Simulizi - change (badiliko)

You're correct. What a wonderful experience I had writing Efraim Donald's character, it was so surreal. I imagine his arc will make a certain amount of impact to educate most of my readers just as it has with you man... hopefully everyone will learn something different from it and not just understanding what's been shown in the story. Thanks Manyanza
 
I imagine his arc will make a certain amount of impact to educate most of my readers just as it has with you man... hopefully everyone will learn something different from it and not just understanding what's been shown in the story. Thanks Manyanza
Indeed, Chief this story I would like 50% of JF's registered members to follow and read because I believe most of us here are between the ages of 25 and 45. There are so many things to learn especially for our age
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Ilikuwa hivi. Maono ambayo Efraim Donald alipewa na "wakala" yule, yalimwonyesha vitu alivyotakiwa kufanya ili aweze kupata mambo aliyohitaji, lakini kwa uchaguzi. Yeye angepata mali alizotaka, lakini pia alitakiwa kutoa malipo kwa njia ya DAMU. Ibada yake kwa wa Lucifer ilimaanisha alitakiwa kutoa sadaka za damu kwa mmoja wa viumbe wa roho aliyekuwa mzawa wake Lucifer, na kiumbe huyo alichukua malipo hayo kwa njia ya damu. Haikuwa kwamba alipewa jina hususa na Lucifer, lakini kiduniani kiumbe huyo wa roho alifahamika kama JINI SUBIANI, na ndivyo ilivyoachwa na kuendelea kutumiwa na wengi kama walivyomdhania ili kumtofautisha yeye na viumbe wengine wa roho kutoka upande huo.

Kwa hiyo uchaguzi ambao Efraim Donald alipewa kwenye yale maono ilikuwa ni kwa masharti; masharti magumu sana. Ikiwa alitaka kupata mali nyingi na kuendelea kuzidumisha, alitakiwa kufanya mambo mengi sana ya kisadaka na kwa mpangilio hususa mpaka kufikia wakati fulani, ndiyo angemaliza na kuacha kutoa sadaka hizo. Masharti hayo yalimhitaji aue mzazi wake, kisha achukue damu yake ya tumboni na kuiunganisha na damu yake kidogo (yaani damu ya Efraim), halafu ampatie roho huyo ili ainywe. Hilo ndiyo lingekuwa lipo la kwanza. Wakala yule alipomnyooshea mkono na kumwonyesha yale maono alikuwa pia anamwingizia Efraim roho ya kiumbe yule ili iishi ndani yake, kwa hiyo kwa maneno mengine ni kwamba SEHEMU ya roho ya JINI SUBIANI ilikuwa ikiishi ndani ya Efraim Donald, ili wakati wa kutoa malipo, au sadaka, yeye Efraim angeiruhusu roho hiyo iuvae mwili wake na kuchukua malipo hayo ya damu kila mara yalipotakikana. Siyo mchezo!

Kwa hiyo ili lipo la kwanza litimie ilimbidi Efraim autoe uhai wa mzazi wake na kuunganisha damu yake kidogo na ya kwake ili ampatie Jini Subiani, na kwa hivyo mwanaume huyo akamtafuta baba yake mzazi ili amuue! Efraim Donald alikuja kumpata baba yake mkoa mwingine, ambaye tayari alikuwa na familia yake nyingine baada ya kumtelekeza yeye na wadogo zake miaka mingi sana nyuma, kwa hiyo hasira ya Efraim kumwelekea ilimchochea kumkamata na kumpa kifo kibaya sana kwa kuuchoma-choma mwili wa baba yake kwa visu karibia kila sehemu ya mwili, na ndiyo akakusanya damu yake na kutokomea nayo. Alifanikiwa kufanya hivyo kwa msaada wa Godwin Shigela, ambaye alimuunga mkono kabisa katika jambo hilo kwa sababu isingeingia akilini mwa Efraim kumtoa mama yake kipenzi kama sadaka.

Baada ya kufanikisha hilo, alipelekwa tena kwa wale mawakala, nao walimwambia namna walivyofurahishwa sana na roho ya ukatili aliyoionyesha, kisha sasa wakamwelekeza jinsi ya kufanya kila mara alipohitaji kuitoa roho ya Jini Subiani iliyokuwa ndani yake ili aweze kuipatia damu hiyo. Alifata maagizo yao vizuri mpaka akafanikiwa kumtoa roho huyo mwovu kwa mara ya kwanza. Kutoka kwa roho huyo ndani yake kulifanya mwili wa Efraim ubadilike.

Angerefuka kufikia futi nane mpaka tisa, ngozi ya mwili wake ingekuwa kama imechanika-chanika na nyeusi sana, viungo vyake vingejipinda-pinda, na mikono na miguu yake ingerefusha makucha yake kwa kiwango kikubwa. Kichwa chake kingekuwa kikubwa sana kwa muundo kama wa kichwa cha anaconda mkubwa, na usoni alitisha balaa. Angekuwa na macho makubwa mekundu yenye lenzi zenye kufanana na zile za nyoka mwenye sumu, na mdomo wake ungekuwa mpana sana wenye meno mengi makali na ulimi mrefu sana mweusi uliojikata mara mbili! Kwa njia hiyo ndiyo angekuwa ameiachia roho ya SUBIANI imtoke, kisha ndiyo roho huyo angekunywa damu kama alivyofurahia.

Baada ya kukamilisha lipo la kwanza kwa kutoa sadaka ya mzazi wake, Efraim Donald aliambiwa kwamba kuanzia hapo mambo mengi yangeanza kumwendea vyema, yaani angefanisika sana. Lakini huo ungekuwa ni mwanzo tu. Hii ilimaanisha kwamba muda ungepita, angepata mali, angeendelea na shughuli zake nyingi, na baada ya muda huo kuisha angetakiwa kuanza kutoa malipo kwa mara nyingine tena kwa njia tofauti kabisa ambayo ingempelekea mpaka kupata utajiri wa kudumu; yaani kama angemaliza kila jambo aliloagizwa kwa usahihi kabisa, ingefikia hatua hangehitaji tena kutoa sadaka hizo za damu. Malipo haya kwa ujumla yaliitwa "MZUNGUKO WA MWISHO." Kwa kuwa sasa alikamilisha malipo ya mwanzo ya damu kwa kumtoa baba yake, Efraim Donald angetakiwa kutulia kwa siku 730 ili mafanikio na mali nyingi zianze kuingia mikononi mwake, kisha baada ya hapo ndiyo angetakiwa kuanza kutoa malipo ya mzunguko wa mwisho ambayo yangemhalalishia utajiri wa kudumu.

Siku hizo alizopewa zilikuwa ni sawasawa na miaka miwili, kwa hiyo baada ya Efraim Donald kutoka hapo, kweli mambo mengi yalianza kumwendea vyema. Alipata mali na ufanisi wake ukazidi kuongezeka, lakini kama ambavyo ilikuwa kwa Godwin tu, wote walitakiwa kuishi kwa akili sana ili wasisahau kwamba walikuwa chini ya viapo ndani ya sakata halisi lililowasaidia kufanikisha mambo yao.

Kufikia kipindi hicho ambacho Godwin alikuwa anamsaidia Efraim, yeye tayari alikuwa ameshamaliza mengi ya masharti aliyokuwa amepewa, kwa hiyo alikuwa na uzoefu mzuri sana uliomwezesha kumsaidia mwenzake kwa usahihi kwenye njia nyingi alizopita mpaka akainua makampuni na kuendelea kukua tu kipesa; tena ndani ya miaka miwili tu! Wengi waliomfahamu Efraim Donald walishangaa sana baada ya kuona mafanikio yake, na mwanaume huyo hakusahau kuwatafuta wale wote waliomwonyesha dharau kipindi cha nyuma na kuwaua kwa vificho; ikiwemo yule jamaa aliyemdhulumu pesa, na wale wanawake watatu waliotoa mimba za watoto wake!

Roho ya kikatili kama ya Jini aliyekuwa ndani yake ilimvaa vizuri sana mwanaume huyo, lakini alionekana kuwa mtu ambaye ni mwema kwa wengi kwa sababu alificha makucha yake kwa ustadi wa hali ya juu. Halima, mama yake, alishangazwa pia na ufanisi wa mwanaye uliokuja upesi na kuuliza mambo yalikwenda vipi, naye Efraim alimwambia hakukuwa na haja ya kuwaza sana juu ya hayo, bali alitakiwa kuishi kwa furaha zaidi kwa sababu sasa maisha kwao yalikuwa ya kung'ara. Alimjengea mama yake nyumba mpya na nzuri sana, na hata ndugu zao wengi walianza kujipendekeza kwa wawili hawa baada ya kuona mambo kwao yamenyooka, ingawa hawakujua ni kwa njia nyingi zilizopinda.

Efraim Donald alikuwa amepewa maagizo ya kutotafuta mtoto kwa kipindi hicho ambacho alipata mali nyingi, lakini kufurahia tendo la mapenzi na mwanamke ilikuwa ruksa. Kwa hiyo mwanaume huyu alitoka na wanawake wengi sana na warembo mno, lakini sikuzote alikuwa makini sana kutojikuta anamtia mimba yeyote kati yao. Yaani hii yote ilimfanya aanze kuishi kwa njia ya mahesabu tu, na uzuri kama siyo ubaya ni kwamba alikuwa na akili nyingi iliyompa faida katika kila kitu alichofanya, na hatimaye, siku 730 zikawa zimekamilika. Ulikuwa umefika wakati wa kwenda kukutana na "mawakala" wa Lucifer kwa mara nyingine ili ishu ya malipo ya "mzunguko wa mwisho" ianze kazi. Wakati huu tayari Efraim alikuwa mzoefu sana, hasa kwa kuwa hata roho ya yule kiumbe mwenye nguvu iliyokuwa ndani yake ilimsaidia kuona mambo mengi kwa njia pana na kuu, kwa hiyo zamu hii alikwenda mwenyewe kwenye mochwari ile ili kupangwa vizuri zaidi.

Baada ya kufika siku hiyo, Efraim Donald alikwenda mbele za viumbe hao kwa njia ile ile kama alivyokuwa ameshazoeshwa na Godwin Shigela, naye akapiga magoti na kusujudu.

"Efraiiimmm.... mwana wa Donald Tumpe..." sauti nzito ya "wakala" ikasema.

"Ndiyo... ni mimi mtumishi wako," Efraim akasema.

"Umekuja na zawadi Efraiiimmm...." sauti hiyo ikasema.

"Ndiyo bwana wangu. Nimekamilisha mambo mengi sana kwa siku zote 730... na kwa umakini... na ninawashukuru kwa msaada wote ambao nimeupata, na sasa mimi kama mtumishi wako ninakuja mbele yenu ili niweze kutoa shukrani kwa malipo ya mzunguko wa mwisho... ninaomba mnipatie nafasi hiyo ili niweze kudumisha ufanisi wote mlionipatia... bwana wangu..." Efraim Donald akasema.

Sauti hiyo ikaanza kucheka kwa njia ile iliyoumiza sana masikio, kama tu ambavyo mtu angechukua masufuria, mifuniko ya bati, na zile sahani za muziki wa ngoma na kuanza kuvipiga-piga vitu hivyo kwa nguvu sana karibu na sikio. Kalakalakalakala.....

"Efraiiimmm...." sauti hiyo nzito ikaita.

"Ndiyo bwana wangu...." Efraim akaitika, akiwa bado amesujudu.

"Unaelewa kazi ya mfanyakazi wa mochwari ni nini?" sauti hiyo ikauliza.

"Ndiyo bwana wangu... ni kupunguza uzito wa hofu inayosababishwa na kifo. Wanawachukua watu waliokufa na kuwapendezesha... halafu mwisho wa siku wanakuja kutupwa chini ya ardhi chafu. Ila siyo kwamba wanafanya hivyo kwa ajili ya wafu, ni kwa ajili ya wafiwa, wanawarahisishia kusema kwa heri, na kupata malipo pia. Hiyo yote ni kwa sababu ya hofu. Watu wanaogopa kufa, na mtu wao wa karibu anapokufa inawalazimu kukumbuka... na kukubali kwamba nao pia watakufa. Tunaishi maisha yetu yote tukielewa kwamba muda wowote ule... bila onyo... bila sababu... maisha yetu yatakata. Ndiyo sababu tuna mifumo kama hii ya mochwari... ili kutusaidia kupambana na hali hiyo ya hofu ipasavyo..."

Efraim Donald alijitahidi sana kutoa jibu lake kama tu ambavyo kiumbe huyo alilielezea mara ya kwanza kabisa yeye kuletwa huku, na jambo hilo likaonekana kumfurahisha sana kiumbe huyo kwa kuwa alianza tena kucheka.

"Vizuri. Umetambua ni kwa nini nilikuuliza swali hilo?" sauti hiyo ikauliza.

"Ndiyo bwana wangu. Nikiwa mtumishi wako... sipaswi kuishi kwa hofu hata kidogo... kwa sababu ninajua hata kifo chenyewe kinakuogopa. Sihitaji msaada wa mtu yeyote kama mtunzaji au msafishaji wa maiti kwenye mochwari... kwa kuwa tayari niko upande wako... ninajua utanipa na kunisafishia chochote kile nikiwa chini ya nguvu zako... nami nitafanya kila kitu unachoniagiza ili kukupa utukufu wewe pekee..."

Efraim Donald alitoa jibu hilo kwa uhakika kabisa. Alijua, na alielewa vizuri sana ni nani aliyekuwa akimtumikia.

Sauti hiyo ikaanza kucheka tena kwa nguvu, kisha ikasema, "Inuka."

Efraim Donald akainuka na kuketi kwa kupiga magoti, huku akiwa ameviunganisha viganja vyake.

"Unakubali kufata kila kitu kama utakavyoamriwa?" sauti hiyo ikauliza.

