Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nora akawa amemaliza kuongea na aliyempigia na kurudi usawa wa Lexi. Alikuwa anataka amsemeshe jambo fulani, lakini akasitisha baada ya kuona Lexi alikuwa anadondosha chozi. Akamwangalia na Valentina, ambaye alikuwa anadondosha machozi pia huku Alexa akimuuliza nini tatizo.

"Lexi... what's wrong?" Nora akamuuliza.

Lexi akajifuta chozi haraka.

"Hamna kitu. Niko sawa," Lexi akajibu.

Valentina pia akajifuta machozi na kumwambia binti yake alikuwa sawa, naye akaendelea kumtazama Lexi. Nora alikuwa anawaangalia wawili hawa kimaswali sana.

"Mnafahamiana?" Nora akauliza.

"Ndiyo ni... rafiki yangu wa zamani. Ni kitambo sana. Sikudhani ningekuja kumwona... tena," Lexi akamwambia.

"Ooh... sawa. Habari yako dada? Naitwa Nora," Nora akamsalimu Valentina.

"Ah... safi. Naitwa Va..Valentina," yeye pia akajitambulisha huku bado akimtazama Lexi.

"Lexi... kuna dharura imetokea. Mdogo wangu... nahitaji kwenda kumwona ila..."

"Usijali Nora. Wewe nenda tu," Lexi akamwambia.

"Lakini vipi kuhusu..." Nora akauliza huku akiangalia vitu walivyonunua.

"Usijali. Nitavipeleka kwa apartment yako. Sijui kama funguo una..."

"Oh, no, tunaacha. Nitawapigia kuwajulisha unazichukua. Asante, ngoja niwahi. Nita... nitakukuta siyo?" Nora akaongea haraka.

"Yeah... utanikuta," Lexi akamwambia huku akimtazama Valentina.

Nora akamwangalia kwa ufupi Valentina, kisha akawaaga kwa pamoja na kuondoka.

Kwa kuwa walitumia gari la Lexi kwenye matembezi yao, Nora akalichukua ili kwenda alikokuwa mdogo wake, naye Lexi angechukua taxi ili impeleke hotelini kwa Nora baadae. Lexi na Valentina wakabaki hapo wakiwa wanatazamana kwa hisia sana. Kisha Lexi akakusanya vitu vyake vilivyowekwa kwenye mifuko sasa na kusogea pembeni bila kumsemesha Valentina lolote. Alexa akawa anamwambia mama yake manano mengi kama 'huyu si ndiyo yule uliyenionyesha kwenye picha' na 'si ulisema amekufa,' naye Valentina akawa hawezi kujibu lolote lile na kubaki kumwangalia tu mtu aliyedhani kweli alikufa.

Lexi akamwonyesha Valentina ishara ya kichwa kuwa amfate, kisha akaanza kuondoka hapo bila kusema lolote. Valentina akajituliza na kumshika mkono mwanae, nao wakaenda sehemu ambayo aliacha kifaa cha kubebea vitu alivyonunua na kuanza kuvipeleka kwenye mahesabu. Mapigo ya moyo ya mwanamke huyu yalidunda kwa kasi sana, akiwa na maswali mengi na matarajio yaliyopita kiasi. Baada ya kumaliza kulipia, naye akabeba mifuko iliyowekewa vitu vyake na kuanza kuelekea nje.

Alipotoka tu, akatazama huku na huku akimtafuta Lexi, naye Alexa akamwonyesha kwa kidole kwamba 'yule pale,' kana kwamba alijua mama yake alikuwa anamtafuta. Valentina akamwona Lexi akiwa amesimama nyuma ya gari fulani huku mifuko yake ikiwa chini, naye akaanza kuelekea sehemu hiyo huku Alexa akitangulia mbele. Lexi akanyanyua mkono wake mmoja kumwonyesha Alexa 'ice cream' ya maziwa na chokoleti iliyofunikwa kwa karatasi lake, naye Alexa akaanza kumkimbilia huku anafurahi. Akafika tu usawa wake na kuikwapua, kisha akaanza kuifungua na kulamba. Lexi akawa anamwangalia mtoto huyu huku anatabasamu, na baada ya Valentina kufika hapo karibu, wakatazamana kwa mara nyingine.

Valentina sasa alikuwa mtu mzima hata zaidi, mwenye miaka 38, lakini mwonekano wake bado ulikuwa mzuri kama wa kijana mdogo. Alipendeza. Wakati huu alikuwa amevaa blauzi nyepesi ya njano yenye uwazi katikati ya kifua chake, na suruali yenye rangi ya maroon iliyombana vyema. Uso wake mzuri ulipendezeshwa kwa make up ya kadiri, naye Lexi akatambua kwamba mwili wa Valentina ulikuwa umeongezeka kiasi, yeye hasa akifurahia zaidi hips zake. Akamshusha mpaka kwenye hips hizo na kutazama hapo zaidi, kwa njia ya uchokozi tu.

"Xander... au... I dont... sielewi... nini kinaendelea?" Valentina akasema.

Lexi akaona kwamba bado Valentina alikuwa na upole wake ule ule.

"Nitakueleza Valentina. Usijali," Lexi akamwambia.

Valentina akaendelea kumwangalia tu usoni. Lexi akamtazama Alexa kwa umakini, kisha akamwangalia na mama yake pia. Valentina akaangalia tu pembeni kwa kuwa alielewa Lexi alichokuwa anauliza. Lakini ilikuwa ni ngumu kiasi kumjibu kwa ishara hasa ukitegemea tayari na yeye alikuwa na maswali mengi ya kuuliza.

"Umenenepa," Lexi akamwambia.

"Tunamwitaga bonge nyanya," Alexa akasema.

Lexi akacheka na kuuliza, "Wewe na nani mnamwitaga hivyo?"

"Na baba," Alexa akajibu.

Lexi akamtazama Valentina, naye akamwangalia. Kisha akaangalia kiganja chake cha kushoto na kuona pete.

"Alexa, shika funguo. Tangulia kwenye gari, nakuja," Valentina akamwambia.

Alexa akazipokea.

"Asante kwa ice cream aunty. Tutaonana tena unipe nyingine, si eti?" Alexa akamwambia Lexi.

"Hmmm... ningependa kama ungeendelea kuwa unamsumbua mama, ila sawa. Tuna dili," Lexi akamwambia.

Alexa akacheka na kuanza kuelekea kwenye gari lao.

"Aunty?" Lexi akamuuliza Valentina.

"Angalau nilimwambia kukuhusu," Valentina akasema.

"Mimi kama mwanamke au mwanaume?"

"Xander huyo ni mtoto. Angeelewa vipi kilichowapata nyie, si angeniona mwendawazimu?"

"Mmm... sawa. Naona kweli ume-move on. Unapendeza sana Valentina," Lexi akamwambia.

"Ona... nahitaji kwenda. Namba zangu hizi hapa..." Valentina akasema huku anampa kadi ndogo.

"Kirefu cha Alexa ni nini?" Lexi akauliza.

Valentina akamwangalia tu.

"Ilikuwaje... ilikuwaje uka..."

"Xander... kama wewe tu ulivyoniambia utanieleza... mimi pia nitakueleza, lakini si sasa. Tutaonana. Usiache kunitafuta," Valentina akasema.

"Na wewe usimwambie yeyote kuhusu mimi kuwa hai. Utaweza?" Lexi akauliza.

Valentina akatikisa kichwa kukubali ijapokuwa hakuelewa ni kwa nini.

Horn za gari fulani zikaanza kupiga sana, naye Valentina akatikisa kichwa huku akiondoka. Lexi akatabasamu akijua ilikuwa ni Alexa ndiyo anamwambia mama yake awahi eti, lakini tabasamu lake likageuka na kuwa simanzi nzito. Kitu alichokuwa amegundua wakati huu ni kitu ambacho hakuwahi kutazamia kabisa kwenye maisha yake kwamba kingekuja tokea. Alikuwa na mtoto. Akainamisha kichwa chake kwa kusikitika, kisha akabeba tu mizigo yake na kuelekea sehemu ya barabara. Akaita taxi moja, naye akaingia na kuanza kuelekea hotelini kwa Nora.


★★★★


Nora alikwenda mpaka kwenye nyumba ya mdogo wake, Asteria. Muda ule wakati yuko supermarket, alikuwa amepigiwa simu na rafiki ya mdogo wake ambaye alimjulisha kwamba hali ya Asteria kwa siku chache zilizopita haikueleweka. Alikuwa nyumbani tu, akinywa pombe kupita maelezo na kulia huku anafanya fujo nyingi.

Rafiki yake aliitwa Germana (kifupi Gema). Huyu alikuwa ni wale marafiki ambao wanang'ang'ania wenzao wenye pesa ili na wenyewe watoke, lakini alimjali Asteria, na hali hiyo iliyoendelea ilimtatiza sana. Aliamua kumpigia simu Nora kwa sababu sasa Asteria alikuwa amejifungia kwenye chumba chake tangu jana, na kila mara alipomwita hakumjibu. Kwa hiyo aliogopa na kumwambia dada yake ili aje kumsemesha.

Nora alifika na kuelekea ndani kule upesi. Kwa mara ya kwanza kabisa akaingia ndani ya nyumba hiyo. Hangejali tena nini kilifanya asitake kuingia hapo, kwa kuwa mdogo wake alikuwa wa muhimu zaidi kuliko chuki yoyote aliyokuwa nayo kumwelekea baba yao. Akafika getini na kupiga kengele, na baada ya sekunde chache Gema akafungua.

"Eh, afadhali dada... sh'kamoo?" Gema akamsalimu.

"Marahaba. Huyo vipi?" Nora akauliza huku akiingia haraka.

"Yaani hata sielewi kiukweli. Tokea majuzi amekuwa ovyo tu. Sijui mpenzi wake amemwacha... yaani sielewi," Gema akasema.

"Ah... yaani nyie watoto jamani!"

Nora akaongea hivyo kwa wasiwasi huku anapandisha ngazi baada ya kufika ndani.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja, nayo ilikuwa pana yenye vyumba vichache tu lakini maridadi sana. Kwa kijana mdogo kama Asteria kuwa na nyumba tayari ilikuwa ni full kujiachia na kuburudika na marafiki tu hapo, kwa hiyo mpangilio wa vitu mara nyingi ungekuwa shaghaalabaghala mpaka siku yeye na rafiki yake wakiamua kufanya usafi wenyewe. Asteria bado alikuwa anasoma chuo kikuu, mwaka wa pili kwenye kozi ya kilimo. Na mbwembwe zake zote haikujulikana kwa nini alichagua kozi hiyo, ingawa kama ungemuuliza angesema tu anaipenda.

Baada ya Nora kufika nje ya mlango wa chumba cha Asteria, akajaribu kuufungua lakini haukufunguka. Akaanza kumwita sana, lakini hakujibu. Nora akamwambia kwa kumtisha kwamba endapo kama asingefungua basi angeuvunja mlango, na anajua nini kingefuata ikiwa Nora angechukua hatua hiyo.

Zikapita sekunde kadhaa za ukimya, na mlango ukasikika ukifunguliwa kwenye kitasa. Nora akaufungua na kuingia ndani, na hapo akakuta mambo mengi yakiwa yamekaa ovyo ovyo tu. Akamwangalia Asteria kwa ufupi, ambaye alikuwa amevaa khanga moja kutokea kifuani, huku nywele zake zikiwa zimevurugika sana kichwani. Sakafuni kulikuwa na chupa nyingi za pombe, naye Asteria akasimama usawa wa kitanda na kumwangalia dada yake.

Nora alimtazama mdogo wake kwa hisia kali sana. Alitaka kujua ni nini iliyokuwa maana ya haya yote aliyokuwa anafanya.

"Umechanganyikiwa?" Nora akauliza.

Asteria akabaki tu kumwangalia kwa njia fulani kama mtu mwenye usingizi. Gema akaingia ndani hapo pia na kusimama mlangoni.

"Ongea. Nini maana yake?" Nora akauliza tena.

"Kwani unataka nini Nora? We si una kazi huko za kufanya? Niache tu mimi nitakuwa sawa," Asteria akasema.

"Unasemaje? Ndiyo nina kazi za kufanya, na isingekuwa ya huu upuuzi wako ningekuwa sehemu fulani sasa hivi. Utaendelea kujiendekeza mpaka lini? Kua Aste. Unajirarua namna hiyo kwa faida gani? Yote haya kwa sababu ya mapenzi?" akauliza Nora kwa hisia.

"Ndiyo! Nilikuwa nampenda sana. Hauwezi kuelewa ameacha pigo kubwa namna gani ndani ya moyo wangu," Asteria akasema kwa hisia.

"Kwa hiyo... ukifanya haya yote ndiyo atakurudia?" Nora akauliza.

"Hawezi. Lakini kama ni kuendelea nitaendelea tu...."

Nora akamkaribia na kumtandika kofi zito usoni. Asteria akakaa kitandani huku akilia, na kuweka kiganja chake kwenye shavu huku ameinamia kitanda.

"Utaendelea kuwa mpumbavu mpaka lini? Eeh?" Nora akauliza.

"Nimekwambia hauwezi kunielewa," Asteria akasema huku bado analia.

"Nielewe nini? Nielewe nini?" Nora akauliza.

"Amekufa," Asteria akajibu.

Nora akatulia kidogo na kumwangalia tu.

Asteria akamgeukia na kusema, "Wamemuua."

"Nini?" Nora akauliza kimshangao.

Asteria akaendelea tu kulia.

Ikambidi Nora asogee karibu yake na kupiga magoti chini, kisha akamshika mikono na kumwangalia machoni kwa umakini. Gema akaingia na kusogea mpaka karibu.

"Nini kimetokea?" Nora akauliza kwa kujali.

"Yaani hata sielewi. Nilikuwa naye... kidogo tu nashangaa ananiambia... nisimjue tena... hhh... Nikam..nikamtafuta... lakini sikumpata. Ndiyo nikaja kumwona... TV... eti amekufa...." Asteria akasema na kuanza kulia tena.

Nora akahisi vibaya sana kwamba alimpiga mdogo wake wakati alikuwa kwenye maombolezo. Akamkumbatia na kuanza kumbembeleza, huku akijitahidi kuyazuia machozi yake kumwagika. Akapanda kitandani na kukaa, huku kichwa cha Asteria kikiwa kifuani kwake akiendelea kumbembeleza.

"Pole Aste... pole sana dear," akasema Nora.

Asteria akawa anajitahidi kujikaza.

"Ulikuwa unasoma naye?" Nora akauliza.

Asteria akatikisa kichwa kukataa.

"I'm sorry. Sikuwahi hata kukutana naye. Pole sana mdogo wangu," Nora akamwambia.

"Pole Aste. Me mwenyewe sikujua," Gema akasema.

"Lakini Aste, umesema wamemuua. Inamaanisha nini? Nani amemuua?" Nora akauliza.

"Me hata sielewi. Wanasema ameuliwa na wale... Mess Makers," akasema Asteria.

Nora akashangaa. Akanyanyua kichwa cha mdogo wake na kumtazama usoni.

"Boyfriend wako aliitwa nani?" akamuuliza kwa umakini.

"Oscar," akajibu Asteria.

Nora akaangalia chini akiwa amechoka akili. Mbona mchezo huu wote ulikuwa na mizunguko mingi namna hii? Aliwaza sana ni kwa nini mambo mengi yalikuwa yanatokea kwa njia hii tokea kundi la Mess Makers lilipozuka, lakini akakosa jibu. Sasa akawa anajiuliza ikiwa Oscar alikuwa anatoka na mdogo wake kimakusudi au la.

"Huyo Oscar... ulikutana naye wapi?" Nora akauliza.

"Mitaa fulani... zamani," akajibu Asteria.

"Zamani... yaani miaka mingi?"

"Kama miwili..."

"Kwa hiyo mli-date kwa miaka karibia miwili?"

Asteria akatikisa kichwa kukubali.

"Okay. Umesema... mara ya mwisho ulipokuwa naye nini kilitokea?" Nora akauliza.

"Hata sielewi. Tulikuwa wote... sijui nini kikampata akaanza tu kupasua simu, akaitupa chooni, halafu akaniambia nisimwambie yeyote kama ninamjua kwa sababu... maisha yangu yangekuwa hatarini. Sikumwelewa... yaani ni kama alijua kwamba siku hiyo angekufa... hhh... sielewi hao watu walitaka nini kutoka kwake, alikuwa kijana wa kawaida tu..." akasema Asteria kwa huzuni.

"Kwa hiyo ni kama kuna watu wengine wamemuua halafu polisi wakawasingizia Mess Makers?" Gema akauliza.

"Hata sielewi..." Asteria akasema.

Nora alikuwa anawaza mambo mengi, lakini kwa sasa alihitaji kwanza kumtuliza mdogo wake. Akamfuta machozi na kumwambia asiogope kwa sababu kila kitu kingekuwa sawa. Kwa sababu Asteria hakujua ikiwa dada yake alijihusisha na msako wa Mess Makers, Nora akamsihi kwamba afuate ushauri wa mwisho wa mpenzi wake, kwamba asimwambie mtu yeyote kuwa alitoka naye kimapenzi, na ikiwa ingetokea watu fulani wenye vyeo vya usalama wakamuuliza, basi angepaswa kumwambia yeye kwanza ili amsaidie kushughulika nao.

Dada mkubwa akaendelea kukaa hapo na mdogo wake, akimsaidia kuondoa mkazo na kumtia moyo zaidi ili afarijike.


★★★★


Lexi alirejea hotelini alikoishi Nora kwa sasa na kuelekea kwenye chumba chake moja kwa moja. Giza lilikuwa limeshaingia, ikiwa ni saa 1 sasa. Aliweka mizigo pembeni, naye akaketi sehemu ya kitanda akitafakari mambo mengi. Kukutana kwake na Valentina kulikuwa jambo ambalo hakutazamia hata kidogo. Na tena kuongezea utata wa hali hiyo ni kujua kwamba alikuwa na mtoto pamoja naye, ambaye hakujua kumhusu pia. Alianza kuwaza ingekuwa vipi kama kipindi kile mambo yote yale mabaya yasingetokea, inamaanisha labda leo angekuwa pamoja na binti yake na mama yake pia.

Kwa jinsi ambavyo maisha yao yalikuwa yamebadilika, nani angeamini sasa hivi ikiwa angekwenda na kusema yeye ndiyo "baba" wa huyo mtoto, wakati alionekana kuwa mwanamke? Alianza kumkumbukia Alexa, jinsi alivyokuwa mzuri na mashavu yake makubwa, naye akatabasamu kwa hisia. Lakini pia alithamini sana kwamba Valentina hakuficha ukweli kutoka kwake ingawa ndiyo walikuwa tu wamekutana baada ya miaka nane, naye akawa anatazamia kwa hamu kuja kuonana naye tena.

Wakati akiendelea kutafakari hayo, ujumbe wa Nora ukaingia kwenye simu yake, akiuliza kama bado alikuwepo hapo, naye Lexi akajibu kwa kusema ndiyo, ila aliboeka kukaa peke yake. Nora akamwambia angefika muda siyo mrefu; ampe kama dakika 15 tu. Baada ya Lexi kukubali, akafumba macho kwa sekunde chache, kisha akanyanyuka kutoka alipoketi na kwenda kwenye vitu vya Nora. Alianza kupekua vifaa vyake vingi, akitafuta hasa makaratasi au makablasha ili kuona kama angepata jambo lolote lililohusiana na kazi ya Nora ya kuwatafuta Mess Makers.

Alipekua na kupekua lakini hakupata taarifa zozote zenye kuvuta umakini wake. Ndipo akasikia sauti nyuma yake.

"Unafanya nini?"

Macho ya Lexi yakakaza huku akitazama mbele. Alikuwa amechuchumaa, hivyo akasimama akiwa anahisi hasira sana na kugeuka nyuma yake. Ilikuwa ni Luteni Michael.

"Unaingia vipi humu bila hodi?" Lexi akamuuliza.

Nyuma ya Luteni Michael walikuwa ni Mario na Hussein.

"Hodi siyo kitu ambayo wewe unajali, kwa hiyo tusipotezeane muda. Nataka useme unafanya nini ndani hapa," Luteni Michael akamwambia.

"Siwezi kukwambia nafanya nini hapa mpaka uniambie kwa nini hujapiga hodi," Lexi akasema.

Hussein akatabasamu na kusema, "I like you."

"Asante. Mimi pia," Lexi akamwambia.

"Mnaona jinsi hicho kiburi kilivyojaa usoni kwake? Nani ameshawahi kuwafanyia hivyo akijua kabisa nyinyi ni nani?" Luteni Michael akawaambia wenzake.

"Kwa hiyo kwa sababu wewe ni mwanajeshi ndiyo napaswa kutetemeka sanaaa? Cheo ulichonacho hakipaswi kuogopwa. Wewe upo kwa ajili ya wananchi, siyo kwa ajili ya kuogopwa," Lexi akamwambia kwa ujasiri.

Luteni Michael akamtazama kwa hasira.

"Kaa kimya, mshenzi wewe! Unaongea na sisi namna hiyo, nitakupasua sasa hivi!" akasema Mario.

"Oya, ndo' nini sasa? Swagger gani hizo kama makoplo, tena wale masharobaro wa chihaya?" Hussein akamwambia Mario kiutani.

"Em' niache na we naye," Mario akasema.

Luteni Michael akamsogelea Lexi karibu zaidi. Lexi hakuonyesha woga wowote ule na kumwangalia tu usoni kwa njia ya kawaida.

"Wewe ni nani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Naitwa Lexi," akajibu.

"Wenzako wako wapi?"

"Wakina nani?"

"Kama unajali sura yako, ongea kila kitu sasa hivi. La sivyo nitakuumiza," Luteni Michael akamwambia kiutulivu.

