunguusha agh... ila sa'hivi angalau..." Blandina akaongea kizembe.

"Hamida yuko wapi?" Namouih akauliza.

"Ameenda kwao," Blandina akasema na kunyanyua mabega yake.

Namouih akauliza, "Unamaanisha nini?"

"Mpumbavu yule... malaya tu. Oh, I mean sisi wote ni malaya, lakini me haki ya Mungu naweza ua malaya anayecheza na mwanaume wangu. Kanajichekesha-chekesha kwake, kanajiona kamefikaaa... ukikauliza kanaleta nyodo za ki(.....)... nikakatimua!" Blandina akasema hivyo na kusonya.

Namouih akatikisa kichwa chake taratibu kwa kusikitika, asielewe hayo yote yalitokea wapi.

Blandina akavuta chupa yenye pombe ndogo na kunywa, kisha akasema, "Nitatafuta mwingine,
wako kibunda. Au unisaidie kutafuta... kama Esma tu, sijui hata ulimtolea wapi, yuko vizuri sana. Afu'... Edward haja-mind lakini kwamba sijatoa taarifa? Ahahahah... isije ikawa na mimi wameniandalia timu ya kunitafuta kama wewe ulipopotea maana duh... Ilikuwa bonge moja la drama. Halafu unajua nini... Samira anasema ile kesi ya upunjaji ameshindwa kuchukua eti alikuwa anataka anipe mimi... nikamwambia hivi we' haujasoma au? Mimi siwezi nikaichukua ghafla tu like I don't got enough shit to worry about ili yeye aende na buzi lake tu kuangalia mechi ya Yanga huko
wakishinda waanze kuvua manguo wafanye ufedhuli hadharani hahahah.... Hivi uliiona hiyo video
Nam? Haki ya Mungu hahah... haki ya Mungu yaani watu wanapenda sifa sana ungeiona... lile likaka limekaliwa na matako machafuuu lakini bado ukiiangalia limeweka tu ulimi mpaka...."

Namouih akaendelea kumwangalia tu kwa huzuni sana, akielewa kuwa kiukweli Blandina alikuwa anaumia sana moyoni mwake mpaka kuanza kuongea na kutenda kwa njia isiyofaa kabisa. Akachuchumaa karibu yake na kumshika usoni taratibu, naye Blandina akaacha kuongea na kubaki amemwangalia rafiki yake huku macho yake yakiwa yamelegea.

"Tatizo ni nini Blandina?" Namouih akauliza kwa upole.

Blandina akaangalia chini na kuanza kulia kwa uchungu sana, jambo lililofanya Namouih ajisikie vibaya mno.

"Niambie rafiki yangu.... niambie..." Namouih akawa anasema huku akimfuta machozi.

"Sijui tu... Namouih... unampenda mtu hata hapendeki... ni maumivu tu... hhh... me ni mpumbavu sana!" Blandina akaongea kwa kwikwi za kilio.

"Ni Draxton? Draxton amekufanyaje Blandina? Niambie..."

"Anaondoka Namouih. Anaondoka sijui kwenda kwa hawala zake wengine.... yaani hata sielewi kwa nini naumia hivi wakati hajawahi hata kunipa lolote kabisa... mimi ni mpumbavu sana..."

"Hapana Blandina usiseme hivyo. Wewe siyo mpumbavu. Amekwambia anaondoka? Amekwambia lini?"

"Alikuja jana... nilikuwa nimefurahi sana lakini akaja na kunivunja moyo Nam.... anasema ananiacha eti... eti anaenda mbali kwa... sababu ambayo sitaelewa... ila ni kwa ajili yangu. Hivi ana akili kweli?
Nimefanya nini kustahili hili? Kumpenda ndiyo ilikuwa kosa langu mimi si ndiyo? Nimempenda bila
kutarajia mengi lakini ananilipa ubaya kwa nini? Kwa nini aniache Namouih? Aaahh..."

Blandina alisema hayo huku akilia sana, na Namouih akaingiwa na simanzi na kudondosha machozi pia. Akamkumbatia kichwani na kuanza kumbembeleza, na alikuwa ameshatambua kwamba rafiki yake hakulala vizuri usiku; au labda hata hakulala kabisa. Akamsaidia kunyanyuka baada ya dakika kadhaa na kumsisitizia waende chumbani, kisha wakaenda pamoja chumbani
kwake Blandina, halafu Namouih akalala pamoja naye kitandani huku akichezea nywele za rafiki yake taratibu ili kumfanya asinzie. Hakuwa hata amemwambia neno lolote la kumfariji, kwa sababu
alielewa chanzo cha hayo yote na alikuwa amepanga kumsaidia kwa njia ya vitendo zaidi kwa maana alielewa sababu iliyofanya Blandina apitie jambo hilo.

Draxton alikuwa amefanya kama alivyosema, kwamba angeondoka huku ili asije kusababisha matatizo, ila sasa Namouih akawa ametambua kwamba mwanaume yule alihitajika zaidi ya alivyodhani. Alihitaji kupata majibu ya maswali yake mengi, na pia kuhakikisha Blandina anakuwa
sehemu nzuri kihisia kutokana na haya yote, na ni Draxton pekee ndiye angeweza kuleta suluhisho la mambo hayo. Alikuwa ameshaanza kuona unyoofu mkuu ndani ya utu wa yule mwanaume, hivyo akawa ameazimia kufanya jambo fulani kurekebisha haya yote.

Hazikupita dakika nyingi sana na Blandina akawa amesinzia, huku bado pumzi zake zikitetema kwa kwikwi ya kilio. Namouih alimwangalia kwa huruma sana, kisha akanyanyuka kutoka kwenye kitanda na kutafuta peni na karatasi, halafu akaandika ujumbe mfupi akimtaka Blandina ajue kwamba yuko pamoja naye hivyo asivunjike sana moyo, kwa sababu mambo yote yangekuwa sawa tu. Akaandika kwamba wangeonana baadaye na yeye Blandina ajitahidi kula akiamka, kisha akaiweka karatasi kitandani hapo na kumwacha hatimaye. Akaenda mpaka kwenye gari lake baada ya kuhakikisha amefunga nyumba hiyo vyema, kisha akaamua kwenda kule ambako Draxton
alikuwa amepanga.