"Nakubali... na niko tayari," Efraim akajibu kwa uhakika.

Mwakilishi huyo akanyoosha mkono wake tena kwa njia ile ile kama mara ya kwanza na kumfanya Efraim Donald aone mambo mengi sana aliyohiraji kuyafanya kwa umakini wa hali ya juu ili hatimaye aweze kukamilisha malipo yake kwa njia ambayo ingempa utajiri wa kudumu. Sasa alionyeshwa mambo kwa njia hii:

Roho iliyoishi ndani yake, aliyoifanyia utumishi kwa kutoa malipo ya damu, ilimtaka aanze kufanya utumishi huo tena lakini zamu hii ikiwa ni kila mwezi. Alitakiwa kumpa Jini Subiani damu changa ya msichana yeyote mwenye umri wa miaka 19 kila ilipofika tarehe 19, na damu hiyo ilitakiwa kuwa karibu na mfumo wa hedhi wa msichana yeyote ambaye angemuua. Zoezi hili lilitakiwa kufikisha wasichana 19, ikimaanisha lingepaswa kuendelea kwa miezi 19. Halafu, baada tu ya kukamilisha sadaka za mwanzo za damu za wasichana wanne, Efraim Donald alitakiwa kuoa mwanamke ambaye alikuwa wa pekee sana. Kusema pekee ilimaanisha kwamba mwanamke huyo asingekuwa aina ya mwanamke ambaye angefikiria hata kutoka nje ya ndoa na mwanaume mwingine mpaka malipo ya mzunguko wa mwisho yafikie hatamu. Pia, kwa muda wote ambao angekuwa amemwoa mwanamke huyo, Efraim Donald hangetakiwa kushiriki naye tendo la ndoa hata mara moja mpaka akamilishe zoezi hilo alilopewa.

Ilikuwa ni jambo fulani tata sana kifikira, lakini Efraim Donald alikuwa ameshakubali kujitoa namna hiyo mpaka ahakikishe linatimia. Kwa hiyo, wakati akiwa ameanza sakata la kuua msichana mmoja mmoja kila mwezi, mwanaume huyu angetakiwa kufanya uchunguzi wa makini sana kutafuta mwanamke ambaye angefaa kabisa kwa ajili ya jambo hili, na kwa sababu haingekuwa jambo rahisi, angetakiwa kuiomba roho yake msaada wa kipekee ili aweze kumtambua mwanamke huyo kwa macho yasiyo ya kibinadamu. Ndiyo tunaweza kusema kwamba "macho" hayo yakawa yamemwangukia Namouih. Mwanamke huyo mrembo ndiye aliyepatikana kufaa zaidi kwa Efraim Donald kwa ajili ya jambo hili, na ndiyo sababu mwanaume huyu akafanya kila jitihada ili kuweza kumpata. Hiyo ndiyo sababu iliyofanya hata kipindi ambacho Efraim hajaanza rasmi kumtongoza Namouih, mwanamke huyu aliona kama mtu fulani anamtazama sana gizani mara kwa mara kwa njia yenye kutisha. Yalikuwa ndiyo hayo "macho" yanamwangalia.

Kila kitu kilikuwa ni kwa mpango na mahesabu ya hali ya juu. Efraim Donald hakuingia kwenye maisha ya Namouih kinagaubaga, ilikuwa kwa njia ya mpango wa siri. Alifatilia maisha ya mwanamke huyo kwa kina na kuunda mpango ambao ungekwenda kupatana na malengo yake, na kwa njia fulani mambo yakawa yamerahisishwa zaidi kwake kutokana na ugonjwa uliompata mzee Masoud, yaani baba yake Namouih. Alitumia maneno mazuri kumnasa, akatoa pesa nyingi, na kuifanyia mambo mengi familia ya mwanamke huyo ili aweze kumwingiza ndani ya pango lake la siri, na kama ujuavyo, alifanikiwa. Ila kuna vitu vingine vilivyotokea na kuongezeka baada ya Efraim kumjua Namouih vizuri zaidi.

Wakati huu ni kweli Efraim Donald alikuwa mkatili na mbinafsi, ila alipokutana na Namouih, alimpenda kutoka moyoni. Mwanamke huyo angekuwa ni sehemu ya mpango wake ndiyo lakini alitaka kuhakikisha kwamba anaendelea kuwa naye hata baada ya kukamilisha utumishi wake wa malipo ya damu kwa Jini Subiani. Alielewa mambo mengi kwa njia pana zaidi, na kujua kwamba hakutakiwa kufanya mapenzi na Namouih kungekuja kusababisha maswali mengi akishamwoa, ndiyo kitu kilichomfanya atake kufanya naye mapenzi KABLA ya kumwoa. Hakungekuwa na shida endapo kama angeshiriki mapenzi na mwanamke huyo kabla ya ndoa, na lengo lake pia lilikuwa kumfanya Namouih abebe ujauzito wake kabla hata hawajaoana, ili wakishaoana mwanamke huyo asikazie fikira sana kuhusu haki yake ya ndoa akiwa tayari na ujauzito na hata akijifungua. Lakini kutokana na Namouih kumkatalia kumpa penzi wakati huo, ikambidi Efraim Donald afikirie njia mbadala ya kuivuruga akili ya mwanamke huyu; hasa ukifika usiku wa ndoa yao.

Mara ambazo Efraim Donald alikuwa amejaribu kuweka jitihada za kufanya mapenzi na Namouih kabla hajamuoa ziligonga mwamba kutokana na mwanamke huyo kuwa bado na hisia zilizovurugika, ila walipoanza kuielekea ndoa yao, Efraim Donald alitambua kuwa mwanamke huyo alianza kumzoea zaidi, na alitazamia kumpa tunda lake la kwanza usiku wa ndoa yao, kwa hiyo Efraim akafanya mpango ili usiku wenyewe kutokee jambo fulani ambalo lingemvuruga kihisia mwanamke huyo, yaani, kifo cha mzee Masoud! Kifo cha baba yake Namouih hakikuwa kwa sababu ya mwili wake kushindwa kustahimili maumivu, bali ni kwa sababu Efraim alitumia uchochezi wake kwa pesa nyingi ili kumlipa mtu fulani kule aweze kumuua mzee Masoud na kutuma taarifa za kifo chake kwa muda hususa ambao Efraim na Namouih ndiyo walikuwa wameingia tu chumbani kwao baada ya kufunga ndoa rasmi. Hayo yalikuwa mahesabu ya hali ya juu na ukatili mbaya sana!

Kwa hiyo baada ya kufanikiwa kuichanganya akili ya mke wake kwa miezi michache kutokana na kifo cha baba yake, mwanaume huyu akawa anaendelea kuua wasichana wengine wenye miaka 19 kila mwezi na kuipa roho yake damu zao, na siyo kwamba ilikuwa tu kutimiza wajibu kwa ajili ya kuudumisha ufanisi wake; alifurahia kabisa ukatili huo. Kwa sababu Namouih hakuwa mwanamke mwenye papara aliweza kutulia kwa miezi mingi bila ya kugusia suala la haki yake ya ndoa, hata mara chache ambazo alitaka kupatiwa penzi na mume wake na Efraim kutoa visingizio vya hapa na pale, alimwacha tu. Lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, Efraim Donald alielewa kwamba mke wake angeanza kuchoka na angekuwa na maswali mengi kichwani, kwa hiyo alihitaji kuendelea kuwa mbunifu zaidi ili kuhakikisha miezi 19 inakamilika na msichana wa mwisho anauawa, halafu mengine ndiyo yafuate. Lakini, mara tu Namouih alipomsimulia kwa mara ya kwanza kuhusu ndoto mbaya alizokuwa ameanza kuota, mwanaume huyo alitambua fika kwamba mambo yangeharibika muda usio mrefu.

Sharti la kuhakikisha kwamba mke wake hatoki ndani ya ndoa na kulala na mwanaume mwingine lilikuwa pana sana. Ikiwa Namouih angemsaliti Efraim kwa kuvutiwa au kutoka kimapenzi na mwanaume mwingine, mwanamke huyo angeanza kuona mambo mengi yaliyokuwa yanamzunguka bila yeye kutambua. Hii ilimaanisha kwamba angeweza hata kumwona Efraim Donald akifanya mambo ya kikatili kwa wasichana wengi kupitia ndoto zake, na hilo lingekuwa jambo zito sana kwa mpangilio wa mambo mengi yaliyotakiwa kukamilishwa na Efraim Donald. Kwa hiyo aliposimuliwa na mke wake yale mambo ya vivuli vyenye kutisha, Efraim Donald alitambua kwamba huenda mke wake alikuwa ameanza kutoka nje ya ndoa au kumpenda mwanaume mwingine; kitu kilichomfanya aanze kumfatilia kisiri.

Siku ile ambayo Namouih alikutana na Felix Haule kujadili kuhusiana na utata wa vifo vya wasichana, hususani kifo cha Agnes, na shuku zake kumwelekea mwanasheria Draxton, ni Efraim Donald ndiye aliyekuwa akiwaangalia kwa umbali mfupi ndani ya gari lake kutokea sehemu ile wawili wale walipokutana. Alifanya hadi makusudi ya kumpigia mke wake simu na kumuuliza yuko wapi, na kwa kufikiri alimdanganya baada ya kusema ametoka ofisini na kwenda kukutana na mtu kikazi ili tu awe na Felix, Efraim akadhani kwamba huyo Felix ndiye aliyekuwa shida. Kwa hiyo, siku hiyo akawa amepanga kuhakikisha kwamba anamwondoa mwanaume huyo kuwa kikwazo haraka sana, na ndicho kitu alichokwenda kufanya usiku huo baada yeye na Namouih kwenda kwenye harusi ya rafiki na kumuaga mke wake akisema anakwenda kukutana na mtu fulani kushughulika na masuala ya kikazi; tena "mkuu wa Cargo." Hii inakumbukwa, siyo?

Ndiyo. Mwanaume huyo alikwenda mpaka eneo alilojua angemkuta Felix, na ilikuwa ni sehemu ile ile yenye kumbi ya starehe ambapo Blandina na Draxton walikutana na Felix na kuzungumza naye kwa ufupi. Efraim Donald, akiwa pamoja na Suleiman, walimsubiri mwanaume huyo atoke sehemu hiyo, kisha wakamfatilia mpaka alipokwenda sehemu nyingine tena kupata kinywaji; kwa sababu kule alikotoka alikuwa anavunga tu kwamba alienda kupata vinywaji ili amchunguze Draxton kwa ufupi.

Felix akiwa sehemu hiyo nyingine sasa, Suleiman alikwenda huko na kutengeneza kisa kidogo cha kupamiana naye, kisha akaweka dawa fulani ndani ya kinywaji chake ambayo ilikuwa na kusudi la kufanya mtu aharishe sana. Felix alimfahamu Suleiman kuwa dereva wa mume wake Namouih, nao wakasalimiana vizuri huku Suleiman akiomba samahani kumpamia, kisha mwanaume huyu akarudi mpaka kwenye gari la Efraim Donald. Suleiman hakuwa dereva-mlinzi tu, alikuwa mkono muhimu wa Efraim kwenye mambo yake haramu pia.

Felix alihisi vibaya sana tumboni mwake baada ya kumaliza kinywaji alichochukua, naye akatoka upesi kwenda kutoa haja kubwa. Choo cha sehemu hiyo kilikuwa kimejaa watu, kwa hiyo akatoka hapo na kwenda upande mwingine uliokuwa na choo cha kulipia, naye akaingia huko na kuanza kushusha haja zake zilizokuja ghafla sana. Alipomaliza mpigo wa kwanza, mwanaume huyu akaanza kuvaa suruali yake na kujiandaa atoke ili aondoke kwenda kutafuta dawa ya kutibu tumbo, na ndipo alipofungua tu mlango akakutana uso kwa uso na Efraim Donald.

Felix alishtuka kwa sababu ya ujio usio rasmi wa mwanaume huyo, lakini pia ni jinsi alivyoonekana. Efraim alikuwa amevalia nguo nyeusi mwili mzima wakati huu pamoja na viziba viganja vyeusi (hand gloves), na nguo hiyo ilikuwa yenye sehemu ya kufunika kichwa chake mpaka kuziba uso kufikia usawa wa macho, na kabla hata Felix hajanena lolote Efraim akamchoma kwa kisu tumboni huku akiuziba mdomo wake kwa nguvu sana. Alimkandamiza sehemu ya nyuma kabisa ya ukuta wa choo hicho, naye akaendelea kumchoma na kumchoma mara nyingi sana tumboni, kisha akafanya kama kulikata kutokea ubavu mmoja kwenda mwingine!

Baada ya Felix kuwa ameishiwa nguvu kabisa na kukata roho, Efraim akaingiza kisu hicho ndani ya mdomo wa mwanaume huyo na kuukata ulimi wake, halafu akautupa ndani ya tundu la choo huku damu nyingi ikitapakaa chini. Kisha akaanza kuvua nguo hiyo aliyokuwa amevaa upesi sana pamoja na hizo glovu mikononi, kitu kilichomfanya abaki na nguo zake za kawaida, halafu akaziweka ndani ya mfuko mgumu aliokuwa nao na kuufunga kwa nguvu. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliweza kuhisi tukio hili kwa sababu sikuzote Efraim Donald alipofanya jambo kama hilo, roho yake ya ndani ilikuwa ikimpa "ulinzi" ili iwe kama vile hakuonekana. Hii haikumaanisha kwamba hakuna mtu ambaye angeweza kuona mambo hayo kama angeingia humo, ni kwamba roho yake ingesaidia kufanya hata WAZO tu la kuingia ndani hapo lisifikirike kwa yeyote mpaka Efraim aondoke. Hiyo ndiyo sababu hata Draxton alipojaribu kufatilia harufu ya mtu au watu waliofanya mauaji ya Agnes na Felix alishindwa kuipata kwa sababu ilikuwa ni kama "imepotea tu."