"Hivi wewe una shida gani? Unanitaka nini mimi? Au hii yote ni kwa sababu ya Nora? Kwa sababu amekukataa?" Lexi akamwambia.

Mario na Hussein wakaangaliana kimaswali.

"Ninakupa sekunde...."

"Hata usijisumbue. Kama unataka kunipiga anza. I dare you," Lexi akasema.

Luteni Michael akakunja ngumi kwa kuhisi hasira kali sana. Mario na Hussein wakawa wametulia tu wakisikilizia nini kingefuata. Luteni Michael akamsogelea Lexi mpaka karibu kabisa na mdomo wake akimwangalia kwa hasira, naye Lexi akanyanyua kidevu juu akimtazama bila hofu.

"Sababu moja inayofanya nisikuue hapa hapa sasa hivi ni kwamba haitaonekana kuwa haki, lakini hiyo haimaanishi siwezi kukutia dole. Hiki kiburi chako kitakwisha leo leo," Luteni Michael akamwambia hivyo.

Kisha akaishika sehemu ya Lexi ya siri na kuiminya kwa nguvu. Lexi alikasirika sana! Akampiga kichwa cha pua na kufanya Luteni Michael arudi nyuma kidogo. Kisha mwanaume huyo akamfata Lexi tena na kumpiga kofi zito usoni, naye Lexi akadondokea kitandani akikunja ngumi kwa kuhisi hasira kali. Mario na Hussein wakawa wanamwambia Luteni wao asimfanyie mwanamke huyo jambo lolote baya, lakini Luteni Michael akamfata kitandani hapo na kumshika shingoni kisha kumvuta kuelekea uso wake.

"Unajifanya mbabe si ndiyo? Sasa ngoja nikuonyeshe!" Luteni Michael akamwambia.

Kisha akamvuta na kumsukuma upande ambao Mario na Hussein walikuwa wamesimama, naye Hussein akamwahi na kumdaka kabla hajaanguka chini vibaya.

"Asante..."

Lexi akamwambia hivyo Hussein, naye Hussein akamwonea huruma kiasi.

"Mwachie," Luteni Michael akamwamuru Hussein.

"Luteni... hivi unavyofanya siyo sawa. Hata kama angekuwa mmoja wa Mess Makers, huyu ni mwanamke, hupaswi kumpiga hivi. Na vipi ACP aki...."

"Nimesema mwachie!" Luteni Michael akamwambia kiukali huku amemnyooshea kidole.

Hussein akamwachia Lexi na kusimama, ambaye pia akasimama na kumgeukia Luteni Michael.

"Unataka kupigana? Come to me," Luteni Michael akasema.

"Oh, no. By all means, ring's yours (hapana... kwa mambo yote, ulingo ni wako)," Lexi akasema kwa ujasiri.

Luteni Michael akatabasamu na kuwaambia wenzake, "Hivi mnaweza kuamini kabisa mwanamke huyu ananichallenge mimi?"

"Kwani wewe ni nani? Wewe ni binadamu kama wengine tu. Hakuna chochote kilicho chenye ubora kuhusu wewe kinachopita kile cha mtu anayekaa kuombaomba pesa barabarani. Tena naweza kusema hata mtu wa namna hiyo ni bora kuliko wewe, kwa sababu ijapokuwa ana hali ngumu, angalau anajua anapotakiwa kuwa. Wewe je? Unajua unapotakiwa kuwa? No. Kwa sababu unafuata tu kila unachoambiwa na viongozi wako kama mbwa!" Lexi akasema.

Luteni Michael akamfata na kwa hasira akampiga ngumi usawa wa mdomo wake. Mario na Hussein wakashangaa sana na kusogea pembeni, kwa kuwa Lexi alianguka na kuanza kutambaa kuelekea mlangoni taratibu. Luteni Michael akamfata na kuzishika nywele zake kwa nguvu, akimvuta kumsimamisha juu. Kisha akamsogelea sikioni kwake huku mkono mmoja akiuweka kwenye shingo yake.

"Nani unamwita mbwa, malaya wewe? Umekosa mwanaume wa kukupa watoto ukahamia kwenye mashine za usagaji, si ndiyo? Sasa kuanzia leo uta...."

Kabla hajamaliza kuongea, mlango wa kuingilia ndani ya chumba hiki ukafunguka. Ilikuwa ni ACP Nora! Alifika tu ndani hapo na kukuta Lexi akiwa ameshikiliwa namna hiyo, huku uso wake ukionyesha maumivu. Alichoka! Luteni Michael akashtuka moyoni, naye akamwachia Lexi, ambaye alidondoka chini huku akipumua kwa nguvu. Yaani Nora alishindwa hata kuongea, alishindwa hata kujongea, alishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea. Mario na Hussein wakatazamana kama kuambiana 'haya sasa,' naye Lexi akamtazama Nora usoni huku mdomo wake ukitoa mchirizi wa damu.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
Mkuu una uandishi mzuri na wa kipekee kabisa yaani kama ungekuwa ni mtangazaji ningekufananisha na Emmanuel Mdemu wa Times FM
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI

★★★★★★★★★★★★★★★


Nora akatembea taratibu na kuchuchumaa chini, akaushika uso wa Lexi na kumwangalia kwa huruma.

"Lexi..." Nora akaita kwa sauti yenye huzuni.

"Niko sawa mheshimiwa... niko sawa," Lexi akajibu huku anatoa tabasamu hafifu.

Nora akainamisha uso wake na kufumba macho. Hivi siyo jinsi alivyotarajia siku yake iende hata kidogo. Alitarajia iwe siku ya kuituliza akili yake, lakini mambo yaliyokuwa yametokea ndiyo yakaivuruga kabisa. Akashusha pumzi, kisha akasimama na kumwangalia Luteni Michael kwa mkazo.

"Nora..."

"Toka," Nora akamkatisha.

"Nora nisikilize, huyu..."

"Mario, Hussein, nawaomba wote mwondoke. Now," Nora akawaambia.

"Lakini Nora, naomba tu uni...."

Luteni Michael alikuwa akimsogelea karibu zaidi wakati alipokuwa anasema hivyo, lakini Nora akaanza kumtandika makofi mengi sana usoni. Akampiga kwa goti sehemu yake ya siri, naye Luteni Michael akaugulia maumivu na kukaza kichwa, lakini akajitahidi asitoe sauti. Nora akamwongezea goti lingine hapo hapo tena, naye Michael akadondoka chini. Alipomtazama, kweli Luteni Michael aliona Nora alikuwa amekasirika sana. Alikuwa anapumua kwa hasira nyingi mno, huku amekunja ngumi kwa nguvu. Mario na Hussein wakamfata Luteni Michael pale chini na kumnyanyua taratibu ili wamsaidie kumwondoa hapo. Luteni Michael alipomwangalia Lexi kwa ufupi, Lexi akampandishia nyusi kichokozi huku anatabasamu, na hilo likamkasirisha sana Michael.

Wanajeshi hawa watatu wakaondoka hapo hatimaye, naye Nora akaufunga mlango na kumsaidia Lexi kuelekea kitandani. Baada ya Lexi kukaa, Nora akatafuta kitu chochote hapo ndani cha kumponya Lexi sehemu alizoumia, kisha akakaa karibu yake na kuanza kumchua usoni taratibu. Akauliza ikiwa kuna sehemu zingine za mwili zilizohitaji tiba, lakini Lexi akakanusha kwa kusema aliumia tu hapo usoni na shingoni. Lexi alipomtazama Nora, aligundua kwamba mwanamke huyo alikuwa anajitahidi kuficha hisia zake nyingi, naye akamwambia inatosha; angekuwa sawa.

Nora alipoacha kumpaka dawa, akatazama tu pembeni na kuanza kulia sana. Alilia huku akiwa amefunika uso wake kwa viganja vyake, na kiukweli jambo hili lilimhuzunisha sana Lexi. Akamshika begani na kumvuta usawa wake, naye Nora akalalia kifuani kwa Lexi huku akijitahidi kujikaza. Wakaendelea tu kukaa namna hiyo hiyo kwa robo saa zaidi, kisha Nora akakaa sawa na kujifuta machozi yaliyobaki. Akamwangalia Lexi, ambaye alimpa tabasamu na kumbonyeza shavuni kichokozi, naye Nora akatabasamu pia.

"Nisamehe Lexi... yaani..."

Lexi akavishika viganja vya Nora kwa pamoja.

"Usijali. Jamaa amefanya tu jinsi moyo wake ulivyomtuma, wala haikuwa na shida sana," Lexi akasema.

"Hapana. Ilikuwa ni tatizo kubwa sana ambalo siwezi nikalifumbia macho. Luteni Michael amevuka mipaka. Ni lazima apewe somo," Nora akasema.

"Utamfanya nini sasa huyo sokwe?" Lexi akauliza kiutani.

"Ahahah... nitajua tu. Ona alivyokuumiza jamani..." Nora akasema huku akiushika mdomo wa Lexi.

Wakatazamana kwa hisia sana, naye Nora akaufata mdomo wa Lexi na kumbusu. Ilikuwa busu ya taratibu tu, kisha Nora akaanza kumpapasa Lexi mgongoni huku akiendelea kumpa denda laini. Lexi alianza kuhisi jambo hilo lingeelekea sehemu ambayo hakuwa akiitaka kwa wakati huu, hasa akijua wazi kwamba mwanamke huyu alikuwa adui yake kwa njia isiyo ya moja kwa moja, hivyo akajitoa mdomoni mwake na kujifanya kama vile sehemu fulani ya mwili wake inauma.

"Vipi Lexi?" Nora akauliza kwa kujali.

"Niko sawa. Kuna sehemu tu hapa shingoni... inauma," akasema Lexi.

"Oh, okay. Basi... aam... ngoja niagize chakula... walete, wewe lala hapa," Nora akamwambia.

Lexi akajivuta taratibu na kujilaza kitandani, huku Nora akimtengenezea mto ili aegamie. Nora akazichezea taratibu nywele za Lexi huku wanapeana tabasamu, kisha akaelekea sehemu iliyokuwa na simu ya mezani na kuomba chakula. Lexi alibaki hapo akimwangalia kwa makini sana. Alikuwa anawaza ingekuwaje siku ambayo dada huyo mwenye moyo mzuri angegundua kwamba mtu aliyeanza kumwamini ndiye aliyekuwa mbaya wake. Alikuwa hata anawaza hivi wakati huu kwa sababu kiukweli alianza kumjali sana Nora, kitu ambacho hakikutakiwa kutokea, lakini tayari ikawa hivyo.

Baada ya Nora kuita vyakula kwa ajili yao, akarudi kitandani na kulala karibu na Lexi, wakiwa wanatazamana tu machoni. Aliyapenda sana macho ya Lexi, naye akawa anatembeza kidole chake taratibu kwenye uso wake. Akamwomba kwa kusema hata wakimaliza kula, Lexi aendelee kukaa naye hapo hapo mpaka kesho, yaani alale pamoja naye usiku huo. Lexi akatikisa kichwa kukubali, naye Nora akafurahi na kumbusu kidogo kichwani, na wawili hawa wakaendelea kulala hapo wakisubiri chakula kiletwe.


★★★★


Luteni Michael, Mario na Hussein walirejea kule kwenye timu yake baada ya kutoka kwa ACP Nora. Bado mwanaume alikuwa na hasira sana, naye aliwaamuru Mario na Hussein wasiseme lolote kuhusu kilichotokea huko hotelini la sivyo wangemtambua. Alipofika tu jengoni kule akawauliza wengine walikuwa wamepata nini kuhusiana na Lexi. Hakupata jibu haraka, kwa kuwa wote walimwangalia kimaswali. Pua yake ilivimba kiasi kutokana na Lexi kumtandika kwa kichwa usoni, hivyo walikuwa wanajiuliza alipatwa na nini. Akawaambia waache kushangaa na waanze kumpa taarifa alizohitaji.

Manengo akamweleza kwamba mwanamke yule anakwenda kwa jina la Lexi Sona, na ni mgeni nchini humu kutokea Ghana. Akamweleza kwamba ameingia nchini kihalali kabisa, na aliishi Pemba kwa muda fulani akifanya kazi kama msimamizi wa biashara ya magari kwenye garage fulani ndogo mpaka alipokuja huku. Luteni Michael akauliza mambo mengi sana ambayo yangemhusisha Lexi na Mess Makers, lakini kiukweli, kwa sababu wanajeshi hawa hawakuwa wamefatilia mambo kwa kina sana, hawakuweza kuona kitu chochote kilichodokeza kwamba alihusiana nao.

Kwa hasira, Luteni Michael akapiga meza kwa ngumi yake, kisha akawaambia wenzake wangeweza kwenda kupumzika lakini kesho asubuhi na mapema wawe hapo kuendelea na kazi. Akaondoka upesi akionekana kuwa mwenye ghadhabu, na wengine wakaanza kuwauliza Mario na Hussein nini kilitokea huko walikoenda. Lakini wanaume hao wakawaambia hiyo ilikuwa ni siri yao, kwamba eti ni "top secret," kwa hiyo wengine hawakupaswa kujua lolote isipokuwa wao tu. Alex, Mario na Hussein wakawaaga wengine pia na kusema wangeonana kesho, huku Hussein akimpandishia nyusi kichokozi Aliyah. Ikabidi Mario amvute mkono ili waondoke hapo, kwa kuwa walikaa pamoja na Alex kwenye nyumba fulani ndogo ya kulipia.

Wakati wakiwa wanaelekea nje, Tariq akaangaliana na Aliyah, na bila mtu mwingine kuona akamtikisia kichwa mara moja kwa ishara ya kumwambia afanye jambo fulani, naye Aliyah akaanza kuelekea nje upesi. Aliwahi kabla Hussein na wenzake hawajaingia kwenye gari, naye akamwita na kumsimamisha. Hussein akaachia tabasamu la furaha akijua mtoto alikuwa amemwelewa, kisha Aliyah akafika karibu yake na kumwambia angependa wakatembee pamoja kabla hajaenda kupumzika. Hussein akatae? Akazirusha funguo za gari usoni kwa Mario na kumwambia yeye na Alex watangulie tu, huku Mario akimtazama kwa kukerwa.



Aliyah alimwongoza Hussein hadi kwenye chumba alichokuwa anakaa. Kilikuwa kwenye nyumba iliyo ya ghorofa, kukiwa na wapangaji kadhaa sehemu hiyo, na yeye Aliyah alikuwa kwenye ghorofa ya tatu. Kufikia wakati walipofika kwenye mwisho wa ngazi kuelekea chumba chake, Hussein alikuwa amepiga naye story nyingi zenye kufurahisha, na Aliyah kiukweli alipendezwa naye sana. Hussein aliongea mno na kila muda ambao mada moja ingeisha angetokeza nyingine yenye kufurahisha hata zaidi. Alijitahidi sana kumfurahisha Aliyah, akijua leo angekwenda kupewa bonge la keki.

Walipoingia tu ndani, Aliyah akaenda moja kwa moja kwenye fridge ndogo ya vinywaji. Kwa kujua kile ambacho kingefuata, Hussein akaamua tu kukaa kimya na kumtazama.

"Unataka bia?" Aliyah akauliza.

"Ningependa juice tafadhali," akajibu Hussein kikejeli.

"Kaa sasa," Aliyah akamuamrisha.

Hussein akaketi kwenye sofa. Alikuwa ameshaanza kuizoea tabia fulani ya Aliyah ya kujifanya kama kibosile. Aliyah alikuwa mrefu wa kadiri, mweupe, na mwenye umbo zuri la kike. Hata kama angevaa nguo za kijeshi isingezuia sehemu za mapaja yake na kalio kuonekana vizuri jinsi zilivyoshiba, na ni kati ya mambo yaliyomvutia zaidi Hussein kumhusu mwanamke huyu.

"Hapa palivyokaa inawezekana kuna njemba imejificha huko ndani. Inabidi niwe chonjo," Hussein akatania.

Aliyah akaanza kumfata huku akicheka, kisha akampatia juice yake. Yeye alikuwa ameshika chupa ndogo ya bia, kisha akainywa nusu chupa huku akiwa amesimama mbele yake. Hussein akawa anamwangalia kwa umakini, akipendezwa na jinsi mabuti yake ya kijeshi yalivyomfanya aonekane kama jemedari wa kiume. Aliyah akaiweka mezani bia yake, kisha bila kupoteza muda akapiga magoti katikati ya mapaja ya jamaa na kuanza kuvuta suruali yake kwa njia iliyomwambia Hussein anyanyuke kidogo ili afanikiwe kuitoa. Njia ya Aliyah ya kwenda moja kwa moja kwenye pointi ilimvutia sana jamaa, naye akatii na kujinyanyua kidogo, kisha Aliyah akaitoa suruali yote na boxer mpaka jamaa akawa mtupu huku chini.

(........).

(........).

"*****... nilihitaji sana hii kitu," akasema Hussein.

Aliyah alikuwa anampa zawadi hii ya kumkaribisha kwake, akimnyonya kwa njia ambayo hangesahau.

Akaitoa mashine yake jamaa mdomoni muda mrefu vya kutosha kusema, "Mkeo huwa hakupi namna hii kwani?" kisha akaendelea kumnyonya.

Ilimchukua Hussein sekunde chache kusawazisha akilini alichosema Aliyah kutokana na kupagawishwa haswa.

"Mimi sijaoa... nina marafiki tu wa vitambo. Walikuwa wanahh...hitaji penzi...kwa hiyo nikawa nawasaidia... ila hii show yako hawajaifikia..."

Aliyah akacheka kidogo na kusema, "Hapa bado!"

(.........).

Kisha Aliyah akaitoa mdomoni kwa ufupi na kuanza kuipekechea mkononi. Hussein akatabasamu, naye Aliyah akamuuliza jamaa kwa maringo, "Luteni Michael naona kama huwa mnamwogopa sana. Ni kwa nini?"

"Tunamheshimu, siyo kumwogopa. Hata nyie pia, siyo?" akajibu Hussein huku amefumba macho.

"Yeah... Nilipomwona wakati mmerudi nikadhani amegongwa na treni usoni!" Aliyah akasema.

"Ahahah... hamna. Kapigwa. Tena kapigwa na mwanamke hahah..." Hussein akafunguka.

"Yule yule Lexi?"

"Yeah. Alikuwa anataka kumkamata, ila demu akamletea nyodo ndiyo akaanza kumshushia kipondo. Lakini na kenyewe kalimuonja... ahahah... na ACP akamkunja," Hussein akasema.

Aliyah akarudia zoezi lake na kuanza kuinyonya tena mashine ya Hussein. (........).

(........).

(........).

(........).

Walitulia kama dakika moja, kisha Aliyah akanyanyuka na kukirudia kinywaji chake. Akamwambia Hussein anaenda chooni mara moja, naye akamwacha hapo jamaa amekaa kwenye sofa akiwa amejiachia kama anasubiri kuchunwa ngozi kwenye sehemu zake za siri. Lakini hakujua kwamba hii ilikuwa ni njia fulani ya kupata ukweli kutoka kwake kuhusu kilichotokea muda ule walipoondoka na Luteni Michael. Aliyah aliingia sehemu ya bafuni na kumpigia simu Tariq, akimweleza yale ambayo Hussein alikuwa amesema. Tariq akampongeza kwa kazi nzuri na kumwambia aendelee kumzuzua tu namna hiyo hiyo kwa leo.

Aliyah akarudi mpaka pale alipoketi Hussein na kukuta jamaa akipasafisha vizuri. Akatabasamu, kwa kuwa alipenda sana njia fulani yenye ucheshi ya kufanya mambo aliyokuwa nayo mwanaume huyo. Akaanza kuvua nguo zake zote na kubaki akiwa mtupu kabisa, kisha akaanza kumfata Hussein ambaye hakuwa amemwona bado. Alipofika nyuma yake, Hussein akageuka na kukutana na mwili mweupe wa mwanamke huyu. Akaachia tabasamu la mbali, naye Aliyah akamsukuma kwenye sofa.

Kisha mwanamke huyo akapanda juu yake akiwa amepiga magoti, naye Hussein akaishusha tena suruali yake mpaka usawa wa magoti. Aliyah akakaa juu ya jamaa taratibu na kutoa pumzi ya juu akihisi raha. Kisha akaanza kupanda na kushuka, akijisugua vizuri katikati ya mstimu wa mwanaume huyo machachari. Wakaendelea kupeana mahaba kwenye sofa mpaka walipopitiwa na usingizi na kulala pamoja usiku huo.



Upande wa Tariq, taarifa aliyokuwa amepewa na Aliyah ilitakiwa kufika kwa Kanali Oswald Deule. Kati ya wanajeshi wale watano walioongezwa kwenye timu ya Luteni Michael, ni hawa wawili ndiyo ambao walikuwa wamewekwa kujua mambo yote yanayoendelea ambayo Luteni Michael hangemweka wazi Kanali, ili wamwambie yeye. Kwa hiyo Tariq akamjulisha Kanali Oswald kuwa Luteni Michael alitaka sana kumkamata mwanamke fulani lakini akaambulia kuabishwa tu na ACP Nora, ikionekana alikuwa anapoteza tu muda wake kwa sababu alikuwa na hisia za kimapenzi kumwelekea mtoto wa huyo wa Jenerali Jacob.

Kanali Oswald akamshukuru Tariq kwa kumjuza kuhusu hilo na kumwambia asiache kumpa ripoti za mambo yoyote yatakayofanyika, na baada ya hapo wakaagana.