Alikuwa anawaza vitu vingi mno hadi kuna wakati akaanza kupoteza umakini mzuri wa kuendesha gari. Ni wakati yuko mwendoni bado ndiyo Efraim Donald akampigia na kuuliza kama alikuwa sawa, naye Namouih akamjulisha kwamba alikuwa ametoka kuja kumwona Blandina kwa sababu hakuwa na hali nzuri. Kwa kuhofia labda Namouih angeweza kujiumiza tena Efraim alimwambia hakupaswa kuondoka bila kumwambia, na labda hata angemtuma Suleiman ili amwendeshe, lakini Namouih akasema alikuwa sawa kuendesha na angerudi nyumbani salama, hivyo Efraim asimuwaze sana.

Mwanamke akawa amefika pale ambapo Draxton aliishi na kwenda ndani kule, naye akawa amepokelewa vyema na yule dada aliyeitwa Rehema. Baada ya salamu na kujuliana hali, Namouih
akamwambia kwamba alifika hapo ili kuonana na Draxton, lakini Rehema akamwambia kwamba huyo kaka hakuwepo. Ni kweli hata gari la Draxton halikuwepo hapo lakini Rehema akamwambia kwamba alimwona mwanaume huyo asubuhi ya leo akiondoka na begi lisilo kubwa sana la kubebea begani kama mchezaji wa tenisi, ikionekana kama lilikuwa na nguo au vitu vyake tu na
alikuwa ameenda safarini labda.

Moja kwa moja Namouih akawa ameelewa jambo hilo lilimaanisha nini, na kwa sababu alitaka
kuhakikisha lengo lake linafanikiwa, akamshukuru tu Rehema na kutoka hapo upesi mpaka akaingia ndani ya gari, na sasa angeelekea sehemu nyingine tena; kule msituni ambapo
mwanaume huyo alikuwa na nyumba ya kujifichia. Namouih alionekana kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwa sababu ya kuchukua hatua za haraka na zenye uhatari ili kupata tu
suluhisho kwa kuwa hakutaka kukata tamaa ili kuhakikisha anafanikisha lengo lake. Alikuwa
ameamua kufanya haya yote kwa ajili ya rafiki yake, lakini pia ili yeye mwenyewe apate ridhiko ndani ya moyo wake kutokana na yote yaliyokuwa yametokea. Ikiwa angekwenda kule msituni na kumkosa Draxton, basi ndiyo angekuwa amepoteza mchezo, lakini hakutaka kujikatisha tamaa kwa
kuwaza hivyo.

Namouih akaendelea kuendesha kuelekea huko mpaka alipofanikiwa kuufikia msitu ule na kuingia ndani zaidi. Zamu hii alikuwa makini sana kukumbuka njia vizuri kama tu ambavyo Draxton alikuwa
amemwelekeza, na kweli wakati huu alikwenda vizuri hadi akafanikiwa kuifikia nyumba ile ya maficho ya mwanaume huyo. Akalisimamisha gari lake umbali mfupi kutokea huko, naye akashusha pumzi ya kuridhika baada ya kuliona gari la Draxton sehemu hiyo. Alipotazama mbele
kule zaidi, aliweza kumwona Draxton kwa mbali, akiwa kifua wazi, na akitazama upande wake pia.
Akashuka kutoka ndani ya gari taratibu na kuanza kuelekea huko.

Kulikuwa na upepo mkali kiasi
uliopeperusha nywele zake zilizobanwa kwa nyuma, na alipozidi kumkaribia pale akatambua kwamba Draxton alimtazama bila kukwepesha macho yake hata kidogo. Ni kwamba bila shaka
mwanaume huyo hakutegemea kumwona hapo, hilo Namouih alilielewa. Akakaribia zaidi upande
wake na kuweza kumwona kwa usahihi sasa. Mwanaume alikuwa ameshika panga mkononi, mwili wake uliojengeka kiume sana uking'aa jasho, na chini kukiwa na magogo mawili yenye matawi-matawi ambayo bila shaka alikuwa anaparua.

Namouih akasimama tu umbali mfupi na kumwangalia machoni kwa umakini. Draxton akaliweka panga chini na kuanza kumfata pia, kisha akasimama mbele yake. Alikuwa amevalia kaptura ile ile ya kijani-cheusi na viatu vyeupe vya mazoezi, na Namouih akamtazama kifuani kwa ufupi na kisha
kumwangalia tena machoni.

"Namouih..." Draxton akaita kwa sauti tulivu.

"Draxton..." Namouih akasema jina lake pia.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumatatu, Jumanne, na Jumatano. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

TANGAZO: Nimebadili namba ya WhatsApp, sitapatikana kwenye ile ya mwanzo tena, bali sasa nitapatikana kwenye hii +255 678 017 280. Karibuni.

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Wawili hawa wakaendelea kutazamana kwa sekunde chache, kisha Draxton akasema, "Karibu."

"Asante," Namouih akajibu.

"Samahani kwa kunikuta hivi, ningejua unakuja...."

"Hapana usijali. Mimi ndiyo niseme samahani kwa kuja bila taarifa. Sina hata namba yako pia," Namouih akasema.

"Yeah, pole kwa hilo. Huku penyewe mtandao ni dim," Draxton akamwambia.

Ukimya ukafata tena, kisha...

"Twende ndani, nitakwambia unachotaka kujua," Draxton akamwambia Namouih.

Tayari mwanaume huyu alikuwa amekisia kwamba mwanamke huyo alikuwa na maswali, hivyo akaelekea mpaka ndani ya nyumba yake ndogo, naye Draxton akamkaribisha aketi kwenye sofa moja. Yeye akaelekea chumbani na kuvaa T-shirt tu, kisha akarudi kwa Namouih na kusimama
usawa wa dirisha moja la kioo; kama kaliegamia. Harufu nzuri sana ya Namouih ilikijaza chumba hicho, naye akawa anamwangalia Draxton kwa njia ya subira.

"Unaendeleaje?" Draxton akaanzisha mazungumzo kwa kuuliza hivyo.

"Niko vizuri tu," Namouih akajibu.