Kwa hiyo baada ya Efraim Donald kumaliza kufanya mauaji ya Felix, alirejea kwa mke wake usiku huo na kumkuta akiwa na yule rafiki yake mpya, mwanamama daktari Salome, naye akaendelea kufanya maigizo yake ya kuwa mume mwema mpaka waliporudi nyumbani na Namouih. Walipokorofishana kidogo kuhusu kwa nini Efraim hampi mke wake haki yake ya ndoa, Namouih ndiyo alipigiwa simu na Blandina kupewa taarifa kwamba Felix alikuwa ameuawa, kwa hiyo haingefikirika kwa mtu yeyote kuwa Efraim ndiye aliyehusika na mauaji yake kwa kuwa muda huo alikuwa pamoja na Namouih na hata akaanza kumbembeleza mpaka kuja kwenda naye msibani. Alijua sana kuficha makucha yake mwanaume huyo, na kufikia wakati huo alidhani kwamba kwa kumuua Felix ndiyo alikuwa amemaliza tatizo la Namouih la kupatwa na ndoto mbaya zenye kumwonyesha mambo yaliyoendana na maovu ya mume wake, akifikiri huyo ndiye aliyekuwa kitovu cha usaliti kutoka kwa mke wake.

Lakini siku ambayo Namouih alikuja kuota tena ndoto mbaya iliyomhofisha mpaka akatukana kwa hasira, ndiyo siku Efraim Donald aliyotambua kwamba kitendo cha kumuua Felix hakikuwa na faida yoyote. Alifanya hadi kumuuliza jinsi ndoto hiyo ilivyokuwa, na Namouih ndiyo akamwelezea kwamba alijiona akiwa mochwari, mara msituni akiwa bila nguo, na aliona kiumbe mwenye kutisha aliyekunywa damu ya mtu baada ya kumuua kikatili sana. Efraim Donald alielewa wazi kabisa kwamba ndoto hiyo ilihusiana moja kwa moja na jinsi mambo yake ya gizani yalivyokuwa, naye akashindwa kuelewa kwa nini bado zilikuwa zikimpata.

Alikuwa ameshamfatilia Namouih vya kutosha kuelewa kwamba mke wake hakuwa akienda nje ya ndoa yao wala kumsaliti kwa kutoka na mwanaume au mwanamke mwingine, kwa hiyo ikawa wazi kwake kwamba Namouih alikuwa ameanza kuvutiwa na mtu fulani bila yeye mwenyewe kutambua hilo. Hiyo ndiyo sababu bado ndoto hizo hazikumwonyesha mambo mengi waziwazi lakini kama angetoka ndani ya ndoa yake na kufanya mapenzi na MTU mwingine, yote aliyofanya Efraim yangefunuliwa kwake.....


β˜…β˜…β˜…β˜…


Efraim Donald akiwa nchini Kenya jijini Nairobi kwa ajili ya kufanya mikutano yake ya kikazi, alikuwa amekutana na rafiki yake wa karibu sana Godwin Shigela, ambaye ndiye aliyempa "msaada" wa kumwinua kutoka kwenye ufukara wa kadiri mpaka kuwa tajiri. Wakiwa wamekutana usiku mmoja kwenye kumbi ya kifahari ya starehe, Efraim akawa amemwelezea rafiki yake namna ambavyo hali ya Namouih ilimkosesha amani, kwa kuwa alikuwa amebakiza msichana mmoja tu wa kuua ili kukamilisha malipo yake ya mzunguko wa mwisho. Yaani kutokea alipomuoa Namouih mpaka wakati huu, alikuwa ameshaua wasichana 18, yule Agnes akiwa ndiyo wa mwisho, na sasa alikuwa akisubiri tarehe 19 ya mwezi uliofuata ili aue msichana wa mwisho kukamilisha jambo hilo.

Haingekuwa ngumu kwake kupata msichana wa miaka hiyo, kwa sababu mara nyingi alitumia wasichana ambao waliishi maisha yao kwa kutojali sana, kama malaya vile. Angechukua mmoja na kwenda naye mbali kujiridhisha, kisha angemuua na kuchukua damu yake ili kwenda kuitoa sadaka kwa roho ya JINI SUBIANI iliyokuwa ndani yake. Siyo kwamba kufanya mambo hayo ilikuwa rahisi, ni kwamba tu alifurahia sana kuifanya ionekane kuwa rahisi kiasi kwamba mpaka kufikia wakati huu hakuna mtu aliyeweza kutambua hila zake. Lakini sasa hivi, hakuwa na lengo la kuchukua msichana yeyote tu, alikuwa anataka kumaliza mchezo huu kwa njia ambayo ingemburudisha sana, na ndiyo sababu alimwambia Godwin kwamba ana mpango wa kupata raha fulani hivi ambayo Subiani angeipenda sana, maana ilionekana kuwa tamu mno. Mpango wake huo ulikuwa umeanza kazi.

Baada ya kujitumbuiza vya kutosha na rafiki yake sehemu hiyo ya starehe, Godwin akamtafutia Efraim mwanamke mweupe mwenye umbo nono haswa ili amtumie kwa ajili ya kumridhisha kimapenzi usiku huo. Efraim Donald kutompa Namouih haki ya ndoa haikumaanisha asingeweza kufanya mapenzi na wanawake wengine, na alipenda sana kufanya mapenzi na wanawake weupe. Hii bila shaka ilikuwa ni kwa sababu ya mke wake. Alikuwa anampenda Namouih, na alitamani sana kwa kipindi kirefu mno kumshika na kumwonyesha namna anavyotaka kumpa penzi murua, lakini alikuwa makini sana kutosahau aina ya maisha aliyotakiwa kuishi. Alikuwa anatazamia kwa hamu kubwa kumaliza haya mambo mengine yote ili hatimaye aje kumuonja mke wake, kama tu alivyosema, na kwa sababu sadaka alizotoa zilikuwa zinaelekea mwishoni alihisi hamu kubwa sana iliyofanya awe kama mtu anayekosa subira.

Lakini yote kwa yote, bado suala la Namouih kuwa na hisia kwa mtu mwingine bila yeye mwenyewe kutambua ni jambo ambalo Efraim Donald alitakiwa kulifatilia kwa kina ili ahakikishe analitatua, kwa sababu kama asingeangalia, lingeweza kumsababishia hitilafu kwenye mipango yake. Akamchukua mwanamke huyo na kumpeleka mpaka kwenye hoteli aliyochukua chumba jijini hapo, naye akapatiwa huduma nzuri sana kwa kupewa penzi, lakini bila shaka la malipo. Sikuzote alipofanya mapenzi na mwanamke mwingine angevuta taswira kwamba yuko na mke wake, kwa kuwa alitazamia kwa hamu sana siku ambayo angemvua nguo yeye mwenyewe na kufanya alichotamani kumfanya kwa muda mrefu sana.

Huyo ndiyo alikuwa EFRAIM DONALD!


β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
PREDICTION.
msichana wa mwisho aliyekwenye rada za efraim, ni mdogo wa namouih
🀣🀣🀣 Kwanini utabiri wakati Elton Tonny yupo? Asante sana Mkuu unaandika vizuri sana na Kiswahili chako ni cha kipekee sana na hii simulizi inaingia sana kwenye akili yangu ma kuhusu hii historia ya Efraim Donald inaakisi maisha ya watu wengi ambao wana hadhi mbele ya jamii lakini nyuma Yao Kuna ya Siri ya hovyo sana Huwa wanafanya. Ninaendelea kukufiatilia Mkuu.
 
Pamoja sana mheshimiwa πŸ’ͺ
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Zikawa zimepita siku tano baada ya Efraim Donald kuondoka nyumbani ili kwenda kufanya mikutano yake nje ya nchi. Kama kawaida, mwanasheria mahiri Namouih aliendelea na kazi yake vizuri sana kwa kuwa wiki hii alifanikiwa kumaliza kesi mbili kwa ushindi; moja ikiwa ni mahakamani na nyingine ikiwa imetatuliwa bila kuihusisha mahakama. Bila shaka Blandina alikuwa pamoja naye kama mkono wake muhimu wa usaidizi katika mambo hayo, na matokeo kuja vizuri kwa upande wao kukaongeza sifa za ubora wao katika kazi na sifa ya kampuni waliyofanyia kazi kwa ujumla.

Mara kwa mara Efraim Donald angewasiliana na mke wake kumjulia hali, naye Namouih angemwambia anaendelea vyema na anasubiri ujio wake kwa hamu. Ndani ya siku hizi chache tokea mara ya mwisho walipoonana pale alipopanga, Draxton hakuwa ameonekana mbele zake Namouih mpaka wakati huu. Walifanya mawasiliano tu kwa njia ya simu, na kwa kiasi kikubwa walikuwa wameweza kuzoeana sana tofauti na ilivyokuwa mwanzoni. Kuna wakati wangejikuta wanatumiana jumbe kwa muda mrefu zilizohusiana na mambo mengi ambayo kwa njia mbalimbali yalifurahisha, ingawa bado walikuwa wanaendelea kusikilizia matokeo ya utafiti wao kuelekea matukio ya mauaji ya wasichana, pamoja na kifo cha Felix.

Kwa muda huo wa siku chache ambazo Efraim Donald alikuwa amesafiri, Blandina na Namouih walikuwa wamepokea mialiko kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya ndoa kutoka kwa mwenzao aliyefanya kazi ndani ya kampuni hiyo hiyo kama wao, na bila shaka wangekwenda kwa kuwa alikuwa ni rafiki, ila Blandina akawa amefikiria kufanya mpango wa kwenda pamoja na Draxton pia. Alimfikishia mpenzi wake wazo hilo, akimshawishi kwa maneno mazuri kwamba ingependeza sana wakienda pamoja, na ingawa Draxton alionyesha kutotaka kwenda mwanzoni, mwishowe akakubali na kusema wangekwenda pamoja.

Blandina alifurahi sana na kumwambia Namouih kwamba Draxton angehudhuria sherehe hiyo pamoja nao, na kiukweli jambo hilo lilimfurahisha Namouih pia kwa sababu, kuna hiki kitu tu kwamba alikuwa na hamu ya kumwona Draxton tena, kama vile alikuwa amemkosa sana. Hakuyapeleka mawazo yake mbali mno lakini kutokana na kuwa mtu pekee aliyejua mambo mengi kumhusu mwanaume yule kulimfanya amwone kuwa muhimu sana; ndiyo moja ya sababu zilizofanya amfurahie mno.


β˜…β˜…β˜…


Sasa ikawa imefika siku hiyo ya sherehe, au sendoff. Ikiwa ni Jumamosi, marafiki hao wawili walimaliza mambo yao ya kikazi mapema na kwenda kujiandaa kwa ajili ya hudhurio lao la sherehe hiyo. Walikwenda pamoja kwenye saluni ya urembo iliyokuwa na spa, nao wakahudumiwa vyema kwa njia walizotaka ili kupendeza haswa. Walikuwa wameamua tu kufanya hivi leo kwa sababu ulikuwa umepita muda bila ya yeyote kati yao kujishughulisha na masuala ya urembo. Na walipendeza haswa.

Blandina alitengeneza kichwa chake kwa kukisukia nywele ndefu na laini zenye mawimbi-mawimbi, zulizokuwa na rangi ya brown-nyeusi, naye Namouih alisuka nywele zake kwa mtindo wa yebo rasta, yaani njia nene kichwani kwa mtindo wa rasta ndefu ambazo zilifikia mpaka mgongoni kwake kama angeziachia, lakini alizisukia kwa upande mmoja wa kichwa chake, na upande mwingine akauacha na nywele zake laini. Alipendeza sana kwa mtindo huo kiasi kwamba kila mtu kwenye saluni hiyo alikuwa akimsifia sana, vile vile na Blandina pia. Blandina hakuwahi kuwa na husuda kumwelekea Namouih kwa sababu ya kuwa mrembo zaidi yake, kwa kuwa yeye alimwona kuwa kawaida sana ingawa mara nyingi rafiki yake ndiyo alisifiwa kupita kiasi. Walipomaliza kujitengeneza vizuri hapo ndiyo wakaelekea majumbani kwao ili kujiandaa vyema kimitoko kwa ajili ya kukiwasha kwenye sherehe ile.

Blandina alivalia kinguo kifupi chenye kuvutika kilichoishia sehemu za mapaja yake. Kilikuwa laini sana, chenye muundo wa ngozi ya simbamarara (tiger), na kiliacha sehemu kubwa ya juu ya matiti yake kwa mbele ikiwa wazi. Kilimpa mwonekano bomba sana wa mwanamke aliyejua kujiachia, na kililichora umbo lake vizuri mno. Miguuni alivaa viatu virefu vyenye rangi ya moto na mkononi alibeba pochi ndogo. Namouih yeye alivaa gauni fulani yenye kuvutika, iliyokuwa ya rangi ya zambarau mchanganyiko na nyeusi hapa na pale, ikiwa na urembo wa vitu vidogo vyenye kumetameta kama almasi kuizunguka. Vazi hili lilikuwa refu, lililofunika sehemu kubwa ya mwili wake na kuacha uwazi mdogo katikati ya kifua chake, na liliubana mwili wake vizuri sana kuchoresha maungo yake vyema pia. Alifunika kichwa chake kwa mtandio au ushungi mdogo wa nguo hiyo hiyo, akiwa anaonekana kufuata ufanani wa desturi ya mwanamke wa kiislamu katika uvaaji wa hijab, na kama kawaida, uso wake ulipendeza sana. Alivaa viatu vya kuchuchumia pia vilivyoacha miguu yake wazi kufikia sehemu za vidole, vilivyokuwa na rangi ya blue-bahari yenye kung'aa. Wanawake hao walidamshi vibaya mno!