★★★★


Asubuhi na mapema ya siku iliyofuata, Nora aliamka na kukuta Lexi akiwa bado amelala pembeni yake. Aliachia tabasamu la hisia nzuri sana, akihisi ni kama kuna jambo fulani kuhusu uhusiano wake na Lexi ambalo lilikuwa geni sana kwake, na hiyo ilimfanya ajihisi tofauti sana. Hakuwahi kukaa kufikiria kwamba siku moja na yeye angewahi kujaribu mahusiano na mwanamke, ijapokuwa kihalisi Lexi hakuwa "mwanamke."

Akaanza kumtekenya usoni kwa kupitisha kucha yake usawa wa midomo yake, kama anaichora, na ghafla kinywa cha Lexi kikafunguka na meno yake kuking'ata kidole cha Nora, lakini kwa wepesi. Hii ilimshtua Nora kidogo, ambaye alifikiri Lexi alikuwa bado kasinzia, lakini kwa kutambua alikuwa anamtania kichokozi, akaanza kucheka huku amefumba mdomo.

Lexi akakiachia kidole cha Nora, kisha akafumbua macho na kumwangalia machoni.

"Good morning," Nora akamwambia.

"Same to you," Lexi akasema.

"Unahisije? Bado maumivu yapo?" Nora akauliza.

"Kwa mbali shingoni, lakini najua itapoa," Lexi akajibu.

"Pole. Nahitaji kwenda kuoga. Kuna sehemu natakiwa niwahi,'' Nora akamwambia.

"Wapi?"

"Ni ofisi mpya nitakayotumia sasa. Nitafatwa na mtu fulani, ananipeleka kunionyesha, ila najua lazima tu atawahi mno kwa hiyo... best be ready..."

"Aaaa... angalau utakuwa mbali na yule sokwe..."

Nora akacheka kidogo na kusema, "Yeah... angalau."

"Okay. Me bado nahisi usingizi. Wewe kapambane na bafu, halafu mimi nitaendelea na uchunguzi wangu hapa hapa kitandani," Lexi akasema na kufumba macho tena.

"Ahahahah... haya bwana," Nora akasema.

Kisha akambusu kwenye paji lake la uso, halafu akatoka kitandani na kuelekea kuoga.



Baada ya kumaliza kujiandaa, Nora alimwangalia Lexi na kuona bado amelala. Akahisi labda kwa sababu ya jambo lililompata jana alihitaji kupumzika sana, hivyo akamwachia ujumbe kwenye simu yake kuwa angewasiliana naye au wangeonana baadae. Akamfunika vizuri kwa shuka, kisha akaelekea nje ambapo tayari mtu aliyetakiwa kumpeleka ofisini kwake alikuwa akimsubiri.

Lakini muda wote huo Lexi alikuwa anajifanya kasinzia tu, hivyo baada ya Nora kuondoka, akanyanyuka na kwenda kujimwagia pia. Akavaa nguo zake haraka na kuondoka hapo upesi mpaka kwenye gari lake. Alikuwa akificha kifaa kile cha mawasiliano maalum na Torres kwenye gari lake, hivyo akakitoa na kuangalia kama Torres alimtafuta tena. Akakuta ametafutwa mara kadhaa jana na asubuhi hii, hivyo akampigia yeye ili kujua yaliyoendelea upande wake.

Torres alimjulisha kuwa kuna jambo la muhimu sana ambalo alitaka kuzungumza na kundi lao lote, hivyo Lexi angetakiwa kwenda kule kwenye nyumba yao ya maficho, a.k.a "chini." Lexi akamwambia huenda ingekuwa ngumu hasa ukitegemea hali aliyokuwa nayo na Kendrick na pia ACP Nora, lakini Torres akasisitiza sana kuwa jambo lililoendelea lilikuwa muhimu kuliko tofauti zao, na alimhitaji sana ili kupanga mambo mengi vizuri. Lexi akatafakari kwa sekunde chache, kisha akamwambia angekwenda huko upesi. Torres akafurahi sana na kusema wote walikuwepo kule tayari, hivyo angemsubiri kwa hamu ili "kikao" chao kianze.

Baada ya kumalizana na Torres, Lexi akaliondoa gari lake hapo na kuanza kuelekea kule kwenye hoteli aliyokaa. Alikuwa anamuwaza Valentina, akikumbuka kuwa alitakiwa kumtafuta kwa simu ili labda wakutane leo, lakini kwa sababu ya mambo kuingiliana haingewezekana. Hivyo akaamua kuacha kumtafuta mpaka wakati mwingine. Akawaza jambo la kumwambia Nora kuhusu yeye kutokuweza kuwa naye baadae, naye akaendelea na safari yake.


★★★★


ACP Nora alifikishwa mpaka kwenye jengo ambalo ofisi yake mpya ya utafiti ingekuwa. Lilikuwa ni Kituo maalum cha Usalama wa Taifa (Defense Agency), nalo lilikuwa na ghorofa 9 kuelekea juu. Lilijengwa hasa kwa vioo sehemu za nje, na eneo lote kulizunguka lilikuwa safi na lililotunzwa vizuri. Akapelekwa mpaka sehemu za ndani, akipishana na watu wengi walioendelea na kazi zao mbalimbali, kisha wakachukua lifti na kupandisha mpaka ghorofa ya mwisho. Huko ndiko kungekuwa na ofisi yake.

Afisa aliyemleta hapo alimwambia kwamba Msimamizi Mkuu wa kitengo cha Huduma za Ulinzi nchini (Ministry of Defence) alikuwa akimsubiria. Nora akauliza kwa nini, naye akaambiwa alikuwa tu anatakiwa kumpokea kwenye ujio wake hapo. Yote haya hayakumpendeza sana Nora, lakini kwa wakati huu aliona ni bora kuwa huku kuliko kuwa karibu na Luteni Michael baada ya kitendo alichomfanyia Lexi.

Walipofika kwenye ofisi ya Msimamizi huyo mkuu, Nora akatabasamu kwa furaha. Alimfahamu, lakini hakujua ikiwa alipatiwa cheo hicho tayari. Huyu alikuwa ni mwanamama Emiliana Ngoyi, yule yule wa tokea kipindi kile cha Demba Group. Alipoingia ofisini kwake, Emiliana akampokea kwa kumbatio, akiwa ndani ya suti ya kike yenye rangi ya blue-bahari, huku Nora yeye akiwa amevaa suti nyeusi ya kike. Wakajuliana hali zao, kisha Emiliana akaanza kumwelezea mambo mengi ya kitengo chao, ingawa kwa kadiri kubwa Nora alifahamu.

Ofisi ambayo Nora angepewa ilikuwa kwa njia fulani kama ofisi ya mpelelezi mkuu, ijapokuwa Nora hangechukua cheo hicho kwa sababu angekuwa hapo kwa muda tu. Katika maongezi yao, Emiliana alimjulisha Nora kwamba leo alitakiwa kwenda pia kwenye mahojiano maalum ambayo yangefanywa kuhusiana na Salim Khan, kwa kuwa huenda naye angeshiriki kuuliza maswali na hata kupata mambo mengi kutoka huko. Nora akakubali mwaliko huo.

Baada ya kumaliza maongezi yao, Emiliana akamsindikiza sasa Nora mpaka kwenye ofisi yake mpya. Alipokelewa na mwanamke aliyekuwa mweupe kiasi, akiwa amevalia miwani machoni, naye akajitambulisha kwa jina la Halima Said. Angekuwa ndiyo msaidizi wake Nora kwenye masuala ya kutuma jumbe, kupokea jumbe, yaani chochote kile ambacho Nora angehitaji kwa muda wote ambao angekuwa hapo. Nora akamshukuru sana Emiliana kwa kila jambo, kisha akaelekea ndani ya ofisi yake kuanza kazi.

Ilikuwa ofisi yenye mpangilio mzuri sana, naye Nora akaenda kwenye meza iliyokuwepo na kuketi kwenye kiti cha kiofisi. Kulikuwa na kompyuta hapo pia, lakini yeye akaitoa laptop yake na kuiwasha. Moja kwa moja alianza kumsoma tena Oscar Amari. Taarifa zote kuhusiana na maisha yake nchini humu zilikuwa fupi, ikionyeshwa tu kwamba alitokea Ghana kama mfanyabiashara na kukaa huku kwa miaka zaidi ya mitatu. Alijaribu kuunganisha vidokezo mbalimbali vyenye uhusiano kati ya Oscar na Kevin Dass, lakini kiukweli hakupata lolote.

Alikuwa na wasiwasi kuhusu hawa watu kwa sababu ikiwa Oscar aliweza mpaka kutoka kimapenzi na mdogo wake, basi wangeweza kuwa sehemu yoyote ile na kufanya lolote walilotaka. Ingawa alijua kuna siri nyingi zilifichika kutoka kwenye serikali yake mwenyewe, alitaka sana kuwafichua Mess Makers upesi ili matatizo haya yote yaishe haraka.



Baada ya muda fulani, ujumbe kwenye simu yake uliingia kutoka kwa Lexi. Akitabasamu kwa furaha, akachukua simu kuusoma, lakini akakuta Lexi amemwandikia kuwa amepatwa na dharura fulani ambayo ingempeleka nje ya mkoa, hivyo baadae hawangeweza kuonana. Ingawa hii haikuwa taarifa nzuri kwake, Nora akampa tu pole na kusema haikuwa na shida, na kumwambia amjulishe wakati ambao angerudi.

Halima aliingia ofisini humo akiwa amemletea Nora kiamsha kinywa. Nora akauliza kama yeye pia alikuwa anapata chai, lakini Halima akasema yeye angepata baadae. Nora akamwambia hapana; afate chai, aje wapate kiamsha kinywa kwa pamoja ofisini humo. Halima alikuwa mwenye kusita kiasi hasa kwa sababu hakutarajia "boss" wake mpya amtendee namna hiyo, lakini Nora akamsisitizia afanye hivyo upesi la sivyo asingekula chakula alichomletea.

Basi dada huyo akatii, na baada ya muda mfupi akaingia ofisini hapo ili kupata chai pamoja na Nora. Kulikuwa na sehemu yenye meza ndogo ya kioo na masofa mawili, hivyo wote wakaketi hapo na kuanza mlo. Nora alipiga story nyingi na mwanamke huyu, akipata kujua maisha yake kwa ujumla, amefanya kazi hapo kwa muda gani, na ikiwa ameolewa na ana watoto. Halima aliongea kistaarabu sana, na upesi Nora akapendezwa naye.

Katika maongezi yao wakiwa wanaendelea kupata chai, simu ya Nora iliita mara kadhaa, lakini alikuwa anaitolea sauti na kuipuuza kwa sababu mpigaji alikuwa ni Luteni Michael. Bado alikuwa na hasira naye, kwa sababu mwanzoni alimwona kama mwanaume anayeweza kuwa rafiki mzuri, lakini kwa kitu alichomfanyia Lexi ndani kwake hangeweza kusahau. Halima akamwambia Nora kwamba na yeye angependa kwenda kwenye mkutano wa leo ambao ungefanywa na Salim Khan, lakini hangeweza kwa sababu za kiofisi. Nora akamwambia asijali, kwa sababu angefanya mpango ili waende wote. Baada ya kumaliza msosi, Nora akarudi mezani kwake ili kuendelea na mambo mengine.

Haikupita muda mrefu sana, naye Halima akaingia ofisini humo tena akiwa ameshika faili moja. Akamwambia kuwa limeletwa na mwanajeshi mmoja hapo, na Nora alipolitazama akatambua lilitumwa kwake na Luteni Michael. Akamshukuru Halima na kumwambia aende. Halima akatoka hapo kurudi kwenye meza yake nje. Faili hilo lilikuwa na karatasi zenye taarifa fulani muhimu. Lakini alipolifungua tu, mbele hapo akaona kikaratasi chenye maneno "I'M SORRY NORA. I HOPE WE CAN TALK SOON," naye Nora akakibandua na kukikunja-kunja kisha kukirusha pembeni kwenye kopo la uchafu.

Alipoanza kupitia mafaili hayo, akaona zilikuwa ni baadhi ya taarifa kumhusu Lexi. Akatikisa kichwa chake kwa kusikitika, kwa sababu aliona ni kama bado Luteni Michael alizidi kumchokonoa pabaya. Akasoma tu mambo mengi yaliyoandikwa hapo, na ijapokuwa kuna vitu ambavyo Lexi hakuwahi kumwambia kumhusu vilivyokuwa hapo, Nora hakuiona hiyo kama sababu ya kumshuku. Akalifunga tu na kuliweka pembeni, naye akainamisha uso wake kwa kuuweka kwenye viganja vyake alivyokunja. Alikuwa akiwaza sana kwa nini Michael aliendelea kulazimisha mno aamini jambo ambalo hakutaka kuamini. Akanyanyua tu uso wake na kuamua kupotezea, kisha akaishika laptop yake ili kuendelea na mambo mengine.

Lakini akatulia kwanza baada ya jambo fulani kuingia kwenye akili yake. Akalichukua faili hilo tena, naye akasoma kwa makini zaidi. Ilikuwa bado haijaingia akilini mwake kuwa alisoma Lexi alitokea Ghana na kuja huku, vile vile na Oscar pia. Hii ikawasha kitu fulani kwenye akili yake. Akaanza kuwaza tena vipi kama jambo hilo lilimaanisha wawili hawa walikuwa na uhusiano wa aina fulani? Ingawa hakutaka kuamini hilo, kitu hiki kikaanza kuisumbua akili yake.

Alianza kutafakari jinsi ambavyo yeye na Lexi walikutana, mpaka kufikia leo ilikuwa ni kama aliingia kwenye maisha yake kwa wakati ambao ulikuwa SAHIHI kabisa kwake. Vipi kama kweli alikuwa mmoja wao? Akawa anatikisa kichwa chake kama kukataa kwamba hilo halingewezekana. Ila alipoanza kukumbukia maneno ya Luteni Michael, kwamba siku ile walipompata tu Oscar, Lexi aliingia ndani ya jengo lile la utafiti na ndipo mambo yao yakaharibika, mashaka yake yakaongezeka. Akachukua simu yake na kujaribu kumpigia Lexi, lakini hakupatikana.

Wasiwasi ukamwingia mwanamke huyu, mwingi sana. Akaendelea kukaa humo ofisini tu akitafakari mambo mengi sana kuhusu Lexi, akitumaini jambo hili lisingekuwa la kweli kumhusu.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Lexi alifika kule "chini" baada ya mwendo wa masaa kadhaa. Alipokelewa vizuri sana na Lakeisha pamoja na Torres, na wengine wakamwambia jinsi walivyomkosa sana. Walishangaa kiasi baada ya kuona ana jeraha dogo usawa wa mdomo na kuuliza alipatwa na nini, naye akasema aliumia tu kidogo lakini alikuwa sawa. Kevin alikuwa hapo pia, akiigiza kana kwamba amefurahi sana kumwona lakini kiukweli alichukia sana uwepo wake hapo. Ni moja kati ya wale watu wanaodharau sana wanawake, na kwa kuwa Lexi alipewa wadhifa fulani wa kuwa kama kiongozi kwao, hicho ni kitu kilichofanya ionekane ni kama yeye na wanaume wengine wanashushwa hadhi.

Baada ya wote kwenda kwenye chumba cha pamoja ili kuzungumza, Lexi akamkuta Kendrick tayari akiwa ameketi kwenye kiti cha mbele zaidi kwenye meza ndefu. Wakatazamana kwa sekunde chache, kisha Lexi akaangaliana na Torres, ambaye alimtikisia tu kichwa kumaanisha akakae, naye akaenda kuketi karibu na Lakeisha. Bado hali haikuwa sawa kati ya wawili hawa, na kiukweli Kendrick alikuwa anatamani sana kuzungumza na Lexi, ila ni kama alikuwa anajizuia tu. Lexi bado alikuwa na hasira naye, lakini hayo yangepaswa kuwekwa pembeni kwanza.

Torres akaanza kuwaambia kuhusu mahojiano yaliyopangwa leo kumwelekea Salim Khan. Wote walifahamu kuhusu milionea huyo kuiachia miradi mingi aliyokuwa ameishikilia kwenye serikali, na hiyo ilimaanisha huenda kulikuwa na ugomvi kwenye kundi lao la Raisi Paul Mdeme.

"Kwa hiyo inawezekana kwenye hayo mahojiano Salim akaropoka kila kitu, si ndiyo?" akauliza Victor.

"Sidhani sana. Hiyo inamaanisha kwamba kazi zake zote illegal zitawekwa wazi pia. Ni kwamba tu anataka kupata public opinion itakayokuwa upande wake, lakini ni wazi hili suala halijawafurahisha wenzake. Yeye kuondoa mkono wake kwenye mambo mengi kutamuumiza sana Mdeme, na kama mnavyojua, sifikirii Mdeme ataruhusu hilo litokee, ingawa haiko wazi kama atachukua hatua fulani," Torres akawaambia.

"Lakini Salim ana nguvu sana. Mdeme ataweza kumgusa?" akauliza Kevin.

"Mdeme hapana. Lakini vipi kuhusu Jacob na Weisiko?" akauliza Torres.

"Yeah... hao jamaa wanaweza wakafanya jambo fulani," akasema Mensah.

"Lakini hiyo inatuhusu sisi vipi? Kama ni kuuana wauane tu," LaKeisha akasema.

"Yes, ndiyo maana tuko hapa. Tunahitaji kujadiliana kujua watafanya nini. Ikiwa watamwacha, baadae tukijaribu kuwafichua itakuwa pointless kwa upande wa Salim, na ikiwa watachukua hatua fulani, basi... maybe... probably... hiyo itakuwa na faida kwetu. Lakini haimaanishi kwamba tunapaswa tukae tu tusubiri lolote maana hii kwa njia fulani inaweza ikatu-impact sisi pia," akasema Torres.

"Kwa hiyo tufanye nini sasa?" akauliza Victor.

"Kwa nini tu tusimtumie Mensah ampasue huyo mwanaume bichwa lake? Na hata hao wengine. Problem solved," akasema Kevin.

"Yeah, halafu mipango yetu yote iwe ya kazi bure," akasema Mensah.

"Mipango ipi? Sijaona jambo lolote likifanyika tokea Oscar alipo...."

"Kevin!" LaKeisha akamkatisha.

Kevin akatulia tu na kukunjia mikono yake kifuani.

Kendrick akamtazama Lexi kwa makini. Lexi alikuwa ametazama mezani akionekana kutafakari jambo fulani.

"Lexi..." Kendrick akaita.

Wote wakamwangalia Lexi. Yeye akageuza kichwa taratibu na kumtazama Kendrick pia.

"Unawaza nini?" Kendrick akamuuliza.

Lexi akatulia kidogo, kisha akasema, "Tutapaswa kwenda."

Wengine wakaanza kuangaliana.

"Kwa nini?" akauliza LaKeisha.

"Kwa sababu Torres yuko sahihi. Jacob na Weisiko hawataruhusu Salim afanye jambo hilo. Ni lazima watafanya kitu fulani leo kwa sababu Salim atakuwa sehemu vulnerable zaidi," Lexi akasema.

"Sehemu ambayo itakuwa na waandishi wa habari ni vulnerable?" akauliza Victor.

"Anamaanisha eneo zima," akasema Torres.

"Sasa kwa nini sisi tunatakiwa kwenda?" akauliza Victor.

"Kwa sababu ile ile ya Oscar. Ikiwa Mdeme alikuwa anataka tu kumkamata mmoja wetu lakini mtu mwingine akatokea na kumuua, hiyo inamaanisha ni Jacob au Weisiko ndiyo walikwenda kinyume naye," Lexi akasema.

Torres akaangalia pembeni na kusema, "Of course... sasa ninaelewa."

"Unaelewa nini?" akauliza Kevin.

"Ni Weisiko na Jacob ndiyo waliomtuma yule assassin kuwafata Oscar na Mensah. Hawataki tukamatwe tukiwa hai kwa sababu... wanaogopa tutaweka kila kitu wazi kuwahusu. Kwa hiyo inaonekana... aisee... Lexi una kichwa dada! Kila mara ambayo Luteni Michael atatukaribia basi huyo assassin anatakiwa kuwepo ili kuzuia tusishikwe, lakini tuuawe. Ndiyo maana hakumuua Luteni ila wenzake tu. Nilikuwa wapi kuona hilo?" Torres akaongea kwa utambuzi.

"Ulikuwa unakula LaKeisha tu," Mensah akasema.

LaKeisha akacheka kidogo.

"Kama Lexi yuko sahihi, basi huyo assassin atakuwepo leo kwa ajili ya Salim," akasema Torres.

"Oookay... kwa hiyo tunatakiwa tuwepo ili kumkamata huyo mpumbavu," akasema Victor.

"Yeah," akajibu Torres.

"Tuna uhakika gani kwamba hilo litatokea? Kwa sababu tu Lexi kasema?" Kevin akaongea.

"No. Ni kwa sababu ubongo wako uliojaa viazi haungeweza kamwe kufikiria mambo namna hiyo," LaKeisha akamwambia.

"Fanyeni Lexi anavyosema. Ni lazima huyo mtu tumkamate," Kendrick akaongea.

"Boss, tukienda tunaweza kuhatarisha usalama wetu wote," Kevin akamwambia Kendrick.

"Kwani nani amesema wewe unaenda?" LaKeisha akamuuliza.

Kevin akashangaa na kumwangalia Lexi.

"Kwa hiyo... nyie wote mtaenda, lakini mimi ndiyo natakiwa kubaki? Na mtatumia njia gani ya haraka wakati muda umeshaisha?" Kevin akauliza.

"Lexi atatupanga. Boss, file ulilotaka nimeshaliweka kwa flash, liko mezani kwako," Torres akasema huku akiondoka haraka.

Wengine pia wakaanza kunyanyuka. Kendrick alikuwa amefurahi sana kwamba Lexi alitokeza jambo jipya hapo, lakini akatulia tu na kuendelea kumwangalia.

Lexi aliposimama na kutaka kuuelekea mlango, Kevin akafika mbele yake kama kumzuia.