"Habari ya nyumbani?" Draxton akauliza.

"Safi tu. Wewe?" Namouih akasema.

"Niko poa. Sorry kwa sababu sijaoga hata, inawezekana harufu yangu inaku...."

"Hapana, usiwaze. Niko sawa," Namouih akamkatisha.

"I suppose umekuja ili tuongee... au ilikuwa ni ili uone kama nimeshaondoka?"

"Aa... cha kwanza. Sikuwa na matarajio ya kukuta umeondoka."

Draxton akitikisa kichwa kama kusema sawa.

"Nimepita unapokaa sikukukuta, ndiyo nikaona nije huku kukuangalia. Ukiondoka utaenda wapi?" Namouih akauliza.

"Bado sijaamua. Na nikiamua hakuna mtu yeyote anayetakiwa kujua," Draxton akajibu.

Namouih akatulia kidogo, kisha akauliza, "Nani alikujengea hii nyumba?"

"Mimi mwenyewe," Draxton akajibu.

"Kumbe?"

"Yeah. Miti mingi huku. Kidogo kidogo mpaka ikakamilika."

"Na hivi vitu ulitengeneza wewe mwenyewe?"

"Nilinunua. Ningevileta hapa kila mara nilipopata nafasi... na... ahah... inaonekana ni kama jana tu lakini ni muda umepita."

"Kwa hiyo huwa una kawaida ya kuja huku... kila siku?"

"Mara moja moja. Sina ratiba hususa. Lakini hata nikiamua kuja huku kukaa mwezi mzima, naweza."

"Vipi kuhusu wale fisi? Huku kuna fisi wengi?"

"La, siyo wengi. Hakuna anayesogea eneo la huku kwa sababu wananiogopa, ila usiku ule inaonekana walichanganywa na mlio wa risasi ndiyo maana ukakutana nao."

"Aaaa... sikuwahi kufikiria hili jiji lina wanyama pori."

"Wapo. Si lazima mpaka kwenye hifadhi, wapo kila sehemu. Ila ni mmoja mmoja."

Namouih akatikisa kichwa kukubali.

"Haupendi wanyama?" Draxton akauliza.

"Hapana, napenda. Namaanisha... siyo wote yaani, siwezi kupenda fisi, au simba, au nyoka, ila wapo naowapenda. Mimi ninafuga paka. Anaitwa Angelo," Namouih akasema.

Draxton akatabasamu kidogo na kusema, "Interesting choice of a name."

Namouih akatabasamu na kutikisa kichwa kuonyesha ameelewa, kisha akamwangalia kwa umakini. Mwanaume huyo kijana alikuwa anamwangalia pia kwa kusubiri swali lingine.

"Nili... nilifanya research kidogo jana na... kuna huyu daktari alikuwa mtaalamu wa masuala ya wanyama na ana jina kama lako, sijui ikiwa mna uhusiano ila... Draxton nahitaji kukuuliza.... una miaka mingapi?" Namouih akauliza.

"Ishirini na tano," Draxton akajibu.

"Umekuwa na miaka ishirini na tano kwa muda gani?" Namouih akauliza tena.

Draxton akatazama chini, kisha akasema, "Miaka 70."

Namouih akabana midomo yake na kuangalia pembeni, kisha akashusha pumzi ndefu kama kusema 'kazi ipo.'

"Okay, this is... this is just crazy. Kwa hiyo... una miaka 95... lakini mwonekano wako ni wa mtoto wa miaka 20. Hauzeeki. Hauwezi kufa. Utaishi milele kabisa, si ndiyo?" Namouih akauliza.

"Hakuna kitu kisichoweza kufa, Namouih. Sema... kwangu mimi labda hakuna kitu kwenye hii dunia
kinachoweza kuniua, lakini kuna sehemu kipo. Natumaini ifike siku ambayo nitakipata," Draxton
akamwambia kwa uzito.

Namouih akamwangalia kama vile amechanganywa sana na jambo hilo, naye akauliza, "Unataka kusema kwamba... hata nikikukata kichwa, nikakitupa mbali huko... bado utaendelea kuishi?"

"Niliwahi kujichoma anesthesia mwili mzima kisha nikajitupa ndani ya mtungi wa tindikali. Sikuweza hata kuhisi maumivu na inawezekana kwa neno fulani labda nilikufa, lakini nilikuja kujikuta juu ya dari la nyumba ya mtu... mwili ukiwa bila alama yoyote. Sielewi baba yangu alifanya nini kunitengeneza niwe namna hii Namouih, lakini nimeshajaribu kutumia njia nyingi sana ili nijiondoe kwenye huu ulimwengu... sijui tu inakuwaje kwamba...." Draxton akaishia tu hapo na kuangalia pembeni.

"Kwa nini umejaribu sana kujiua?" Namouih akauliza.

Draxton akabaki kimya.

"Kwa nini uchukue hatua za namna hiyo mara nyingi sana? Niambie ukweli tafadhali. Kwa nini unajichukia hivyo? Ni kwa sababu ya watu ambao umewaumiza?"

"Ndiyo."

"Unajua Draxton... haya yote yananishangaza. Huyo mnyama sijui nini, ni mkubwa sana. Ulikuwa wapi ulipowaumiza watu? Mbona... haijawahi kusikiwa kokote kuhusu kitu kama hiki? Ungewezaje kujificha kwa muda mrefu hivyo wakati unasema ukibadilika unapoteza control? Na kwa nini ulikuja Tanzania? Kwa nini siyo Atlanta, Misri, au nchi za mbali zenye mabarafu.... yaani... Draxton sielewi... ni nini hiki?"

"Haina haja ya kukuelezea vitu vingi Namouih. Sikai tena huku. Ninaondoka. Nataka nisahaulike...."

"Haitakuwa rahisi kwangu kukusahau," Namouih akamkatisha.

Draxton akabaki kumtazama.

"Namaanisha... ona... kiukweli, mambo niliyojionea ni ya ajabu sana. Na... mimi ni mtu ambaye huwa napenda kuelewa vitu vizuri zaidi ili...."

"Ili iweje? Namouih mimi siyo binadamu wa kawaida. Siwezi kusaidika," Draxton akamwambia.