Marafiki hawa walikuwa wamekubaliana kukutana sehemu ambayo hafla hiyo ya sherehe ingefanyikia kwenye mida ya saa mbili usiku, hivyo baada ya kujipa mionekano yao bomba wakaelekea huko hatimaye. Blandina alikuwa amemwambia Namouih kwamba Draxton tayari alikuwa amefika huko baada ya kutoka kwenye shughuli zake kwa hiyo alikuwa akimsubiria, na jambo hilo likamwongezea Namouih hamu ya kutaka kufika huko. Sehemu ambayo sherehe hiyo ya sendoff ingefanywa ilikuwa kwenye ukumbi maridadi sana wa hoteli kubwa ya kifahari, ambao ulikuwa umejengwa orofa ya chini kabisa ya jengo; kwa maneno mengine, chini ya ardhi. Wageni wengi walikuwa wameanza kufika hapo na kuingia ndani kule, naye Draxton alikuwa amesimama upande wa nje kwenye sehemu ya kuegeshea magari; akiwa ameegamia gari lake kwa subira kumngojea Blandina wake.

Aliyeanza kufika hapo kati ya marafiki wale wawili alikuwa ni Namouih. Draxton alilitambua gari lake upesi, ile Vanguard ya maroon-nyeusi, naye akaendelea kulitazama mpaka lilipopelekwa sehemu hiyo ya maegesho na kusimama tuli. Kisha Namouih akashuka sasa na kuanza kutembea taratibu huku ameshika pochi ndogo kiganjani. Hakuwa amemwona Draxton pale alipokuwa amesimama, hivyo mwanaume huyo akampungia mkono kidogo, na baada ya Namouih kumwona, akaachia tabasamu la mbali lakini kwa furaha sana. Akaendelea tu kusimama hapo hapo huku akimwangalia, naye Draxton akatabasamu pia. Mwanaume alikuwa amevaa jaketi gumu jeusi (leather jacket) lililofunika T-shirt nyeupe kwa ndani iliyokuwa na michoro ya radi zenye rangi mbalimbali, suruali ya jeans ya rangi ya samawati iliyokoza sana, na viatu vyeusi vigumu vyenye muundo mzuri sana ulioendana na suruali aliyovaa (formal leather shoes). Mwonekano wake ulipendeza pia, na Namouih akaanza kuelekea mpaka pale jamaa alipokuwa amesimama.

Kama mtu yeyote ambaye hakuwafahamu angewaona, basi angefikiri walikuwa ni wapendanao maana Namouih alikuwa mrembo sana na Draxton alikuwa mwanaume mzuri, yaani walipendezeana. Ila watu hawa walijielewa na walifurahia zaidi urafiki waliokuwa nao, na baada ya Namouih kumfikia karibu zaidi, kama kawaida mwanaume huyo akainamisha uso wake kidogo baada ya kuingiza harufu nzuri ya Namouih kwenye pua zake, naye alipomwangalia tena akakuta Namouih anatabasamu tu. Mwanamke akamsalimu vizuri, naye Draxton akaitikia vizuri pia.

"Umependeza," Namouih akamwambia.

"Ahah... mwanaume huwa hapendezi," Draxton akasema.

"Ahahahah... huwa anafanyaje sasa? Anang'aa?" Namouih akauliza.

"Angalau ukisema kwa njia hiyo... inakubalika," Draxton akasema.

"Ahahahah... wanaume bwana..."

"Ni kweli. Ukiniambia nimependeza inanifanya nihisi labda kuna lipstick mdomoni mwangu..."

"Ahahahah... unayatoa wapi hayo mawazo?"

"Kuna wakati niliwahi kupanda bus... nilikuwa nimekaa siti moja na mwanaume fulani, akasema nimependeza. Sikumwelewa na kuchukulia ni kawaida kwa hiyo nikamwambia asante. Mpaka alipoanza kulazimisha nimpe namba ndiyo hiyo 'umependeza' ikaeleweka akilini sasa..."

Namouih akacheka sana. "Yote hiyo kwa sababu ulikuwa umependeza?"

"Alikuwa anasema me mzuri... kanipenda..."

"Jamani..."

"Unafikiri alikuwa anawaza nini?"

"Kwamba we' ni shosti?"

"Ahahahah... ndiyo hivyo. Nilijuta kusema asante mtu akiniambia hivyo..."

"Ahahahah... umenifurahisha Draxton. Ila hayakuwa makosa yake."

"Kwa nini?"

"Una sura nzuri sana," Namouih akamwambia bila kupindisha.

Draxton akatulia kidogo, kisha akasema, "Well, kwa sababu wewe siyo huyo jamaa, nitasema asante."

Namouih akacheka kidogo.

"Umependeza pia. Sana," Draxton akamwambia.

Namouih akamtazama kwa macho yenye upendezi mwingi, naye akasema, "Asante Draxton."

"Sitakuficha... nahisi kuja leo hapa siyo wazo zuri sana," Draxton akasema.

"Kwa nini? Yaani wewe kuja hapa siyo vizuri?" Namouih akauliza.

"Yeah. Inaweza ikatokea... you know..."

"Ahahah... Draxton relax. Kila kitu kitakwenda sawa. Utafurahia mambo mengi halafu... utaona namna ambavyo Blandina anajua kujiachia sana kwenye party kama hizi..."

"Eti eeh?"

"Acha! Yule mwanamke ni mwisho," Namouih akasema.

Draxton akatabasamu kidogo na kusema sawa, angejitahidi kutulia ili kumpa wakati mzuri mpenzi wake pia. Namouih alikuwa ameshatambua kwamba wengi kati ya wanaume na wanawake ambao walikuwa nje hapo walimtazama sana yeye na Draxton, lakini mwanamke hakuona haja yoyote ya kuwapa umakini wake hata kidogo.

Dakika si nyingi sana zilizopita na Blandina akawa amefika hapo. Mwanamke huyu ndiyo aliyeongoza zaidi kuangaliwa kwa sababu ya jinsi alivyovaa, na kiukweli hata Namouih alishangaa kiasi kuona jinsi alivyovalia. Alionekana kama vile mtu anayetaka kujielekezea fikira yeye pekee tu, kama malaya vile, na kiukweli lengo lake lilikuwa kunyanyua macho na midomo ya watu kumwelekea ingawa hakuwa na sifa ya umalaya; huo ulikuwa ni uzungu tu. Mwili wake mnono wenye ngozi laini ulivutia macho ya wengi, hususani Draxton, ambaye hangeweza kujizuia kumwangalia kwa matamanio.

Mrembo huyo akamfikia Draxton karibu na kumkumbatia, kisha akambusu kinywani bila hofu yoyote ile. Namouih akatabasamu tu na kusogea pembeni kidogo, na ndipo Blandina akamgeukia na kumsalimu kwa shauku pia. Namouih na Draxton wote walimsifia kwa kupendeza sana, naye akamsifia Namouih kwa mwonekano wake pia. Kwa kuwa sasa walikamilika hapo, wakaelekea ndani kule ili kutafuta sehemu nzuri ili wakae. Blandina alikuwa anasema ikiwa Marietta na Dantu wangekuwepo sehemu hiyo ingependeza hata zaidi, kwa sababu kufikia wakati huu marafiki zao hao walikuwa wameshaondoka jijini hapo.

Waliingia ukumbini na kutafuta meza iliyokuwa na viti vitatu pekee kuizunguka, iliyofaa kwa ajili yao tu na siyo kuongeza mtu mwingine. Ukumbi huo ulipendeza sana kwa kuzungukwa na vitu na watu wa gharama; pesa ilikuwa itikadi kuu hapo. Wakaletewa vinywaji huku wakiendelea kutazama jinsi taratibu za sherehe zilivyoendeshwa, kukiwa na watu wengi pia waliokuwa wageni waalikwa. Kama ilivyo ada ya sherehe za sendoff, watu walifurahia manjonjo ya semi kutoka kwa MC, maharusi wakipewa zawadi na salamu kutoka kwa marafiki, vitumbuizo vya muziki, na hatimaye ukawa umefika muda wa kupata chakula.

Ingawa huu ndiyo wakati unaopendwa zaidi katika sherehe, Namouih alihisi kuboeka kila mara alipohudhuria sherehe kama hizi na kutakiwa kwenda kupanga foleni kwa ajili ya chakula. Hakupenda tu, ingawa hiyo ndiyo ilikuwa desturi ya sherehe nyingi kama hizo. Blandina akawa anamwambia aache mashauzi yake ili waende kupata chakula pamoja, lakini Namouih akasema yeye alitosheka na vinywaji tu hivyo angebaki hapo. Blandina hakutaka kuendelea kumlazimisha, naye akamwambia Draxton waende kuchukua chakula kabla hawajakuta imebaki miguu ya kuku pekee.

Draxton akamwangalia Namouih, naye akamsisitizia mara moja tu kwenda kuchukua chakula kwa sababu aliona ni jambo linalofaa zaidi. Namouih akatulia kidogo akimwangalia Draxton machoni, na kwa msisitizo huo mmoja wa mwanaume huyu Namouih akakubali kwenda. Blandina akawa anamwambia aache kuwa anajifaraghua sana mtoto wa matawi, naye akamshika Draxton mkono na kuanza kumwongoza kuelekea upande waliohudumia vyakula huku Namouih akifuata nyuma. Alimwangalia sana Blandina; jinsi alivyokuwa na shauku alipoongea na mwanaume wake huyo mwenye siri nzito ambazo ni Namouih pekee ndiye aliyezifahamu, na hangeweza kujizuia kumwonea fahari rafiki yake kwa sababu ya kujua kiundani aina ya mtu aliyekuwa anatoka naye kimapenzi.

Wakachukua vyakula na kurudi kuketi tena, na wakati huu muziki ulioendelea ulikuwa wa nyoyo, taratibu ili watu wajinome bila kupaliwa. Wakiwa wanakula, Blandina angefanya vitu kama kumlisha Draxton au kumbusu kinywani makusudi kabisa ili mtu yeyote akiwaona ajue kwamba huyo ndiyo alikuwa mwanaume wake, na Namouih akakaa kuzuga kwamba hakuwapa umakini; ila hata yeye aliwatilia maanani sana. Akawa anaangalia jinsi Draxton alivyoonyesha kufurahia sana uhusiano wake na Blandina ingawa kuna mambo mengi yaliyomzuia kumwonyesha rafiki yake mapenzi kwa asilimia zote, na yeye kuelewa hilo kulimfanya apendezwe na Draxton hata zaidi; kwa njia ya upendezi wa kawaida tu.

Watu wengi wakiwa wanaendelea kula huku MC akiwa anashughulika na baadhi ya mambo yenye kuburudisha, Namouih akamwangalia Draxton na kugundua kitu fulani. Alikuwa ameanza kuonyesha hisia fulani hivi usoni ya mtu anayeficha maumivu, naye akakikunja kiganja chake kilichokuwa mezani kwa nguvu sana na kusitisha kuendelea kula. Namouih akaendelea kumtazama kwa umakini, hata Blandina akatambua kwamba mpenzi wake aliacha kula. Akauliza vipi, naye Draxton akasema yuko sawa tu. Blandina akamlisha mpenzi wake kwa mara nyingine tena, naye Draxton akala na kutulia. Lakini Namouih akaendelea kumwangalia na kugundua kwamba alikuwa anajifanya tu kuwa sawa ila bado kuna kitu kilikuwa kinamsumbua. Akaangalia chakula chake akidhani labda alitafuna mboga ya majani lakini hakuwa ameweka majani kwenye chakula chake kabisa.

Ndipo Draxton akamwambia Blandina anaelekea nje mara moja, naye akaenda na kuwaacha marafiki hao sehemu hiyo. Namouih hangeweza kujizuia kuwaza kuhusu hali ya mwanaume huyo, hivyo akaamua kwenda huko aliko ili kuona kama angehitaji msaada na chochote ambacho hangeweza kumwambia Blandina kwa sasa. Akamwambia shoga yake kuwa anaelekea choo cha wanawake, naye akatoka na kwenda moja kwa moja nje ya jengo hilo akimwacha Blandina anachezea simu yake kuperuzi. Namouih alipokuwa anaelekea nje, akasimamishwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa anataka wazungumze kidogo, na baada ya Namouih kumsikiliza na kutambua nia yake ilikuwa kumtongoza, akaachana naye na kumpita ingawa jamaa aliendelea kusisitiza apewe namba.

Akatoka mpaka nje ya ukumbi. Hakumwona Draxton sehemu yalipokuwa yameegeshwa magari yao, hivyo akaamua kutoka mpaka nje ya geti kuangalia kama alikuwa nje ya ukuta wa kuzungukia hapo. Kweli akamwona mwanaume huyo akiwa amesimama usawa wa nguzo moja ya umeme, na hakukuwa na watu wengi zaidi ya mpita njia mmoja mmoja tu eneo hilo kuelekea barabara kuu, ambako ndiyo palionekana kuwa na watu zaidi kuliko hapa.

Namouih akamfata mpaka karibu na kumkuta akijitahidi kupumua kwa utaratibu, naye akamwita kwa sauti ya upole. "Draxton..."

Alikuwa amemwita hivyo kutokea nyuma yake, lakini mwanaume hakuitika wala hakugeuka.

"Nini tatizo? Kuna shida... chakula kimekufanya ujihisi vibaya?" Namouih akauliza kwa kujali.

"La..." Draxton akajibu kwa sauti ya chini huku akiendelea kupumua kwa uzito.

Namouih akamsogelea karibu zaidi na kumshika begani. "Niambie nini kinakusumbua," akasema.

"Anataka kutoka," Draxton akajibu.

Namouih akashangaa na kuutoa mkono wake begani kwa mwanaume huyo. "Sasa hivi? Kwa lazima?" akamuuliza.

Draxton akatikisa kichwa kukubali.

"But... kwa nini... anataka kula au?"