"Unajua kukaa huku nahisi ni kama adhabu, siyo kulindwa. Niruhusu na mimi nije na nyie leo. Tafadhali," Kevin akasema kwa sauti ya chini.

"Wewe tuliza tako lako huku bana," Mensah akamwambia na kumpita.

Lexi akataka kupita pembeni, lakini Kevin akamzibia njia tena.

"Kevin... we ni mjinga?" LaKeisha akamuuliza.

"Boss, Lexi, sikieni. Mimi kiukweli nime...."

"Kevin... mpishe," Kendrick akamkatisha namna hiyo.

"Boss!" Kevin akasema kinyonge.

Akamwangalia tena Lexi machoni, ambaye alikuwa anamtazama kiumakini sana, naye akampisha na kumwacha atoke.

"Asshole!" LaKeisha akamwambia hivyo na kutoka pia.

"Ahahahah... usicheze na huyo demu, atakuja akuzibe siku moja," Victor akamwambia pia huku akicheka, kisha naye akaondoka.

Kevin alibaki kumtazama Kendrick kwa njia ya kutaka aonewe huruma, lakini Kendrick akanyanyuka tu na kumpita bila kumsemesha lolote. Tokea mpango wake aliomshawishi Kendrick afanye ulipovurugwa na Lexi, boss wao huyo hakuwa amemsemesha lolote lile, ikionekana ni kama alimkasirikia kwa njia fulani kwa sababu ya kumsababishia utofauti na "binti yake" kipenzi. Jamaa akakunja ngumi kwa hasira sana, akiweka chuki kuu moyoni mwake, naye akajiahidi kwamba ni lazima angefanya kitu fulani kuhusiana na haya yote.


★★★★


Mkutano wa mahojiano maalum ambayo yangefanywa kuhusiana na milionea Salim Khan kuacha kuunga mkono mingi ya miradi ya serikali ulikuwa umewadia. Maandalizi mengi yalifanywa na waandishi wa habari walifika mapema kwenye ukumbi ambao yangefanyikia. Ilikuwa ni kwenye mida ya jioni sasa, huku giza likivizia kwa mbali kadiri ambavyo watu waliendelea kuongezeka. Kwa kawaida mambo kama haya yangefanywa pakiwa bado mchana, lakini kwa sababu zake Salim alitaka iwe jioni.

Viongozi kadhaa wa mkoa walikuwepo pia, naye ACP Nora alifika hapo pamoja na Halima ambao kwa pamoja walikaribishwa na Emiliana Ngoyi pamoja na Secretary Joachim. Nora alimweleza Joachim kwamba walipaswa kuwa macho kuelekea hafla hiyo kwa kuwa kwa njia fulani ilihusiana na utata wa Mess Makers waliokuwa wanaufuatilia, naye Joachim akamhakikishia kuwa mambo yote yangekuwa sawa.

Upande wa nje ndiko watu kadhaa walikuwepo wakipeana salamu na kuwakaribisha wengine waliofika hapo, na hatimaye wakafika wageni ambao hawakutarajiwa kufika. Ilikuwa ni Jenerali Jacob Rweyemamu, akiwa pamoja na Luteni Jenerali Weisiko, nao wakapokewa kwa shauku kama vile ndiyo walikuwa wageni rasmi. Jenerali Jacob hakuwa akionekana mara nyingi hadharani, hivyo kwa wengi kumwona hapa walijua bila shaka aliliona suala hili kuwa muhimu mno mpaka kuamua kuja. Baada ya baadhi ya watu kusalimiana nao, wawili hawa wakaelekea ndani pamoja kusubiri Salim afike hapo.

Kwa mara ya kwanza kabisa katika kipindi kirefu, Jenerali Jacob alikutana ana kwa ana na binti yake, yaani ACP Nora, nao waliangaliana kiufupi kutokea pande tofauti zenye viti kwa ajili ya wadau ambao wangekuwepo hiyo siku. Nora alimpuuzia upesi na kuketi tu pamoja na Halima, naye Weisiko akamsihi Jenerali Jacob akae pia kwa sababu huu haukuwa wakati mzuri sana kuingiza hisia hapo. Secretary Joachim hata akamtumia Nora ujumbe kwa simu kuuliza kama alijua Jenerali angekuja, lakini akakanusha na kusema hakutaarifiwa hilo. Uwepo wa baba yake hapo ulimkera sana, lakini kama kawaida yake akampuuzia tu na kuendelea kusubiri kilichompeleka.

Katika kundi la waandishi wa habari walioingia ndani ya ukumbi huo, LaKeisha pamoja na Victor walikuwepo pia. Walijichomeka ndani hapo na kujifanya kama walikuwa waandishi wa habari kutoka kituo fulani, na hii ilisaidiwa na vitambulisho bandia ambavyo Victor alitengeneza kwa ajili yao. Walikuwa na vifaa vidogo masikioni ambavyo vingesafirisha mawimbi ya sauti kwa wenzao kuwaambia yaliyoendelea ndani endapo kama kuna jambo lingetokea.

Upande wa nje wa jengo hilo la ghorofa, Lexi pamoja na Mensah walikuwa ndani ya gari ndogo aina ya Polo wakisubiri kutokea umbali mfupi. Ni wawili hawa tu ndiyo waliokuwa ndani ya mavazi yao ya mapambano, tayari kabisa kuonyesha vitendo wakati ambao shida zingeanza.

★★

Haukupita muda mrefu sana, na hatimaye Salim Khan akawa amefika eneo hilo. Alilindwa na watu wenye silaha nzito na waliokuwa na mwonekano wa kikomando, nao wakamsindikiza alipoingia kule ndani ya ukumbi. Lexi aliwakumbusha LaKeisha na Victor kwamba walipaswa kuangalia sehemu za pembeni za eneo hilo la ndani kuona ikiwa wangepata kitu ambacho hakijakaa sawa, na Torres, ambaye alikuwa amebaki kule "chini" awe macho kwenye mitambo yake ili kumpa habari yoyote yenye kuvuta uangalifu.

Basi, baada ya Salim Khan kufika ndani kule na kupokelewa na wengi, akawatazama Jenerali Jacob na Weisiko, ambao wao walikuwa wamekaa tu wakimwangalia kwa kutopendezwa, naye Salim akachekea pembeni na kupanda sehemu iliyokuwa kama jukwaa dogo lenye meza ndefu. Akaketi kiti cha kati na kuanza kutoa salamu tena kwa wote, kisha akaanza kuongelea kuhusu mafanikio ambayo yeye na kampuni zake zimeiletea nchi hii kwa miaka mingi.

Waandishi wa habari walipokuja kupewa fursa za kuanza kuuliza maswali, wengi waliuliza maswali ambayo yalikuwa yanalenga ni kwa nini sasa Salim aliamua kuiachia miradi mingi ambayo bila shaka ingeporomoka kwa kuwa kipindi hiki kilikuwa kigumu hasa kwa sababu ya Mess Makers. Salim akaeleza kwamba kwa miaka mingi amejitahidi sana kuwekeza chochote alichoweza kwenye serikali na kusaidia katika maendeleo, lakini kama tu ambavyo hali imekuwa ngumu kwa serikali wakati huu, imekuwa ngumu kwake pia. Akasema kwa kujitutumua kuwa ni kama tokea wakati ambao Mess Makers wameizingua serikali yeye ndiyo aliyebaki kuibeba, na sasa kuna watu ambao wanachukulia hiyo kwa faida mbaya sana na kumbebesha mizigo mizito mno.

Maswali mengi yalizuka. Wengi waliuliza ina maana Raisi alikuwa ameshindwa kurekebisha hali? Kwa nini amtegemee Salim wakati yeye ana nguvu kubwa akiwa kiongozi wa nchi? Na ni kwa nini hakuwa hata ameomba msaada kutoka nje kuhusu kuwatafuta na kuwadhibiti Mess Makers? Aliogopa nini? Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko waliona kwamba Salim Khan alifanya haya yote kama kuwakomoa wao na kundi lao ambalo jamaa ndiyo alikuwa anatengeneza njia ya kulivuruga.

Waandishi wa habari walipokuwa wakiendelea na maswali huko ndani, Lexi pamoja na Mensah wakasikia sauti ya helicopter ikipita eneo hilo. Giza lilikuwa limeshaingia, lakini wakaiangalia kwa umakini kuona ingeelekea wapi. Ilipita karibu kabisa na jengo hilo walilofanyia mkutano ule, kwa juu, nayo ikaelekea upande mwingine tofauti. Lexi akamjulisha Torres kuwa kuna helicopter imetoka kupita hapo muda siyo mrefu, atafute ni ya wapi na rubani angekuwa nani kabla haijaharibiwa.

Torres akauliza ni kwa nini Lexi alifikiri helicopter hiyo ingeharibiwa, naye akamwambia inaonekana ilimshusha mtu kule juu, labda mtu wao yule waliyekuwa wanamtaka, hivyo bila shaka watu hao wangejitahidi kuharibu jambo lolote ambalo lingeweza kutumiwa kama ushahidi, lakini yeye Lexi alichotaka hasa kujua ni ilikokuwa imetokea. Lexi pamoja na Mensah wakawataarifu LaKeisha na Victor kuhusu jambo hilo na kuwaambia wawe macho sana, kisha wawili hawa wakafunika sura zao, Mensah akibeba bastola yake, nao wakaanza kuelekea karibu zaidi na jengo lile.

Ilikuwa ni wakati huu ndipo Salim Khan alisema kiutani kwamba alihitaji "dinner" kwanza, hivyo angeenda kupata chakula halafu angerudi wakati mwingine kujibu maswali mengi zaidi, naye akanyanyuka na kuanza kuondoka. Waandishi wengi bado walikuwa na maswali kama yote, wakiendelea kuuliza na kumfuata, huku Salim akiondoka pamoja na walinzi wake. Alielekea mpaka kwenye lifti na kuingia na walinzi wake, kisha wakaanza kupanda ghorofa za juu. LaKeisha akamwambia Lexi yaliyokuwa yanaendelea, naye Lexi akatambua kwamba mtu yule bila shaka angekuwa ameingia kwenye sehemu ya lifti. Akawaambia LaKeisha na Victor waondoke huko haraka ili wajiunge na Mensah kwenye gari kubadili mavazi, wakati yeye akitangulia kumfata.

Lexi alikuwa sahihi kabisa. Kwa sababu ni "silaha" yule wa Weisiko ndiyo alikuwa amefika huko, naye aliingia upande wa juu wa lifti kwenye nyaya nene zilizoiendesha. Wakati lifti ilipokuwa bado ikisonga kuelekea juu, akachukua mtungi mdogo sana wa gesi fulani na kufungua mlango wa juu wa lifti hiyo, kisha akaifungua sehemu ya gesi hiyo na kuitupia kwa ndani. Salim na walinzi wake walishtuka sana. Waliangalia juu na kutoona chochote kwa kuwa gesi hiyo ilijaza moshi mzito na kuwamaliza nguvu kabla hata hawajafikiria kufanya lolote. Wote wakaanguka na kupoteza fahamu zao ndani ya lifti hiyo iliyokuwa imebakiza hatua chache tu kufika ghorofa ya mwisho.

"Silaha" huyo akafungua mlango huo mdogo wa juu, yeye akiwa amevaa kizuizi cha kuingiza gesi puani na mdomoni, kisha akaingia ndani hapo haraka akiwa ameshika kamba nene iliyofungwa kama kitanzi mwishoni na kuipitisha shingoni mwa Salim. Alipoangalia zimebaki ghorofa ngapi, akaona imebaki moja na mlango wa lifti ungefunguka, hivyo akawahi kupanda juu kule upesi na kuuacha mlango ule mdogo wa juu wazi, naye akapanda juu zaidi, kisha akatoa kifaa fulani kidogo cha kukata chuma kutoka kwenye mkanda wake kiunoni na kuanza kuzikata nyaya zile zilizoishikilia lifti.

Wakati lifti ilipokuwa imefika tu mwisho na kufungua milango yake, kulikuwa na watu watatu hapo nje wakisubiri kuingia, nao wakashangaa sana baada ya kuona mambo yote ya ndani hapo. Walitambua watu waliokuwa wamelala humo walikuwa ni walinzi, na aliyewekewa kitanzi shingoni alikuwa ni Salim Khan. Mmoja akasema kwa wengine wawahi kuita msaada, lakini ikawa kuchelewa. "Silaha" yule alikuwa ndiyo amemaliza tu kukata nyaya nene ya mwisho, hivyo lifti hiyo ikaachia na kuanza kurudi chini kwa kasi sana!

Kamba ile aliyomfungia Salim shingoni ilikuwa imefungwa huko huko juu, hivyo lifti ile ilipoachia, kamba hiyo ikamning'iniza Salim kwa njia ya kunyonga. Hii ilifanya sehemu ya mkono wake wa kushoto ivunjike (yaani kukatika kabisa) kwa sababu mwili wake ulikuwa mnene kiasi na hivyo lifti iliposhuka na yeye kuvutwa, alipitishwa kwenye mlango ule mdogo wa juu na kubaki amening'inia.

LaKeisha pamoja na Victor walikuwa tu ndiyo wamefika nje, pale waliposikia sauti ya kishindo kikubwa sana kutokea kule ndani. Kiliwashtua wengi sana, na baadhi ya waandishi waliokuwa nje tayari wakaanza kurudi ndani tena. Victor akamtaarifu Lexi kuhusu hilo, naye Lexi akasema abaki kujua ni nini, lakini LaKeisha amfate Mensah kisha wamsubiri Victor mpaka atakapotoka kule ndani. Lexi tayari alikuwa amezungukia upande mwingine wa jengo peke yake, akiwa mwangalifu sana ili asitambulike. Alitazama kule juu kwa umakini kutokea alipokuwa, naye akamwona mtu yule akiruka kutoka juu ya ghorofa hilo mpaka kwenye ghorofa lililokuwa jirani. Lexi akasema amemwona na angeanza kumfata, hivyo Torres awaongoze Mensah na Lakeisha kuhusu kule ambako angekwenda baada ya Victor kujiunga nao. Alikimbia kwa kasi sana na kuvuka njia nyingi ambazo kufikia wakati huu hazikuwa na watu wengi sana kwa sababu ya wengi kwenda kujua kishindo kile kilitokana na nini.

Wakati Lexi akiwa bado anakimbilia upande wa adui, Victor aliwataarifu wenzake wote sasa kuwa Salim Khan aliuliwa kwa kunyongwa ndani ya lifti, na lifti hiyo ilikatwa na kuangushwa mpaka chini ikiwa na wanaume sita wa ulinzi ndani yake, nao pia wakiwa wamekufa baada ya kuvunjwavunjwa kwa viungo vyao. Taarifa hiyo haikuwa nzuri au mbaya kwa Mess Makers, kwa sababu lengo lao hapa lilikuwa ni huyu mtu asiyejulikana ambaye alimuua Oscar, hivyo Torres akamwambia Victor ajiunge na wenzake ili wakamsaidie Lexi.

Lexi alifanikiwa kumwona mtu yule akishuka kutoka kwenye ghorofa lingine na kuanza kukimbilia upande ambao Lexi alijua kulikuwa na uwanja mpana wa mazoezi, naye akaongeza kasi na kumzungukia kwa mbele. Kule "chini," aliyekuwa amebaki pamoja na Torres ni Kendrick na Kevin, nao walikuwa wakifuatilia kila jambo kwa umakini pia. Kendrick akamuasa Lexi awe makini sana kwa sababu iliwezekana huu kuwa mtego, naye Lexi akasema angekuwa makini.

"Silaha" yule alifika sehemu ya pembezoni ya uwanja huo na kusimama huku akiwa anapumua kwa nguvu sana. Usiku huu alivalia nguo zile nyeusi kama kawaida yake, lakini wakati huu kiziba uso chake kilikuwa kwenye uso mzima na kuacha sehemu ndogo tu kwa ajili ya macho. Wakati akiwa ametulia hapo akisubiri jambo fulani, akahisi mtu akija nyuma yake, naye akachomoa kisu kutoka kwenye mkanda kiunoni kwake haraka na kukirusha upande huo wa nyuma. Lakini ilikuwa ni Lexi, naye akakikwepa na kumrukia mtu huyu na wote kuanguka chini, kisha wakasimama na kuangaliana wakiwa wamejiweka tayari kupambana.

Hii ilikuwa ni mara ya tatu wanakutana, na Lexi alikuwa anataka kuifanya iwe mara ya mwisho. Alikuwa na lengo moja tu hapa, kumlipizia kisasi Oscar kwa kile ambacho mtu huyu alimfanyia, na kisha kukikata kichwa chake na kukituma kwa Jenerali Jacob kama ujumbe kuwa akicheza vibaya na Mess Maker mmoja, amecheza vibaya na wote. Bila kusubiria refa aitwe, Lexi akamfata mtu huyo na kuanza pambano naye. Walikuwa wanapigana kwa njia zenye ustadi sana, na kila mara ilionekana ni kama hawangeweza kuumizana kwa sababu kila mmoja wao alijua kuyazunguka mapigo ya mwenzie.

Lexi alitambua kuwa mtu huyu alipigana kwa mtindo fulani wa "Tai chi," hivyo yeye akaanza kutumia mitindo mingi yenye kuchanganya kwa wakati mmoja. Mtu huyu alikuwa akitafuta njia nyingi sana za kumpiga Lexi kwa mtindo ule unaowamaliza nguvu maadui zake, lakini akagonga mwamba. Ijapokuwa mtu huyu alifanikiwa kumpiga Lexi hapa na pale, Lexi alimpiga chenga nyingi haswa na kufanikiwa kumtandika sehemu fulani za mwili zenye udhaifu, na mtu huyu akaanza kuonekana kuishiwa ujanja. Akatoa kisu na kutaka kukitumia kumkata tumboni, lakini Lexi akazungusha mikono yake na kumpiga kwa teke mgongoni, kisha akamfata na kumkaba shingoni akiwa nyuma yake. Alikuwa na hasira sana, na baada ya kuona nguvu zinamwishia mtu huyu, akamrusha pembeni na kubaki akimwangalia huku anapumua kiuchovu.

Wakati Lexi alipokuwa amemrusha mtu huyo namna hiyo, ilifanya kificha uso cha mtu huyo kidondokee pembeni, naye akawa anajivuta chini taratibu kama anatambaa kwa tumbo kuelekea mbele, kwa hiyo bado Lexi hakuwa ameiona sura yake. Lakini alipoanza kumfata taratibu, akatambua kuwa nywele za mtu huyo zilikuwa ndefu na laini, zilizobanwa nyuma ya kichwa chake kwa njia iliyomfanya Lexi atambue kuwa huyu alikuwa mwanamke. Akaokota kiziba uso chake kile, kisha akamsogelea karibu zaidi na kumponda nacho kisogoni. Mtu huyo hakugeuka, naye Lexi akatambua kuwa hakutaka aione sura yake, hivyo akamkalia mgongoni na kuvuta nywele zake kwa nguvu sana. Mwanamke huyu akatoa sauti ya maumivu kidogo na kujaribu kufurukuta, lakini Lexi akamdhibiti.

"I'm going to kill you the same way you killed my friend (nitakuua kwa njia ile ile uliyotumia kumuua rafiki yangu)."

Lexi akanong'oneza maneno hayo kwenye sikio la mwanamke huyo, naye akakishika kichwa chake na kutaka kukinyonga kwa nguvu, lakini mwanamke huyo akatumia wepesi wake kuugeuzia mwili upande ambao Lexi aliipeleka shingo yake, hivyo sasa akawa amelalia mgongo wake. Lexi alikuwa ameweweseshwa kidogo kutokana na hilo, lakini akamwahi tena na kuikaba shingo yake kwa kiganja kimoja, huku akitaka kumtandika ngumi usoni kwa kingine, pale mkono wake ulipoganda hewani tu baada ya kutokuamini kile alichokiona. Yaani hakuamini kabisa macho yake. Alimwangalia mwanamke huyu kwa mshangao wa hali ya juu, asiamini na asiamini kwamba kweli alichokiona kilikuwa halisi. Mkono aliokuwa ametumia kumkaba shingoni ukalegea, na ngumi yake ikashuka. Alihisi kuishiwa nguvu ghafla kwa sababu hakutegemea jambo hili hata kidogo.

"Azra?!"

Lexi akaita hivyo kwa sauti ya chini, yenye kuonyesha hisia sana. Mwanamke huyo akakunja uso wake kimaswali, naye akakusanya nguvu na kumsukuma Lexi ambaye alidondokea pembeni yake. Lexi akajivuta chini hapo na kuendelea kumwangalia kimshangao, huku mwanamke huyo akijishika shingoni akiwa anamwangalia adui yake kwa hasira.

"Azra... A... Azra..."

Lexi akaendelea kuita jina hilo, kwa sababu mwanamke huyu alikuwa na sura kama ya mdogo wake wa kike, ambaye alijua miaka mingi iliyopita alipoteza uhai pamoja na watu wengine wa familia yake. Alishindwa kuelewa nini kilikuwa kinaendelea, na mwanamke huyo akasimama na kubaki anamwangalia Lexi kimaswali. Lexi alielewa kwamba hangeweza kumtambua yeye ni nani kutokana na kiziba uso chake usoni, hivyo naye akasimama na kuanza kukitoa. Mwanamke huyo alikuwa anamshangaa sana kwa nini anafanya yote hayo, na baada ya Lexi kuivua mask yake, akamkazia macho kwa uangalifu.

Lexi alikuwa anamwangalia kwa matumaini mengi, akifikiria huenda huyu alikuwa ni mdogo wake, na labda kumwonyesha sura yake kungebadili mambo, lakini haikuwa hivyo. Mwanamke huyo akakunja uso na kuanza kumfata tena, kisha akaendelea kumshambulia.