"Basi nakuomba unisaidie mimi," Namouih akasema.

"Nikusaidie kwa lipi?"

"Usiondoke."

Draxton akaendelea kumtazama kwa umakini, naye Namouih akasimama na kumwangalia kwa umakini pia.

"Najua hii ni ajabu, lakini nakuomba usiondoke," Namouih akasema.

"Kwa nini?"

"Kwa ajili ya Blandina. Nataka pia unisaidie... ili nijue nani alimuua rafiki yangu Felix namna ile,"
Namouih akamwambia.

Draxton akatazama pembeni.

"Ulisema ungenisaidia kumtafuta muuaji ili alipie kwa alichokifanya. Ninakuomba ubaki... unisaidie.
Please," Namouih akamsemesha kwa ushawishi.

"Namouih... sasa hivi itakuwa ngumu kwa sababu umeshajua...."

"Haitakuwa na shida, sitamwambia yeyote. Na hata kama ningesema kwa mtu, nani angeamini?"

"Siyo tu kuhusu hilo. Namouih huwa inaniumiza sana kumwona Blandina akiteseka kwa sababu hanielewi vizuri, na mimi huwa sipendi kabisa... kumuumiza. Ni bora kama nikiondoka tu ili nisiendelee kumpa nothing but pain..."

"Hujafikiria kwamba ukiondoka ndiyo ataumia hata zaidi? Umeshamwona jinsi alivyo baada ya wewe kumwambia kwamba unaondoka?"

"Najua, lakini atapona baada ya muda. Ni bora aumie kuachwa lakini siyo kuendelea kuwa na mtu ambaye hatampa faida yoyote."

"Labda... labda...."

"La, Namouih, Blandina hapaswi kujua kuhusu hili," Draxton akaongea kwa uthabiti.

"Hataamini mpaka aone. Draxton kwa nini unaogopa sana kuwa naye? Kama unasema unamjali ni kwa nini unahofia kwamba utamuumiza? Unaweza kukaa naye mbali every Time hilo jitu likikusumbua, then ukiwa fine, mnakuwa wote na...."

Namouih akaishia hapo baada ya kutambua jambo fulani. Macho ya Draxton yalilengwa na machozi. Kwa akili ya haraka, Namouih akawa amejua sasa kwamba jambo hili lilikuwa zito kuliko alivyodhani. Hofu ya Draxton kumuumiza Blandina ilisababishwa na jambo fulani ambalo liliwahi kumpata mwanaume huyu, naye Namouih akawa anataka kujua ni nini.

"Draxton... uliwahi kupenda mwanamke... halafu ukamuumiza?" Namouih akauliza kiupole.

Draxton akaendelea tu kumwangalia, kisha akageukia upande mwingine kuonyesha kwamba hakutaka kujibu hilo. Taratibu Namouih akamfata, na sasa akiwa amemkaribia, akamwona Draxton akifanya ile kawaida yake ya kufumba macho taratibu kama vile anavuta hisia fulani hivi, lakini
akaona asimuulize kuhusu hilo kwanza.

"Draxton..." Namouih akamwita kwa sauti ya chini.

"Naam..." Draxton akaitika bila kumtazama.

"Hautaniambia nini kilitokea?"

"La."

"Kwa nini?"

"Sikai tena huku, kwa hiyo hakuna haja..."

Namouih, akiwa na uhitaji mkubwa wa kumshawishi, akakishika kiganja chake. Zamu hii hakikuwa cha moto sana kama mara ya mwisho alipokigusa, naye Draxton akamwangalia kwa umakini.

"Tafadhali usiondoke..." Namouih akamwomba.

Draxton akakitoa kiganja chake kutoka kwa Namouih, kisha akasema, "Unaniomba nisiondoke
wakati unajua kabisa kwamba mimi ni mnyama?"

"Hapana. Siyo wewe. Hiyo ni sehemu nyingine tu ndani yako. Sasa nimekuelewa vizuri. Wewe ni mtu mzuri. Na ninajua utanisaidia sana kwa kuwa na mimi nitataka kukusaidia, kwa njia yoyote ile
nayoweza. Ni jambo lisilofikirika kwa yeyote kwamba unaweza kubadilika na kuwa mnyama mkali, kwa sababu umejitahidi vizuri mno kuficha hilo, na mimi nisingetambua kama nisingeku-push. Blandina... anakupenda sana. Sijawahi kuona akipenda mtu mwingine namna hiyo, na sasa nimeelewa kwamba anachopenda kwako ni huu utu wako mzuri. Huwa ananiambia namna
ambavyo hataki kukupoteza, na baada ya wewe kumwambia unaondoka Draxton... amevunjika
sana... yaani nahofia anaweza hata kujiumiza. Wewe pia najua hutaki avunjike moyo ndiyo maana bado ulikuwa naye... kwa sababu unampenda pia. Ukiondoka... ataharibika sana Draxton," Namouih
akaongea kwa hisia sana.

"Lakini nini itakuwa maana ya mahusiano yetu asipojua kwa nini siwezi kumpa anachostahili?"
Draxton akauliza kwa hisia sana.

Kauli hiyo ilimgusa sana Namouih. Ilimfanya amuwaze Efraim Donald, kwa sababu mume wake huyo alikuwa amemnyima haki yake kwa muda mrefu sana na jambo hilo likamfanya mwanamke ahisi ni kama anaadhibiwa. Ikiwa Blandina angehitaji kupitia hali kama hiyo pia isingekuwa jambo zuri, lakini angalau yeye hakuwa ameolewa kabisa na Draxton. Ni kwamba tu angalau Draxton alionyesha kutotaka Blandina apitie hiyo hali ijapokuwa asingeweza kumwambia
kinachomsumbua, tofauti na Efraim, ambaye hakusema lolote, na hakuonekana kutotaka Namouih
aipitie.

"Itakuwa ni unafiki na maigizo, na mwishowe atachoka. Huko ni kujisumbua na kupoteza muda
Namouih. Tatizo ni kwamba... no, linapaswa kuwa jambo zuri kwamba ninamjali Blandina, lakini kwa sababu ya haya yote... linageuka kuwa tatizo. Nakuwa sitaki avunjike moyo, hivyo anaendelea kuwa naye, lakini sitaki tena...."

Ikabidi Namouih amkatishe kwa kukishika kiganja chake kwa mara nyingine tena. Draxton akatulia na kubaki amemwangalia.

"Draxton... tafadhali usiondoke. Wewe ni mkubwa kwangu, una busara, unajua mambo mengi. Najua unaelewa ni jinsi gani navyohisi baada ya kukupiga risasi. Ulikuwa sahihi kabisa, kwa sababu hata kama hukufa huo usiku... ungekuwa wa kawaida ungekufa. Umenifumbua macho kuona kweli nilichokuwa nataka kufanya hakikuwa sahihi, na ninataka kukuonyesha kwamba nitarekebisha hilo..."

"Hauna haja ya kurekebisha chochote Namouih...."

"No, ninataka kurekebisha mambo. Tafadhali nisaidie, tusaidiane, kwa sababu sasa hivi kila nikinawa mikono yangu nachoona ni damu yako tu iliyomwagika nilipokupiga risasi, na ninajua ni wewe tu ndiyo utakayeweza kunisaidia ili iwe misafi tena. Please Draxton..."

Namouih aliongea maneno hayo kama tu Draxton alivyoyasema usiku ule, na mwanaume huyu
akamwangalia sana kisha akatazama chini. Kwa kutambua kwamba bado alikuwa amekishika kiganja cha Draxton, Namouih akakiachia na kurudi nyuma kidogo huku bado akiwa anamtazama kwa matumaini.

"Okay, kwa hiyo unataka nibaki, nikusaidie na ishu ya Felix, halafu baada ya hapo?"

"Tutaona na jinsi mambo yatakavyokuwa. Bado ninataka...."

"Usihisi hatia kwa kilichotokea Namouih. Ikiwa ingewezekana basi ingefaa kama usiku ule ningekufa, mimi nilikuwa sitaki tu unione nikiwa vile kwa sababu nilihofia usalama wako. Sijui ni kwa nini sikukuua baada ya kubadilika lakini ile ilikuwa bahati tu. Unaponiambia nibaki, unaongeza uwezekano wa mimi kubadilika tena na inaweza kusababisha matatizo kwa sababu...." Draxton akaishia hapo.

"Kwa sababu gani?" Namouih akamuuliza.

"Kila mara nikibadilika, ndiyo anapata nguvu zaidi. Nahofia itafika siku nikigeuka kuwa vile halafu
nisiweze kurudi kuwa mimi... na hapo ni wengi wataumia zaidi," Draxton akamwambia.

Namouih akatabasamu kidogo.

"Nini kinafurahisha?" Draxton akauliza.

"Hapana. Ni kwamba tu... unaongea utadhani tuko kwenye movie," Namouih akasema.

"Unafikiri nachosema ni masihara?" Draxton akauliza kiuthabiti.

"Najua unawaza kuhusu hali za wengine, lakini usiwe hivyo. Mbona muda huo wote umejitahidi kuwa normal na haujaumiza yeyote?" Namouih akasema.

Draxton akainamisha uso wake.

"Nakuelewa Draxton. Hakuna mtu anayependa kuonwa kuwa mnyama mkatili labda akichagua kuwa hivyo, na hiki siyo kitu ambacho ulichagua. Kwa hiyo usijali, sitakuona hivyo. Ila hakikisha tu kwamba hauningati," Namouih akajaribu kutania kidogo.

Draxton akamtazama kwa macho yake makini.

"Am sorry. Nitahakikisha naitunza siri yako, hata Blandina sitamwambia. Kwa hiyo... naweza kuchukulia kwamba umekubali kubaki?" Namouih akauliza.

Draxton akamwangalia sana, kama anatafakari cha kumwambia, kisha akatikisa kichwa kuonyesha
amekubali.

Namouih akatabasamu kidogo na kusema, "Asante. Ninajua utanisaidia sana. Blandina pia."

Draxton akatikisa tu kichwa chake tena.

"Najua hamko sehemu nzuri sana wakati huu... tafadhali mtafute uongee naye... anakuhitaji sana
Draxton, yaani ni kama amechizi," Namouih akasema.

"Sijui hata nitamwangalia vipi usoni tena baada ya nilichomfanyia..."

"Usijali, itakuwa sawa tu. Blandina hatarajii mambo mengi sana kwako... kuwa nawe tu inamtosha,"
Namouih akasema.

Draxton akaangalia chini na kushusha pumzi.

"Okay... me ngoja nikuache. Ikiwa ulikuwa unafikiria kuichoma hii nyumba moto usifanye hivyo, sawa?" Namouih akasema kiutani.

Angalau wakati huu akawa amefanikiwa kumfanya Draxton atabasamu kwa mbali, na mwanaume huyu akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa hilo huku akiendelea kumtazama.

Namouih akatabasamu pia na kusema, "Inashangaza kidogo lakini... hatujawahi kuachiana namba
za mawasiliano."

"Ninayo yako, sijawahi tu kuitumia ujumbe wala.... nitakutumia text afu'...."

"Yeah, yeah, nitai-save, itakuwa vizuri..."

"Okay."

Wawili hawa wakaendelea kutazamana kwa ufupi, kisha Namouih akasema, "Tutaonana."

"Sawa," Draxton akajibu.

Mwanamke akaondoka ndani hapo na kuelekea mpaka ndani ya gari lake. Alitulia kwa sekunde kadhaa akiitazama sehemu hiyo. Kuna kitu ndani yake kilichomfanya ahisi kama amani fulani hivi baada ya kufanikiwa kumshawishi Draxton abaki, na hiyo ikamfanya afurahi. Sasa akawa na hamu ya kufanya kazi pamoja na mtu huyo mwenye uajabu sana ambaye hakuwahi kufikiri angekuja kukutana naye katika maisha yake yote. Akawasha gari lake na kuondoka hapo.

★★

Namouih alifanikiwa kutoka msituni na kuelekea moja kwa moja mpaka kwenye nyumba ya Blandina. Alimkuta rafiki yake akiwa ameshaamka na sasa alikuwa akifanya usafi. Blandina alilala kwa muda mrefu na hata alipoamka aliendelea tu kujilaza kitandani, ndiyo akanyanyuka na kupika chakula kidogo, akala, akatulia, na sasa ndiyo alikuwa anafanya usafi. Ujio wa Namouih hapo kwa mara nyingine tena ulimfariji sana, naye akampakulia chakula pia na kukaa pamoja naye ili wazungumze kwa kuwa angalau sasa alikuwa ametulia kidogo kihisia.

Blandina akafunguka kuhusu mambo mengi, akisema namna alivyoumizwa sana na kitendo cha
Draxton kuamua kumwacha, katika maana ya kwamba waachane kabisa. Ilipokuja kwenye suala la
mahusiano, mwanamke huyu alikuwa amepita kwa wanaume wengi, lakini aliona kwamba kiwango
cha upendo alichokuwa nacho kwa Draxton kilizidi hao wote, kwa hiyo alikuwa amevunjika sana moyo. Namouih akamtia moyo kwa kusema asikate tamaa, kwa maana hajui kesho ingekuwa vipi na Mungu angekuwa amemwandalia nini, kwa hivyo asipoteze matumaini kabisa juu ya hilo bali asubiri tu baraka nyingine kutoka kwa Mola. Blandina alithamini maneno ya rafiki yake na
kuyakubali, na wanawake hawa wakaendelea kukaa pamoja hapo wakiongelea vitu vingi vyenye
kuchangamsha fikira, kama ile video ya mashabiki wa Yanga aliyoiongelea Blandina mapema siku
hiyo.

Baada ya kutumia muda mrefu pamoja na rafiki yake, Namouih akamuaga hatimaye ili aelekee
nyumbani kupumzika. Alihisi furaha na amani moyoni mwake, kama kujua kwamba angalau siku ya kesho ingekuwa na jambo fulani zuri alilotazamia kwa hamu, kwa hiyo angetakiwa kusubiri kuona matokeo mazuri ya jitihada zake. Akafika nyumbani mida ya saa tatu usiku, na mume wake bado hakuwa amerudi hivyo akaenda kuoga kisha kutulia tu; akipitia mambo ya hapa na pale kwenye simu yake.

Alikuja kupata ujumbe mfupi kwenye simu yake kutoka kwa namba ngeni, mwenye namba akijitambulisha kuwa Draxton, naye akatabasamu kwa mbali na kumjibu kwa kusema ameiona na angeitunza. Akamuuliza ikiwa tayari alirudi pale alipokuwa amepanga, naye Draxton akakubali na kumwambia angeanza kufatilia ile ishu ya kifo cha Felix haraka kabla ya yote. Namouih akafurahi sana kujua hilo, naye akamwambia wangekuwa wote kwenye sakata hilo la kumtafuta muuaji. Akafanya pia maongezi na baadhi ya rafiki zake kwa simu, kama Mwantum, Oprah, na Salome. Salome hasa ndiye aliyepatana naye vizuri kimaongezi kwa kuwa ni muda ulikuwa umepita tokea mara ya mwisho walipoongea kabla ya msiba wa Felix, na daktari yule wa ushauri na saha akawa ana hamu ya kuonana na Namouih ili wazungumze tena. Kwa kufikiria kwamba hilo lilikuwa wazo bora hasa kwa sababu na yeye Namouih alihitaji ushauri kidogo, akamwambia kama vipi wakutane kesho mahali fulani akiwa nje ya kazi ili kutumia muda pamoja, naye Salome akawa ameridhia hilo.

Baada ya kumaliza maongezi na Salome, akamtafuta na mmoja wa wapelelezi ambaye alifanya kazi na Felix kuuliza kama kulikuwa na taarifa zozote mpya kuhusiana na muuaji, lakini bado tu uchunguzi ulikuwa unaendelea bila kuleta matokeo mazuri. Akaachana naye na kubaki anawaza kwamba huenda hata watu hao walikuwa wameshapuuzia suala hilo kabisa, hivyo labda yeye na Draxton wangefanikiwa kupata ukweli juu ya jambo hilo. Kwa kuwa Namouih alikuwa amekula kwa Blandina jioni hiyo, hakuhisi njaa, hivyo Esma akapata chakula kisha akaelekea kulala. Efraim Donald alichelewa kurudi sana mpaka inafika saa sita usiku hakuwahi amefika hapo nyumbani, kwa hiyo Namouih akaingia chumbani kulala tu. Lakini bado hakupata usingizi kwa wepesi kama jana kutokana na kuwaza mengi. Zaidi ya vitu vyote
vilivyokuwa kichwani kwake ilikuwa ni Draxton. Jinsi maisha ya mwanaume yule yalivyokuwa, yaani
alistaajabisha sana. Alikuwa mzee wa miaka 95 lakini alikuwa na pigo za kijana kama wa karne hii. Akawa anawaza labda hakupaswa kumficha Blandina kuhusu Draxton kubadilika kuwa mnyama lakini akakumbuka namna ambavyo mwanaume yule alionyesha kutatizika sana kihisia ilipohusu jambo hilo, na hiyo ikafanya aheshimu tu maamuzi yake.

Imefika saa saba usiku ndiyo Efraim Donald akawa amefika nyumbani, naye akamkuta mke wake akiwa amejilaza kitandani huku anamwangalia. Akamsalimu na kuuliza kuhusu hali yake, na
Namouih akamwambia alikuwa sawa tu. Mwanaume huyo alikuwa ameshakula huko kwenye mikutano yake hivyo akaingia tu kujimwagia maji na kurudi kupanda kitandani, naye akambusu mke wake kwenye paji la uso huku akimsimulia namna ambavyo mambo yalikuwa mengi.
Akamwambia pia kwamba aliagiza mtu mmoja aende kulitoa lile gari la Namouih lililoharibika kule
walikolipeleka ili lifanyiwe matengenezo mazuri zaidi kwenye moja ya maduka yake ya magari yenye mafundi wazuri sana.

Namouih alikuwa anamwangalia sana mume wake, kisha akaanza kutembeza kiganja kwenye kifua chake kwa njia ya kumliwaza, halafu akaanza kuubusu mkono wake sehemu ya begani kama kumpa kitulizo. Efraim alikuwa ametulia na kufumba macho yake kama anatafuta usingizi, na baada ya Namouih kuufikisha mkono wake sehemu ya siri ya mume wake na kuishika kwa juu, Efraim akajigeuzia upande mwingine wa kitanda ili aulaze vyema mwili wake kwa ajili ya kusinzia. Namouih akafumba macho kwa kuhisi mfadhaiko kama ilivyo kawaida ingawa alitegemea kwa njia
moja au nyingine kukataliwa ombi lake, na kwa kuwa leo aliomba kwa vitendo, akapewa jibu kwa vitendo pia.

Mwanamke akajigeuzia upande wake wa kitanda na kulala akiwa amejikunja, akihisi maumivu moyoni mwake yaliyosababishwa na yeye kuendelea kukataliwa bila sababu yoyote. Akawaza labda Efraim alikuwa anasumbuliwa na jambo zito au lisilofikirika kama tu Draxton, lakini shida ya Draxton haikuwa kitu cha kijuujuu tu. Hakujua ni kwa nini jambo hili kwenye ndoa yake liliendelea kuwa namna hii, lakini sasa akaanza kufikiria labda angehitaji kutafuta suluhisho mbadala. Usingizi ukamchukua yeye pia hatimaye.

★★★

Siku iliyofuata, asubuhi na mapema Blandina tayari akawa ameamka na kuanza kujiandaa kwenda kazini. Alikuwa ameamka huku kichwa kikimuuma afadhali ya kilivyomuuma jana lakini akanywa tu
dawa ya kutuliza maumivu ili awe sawa zaidi. Kama kawaida yake, alijipa mwonekano mzuri sana wa kiofisi uliompendeza sana, hata kama mtu angemwangalia isingekuwa rahisi kufikiri kwamba
ana mkazo wa kihisia. Akajiahidi tu kwamba leo angeianza siku yake kwa kufanya kazi kwa bidii ili
ayaondoe mawazo mabaya kichwani na kujitahidi kusonga mbele.

Baada ya kumaliza kila kitu, akatoka nje na kwenda kulifungua geti lote la nje ili atoe gari, na hapo hapo mapigo yake ya moyo yakaanza kumwenda mbio baada ya kumwona Draxton akiwa amesimama nje ya nyumba yake. Geti lilikuwa limefunguka mpaka mwisho sasa, na nafasi
iliyoachwa katikati ya upande wa ndani na nje ndiyo iliyowatenganisha wawili hawa, nao wakawa
wanatazamana machoni kwa umakini. Blandina hakuwa ametarajia kabisa kumwona Draxton
hapo, hivyo ni mshtuko iliofanya mapigo yake ya moyo yadunde kwa nguvu kupita kawaida, lakini jambo hilo pia likafanya hisia zake alizokuwa anajaribu kuzituliza zivurugike tena.

Draxton akapiga hatua chache mbele na kumfikia karibu zaidi, na Blandina akawa anamwangalia machoni kwa umakini.

"Blandina..." Draxton akaita.

"Umefata nini? Kuna kitu ulisahau?" Blandina akauliza.

"La. Nime... nimekuja kukuona..."

"Ili iweje?"

"Nahitaji kukwambia jambo fulani..."

"Ongea haraka... nachelewa kazini," Blandina akaongea kwa uthabiti.

"Nakupenda Blandina," Draxton akasema kwa hisia.

Blandina akatulia kidogo, kisha akaanza kucheka. "Ahahahah... kwa hiyo? Unataka nifanye nini? Unataka nikubebe?" akamuuliza.

"Nakuomba unisamehe..."

"Nikusamehe kwa lipi? Wewe si umeshaamua unachotaka kufanya? Kifanye maana mahusiano hatuna tena...."

"No, si kuhusu hivyo tu. Ninakuomba msamaha kwa kukuumiza... kwa kukufanya ulie... kwa kukutesa Blandina. Haustahili hayo kabisa, na mimi ni mbinafsi mkubwa. Nimekuzoea sana Blandina, na bado ninakupenda... ndiyo maana msamaha wako ni muhimu sana kwangu," Draxton akasema kwa hisia sana.

Blandina akawa anamwangalia huku pumzi zake zikianza kuongezeka kasi.

"Nahitaji tu unisamehe kwa nilivyokutendea, na... sitarajii jambo lolote kwa sababu mimi sikustahili
Blandina... sistahili kabisa kupendwa na wewe. Ila naomba tu ujue kwamba una sehemu muhimu sana ndani ya moyo wangu... ikiwa hilo litajalisha kwa njia yoyote. Sita... sitaondoka Blandina. Kuna jambo fulani bado nahitaji kufanyia kazi na nilikuwa nimekurupuka tu jana mpaka kukwambia yale.... naomba tu kwa muda ambao nitaendelea kuwepo kuwe na amani kati yetu... maana najua nimekosea sana kuomba tuendelee kuwa pamoja," Draxton akamwambia.

Blandina alikuwa amemtazama kwa njia fulani ya kuhukumu, kisha akacheka mara moja huku akitikisa kichwa na kupiga ulimi wake ndani ya mdomo.

"Jana nilikuwa nataka kusema kwamba... ninahitaji kusafisha maisha yangu ili niweze kukupa
mapenzi kwa njia itakayokufurahisha zaidi... ila mimi tayari nilikuwa nimeridhika kuwa nawe. Nataka tu nikuridhishe wewe kwa asilimia zote, ndiyo maana kuna mambo nataka kufanya kwanza ili...." Draxton akaishia tu hapo na kuangalia chini baada ya kushikwa na simanzi.

Blandina akaanza kulengwa na machozi.

"Nafikiri tutaendelea kuonana. Kwa chochote kile kilicho ndani ya uwezo wangu Blandina... niko hapa kwa ajili yako," Draxton akamwambia.

Blandina akawa anajikaza asilie, naye Draxton akatikisa kichwa chake mara moja kama kumuaga, kisha akaondoka hapo. Mwanamke huyu alibaki amesimama tu sehemu hiyo, akiwa kama amegandishwa kutokana na kutoelewa kwa nini mambo yalikuwa yanazunguka kwa njia hiyo; tena kwa kasi sana. Jana kilisemwa kile, leo kimesemwa hiki, kesho bila shaka kingesemwa kingine tena. Hakuwa tayari kuruhusu moyo wake upeperushwe kama karatasi iliyomaliza kutumiwa na kuonwa kama haina thamani, lakini sikuzote kulikuwa tu na kitu fulani kilichomvuta kihisia aliposikiliza maneno ya Draxton, na hilo lilimfanya awe kama mtu dhaifu mbele yake.

Ni kwamba bado Blandina alimpenda sana Draxton, lakini sasa akawa hajui ni nini ambacho angetakiwa kufanya ili hali hii isiendelee kumwandama kwa njia mbaya. Kama Draxton alichokuwa anataka ni amani tu basi angeipata, naye Blandina akajiahidi kwamba asingeruhusu hisia zake zimwongoze vibaya na hivyo kuja kumsababishia maumivu mengi tu tena. Akalitoa gari lake hapo na kufunga geti la nyumba yake, kisha akaelekea kazini.

★★

Upande wa Namouih, siku ilikuwa imeanza vizuri tu kwa yeye kupumzika tena nyumbani baada ya
mume wake kuondoka kwenda kazini. Alikuwa ameshawasiliana na Draxton kwa njia ya ujumbe ili
kumuuliza kama angepata nafasi waweze kukutana na kuzungumza, naye Draxton alikuwa amemwambia kwamba mida ya saa sita kuelekea mchana zaidi angekwenda kule msituni kwenye nyumba yake kufanya mambo ya kuihakikishia usalama zaidi hiyo nyumba maana siku si nyingi mvua zingeanza, hivyo asingekuwepo huku, labda wapange kukutana siku nyingine. Lakini
Namouih akamwambia haingekuwa na shida kwa sababu hakuwa na mambo mengi ya kufanya kwa leo hivyo angemfata tu huko huko ili wazungumze, naye Draxton akakubali lakini akamsihi sana awe mwangalifu ili asije kufatiliwa na yeyote kufika huko.

Akawa amewasiliana na rafiki yake kipenzi, Blandina, ambaye sasa alikuwa ameshafika kazini. Waliongea kwa ufupi tu kwa Namouih kumjulia hali na kuulizia mapya, na ndiyo Blandina akawa amemwambia kwamba Draxton alikwenda nyumbani kwake asubuhi hiyo kuomba msamaha na kusema alikuwa anabaki. Namouih akafurahi sana na kumwambia hiyo ndiyo baraka ambayo Mungu alikuwa amemshushia, lakini bado Blandina akawa hana uhakika ni jinsi gani mambo mengi yangeendelea maana hisia zake tayari zilikuwa zimevurugika. Namouih akamwambia wangeongea zaidi wakikutana tena baadaye, kwa hiyo wakaagana na Namouih akamtakia
mwenzake kazi njema kwa kuwa yeye alipanga kwenda kazini siku ya kesho.

Baada ya kupata kiamsha kinywa hapo hapo nyumbani, Namouih akachukua gari lake la Vanguard
na kuondoka kwenye mida ya saa tano hivi, kwa sababu alikuwa na miadi ya kwenda kuonana na yule rafiki yake daktari, yaani Salome. Walikuwa wameongea tena asubuhi hii, naye Salome akawa amemwambia wakutane kwenye sehemu fulani kama mghawa wa kisasa mida ya saa sita mchana, ndiyo alikuwa na nafasi kwa ajili ya maongezi yao aliyoyasibiri kwa hamu pia. Kwa hiyo Namouih akatia gari mwendoni taratibu ili kuelekea huko, akiwa amependeza kama kawaida yake ingawa yeye alijiona kuwa kawaida tu.

Kuna wakati akawa amefika sehemu ya barabara yenye taa za barabarani na kulisimamisha gari kutokana na taa kuwa nyekundu, naye alipoangalia kwenye kioo cha pembeni aliweza kuona gari dogo jeupe aina ya Polo likiwa umbali mfupi nyuma kutokea pale alipokuwa. Siyo kwamba alipendezwa nalo, ni kwamba kwa muda fulani ni kama alikuwa akiliona sana gari hilo mpaka sasa, na hiyo ikafanya ahisi labda kulikuwa na mtu anayemfatilia, au labda yalikuwa mawazo yake tu. Baada ya magari kuruhusiwa kwenda akaendelea kuendesha huku akitazama kioo mara kwa mara, na bado gari hilo liliendelea kuonekana likitumia njia aliyotumia kwa umbali fulani; lakini
halikuacha kumfata.

Akiwa ameingiwa na mashaka zaidi sasa, akawa amelifikisha gari lake nje ya sehemu ile aliyotakiwa kukutana na Salome na kuamua kushuka ili ahakikishe jambo hili kwa asilimia zote. Akawa amesimama karibu na gari lake akijifanya kuongea na simu, huku akipiga jicho la wizi upande ambao gari lile lilitokea ili kuona kama lingepitiliza, lakini ndiyo likaegeshwa upande tofauti na wake kwa umbali mfupi. Sasa Namouih akawa ametambua kwamba alikuwa shabaha ya mtu,
naye akashusha simu yake na kuufunga mlango wa gari kwa nguvu. Alikuwa ameingiwa na hasira, naye akataka kujua ni nani aliyekuwa anataka kuanzisha mchezo wa kipuuzi kumwelekea.

Kwa ujasiri mkuu, akaanza kuelekea upande wa gari hilo, moja kwa moja kabisa mpaka alipolifikia karibu zaidi na kuanza kugonga kioo cha mlango ili mwenye nalo ajionyeshe yeye alikuwa nani. Akawa anakibamiza kwa kutumia funguo ya gari lake huku akisema aliye ndani afungue upesi la sivyo kungekuwa na shida, na ndipo kioo kikashushwa. Namouih alishangazwa sana baada ya kumwona aliyekuwa ndani ya usukani, akiwa si mwingine ila yule dereva-mlinzi wa mume wake,
Suleiman! Mwanaume huyo alikuwa anamfatilia mke wa mwajiri wake kwa sababu gani?



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Itakuwa ikiruka hapa siku za Jumatatu, Jumanne, na Jumatano. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…