"Sijui. Najaribu... kutafuta utulivu... ila ana-force sana... sidhani kama nitaweza kumzuia... atatoka," Draxton akaongea kwa shida kiasi.

Namouih, akiwa ameingiwa na wasiwasi, akasema, "Okay. Okay aa... unahitaji kumwacha tu atoke kama ambavyo huwa unafanya. Twende urudi kule ujifunge minyororo... au... au... au kwanza tukakutafutie nyama... na sasa hivi tutapata wapi nyama kubwa ni usiku...."

"Namouih... usiongee hivyo. Hautakiwi kuhusika kwa lolote juu ya hili, umenielewa?"

Draxton aliyasema maneno hayo kwa ukali kiasi, kitu kilichofanya Namouih atambue kwamba kweli upande wake mkali ulikuwa umeanza kuvizia kutoka ingawa akili yake kama Draxton bado ilikuwepo.

"Nakuomba urudi ndani, usiseme lolote kwa Blandina... nitampigia," Draxton akasema.

"Lakini Draxton, unahitaji ku...."

Namouih akaishia hapo baada ya Draxton kumwangalia kwa yale macho yake makali, kisha mwanaume huyu akaanza kuelekea upande wa ndani ili achukue gari lake na kuondoka haraka baada ya kushindwa kujipa utulivu. Namouih alibaki kumwangalia tu kwa huruma mpaka alipoliondoa gari lake hapo, kisha yeye akaanza kuelekea ukumbini taratibu huku akimuwaza sana. Hali yake ya kubadilika ilikuwa imekuja ghafla, na kwa kumjua Draxton vizuri, bila shaka alikuwa anajilaumu kwa kuwa sehemu ambayo aliona hakutakiwa kuwa. Mwanamke akaenda mpaka ndani na kumwona Blandina anakuja upande wake wa kutokea, naye akasimama baada ya rafiki yake kumfikia karibu.

"Nam... Draxton ameondoka! Can you believe this?" Blandina akaongea kwa njia ya kulalamika.

"Ameondoka?" Namouih akauliza kwa sauti ya chini.

"Eee... si alisema anatoka nje mara moja? Sa'hivi kanipigia eti anasema kapata dharura kwo' ameenda wapi sijui agh... yaani me hata simwelewi. Dharura gani usiku wa Jumamosi?" Blandina akasema kwa njia ya kuudhika.

"Okay, usijali Blandina... labda kweli amepatwa na dharura. Relax," Namouih akamtuliza.

Blandina akajishika kiunoni tu kuonyesha ameishiwa raha.

"Kuna nini sasa hivi?" Namouih akauliza.

"Humo? Agh, yaani hata sielewi... mood ishakata tayari. Kama vipi niende zangu tu nyumbani kulala," Blandina akasema.

Namouih akawaza jambo fulani, kisha akasema, "Me mwenyewe nimeboeka afu'... nahisi kama kichwa kinauma. Twende tu."

Blandina akatulia kidogo, kisha akasema, "Sawa. Yaani Drax awe amepatwa na dharura ya maana la sivyo nitammeza nikijua ananiletea uzushi."

Namouih akatabasamu tu, naye Blandina akaongoza kutoka nje akifuatwa na rafiki yake.

Wakatembea kuelekea magari yao huku Blandina akimpa Namouih mapendekezo fulani kuhusiana na kazi, nao wakaagana kwa kumbatio na kila mmoja kuingia kwenye gari lake, kisha wakaondoka pia eneo hilo. Blandina alijihisi vibaya kiasi baada ya mpenzi wake kumwacha tu ghafla na kuondoka, naye akawa anatazamia majibu mazuri kutoka kwa mwanaume huyo ili kuhalalisha matendo yake ambayo Blandina aliyaona kuwa ni ukatili wa kihisia. Kwa upande wake Namouih, alielewa wazi kwamba Draxton hakuwa na msaada wowote ule kukabiliana na hali iliyokuwa ikimpata, na aliwaza mengi kuhusu ni nini kingetokea endapo kama mwanaume huyo angechelewa kufika kule msituni na ikatokea amebadilika kabla ya kujifunga minyororo. Alijihisi ni kana kwamba yuko ndani ya sinema fulani hivi, lakini uhalisia wa jambo hili ukamfanya awaze jambo moja tu; kumsaidia Draxton.

Hivyo kuondoka kwa Namouih kwenye sherehe ile haikuwa kwa sababu alitaka kwenda nyumbani kupoza maumivu ya kichwa kwa kupumzika, bali alikuwa amedhamiria kwenda msituni kule ili ampatie mwanaume yule msaada wowote ambao angeweza kumpa. Hiki kilikuwa ni kiwango cha juu sana cha kujali kutoka kwa Namouih, naye akatia mwendo wa gari kasi zaidi ili aweze kumwahi Draxton.

β˜…β˜…

Draxton aliendesha gari upesi kuelekea msituni kule akiwa anachanganywa sana kwa kuona vitu mara mbili-mbili, yaani kwa macho yake na macho ya mnyama wake wa ndani, yaliyokuwa yanaingiliana kadiri alivyoendelea kujizuia ili asibadilike kabla hajafika huko. Alijitahidi sana mpaka akafanikiwa kuifikia nyumba yake ya msituni, lakini hangeweza kwenda ndani kule kubadili nguo kutokana na kutambua kwamba badiliko lake lilikuwa karibu sana. Hivyo akashuka tu kutoka ndani ya gari na kuanza kuelekea sehemu ile yenye minyororo, akiyumba huku na kule lakini akikaza kichwa chake ili afanikiwe kufika. Hakutegemea kabisa kwamba mnyama wake wa ndani angelazimisha kutoka siku hii, kwa sababu mara nyingi kila mara ambapo angebadilika kwa kawaida muda mrefu ungepita kabla ya kuja kubadilika kwa mara nyingine tena, lakini tokea wiki chache nyuma kuna jambo lililokuwa likisababisha hali hiyo iwahi bila yeye kutambua chanzo ni nini.

Akafanikiwa kufika sehemu hiyo akiwa anapumua kwa nguvu sana, jasho likimtoka mwili mzima, na akihisi jinsi mwili ulivyochemka haswa, naye akaanza kuelekea kwenye minyororo ile akijivuta kwa nguvu zake zote kama Draxton. Mnyama wake ni kama alikuwa anamzuia kuifikia minyororo hiyo, na ngozi ya Draxton pamoja na nywele zake zikaanza kubadilika rangi hatimaye, na nywele kurefuka. Lakini akafanikiwa kuifikia minyororo hiyo, naye akaanza kuinyanyua haraka ili aufunge mwili wake. Mwishoni mwa minyororo hiyo kulikuwa na vyuma vilivyozunguka kwa mtindo kama wa pingu lakini zenyewe zikiwa nene na pana zaidi, hivyo kuziingiza kwenye mikono, shingo, na miguu ilikuwa rahisi sana, lakini mara ambapo angebadilika tu, ukubwa wa mnyama huyo ungefanya minyororo imbane na hivyo kumzuia kwenda popote endapo angejaribu kujinasua.

Baada ya kujivalisha hivyo, akaanza kujitahidi kuutafuta utulivu wa kumwacha mnyama atoke, lakini kwa sababu alikuwa amejikaza kwa muda mrefu hiyo ilifanya mnyama huyo atake kutoka kwa nguvu zaidi, kwa hiyo maumivu aliyohisi yakaongezeka na kufanya mwili wake ushindwe kustahimili au kukazia fikira utulivu, na badala yake ukajikaza hata zaidi. Kwa hiyo akawa amepiga magoti huku akiendelea kuhangaika na maumivu yake, akiomba pindi hiyo mbaya iwahi kupita ili asiendelee kuyahisi maumivu hayo makali tena.

Ni ndani ya wakati huo huo ndiyo Namouih alikuwa amefikia eneo hilo la nyumba ya Draxton na kuliona gari lake pale, mlango wa mbele ukiwa wazi kumwambia kwamba mwanaume alikuwa ameshashuka. Akajipa ujasiri na kutoka kwenye la kwake pia, naye akalifata gari la Draxton na kutazama nyumba ile. Palikuwa na giza kweli kweli, mwanga wa taa za gari pekee ndiyo ukimulika eneo hilo la mbele, naye akaanza kuelekea nyuma ya nyumba hiyo huku akimulika kwa tochi ya simu yake. Akaifikia njia ile iliyoelekea sehemu ambayo Draxton angekuwa ameenda kujifungia, na hapa ndipo akaanza kusikia sauti yake kwa mbali.

Ilikuwa sauti ya miguno ya maumivu kutoka kwa Draxton, na hofu ya kujali ni nini kilichokuwa kinampata mwanaume yule ikamsukuma Namouih aanze kwenda ili amwangalie kwa ukaribu. Alikuwa akiweweseka mara kwa mara kutokana na viatu vyake vya kuchuchumia kumpa shida kwenye utembezi wake wa haraka, lakini hakuacha kusonga mbele. Ikiwa angesimama hata mara moja kujiuliza ni kwa nini alikuwa ameacha mambo mengine yote ili tu kuja kwa Draxton, jibu lingemshangaza yeye mwenyewe, lakini fikira zake zilikazia zaidi kwenda tu na kuona kama angeweza kutoa msaada kwa njia yoyote.

Alifika usawa wa mti mmoja na kuanza kuona kitu fulani kwa mbele zaidi kikifurukuta, yaani mwili wa Draxton, ulioonekana kiasi kutokana na kuwa mweupe, na mwili huo kutuna sana ulisababisha nguo alizokuwa amevaa zichanike-chanike. Ingawa mwanamke huyu hakuona mambo mengi vizuri, alijua huyo alikuwa ni Draxton akiwa ndani ya minyororo mizito tayari. Akaamua tu kusimama hapo hapo, mapigo ya moyo wake yakikimbia kwa kasi sasa, naye akaanza kusikia namna Draxton alivyozidi kulia kwa maumivu zaidi, lakini kwa muungurumo. Ndipo sasa Namouih akaanza kuona jinsi mwili wa Draxton ulivyoanza kuwa mweupe, siyo weupe ule wa uzungu, weupe wa rangi nyeupe, kumaanisha manyoya mengi yalikuwa yakienea mwilini mwake na mnyama yule ndiyo alikuwa anatoka. Kadiri manyoya yake yalivyozidi kuonekana ndivyo ukubwa wake ulivyozidi kuongezeka, na ndipo muungurumo mkubwa ukasikika kutoka hapo huku sauti za minyororo ikijigonga kwa nguvu ikiambatana nayo.

Namouih sasa akawa ameshuhudia kwa macho yake mwenyewe jinsi badiliko hilo lilivyokuwa, na kiukweli aliachwa hoi. Ilikuwa ni kitu chenye kustaajabisha sana. Sasa mnyama huyo mwenye kufanana na mbwa-mwitu, mwenye mwili mkubwa na nguvu nyingi sana, akawa anajivuta kwa nguvu na kuishia kujipiga chini tu kutokana na minyororo kumkaza vyema, naye akaendelea kuunguruma kwa hasira. Kisha akatulia, ghafla kabisa. Ikawa ni kama eneo lote halina sauti yoyote ile kabisa. Namouih akaendelea kutazama huko na kuona jinsi lilivyokuwa linazunguka fulani hivi kama kutafuta kitu, taratibu sana, na ndiyo hapa mwanamke huyu akarudiwa na kumbukumbu kwamba hakuwa ameizima tochi ya simu yake mpaka wakati huo. Akaiwasha na kubofya kwenye kioo, kisha akaizima tochi upesi, na alipoangalia kule tena, akakuta mnyama huyo anamtazama yeye moja kwa moja.

Namouih akaushika mti uliokuwa karibu yake na kuuficha mwili wake kiasi, lakini bado akawa anamwangalia machoni tu. Giza hilo lilifanya macho ya mnyama huyo yaonekane vyema kama tu mwili wake mweupe. Hayo macho makali, yenye giza fulani kuyazunguka na lenzi za blue zilizong'aa, yalimtazama Namouih kwa njia iliyomwambia lilikuwa linawaza kitu kimoja tu, yaani kujinasua kutoka kwenye minyororo na kumrarua-rarua. Ingawa alikuwa jasiri vya kutosha kuendelea kusimama hapo, bado alihofia usalama wake pia kwa kuwaza ingekuwa vipi endapo kama lingejaribu kujinasua na kuikata minyororo ile. Ingekuwa ndiyo habari kwisha.

Lakini, mnyama huyo mwenye kutisha akaendelea kumwangalia tu Namouih, bila kuonyesha hasira kama mwanzoni. Hapa ndiyo Namouih akaanza kukumbukia jinsi usiku ule lilivyomkaribia na kutishia kumrarua lakini likaacha tu. Llilikuwa jitu hatari la kinyama, lakini ndani yake alikuwepo mtu mzuri pia aliyehangaika nalo kwa muda mrefu sana. Alikuwa hapo kwa ajili ya huyo mtu na siyo lenyewe, kwa hiyo kwa vyovyote vile asingeondoka hapo. Wakiwa bado wanatazamana, mnyama huyo akaanza kuunguruma tena kwa sauti ya chini, halafu akaanza kupeleka kichwa chake huku na huko kama vile anapatwa na shida fulani hivi. Namouih akajitoa mtini ili amwangalie kwa umakini zaidi, na sasa lilikuwa linaunguruma huku likijigonga-gonga mtini na kupata shida kusimama vizuri. Mwanamke akawa anajiuliza hiyo ilikuwa ina maana gani, kwa sababu alitambua kwamba lilifanya hivyo si kwa hasira za kinyama, bali kuna kitu kingine kilikuwa kinalikorofisha.

Akaendelea kumtazama tu, naye akaona jinsi mwili wa mnyama huyo ulivyoanza kupungua na kupungua kadiri alivyoendelea kujibamiza kwa nguvu na kuunguruma. Namouih akaanza kupiga hatua chache kuelekea mbele, taratibu, akiwa kama vile amepagawa na kusahau hatari iliyokuwa mbele yake. Mnyama huyo akalala chini kabisa na kuendelea kupungua ukubwa, na hatimaye sauti za muungurumo zikaanza kuwa za kibinadamu. Ikaanza kuwa wazi kwa Namouih kwamba Draxton alikuwa anarejea, naye akawasha tochi ya simu yake na kuharakisha pale chini ili amsaidie. Alipofika karibu zaidi, tayari mwili wa Draxton ulikuwa umerudia kawaida yake, isipokuwa nywele zake kuwa nyeupe, ndefu, na laini sana kichwani kwake. Alikuwa akipumua kwa nguvu huku akitoa sauti za kukwaruza, naye Namouih akafika hapo chini na kuukumbatia mwili wake kutokea nyuma. Alimshikilia kwa nguvu huku akijitahidi kumtuliza kwa kufanya "shh," naye Draxton alikuwa anatetemeka huku amefumba macho kwa nguvu. Hali yote hiyo ilimtia Namouih simanzi nyingi, mpaka akaanza kulia. Alimwonea huruma sana.

Akiwa ameendelea kumshikilia namna hiyo, Namouih akatambua kwamba Draxton hakuwa na nguo yoyote kabisa mwilini, hivyo akamwachia kwa ufupi na kuitoa nguo yake ndogo kama ushungi iliyokuwa imefunika sehemu ya kichwa chake kufikia mgongoni, yaani akiikata kabisa kutoka kwenye nguo yake, kisha akaipitisha kwenye sehemu nyeti za Draxton kwa uangalifu ili kumsitiri, na uzuri ni kwamba giza lilisaidia asione utupu wake. Akamfunga vizuri sana, kisha akaanza kuiondoa minyororo ile kutoka mwilini kwa Draxton, halafu akamkaribia usawa wa kichwa na kuanza kumsemesha. Ilikuwa ni kama Draxton hakusikia lolote kwa sababu hakutoa itikio kwa chochote kile kilichosemwa na Namouih, hivyo mwanamke akaamua kumsaidia anyanyuke ili amrudishe kule kwenye nyumba.

Haikuwa rahisi hata kidogo kwa Namouih kufanya hivyo, lakini akakomaa na kukomaa mpaka alipoweza kumpa egamio kwenye mwili wake ili atembee pamoja naye. Draxton alikuwa kama mgonjwa aliyezidiwa, akitembea kilegevu sana na mara kwa mara kufanya wote wadondoke, lakini Namouih hakukata tamaa mpaka alipofanikiwa kumfikisha ndani ya nyumba ile. Mwanamke alikuwa akipumua kwa uchovu kutokana na mwili wa Draxton kuwa imara na wenye uzito, na baada ya kuingia ndani ya nyumba, akampeleka mpaka ndani ya kile chumba kidogo na kumlaza kitandani. Alikuwa akiona vitu kwa msaada wa tochi ya simu yake aliyoishikilia kwa mdomo, lakini sasa akawasha sakiti ndogo ya betri lililozifanya taa zile za bomba zilizogundishwa ukutani ziwake; kwa mianga yenye rangi ya blue na nyeupe iliyofanya papendeze sana.

Akaifata kabati ile yenye droo na kufungua mbili, akachukua taulo baada ya kupata moja, kisha akaitumia kumfungia kuanzia kiunoni kwake na kuuondoa mtandio ule ulioziba sehemu zake za siri. Hakukuwa hata na muda wa kuwaza namna ambavyo Draxton alijengeka vyema kiume; mwanamke akaenda sehemu ya sebule kutafuta maji ili aje kuyatumia kumkanda jamaa kwa kuwa bado mwili wake ulikuwa na joto kali sana. Uzuri ni kwamba Draxton alitunza maji mengi ya kunywa hapo, na Namouih akatoa chupa moja na kurudi kwa mwanaume huyo tena. Akavuta kiti kimoja na kuketi usawa wa kichwa cha Draxton, naye akawa anamimina maji kwenye kitambaa chake kisafi na kumkanda sehemu ya kichwani mpaka kufikia kifuani kwake. Hakujua ikiwa hii ilikuwa na msaada mkubwa lakini alifanya hivyo tu ili kulipunguza joto lake kwa sababu ilikuwa ni kama ana homa kali.

Akawa anaendelea kumfuta taratibu huku Draxton akiwa amefumba macho na kupumua kwa utaratibu sasa. Kuna nyakati ambazo Namouih angemwangalia sana usoni na kutamani afumbue macho ili aweze kumpa pole kwa kilichotokea, lakini muda ukazidi kusonga mbele mpaka pale mwanamke huyu alipozidiwa na usingizi kutokana na uchovu, naye akakilaza kichwa chake pembeni ya kichwa cha Draxton na kuuruhusu usingizi umchukue pia.



β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

e-mail: eltontonny72@gmail.com
 
Mheshimiwa Elton Tonny tuko pamoja kazi nzuri sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sijui next episode itakuwaje kwa Efraim Donald (Jini Makata). Maana kitakachoendelea kati ya Draxton na Namuyi ni lazima jamaa atapata notification. Samahani Wadau kwa huu utabiri wangu feki 🀣🀣🀣
 
CHANGE

Story by Elton Tonny

Urafiki, Familia, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Ukatili, Mauaji, Mambo yasiyotazamiwa, Mambo yenye kuhofisha

R-rated 18+

Enjoy!

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Draxton anafumbua macho yake na kujikuta yupo ndani ya chumba chake kidogo. Kabla hajajiuliza ni jinsi gani alifika hapo, anavuta harufu nzuri sana kwake anayoifahamu vyema, naye anafumba macho kuisikilizia vizuri zaidi. Anafumbua macho yake na kugeuza shingo yake upande mwingine wa kitanda, na hapo anamwona Namouih, akiwa amelaza kichwa chake kitandani karibu kabisa na chake, na akiwa amesinzia kwa kile kilichoonekana kuwa uchovu. Kiganja cha mwanamke huyo bado kilikuwa kimeshika kitambaa chake alichotumia kumkandia, naye Draxton alipojitazama mwilini akaona ni taulo tu ndiyo iliyokuwa imemsitiri.

Akatazama juu tena na kubaki kutafakari vitu. Mwanamke huyu hakutakiwa kuwa hapo. Ni kwa nini alikuwa na king'ang'anizi sana? Na kama ni jambo lingine lililomchanganya ilikuwa ni wakati alioamka. Kwa uzoefu wake alitambua kwamba bado haikuwa imefika alfajiri, ikimaanisha ni muda mfupi tu ulikuwa umepita tokea alipobadilika mpaka kufikia sasa. Ni nini kilichokuwa kimefanya awahi kurudia hali ya kawaida kabla ya asubuhi kufika kabisa? Namouih alikuja huku wakati gani? Maswali hayo kichwani kwake yalimpa wazo fulani, wazo ambalo hakutaka kabisa liwe ndiyo sababu ya haya yote kutokea. Ikamfanya akumbuke vitu vingi mno, naye akaingiwa na simanzi.

Akaanza kusikia sauti za kuguna kutoka kwa Namouih, na alipomtazama akagundua kwamba alikuwa anaota, tena ndoto mbaya maana uso wake ulionyesha kutatizika. Ikambidi Draxton ajinyanyue na kuketi, akihisi maumivu mwilini kama ya mtu aliyeanza kufanya mazoezi ya viungo, naye akaifunga vizuri zaidi taulo kiunoni halafu akarudi kulalia ubavu wake mmoja ili amwamshe mwanamke huyu mrembo kwa ustaarabu. Akawa anapitisha kiganja chake nyuma ya kichwa cha Namouih huku akimpuliza usoni taratibu, na hisia ambayo mwanamke huyu alipata ikaanza kusaidia ndoto imwondoke na yeye kuanza kurejesha ufahamu wake kwa kuamka.

Akafumbua macho taratibu, akiwa bado na kumbukumbu ya ndoto mbaya ya muda mfupi nyuma, lakini hakuhisi msisimko wa hofu. Kufumbua kwake macho kulimkutanisha na uso wenye kujali wa Draxton, na kwa sekunde chache akabaki kumtazama tu kwa umakini. Kwa sasa Draxton alikuwa amerudia hali yake ya kawaida, lakini nywele zake kichwani zilikuwa nyeupe bado na ndefu, zilizofunika pande za kichwa chake kufikia mbele ya paji lake la uso kwa njia fulani utadhani alikuwa amevaa wigi.

Namouih akanyanyua kichwa chake na kufikicha macho yake kisha kuendelea kumtazama, naye Draxton akazirudisha nywele zake nyeupe upande mmoja wa bega ili uso wake uwe wazi zaidi, na wakati huu alikuwa akimwangalia Namouih kwa njia fulani kama anasubiri aseme ni kwa nini alikuwa sehemu hiyo kwa wakati huo.

"Umeamka zamani?" Namouih akauliza kwa sauti ya chini.

Draxton akabaki kumtazama tu.

Namouih akachukua simu yake pembeni kuangalia muda, naye akakuta ni saa tisa usiku. Akamtazama Draxton tena. Yaani alionekana kama mvulana mdogo usoni kwa jinsi ambavyo nywele zake zilipendezesha kichwa chake, na Namouih alielewa kwamba bila shaka zingehitaji kunyolewa baadaye.

"Mbona unaniangalia hivyo?" Namouih akauliza baada ya kuona amekaziwa macho tu.

"Nilikwambia nini Namouih? Na wewe umefanya nini?" Draxton akauliza.

"Hiyo ndiyo asante ya kukutoa msituni usiku ukiwa uchi?"

"Sikuhitaji msaada wako. Namouih... inapokuja kwenye suala hili nakuomba ukae mbali na mimi. Unajihatarisha bila sababu yoyote ile ili iweje? Kuonyesha kwamba unanijali sana au?"

"Kwani ni dhambi kukujali?"

"Uliniambia nibaki nikusaidie... masuala mengine yaache kama yalivyo, nitadili nayo mwenyewe. Kaa mbali na mimi Namouih!"

"Kwa nini unakuwa mkali? Shida ni nini Draxton?"

"Shida ni kwamba...."

Draxton akaishia hapo na kubaki amemwangalia tu mwanamke huyo machoni. Namouih aliweza kutambua kwamba kuna kitu kilichokuwa kinamfanya mwanaume huyu aogope sana kumuumiza, kumaanisha alimjali pia, lakini akawa anataka kujua hicho kitu ni nini hasa.

"Niambie. Nielezee ni kwa nini hutaki niwe karibu yako kukusaidia hata ingawa... hata ingawa ninajua hautaniumiza," Namouih akasema.

"Usiwe na uhakika kwamba sitakuumiza Namouih, ni kwamba bado tu sijakuumiza, na wewe unavyoendelea kujisogeza kwangu ndiyo unalikaribisha hilo," Draxton akamwambia.

"Ni nini kilitokea Draxton?" Namouih akauliza kwa upole.

Draxton akabaki tu kimya.

"Niambie... tafadhali... ninataka kukuelewa vizuri zaidi Draxton..."

Draxton akajivuta kutoka kitandani huku akisema, "Hautakiwi kuelewa lolote... na ilikuwa makosa mimi kubaki huku."

Akazifata droo na kutoa T-shirt moja nyeusi ili avae.

Namouih akanyanyuka kutoka kwenye kiti na kumsogelea huku akisema, "Draxton usiseme hivyo. Niambie tafadhali. Huu woga wako wa kuniumiza unatokana na ile kauli kwamba sikuzote ni lazima tatizo litatokea ukianza kumjali sana mtu, si ndiyo? Lakini haliwezi kutokea endapo kama huyo mtu hajui kuhusu siri yako, na kwa hii instance ni mimi ndiyo ninayejua na si Blandina. Kinachofanya ufikiri utaniumiza ni kwamba nimeendelea kujiweka karibu nawe, lakini mbona hata ulipokuwa umegeuka kuwa mnyama mara ya kwanza nakuona vile haukuniumiza? Kuna jambo lingine Draxton... jambo lingine linalokusumbua. Na nafikiri ni kwa sababu yangu. Tafadhali niambie..."

Namouih aliongea kwa hisia sana. Draxton akawa anamwangalia tu kwa umakini huku mwanamke huyo akionyesha hamu ya kutaka kujua ukweli.

"Niambie. Ni kwamba... unanijali mimi zaidi hata ya unavyomjali Blandina?" Namouih akauliza swali hilo moja kwa moja kabisa kuonyesha ni jambo alilokuwa ameshafikiria mapema.

Draxton akamwangalia kwa umakini sana, akiona hapa hakukuwa na haja tena ya kumficha mwanamke huyu ukweli. Akavaa T-shirt yake na kuangalia chini kwa sekunde chache, kisha akatikisa kichwa chake kukubali na kusema, "Ndiyo... uko sahihi. Lakini siyo MIMI."

Jibu hilo likamchanganya Namouih kiasi. "Unamaanisha nini?" akamuuliza.

"Ni upande wangu wa pili ndiyo unakujali namna hiyo Namouih," Draxton akasema.

"Excuse me?!" Namouih akashangaa.

Draxton akaifunga droo taratibu huku akionekana kuingiwa na huzuni. Pamoja na kwamba jambo hilo lilimshangaza, Namouih alijua kulikuwa na kisa cha kina zaidi kilichofanya liwe baya kwa mwanaume huyu, naye akamshika mkononi taratibu.

"Draxton... nieleweshe. Hilo linawezekanaje? Yaani... huyo mnyama ana hisia kwangu?" Namouih akauliza.

"Ni jambo gumu lakini... huwa inatokea... imeshatokea," Draxton akamwambia.

Namouih akaendelea kumwangalia kwa umakini, naye Draxton akaegamia kabati yake ya droo huku akionekana kuwa na simanzi usoni.