"No... Azra... subi.... wait...."

Lexi akawa anajitahidi kukwepa mapigo yake na kumwambia aache ili waongee, lakini ilionekana ni kama wehu ulikuwa umempanda mwanamke huyo kwa sababu hakutaka kusikiliza. Lexi hakuelewa kwa nini mdogo wake hakumtambua, na hii ilimfanya ahisi simanzi nzito moyoni mwake. Mwanamke huyu akafanikiwa kumpiga Lexi sehemu za viwiko na mabegani kwa mtindo wake ule uliomfanya apoteze nguvu mikononi, naye Lexi akapiga magoti chini. Mwanamke huyo akaokota kisu na kutaka kumchoma nacho, lakini Lexi alipomwangalia usoni kwa huzuni, mwanamke huyo akasita kidogo. Alibaki kumtazama Lexi kimaswali sana, huku Lexi akidondosha machozi kwa hisia.

"Lexi!"

Wawili hawa wakashtushwa na sauti hiyo kutokea upande ule walikotokea mpaka kufikia uwanjani hapo. Ilikuwa ni LaKeisha ndiye aliyeita hivyo, na baada ya Lexi kugeuka akamwona Mensah akiwa ameelekeza bastola yake kwa mwanamke huyu aliyekuwa na sura ya mdogo wake, hivyo akajitahidi kusimama upesi na kumziba. Risasi mbili alizofyatua Mensah zilimpata Lexi kifuani, lakini hakuumia kutokana na nguo yake kuzizuia, naye akadondoka chini tena.

Mwanamke huyo akashangaa sana baada ya kuona jambo alilofanya Lexi, lakini akageuka hapo hapo na kuanza kukimbilia upande mwingine, na Mensah alipotaka kumpiga risasi zingine, Lexi akamwambia kwa sauti ya juu kuwa amwache. LaKeisha na Victor wakafika hapo chini na kujitahidi kumnyanyua Lexi, huku wakimwangalia mwanamke yule anatokomea gizani. Mensah alipofika karibu akamuuliza Lexi ni nini maana yake kumzuia asimpige adui yao huyo na kumwacha atoroke, naye Lexi akabaki tu kupumua kiuchovu huku akiwa amechoka sana kiakili.

Alijiuliza sana swali hili: Iliwezekanaje Azra kuwa hai?




★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

Hapo ndiyo hitimisho la msimu wa pili wa FOR YOU. Sehemu zitakazofuata zinaanzisha msimu wa tatu. Karibu ujipatie full season 3, bado ni ndefu sana.

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Kwa akili ya haraka, Omari akapinda mgongo, naye Hussein akarudi nyuma kisha kukimbia kwa kasi na kudunda kwenye mgongo wa Omari, akiruka sarakasi hewani na kujirusha mpaka upande wa ndani. Nathan Masunga bado alikuwa hapo na kushtuka baada ya kuona hilo, hivyo akaanza kukimbia kuelekea kwenye nyumba. Hussein akanyanyuka haraka na kufungua mlango wa geti, kisha kwa kasi akaanza kumkimbiza Nathan huku wenzake wakiwa wanakuja kwa nyuma pia. Alifanikiwa kumwahi kabla hajaufunga mlango wa ndani na kumsukuma kwa nguvu mpaka akaanguka chini. Ndani hapo palikuwa pazuri sana, pakipangiliwa vyema na vitu vingi vikiwa vya gharama.

Nathan alikuwa mwanaume mwenye miaka 50, naye alikuwa mfupi na mwenye kitambi kiasi. Akawa anajisogeza nyuma akiwa anamwangalia Hussein kwa hofu, na ndipo Luteni Michael na wengine wakaingia pia. Vedastus na Omari wakaelekea sehemu za jikoni na vyumbani ili kuona ikiwa kulikuwa na mtu yeyote, huku Luteni Michael na Hussein wakimzingira mzee huyo.

"Una mbio kwa mtu aliyevunjika mguu na mwenye kitambi!" Luteni Michael akamwambia.

Hussein akacheka kidogo.

"Tafadhali msiniumize... mimi... mimi..."

"Wewe nini?" Luteni Michael akamuuliza.

Nathan akawa anapumua tu kwa kutetemeka. Vedastus akarejea kutokea chumbani akiwa amemshikilia mwanadada wa miaka kama 20 hivi, akiwa amevalia khanga moja kutokea kifuani, kisha akamwachia alipomfikia Nathan na yeye kukaa karibu na mzee huyo huku akiogopa. Ni bunduki zao hasa ndiyo zilizowaogopesha sana.

"We pimbi... kwa nini umekimbia? Unatujua sisi?" Luteni Michael akamuuliza.

"Ha..hapana..." Nathan akajibu.

"Huyu ni nani? Mke wako?" Luteni Michael akauliza tena.

Nathan akatikisa kichwa kukataa.

"Ni nani sasa kama siyo mke wako?" Omari akauliza.

"Ni... dada wa kazi," Nathan akajibu.

Omari na Hussein wakacheka.

"Mzee mzima unakosa busara kula vischana vidogo? Halafu eti hawa ndiyo wenye pochi kubwa nchini... ona wanayoyafanya!" Vedastus akasema kwa kukerwa.

"Ninakupa sekunde 15 unieleze ni kwa nini umetukimbia, kwa nini hujavunjika mguu, na kwa nini mliiba zile pesa na wapumbavu wenzako," Luteni Michael akasema.

"Nini?" Nathan akauliza.

"Omari..." Luteni Michael akaita na kuitoa bastola yake.

"Moja... mbili..." Omari akaanza kuhesabu.

"Subiri, subiri, subiri, nita..nitakwambia kila kitu. Ona... mimi jamaa alinipa tu hela ili nisiende kazini siku hiyo lakini sijaiba pesa mimi... nakuapia kijana wangu!" Nathan akasema kwa hofu.

"Unamaanisha nini?" Luteni Michael akauliza.

"Yaani... mimi... nililipwa tu nisiende work... ndiyo nikaja kusikia kuhusu hiyo kitu... basi. Ni hivyo tu..."

"Ongea kama mtu mwenye akili anayejua akisema utumbo, ubongo wake utapasuliwa," Luteni Michael akamtisha kwa kumnyooshea bastola kichwani.

"No, no, no... ona... naapa kabisa kwa jina la Mungu sijaiba pesa. Haki ya Mungu. Mimi mwenyewe nilishangaa sana alipofanya hivyo hata sikuelewa..." Nathan akasema kiuoga.

"Ni nani huyo?" Hussein akauliza.

"Ni kijana fulani hivi. Nilikuwa naenda kwenye club moja hivi... nilikutana naye huko. Baadae tukajenga urafiki maana alionekana kuwa na pesa na alinisaidia kwa mambo ya hapa na pale... akawa kama rafiki yangu. Ndiyo baadae tulikuja kucheza mchezo fulani wa ku-bet mimi na yeye. Akaniambia nikipoteza basi siku fulani niache kwenda kazini na yeye akipoteza angenipa pesa nyingi. Alipopoteza... akanipa pesa... akasema angenipa double kabisa kama ningethubutu kuacha kwenda kazini siku hiyo ambayo ndiyo wale jamaa walikuja kuiba... lakini mimi sikuelewa kabisa maana yake wala nini... kwa hiyo nikakubali tu na yeye akanipa..." Nathan akaeleza.

"Alikupa shilingi ngapi?" Luteni Michael akauliza.

"Mwanzoni alinipa milioni 2, halafu akaniongezea milioni 3 zingine. Ana pesa sana huyo kijana inavyoonekana maana nilikuwa namwona hata kwenye kamari..."

"Tulia. Yaani wewe mtu mzima unakubali kupokea pesa yote hiyo ili tu uache kwenda kazini? Unatuona sisi mafala eti?" Luteni Michael akasema kiukali.

"Hapana, hapana, siwadanganyi jamani! Ni kweli! Mimi... nilipokea kwa kuwa sikuona noma, na nilikuwa namwamini maana alikuwa tight sana nami mpaka kufikia wakati huo na...."

"Anaitwa nani?"

"Aaa... Erick... anaitwa Erick..."

"Una picha yake?"

"Hapana. Hatukuwahi kupiga picha..."

"Marafiki hao!" Hussein akasema.

"Unajua kwamba unahusishwa na wizi wa matrilioni ya pesa kwa sababu hiyo? Nieleze ni kwa nini inasemwa ulijeruhiwa na kuvunjika mguu wakati hapa umetoka kukimbia kama swala anayewindwa. Au labda ni mguu mwingine ndiyo umevunjika?" Luteni Michael akauliza.

"Sidhani, maana ndiyo alikuwa ametoka kuuingiza kwenye shimo la huyu binti," Vedastus akasema.

"Hivi kwanza umemkuta kavaa khanga au suti yake ya kike tu?" Hussein akauliza kiutani.

"Vyote!" Vedastus akajibu, naye Hussein akacheka.

"Nijibu," Luteni Michael akamwambia Nathan.

"Mimi ndugu nilikaa tu nyumbani siku hiyo kumridhisha jamaa. Tena kiukweli nilimwona kama mtu aliyelewa kwa sababu hicho kitu alichoniomba nifanye hakikuwa kizito kwangu. Ningeenda tu kazini siku iliyofuata na kusema nilipatwa na tatizo fulani, basi. Sasa... nilipokuja kusikia wizi umetokea nilishangaa sana, nikajiuliza kama huyo jamaa aliniseti au aliniokoa, yaani sikuelewa. Nikaamua tu kukaa kwanza nyumbani nisikilizie nini kingefuata, ndiyo baadae wakaja watu hapa kwangu wakaniambia nilipaswa kukaa hapa hapa nisitoke kabisa..."

"Wakina nani?" Luteni akauliza.

"Ni... watu fulani kutoka serikalini sijui... walionekana kuagizwa na mtu wa majuu. Wakaniambia nikae na nikitafutwa nisiseme lolote kwa yeyote yule mpaka wao wanitafute..."

"Lengo lao lilikuwa ni nini?"

"Sijui kijana wangu. Mimi hata hawakuniuliza nilikuwa wapi siku ile, wakaniambia tu nifanye hayo la sivyo... la sivyo ningeumia. Kwa hiyo nikakubali tu..."

Wanajeshi wakaangaliana kwa ufupi.

"Na huyo Erick?" Luteni Michael akauliza.

"Erick sikumwona tena tokea hapo. Yaani hata tu ile kunipigia simu hakunipigia ijapokuwa mimi mara nyingi nilijaribu kumtafuta lakini... sikumpata tena..."

Luteni Michael akarudisha bastola yake kiunoni.

"Familia yako iko wapi Nathan?" Vedastus akamuuliza.

"Nilitalikiana na mke wangu mwaka jana. Wanangu wako shule Tanga na Mwanza, kwa hiyo hapa niko peke yangu..."

"Siyo peke yako fala wewe, huyo ni paka au?" Omari akamwambia Nathan, akimaanishia dada wa kazi.

"Unaikumbuka sura ya huyo Erick vizuri?" Luteni Michael akamuuliza.

"N..ndiyo... namkumbuka," Nathan akajibu.

"Sasa nisikilize. Unakuja pamoja nasi kusolve hii ishu. Nenda kavae," Luteni Michael akamwambia.

"Lakini, lakini... sitakiwi kutoka! Nikitoka wanaweza wakani...."

"Hawatakufanya chochote. Sisi tutakulinda. Na ninataka nijue ni nani anayekuandama namna hiyo, kwa hiyo wewe utakuwa mwaliko mzuri ili waje kwangu. Kavae," Luteni Michael akasema.

Nathan Masunga akanyanyuka huku akionyesha unyonge, kisha akaanza kuelekea chumbani akifuatwa na Omari. Mwanadada yule akawa amebaki hapo na khanga yake akiangalia chini tu.

"Na huyu tunamfanyaje?" Vedastus akauliza.

"Tunamfanya," Hussein akajibu kimasihara, na mdada huyo akamwangalia.

"Unaitwa nani?" Luteni Michael akamuuliza dada huyo.

"Saida..." akajibu.

"Karoli?" Hussein akauliza kiutani.

"Umeanza kutoka na huyo mzee tokea kipindi gani?" Luteni Michael akamuuliza.

"Kabla... kabla hata hajatalikiana na mke wake," Saida akajibu kwa hofu.

Wanajeshi wakatikisa vichwa kwa kusikitika.

"Simama..."

Luteni Michael akamwambia hivyo, na binti huyo akasimama.

"Tunaondoka na huyo mtu wako. Wewe utakaa hapa mpaka atakaporudi. Fanya mambo yako hapa, fanya usafi, pika, angalia TV, masturbate kidogo, lakini usiondoke hapa, na usiongee na yeyote kuhusu yaliyotokea humu, la sivyo tutajua na tutakufunga. Umeelewa?" Luteni Michael akamwambia kwa kumtisha.

Saida akatikisa kichwa chake kukubali. Kisha Luteni Michael akamwambia aende chumbani kwake kuvaa pia. Saida akaondoka haraka haraka huku wanaume wakiangalia jinsi kalio lake lilivyotikisika kwenye khanga kwa nyuma.

Hussein akawa anachekea kwa chini, kisha akamwambia Luteni Michael, "Eti masturbate kidogo..."

Vedastus akacheka kidogo pia.

Nathan Masunga akarejea akiwa amevaa shati jeupe na suruali nyeusi ya kitambaa, pamoja na viatu vyeusi akionekana kama anakwenda ofisini. Ni hapa ndipo Luteni Michael akatafutwa na Mario, ambaye alimwambia kwamba hawakupata jambo lolote lenye nuksi upande wao walikoenda kwa Eunice Shirima. Luteni Michael akamwambia kwamba wao walipata, hivyo walikuwa wakijiandaa kurudi kule kwa Bobby. Mario akasema kwamba walikuwa wamepita hotelini na ACP Nora na Mishashi kupata kiamsha kinywa kwanza, hivyo wangewakuta huko baada ya muda fulani.

Luteni Michael akakata simu na kumpigia Bobby, kisha akamwambia atafute msanii mzuri wa uchoraji (sketch artist) kutoka katika vitengo vyao, ampeleke hapo ili wakutane na Nathan Masunga. Mpango wake ulikuwa kwamba Nathan aseme jinsi alivyoikumbuka sura ya huyo Erick, waichore kwa kutumia vifaa maalumu vya mchoraji huyo, kisha waweze kujua huyo Erick ni nani hasa.

Baada ya hayo, Luteni Michael akawaambia wenzake kwamba angewapeleka pamoja na Nathan mpaka kule, kisha yeye angekwenda kusuluhisha tatizo lolote ambalo lingejitokeza kutokana na Bobby kuingia kimarufuku kwenye mifumo ya kiteknolojia ya Ikulu. Alipanga kuongea na Kanali Oswald uso kwa uso ili amweleweshe ni kwa nini aliruhusu mmoja wa watu wa timu yake wafanye hivyo, na ili Kanali Oswald asaidie kumsafishia njia endapo watu wa Ikulu wangemzingua. Kwa hiyo wote wakaondoka hapo baada ya kuelewana.

★★

Walifika kule jengoni kwa Bobby na kumpeleka Nathan ndani, kisha Luteni Michael akaondoka kama alivyodhamiria. Bobby tayari alikuwa amefanya mpango wa kumleta mchoraji hapo, hivyo bwana Nathan akakaa kusubiri. Baada ya dakika kadhaa, ACP Nora, Mario, na Mishashi wakawa wamefika pia, wakiwa wamewaletea na wengine vyakula vyepesi. Nora akaketi na Nathan ili kuzungumza naye kiufupi, akimuuliza mambo mengi kuhusiana na utata huu, naye Nathan akatoa kila kitu alichofahamu. Nora alimwona kuwa aina ya mtu anayejitanguliza yeye kwanza na pesa tu maishani badala ya masilahi ya wengine, na baada ya kumhoji moja mbili tatu, akaketi na Bobby kuendelea na tafiti zingine.

Mchoraji waliyekaa kumsubiri alichukua muda mrefu sana bila kufika hapo, mpaka inafika saa 10 jioni bado hakuwa amefika. Luteni Michael akawa amerejea jengoni hapo muda huo, naye akawaambia kwamba suala la ku-hack Ikulu alikuwa amelisafisha tayari hivyo hawakupaswa kuwaza tena. Alipouliza kwa nini mchoraji hakuwa amefika, Bobby akamjulisha kuwa alisema yuko njiani lakini kwa sababu zisizojulikana bado hakuwa amefika. Kwa hiyo Luteni Michael akawaambia watu wake wakapate chakula kwanza, na waende pamoja na Nathan ili kumpa chakula pia. Yeye tayari alikuwa amekula, hivyo angekaa kusubiri mchoraji afike. ACP Nora, Mishashi, pamoja na Alex wakabaki pia kwa kusema hawahisi njaa, hivyo wakawa hapo kubadilishana mawazo ya hapa na pale.

Muda mfupi kutokea hapo, mchoraji huyo akawa amefika. Alikuwa mwanaume wa makamo, mrefu, na alionekana kuwa mstaarabu sana. Akaeleza kwamba gari lake lilipatwa na shida njiani na hiyo ndiyo sababu iliyomchelewesha sana. Moja kwa moja akaelezewa kwamba alihitajika kumchora mtu ambaye alikuwa akifuatiliwa na jeshi, lakini mwenye kumpa vielelezo alikuwa ametoka kidogo kwenda kula hivyo angepaswa kumsubiri arejee. Mchoraji huyo aliitwa Samuel, naye akakubali na kusubiri hapo huku akiongea mawili matatu na wenyeji aliowakuta.

Nora aliangalia simu yake na kukuta ujumbe mfupi kutoka kwa Lexi, ambaye aliuliza ikiwa yuko huru ili wakutane kule kupiga glasi mbili tatu za wine. Nora alikuwa ameshaanza kutabasamu tu baada ya kuona ujumbe huo, naye akamwambia kuwa angefika huko bila shaka, akijua uchoraji huu ungechukua muda. Hivyo akamwambia Luteni Michael kwamba alitaka kwenda sehemu fulani, na kama angekuwa hajarudi kufikia muda ambao wangekuwa wamekamilisha uchoraji basi angemjulisha ili afike haraka. Luteni hakuwa na kipingamizi, naye Nora akaondoka hapo upesi.

Ilikuwa imeshatimia mida ya saa 11 kabisa, naye Nora akaamua kwenda hotelini alikokaa ili kujimwagia tena na kubadili nguo. Yaani hakujua ni kwa nini lakini alianza kuchukulia kukutana kwake na Lexi kama "date" kabisa. Alipomaliza kijisafisha, akavaa nguo nzuri na kuanza kuelekea kule Sea House.


★★★★


Upande wa ile sehemu ya maficho ya Mess Makers, ambayo waliita "chini." Wakati huu waliokuwepo huko ilikuwa ni LaKeisha, Kevin, pamoja na Torres tu, wengine wakiwa sehemu zingine nchini. Kevin alikuwa kwenye chumba chake akijilalia mwenyewe, akiwa bado ameboeshwa sana na uamuzi wa yeye kutakiwa kuwa huko "chini" muda wote.

LaKeisha bado alikuwa anamchokoza Torres tokea wakati ule alipomtekenya pajani. Alikuwa anaendelea kumwonyesha kwamba anamtaka kimapenzi, lakini jamaa alimwambia kuwa hahitaji jambo hilo. Kwa sababu LaKeisha alikuwa amekaa na Torres muda mrefu tokea wapo kule Ghana, alijua kwamba Torres alikuwa na muda mrefu hajafanya mapenzi na mtu, hata alipofika Tanzania, hivyo alikuwa akimtania sana kwamba aidha yeye ni shoga au hajui tu jinsi ya kumridhisha mwanamke. Mara kwa mara tokea walipobaki wenyewe hapo, LaKeisha angejaribu kumzuzua kwa kumshika sehemu zenye kuamsha hisia za kimahaba, au kupita mbele yake akiwa nusu uchi kabisa makusudi, lakini bado Torres alikuwa amekaza tu.

Kihalisi LaKeisha alikuwa ameanza kuvutiwa sana na Torres. Alimwona kama mtu fulani mwenye uvutio wa hali ya juu ambao alikuwa anajaribu kuuficha, na kwa kumchokoza hivi, alikuwa anajaribu kuufichua. Aliipenda akili yake sana pia, naye alitaka kuona kama anaweza kufanya mambo mengi zaidi ya yale aliyomzoea kufanya, yaani kumshughulikia mwanamke ipasavyo. Huyo ndiyo alikuwa Lakeisha, mwanamke aliyependa sana "challenge." Sasa hata wakati huu akawa bado anamchokonoa jamaa ili apate chochote kutoka kwake, lakini bado Torres akawa anamzimisha tu.

Torres akiwa ameketi kwenye kiti kidogo huku anasoma mambo fulani kwenye kitabu, LaKeisha akaja usawa huo na kusimama mbele yake. Torres akaanza kuiangalia miguu yake kutokea chini, akimpandisha taratibu mpaka usoni. LaKeisha alikuwa amevalia kiblauzi chepesi kilichokatwa sehemu ya ubavu na kufanya tumbo lake liwe wazi, huku chini akivalia chupi laini ya rangi ya pink. Mkononi alishika kikombe cha udongo chenye chai, huku akimwangalia jamaa kwa nyodo.

"What do you want? (unataka nini?)" Torres akamuuliza.

"You (wewe)," LaKeisha akajibu.

"Am not here (siko hapa)," Torres akajibu na kuendelea kusoma.

"Can you never be less boring? (hivi hauwezi kuacha kamwe kuboa?)"

"Ever... (kamwe)"

"Yaani you're home alone with a hot bitch, and all you do is read? We in the f(......) stone age or what? (yaani uko nyumbani na malaya mkali halafu unachokifanya ni kusoma tu? Hivi tuko kwenye zama za mawe au?)"

Torres akabaki kimya tu.

"Tell me honestly. What is your problem? (Hebu niambie.. tatizo lako ni nini?)"

Kimya.

"It may be that you don't like me, or you just have a bad taste with women, but you gotta show some respect when a gal offers you some knock up... (inawezekana havutiwi nami, au una ladha mbaya tu kwa wanawake, lakini unapaswa kuonyesha heshima msichana akikupa ofa ya kumgonga..)" LaKeisha akasema.

Torres akachekea kwa chini bila kutoa sauti. LaKeisha alimfurahisha sana ijapokuwa hakujua hilo.

"So you wanna play it this way, huh? Fine (kwa hiyo unataka tucheze namna hii, siyo? Sawa)," LaKeisha akasema.

Torres akiwa anaendelea tu kusoma, akashtuka baada ya LaKeisha kuanza kukimwagia kitabu chake chai ya moto iliyofanya sehemu za vidole vyake ziungue kidogo. Akakiachia na kusimama akiwa ameshangaa sana.

"What do you... what do you think you're doing?! (unafikiri unafanya nini?)" Torres akamuuliza.

"Helping you read (nakusaidia kusoma)," LaKeisha akajibu kwa nyodo.

"Unajua... that book is sole... sitapata kingine, umeniharibia kichwa wewe!" Torres akasema kiukali.

"Oops! My bad. So, what are you gonna do about it? (oops... ni mbaya.. kwa hiyo utafanya nini kuhusu hilo?)" LaKeisha akamuuliza kikejeli.

Torres akamwangalia tu na kutikisa kichwa, kisha akakiokota kitabu chake kilicholowana sasa.

"Damn! Man una swagger kama za kuku! Una undugu na Elton John?" LaKeisha akamuuliza.

Torres akakiweka kitabu pembeni na ghafla kuishika shingo ya LaKeisha kama anamkaba. Akaanza kumsukuma mpaka sehemu ya ukutani kwa nguvu sana, naye LaKeisha akataka kumpiga na kikombe kile cha udongo lakini Torres akakiwahi na kuukaza mkono wake kwa chini. Alikuwa amemkaribia sana usoni huku akimkaba kwa nguvu kiasi, naye LaKeisha akawa anatabasamu kibabe.

"There it is..." LaKeisha akasema.

"What I am, what I do, what I don't, is none of your f(......) business. Next time you play bitchy on me I'll squash you like an insect. Do we understand each other? (kile nilicho, kile nachofanya, kile nisichofanya, ni mambo ambayo hayakuhusu hata kidogo.. ukija kunichezea kimalaya tena nitakusaga kama mdudu.. tunaelewana?)" Torres akasema kwa sauti thabiti.

"Please... do. I want you to squash me right now! (tafadhali.. fanya hivyo.. nataka unisagesage sasa hivi!)" LaKeisha akasema kibabe.

Torres akalegeza mkono aliotumia kuikaba shingo ya mwanamke huyu, naye LaKeisha akanza kushusha pumzi kwa nguvu huku anamwangalia kibabe bado. Torres alipotaka kumwacha, LaKeisha akaung'ang'ania mkono huo jamaa aliotumia kumkaba, na kuuweka tena kwenye shingo yake kama vile anataka amkabe tena. Torres akabaki kumtazama tu, na bado alikuwa ameudhika, lakini LaKeisha akapeleka mchezo huu hatua nyingine baada ya kuishika sehemu ya siri ya Torres iliyofichwa ndani ya kaptura nyepesi aliyokuwa amevaa.

Kwa sababu fulani wakati huu Torres akamwachia tu, kutokana na ukweli kwamba alikuwa amepandisha hisia kali alipokuwa karibu na mwili wa LaKeisha. Wakaendelea kutazamana tu, huku mkono wa Torres ukiwa kwenye shingo ya LaKeisha bila kuikaza kwa nguvu kama awali, na mkono wa LaKeisha ukiwa unaivuta-vuta mashine ya jamaa taratibu.

LaKeisha akaachia tabasamu la kiburi baada ya kuona kwamba wakati huu alimweza jamaa, kisha akamsogeza nyuma kidogo huku akiwa bado kaishika sehemu ile ya kati ya Torres, bila kuacha kumwangalia machoni. Torres alimtazama binti kama vile mtu mwenye chuki naye, huku kwenye akili yake akijua wazi ndiyo itikio ambalo LaKeisha alikuwa analitafuta.

Kisha mwanamke akashuka taratibu mpaka chini na kupiga magoti, naye akaishika kaptura ya Torres na kuishusha chini. Torres sasa alikuwa ameamua kumwachia mwanamke huyu ajithibitishie alichotaka kujua, na kwa kweli LaKeisha alivutiwa sana baada ya kuona kwamba Torres alificha jambo zuri sana.

"Kai masoyi ne na gaske, ba ku ba? (You are a real sweetheart, aren't you?/Wewe ni mtu mwenye mambo mazuri sana au siyo?)" LaKeisha akaongea kihausa.

"Karya... (bitch/malaya)" Torres akajibu kwa kihausa pia, naye LaKeisha akatabasamu.

Mwanamke akaanza kumpatia penzi la mdomo kwa upendo mwingi. Torres akawa akiutazama mwili maridadi wa mwanamke huyu jasiri. Hapa hangeweza kukataa kwamba kiukweli LaKeisha alivutia, na alikuwa na hamu ya kumeonyesha upendo pia. Wawili hawa wakaendelea kupeana mapenzi ndani hapo kwa dakika nyingi zaidi. Torres alitaka kumfurahisha mwanamke huyu pia. Hakujua ikiwa hili lingekuwa ni jambo la kudumu baina yao, hivyo aliona ni vyema ampatie msichana kumbukumbu nzuri kila mara ambayo angekumbuka penzi hili alilomshurutisha wafanye. Alijikaza kidogo asicheke kutokana na ukweli kwamba hakuwahi kumsikia mwanamke huyu akisema maneno kama 'Mungu wangu' au 'Jesus' kwa muda wote aliomfahamu.

LaKeisha alikuja kupiga kelele nyingi mwishoni baada ya kuridhishwa kwa mara ya kwanza na mwanaume huyo. Akajigeuza na kumtazama akiwa ameketi kilegevu.

"Nafikiri Kev amekusikia," Torres akasema.

"He can go to hell. I didn't think you had it in you (aende kuzimu.. sikufikiri ungekuwa na huu uwezo)," LaKeisha akasema.

"Well, now you know (basi sasa umejua)," Torres akajibu.

"Bado nakuhitaji Torre, kama utaweza lakini. Mara mbili usiku na mara moja tena asubuhi, sawa?" LaKeisha akamwambia.

"Is that a challenge?" Torres akauliza.

"You bet it is," LaKeisha akajibu.

"Mmmm... poa. Kama vipi tuanze kabisa..."

Torres akasema hivyo huku akimnyanyua kumbeba na kufanya LaKeisha acheke. Akatembea pamoja naye akimpiga denda kuelekea sehemu iliyokuwa ni chumba chake na kumrusha kitandani. Wawili hawa wakaendelea na mchezo wao mpya na mtamu sana kadiri dakika zilivyozidi kusonga......


★★★★


Ni ndani ya wakati huo huo ambao Torres na Lakeisha walikuwa wamepatana mpaka kuanza kupeana mapenzi huko mafichoni kwao ndiyo Nora alikuwa amefika kule Sea House kukutana na Lexi. Mwanamke huyu alivalia kwa njia ya kawaida tu, siyo kwa mwonekano wake wa kiofisi wa suti za kike au koti gumu (leather jacket) na T-shirt kama kawaida yake. Wakati huu alivaa nguo nyepesi tu; T-shirt nyekundu yenye mikono mifupi iliyobana kiasi, na suruali nyeupe ngumu yenye kubana kiasi pia, huku miguuni akivaa viatu vya kawaida aina ya simple zenye rangi nyeusi. Nywele zake alizokuwa akizibana muda wote tokea Asteria kumsuka, wakati huu aliziachia na kuzisokota kwa pande mbili, yaani upande mmoja wa bega likalalia fundo moja na upande mwingine hivyo hivyo pia.

Ilikuwa imeshafika saa 12 jioni sasa, na baada ya kumkuta Lexi akiwa ameketi pale, akamwita huku akimkaribia taratibu. Lexi alikuwa amevalia T-shirt ya mikono mirefu yenye rangi ya zambarau, iliyoficha vyema ngozi yake mpaka kufikia shingoni na suruali ya mazoezi yenye rangi ya kijivu, huku miguuni akivaa viatu kama mabuti ya rangi ya kaki. Akawa anamwangalia Nora huku akitabasamu mpaka alipofika hapo, kisha akaketi kwenye kiti cha pembeni yake. Kulikuwa na chupa mbili za wine aina ya Imagi, ambazo zilikuwa ni ndogo sana, naye Lexi alikuwa ameshikilia moja.

"Karibu mheshimiwa," Lexi akasema.

"Asante. Hako kambilikimo umekaibia wapi?" Nora akauliza kiutani.

"Haka ka-Imagi? Leo sijaiba nimenunua, lakini bado sijalipa. Tukimaliza tu tukimbie kabla Elias hajanitafuta," Lexi akatania.

Nora akacheka kidogo, kisha Lexi akampatia ile Imagi nyingine.

"Dodoma? We si ulisema haunywi wine za Tanzania asilia?" Nora akauliza.

"Ndiyo. Lakini nimeona nianze tu kujaribu..."

"Kwa nini?"

"We' ndiyo sababu. Nataka kujaribu vitu ambavyo rafiki yangu anatumia ili nione kama nitaipata furaha anayoipata..."

"Ahahah... sawa. Ila haka me sijawahi kunywa. Ni kazuri?"

"Sana. Nimekapenda. Onja..."

Nora akaifungua na kunywa wine kiasi, kisha akasema ni nzuri pia.

"Umependeza leo. Kama msichana wa high school," Lexi akamwambia.

"Ahahahah... acha basi..."

"Kweli kabisa. Nilivyokuona hapo nikadhani umetoka kutolewa out. Au ndiyo unaenda out?"

"Hapana. Nimevaa kawaida tu mbona. Na... nilikuwa nimetoka kwenye kazi kwa hiyo nikaenda kubadili mavazi kidogo..."

"Aaaa... sawa. Vipi kazi lakini? Umemtia bwege gani mbaroni leo?" Lexi akauliza.

"Emm... naweza kusema mambo yako jinsi yalivyo tu. Kuna kazi moja mimi na wenzangu tunaifatilia, angalau kuna mambo yameanza kujiweka vizuri," Nora akasema.

Kauli hiyo ikavuta umakini wa Lexi.

"Okay. Halafu inaonekana unapiga kazi wewe! Hivi huwa hata unapumzika?" Lexi akauliza.

"Ndiyo. Mimi kiukweli napenda sana kufanya kazi, hasa zikiwa ngumu. Ninapenda kutatua mambo mazito, na sikuzote mtu ukifanya kazi ngumu na matokeo yakaja vizuri unajua unapata furaha, si ndiyo..."

"Yeah..."

"Yeah, kwa hiyo iko hivyo..."

"Unamaanisha kwamba kuna kazi ngumu sana mnafanya sasa hivi eeh?"

"Ndiyo. Ni moja kati ya challenge kali sana ambazo nimewahi kuzipitia, lakini ninajua muda siyo mrefu tutatatua tu..."

"Challenge... kama Mess Makers vile?"

"Ndiyo..."

"Iih! Subiri... unataka kuniambia kwamba wewe unafanya kazi ya kuwatafuta hao jamaa?" Lexi akaanza kumchimba kijanja.

"Yeah..."

"Wow! Ah, saluti mheshimiwa rafiki..."

Nora akacheka kidogo.

"Ijapokuwa nawaona jamaa kuwa hatari lakini kiukweli wanawazungusha sana. Mpaka sasa mmewapata wangapi?"

"Hatujapata yeyote. Lakini kuna kitu tunafanyia kazi sasa hivi haitachukua muda mrefu tutawashika," Nora akasema na kunywa wine kidogo.

Uso wa Lexi ukawa makini kidogo. Alihitaji kujua ni kitu gani ambacho walikuwa wanafanyia kazi, lakini alijua pia kumuuliza moja kwa moja ni kitu gani hicho ingemfanya Nora amshtukie.

"Wakati wa kulala ukiutoa, ni muda mchache sana naotumia kupumzisha akili. Lakini muda wa kupumzika angalau kwa wakati huu nakuwa naufurahia... pamoja nawe. Company yako imeni...wear sana ndani ya hizi siku chache tulizojuana," Nora akasema.

Lexi akatabasamu na kusema, "Mimi pia nafurahia company yako mheshimiwa. Unapaswa kujitahidi kupumzika sana lakini hata kama mpango ni kustaafu ukiwa kijana bado."

"Ahahahah... ni kweli. Sema tu mimi siyo mtu wa kuacha mambo yakiwa hayajakamilika. Ni mpaka utata uishe ndiyo natafuta muda mrefu wa kupumzika," Nora akasema.

"Angalia lakini usije'anguka siku moja kwa sababu ya pressure kubwa unayojipa," Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu huku akiyaangalia macho ya Lexi. Ilikuwa ni macho tu hayo ndiyo yaliyomfanya aufurahie zaidi uso wa "mwanamke" huyu.

Lexi akawa ametafakari jambo fulani, kisha akauliza, "Kwa hiyo hata na hapa ukitoka tena unaenda kuendelea na kazi?"

"Yeah, nadhani. Lakini tuachane na kazi. Nataka uniambie huko kwenu Pemba huwa mnafanya mambo gani mengi kujifurahisha," Nora akasema.

"Oh, Pemba ni pazuri. Kuanzia tamaduni mpaka mipasho ya kina Kopa, ni full raha tu..."

Nora akacheka na kuendelea kumsikiliza.

Lexi akajitahidi kumwambia mambo aliyojua kuhusu mkoa wa Pemba, kisha akamwambia anataka kwenda pale Sea House mara moja ili kufata kinywaji kingine haraka na kurejea. Nora akakubali, naye Lexi akaondoka. Lakini aliigiza tu kuondoka kwa kuwa alipofika usawa wa vichaka vya kukaribia sehemu hiyo, akajibanza, na kama matarajio yake, akamwona Nora anatoa simu na kupiga kwa mtu fulani. Alitumia umakini wa hali ya juu sana kuweza kusikiliza maneno ya Nora ijapokuwa alikuwa kwenye umbali fulani, naye akaweza kusikia Nora akisema mambo kama hayuko mbali sana, na wakikaribia tu kumaliza ajulishwe ili awahi huko upesi. Lexi akaondoka baada ya kuona Nora ameshusha simu yake.

Baada ya dakika tano hivi, Lexi akarejea hapo akiwa na Imagi zingine mbili na kuketi.

"Mm... umeleta zote hizo kwa ajili yako?" Nora akauliza.

"No, moja kwa ajili yako," Lexi akajibu.

"Ooh... nahofia nitaanza kusinzia ikiwa nitakunywa nyingine..."

"Siyo kali sana hizi..."

"Eti eeh? Basi zinywe wote wewe..."

Lexi akacheka.

Nora akawa anamwangalia sana mpaka Lexi akajishtukia.

"Vipi mheshimiwa, mbona unaniangalia hivyo?" Lexi akamuuliza.

"Macho yako mazuri sana Lexi," Nora akafunguka.

Lexi akabaki kumtazama tu. Nora akajishtukia kuwa alisema jambo ambalo huenda halikuwa sawa kwa njia fulani.

"Oh, samahani... nime... namaanisha wewe ni.... ila... katika njia ya kawaida. Nafikiri wine imenikolea," Nora akasema kiajabu-ajabu na kunywa tena wine.

"Sijui labda unataka kwenda kuogelea, au kuna kitu unataka kuniambia?" Lexi akauliza baada ya kuwa amemsoma.

"Kuogelea?"

"Yeah..."

"Kwa sasa hivi? Sijavaa nguo ya kuogelea kama unavyoona..."

"Ahahahah... ndiyo najua. Namaanisha, nahisi kama vile kuna kitu unataka kusema lakini unajizuia," Lexi akaongea ukweli bila kupindisha.

Nora akamwangalia tu.

"Siyo lazima ukae nayo kama siri, niambie tu. Kwa mfano, mimi siri yangu ni kwamba napendaga kukaa ndani uchi nikiwa nimeboeka..."

Nora akacheka na kusema, "Siyo siri tena..."

"Siyo siri tena," Lexi akamalizia.

"Ahahah... hamna kitu wala. Nisamehe kama nimekufanya unione wa ajabu," Nora akamwambia.

"Hamna kitu kama hicho. Besides... ninajua unachofikiria," Lexi akamwambia.

"Kweli?" Nora akamuuliza kiudadisi.

"Ndiyo..."

"Nawaza nini?"

"Unawaza... kwamba kwa mwanamke wa aina yangu, kuna vitu vingi sana ambavyo nimewahi kufanya lakini wewe hukuwahi kufikiria kufanya. Kuwa hapa pamoja nami inakufanya ujihisi utofauti fulani, na unataka sana kujua ni mambo yapi mtu kama mimi napitia kwa sababu ninaonekana kuwa na siri nyingi... na kwa kuwa wewe ni mtu ambaye unapenda kufichua siri, unataka kuzijua na zangu... unitalii mimi... ujue inakuwa vipi kuwa mimi.... hata unawaza ingekuwa poa zaidi kuniona nikiwa bila nguo...." Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu kwa hisia huku akimwangalia sana.

"Unawaza pia kwamba mimi ni mzuri. Unafikiri mimi ni.... mrembo..." Lexi akasema.

Nora akaangalia chini kidogo, kisha akatikisa kichwa kukubali na kumtazama tena.

"Halafu sasa unawaza... nini kitafata baada ya mimi kusema hivi vitu. Unataka kuona kwa mtu wa aina yangu... nitafanya nini nikiwa nimeshajua kwamba unawaza vitu hivyo juu yangu..."

Nora alipendezwa sana na maneno ya Lexi. Kiukweli alianza kuhisi ni kama alikuwa anaongea na mtu tofauti na yule aliyemwona mbele yake, bila kujua kihalisi kuwa ndani ya mwili wa mwanamke huyo ilikuwa ni mwanaume. Wakaendelea kutazamana kwa sekunde chache, kisha Lexi akamsogelea karibu kabisa na uso wake. Nora alikuwa ameshikwa na msisimko fulani hivi wa ajabu, akitarajia mengi sana hapo, naye Lexi akaisogeza midomo yake mpaka kwenye midomo ya Nora na kumpiga busu laini.

Lexi akaanza kuinyonya midomo ya Nora taratibu, naye Nora ni kama akawa anamfungulia njia tu Lexi ili atalii mdomo wake. Lexi alimpa denda nzuri sana karibia sekunde 30, kisha akajitoa mdomoni mwake na kujirudisha nyuma huku akimwangalia kwa makini. Nora yeye akawa anamwangalia kama mtu asiyeelewa hisia zake vizuri, kwa sababu Lexi ndiye aliyekuwa "mwanamke" wa kwanza kuwahi kumpiga busu katika maisha yake, hivyo hisia alizomjengea hapa zilikuwa na utofauti fulani mkubwa.

"Unaonaje?" Lexi akamuuliza.

Nora akabaki tu kumtazama na kushia kusema, "Aam...."

Simu ya Nora ikaanza kuita. Akaichukua kutoka mfukoni mwake na kukuta ni Mario, naye akapokea. Mario alikuwa anamjulisha kwamba mchoro wa sura ya huyo "Erick" ulikuwa umekamilika, nao walikuwa wameshaanza kutafuta ufanani wa picha hiyo na mtu halisi, hivyo Nora akasema angefika upesi. Lexi, akiwa anajifanya hasikilizi maongezi hayo, akatambua kuwa kulikuwa na jambo fulani kuu linaendelea.

"Lexi... nahitaji kwenda. Tuta... tutakutana tena... nafikiri," Nora akamwambia na kusimama.

"Okay, you know what? Mimi pia nitaondoka maana itaboa kukaa hapa peke yangu. Twende," Lexi akasema na kunyanyuka pia.

Wakaviacha viti vile pale, huku Lexi akizibeba zile Imagi mbili na kuondoka pamoja na Nora.

Walipofika sehemu ambayo Nora aliegesha gari lake, Lexi akamuaga na kuelekea upande mwingine, kisha Nora akaingia upesi ndani ya gari na kuliwasha. Lakini alipolirudisha nyuma kidogo, akatambua kulikuwa na tatizo kwenye tairi, naye akashuka na kukuta pancha kwenye matairi mawili. Akakasirika na kujiuliza zilitokea wapi wakati aliliacha gari bila pacha hapo. Lakini msababishi wa pancha hizi alikuwa ni Lexi. Alipomwacha Nora wakati ule kwa kigezo cha kufata vinywaji, alikuja na kulitia pancha gari la Nora kwa makusudi, akiwa na lengo fulani akilini.

"Vipi Nora?"

Nora akageuka na kukuta ni Lexi ndiyo amemuuliza hivyo.

"Lexi... bado hujaondoka?" akamuuliza.

"Yeah... nilikuwa nataka kuondoka nikaona umeshuka tena kutoka kwenye gari. Kuna tatizo?" Lexi akauliza kama vile haelewi somo.

"Puncture. Mbili kabisa. Na ninahitaji kuwahi sijui kama kwa... nitachukua taxi tu," Nora akasema.

"Oh no, ikiwa unahitaji, twende kwa gari langu. Kuna nafasi ya kutosha," Lexi akasema.

"Okay, asante sana Lexi..."

"Bila shaka... let's go..."