"Ilianza na mama. Mama yangu... mama yangu ndiyo pekee aliyeweza kuzoeana na huu upande wa pili kwa sababu nilikua nikiwa naye kwa miaka mingi... kwa hiyo upande huu ukajifunza kumjali pia... kama tu mnyama wa kufugwa. Kuna vitu nilikuwa navitamani maishani hasa kama kijana, niwe natembea, niwe na marafiki, michezo, kwenda shule pamoja na wengine... na hata kuwa na girlfriend pia..."

Draxton akasema hayo na kutabasamu kidogo, naye Namouih akatabasamu pia lakini kwa njia ya huruma.

Draxton akaendelea kusema, "Ilikuwa ngumu sana kwangu kuishi kwa kujificha, nilijiona kama mfungwa ingawa nilikuwa na company yake, na kwa sababu ya kutoridhika nikajaribu kutoka nje siku moja ili nikajifurahishe... nikajichanganye na watu yaani.... ikaanza kuwa zoea. Muda si muda nikawa simsikilizi mama kwa kujiona nina control nzuri.... usiku mmoja nikaondoka tulipokuwa tunaishi na kwenda mbali sana bila kumwambia chochote. Nilikoenda.... nilipoteza control na kuua watu 26 Namouih... watu 26!"

Namouih akatikisa kichwa kwa kusikitika.

"Vifo vya watu wengi namna hiyo... sababu ikiwa ni mnyama mkali, oh labda ametoroka zoo, labda kaingia town kutoka milimani, hivyo ndivyo wengi walivyowaza lakini hawakuweza kumpata huyo mnyama kwa sababu haikuwa mnyama kwa asilimia zote. Ilikuwa ni mimi. Mimi ndiyo niliyewaua..."

"Hapana Draxton, usiseme hivyo..."

"Kama tu ningebaki ndani... na mama yangu... nisingeamka sehemu ya mbali nikiwa na damu za watu midomoni mwangu..."

Namouih akafumba macho na kuinamisha uso chini.

Draxton akavuta pumzi na kuishusha kwa nguvu, kisha akaendelea kusema, "Kwa hiyo... ikiwa kama muujiza tu kwamba sikukamatwa, nikarudi kwa mama... muuaji. Haijapita muda mrefu nikagundua kwamba alikuwa na cancer kwenye ini... stage 4... na hakukuwa na njia yoyote ya kumwokoa tena maana hata hospitali alizojaribu kuulizia uwezekano wa transplant kwa hali yake ilishindikana. Sikutaka aniache, lakini akaniacha. Mtu pekee aliyeweza kunitunza vizuri nikiwa na hali yangu akaniacha. Hata damu yangu haikuweza kumsaidia. Sikutaka kuendelea kuishi tena. Nilijaribu kujiua mara nyingi, na kila mara upande wangu wa pili ulipotoka kwa sababu ya mimi kufanya hivyo ningesababisha vifo. Haikuwa rahisi kunitia hatiani kwa sababu kilichofatiliwa ilikuwa ni mnyama na siyo mtu ambaye wangekuja kukuta amelala tu barabarani. Katika kufanya hayo yote nilikuwa navunja ahadi ambayo nilimpa mama kabla haja.... nilimwambia ningeendelea kuishi kwa siri na kujitahidi nisimuumize yeyote, lakini nikaivunja!"

Draxton akiwa anasema "nikaivunja" alikuwa anajipiga kwa nguvu kichwani, naye Namouih akaushika mkono wake ili kumzuia. Mwanamke akaendelea kumtazama kwa hisia sana, akielewa kwamba bado kuna mengi aliyotakiwa kujua.

"Kila sehemu niliyokwenda... yaani... ikawa wazi kwangu kwamba hakuna kitu ambacho kingeweza kuniondoa duniani, na sikutakiwa kujipeleka kwa watu kwa sababu only God knows wangeitumia vipi damu yangu ikiwa ningejionyesha kwao. Mama alikuwa ameniambia niendelee kutafuta sababu ya kuishi hata kama nitabaki kuwa mwenyewe... kwamba ipo sehemu fulani inanisubiri... na baada ya muda fulani Namouih... niliipata. Niliipata nilipokwenda Venezuela. Nilikutana na mwanamke mwenye moyo mzuri sana. Na ilikuwa kwa bahati mbaya tu lakini nilimpenda. Nilimpenda sana. Ila kilichokuja kunifanya nitambue kwa nini nilimpenda sana ni kujua kwamba upande wangu wa pili ulimpenda pia. Ulimpenda the same way kama ulivyokuwa unampenda mama, kwa hiyo mbele yake... upande wangu wa pili ungekuwa dhaifu. Ah... Namouih sijui hata ikiwa unaelewa nayokwambia...."

"Ndiyo naelewa Draxton... tafadhali endelea..." Namouih akasema kwa hisia sana.

"Angalau kufikia wakati huo niliweza kujichanganya na watu, na nilikuwa nimeanza kuzoea tabia za upande wangu wa pili kwa hiyo niliweza kuwa mwangalifu. Vitu, au tabia za watu zingeonekana kuwa kawaida kwangu, lakini ilipokuja kwa Ramona, kila kitu kumhusu kilikuwa kizuri kupitiliza. Aliitwa Ramona... alikuwa... special. Na yeye alikuja kugundua kuhusu hali yangu lakini sikumuumiza kama nilivyohofia. Alikuwa tayari kuwa nami licha ya hilo, na alinisaidia sana kila mara ambapo ningebadilika ili watu wengine wasijue. Alikuja kufikiri kwamba ningeweza.... kulala naye bila kumuumiza, akiniambia imani yake kwangu ina nguvu nyingi itakayonisaidia kuweza ku-experience jambo hilo zuri kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu... lakini nilijua wazi hilo lisingewezekana. Nilimwambia sana tusifanye hivyo lakini akanitia moyo kwamba angeweza kunisaidia.... Namouih... nilimuua kwa sababu ya jambo hilo... nilimtafuna Ramona, Namouih!" Draxton akasema hayo huku machozi yakijaa machoni mwake.

Namouih sasa akawa ameelewa. Kumbe hiki ndiyo kitu ambacho huu muda wote kimekuwa sababu kuu ya mwanaume huyu kujichukia sana na kuogopa kumuumiza Blandina. Bila shaka alikuwa akimaanisha kwamba katika harakati ya kutaka kupeana mapenzi na mwanamke, ilikuwa ngumu kwake kuziongoza hisia za upande wa pili endapo kama ungetoka jambo hilo likiwa linaendelea. Ndiyo kitu ambacho kilimfanya amkimbie Blandina mara ya kwanza na kuendelea kumkatalia kushiriki naye mapenzi. Hilo Namouih alilielewa. Lakini ikiwa Draxton alikuwa anampenda Blandina, ni kwa nini upande wa pili wa mwanaume huyo umjali yeye Namouih zaidi badala ya rafiki yake?

"Draxton.... I am so sorry. Pole sana kwa kupitia mambo mengi magumu mno," Namouih akamwambia huku sasa akimshika begani.

"Blandina ni mwanamke mzuri Namouih. Ananipenda sana bila kujua mimi ni nini, na ninakuwa mnafiki kwake kwa kuendelea na uhusiano wetu bila kumwonyesha upendo namna anavyostahili. Naogopa kwamba itafikia wakati nitapaswa kumwambia ukweli, na kwa jinsi alivyo, yeye pia anaweza kufikiri kwamba ataweza kunisaidia. Sitaki kurudia historia Namouih. Roho huwa inaniuma sana... tokea Ramona, sijawa na mwanamke mwingine kwa sababu hiyo. Lakini bado natumaini labda maneno ya mama kuhusu kuwepo kwa sababu ya mimi kuendelea kuishi ni kweli, ndiyo maana najipa nafasi kwa Blandina. Ila... kila nikifikiria kujaribu... naogopa Namouih... nitamuumiza...."

Namouih akaangalia chini kwa huzuni.

"Ni suala la mimi kutoweza kuji-control vizuri inapokuja kwa Blandina. Nimempenda yeye... lakini upande wangu wa pili umekupenda wewe. Nahofia naweza kuja kukosa control mbele yako, na upande wangu mbaya ukikushika Namouih... hautakuachia," Draxton akasema.

"Ahh... sielewi Draxton. Unasema upande wako wa pili umenipenda, halafu utaniumiza? Ikiwa hilo jitu liliweza kumzoea mama yako, basi hata na mimi...."

"La Namouih, mambo hayako hivyo. Mama iliwezekana vile kwa sababu alikuwa nami toka nipo mdogo. Hata Ramona nilikaa naye kwa miaka kadhaa, na ndicho kilichonifanya nidhani kwamba ningeweza kuji-control... au labda upande huu wa pili. Ila sikufikia hata hatua ya kuwa mnyama kikamili na nikamuumiza... nikampoteza milele kwa sababu ya imani yake kwangu. Jinsi unavyonionyesha kuniamini ni kama Ramona tu. Na jinsi unavyoendelea kujiweka karibu yangu ndiyo unafanya upande wangu wa pili uvutwe nawe hata zaidi, na hilo linaniathiri mimi pia. Sijui kama unaelewa uzito wa hili jambo Namouih?"

Namouih akaendelea kumwangalia tu usoni kwa hisia.

"Nathamini sana jinsi unavyoonyesha kunijali, lakini unajiweka hatarini. Wewe ni mke wa mtu Namouih, na mawazo yangu ya upande wa pili kukuelekea hayafai. Kila mara nikivuta harufu yako...." Draxton akaishia hapo tu na kubaki amemwangalia.

Namouih, akiwa amekwishaelewa kila kitu kwa asilimia zote sasa, akainamisha uso wake na kufumba macho kwa huzuni.

Draxton akasimama vizuri na kufungua droo nyingine, na mkono wa Namouih uliokuwa bagani kwake ukashuka. Mwanaume akatoa bukta ndogo ya samawati na kuifunga droo tena, kisha akainama na kuvuta boksi lile kubwa pembeni ya kabati hiyo, na humo akatoa blanketi kubwa lenye rangi mbili mchanganyiko wa pink na maziwa (cream), naye akakisogelea kitanda na kuanza kukivalisha vizuri blanketi hilo. Namouih alikuwa akimwangalia tu sasa, kwa hisia sana, kwa sababu kisa chote cha mwanaume huyo kilijaa magumu mengi mno yaliyofanya atie huruma kuwa mtu aliyeyapitia. Fikira za kufanya lolote ili kumsaidia alikuwa nazo bado, lakini baada ya kujua haya yote sasa angemsaidia vipi? Ikaonekana kwamba kweli msaada wa kumpatia mwanaume huyu ilikuwa ni kukaa mbali naye, kwa sababu Draxton hakutaka kujipa sababu nyingine ya kuwa na hatia kwa makosa ambayo angeyafanya bila kudhamiria.

Draxton sasa akawa amemaliza kulitandika blanketi kitandani, naye akachukua shuka lingine jepesi na jeupe, kisha akamwangalia Namouih na kukuta bado anamtazama sana.

"Nashukuru kwa kuja kunisaidia... na... samahani kwa kusema baadhi ya vitu kwa ukali. Ni ngumu kiasi kukwambia nachotaka na wakati huo huo akili yangu ikipingana nami..." Draxton akaongea hivyo na kutabasamu kwa mbali, akiwa anajaribu kutania yaani.

Namouih akaanza kulengwa na machozi bila hata yeye mwenyewe kuelewa ni kwa nini.

"Tafadhali nakuomba urudi kulala. Me nitalala huku kwenye sofa. Hilo saa moja au mawili yaliyobaki kwa ajili ya kupumzika yatasaidia kukupa nguvu kukikucha. Natumaini tu niliyosema hayatakufanya uote ndoto mbaya tena..." Draxton akawa amejaribu kuongea kwa njia ya utani tena, naye Namouih akaangalia chini tu kwa huzuni.

Mwanaume akainama na kuvuta droo ya chini kabisa, kisha akatoa kiboksi kidogo chenye mashine ya kunyoa nywele na kuibeba na ile bukta, halafu akafunga droo kwa mguu wake na kuliweka shuka lile kwenye kitanda hapo kisha kutoka ndani ya chumba hicho hatimaye. Namouih akatikisa kichwa chake kwa kusikitika sana na kuketi kitandani kama amejitupia kwa nguvu. Akawa anatafakari kila kitu alichoambiwa, na kiukweli kuna sehemu fulani ndani ya moyo wake iliyotamani sana kuweza kufanya jambo fulani ili kumsaidia hasa kwa sababu alimjali zaidi baada ya kumwelewa kwa kina. Akawaza sijui ingekuwa busara kumwambia Blandina? Lakini hapana, kwa sababu ni kitu ambacho Draxton hakutaka.

Akajilaza tu kitandani na kuendelea kuwaza na kuwazua kuhusu njia ya kumsaidia mwanaume huyo mpaka usingizi ulipomchukua kwa mara nyingine tena. Kwa upande wake Draxton, yeye hangeweza kupata usingizi kabisa baada ya jambo lililokuwa limempata usiku huo, hivyo aliendelea tu kukaa kwenye sofa akitafakari vitu vingi sana hasa baada ya kukumbuka mambo mengi yenye kuumiza aliyopitia kwenye maisha yake.


β˜…β˜…β˜…


Namouih alikuja kufumbua macho yake muda fulani baada ya kusinzia kitandani pale, na kulikuwa na sauti ya kelele nzito kutokea juu ya nyumba hii iliyomwambia kwamba mvua ilikuwa inanyesha. Draxton alikuwa ameitengeneza vizuri sana sehemu hii kwa sababu hakuna hata tone moja la maji lililopita ndani, naye Namouih akajinyanyua taratibu na kuichukua simu yake. Bado alikuwa na wenge zito la usingizi, hivyo akafikicha macho yake na kutazama saa kukuta ni saa mbili ya saa tatu asubuhi.

Mvua hiyo ilisikika kwa nguvu sana kumaanisha ilikuwa kubwa mno, hata sauti za radi nzito zilisikika, naye Namouih akajitoa kitandani na kuanza kuuelekea mlango. Wakati huu hakuwa na viatu miguuni, hivyo akatembea taratibu na kuifikia kingo ya mlango na kuchungulia sehemu ya sebule ile ndogo. Macho yake yakatulia sehemu moja tu, na hapo ilikuwa ni mlangoni kuingilia ndani ya nyumba hiyo, ambapo Draxton alikuwa amesimama kwa kuegamia. Mwanaume huyo alionekana kwa nyuma, akiwa amevaa T-shirt yake nyeusi na bukta ile ya samawati, na kichwa chake sasa hakikuwa na nywele zile nyeupe kumaanisha alizinyoa na kupaka dawa nyeusi kichwani kwenye nywele ndogo alizobakiza.

Namouih akaendelea kumwangalia tu kwa umakini, akiwa anakumbuka vyema mambo yote aliyoambiwa masaa kadhaa nyuma, naye akatoka sehemu hiyo na kuanza kumfata taratibu. Aligundua haraka kwamba bila shaka Draxton alivuta harufu yake kwa kuwa mwanaume huyo aliacha kuegamia sehemu hiyo na kugeuka nyuma kumtazama. Namouih akasimama kiufupi na kuangaliana naye machoni, na ulikuwa ni utizami uliobeba hisia nyingi sana kutoka kwa wawili hawa, kisha mwanaume huyo akarudi kutazama tu nje. Mwanamke akaendelea kumfata taratibu na kufika usawa wake, kisha naye akasimama kwenye kingo ya mlango akitazama nje.

Maji mengi yalionekana kuelekea upande mmoja wa msitu, na Namouih akatambua kwamba gari lake lilikuwa limeacha kutoa mwanga wa mbele, ikimaanisha ni Draxton ndiye aliyekwenda kuzizima muda fulani nyuma. Maji ya mvua hayakuwafikia hata tone kwa upande huo wa mbele kwa sababu nyumba ilijengewa kama dari la mbao zililoziba upande wa mbele kwa kutokeza sana, kama kofia kichwani inavyoziba uso kwa mbele. Hakukuwa na neno hata moja lililosemwa kutoka kwa wawili hawa, na mara kwa mara Namouih angemwangalia Draxton kwa jicho la chini, lakini hakukuwa na chochote kilichotendwa na wanasheria hawa.

Ndipo Namouih akaanza kukisogeza kiganja chake taratibu kuelekea mkono wa Draxton, na kidole chake kidogo kikagusa kidole kidogo cha Draxton pia. Macho ya Draxton yakashuka chini kidogo, lakini hakuitazama mikono yao kabisa. Namouih hakusita kuendeleza jambo hilo, kwa sababu akakiingiza kabisa kidole chake kidogo kwenye kidole hicho cha Draxton na kuvifunganisha, kitu kilichofanya Draxton amtazame usoni taratibu. Namouih akamwangalia pia, sura yake ikionyesha hisia sana, naye Draxton akakaza macho yake kiasi; kama anamuuliza kitu fulani. Namouih akaendelea tu kumwangalia, ikiwa kama anamwambia jambo fulani bila kunena, naye Draxton akawa amemwelewa.

Mwanaume huyu akaendelea kumwangalia kama vile haamini kabisa mawazo ya mwanamke huyu, naye Namouih akaviingiza vidole vyake zaidi kwenye kiganja cha Draxton huku mapigo yake ya moyo yakikimbia kwa kasi sasa. Draxton akatikisa kichwa kwa njia ya kuonyesha kwamba kile ambacho Namouih alikuwa anafikiria hakikuwa sahihi, na jambo hilo lilimshtua sana. Lakini Namouih akamgeukia vizuri zaidi, kisha akaanza kumsogelea huku akimwangalia kwa hisia sana, naye Draxton akafumba macho yake na kuinamisha uso wake baada ya harufu nzuri ya mwanamke huyo kumwingia vyema puani kwa ukaribu huo.

Kuna sababu fulani kwa wakati huu iliyomfanya Namouih apende sana kumwona Draxton akifanya hivyo tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, na ilikuwa kwa sababu sasa alimwelewa vizuri zaidi. Hakujua ni nini tu kilichokuwa kinamsukuma kufanya kitendo hiki lakini alikuwa ameridhia kwa asilimia zote kujiweka karibu zaidi na Draxton, na kiukweli, alikuwa anaogopa. Lakini bado akawa anataka kuizima hofu yake, hofu ya mawazo ya vitu vibaya ambavyo vingeweza kumpata, kwa kuwa hii haikuwa kwa sababu tu alitaka "kumsaidia" Draxton, bali ni kwa sababu alitaka KUWA na Draxton.

Mwanamke huyu akaushika uso wa Draxton kwa kiganja chake kingine, naye Draxton akawa ameinamisha uso wake bado na kusema, "Namouih.... nini unafanya?"

Ilikuwa ngumu kiasi kusikia alichosema kutokana na sauti kubwa ya mvua, lakini Namouih alielewa kile ambacho mwanaume huyo aliongea. Akaunyanyua uso wa Draxton ili watazamane, na kwa ukaribu huo Namouih alipendezwa sana na macho ya Draxton. Hakuwahi kuyaangalia vizuri sana lakini wakati huu aliweza kuona jinsi yalivyokuwa mazuri mno.

"Sijui ninachotaka kufanya... lakini moyo wangu unataka nikifanye," Namouih akasema kwa hisia.

Draxton akaanza kutikisa kichwa chake kukataa. "Hukuelewa chochote kati ya mambo niliyokwambia? Namouih... nakuomba... nakuomba ukae mbali na...."

"Hapana.... sitafanya hivyo," Namouih akamkatisha.

Draxton akaushika mkono wake na kuutoa usoni kwake, kisha akasema, "Usinifanye nijute kukujua Namouih."

Namouih akatabasamu kwa hisia, kisha akamwambia, "Najua Draxton. Lakini bado sitaondoka upande wako. Nimekuelewa vizuri sasa. Nafikiri najua jinsi ya kukusaidia."

"Sitaki uni.... si... sitaki unisaidie... kaa mbali na...."

"Kilichompata Ramona ilikuwa ni kwa sababu aliweka imani kwako tu!" Namouih akasema kwa hisia.

"Unamaanisha nini?"

"Hhh... aliweka imani kwako tu Draxton... kwamba hautamuumiza... lakini hakukufundisha namna ulivyopaswa kumwamini YEYE... ndiyo sababu imani yake kwako ikamfanya adhani ungeweza kila kitu mwenyewe hata ulipoanza kubadilika...."

"Unaweza vipi kuongea namna hiyo kama vile ulimwona... au kumjua?"

"Mimi ni mwanamke Draxton, lakini pia nimekuelewa kwa njia tofauti. Sitafanya hivi ili kukusaidia tu... ni ili na mimi unisaidie pia," Namouih akamwambia.

"Sielewi chochote unachojaribu ku... aagh!" Draxton akasema hivyo na kuonyesha kama anaumia kichwa.

"Nini Draxton?" Namouih akauliza kwa kujali.

"Naomba uende chumbani Namouih... kaa mbali na mimi..." Draxton akasema hivyo na kuanza kumsukuma taratibu kwa mkono mmoja.

"Draxton.... mwachie..." Namouih akasema.

"Nini?"

"Let him come out," Namouih akasema.

"Namouih!" Draxton akashangaa.

"Please nakuomba uniamini...." Namouih akasema.

Draxton akaonyesha kukasirika na kuamua kwenda chumbani ili ajifungie huko kutafuta utulivu. Hisia zake kumwelekea Namouih zilikuwa zinalazimisha kutoka kwa njia ambayo alijua ingesababisha atende vibaya, hivyo akaona kumwepuka ndiyo suluhisho zuri kwa sababu hakuelewa hata mwanamke huyo alikuwa anatoa wapi mawazo hayo. Alikuwa ameanza kuelekea upande ule wa chumba lakini mkono wake ukashikwa na Namouih, aliyekuwa amemfata na kumfanya Draxton amgeukie.

"Draxton please nisikilize...."

"Namouih this is wrong. Siwezi kufanya hivi, mbali na hii kuwa jambo baya na kukuumiza, ninaweza kusababisha uka...."

Draxton akaishia hapo na kubaki amemwangalia mwanamke huyo machoni. Namouih akaendelea kumwangalia pia kwa hisia, na ikawa kama vile Draxton anatafakari kitu fulani. Namouih akasogea karibu yake kidogo na ile anataka kusema kitu fulani, Draxton akamvuta ghafla na kuubana mwili wake kwake kwa nguvu, kisha akaanza kumpiga busu mdomoni moja kwa moja!

Ingawa Namouih alikuwa ameshtushwa kiasi na jambo hilo, akafumba macho taratibu na kuanza kuisikilizia vizuri busu hii kutoka kwa mwanaume huyo kwa sababu ilifanya hamu yake ya kimahaba ipande sana. Draxton akaunyonya mdomo wake kama mara tano kwa namna hiyo huku Namouih akiwa amelegea kiasi kwa nyuma, kisha akajitoa mdomoni mwake na kumwangalia machoni. Alikuwa amekishika kichwa cha Namouih kwa nyuma na kiuno chake, akiwa amemshikilia kama vile anataka kumbatiza kwenye maji mengi, kisha akamwambia....

"I love you."

Maneno hayo yalimfanya Namouih amwangalie kama amezubaa kiasi kwa sababu yalikuja ghafla sana bila matarajio yoyote kabisa, kisha Draxton akaanza tena kumbusu kimahaba mwanamke huyu. Wakati huu alimbusu taratibu na kwa hisia sana, naye Namouih akawa anarudisha busu hiyo kwa kuonyesha hamu kubwa pia. Akainyonya midomo yake huku sasa Namouih akianza kusimama wima, naye akawa analishika kalio lake na kuliminya kwa nguvu, kitu kilichofanya Namouih aanze kuguna ndani ya mdomo wake katikati ya busu yao tamu. Halafu Draxton akamgeuza, na sasa Namouih akiwa amempa mgongo kwa ukaribu, jamaa akaanza kuibusu shingo yake kwa nyuma huku mikono yake akiitumia kuyasugua matiti ya Namouih ndani ya nguo aliyokuwa amevaa, na mwanamke huyu akawa amefumba macho huku ameachama mdomo wake na kupumua kijuu-juu.

Baada ya sekunde hizo chache za kupandishiana hamu, Draxton akamwachia na kurudi nyuma kabisa, naye Namouih akamgeukia na kumwangalia machoni kimaswali kiasi. Draxton alionekana kupumua kwa nguvu sana, naye akausogelea ukuta wa hapo na kuuegamia huku akiendelea kupumua kwa nguvu, na Namouih akamfata taratibu na kumshika shingoni kwa mikono yake. Ilikuwa ya moto kweli, lakini Namouih hakuitoa mikono yake hapo.

"Draxton.... mwachie..." Namouih akasema.

Draxton akatikisa kichwa kukataa huku ameinamisha uso wake.

Namouih, akimwangalia kwa hisia sana, akaita kwa sauti ya chini, "Max..."

Draxton akanyanyua uso wake na kumtazama machoni kwa mkazo.

"Mwachie..." Namouih akasema hivyo na kupitisha viganja vyake mashavuni kwa mwanaume huyu.

Draxton alikuwa akiendelea kumtazama sana, huku bado akijitahidi kujikaza, na ni jambo moja tu lililokuwa limeteka hisia zake. Ilikuwa ni kitendo cha Namouih kumwita "Max" ndiyo kilichomfanya ahisi ni kama ana ukaribu mkuu sana na mwanamke huyu, kama jinsi ilivyokuwa kwa mama yake tu. Hakuna yeyote aliyemwita hivyo kwa kipindi kirefu sana. Bado alikuwa anaona mambo kama Draxton lakini nguvu zake zilikuwa zinatoka kwa njia ya mnyama mkali, kwa hiyo alikuwa anahofia kumuumiza Namouih. Alielewa kwamba mwanamke huyu alichotaka ilikuwa yeye kutojikaza, na kwa sababu ya kuhisi udhaifu fulani hivi mbele ya Namouih, Draxton akaamua kujiachia. Akafumba macho huku akiendelea kupumua kwa nguvu kiasi, na viganja vya Namouih bado vikiwa vimeushikilia uso wake huku mwanamke huyo akimwangalia kwa hisia sana.

Ndipo nywele za Draxton zikaanza kuota taratibu kichwani kwake, zikirefuka na kuanza kubadilika rangi, naye Namouih akawa anamtazama kwa umakini. Draxton akafumbua macho yake ghafla na kumtazama Namouih, na mwanamke huyu akaingiwa na msisimko wa kushtuka kiasi kwa sababu yalikuwa yale macho ya blue yenye kutisha. Lakini Namouih hakuuachia uso wa mwanaume huyo, ambaye sasa alikuwa anapumua kwa njia fulani ya hasira, na ngozi yake ikaanza kuwa nyeupe. Lengo la Namouih lilikuwa kuhakikisha Draxton hapitilizi, na kama alivyomwambia muda mfupi nyuma, angeweza kufanya hivyo kwa kumfundisha Draxton jinsi ya kumwamini yeye Namouih, siyo tu Namouih kumwamini Draxton. Hiyo ilimaanisha nini? Ampe mapenzi kwa njia ambayo hakuwahi kumpa mwanaume yeyote kabla!




β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…

ITAENDELEA

β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…β˜…


Usikose sehemu za mwendelezo wa hadithi hii kali ya CHANGE. Ni story nzuri na ndefu sana. Waweza ipata nakala yote kwa gharama nafuu sana. Karibu WhatsApp au kwa E-mail yangu.

WhatsApp no: +255 678 017 280

eltontonny72@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…