Wawili hawa wakaelekea kwenye gari la Lexi. Ilikuwa ni gari aina ya Audi SR7 Sportback nyeusi, na baada ya Nora kuiona akamwambia Lexi kweli sasa amethibitisha zaidi kwamba mwanamke huyo alikuwa wa kishua. Lexi akampatia funguo Nora ili yeye mwenyewe aendeshe mpaka kufikia alipohitaji, naye Nora akakubali na kuwaondoa hapo. Nia ya Lexi ilikuwa ni kutaka kujua Nora na wenzake walipoweka makao na kufanya uchunguzi wao, ili ikiwezekana apange na timu yake kuja kupavamia wakati ambao hawangekuwepo na kuiba au kuharibu kila kitu walichofanyia utafiti.

★★

Nora aliendesha mpaka huko na kuegesha gari umbali mfupi kutokea jengo lile. Akamshukuru Lexi na kushuka, kisha akawahi kuelekea ndani kule. Sasa Lexi akawa amepaona, lakini tena bado alitaka kujua ni nini kiliendelea kwa wakati huu, na baada ya kufikiria njia kadhaa, ni kama muujiza ukawa umetokea. Nora alikuwa ameisahau simu yake ndani ya gari, hivyo Lexi akaichukua na upesi kuelekea huko kwa kigezo cha kutaka kumpelekea simu Nora ili aweze kuchungulia baadhi ya vitu humo ndani.

Jengo hili lilikuwa limejitenga sana na majengo mengine kwenye eneo lililo na uoto wa asili, kukiwa na vyuma vyuma vingi nje na makontena mawili ya magari makubwa kwa nje yaliyoachwa kwa muda mrefu. Alipofika langoni, Lexi alisukuma tu na kuingia kwa kujiamini kabisa, na hapo akaweza kuwaona wanaume kadhaa pamoja na Nora kwa mbele, kutia ndani Nathan. Aliyeanza kumwona Lexi alikuwa ni Vedastus, naye akamwangalia kiukali na kuanza kumfata.

"Wewe! Unafanya nini humu?"

Swali la Vedastus likawafanya wengine waangalie upande wa mlango wa kuingilia, naye Nora akamwona Lexi.

"Aa... samahani... nilikuwa...."

"Njoo hapa. Nani amekuruhusu kuingia humu?" Vedastus akamuuliza kiukali huku akimfata.

"Veda, Veda, subiri... namfahamu..." Nora akamwambia kwa tahadhari.

"Nani huyo?" Luteni Michael akamuuliza.

"Ni rafiki yangu. Lexi... njoo," Nora akasema.

Lexi akampita Vedastus akijifanya anaogopa fulani hivi, naye akafika usawa wa Nora, aliyesogea kukutana naye.

"Vipi?" Nora akauliza.

"Ulisahau simu yako," Lexi akasema na kumpatia.

"Oh, asante," Nora akaipokea.

Kwa jicho la kuibia, Lexi alitazama screen ya kompyuta alipokaa Bobby, na hapo akaona picha iliyofanya mapigo ya moyo wake yaanze kukimbia kwa kasi.

Ilikuwa ni picha ya Oscar!



★★★★★★★★★★★★★★★★★★
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★


MIAKA NANE ILIYOPITA....


Turudi tena mpaka usiku ule ambao familia ya Meja Casmir ilishambuliwa na Luteni Weisiko pamoja na wanajeshi wake wawili. Baada ya Weisiko na Goko kuwaua wazazi wa watoto wale watatu, Casmir na Alice, pamoja na msaidizi wao wa kazi Salome, watoto walikimbilia msituni huku Xander, akiwa ndani ya mwili wa Sandra, akiwa na maumivu tumboni kutokana na kuchanwa kwa kisu, naye Sandra, akiwa ndani ya mwili wa Xander, akihisi maumivu pia kwenye paja lake baada ya kuchunwa na risasi aliyofyatuliwa na Goko.

Kutokana na jinsi watoto walivyokuwa wakikimbia polepole hasa kwa sababu ya Sandra kumshikilia Xander kutokana na mwili wake kuishiwa nguvu kwa sababu ya kisu alichochomwa tumboni, Xander akawaambia wenzake wamwache nyuma ili dada zake wakimbie pamoja. Sandra akawa anakataa, lakini Xander akamshawishi kwa kumwambia ni bora hata kama akifa yeye lakini ndugu zake wawe na nafasi kubwa ya kupona kuliko ikiwa wote watauliwa. Kwa hiyo akamwambia waelekee upande mmoja, halafu yeye atajitahidi kuelekea upande mwingine akiacha viashiria kwa wanaume wale ili wamfate yeye tu. Sandra akiwa kwenye mwili wa Xander alilia sana. Azra alilia pia mno, nao wote wakamkumbatia ndugu yao, kisha akawasihi wawahi haraka maana alijua Weisiko na mwenzake walikuwa nyuma yao.

Sandra, akiwa kwenye mwili wa pacha wake akaondoka na Azra kuelekea upande mmoja, wakimwacha Xander anajiandaa kuelekea upande mwingine. Alijitahidi kukimbia pamoja na Azra kwa uangalifu ili kuwaepuka maadui, huku Azra naye akijikaza sana kukimbia ingawa alikuwa amechoka. Walikimbia na kukimbia bila ujuzi wowote wa walikokuwa wakielekea, na kwa sababu ya kutotambua uelekeo wao ikawa ni kama wanazunguka msitu tena na kurudia njia ile ile waliyotokea. Azra akafikia ukomo wa pumzi zake, naye akamwomba "Xander" wapumzike kidogo kwa kuwa hangeweza kuendelea kukimbia. Sandra kwa kuhofia usalama wao, akaamua tu kumbeba mgongoni ili waendelee kukimbia, akitumia vizuri nguvu ya mwili wa kaka yake ili iwafikishe mbali. Kichwani kwake alimuwaza sana Xander, angekuwa kwenye hali gani kwa hizo dakika chache walizotengana.

Wakati akiendelea kukimbia hivyo, akaukwaa mguu wake na kudondoka pamoja na Azra. Bado alihisi maumivu kwenye paja lake, lakini akawa anajitahidi kumnyanyua mdogo wake ili waendelee kukimbia. Azra sasa akasema angeweza tena kukimbia, lakini shida ikawa kwa Sandra. Alihisi mguu wake ukiwa mzito sana, kama vile ulikuwa umeanza kufa ganzi, kwa maana kila alipojaribu kusimama vizuri asingeuhisi vyema, na hilo likasababisha awe anadondoka tu. Azra akajitahidi kumsaidia ili waondoke pamoja, na ni hapa ndipo wakaanza kusikia sauti za hatua zikija upande wao. Kwa kutambua bila shaka ilikuwa ni adui, wakaendelea kujivuta kwa pamoja ili kumwepuka, lakini Sandra akamwambia Azra wajifiche tu sehemu fulani ili adui yao awapite, kwa kuwa kuendelea kukimbia namna hiyo hakungeleta matokeo mazuri sana.

Kwa hiyo wakaketi kwenye kichaka kimoja ambacho kilikuwa na miiba midogo-midogo, na ingawa iliwachoma lakini wakajikaza tu na kuendelea kutulia. Kutulia huku kulifanya maumivu kwenye paja la Sandra yasikike zaidi, lakini akajitahidi tu kujikaza pia. Hazikupita sekunde nyingi, nao wakamwona mtu fulani akifika hapo kando yao. Kwa haraka wakatambua ilikuwa ni Luteni Weisiko, naye Sandra akambana zaidi Azra kwake ili wasitikisike. Luteni Weisiko akasimama hapo kwa sekunde chache, kama akitathmini watoto walikuwa wameelekea wapi, kisha akaendelea kukimbilia upande mwingine.

Baada ya Sandra na Azra kuona ameondoka, wakajitoa kwenye kichaka hicho, naye Azra akamwambia aliyemwona kama Xander kwamba wangepaswa kurudi nyuma ili kumtafuta "Sandra." Lakini Sandra akasema hata hakujua walikokuwa, hivyo hangejua wapite wapi labda mpaka wasubiri kukuche, lakini Azra akasisitiza kwamba walipaswa kurudi kumsaidia ndugu yao hasa kutokana na jinsi alivyoumia. Sandra akiwa anafikiria nini cha kufanya, wote wakastushwa na sauti ya Luteni Weisiko ikisema, "Njooni na mimi, nitawapeleka kwa dada yenu."

Wawili hawa walishtuka sana na kutazama upande ambao walimwona Luteni Weisiko akiwa amesimama huku anawaangalia. Hofu ikawajaa sana, naye Sandra akamwambia Azra akimbie haraka. Azra akaanza kukimbia kuelekea upande mmoja, naye Sandra akaanza kuelekea huko huko. Luteni Weisiko akaendelea kusimama hapo hapo na kutabasamu tu, kisha akaikoki bunduki yake na kuanza kuwafata kwa kasi. Ilikuwa ni kama alipenda sana mchezo huu wa paka na panya, na baada ya kuwakimbiza kwa hatua kadhaa, akawaona wakiwa kwa mbele wanakimbia, wakijitahidi kuokoa maisha yao.

Walikuja kufika sehemu ambayo ilikuwa na eneo lenye uwazi kidogo bila kuwa na miti bali majani tu chini, na baada ya Luteni Weisiko kuingia hapo akasimama na kuielekeza bunduki yake kwa Azra, aliyekuwa mbele zaidi, naye akafyatua risasi iliyompata nyuma ya mguu wake wa kushoto. Azra alipiga kelele ya maumivu na kudondoka chini, lakini ni wakati tu amedondoka chini ndiyo akapiga kichwa chake kwa nguvu sana kwenye jiwe dogo na kupoteza fahamu.

Sandra akiwa ndani ya mwili wa Xander alipiga kelele ya kilio baada ya kushtushwa na sauti ya risasi hiyo, naye akaanguka chini akiwa amejikunja kwa woga mwingi. Luteni Weisiko akajisawazisha na kuanza kumwelekea mpaka pale alipokuwa, na alipofika karibu, akamwelekezea bunduki yake kichwani kama anataka kumfyatua kwa risasi. Sandra akawa anamwangalia huku analia na kuficha uso wake kwa mikono. Weisiko akawa anataka kukivuta kifyatulio cha risasi, lakini akasikia mlio wa risasi nyingine kutokea upande tofauti na huo. Akatazama upande huo wa msitu na kukisia kwamba bila shaka ilikuwa ni Goko ndiye aliyempata pacha wa kike na kummaliza, hivyo akaishusha bunduki yake na kumtazama tu pacha huyu wa kiume.

"Umebaki wewe," Luteni Weisiko akamwambia hivyo "Xander" huku akitabasamu.

"Tafadhali... usiniue... please..." Sandra akawa anaomba kwa sauti tetemeshi.

Luteni Weisiko akachuchumaa na kumtazama kwa ukaribu. Sandra akawa anajivuta nyuma kwa woga.

"Unajua hapa ni sawa na kama umeshakufa kwa sababu... hata nikisema nikuache, huu msitu una wanyama wakali. Ni bora tu nikusaidie ili wasikutafune..." Weisiko akasema.

Sandra akawa anatikisa kichwa kukataa.

"Cha risasi ni rahisi zaidi kuliko meno. Au unataka kutafunwa? Si bora hivi?" Weisiko akauliza kikejeli.

"Una watoto?" Sandra akauliza.

Luteni Weisiko akabaki tu kumtazama.

"Ikiwa ungekuwa nao... na uko sehemu fulani ukijua kabisa wanapatwa na mambo kama haya yanayotupata sisi... ungefanya nini?" Sandra akauliza.

Luteni Weisiko akainamisha uso wake kama anatafakari jambo fulani. Yeye aliona ni kama Xander ndiyo anamuuliza hivyo, na kiukweli maneno yake yalimgusa kwa kiwango fulani.

"Nitakupa dakika mbili tu za kufanya chochote kile unachotaka kufanya. Baada ya hapo...." Luteni Weisiko akaishia tu hivyo na kusimama.

Sandra akaanza kujivuta kuelekea kule alikoangukia Azra. Akafika mpaka karibu yake na kuanza kumpepesa ili aamke, lakini akawa ametulia tuli tu. Aliposikiliza mapigo yake ya moyo, akatambua kwamba bado alikuwa hai, naye akamgeukia Luteni Weisiko kukuta tayari akiwa amewakaribia.

"Please usiniue... please... I'm begging you..."

Luteni Weisiko akaonekana kutojali kilio cha kijana huyu na kuielekeza bunduki yake kwake kwa mara nyingine. Sandra akajisawazisha na kupiga magoti, akiwa ameviunganisha viganja vyake.

"Usiniue tafadhali. Azra... mdogo wangu ananihitaji. Ana tatizo la upumuaji, ana... ana... ananihitaji... tafadhali...." Sandra akaendelea kuomba.

Maneno haya ya Xander (Sandra) yakamfanya Luteni Weisiko aishushe bunduki yake kidogo. Ni kama alikuwa anatafakari jambo fulani baada ya Xander (Sandra) kusema kwamba mdogo wake alikuwa na tatizo la upumuaji, naye akamwangalia Azra pale chini. Lakini akayakaza meno yake na kumwangalia tena "Xander." Akainyanyua bunduki yake kwa njia yenye uhakika zaidi wakati huu, naye akaikoki tayari kumfyatua risasi.

"Usiniueee... pleeease... please usi... usiniueee..." Sandra akaendelea kumwomba hivyo Luteni Weisiko, naye Weisiko akawa kama anataka kufyatua lakini anasita.

Kutokea kichwani kwake, Sandra akasikia sauti ya pacha wake ikimwita, 'Sandra... Sandra...' na kwa sababu hakujua ilitokea wapi, akatafuta utulivu kidogo ili aweze kumsemesha pacha wake pia.

Luteni Weisiko akawa bado amemwelekezea bunduki, naye akasema, "Nisamehe... hii ni sehemu tu ya kazi yangu."

Sandra akafumba macho yake na kuamua kujaribu kuongea kwa kutumia akili yake pia, akiwa ameshakubaliana na matokeo. Ilikuwa ni muhimu sana kwake pacha wake asikie maneno yake ya mwisho.

'Xander... popote ulipo... jua nakupenda sana pacha wangu... tafafhali pambana usalimike... usisahau hili kamwe... for me...'

Lakini kabla hajamaliza maneno yake, Luteni Weisiko akamfyatua kwa risasi kichwani, naye akaanguka chini karibu kabisa na alipokuwa amedondokea Azra. Luteni Weisiko akakaza meno yake kwa nguvu na kutazama pembeni, akiwa kama mtu aliyefanya jambo hilo kwa shingo upande. Lakini akajikumbusha yeye ni nani, mwanajeshi mtiifu ambaye hakupaswa kuruhusu hisia zimkengeushe kutoka kwenye "mission" aliyopewa, hivyo akajisawazisha akili tu na kuwaangalia tena watoto hao, kisha akaanza kuwasogelea chini hapo. Mkono wake uliokuwa umepigwa kwa risasi bado ulitoa maumivu, lakini akawa anaupuuzia tu.

Alipowakaribia zaidi, akachuchumaa na kumwangalia Azra. Kwa hapo angeweza kuhisi tu kwamba binti huyo bado alikuwa hai, naye akaushika uso wake mweupe ambao ulionekana vyema kwenye giza hilo la msitu. Alimwangalia mno binti huyo mdogo, na kumbukumbu kadhaa za matukio ya kipindi cha nyuma zikamwingia akilini mwake.

Luteni Weisiko alikuwa na mtoto wa kike, ambaye kwa sasa hakuwa hai. Binti yake huyo alikuwa mweupe kufata weupe wa mama yake, ambaye Luteni Weisiko aliachana naye kwa kuwa mwanamke huyo hakupenda tabia za kitemi-temi za mwanaume huyu. Lakini Weisiko alimpenda sana binti yake ingawa hakumpa muda mwingi wa kuwa pamoja naye kama mzazi. Binti yake huyo aliitwa Mary, naye alikuwa na tatizo la upumuaji ambalo liliongezeka sana kufikia wakati alipokuwa na miaka 13; rika kama la Azra tu.

Kipindi fulani Weisiko alipokuwa kazini, binti yake alishikwa na mkazo mbaya sana kwenye mapafu, na mama yake alijaribu kumtafuta Weisiko ili amsaidie kuweza kumpatia matibabu ya haraka, lakini Weisiko alichelewa, na hivyo mtoto huyo akapoteza uhai. Mzazi mwenza alimlaumu sana Weisiko kwa kifo cha bintiye, akisema alikuwa na uwezo mzuri tu wa kumpatia matibabu mapema sana hata nchi za nje, lakini akampuuzia. Ila ukweli ni kwamba Luteni Weisiko alikuwa na deni kubwa wakati huo ambalo alikuwa akilipia fidia mfululizo, ndiyo sababu hakuweza kulipia matibabu ya hali ya juu kwa ajili ya binti yake.

Mwanamke huyo aliyezaa naye alikuwa msusi tu kwenye saluni za wanawake, hivyo hakuwa na kipato cha kutosha na alihangaika kwa muda mrefu na binti yake. Kwa hiyo alimlaumu sana Weisiko kwa kuwa aliona kwamba mwanaume huyo kwa mtoto wao alikuwa baba jina tu. Weisiko pia alijilaumu mno kwa kukosa kumsaidia binti yake, na ndiyo kutokea hapo akaapa kufanya kila alichoweza ili kupata pesa nyingi zaidi kwa sababu aliona jinsi maisha yalivyokuwa na hasara bila kuwa na pesa ya kutosha. Akaanza kujihusisha na masuala haramu ya chini chini ambayo ndiyo mpaka yakapelekea yeye kujiingiza katika visa hivi viovu ili tu apate jambo ambalo aliona ndiyo muhimu zaidi lililobaki kwenye maisha yake: pesa.

Kwa hiyo kumwangalia Azra kulimfanya aone ni kama anamtazama Mary kwa mara nyingine tena. Maneno ya "kaka yake" kwamba Azra alikuwa na tatizo la upumuaji, yalichochea hata zaidi hisia hizo kumwelekea binti huyu, naye akahisi eti ni kama alipaswa "kumsaidia," kana kwamba anapewa nafasi ya pili ya "kumsaidia" mtoto huyu kwa kuwa wa kwake alishindwa. Akili yake ilikuwa imeingiwa na suto kubwa kwa sababu ya mambo maovu aliyofanya, kwa hiyo fikira ya "kumsaidia" mtoto huyu ikaonekana kama njia yake ya kujiaminisha kwamba alikuwa na moyo mzuri.

Akatoa simu maalumu ya kijeshi (walkie talkie) na kupiga kwa Kanali Jacob Rweyemamu ili kumtaarifu kwamba mambo yalikamilika. Baada ya kupokelewa, Luteni Weisiko akasema tu, "Mission Accomplished," kisha akarudisha kifaa hicho mfukoni na kuanza kumnyanyua Azra kwa mkono mmoja. Aliweza kuona jinsi ambavyo damu nyingi zilivuja mguuni kwake, naye akachana sehemu ya nguo ya "Xander" na kumfunga Azra sehemu iliyovimba kwa risasi. Akambeba begani kwake kama vile windo la swala, kisha akaanza kuondoka naye.

Alikwenda taratibu kama vile hakukuwa na tatizo lolote kabisa mpaka akafika kule ambako kulikuwa na nyumba ile alikowaua wazazi wa watoto hawa. Akampeleka Azra mpaka ndani ya gari walilokuja nalo hapo, naye akaanza kumtafuta Goko kwa kifaa kile cha mawasiliano. Alifikiri angemkuta huku tayari kwa sababu alisikia risasi ile iliyofyatuliwa kutokea upande ambao alimwambia aende. Kwa sababu hakuweza kumpata, akaona tu aondoke hapo ili kumpeleka binti huyu kwenye matibabu. Alimwangalia kwa mara nyingine na kuona bado yuko hai, naye akawasha gari na kuondoka hatimaye.


★★★★


Akiwa bado mwendoni, Weisiko aliongea na baadhi ya vijana wa kundi lao na kuwaeleza kile yeye na wengine wawili walichofanya usiku huo, naye akawaamuru baadhi kwenda sehemu ile alikotoka ili kuteketeza miili ya wale waliowaua. Akawapa maagizo hususa kabisa kwamba walipaswa kupeleka na miili mingine ya watu waliokufa ili kuichoma kwa moto pamoja na ile ambayo wangeikuta, na walipaswa kumaliza hayo yote kabla ya jua kuchomoza. Akamalizana nao na kuendelea na safari yake, akiwa na lengo la kumpeleka Azra kwenye hospitali ya jeshi. Yaani ilikuwa ni kama akili yake imekufa ganzi kabisa, akifanya mambo kwa njia aliyoona kuwa sahihi, na hakuna kitu chochote ambacho kingemzuia.

Alifika kwenye hospitali ndogo ya jeshi na kupokelewa na baadhi ya vijana ambao alikuwa ameshawapanga. Walimpokea kwa njia yenye umakini ili kuwaficha wengine ambao hawakuwa wa kundi lao kuhusiana na yaliyotokea. Eneo la huku lilikuwa kwenye kambi kubwa sana ya kijeshi ambako wanajeshi wengi waliishi. Kwa hiyo vijana wake hao wakampeleka Azra kwenye chumba cha matibabu, na daktari wa upasuaji (akiwa ni mwanajeshi pia) akafika na kuanza kumhudumia mtoto.

Weisiko aliketi kwenye kitanda cha pembeni ndani ya chumba hicho hicho, akiwa anatolewa risasi mkononi mwake, na hakuna yeyote aliyepaswa kuuliza ni nini kilikuwa kimetokea. Walipaswa kuwapa tiba, halafu waendelee na mambo mengine. Weisiko akawaambia watu wake wamwangalie vizuri sana huyo mtoto, yaani wafanye lolote lile lakini asife, nao wakaendelea kujitahidi kumpa Azra huduma mpaka inafika asubuhi. Walifanikiwa kuitoa risasi mguuni kwake na kumshona, nao wakatibu sehemu ya kichwa chake iliyoumia na kuifungia bendeji. Sasa mtoto akawa anasubiriwa kurejesha fahamu.

Taarifa kumhusu Azra kuwa hapo zilipaswa kuwa za siri sana, ikiwa ni amri kutoka kwa Luteni Weisiko. Lakini alijua kwamba huenda asingefanikiwa kuficha hili kwa wakuu wengine kwa muda mrefu sana, hivyo asubuhi hiyo akaamua kumwambia Kanali Jacob Rweyemamu kila kitu akichofanya. Kanali Jacob kiukweli alimshangaa na kuuliza ikiwa akili yake ilikuwa imekongoroka au alikuwa anataka kuwaletea matatizo mapema. Lakini Luteni Weisiko akamwambia kuna hali ilimsukuma kumsaidia mtoto huyu, hasa kwa sababu alimkumbusha kuhusu binti yake aliyeshindwa kumwokoa.

Kanali Jacob akamwambia kwamba hilo halikujalisha hata kidogo. Ikiwa msichana huyo angeamka na kusema kila jambo lililotokea basi mambo kwao yangeharibika. Akamuuliza Luteni Weisiko angewezaje kuzuia hilo, ndipo Weisiko akamwambia kwamba alipanga KUMSAHAULISHA Azra mambo yote yaliyotokea. Yaani alitaka mtoto huyo apoteze kumbukumbu ya mambo yaliyotokea, lakini pia kuhusu yeye ni nani KABISA. Kanali Jacob alipouliza nia yake ya kufanya hayo kiukweli ilikuwa nini, Weisiko akasema alitaka kumfanya Azra kuwa kama "binti yake," kwa sababu kila kitu kumhusu huyo mtoto kilimkumbusha kuhusu Mary. Akamwomba sana Kanali Jacob amkubalie kuhusiana na hili, akisema ana njia ya kufanya hivyo, na hakuna jambo lolote ambalo lingeharibika kwa kuwa amehakikisha mipango yao yote imekwenda "salama."

Pamoja na kwamba Kanali Jacob aliona suala hili kuwa upuuzi wa hali ya juu, akamkubalia tu, naye akamwambia angetumia uchochezi wake kuhakikisha Azra anaendelea kuwa siri hapo kwenye hiyo hospitali. Lakini akamweka wazi kwamba Azra kuendelea kuwa hai nchini humu hata kama asingekumbuka lolote bado kungekuwa hatari kwao, hivyo akapendekeza kwamba walipaswa kumhamisha na kumpeleka nje ya nchi. Akiwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu ingesaidia kumfanya asahaulike kabisa hasa kwa sababu watu wangefikiri ameshakufa kama tu watu wa familia yake, naye Weisiko akakubaliana na hilo.

Lakini kwanza wangehitaji kumalizia sehemu muhimu ya mipango yao iliyobaki, yaani, kuwaondoa Jenerali Pingu Senganya na Luteni Jenerali Geneya Oyayu, ndiyo wangeanza harakati za kumsafirisha Azra.


★★★★


Baada ya wiki moja hivi kupita, Azra alirejesha fahamu zake. Alijikuta akiwa ndani ya chumba cheupe, kilichokuwa na mwonekano kama wa vyumba vya hospitali lakini cheupe kupita maelezo. Alikuwa amewekewa 'drip' kwenye mishipa, na aliweza kuhisi jinsi ilivyokuwa ngumu kunyanyua baadhi ya sehemu zake za mwili. Alikuwa akijiuliza alifikaje humo, na kitu chenye kumhofisha hata zaidi ni kwamba hakuwa na kumbukumbu yoyote ya mambo yaliyompata mpaka kufika sehemu hii. Alijaribu na kujaribu kuvuta taswira ya vitu vingi kuhusu yeye, lakini ilikuwa ni kama kichwa chake kilikuwa tupu kabisa.

Hali hii ya kutojielewa ilimfanya aogope sana, hasa kwa sababu alikuwa binti mdogo mno. Akaanza kujaribu kunyanyuka, lakini akashindwa. Akaanza kulia sana, kwa sauti ya chini, na ndipo akaingia mtu aliyemwona kama mwanaume wa kawaida tu. Kwa sababu hakumtambua, mwanzoni alionyesha kuogopa, lakini mwanaume huyo akaanza kumtuliza kwa kumwambia yeye alikuwa ni baba yake. Huyu alikuwa ni Luteni Weisiko.

Akaanza kumdanganya Azra kwa maneno mazuri sana na kumfanya atulie. Akamdanganya kwa kumwambia kwamba jina lake lilikuwa ni Mary. Alimweleza kwamba alipatwa na ajali mbaya sana na ndiyo maana alikuwa kwenye hospitali hiyo kimatibabu. Akasema kwenye hiyo ajali waliwapoteza mama yake na ndugu zake wengine, kwa hiyo walikuwa wamebaki peke yao tu. Azra hangeweza kukumbuka chochote wakati huu kwa sababu ndani ya wiki hiyo tayari Luteni Weisiko alikuwa amefanya ule mpango wake wa kuipoteza kumbukumbu ya binti kwa kutumia madawa fulani. Kwa hiyo yeye kuwa hapo peke yake na kuonyesha anamjali sana Azra, kukafanya binti amwone kuwa mtu wa kuaminika na wa karibu zaidi kwake, hivyo kujihisi salama.

Weisiko akaendelea kukaa na Azra hapo kwa muda mrefu, akimwambia kwamba angempeleka nje ya nchi apate matibabu bora zaidi ili apone haraka. Azra hakuweza kusema lolote lile kwa kipindi hiki. Muda wote alikuwa kimya tu, na akiitikia mambo machache kutoka kwa Luteni Weisiko kwa kutumia ishara. Hata wakati ambapo watu wengine kama wauguzi wangeingia, angeonyesha kuwahofia na kujificha kwa Weisiko, naye angemtuliza. Mambo yote mabaya yaliyompata kwa sababu ya mwanaume huyu yakawa yametoweka kwake, na sasa ikawa kama vile huyu ndiyo mkombozi wake.

Siku kadhaa zilizofuata, Luteni Weisiko, kwa msaada wa Kanali Jacob, akawa amefanya mipango tayari ili kumtoa Azra nchini huku na kumpeleka nchini India. Kanali Jacob alijuana na watu kule ambao wangeweza kumhifadhi binti huyo sehemu ya mbali kwa muda mrefu, naye Weisiko akamhakikishia Azra kwamba angekwenda huko pia baada ya kumaliza kazi fulani huku ili wawe pamoja, kwa kuwa Azra angetangulia. Binti bado hakujihisi usalama mikononi mwa watu wengine, hivyo kwenda na hawa wageni ndiyo ilimfanya aogope hata zaidi. Lakini Weisiko alikuwa amemwambia asiogope, kwa sababu alipaswa kujitahidi kuwa imara zaidi kwa ajili ya "baba yake" ili waje kuwa pamoja.

Kwa hiyo binti akapaa kuelekea kwenye himaya mpya kabisa kwenye maisha yake, akiyaacha maisha ya zamani na kwenda kuanza mapya kabisa.


★★★


Mwanaume aliyekuwa amemchukua Azra na kumpeleka India aliitwa Vivek Nambiar. Huyu alikuwa ni mshiriki mkubwa kutoka kwenye shirika kubwa la kimisaada kutokea India, ambalo lilikuwa na sehemu kubwa pia nchini Tanzania kwa miaka mingi. Lakini kama vile Makamu wa Raisi Paul Mdeme na Kanali Jacob tu, mwanaume huyo alikuwa ni mfisadi wa hali ya juu, akitumia njia mbaya kujipatia mali huku akijifanya mwema kwa kujihusisha na utoaji wa misaada.

Kikundi cha watu wa jamii yao kilikuwa nchini Tanzania, na ingawa wengi walifanya mambo mengi kama kusaidia katika sekta za elimu, afya, na mahitaji mbalimbali kama maji, bado watu kama Nambiar walifanya uovu usioonekana kwa njia ya moja kwa moja kupitia shughuli hizo hizo. Kwa hiyo lengo la Kanali Jacob Rweyemamu la kumpeleka Azra mafichoni lakini kwa mwanaume huyo kihususa, ilikuwa ni ili amjenge kuwa aina ya mtu ambaye angekuja kuwa msaada katika mipango yao ya baadae.

Sehemu ambayo Azra alipelekwa ilikuwa kwenye eneo lililojulikana kama Kerala, lakini ilikuwa ndani sana kwenye milima na misitu. Huko kulikuwa na majengo ya kale ambayo yalionwa kama mahekalu, na yalitunzwa kisiri sana kwa muda mrefu. Nambiar alijuana na baadhi ya watu wa huko, ambao walikuwa na tamaduni zile za ndani sana. Mara nyingi walipeleka watu fulani huko ili kuwatengeneza kwa njia mbalimbali kuendana na viwango vyao kiakili na kimwili, lakini hasa watoto wadogo. Wangefundishwa tamaduni za hapa na pale, kisha baadae wangekuja kutumiwa katika masuala mbalimbali kijamii ili kuonyesha tamaduni hizo, au watu hao waliowatunza kupata malipo ya hali ya juu kutoka kwa watu waliowapeleka watoto hao huko.

Kulikuwa na mafunzo ya aina mbalimbali hasa kwa ajili ya maonyesho, muziki, kupigana, na kujihami, na baada ya Azra kukaa huko kwa kipindi cha mwaka mzima, mwanamke mmoja mzee aliyeitwa Madhava Gopinath, ambaye alikuwa mmoja wa walimu huko, aliona kitu fulani ndani ya Azra ambacho kilimwambia kwamba binti huyo angeweza kujifunza mtindo fulani wa kupigana uliokuwa nadra sana kwa wengine kufundishwa.

Mtindo huo ulifundishwa karne na karne nyingi zilizopita, lakini ulikuwa ni mtindo hatari sana endapo ungetumiwa vibaya. Hivyo kwa muda mrefu uliacha kufundishwa, na hata wengi walidhani haukuwahi kuwepo. Ni mtindo uliohitaji kiwango cha juu cha imani kutoka kwa mwalimu ili amfundishe mwanafunzi ambaye alionekana kuwa na utu unaofaa ili kutoutumia vibaya. Na mwanamke huyo akaona jambo hilo kwa Azra.

Kwa muda wote ambao Azra aliishi huko, hakuwa akiongea. Mwanzoni alikuwa akijitenga lakini baada ya muda akawa akichangamana na wengine na kufuata maagizo yote aliyopewa, lakini bado alikuwa haongei kwa mdomo. Mwanamke huyo mzee alianza kujenga ukaribu naye zaidi na hivyo kumwelewa vizuri hata zaidi, kwa hiyo baada ya muda alianza kumfundisha njia hiyo pekee ya kupigana na kujihami. Hii haikuwa kati ya mitindo ambayo Kanali Jacob na Weisiko walitazamia Azra kufundishwa, kwa hiyo ikawa ni nyongeza ya siri kwenye mafunzo yake.

Mwanamke huyo alimfundisha mambo mengi sana, na Azra akampenda kama bibi yake. Weisiko alikuwa na kawaida ya kwenda India ili kutumia muda pamoja na "binti yake," na kwa kipindi cha miaka michache ambayo Azra aliendelea kuishi India, alipata aina fulani mpya ya furaha na kujihisi huru na salama. Lakini hilo lisingechelewa kuharibiwa.


★★★


Baada ya Azra kuwa ameishi India kwa miaka zaidi ya saba, Weisiko, sasa akiwa ni Luteni Jenerali, alikwenda na kumchukua kutoka huko ili kumrudisha nchini. Sasa akiwa ni mwanamke mdogo, aliyekuwa na sura nzuri na mwonekano wenye kuvutia, alirudi kwenye nchi yake ambayo hakuwa na kumbukumbu ya mambo mengi kuihusu. Hii Ilikuwa ni kwa sababu kwa kipindi chote alichoishi India alikuwa akipewa dawa kupitia Weisiko ambazo alifikirishwa zilikuwa zinamsaidia kiafya, lakini ndiyo zilikuwa zinafanya asikumbuke maisha yake ya zamani. Angalau wakati huu aliweza kuzungumza tena, na alijua lugha tatu; Kiingereza, Kihindi, na Kiswahili, ingawa hakuzungumza Kiswahili kabisa.

Luteni Jenerali Weisiko alimpeleka binti yake huyu kwenye makao yake mapya, ambako Ilikuwa ni kwenye moja kati ya nyumba za kifahari za Weisiko. Hii ingekuwa nyumba ya Azra pekee, naye alifurahia sana kuona kwamba "baba yake" alikuwa amempatia zawadi nzuri kama hiyo kwenye siku yake ya kwanza nchini humu. Alitarajia kwa hamu sana kuanza kukutana na watu wengine na hata kujenga marafiki, lakini matarajio yake yakazimwa baada ya Weisiko kumwambia kwamba asingeweza kwenda sehemu yoyote ile na kuchangamana na watu isipokuwa mpaka amwambie kufanya hivyo.

Kwa kutoelewa sababu, Azra aliuliza ni kwa nini, na ndiyo hapa Weisiko akaanza kuijaza akili yake kwa uwongo mwingi sana kuhusiana na maisha yake ya nyuma. Alimwambia sababu iliyofanya mpaka akashindwa kukumbuka mambo ya nyuma ni kutokana na ile "ajali" iliyompata, lakini kuna watu ambao waliisababisha ajali hiyo na hivyo kuharibu maisha yao wakiwa familia. Alimwambia kuwa watu kama hao wangetaka kumdhuru endapo wangejua aliokoka, na ndiyo sababu alimhamisha kutoka huku na kumpeleka Kerala. Akamwambia mafunzo aliyopokea kule yalikuwa ili kumsaidia awe imara, lakini pia endapo maadui wao wangewazingua basi amsaidie kuwafutilia mbali.

Azra alichanganywa sana mwanzoni. Alikuwa amefundishwa kutumia vipawa vyake KUJIHAMI na siyo KUUMIZA mtu, lakini Weisiko alichokuwa anamwambia ilikuwa kwamba endapo angemwomba amshughulikie mtu na kumwondoa kabisa, basi atii. Weisiko alijiweka kwenye upande ulioonekana kuwa mwema, akisema hangemwomba kamwe aue mtu asiyekuwa na hatia, bali wale tu ambao walifanya mambo mabaya kupitiliza. Akamwambia ndiyo sababu alihitaji kukaa kwa siri ili kulinda utambulisho wake. Kwa sababu Azra alimheshimu kama "baba yake" aliafikiana na yale aliyokuwa amemwambia, ijapokuwa moyoni mwake hakuhisi amani.

Kwa hiyo baada ya muda fulani kupita akiwa nchini, Azra aliendelea kukaa mwenyewe, na maisha kwake yalikuwa mazuri na ya hali ya juu kutokana na vitu alivyopewa na Weisiko. Hakuwa tu mtu wa kukaa ndani ya nyumba asubuhi mpaka asubuhi, kwa sababu mara kwa mara alitoka na kwenda kutembea sehemu mbalimbali akiwa mwenyewe, lakini kwa umakini wa hali ya juu. Aliwakumbuka sana baadhi ya watu waliokuwa kama marafiki kwake kule India, na hata mara kwa mara angehisi uhitaji wa kujenga marafiki huku, lakini Weisiko aliendelea kuwa karibu naye kama "baba" ili kutomfanya ahisi upweke.

Ndipo baada ya siku kadhaa kupita baada ya tukio la wizi wa trilioni 20 kwenye benki kuu, Luteni Jenerali Weisiko alikuja kwake na kumwambia kuwa angempa "mission" mpya iliyomhitaji kuwakamata watu wa kundi la Mess Makers na kuwaua. Azra alihofia kwamba huenda asingeweza kutimiza aliyotaka "baba yake," lakini Weisiko akamwambia hakupaswa kuogopa. Alimwambia njia walikuwa wameshamtengenezea, hivyo yeye angepaswa kufanya vitendo tu na kujiondoa sehemu za tukio haraka bila kutambulika. Alitumia kigezo cha kwamba Mess Makers waliumiza na kuua watu wengi tokea walipolipua mabomu kwenye majengo yale, na bado walikuwa wakiendelea kuisumbua serikali, hivyo msaada wake wa siri ungethaminiwa sana.

Azra alikuwa amefunzwa kuwa makini sana, hivyo aliuliza kwa kina mambo aliyohitaji kufanya, ikiwa labda angeshambuliwa na mtu ambaye hakutakiwa kumuumiza, naye Weisiko akatoa kibali cha kuua tu. Alimwambia ilikuwa ni muhimu kwake kufanikiwa katika yote aliyotakiwa kufanya, kwa sababu Raisi alikuwa ameiharibu nchi sana. Ijapokuwa mwanzoni Weisiko alimshawishi kwa kusema anafanya hayo kama njia ya kuwasaidia watu, Azra alikuwa na akili kutambua kwamba kwa jambo hili Weisiko alikuwa anamtumia kama silaha yake maalum, lakini akaacha iwe hivyo tu ili kumridhisha "baba yake" huyo.

Kazi ya kwanza katika mishe hiyo ilikuwa ni kuiweka timu ya Luteni Michael na ACP Nora karibu na macho yake, ili hatimaye aweze kuwafikia Mess Makers. Haikuwa rahisi kwake hata kidogo mara ya kwanza kabisa alipolazimika kuwaua wanajeshi wale watatu, Vedastus, Omari, na Mishashi, pamoja na Oscar Amari wa Mess Makers. Usiku huo alipotoka kwenye mauaji hayo aliyoyafanya kwa mikono yake mwenyewe, alikwenda sehemu ya mbali na kuanza kulia sana. Alilia mno, kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuondoa uhai wa wanadamu wenzake. Tokea alipopelekwa India, Azra alikuwa mwenye uhitaji wa kujua ni nini lililokuwa kusudi la maisha yake, na sasa ikawa ni kama limefunuliwa wazi mbele yake. Akaamua tu kuliishi sasa, kwa kuwa hicho ndiyo kitu alichotengenezwa kuwa; muuaji.

Weisiko alimmwagia sifa baada ya matokeo ya kwanza ya kile alichofanya, akifikiri kwamba Azra alifurahia sana, lakini kiukweli alikuwa amembomoa kupita maelezo. Furaha aliyokuwa amekuja nayo nchini ilitoweka kuanzia usiku huo alipowaua wanaume wale, na moyo wake ukaanza kugeuka kuwa mgumu zaidi kwa sababu ya hisia za kujichukia. Hakuwekwa wazi kuhusu mambo ambayo Mdeme alikuwa amefanya pamoja na kundi lake kwa muda mrefu, akifikirishwa kwamba yeye yuko upande sahihi kwa sababu ya uwongo ambao "baba yake" alikuwa akiilisha akili yake.

Kwa hiyo kutokea hapo angeendelea kutulia mpaka akiambiwa cha kufanya na Weisiko, naye angetekeleza aliyoambiwa ili tu kumfurahisha, mpaka wakati ambao aliagizwa kumuua Salim Khan....


★★★★


WAKATI ULIOPO....


Siku hiyo ambayo Salim Khan alinyongwa kwenye lifti kikatili sana, Azra alipatwa na jambo fulani ambalo liliisumbua akili yake baada ya kufanya mauaji hayo. Wakati akiwa anapigana na mmoja wa Mess Makers, yaani Lexi, alishindwa kuelewa ni kwa nini mwanamke huyo alijifichua kwake, halafu akaanza kumwita kwa jina la "Azra." Aliendelea kupigana naye, huku Lexi akijitahidi kumwambia aache, lakini Azra hakusikiliza na kufanikiwa kumpiga kwa mtindo wake uliommaliza nguvu Lexi mikononi.

Azra aliposhika kisu na kumfata Lexi akiwa na nia ya kuikata shingo yake, mkono wake ukasita baada ya akili yake kuanza kumwonyesha picha fulani ya mwanamke huyu, kama vile aliwahi kumwona kipindi cha nyuma. Alishindwa kuelewa hiyo ilikuwa ni kwa nini, lakini hisia aliyoipata ilimfanya ahisi ni kama anamfahamu, tena vizuri sana. Akashindwa hata kupitisha kisu kwenye shingo yake kutokana na kuchanganywa na hali hiyo, na ndipo wenzake na Lexi wakafika hapo.

Kwa sababu ya kutotarajia, Azra alishtuka na kuwa kama amepoteza umakini wake, na wakati Mensah alipomwelekezea bastola, akashangaa sana baada ya Lexi kumkinga na kupigwa yeye badala yake. Hapa ni kama umakini ndiyo ukamrudia, naye akatoka eneo hilo upesi na kukimbia kwa kasi yote. Akiwa anakimbia alisikia vizuri sana jinsi mwanamke yule aliyekuwa anakaribia kumchinja alipomwambia mwenzake kwamba asimpige (Azra) risasi, naye Azra akafanikiwa kukimbilia upande mwingine wa uwanja huo na kujificha pembeni ya ukuta; pakiwa na giza.

Maswali mengi sana yalipita kwenye kichwa chake. Mwanamke huyo alikuwa ni nani? Na kwa nini alimkinga asipigwe na risasi? Ni kwa nini alimwita kwa jina ambalo hakuwa na utambuzi wowote kulihusu? Na jambo la muhimu hata zaidi, ni kwa nini yeye Azra alishindwa kumuua alipopata nafasi rahisi zaidi? Kwa kukosa majibu sahihi na kufikiria hali aliyokuwa ndani yake, akaamua tu kuondoka eneo hilo haraka.


★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom