Simulizi: For You

dah kit kinazid kuchanja mbuga
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


"Hatimaye!" Nora akasema kwa njia yenye kejeli.

Lexi akaendelea tu kumtazama.

"Caught in the act. Ahah... nakuogopesha bado? Mbona inaonekana ni kama mimi ndiyo nayepaswa kuogopa? Mm? I mean... hao watu wote walio hapo chini wananifanya natetema kwenye mabuti yangu sasa hivi," Nora akasema.

"Nora..."

"SHUT UP!" Nora akafoka kwa nguvu.

Lexi akatulia tu. Pumzi za Nora zikaanza kuongezeka kasi. Alikuwa na hasira kali sana kwa kuhisi amesalitiwa.

"Sogea hapa," Nora akasema.

Lexi akaendelea kusimama tu.

"Nimesema sogea, sitaki mchezo, nitakupasua kichwa!" Nora akasema kwa ukali.

Lexi akatii. Hakuona haja tena ya kukimbia, na kiukweli ilikuwa ni kama hisia za maumivu za Nora zilimfanya ajutie sana, na hiyo ikamtia udhaifu. Akatembea taratibu mpaka sehemu hiyo iliyokuwa na uwazi kiasi, naye akasimama hapo huku Nora akiwa bado amemwelekezea bastola.

"Kwa hiyo... familia yako... iliyokuwa na matatizo mengi sana kwa hizo siku mbili... ndiyo Mess Makers?" Nora akauliza.

"Hautaweza kuelewa.... kuna mambo mengi...."

"No, sihitaji kuelewa chochote. Kila kitu kiko wazi. Wewe ni mwizi. Wewe ni muuaji. Wewe ni mwongo. Wewe ni mshenzi Lexi!" Nora akasema.

Lexi akabaki kumtazama.

"Hivi akili yangu ilikuwa wapi? Yaani... unajua kama ni tuzo, we mwanamke unastahili tuzo ya mwaka ya kuwa mshenzi bora kuliko washenzi wote waliowahi kuwepo. Akili yako imejaa uozo, na mimi... ukaniambukiza. Nijitetee kwamba nilikuwa sijui? Unajua siyo natural kabisa, labda uliniroga. Mimi kutoka tu na mwanamke haikuwahi kuingia akilini mwangu. Ulifanyaje? Uchawi wa 'Mess Makers,' si ndiyo? Unapata faida gani Lexi kwa kuumiza hawa watu wote? Kwa kuniumiza mimi? Mbona uko tofauti kabisa na kile ambacho sura yako inaonyesha? Kwa nini unafanya mambo yote haya? Eeh?" Nora akazungumza kwa hisia.

Lexi akadondosha chozi na kusema kwa mkazo, "Ni kwa sababu ya baba yako."

Nora akakunja uso wake kimaswali.

"Baba yangu amefanya nini?" akauliza.

"Ni yeye ndiye chanzo cha maisha yangu kuwa namna hii. Aliniibia aina ya maisha ambayo nilitaka kuwa nayo nikiwa bado mdogo... na ingawa najua hutaweza kunielewa leo, ipo siku utaelewa," Lexi akasema kwa hisia.

"Ahah... ahahahah... Unapenda maigizo sana. Lakini unajua... unastahili pongezi. Hakuna mtu ambaye amewahi kufanya mambo uliyofanya kwenye hii nchi, na hapo kiukweli lazima tu nikupe respect. Ila ukitegemea kwamba baada ya kila kitu ambacho umefanya kuna mtu ataamini upuuzi wowote unaoongea... dada yangu umefeli sana. Yaani wewe haufai. Wewe ni nyoka zaidi ya nyoka. Na unajua sikuzote mwisho wa nyoka ni kupondwa tu kichwa... na hicho ndiyo kitakachokupata wewe," Nora akasema.

"Basi unasubiri nini? Niponde," Lexi akasema.

"Nini?"

"Niponde kichwa sasa hivi!" Lexi akasema kwa sauti yenye ukali.

"Usinisemeshe hivyo Lexi, nitakupasua!" Nora akamwonya.

"Go ahead. Do it!" Lexi akamwambia na kuanza kumfata.

"Usinijaribu Lexi! Tulia hapo hapo ulipo...."

"Unafikiri mimi nilipenda kuwa na maisha ya namna hii? Unafikiri sikutaka kuja kuoa, kuwa na watoto, kuishi maisha mazuri ya familia? Nilitaka kuwa na vitu hivyo, lakini baba yako akaviiba kutoka kwangu!" Lexi akaongea kwa hasira.

"Acha kuongea upuuzi! You're nothing but a psychopath!" Nora akasema kwa ukali.

Lexi akasimama mbele ya bastola ya Nora na kusema, "Maybe I am. Na kila kitu ambacho nimefanya sijafanya kwa sababu za kibinafsi tu. Ndiyo kuna watu wameumia, lakini angalau sikuwaumiza kwa kudhamiria. Baba yako aliua watu zaidi ya 200, wazazi wangu included. Ungejua, ungekuwa unajua hata chembe ndogo ya mambo niliyopitia usingenihukumu hata kidogo," Lexi akaongea kwa mkazo.

Nora akawa anatikisa kichwa kukataa mambo aliyosikia.

"Haijalishi nimefanya nini. Sijutii. Na sitajali hata mbwa yeyote akisema nini. Na kwa sababu hiyo, ninakuomba ukipasue kichwa changu," Lexi akasema.

Nora akawa anapumua kwa hasira.

Lexi akasogea nyuma kidogo na kusema, "Do it."

Mikono ya Nora iliyoshikilia bastola ikaanza kushuka taratibu na kufanya batola hiyo ielekee kifuani kwa Lexi.

"Oh reminder, unajua hii ni proof, kwa hiyo usipige kifuani, nilenge kichwa ukipasue!" Lexi akasema kwa ukali.

Nora akaendelea kumtazama kwa hisia nyingi zilizovurugika, akihisi kusalitiwa, hasira, hatia, huzuni, na kuchanganywa sana na kila jambo. Alishindwa kuelewa ikiwa hicho ndani ya Lexi kilikuwa ni kiburi, au kuna jambo lingine lililokuwa nyuma ya pazia kubwa lililoficha siri nyingi kumhusu "mwanamke" huyo. Hasira aliyokuwa nayo ilimtaka ampasue kichwa ukweli, lakini kuna kitu kikawa kinamzuia.

Lexi alikuwa anamwangalia kwa njia fulani iliyoonyesha huzuni, akitambua ni jinsi gani mwanamke huyu alivyokuwa ameumizwa sana kujua ukweli kumhusu. Lakini alijua pia kwamba kwa jinsi mambo yalivyokuwa yamejitengeneza mpaka kufikia hatua hii, isingekuwa rahisi sana kumshawishi Nora kukubali kwamba upande aliotumikia ulikuwa mbaya sana, kwa hiyo kama angeamua kumuua, basi alikuwa tayari kwa hilo.

Wakiwa bado wanaangaliana huku Nora akiwa bado ameielekeza bastola yake kwa Lexi, gari mbili ngumu sana za kijeshi zikaingia eneo hilo walilosimama kwa kuvunja kuta za pembeni zilizozunguka jengo hilo kubwa. Wote walibaki kuzitazama tu mpaka ziliposimama usawa wao, kisha kwenye gari la kwanza wakashuka wanaume wawili na mwanamke mmoja, waliovalia nguo za kijeshi huku wakiwa wameelekeza bunduki kwa Lexi na Nora na kuanza kuwafafa. Hao walikuwa ni Tariq, Rachel na Zachary. Nora akawatambua haraka wale walioanza kushuka kwenye gari la pili, nao walikuwa ni Alex, Mario, Hussein na mwanaume wa kazi, Luteni Michael mwenyewe.

Nora akashusha mikono yake iliyomwelekezea Lexi bastola, ambaye alikuwa amesimama kwa utulivu tu huku anamwangalia Nora machoni kwa hisia. Luteni Michael akawa anawaelekea huku amekaza sura yake kwa hasira.

"Nilichosema Nora, na wewe ukajifanya unajua sana kusoma mioyo. Nini hiki sasa? Rafiki yako ndiye msaliti," Luteni Michael akawa anaongea.

Nora akabaki kumtazama tu. Wanajeshi wa Luteni Michael wakawa wamewazingira Lexi na Nora huku wamewaelekezea bunduki mpaka Luteni alipofika karibu zaidi.

"Unapaswa ujue njia za mwovu sikuzote ni fupi malaya wewe. Umefanya wengine watoroke ndiyo, lakini nitahakikisha unapanua mdomo kusema wako wapi kama unavyowatanulia hiyo shombo yako!" Luteni Michael akamtolea maneno makali Lexi.

Lexi akabaki kimya tu. Hakuwa na njia nyingine ya kutoroka hili. Luteni Michael akamsogelea karibu zaidi akimwangalia kwa hasira. Baadhi ya majasusi wale waliokuwa wameumizwa kwa risasi wakawa wanawaambia wawapatie msaada, naye Alex, Rachel, pamoja na Zachary wakawafata ili kuwapa huduma na kuita magari ya hospitali ya dharura.

"Ahah... Mario, Hussein, bado mnamwona huyu kuwa rafiki mtakatifu na wa kawaida tu wa ACP? Angalieni hao jamaa wote hapo chini, mwanamke ndala ndefu kweli kweli! Tukikutoa hapa mpumbavu wewe na kukupeleka sehemu nyingine, jua kwamba utaumia sana. Kwa hiyo ni bora useme washenzi wenzio walipo malaya mkubwa wewe!"

Luteni akaendelea kutoa kashifa, lakini Lexi akabaki kimya tu.

"Mhm... nisingetarajia lolote la maana kutoka kwa mtu kama wewe. Toka mara ya kwanza nilipokuona nilijua tu wewe ni mfano halisi wa Shetani. Unatia sana kinyaa. Tundu la mama yako ni lazima liwe linajuta kukuleta kwenye hii dunia..."

Wee! Hapo Luteni Michael akawa amegusa pabaya. Lexi akamtazama kwa hisia kali sana. Maneno yake mengine yote kumhusu angeweza kuyapuuzia, lakini baada ya kumkashifu na mama yake, alishikwa na hasira kali kupita maelezo.

"Na itakuwa wazi zaidi baa...."

Kabla Luteni Michael hajamaliza kuongea, Lexi alimtandika ngumi mbili za haraka na nzito sana usoni kwake, kisha akaivuta nyingine ya nguvu sana huku akiruka na kumtandika usoni tena. Wanajeshi wake wakaanza kumfuata Lexi, lakini Luteni Michael akawazuia baada ya kurudi nyuma kidogo. Akawaambia watulie ili ashughulike naye yeye mwenyewe. Kisha akaanza kumfata na kujaribu kumshika, lakini Lexi akaipiga pembeni mikono yake kwa nguvu na kumwasha kofi usoni! Wengine wakabaki kuwaangalia kwa mshangao kiasi.

Luteni Michael akakasirika na kumrushia ngumi, lakini Lexi akakwepa na wakati huo huo kumpiga tumboni na chini ya kidevu kwa kasi sana. Muda si muda, wawili hawa wakawa wanapigana. Walipigana kama wanaume, ijapokuwa Lexi alionekana kuwa mdogo sana kwa Luteni Michael hasa kutokana na mwili wake kuwa wa mwanamke. Nora alikuwa anawaambia kwa sauti ya juu waache, lakini wakaendelea kutandikana sana. Luteni Michael alikuwa anashangaa kiasi kuona jinsi ambavyo Lexi alimsumbua sana, hata alipompiga ngumi zake nzito, "mwanamke" huyu alikuwa na kiwango cha juu sana cha kustahimili maumivu na kuendelea kupambana naye bila woga wowote.

Pamoja na Luteni Michael kuwa na mwili mkubwa na uliokomaa sana, Lexi hakuwa nyuma kujibu mapigo yake. Alitumia mtindo wa kupigana kama bondia fulani hivi, na sasa akaonekana akivuja damu puani na pembezoni mwa jicho lake, huku Michael akiwa na vimbe (nundu) kadhaa usoni kwa sababu ya ngumi za haraka za Lexi. Wakaangushana chini wakiwa wanaendelea kutandikana haswa, na kufikia hapa walikuwa wamesogea usawa ule wa kuta zilizobomolewa magari yale mawili yalipoingia hapo.

Luteni Michael akaja juu ya Lexi na kuanza kushusha ngumi nzito akilenga uso wake, lakini Lexi akawa anauziba, kisha kwa akili akamgeuza na yeye ili awe chini, naye akawa anampiga ngumi za tumbo Michael huku jamaa akimkaba kwa mkono wake mmoja usawa wa ubavu wake. Lexi hakukata tamaa. Maneno yale ya Luteni Michael yalifanya kumbukumbu za mama yake zimrudie, jinsi alivyouliwa usiku ule mbele yake. Hangeweza kuvumilia mtu yeyote ambaye angesema jambo baya kumhusu.

Nora alikuwa anapiga sana kelele kumwambia Luteni Michael aache kupigana na mwanamke, huku Mario na Hussein wakimshikilia kwa nguvu ili asijiingize pale, na wao wakitazama pambano hilo zito. Luteni Michael akafanikiwa kumsukuma Lexi pembeni, kisha akaokota jiwe la tofali moja lililobomoka chini hapo na kumrukia nalo akitaka kumpiga, lakini Lexi akakwepa kwa kujiviringisha akiwa amelala chini bado. Kwa mtindo wa sarakasi, Lexi akajinyanyua kwa kuizungusha miguu hewani na kufanikiwa kumtandika usoni kwa mguu mmoja, naye Luteni Michael alipoweweseka kidogo, Lexi akausawazisha mwili wake na kumpiga miguuni, jambo lililofanya Michael aanguke na kubamiza kichwa chake chini kwa nguvu.

Maumivu yaliyompata wakati huu yalikuwa makali, na kwa sekunde chache akashindwa kujinyanyua baada ya pigo hilo, na hapo hapo Lexi akamfuata chini na kuendelea kumtandika ngumi za usoni. Alikuwa anampiga huku analia kwa hasira nyingi, huku Luteni Michael akijaribu kuficha uso wake na kumdhibiti kwa wakati ule ule, lakini bado Lexi akaendelea tu. Jambo hili liliwashangaza hata wanajeshi wa Luteni Michael kwa sababu ilionekana ni kama Lexi amemzidi nguvu mwanaume huyo.

Kwa hasira alizokuwa nazo, Lexi akachukua jiwe zito la tofali lililokuwa pembeni kidogo na kulinyanyua juu ili amponde nalo kichwani, na ile Tariq alipotaka kuwahi ili amzuie, Lexi akafanikiwa kulishusha kwa nguvu na kuponda! Wote walishangaa sana na kubaki wametazama tu chini hapo, na Tariq akasimama akimwangalia Lexi kwa makini. Wanajeshi wote walikuwa wanaangaliana wasiamini kama kweli Luteni wao mwenye mafunzo na uwezo mkubwa alikuwa ameshindwa kwenye pambano hilo na "mwanamke."

Lexi akawa anapumua kwa nguvu na kwa kasi sana, huku jasho na damu vikimtoka usoni. Akajitoa juu ya Luteni Michael taratibu na kukaa pembeni, akipumua kwa uchovu huku anamwangalia Luteni huyo. Luteni Michael akaangalia tofali hilo taratibu, ambalo Lexi alikuwa ameponda pembeni kidogo tu na kichwa chake, na siyo yeye. Lexi akageuza shingo yake taratibu na kumtazama Nora usoni kwa hisia, akihisi maumivu mengi mwilini mwake, naye Nora akashindwa kujizuia kumwangalia kwa huruma.

Mario na Hussein wakamwachia Nora na kwenda kumsaidia Luteni Michael asimame, naye Tariq pamoja na Alex wakamnyanyua Lexi na kumfunga pingu mikononi. Luteni Michael alikuwa anamtazama Lexi kimaswali sana. "Mwanamke" huyo angeweza kumuua kama alitaka, lakini hakufanya hivyo. Hakujua lengo lake lilikuwa nini, au alijaribu kuthibitisha nini, lakini hiyo haikuwa sababu ya kumwona kuwa mtu mzuri. Bado alimchukia sana kwa sababu ya mambo mengi yeye na watu wake waliyofanya.

Luteni Michael akawaamuru wanajeshi wake wampeleke Lexi ndani ya gari, nao wakatii na kumpeleka upesi. Bado Nora alikuwa amesimama hapo tu kama mtu aliyeghafilika sana, hivyo Luteni Michael akamfata na kumwambia walipaswa kuondoka haraka. Akamwongoza mpaka kwenye gari lake (Nora) na kuingia pamoja naye, kisha akamwomba yeye ndiyo aendeshe, nao wakaondoka kutoka kwenye jengo hilo. Tariq, Alex, Mario na Hussein ndiyo ambao waliongoza gari lililombeba Lexi, wakiwaacha Rachel na Zachary pamoja na majasusi wale walioumizwa ili kuangalia mahitaji yao mpaka msaada ukifika.

Jengo hilo la kampuni ya Kendrick lilikuwa limegeuka kuwa kama uwanja mdogo wa vita kwa usiku huo. Mambo yaliharibika sana. Mtu muhimu zaidi wa kundi la Mess Makers alikuwa amekamatwa, na hii ilikuwa ni pigo kubwa kwa wale waliobaki. Lexi alikuwa akimuwaza sana Azra. Alikuwa tu ametoka kumwahidi kwamba hangeruhusu jambo lingine liwatenganishe, lakini sasa akawa mbali naye tena. Mara nyingi hisia huongoza watu kuchukua maamuzi mabaya, na kila mara alipofikiria jinsi alivyohatarisha uhai wake kwa sababu ya hisia zake, akajiona mbinafsi sana kwa kuwa ni kama alimsahau Azra. Sasa isingekuwa rahisi kutoka mikononi mwa wabaya wao, na hapa alijua kilichokuwa kikimsubiri huko mbele ni kifo tu.

Kulikuwa na ukimya sana baina ya Luteni Michael na ACP Nora kwenye safari hii ya kumpeleka Lexi akiwa mfungwa rasmi. Luteni Michael alimjulisha Kanali Oswald Deule kwamba alikuwa amemkamata mtu aliyeamini kuwa kitovu kikubwa cha kundi la Mess Makers, na sasa walikuwa njiani kumpeleka kwenye sehemu yao ili kumfunga. Lakini Kanali akamwambia wampeleke kwenye jengo lile maalumu la usalama wa taifa ili wakamhoji huko, akisema kwamba yeye alikuwa huko pamoja na viongozi wengine pia.

Luteni Michael akatii, na safari ya kuelekea huko ikaendelea.


★★★★


Baada ya kumfikisha Lexi huko, Luteni Michael na ACP Nora walikwenda pamoja naye mpaka sehemu za ndani za jengo hilo, na kadiri walivyozidi kuingia ndani ndivyo wanajeshi kadhaa walivyoongezeka ili kuwasindikiza. Walipofika sehemu fulani za ndani zenye korido kadhaa zilizoachana, Lexi akapelekwa upande mwingine, nao wakina Luteni na ACP wakaelekea ule mwingine. Lexi alikuwa akipelekwa sehemu yenye chumba maalumu cha mahojiano, na wengine wakaelekea kwenye ofisi ambayo viongozi wale wengine walikuwepo.

Walipofika kwenye ofisi hizo, Luteni Michael na ACP Nora waliwakuta viongozi wawili wa jeshi la nchi; Kanali Oswald Deule pamoja na Kapteni Erasto Shimuye, na viongozi wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Donald Ngassa na Kamishna wa Polisi (CP) Patrick Msuwa. Luteni Michael na ACP Nora wakawapa wote salamu za heshima, kisha wakaanza kuwaelezea yale yote yaliyotokea. Muda ulikuwa umesonga sana, ikiwa inakaribia saa 7 usiku sasa, lakini hakuna yeyote hapo aliyewaza kuhusu usingizi.

Nora alilaumiwa sana kwa sababu ya kuamini mtu ambaye alikuwa ni adui, na hivyo kusababisha siri za mipango yao mingi kuwa wazi kwa watu hao waliowaona kuwa wabaya. Mambo mengi yakasemwa kuhusu mipango yao kuharibika na ikaonekana kwamba Nora alikuwa amechangia sana kuleta matatizo hayo. Mwanamke huyu alibaki kimya tu akipokea lawama hizo, na kiukweli hakukazia sana fikira walichosema kwa kuwa akili yake ilikuwa ikitafakari yale yote yaliyotokea, na ambayo Lexi alimwambia kwenye jengo lile.



Lexi akawa ameketi kwenye kiti mbele ya meza fupi, akisubirishwa mahojiano kati yake na mtu ambaye angehusika. Alifahamu vizuri hatua na taratibu hizi, hivyo akawa ametulia tu huku mikono yake ikiwa juu ya meza ikifungwa kwa pingu. Nguo zake maalum za mapambano zilikuwa zimeondolewa mwilini mwake, hivyo sasa alikuwa amebaki na T-shirt nyeusi yenye mikono mirefu na suruali nyeusi pia; za mtindo wa aina moja.

Kuna mwanamke fulani akaingia ambaye alikuwa amevalia nguo za kijeshi pia, naye akaanza kuusafisha uso wa Lexi uliokuwa umechafuliwa kwa damu na uvimbe mdogo sehemu kadhaa. Lexi alitulia tu, akiliona jambo hili kama kejeli ya aina fulani ambayo watu hawa walikuwa wakimfanyia, na baada ya mwanamke huyo kumwekea plasta chache usoni, akatoka ndani hapo.

Chumba hiki kilikuwa kidogo, chenye mwanga hafifu wa taa iliyomulika kutokea juu ya ukuta katikati, nacho hakikuwa na kitu kingine chochote zaidi ya meza hiyo, viti viwili, na Lexi pekee. Kutokea juu ya ukuta mmoja kulikuwa na kitu kama kioo kipana, ambacho Lexi angeweza kujiona kila wakati alipokiangalia. Nje ya chumba hicho walikuwepo wanajeshi kadhaa waliolinda sehemu hiyo.



Luteni Michael, Kapteni Erasto, Kanali Oswald, IGP Donald, CP Patrick, na ACP Nora walitoka kwenye ofisi za kule walikokuwa na kuja upande wa pili wa chumba hicho ambacho Lexi alikuwa amewekwa. Walikuwa bado wakijadili kuhusiana na kukamatwa kwake baada ya kufahamika kuwa alikuwa mmoja wa kundi la Mess Makers, na ni hatua zipi zichukuliwe dhidi yake kwa sababu ya kundi hilo kusababisha hasara nyingi kitaifa.

Kanali Oswald Deule, akiwa ndiyo mwenye cheo kikubwa zaidi kwa waliokuwa hapo, alipendekeza kwamba baada ya kufanya jitihada zote za kuhakikisha Lexi anatoboa siri zote za kundi lao, walipaswa kumpa mateso makali sana ili iwe somo na fundisho kwa wengine. Ijapokuwa lilikuwa ni jambo lililokubaliwa na wengine, halikumpendeza Nora hata kidogo. Akawaambia kwamba hakukuwa na haja ya kumuumiza mwanamke huyu kwa sababu haingesaidia lolote; kwamba walikuwa wameshamkamata, hivyo kama ni kumtumia ili kuwapata wengine, na hasa Kendrick Jabari, basi ingetosha, na njia inayofaa zaidi ya kumwadhibu ni kifungo.

Lakini pendekezo lake lilipuuzwa, naye Kanali Oswald akamwambia Luteni Michael kuwa ikiwa baada ya Kapteni Erasto kumhoji Lexi na mwanamke huyo asiseme lolote, basi amfunge kwenye chumba chenye giza na kupeleka wanajeshi wampe mateso mpaka aseme kila kitu; lakini wahakikishe hafi. Alijua fika kwamba Lexi alikuwa mtu imara sana, hasa baada ya kuambiwa mambo aliyoyafanya kwa wale majasusi na maaskari muda mfupi nyuma, hivyo akamsihi sana Luteni Michael atumie njia mbadala kila wakati ili kuweza kumvunja (kiakili) na kumfanya amwage mtama.

Nora akaomba yeye ndiye awe wa kumhoji Lexi kwa kuwa kwa kipindi fulani alikuwa pamoja naye sana hivyo alijua jinsi ya kuzungumza naye kwa njia ambayo ingemfanya afunguke kwa mambo mengi, lakini Kanali Oswald akapinga hilo na kumwambia kwamba wakumhoji angekuwa ni Kapteni Erasto na si mwingine. Luteni Michael alimwangalia Nora kwa umakini, akijua kabisa kwamba mwanamke huyu alikuwa akiumia kihisia kwa sababu mtu aliyemwamini alikuwa ndiye mtu aliyemsaliti kwa muda mrefu sana. Alimwonea huruma kwa kiasi fulani, lakini alitaka pia amwonyeshe ni jinsi gani alikuwa amekosea sana kumwamini mtu kama Lexi. Na sasa alikuwa akijionea.

Baada ya hapo, Kapteni Erasto akatoka walipokuwa na kuingia kwenye chumba kile alichokuwepo Lexi. Kilikuwa kimejengwa kwa chini kutokea walipokuwa wengine, hivyo wao waliweza kuwaona kupitia kioo kile kipana, lakini ambacho kama ungekuwa kwa ndani usingeweza kuona nje. Yaani, Lexi na Kapteni Erasto wakiwa ndani ya kile chumba wasingeweza kuwaona wakina Kanali, Luteni, IGP, CP na ACP Nora kwa kule juu, lakini hawa wangeweza kuwaona. Kulikuwa na vifaa vidogo vya sauti vilivyounganishwa kutokea kwenye chumba kile, hivyo wakina Nora wangeweza kusikia maongezi yao. Jeshi lilikuwa kimaendeleo zaidi!

Kapteni Erasto akaketi kiti cha pili na kutazamana na Lexi machoni. Alimwangalia kwa njia ya kawaida tu, naye Lexi alikuwa akimtazama kwa njia ambayo haikuonyesha hisia yoyote kabisa; yaani hakuogopa hata kidogo, bali alikuwa ametulia kabisa huku uso wake ulioumia ukionekana kuwa na damu zilizokauka kwa mbali baada ya "kusafishwa." Kapteni Erasto akatabasamu kikejeli, kisha akaweka mikono yake juu ya meza na kufanya kama anasogeza uso wake kumwelekea ili amtazame vizuri zaidi.

"Mambo vipi?" akamuuliza.

Lexi akabaki kimya tu.

"Sihitaji kujitambulisha maana unafahamu mambo mengi sana, kwa hiyo nitachukulia na mimi unanifahamu. Inawezekana hadi unajua mlango wa nyumba yangu una rangi gani," Kapteni akasema.

"Nyeupe," Lexi akajibu.

"Ahahahah... wewe una... unajua kila kitu eti? Ni mfano halisi wa mfano wa Mungu au siyo?" Kapteni Erasto akauliza.

Lexi akakaa kimya.

"Tusijizungushe sana. Nafikiri unajua jinsi hii inavyokwenda. Nataka uniambie kila kitu kuhusu operesheni zenu, na baada ya hapo, labda hata tunaweza kulegeza kifungo utakachopewa. Unaonaje binti?" Kapteni akasema.

Lexi akabaki tu kimya, akimwangalia kama vile hajaelewa chochote kilichosemwa.

"Ngoja nikuulize kitu. Unampenda Raisi wetu?" Kapteni akauliza.

Lexi akabaki kimya tu.

"Mm? Unampenda? Humpendi? Kwa nini haumpendi?"

Kimya.

"Wewe na wenzako kuiba mabilioni ya pesa inaonyesha hamna upendo wowote kwa hii nchi, na kwa Raisi wetu. Lakini watu wote wanampenda Raisi. He's great! Nyie mna shida gani? Eeh? Kama usipompenda Raisi, utampenda nani sasa?"

"Masanja Mkandamizaji anatosha," Lexi akajibu.

"Ahahahah... kwa nini unampenda Masanja Mkandamizaji?"

"Kwa sababu mama yangu alimpenda, baba yangu alimpenda... na dada yangu alimpenda," Lexi akasema kwa hisia.

"Hiyo ndiyo sababu? Kwa hiyo kama mama yako angekuwa mpumbavu, baba yako angekuwa mshenzi, na dada yako angekuwa mjinga, wewe ingekuwa vipi?" Kapteni Erasto akauliza kwa dharau.

"Basi ndiyo ningempenda Raisi," Lexi akajibu kwa uhakika.

Kanali Oswald, akiwa kwenye upande wa pili wa chumba hiki, hakuweza kujizuia kutabasamu kidogo kutokana na jinsi Lexi alivyoonyesha ujasiri mwingi. Nora alikuwa akisikiliza huku wasiwasi mwingi ukimvaa kwa sababu alijua mambo haya yote yangeishia wapi.

"Okay. Siyo wote wanaompenda Raisi, lakini siyo lazima kumpenda mtu ili kuthamini mambo aliyokufanyia. Na Raisi wetu amefanya mambo mengi kwa ajili ya nchi hii. Wewe na wenzako mmeweza kuiba moja kati ya mambo ambayo yangesaidia kupanua mafanikio hata zaidi..."

"Na ufisadi pamoja na umwagaji wa damu kwa kwenda mbele..." Lexi akamkatisha.

"Una uhakika gani na hayo unayosema? Mm?"

Lexi akatazama pembeni.

"Hauvunjiki kirahisi eti? Mtu unaonekana kuwa mwenye akili timamu... eti unaenda kuiba mia mbili benki na wahuni wenzako wa majalalani! Akili yako ina akili? Naelewa kwamba baba yako alichomwa moto kama muhindi, lakini hayo siyo makosa yetu...."

Lexi akakaza ngumi kwa kuhisi hasira sana.

"Halafu nasikia eti umepigana hadi na Luteni... ahahahah... haki ya Mungu. Ngoja nikwambie kitu. Kuna kipindi fulani, watu fulani, walifikiri kwamba wanaweza kubadili mambo fulani kwa sababu tu wana vifaa fulani mikononi mwao. Matumaini ya kwamba... wangekuwa huru, au wangepata vyeo vikubwa, ama mshahara mnono zaidi, yakawafanya watumie vifaa hivyo kuanzisha uasi. Walifanikiwa kwa kiasi fulani, lakini hawakujua ni nini maana ya ushindi. Ushindi... ulikuwa ni dhidi yao. Nafikiri unajua naongelea nini, hasa kama utakuwa ulisoma historia ya nchi. Watu kama hao, ndiyo kama nyie. Mnafikiri kwamba kwa sababu mmeweza kunyakua na kukimbia umbali fulani, basi mtaweza kujificha. Uko mbele yangu sasa kuthibitisha kwamba hilo haliwezekani hata kidogo. Ahahahah... unahisije? Bado unajiona kuwa mshindi?" Kapteni Erasto akaongea kwa njia yenye dharau.

Lexi akatabasamu kidogo, kisha akasema, "Nilifikiri ulisema hautajizungusha sana... lakini una mdomo mrefu malaya tupa kule."

"Wisecracking, hilo nalifahamu kukuhusu. Nataka uniambie... Kendrick Jabari yuko wapi, na operesheni zake zote ziko maeneo yapi?"

"Unanionaje, me ni GPS?" Lexi akauliza kikejeli pia.

"Binti ni bora useme wakati ninakuomba kistaarabu, la sivyo... aagh unajua kitakachotokea. Sema tu haujui ni jinsi gani kitakavyotokea. SEMA!" Kapteni Erasto akafoka.

Lexi akawa anamtazama tu bila wasiwasi.

"Nikinyanyuka kutoka hapa, nikaenda nje, jua kwamba hiyo ndiyo tiketi yako ya mwisho ya maongezi ya kistaarabu. Kitakachofuata... ni bora uongee sasa hivi. Itaku-save maumivu mengi. Najaribu kukusaidia kwa kuwa una akili, lakini unapaswa tu kuitumia vizuri. Kwa mara ya mwisho, niambie Kendrick Jabari yuko wapi... na operesheni zake zote zilizobaki ziko wapi?" akauliza tena.

Lexi akawa ameangalia upande wa kioo kile. Ni kama alikuwa akimwangalia mtu pale, na ijapokuwa hakuweza kuona yeyote, upande wa pili Nora aliweza kumwona vizuri sana, na ilikuwa ni kama wanatazamana kwa hisia mno. Baada ya Kapteni Erasto kuona Lexi havunjiki kiurahisi, akatikisa kichwa taratibu, kisha akanyanyuka na kuondoka hapo. Alirudi upande wa pili wa chumba hicho na kusema kilichobaki tu hapo ni kumpatia mateso makali sana mpaka aseme ukweli wote; na si vinginevyo.

Kanali Oswald Deule akawaambia watatu hawa wa Jeshi la Polisi, yaani IGP Donald, CP Patrick, na ACP Nora, kwamba sasa kwa kuwa walimshika Lexi, mambo ambayo yangefuata katika kushughulika naye ingekuwa ni masuala ya kijeshi, kwa hiyo kwa kuwa kila kitu kingekuwa chini ya mikono yao basi walipaswa tu kuondoka na kumwacha hapo ili washughulike naye wenyewe. IGP Donald Ngassa na CP Patrick Msuwa hawakuwa na neno, lakini bado ACP Nora alitaka kujua ni aina gani ya mateso waliyotaka kumpa, na kwa nini walisisitizia sana jambo hilo.

Kwa njia yenye kejeli, Kanali Oswald akamwambia Nora kwamba hiyo ndiyo njia ya baba yake ya kufanya mambo kama alikuwa hajui, kwa hiyo alipaswa kuacha kuuliza-uliza maswali na kufata kile alichoambiwa. Kihalisi, Kanali Oswald alikuwa na nia nyingine, na hili ni jambo ambalo Nora aliweza kuhisi. Wakuu hawa wa jeshi wakawaambia wakuu hawa wa polisi waondoke sasa, nao wakatii na kutoka ndani ya chumba hicho, wakiwaacha wawili humo. Luteni Michael hakuwepo ndani ya chumba hicho wakati huo.

Baada ya watatu hao kuwa wametoka ndani ya chumba hicho, Nora akasema alihitaji kuelekea choo kwa ajili ya haja, hivyo wenyewe watangulie tu naye angewakuta huko nje ya jengo. IGP Donald na CP Patrick wakatangulia, huku Nora akijifanya kuelekea upande mwingine, lakini alipoona wameishia, akarudi tena usawa wa chumba kile walichotoka na kusimama karibu hapo. Akaanza kusikiliza maongezi ya Kanali Oswald na Kapteni Erasto ndani humo huku akijifanya amesimama tu hapo akisubiria mtu fulani.

"Lakini bado hawajaipata, kwa hiyo nafikiri kumuua itakuwa kazi bure tu..." Kapteni Erasto akasikika.

"Na hata sidhani kama kumtesa itasaidia maana huyu binti ni mtata sana, anaweza kuwa tayari kufa kwa ajili ya Jabari lakini siyo kum-snitch," akasema Kanali Oswald.

"Kwa nini unasema hivyo?"

"Fikiria alikuwa tayari kujitoa ili Jabari akimbie. Anajiamini sana..."

"Kanali... kuna aina za mateso ambazo ni lazima akizipitia atasema tu kila kitu..."

"Mambo siyo rahisi kama unavyofikiria. General alikuwa anamtaka sana aliposikia tu jina lake kwa mara ya kwanza na kuagiza atafutwe upesi na kupelekwa kwake; mzima au akiwa amekufa. Hiyo inakwambia nini? Siyo Jabari tu ndiyo dili kubwa hapa, ni huyu msichana. Kuna mambo mengi anayojua ambayo General anataka kuhakikisha hayafiki mbali. Huyu na kundi lao wamefanya mengi kumzingua Raisi na General. Kwa nini? Kila jambo linafanya nitake sana kuelewa mambo yote yaliyofichwa... lakini kuna vizuizi vingi sana," Kanali Oswald akasema.

"Sasa... kama ni hivyo, kwa nini umewaambia wengine kuwa atapitia mateso mpaka aseme ukweli ikiwa hiyo siyo...."

"Nimewaambia walichohitaji kusikia. Unapaswa ufikirie mbali Erasto. Fikiria kwa kina ni nini tutapata tukimpeleka huyu malaya akiwa hai kwa General. Nafikiri anamhitaji zaidi akiwa hai kuliko akiwa amekufa, ili labda afurahie zaidi kumuua yeye mwenyewe. Nataka sisi ndiyo tuwe wa kwanza kumpeleka, na ninajua tunaweza kupata faida kubwa sana," akasema Kanali Oswald.

"Oooh... okay... sasa ninaelewa. Kuna siri imejificha hapa kati, na huyu demu anaijua. Ikiwa tuta... tutampeleka kwa General akiwa hai na kusema atuingize kwenye mipango yao, basi na sisi tutafurahia mambo mengi kama Weisiko tu sivyo?" Kapteni Erasto akauliza.

"Angalau umenipata! Hahahah..." Kanali Oswald akasema.

"Kwa hiyo tunamtoa hapa muda siyo mrefu?" Kapteni Erasto akauliza.

"Ndiyo. Nimeshafanya mipango. Anapelekwa sehemu nyingine kwanza," Kanali Oswald akaongea.

Nora, bado akiwa nje mlangoni hapo, alisikia vizuri sana yale waliyosema. Sasa mambo mengi hata zaidi yaliendelea kumchanganya.

"Nora, vipi?"

Akashtushwa na sauti ya Luteni Michael akiuliza hivyo, ambaye alikuwa amefika hapo bila yeye kutarajia na kumfanya ajiulize ikiwa alitambua kwamba alikuwa anasikiliza maongezi ya viongozi wale. Kanali Oswald na Kapteni Erasto nao pia wakawa wamemsikia Michael kutokea mlangoni kule, naye Erasto akaanza kwenda kuona nini kilikuwa kinaendelea.



★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Mkuu shukran sana mambo yanazidi kuoamba moto[emoji4][emoji4][emoji4]
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA THELATHINI NA TISA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


"Aam... Michael... nilifikiri umeondoka?" Nora akauliza kwa sauti ya chini.

"Hapana kuna masuala..."

"ACP Nora, unafanya nini hapa? Si tumewaambia mwende?" Kapteni Erasto akamkatisha Michael baada ya kutoka.

"Samahani, nilihitaji kuonana na nyie tena. Ninaomba mnikubalie ombi langu," Nora akamwambia Kapteni.

"Ombi gani?" Kapteni Erasto akauliza.

"Najua mambo mengi hayajakaa sawa, lakini ninaomba mwelewe kuwa kwa kipindi fulani nilimjali sana mwanamke huyu. Roho inaniuma sana kwa kitendo chake cha kunisaliti... na kusababisha nihisi kama mimi ndiyo nimewasaliti nyie wote. Ijapokuwa najua hastahili wema wowote kutoka kwetu, ninaomba angalau nimpatie chakula..." Nora akamwambia.

Luteni Michael na Kapteni Erasto wakatazamana kwa ufupi, kisha wakamwangalia tena Nora.

"Ninajua huenda hii ndiyo ikawa mara ya mwisho nitamwona. Kulikuwa na maswali mengi sana niliyotaka kumuuliza, lakini hakujawa muda wala nafasi ya kutosha. Naelewa mimi ni mpumbavu. Na ndiyo upumbavu wangu ambao unanifanya niendelee kumjali ijapokuwa ameniumiza sana. Tafadhali naomba kwa hili unikubalie Kapteni," akasema Nora kwa hisia.

"Kumpa chakula? Sasa hivi? Unajua hastahili hata kupewa maji kwa matatizo yote waliyo..."

"Erasto..."

Kapteni Erasto akakatishwa na Kanali Oswald, aliyekuja nyuma yake na kumshika begani. Erasto akasogea pembeni kidogo kumpisha.

"Haina haja ya kumbania sana. Kama anataka kumpa chakula, mwache ampe chakula," Kanali Oswald akasema.

Nora akatazama chini kwa huzuni. Luteni Michael alikuwa anamwangalia kwa huruma sana.

"Kila mtu hukosea. Nilifikiri ungemchukia kwa alichofanya lakini bado inaonyesha unampenda sana, au nimekosea?" Kanali Oswald akamuuliza Nora.

Nora akabaki tu kimya. Luteni Michael aliweza kuiona njia ya kuongea ya Kanali Oswald ikiwa imejaa kejeli nyingi, lakini kwa mambo haya hangeweza kumtetea Nora hata kidogo.

"Unataka kumpelekea wewe mwenyewe siyo? Unataka sana kumwona?" Kanali Oswald akamuuliza Nora.

Nora akamtazama na kutikisa kichwa chake kukubali. Kanali Oswald naye pia akatikisa kichwa chake.

"Okay. Waweza kumpatia chakula. Kuna sehemu hapa ambayo..."

"Ndiyo, naifahamu. Nitamfatia mimi mwenyewe. Asante sana Kanali," Nora akamwambia huku machozi yakimlenga.

Wanaume wote watatu walimwonea huruma kwa kiasi fulani, naye akaondoka kuelekea sehemu ambayo walitengeneza vyakula mbalimbali ndani ya jengo hilo kwa ajili ya watu wa hapo.

"Sasa hivi saa 7, halafu anawaza kumpa chakula? Wanawake ni wanawake tu," Kapteni Erasto akasema.

Kanali Oswald akatabasamu.

"Luteni, gari la kumsafirisha liko tayari?" Erasto akamuuliza Luteni Michael.

"Ndiyo mkuu. Aam... nilitakiwa kuongoza msafara huu lakini nimepata taarifa kwamba haitakuwa hivyo. Hiyo ni kwa nini?" Luteni Michael akauliza.

"Kuna mipango imebadilishwa. Usijali. Atafikishwa salama," Kanali Oswald akasema.

"Lakini Kanali..."

"Luteni... hii ni amri. Wewe unatakiwa tu kutii. Umefanya kazi nzuri sana kumkamata. Kuanzia hapa sasa mambo yote yanayomhusu tutadili nayo sisi, imeeleweka?" Kapteni Erasto akamwambia.

Luteni Michael hakuelewa kikamili yaliyokuwa yanaendelea lakini akakisia kuna jambo lilifichika. Ijapokuwa hivyo, akatikisa kichwa chake kukubali, kisha akapiga saluti na kuondoka sehemu hiyo.



Baada ya muda mfupi, Nora akawa amerejea na chakula kwa ajili ya Lexi; wali na nyama iliyotengenezwa vizuri sana. Kapteni Erasto akakikagua chakula hicho kuhakikisha hakukuwa na nuksi yoyote ambayo huenda Nora angekuwa ameificha. Kanali Oswald alikuwa anamwambia Kapteni aache kuwa mkaguzi sana maana Nora alihitaji kuonyeshwa kwamba anaaminika ijapokuwa alikuwa amekosea. Baada ya kutoona lolote kwenye chakula hicho, Kapteni Erasto akakitoa kijiko na kumwambia Nora kwamba Lexi angekula chakula hicho kwa mikono.

Mwanamke hakuwa na tatizo na hilo, naye akawashukuru kwa mara nyingine na kuingia upande wa chumba alichokuwemo Lexi. Alipoingia, Lexi alikuwa ameinamisha tu kichwa chake chini, ila baada ya kumwona Nora akanyanyua shingo na kumwangalia machoni kwa hisia sana. Nora alikuwa anamtazama kwa hisia pia huku akiwa ameshikilia chakula hicho na maji mikononi, kisha akasogea mezani hapo na kuviweka mbele yake. Lexi akawa anamwangalia tu machoni, naye Nora akaendelea kusimama hapo akimtazama kwa umakini.

"Mwanzoni nilikuwa nataka kujua sababu ya haya yote uliyofanya, nikitumaini labda ulikuwa... unalazimishwa kuyafanya. Lakini kumbe uliyafanya kwa kudhamiria. Nikuulize... kila kitu ulichoniambia toka tumekutana, kilikuwa ni uwongo, si ndiyo? You just made everything up so... ili unitumie kutimiza haja zako... si ndiyo?" Nora akamwambia kwa hisia.

"Nora... najua nimekuumiza sana, lakini..."

Kabla Lexi hajamaliza kuongea, Nora akamwasha kofi zito la usoni! Kutokea upande wa pili wa chumba hicho, Kanali na Kapteni waliangaliana na kutikisa vichwa vyao huku wanatabasamu kwa njia ya kufurahishwa na jambo hili. Lexi akawa ameinamisha tu uso wake baada ya kutandikwa kofi hilo, naye Nora akawa anapumua kwa hasira.

"Hauwezi kujua ni jinsi gani umeniumiza. Ulinidanganya! Siamini ningeweza kuwa mpumbavu kiasi hicho, lakini umehakikisha hilo limefanikiwa..." Nora akamwambia kwa hisia sana.

Lexi akanyanyua uso na kumtazama kwa huzuni.

"Unajua kinachoumiza hata zaidi? Ni kwamba ijapokuwa umenifanyia mambo yote hayo... bado kuna sehemu fulani ndani yangu inataka yasiwe kweli. Bado ninataka kukusikia ukisema kwamba hauna hatia... kwa sababu sitaki iwe kweli... kwa sababu... kwa sababu bado...."

Nora akashindwa kuendelea na kuanza kudondosha machozi. Lexi naye akadondosha chozi akijisikia vibaya sana kuona jinsi Nora alivyoumia. Nora akajikaza na kufuta machozi, kisha akaketi kwenye kiti cha pili. Akawa anamwangalia kwa hisia kali sana.

"Nitastahili kila jambo baya ambalo litanipata kwa sababu ya upumbavu wangu, kama itakavyokuwa kwako. Nitakuwa tayari kupokea adhabu zozote za makosa yangu, kwa sababu hiki ndiyo nilichoamua sasa. Kama hii itakuwa ni mara ya mwisho kukuona... na mimi nataka nikupe adhabu... adhabu ambayo bado inaonyesha ni jinsi gani ulivyoupeleka mbali sana upumbavu wangu... kula," Nora akamwambia kwa hisia.

"Nora..."

"Kula. Nataka kukuona unakula. Sijui utakuwa chini ya hali gani baada ya hapa, lakini nataka kukuona unakula chakula kabla ya hayo yote. Hiyo ndiyo adhabu yangu kwako. Kula Lexi..." Nora akasema.

Lexi alibaki kumtazama sana kwa hisia nyingi za huzuni. Alielewa kwamba Nora aliumizwa sana na vitendo vyake alivyoviona kuwa ni usaliti, lakini bado mwanamke huyo alimwonyesha ni jinsi gani alimjali licha ya hayo yote, na hii ilimfanya Lexi aumie sana moyoni mwake. Kama tu Nora alivyosema, hii ingekuwa ni adhabu kwake kwa sababu yeye alimtendea kwa njia mbaya, lakini mwanamke huyu akamtendea kwa njia nzuri. Hivyo aliona Nora alikuwa akijaribu kumfanya ahisi hatia sana.

"Dah, yaani mambo ya wanawake bwana!" Kapteni Erasto akamwambia Kanali Oswald upande wa pili wa chumba hicho.

"Eti Nora... mtoto wa General anampenda mwanamke mwenzake. Hahahah... bado naiona hii kuwa ngumu kumeza," akasema Kanali Oswald.

"Kumpenda... kumpenda kiaje yaani?" Kapteni Erasto akauliza.

"Fungua macho yako Erasto. Huyu mwanamke anampenda huyo malaya kama wewe unavyompenda malaya wako. Kila kitu anachofanya... bado anampenda mno. Huyo ndiyo sababu iliyofanya Luteni Michael akatemwa. Ahahah... vijana wa siku hizi ni maumivu sana... yaani hata akiamua kupenda mnyama atapenda tu," Kanali Oswald akasema.

"Duh! Kweli inashangaza. Lakini haina shida tena, maana baba yake atamsaidia kumsahau muda si mrefu," akasema Kapteni Erasto.

"Shhh... punguza sauti, mtoto wa mfalme akisikia!" Kanali Oswald akatania, na wawili hawa wakacheka sana.

Lexi bado alikuwa anamwangalia tu Nora machoni, naye Nora akanyanyuka na kufungua maji, kisha akamnawisha mikono yake iliyokuwa imefungwa kwa pingu. Kwa ukaribu huu Lexi alimwangalia sana Nora akijihisi vibaya moyoni, lakini Nora alikuwa anafanya mambo haya kwa njia ambayo ilimzidishia huzuni hata zaidi Lexi. Kisha Nora akasogeza chakula kile karibu na kurudi kukaa tena.

"Kula tafadhali. Ikiwa umebakiza aina yoyote ya hisia ndani yako... nakuomba ule," Nora akamwambia.

Lexi akaangalia pembeni kidogo na kufumba macho yake, kisha akajisawazisha na kukisogelea chakula vizuri. Akaanza kula tu bila kumwangalia usoni Nora, na kadiri alivyoendelea kula ndivyo alivyojihisi vibaya sana moyoni mwake. Nora aliweza kuona machozi kwenye macho ya Lexi, naye kiukweli aliumia sana moyoni mwake kwa sababu ya mambo yote aliyokuwa amemwambia, lakini hakuwa na uwezo wa kujizuia wala njia nyingine ya kufanya jambo hili.

Lexi akaendelea kula tu taratibu huku Nora akimwangalia, na baada ya kuingiza nyama nyingine mdomoni, akatulia kidogo, kisha taratibu akamtazama Nora machoni mwake. Waliangaliana kwa ufupi, naye Lexi akaangalia chini tena na kuendelea kutafuna taratibu. Nora akanyanyuka na kuuelekea mlango, na baada ya kuufungua ili atoke, akageuka kwa mara nyingine na kumtazama tena Lexi, ambaye alikuwa anamwangalia kwa umakini sana. Nora akatikisa kichwa kwa njia ya kusikitika, kisha akatoka humo. Lexi hakuendelea tena kula na kukaa tu akimtafakari mwanamke huyo.

ACP Nora akaenda kwa Kanali na Kapteni kuwashukuru kwa kumruhusu amwone mwanamke huyo, naye akaondoka jengoni hapo hatimaye. Mipango ya kumtoa Lexi hapo ikaanza haraka sana, wanajeshi kadhaa wakiitwa mpaka kwenye chumba kile ili wamwongoze mpaka kwenye gari ambalo lingempeleka kule ambako Kanali Oswald alidhamiria apelekwe.

Akiwa amefungwa kwa pingu mikononi, Lexi alionekana kuwa mnyonge sana kwa kuwa alitulia mno mpaka wanamwingiza kwenye gari la kijeshi. Aliketi katikati ya wanajeshi wawili, na wawili wengine upande uliotazamana naye. Mbele ya gari kulikuwa na wanajeshi wawili, hivyo kulikuwa na wanajeshi sita ndani ya gari hilo wenye silaha. Aliyeendesha gari hili ni mwanajeshi ambaye alifahamiana sana na Kanali Oswald kwenye masuala yao yaliyoendeshwa kwa siri, hivyo alijua alipopaswa kumpeleka Lexi ilikuwa ni sehemu kwa ajili ya Jenerali Jacob Rweyemamu.

Gari liliondoka muda mfupi tu baada ya Lexi kuingizwa humo, ikiwa ni mida ya saa 8 usiku.


★★★★


Kwa kutumia njia nyingi za mkato kutokana na ujuzi wake wa maeneo, Torres alifanikiwa kuwatoa Mess Makers jijini na kuwapeleka mpaka kule kwenye nyumba yao ya maficho. Kiukweli walikuwa wametumia masaa machache isivyo kawaida, na sasa angalau wakawa wamefanikiwa kufika kwenye sehemu yao hiyo salama.

Hali baina yao wote haikuwa nzuri hata kidogo. LaKeisha alikuwa akilia kwa chini chini, na wanaume walikuwa kimya tu. Azra naye alishikwa na hofu kwa kadiri fulani kwa kuwaza ni nini ambacho kingekuwa kimempata Lexi, kwa kuwa alikuwa ameanza kumwingia sana kihisia. Baada ya kuwa wamefika ndani, Kevin aliwapokea na kuona jinsi walivyokuwa wameghafilika sana. Akawa anawauliza ni nini kilikuwa kimetokea, akijifanya kama haelewi somo.

"Torres, that was the stupidest thing you could have done! You shouldn't have left her! (ulichokifanya kilikuwa ni ujinga wa hali ya juu.. usingemwacha!)" LaKeisha akamwambia Torres.

Torres akaketi tu na kuinamisha kichwa kimasikitiko.

"Nini kimetokea jamani?" Kevin akauliza.

"Wametujua. Tumejulikana kote yaani," Victor akasema.

"Nini? Kivipi?" Kevin akauliza.

"Boss, we have to go and get her. If they capture her, they'll kill her (..tunapaswa kumfata.. wakimkamata watamuua)," LaKeisha akamwambia Kendrick.

"Subiri. Unataka kusema kwamba Lexi amekamatwa? Lexi amekamatwa?!" Kevin akajifanya kushangaa.

"Boss..." LaKeisha akamsemesha Kendrick.

"Haitakuwa rahisi Keisha," Kendrick akajibu kwa upole.

"So what, tunapaswa kumwacha tu?" LaKeisha akauliza kwa hisia.

"Boss, kila mara mmoja kati yetu alipokuwa kwenye shida, Lexi angetuongoza kufanya kila tulichoweza ili kutoa msaada. Sasa hivi yeye yuko kwenye shida, ni lazima tumsaidie," akasema Victor.

"Ndiyo. Ni lazima tumfate," akasema LaKeisha.

"Wamemkamata vipi Lexi?" Kevin akauliza.

"Walikuja tu ghafla tulipokuwa. Lexi alijua kwamba kundi lao lililokuwa linakuja pale ni kubwa zaidi. Alikuwa anajaribu kuwapotezea muda ili sisi tutoroke. Alikuwa anatulinda... hasa mdogo wake. Kama tu tungekuwa tumejiandaa mapema..." Victor akaongea.

"How the f(...) did they know? Just how? (walijuaje? walijua kivipi?)" Mensah akauliza.

Torres akafikicha viganja vyake na kunyanyuka, na bila kusema lolote akaanza kuelekea kule chini kwenye mitambo yake. Wengine wakaanza kuangaliana, kisha nao wakaelekea huko kwenda kuona alitaka kufanya nini. Kevin akajikaza na kuwafata pia huku akiombea Torres asitambue kile alichofanya. Baada ya Torres kufika kwenye mitambo yake, akaanza kuangalia mambo ya hapa na pale ili kujua ni jinsi gani taarifa zile kuhusu wao zilivyofika mpaka kwenye mifumo ya nje na mitandao ya kijamii. Akatoa macho kimshangao baada ya kutambua kwamba ni mitambo yake ndiyo iliyotuma taarifa hizo, lakini hakuwa na kumbukumbu zozote za kufanya jambo kama hilo.

"Torre, what is it, what did you find? (vipi, umepata nini?)" LaKeisha akamuuliza.

Torres akainamisha uso wake, kisha akapiga ngumi kwenye meza ya hapo akionyesha hasira, naye akatoka kwa kasi na kumfata Kevin, kisha akamshika kwenye nguo yake na kumsukumia mpaka sehemu ya kuta (huko huko chini). Wengine wakashangaa na kujiuliza nini kilikuwa kinaendelea.

"What did you do? (umefanya nini?)" Torres akamuuliza kimkazo.

"Torres vipi? Mbona sikuelewi mwanangu?" Kevin akauliza.

"Torres?" Kendrick akaita.

"That info about us... hizo taarifa zote kutuhusu zimetokea huku. Kwenye kompyuta zangu," Torres akasema huku akiwa bado amemshikilia Kevin.

Wengine wakashangaa.

"Nini?" Victor akauliza.

"Ulifanya nini Kevin? Uliwasha kompyuta zangu?" Torres akauliza.

"Bro, mimi sijui unachokisema. Ulishaweka wazi kwamba hatupaswi kugusa madude yako, nifanye hivyo ili iweje?" Kevin akajitetea.

"Nitakuua Kevin! Sitaki masihara. Hizo taarifa hazingeweza kutoka zenyewe tu, na ni wewe ndiyo ulikuwa umebaki hapa. Niambie ukweli!" Torres akaongea kwa ukali.

Kevin akaitoa mikono ya Torres kwenye nguo yake kwa nguvu.

"Sijagusa kompyuta zako! Nyie watu mna nini? Sawa kuna mambo mengi hamyapendi kutoka kwangu lakini ndiyo mnilaumu tu kwa kila jambo baya? Mimi tokea lini nikajua kutumia makompyuta? Tena hayo madude yako magumu? Niwafichue nyie kwa faida gani wakati na mimi niko hapa?" Kevin akaongea kwa ukali.

"Imewezekana vipi hizo taarifa kutoka kwako Torres?" Kendrick akauliza.

"Sijui boss. Na zimekwenda ndani ya muda mfupi tu tulipoondoka kutoka huku. Nilihakikisha kila kitu kiko secure, hivyo ni lazima kuwe na mtu aliyekorofisha. Na ni huyu ndiye aliyekuwepo hapa," Torres akasema kwa hasira.

"Sikia Torres. Sasa hivi Lexi amekamatwa... tunapaswa kuwa na umoja, halafu wewe unaona ni bora kunipa lawama tu, itasaidia nini? Ni makompyuta yako, ulipaswa kuyaweka vizuri ili yasiharibu mambo, ona sasa! Na hapa tena ni makosa ya Kevin, eh Mensah? Boss, najua mimi sina kiwango kama cha wengine cha kutoa faida hapa, lakini mimi siyo snitch. Kama mnaona itawapa faida kunilaumu kwa hili, basi nifanyeni mnachotaka. Mimi ni mjenzi, toka lini nikajua haya mamitambo yenu... aah aisee!" Kevin akajifanya kama mtu aliyeonewa sana.

Wengine walikuwa wanamwangalia kwa mashaka, na Torres akawa anamtazama kwa hasira.

"Na nyie wote kabisa mmegundulika?" Kevin akauliza.

"Ni sisi wote... kutoa LaKeisha na Torres," Victor akasema.

"Sisi wote, hadi mimi, na Oscar? Lakini me tayari si walikuwa wananijua, mmeona sasa? Kama ni kompyuta zako basi tuseme zinakujua wewe tu, na mpenzi wako, zikawabagua nyie, halafu sisi wengine woote ndiyo zikaona zitubwage chini. Singeweza kukufanyia hivi boss hata kama ningekuwa nimesomea hayo madude kama huyu jamaa. Umenisaidia sana. Torres... najua huu siyo muda mzuri kukwambia hivi, lakini hata wewe unajua kwamba haya ni makosa yako. Haukuwa tu mwangalifu, kwa hiyo acha kunilaumu mimi, na uanze kufikiria ni nini tunafanya. Labda hata hao jamaa wako njiani wanakuja hapa sasa hivi," Kevin akasema.

Mwanaume huyo alikuwa anajifanya kuonyesha busara kubwa sana, lakini unafiki aliokuwa nao ulikuwa mbaya kupita maelezo.

"Torres..." Kendrick akaita.

Torres akamgeukia.

"Location yetu wameijua?" Kendrick akauliza.

"Hapana. Bado tuko secure. Lakini wameshaanza kuweka kila aina ya mtego kimtandao na kufatilia bio zenu ili kupata vigezo vitakavyowasaidia kuwakamata," Torres akaongea, lakini kwa huzuni.

"Basi tunatakiwa tufanye mchakato wa haraka kuwazuia zaidi ili wasitufikie. Si utaweza kufanya hayo?" Kendrick akamuuliza.

"Ndiyo," Torres akajibu.

Kendrick akamgeukia Azra, aliyekuwa amesimama pembeni. Akawaangalia na vijana wake, ambao walionekana kupoteza matumaini kwa kadiri fulani. Akaanza kusema, "Kwa sababu wamejua kuhusu mimi, sasa itakuwa ngumu kuukamilisha mpango wetu. Tutapaswa kuuweka pembeni kwanza, na priority namba moja kutokea now ni kujua Lexi yuko wapi, na kufanya kila tuwezalo kumsaidia. Hata ikihitajika, LaKeisha...."

"Yeah..." LaKeisha akaitika.

"...utapaswa kumtoa Zelda," Kendrick akasema.

"Okay. Ikihitajika," LaKeisha akapigia mstari.

Kendrick akageuka na kuanza kuondoka, na alipomkaribia Azra, akamshika begani, kisha akampita na kutoka.

Torres alimwangalia Kevin kwa hisia kali sana, akiwa bado anahisi ni yeye ndiye ambaye alisababisha haya yote, naye Kevin akatazama tu chini. LaKeisha akajaribu kumshika Torres ili waondoke kwenda kupumzika, lakini Torres akautoa mkono wake kwake na kwenda kwenye kompyuta zake ili apige kazi; jamaa hakuwa na muda wa kupumzika. LaKeisha akamwonea huruma sana, naye akaamua tu kwenda na kukaa pembeni yake. Victor na Mensah wakaondoka sehemu hiyo na kwenda vyumbani kwao, wakimwacha Azra anamwangalia sana Kevin.

Mwanaume huyo akamsogelea karibu Azra na kumwambia asihofu, wangempata tu dada yake, kisha naye akampita na kuondoka. Alipofika upande wa juu, Kevin akashusha pumzi ndefu ya ahueni, naye akaachia tabasamu la kiburi kwa kuweza kuitoroka hali hiyo ambayo ingempa shida haswa. Ingawa siyo wote waliokamatwa, akahisi amefanikiwa sana kwa sababu Lexi kukamatwa ilikuwa pigo kubwa kwa wengine, na hivyo akaridhika na hilo. Kwa hiyo kuanzia hapo angeendelea kujiweka upande wao, ili aendelee kutafuta njia zingine za kuwaharibu hata zaidi.


★★★★


Baada ya mwendo wa zaidi ya nusu saa, Lexi bado alikuwa katikati ya ulinzi wa wanajeshi wanne wenye silaha na wenye kuongea mambo mengi yenye kuchukiza kuhusu mwonekano wake. Wawili walioketi pembeni yake walimfanyia dhihaka kuhusu urembo alionao, na hata mara kwa mara kumshika-shika mwilini kwa njia zenye kuamsha hisia za kimahaba. Walikuwa wakifurahia sana uonevu huo, lakini aliyeendesha aliwakanya kuwa hawakupaswa kuvuka mipaka yao, la sivyo wangepata shida kutoka kwa wakuu wao.

Lexi alihisi hasira sana, lakini bado aliendelea kuwa mtulivu. Alikuwa akisubiria wakati mwafaka wa jambo fulani, na sasa akaona muda huo ulikuwa umefika. Wakiwa bado mwendoni, akaanza kukohoa sana, naye akajiziba mdomo kwa mikono yake na kuendelea kukohoa. Wanajeshi wa pembeni walikuwa wanamtania kwa kusema aache "kubanja" kwa kuwa haimfai mwanamke, lakini yeye Lexi alikuwa akijikoholesha namna hiyo na kuisogeza mikono yake karibu na mdomo ili atemee pini ndogo kutoka mdomoni mwake bila wanajeshi kutambua hilo.

Baada ya kujisawazisha kutokana na kukohoa huko, akaketi vizuri tena kwa utulivu, huku akitumia pini hiyo ndogo kufungua pingu kisiri. Alikuwa akitumia akili sana kuweza kuiingiza pini hiyo ndani ya tundu la funguo na kuchokonoa kimya kimya, na baada ya jitihada za dakika kadhaa, akahisi kifungo cha pingu kimeachia. Bado akaendelea kujifanya kama pingu zilikuwa zimeikaza mikono yake, hivyo kwa umakini, akaanza kuwaangalia wanajeshi hawa walioketi naye na kuunda mpango wa haraka sana kichwani kwake ili aweze kuwachengua wote na kutoroka upesi.

Alipoona wote wakiwa wamezubaa, kwa kasi sana akashika chuma ya juu ya sehemu hiyo ya gari kwa mikono yake na kuinyanyua miguu, kisha akaisukuma mbele kwa nguvu sana na kukanyaga nyuso za wanajeshi wale wawili waliotazamana naye. Viatu vyake vigumu viliwatia maumivu sana kwa kuvunja pua zao na kuwapigisha visogo kwa nguvu kwenye gari. Wale walioketi pembeni yake hawakuwa hata na muda wa kushtuka, na papo hapo Lexi akawa ameachia chuma lile la juu na kuwatandika kwa viwiko katikati ya shingo zao na kufanya waanze kukohoa kwa maumivu. Alikuwa amedondokea chini sasa, na kwa ustadi wa hali ya juu akajigeuza na kuanza kuwafumua haraka-haraka sana sehemu nyingi zenye udhaifu.

Wanajeshi wale wawili mbele waliweza kusikia vishindo na sauti za wenzao wakitoa kelele za maumivu kutokea nyuma, hivyo aliyeendesha akaona alisimamishe gari haraka sana. Kufikia wakati ambao gari lilisimama tuli, Lexi alikuwa amekwishavunja shingo za wanajeshi wale wawili waliokuwa wanamshika-shika, huku wawili wengine wakiugulia maumivu kwenye sehemu zao za siri baada ya kuwa amewapiga hapo. Akiwa anajua kabisa kwamba wanajeshi wale wa mbele wangeshuka ili kuja kutoa msaada, akachukua bunduki moja na kufyatua risasi pembezoni mwa gari, hivyo wale waliokuwa nje wakalala chini ili kuepuka kupigwa.

Lexi alitumia akili kufyatua risasi na mlango wa nyuma wa gari hilo, kisha akatoka kwa mtindo wa kujinyanyua kwa mikono mpaka juu ya gari kwa kasi sana na kulala hapo juu. Mwanajeshi mmoja aliyelala chini hapo nje alipoona risasi zimeacha kufyatuliwa, bila kutumia akili na yeye akaanza kufyatua kuelekea sehemu ile ya gari ili zimmalize Lexi humo humo ndani kwa ndani. Lexi akawa anajiviringisha taratibu kuelekea mbele ya gari, na yule mwanajeshi ambaye alikuwa anaendesha gari hilo akamwambia mwenzake kwa sauti ya juu aache kupiga risasi kijinga.

Eneo hili walilokuwa wamefikia lilikuwa ni katikati ya jiji, lakini kwenye upande ambao hakukuwa na shughuli nyingi sana au watu watu wengi; hasa kwa muda huo wa usiku. Lexi akiwa ameendelea kujilaza juu hapo kwa uangalifu, wanajeshi hawa wakaanza kutambaa kuelekea upande wa nyuma wa gari hilo, na yule aliyekuwa analiendesha akatoa ishara kwa mwenzake kuwa anyanyuke ili aangalie kama huyo mwanamke alikuwa amekufa, kwa sababu kihalisi risasi hizo zingekuwa zimewaua na wanajeshi wenzao.

Wakati mwanajeshi huyo akianza kufanya kama alivyoambiwa, Lexi akajitelezesha kupitia kioo cha mbele ya gari na kutua chini kwa ukimya, kisha akachuchumaa hapo kwa sekunde kadhaa akiangalia sehemu nzuri ya kukimbilia, naye akatoka upesi sana. Mwanajeshi yule akaufungua mlango haraka na kuelekeza bunduki yake ndani hapo, kukuta ni wanajeshi wenzake wanne tu ndiyo waliotobolewa-tobolewa na risasi nyingi sana, na damu zikitapakaa ndani hapo. Alishangaa sana kutomwona Lexi, naye akamwangalia yule mwingine wa nje kwa kuchanganyikiwa. Mwanajeshi huyo akasogea hapo na kukuta hali hiyo pia, kisha wote wakaanza kuangalia huku na kule wakimtafuta Lexi.

Mwanajeshi yule aliyekuwa anaendesha gari hilo akafanikiwa kumwona Lexi akiwa anaishia kwenye kona moja pembeni ya eneo hilo, naye akamwonyesha mwenzake na wote wakaanza kumfukuza kwa kasi sana. Mitaa hii ilikuwa na majengo kadhaa kwa umbali mfupi kutokea walipokuwa, hivyo wakamkimbiza Lexi mpaka kufikia sehemu ambayo ilianza kuonekana kuwa yenye kona kona nyingi sana ambazo bila shaka zilitumiwa kwa ajili ya shughuli, lakini hakukuwa na watu sehemu hiyo. Inaonekana kwa watu wachache ambao wangekuwepo, walikimbia baada ya kusikia sauti za milio ya risasi, hivyo kulikuwa na uwazi mkubwa sana.

Kila mara ambayo wanajeshi hawa wawili walimkaribia Lexi, angewapiga chenga na kutokezea sehemu nyingine ya mbali, hivyo waliendelea kwa bidii kumfukuzia bila kukata tamaa. Walikuwa wanaulizana mwanamke huyo aliweza vipi kufungua pingu zake, nao wakatambua kweli walikuwa wamemshusha hadhi kijinga kwa kutomfunga na miguu. Baada ya dakika chache za kujitahidi kumkimbiza, walifika sehemu ambayo ilikuwa na barabara refu lililoelekea upande mmoja bila kuwa na majengo pembeni, hivyo waliweza kumwona akiwa kwa mbali anajitahidi kuufikia upande ambao ulikuwa na jengo ili awaponyoke.

Mwanajeshi mmoja akasimama na kulenga shabaha kwa bunduki yake, kisha akafyatua risasi iliyompata Lexi nyuma ya bega lake la kulia! Aliumia sana. Akaanguka chini na kuviringika mara kadhaa kwa kasi, lakini kwa kustaajabisha akajinyanyua tena upesi na kuendelea kulikimbilia jengo lile dogo ili afanikiwe kujikinga hapo. Hii iliwashangaza wanajeshi kwa kuwa walifikiri walikuwa wamempatia sasa, hivyo wote wakaanza kufyatua risasi kumwelelekea ambazo hazikumpata baada ya yeye kufanikiwa kujibanza kwenye jengo lile la mbali. Wakaacha kupiga risasi na kuendelea kumkimbilia kwa kasi.

Lexi alitulia hapo alipojibanza kwa sekunde chache akihisi maumivu mengi sana sehemu hiyo ya juu ya mgongo wake. Alikaza meno na macho yake kwa nguvu sana, kisha akaanza kujitahidi kukimbia tena. Alikuwa anakimbia huku anajigonga-gonga hapa na pale, na sasa akawa anaingia kwenye kona za majengo tofauti-tofauti ili kuwapoteza wanajeshi wale. Lakini ijapokuwa aliwaacha mbali kiasi, watu hawa walikuwa wakiendelea kumfatilia kwa kuangalia matone ya damu yaliyodondoka chini kutoka kwenye jeraha lake la risasi, hivyo walijua tu bila shaka wangemkamata muda siyo mrefu.

Lexi alianza kupishana na watu wachache hapa na pale ambao walimwangalia kwa kushangaa sana, nao walikuwa wamesikia milio ile ya risasi kutokea kule alipokuwa. Akiwa bado anahisi maumivu mengi na kukosa nguvu ya kutosha kukimbia, akafikiria labda aingie sehemu fulani iliyojificha ili atulie hapo na kuwafanya wanajeshi wale wapitilize, lakini alijua akilini mwake kwamba angekuwa tu akiwatengenezea njia rahisi ya kumkamata. Hakujua aelekee wapi zaidi, lakini alijua kwamba alipaswa kuendelea kukimbia.

Ni wakati akiendelea kukimbia na maumivu yake mengi pale alipopamiana na mtu mwingine njiani na kudondoka. Akaanza kujinyanyua na kujisawazisha ili aendelee kukimbia, lakini mtu huyu akamshika mikononi kama vile anamzuia. Lexi bila kumtazama vizuri akataka kujivuta kwa nguvu, lakini mtu huyu akamsemesha.

"Alexandra!"

Lexi akamtazama usoni na kushangaa kiasi. Sura hiyo aliifahamu vizuri sana. Alikuwa ni mtu ambaye alimjua yeye kama Alexandra kwa sababu ya kuwa ndani ya mwili wa pacha wake, na ulikuwa umepita muda mrefu sana bila kufikiri angewahi kuja kumwona tena. Alikuwa ni mwanaume kijana, na sura yake ikamkumbusha kwamba kijana huyu aliwahi kusoma pamoja naye chuoni.

Alikuwa ni Isiminzile!



★★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★★

Mambo yanaxidi kupamba moto. Karibu WhatsApp kwa episode zilizobaki. Bado ni ndefu.

WHATSAPP +255 787 604 893
 
👏👏👏👏
Mkuu Elton Tonny unatufungua akili na kutuburudisha na kutujenga kisaikolojia ya kuwa katika maisha jambo lolote lisilotarajiwa kwenye maisha linaweza kukupata. nitakutafuta aiseee.
 
Hatare sana, unpredictable…Shukran sana Mkuu [mention]Elton Tonny [/mention] ikikupendeza tuwekee ka episode kamoja ka kutafutia tafakuri kali itakayomhusu Kevin
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI

★★★★★★★★★★★★★★


"S... Simi... Simi...." Lexi akawa anasema.

"Alexandra... njoo... twende... twende huku..." Isiminzile akamwambia.

Akamsaidia Lexi kusimama vizuri, kisha akaanza kuongozana naye kuelekea upande mwingine wa barabara na kuvuka majengo kadhaa mpaka walipofikia usawa wa gari lake aina ya Hilux, ambayo ilikuwa ni pickup nyeusi. Isiminzile akaenda na kufungua mlango wa nyuma wa gari hilo na kumwambia Lexi aingie na kujilaza kwenye siti za nyuma za gari hilo, naye akatii na kuingia haraka.

Isiminzile akaufunga mlango upesi na kuanza kurudi upande ule aliotokea na Lexi. Wakati wakilifuata gari lake, damu zilizodondokea chini zilikuwa zimeishia kwenye jengo la nyuma kidogo kutokea gari lake lilipokuwa, hivyo akaenda na kujisimamisha hapo mpaka wanajeshi walipofika ndani ya sekunde chache. Wakamkuta akiwa amesimama huku akionekana kushangaa, nao kwa ukali wakamshika na kumuuliza kama alimwona mwanamke fulani mweupe akikimbilia upande huo.

"Sema!" mwanajeahi mmoja akafoka huku akipumua kwa kasi.

"Nn..ndiyo nimemwona!" Isiminzile akakubali.

"Ameelekea wapi?" mwingine akamuuliza.

"Amenipita hapa... anavuja damu... si ndiyo huyo?" Isiminzile akauliza.

"Eee... yuko wapi?!"

"Ameelekea huko hivi..."

Isiminzile akadanganya kwa kuwaonyeshea upande tofauti na gari lake lilipokuwa. Bila kuchelewa wanajeshi wale wakaanza kuelekea huko kwa kasi sana. Kwa kiasi fulani, Isiminzile alikuwa akiogopa sana, lakini baada ya wanajeshi wale kuondoka, akarudi upesi kwenye gari lake na kumkuta Lexi akiwa bado amejilaza ndani yake. Akaingia kwenye usukani na kuliwasha, kisha akaanza kuligeuza haraka ili amwahishe kwenye hospitali ya mbali kidogo na eneo hili ili kumwepusha na wanajeshi wale.

Lexi alikuwa akiugulia maumivu ya risasi kwa sauti ya chini, huku akihisi mkono na sehemu kubwa ya mwili wake unakufa ganzi kutokana na kupoteza damu nyingi. Isiminzile aliendesha gari kwa kasi huku akimwangalia "mwanamke" huyu kupitia kioo, mpaka akamfikisha kwenye hospitali moja iliyowachukua kama dakika 7 hivi kuifikia. Akawahi kushuka haraka na kumfata huko nyuma, kisha akamsaidia kutoka ndani ya gari. Lexi alitaka kuweka kipingamizi kuhusu kwenda kule ndani, lakini Isiminzile akasisitiza sana waende kwa sababu alikuwa amepoteza damu nyingi sana.

Wakaelekea pamoja mpaka ndani ya jengo lile, na wauguzi kadhaa wakaja kumsaidia Lexi kuelekea chumba cha matibabu ya dharura. Ilikuwa ni hospitali kubwa ya kibinafsi iliyomilikiwa na wahindi, na baada ya Isiminzile kuulizwa ni nini kilikuwa kimesababisha mpaka mwanamke huyu akapigwa risasi, akasema kwamba alikuwa sehemu mbaya kwa wakati mbaya kwa kuwa maaskari walikuwa wanamkimbiza mwalifu fulani na kujaribu kumpiga risasi lakini kwa tukio baya ikampiga Lexi. Alipoulizwa uhusiano wake na Lexi, Isiminzile akasema alikuwa ni mchumba wake, naye angelipia gharama zake zote zilizohitajika.

Lexi akiwa kwenye chumba kile cha matibabu, alikataa kuchomwa sindano ya usingizi na kusema waitoe risasi akiwa bado macho. Akaomba watumie tu sindano ya ganzi ili kupunguza maumivu yake, lakini akakataa katakata kuchomwa ya usingizi. Daktari akafanya kama alivyoambiwa kwa kuwa aliona mwanamke huyu alikuwa anaelewa kile anachoomba. Akasaidizana na wauguzi kuitoa risasi, kisha wakaanza kufanya taratibu za kushona sehemu hiyo ya bega iliyotobolewa, halafu waifunike. Yote hayo yalichukua muda mrefu kiasi mpaka inafika saa 9.

Wakati Lexi akiwa anaendelea kupewa huduma, muuguzi mmoja alimtambua. Alikuwa amemwona kwenye mitandao ya kijamii kuwa mmoja kati ya watu wa kundi la Mess Makers, naye akammwomba daktari watoke nje ya chumba hicho mara moja ili wazungumze. Akaanza kumwambia kuhusu jambo hilo, na wakati alipokuwa akiongea vitu hivyo hapo nje, Isiminzile alikuwa amesimama pembeni akiwasikiliza bila wao kutambua uwepo wake. Daktari yule akamwambia muuguzi kuwa asiseme wala kufanya jambo lolote ambalo lingemshtua mwanamke huyo, ili yeye aende kuwataarifu mapolisi kwa njia ya simu waje kumkamata. Muuguzi akakubali na kurudi kwa Lexi, naye daktari akaelekea kwenye ofisi yake kufanya jambo hilo.

Isiminzile akaingia upesi kwenye chumba alichokuwepo Lexi na kukuta wauguzi watatu kutia ndani yule aliyemtambua Lexi, naye akamsogelea Lexi karibu zaidi. Wauguzi wale wakaanza kumfukuza kwa kusema hakutakiwa kuingia kwenye chumba hicho, naye Isiminzile akamwambia Lexi hivi, "Tunapaswa kuondoka." Lexi hakuhitaji maelezo zaidi. Akajitoa kitandani na kuanza kuvaa T-shirt yake, ingawa alihisi maumivu kupita kiasi. Wauguzi wale wakawa wanauliza ni kitu gani wanafanya, na yule mmoja akawaambia kwamba huyu mwanamke ni mmoja wa "magaidi" wanaojiita Mess Makers.

Lexi akajitahidi kupitisha T-shirt yake mwilini ingawa kidonda chake kikubwa hakikuwa kimefunikwa bado, kisha akachukua dawa za kupunguza maumivu na kuanza kuondoka huku akizibugia. Wauguzi wakawa wanajaribu kuwazuia kwa kutumia nguvu, lakini Lexi akajitahidi kuwatandika wawili kwa njia ambayo iliwaumiza kidogo, naye Isiminzile akamdhibiti mmoja wao na kusaidia watoke hapo haraka. Waliondoka upesi kabla ya wauguzi wale kuanza kuita msaada, na uzuri kwa wakati huu hakukuwa na watu wengi kwenye hospitali hiyo. Wakaelekea mpaka kwenye gari la Isiminzile, naye akaliondoa hapo upesi.

Wakiwa ndiyo wameanza mwendo, Lexi alionyesha kuwa na maumivu ya hali ya juu ingawa alijitahidi kujikaza. Kichwa kilimuuma, mwili ulimuuma, na kuna viungo vyake ambavyo bado hakuvihisi vyema kutokana na ganzi kuenea mwilini. Isiminzile akasema kwamba angempeleka kwake, lakini Lexi akakanusha na kumwambia kwa sababu amemsaidia, yeye pia alikuwa amejiweka hatarini. Akamwomba atoe simu yake kisha apige namba fulani. Isiminzile akatii. Baada ya kupiga, namba hiyo ikawa haipatikani. Lexi akatambua kwamba bila shaka wenzake walikuwa wameziharibu simu zao za kawaida, hivyo akamwambia Isiminzile apige nyingine, halafu aseme tu hivi, "Zelda hajambo? Mwambie anipitie pale pale alipopitia," kisha akate bila kusikiliza chochote.

Ingawa Isiminzile hakuelewa jambo hilo, akafanya kama alivyoambiwa, na baada ya kupiga namba hiyo akasema maneno hayo, kisha akakata upesi.



Ni wakati huo huo ndiyo Torres alipokuwa bado akikaza misuli ya mitambo yake pale namba fulani ilipopiga kwenye kifaa kile maalum cha mawasiliano ya Mess Makers, kama ambavyo wote walikuwa navyo. Alishangaa kiasi kuona namba hiyo ngeni, naye akaiunganisha upesi kwenye mifumo ya kompyuta zake ili akipokea, hata kama ingekuwa ni mtego, basi wanaoutega wasiweze kujua sehemu alipo. LaKeisha bado alikuwa pembeni yake muda huo, pamoja na Azra, nao wakaweka umakini kuona ni nini kingefuata.

Ndipo baada ya kupokea, Torres, Azra, na Lakeisha wote wakasikia sauti ya mwanaume ikisema "Hallo... Zelda hajambo? Mwambie anipitie pale pale alipopitia," kisha simu ya mwanaume huyo ikakata mawasiliano. Torres alikunja uso wake kimaswali. LaKeisha akamuuliza hicho kilikuwa ni nini, ni nani aliyekuwa anamuuliza ikiwa Zelda hajambo, na alimjua vipi Zelda. Azra akawa wa kwanza kutambua kwamba hiyo ni njia ya Lexi ya kuwasiliana nao kwa kificho, na baada ya kumwambia hivyo Torres, jamaa akaanza kufatilia namba hiyo ilikuwa wapi. Akapata kuona kwamba ilikuwa jijini Dar, ikitembea kutoka huko, yaani kwa usawa wa barabara ya kuelekea nje ya mji.

Torres sasa akawa ametambua kwamba Lexi alikuwa anamtumia ujumbe kumwambia alipo ili afanye jambo fulani kwenda kumsaidia, na ilionekana alikuwa akitoroka. Akamwambia hayo LaKeisha, na LaKeisha akatoka upesi kwenda kuwaita wengine. Baada ya wote kuwa wamefika na kuambiwa yaliyoendelea, Kendrick akawapa ruhusa Torres, LaKeisha na Azra kwenda huko upesi ili kumsaidia Lexi, kwa kuwa ni wao tu ndiyo ambao hawakujulikana bado, na hivyo uwezekano wa kumleta Lexi hapo bila wao kufatiliwa ulikuwa mkubwa. Alijua kwamba kutokana na wao kutoroka usiku huo, ulinzi na ufatiliaji kutoka kwa watu wa usalama ungekuwa mkubwa hata zaidi, kwa hiyo watatu hao wangetakiwa kwenda wakiwa katika hali ya kawaida lakini kwa tahadhari kubwa sana.

Bila kuchelewa, watatu hao wakaondoka hapo kwenye sehemu yao ya maficho, wakitumaini kuwahi na kukutana njiani pamoja na Lexi ili kumrudisha huku. Yaani hawa watu walikuwa hawapumziki! Habari hizi hazikumfurahisha Kevin hata kidogo, ambaye alikuwa anashangaa ni jinsi gani Lexi angekuwa ametoroka ikiwa alikamatwa kweli. Akabaki tu kuombea kwamba huko ambako Torres, LaKeisha na Azra wangekwenda na wenyewe wakamatwe pamoja na Lexi, kwa sababu hakutaka mwanamke yule arudi hapo tena.


★★★★


"NINI?!"

Hilo lilikuwa ni swali lililoulizwa kwa sauti ya juu sana na Kanali Oswald Deule baada ya kupokea taarifa kwamba Lexi ametoroka. Alishindwa kuelewa iliwezekanaje mwanamke huyo mmoja awatoroke wanajeshi sita wenye silaha kali, tena akiwa amefungwa. Taarifa hizo alizipata kupitia kwa mwanajeshi yule aliyekuwa akiendesha gari ambalo lilitumiwa kumsafirisha Lexi kuelekea kule walikodhamiria.

Kanali Oswald alikuwa pamoja na Kapteni Erasto pia wakati akiongea na mwanajeshi huyo kwa simu. Akamwamuru mwanajeshi huyo pamoja na mwenzake wafanye juu chini kuhakikisha Lexi anakamatwa kabla jua halijachomoza, yaani wamtafute kila kona ya eneo hilo na kila nyumba, la sivyo kungekuwa na adhabu mbaya sana kwa ajili yao. Akawaambia angewaongezea watu wa kuanza kumsaka, na kwa sababu mwanajeshi yule alikuwa amemwambia kwamba walimpiga risasi Lexi, Kanali Oswald akasisitiza wakague na hospitali za kuzunguka eneo hilo lote pia. Kisha akakata simu na kuirusha pembeni kwa nguvu akiwa anapumua kwa hasira kali.

"Hawa vijana ni washenzi sana!" akasema Kanali Oswald.

"Tokea mwanzoni nilihisi kabisa kwamba kuna jambo halingeenda sawa maana huyo mwanamke ni mchawi siyo kama anavyoonekana. Haiwezekani... yaani haiwezekani kabisa eti atoroke... aisee! Hivi kwa haya mambo watu tunalala saa ngapi?" akasema Kapteni Erasto kwa kuudhika.

"Zungusha magari na upige blockade kwenye njia zote za kutoka ndani ya jiji. Hakutakiwi kuondoka hata kwa mabasi ya abiria bila kukaguliwa alifajiri ya leo, umenielewa?" Kanali Oswald akatoa amri.

"Nimeshatoa agizo hilo mkuu. Najua ndani ya muda mfupi tutazipata habari zake," Kapteni Erasto akasema.

Kanali Oswald alikuwa anazunguka huku na huku ndani ya chumba hicho walichokuwa kwa kukosa amani kabisa.

"Kanali... utamjulisha General kuhusu jambo hili wakati gani?" Kapteni Erasto akamuuliza.

"No, no. Sitamwambia lolote mpaka nihakikishe huyo malaya amerudishwa mikononi mwetu. Hili suala halipaswi kumfikia kwanza, umenielewa? Liwe kama halijatokea kabisa!" Kanali Oswald akasema.

"Lakini vipi kama... je kama asipokamatwa?" Kapteni Erasto akamuuliza.

Kanali Oswald akamfata na kumtandika ngumi nzito tumboni. Kapteni Erasto alihisi maumivu na kubaki ameinama huku ameshika tumbo lake.

"Atakamatwa mpumbavu wewe! Si umetoka kuniambia ndani ya muda mfupi tutazipata habari zake? Na iwe hivyo. Kwa sababu ikiwa hatakamatwa nitahakikisha nakuua kwanza kabla Jenerali hajaniua mimi. Unaelewa matapishi yangu?" Kanali Oswald akafoka kwa hasira.

"Ndiyo mkuu," Kapteni Erasto akajibu bila kumtazama.

Kanali Oswald akasogea pembeni akiwaza mambo mengi sana. Alikuwa na wasiwasi mwingi kwa kuwa alijua kama Lexi hangekamatwa, basi Jenerali Jacob angekasirika kupita maelezo. Na ni wakati huu alipokuwa tu anamfikiria Jenerali Jacob simu yake ikaita, na mpigaji hakuwa mwingine ila Jenerali mwenyewe. Akafumba macho na kumeza mate, kisha akajituliza na kupokea.

"Habari za wakati huu Jenerali Jacob?" Kanali Oswald akatoa salamu huku anamwangalia Kapteni Erasto.

"Kanali... mmefikia wapi?" sauti tulivu ya Jenerali Jacob ikasikika.

"Aa... bado yuko barabarani analetwa huko. Usijali kuhusu lolote General, enjoy usingizi wako tu, kila kitu kitakuwa sawa kufikia asubuhi," akasema Kanali Oswald.

"Ikiwa unasema kila kitu kitakuwa sawa inamaanisha kuna kitu hakiko sawa. Kuna tatizo lolote?" Jenerali Jacob akauliza.

"No, no, no, sijamaanisha hivyo. Ni kwamba tu... sasa hivi ni usiku kwa hiyo... kila jambo kama..."

"Kanali..."

Oswald akakatishwa na mmoja wa wanajeshi waliofanyia kazi kwenye jengo hilo aliyeingia hapo ofisini ghafla. Kapteni Erasto akamzuia kwa ishara kumwambia akae kimya kwanza.

"Ndiyo General... everything is under control. Umeniamini katika hili mkuu, sitakuangusha. Nitamfikisha huko haraka na... kama tu tulivyoongea," akasema Kanali.

"Hmm... okay. Wacha nirudi kulala sasa. Nategemea mambo mazuri sana nikiamka asubuhi na kwenda kule. Kazi nzuri sana Kanali," Jenerali Jacob akasema.

Kanali Oswald akafumba macho kwa kuhisi hofu hata zaidi.

Simu ikakatwa, naye Kanali Oswald alikuwa anahisi ni kama Jenerali Jacob alikuwa anamwambia mambo kwa njia ya kebehi; yaani ni kama tayari alijua kuhusu Lexi kutoroka ila akawa anamchezea akili. Ikiwa hiyo ilikuwa ndivyo mambo yalivyo, basi Kanali Oswald akatambua kwamba alikuwa amejivuruga sana.

"Una shida gani?" Kapteni Erasto akamuuliza mwanajeshi yule aliyeingia.

"Tumepata taarifa kuhusu mwanamke mweupe aliyepigwa risasi kuingia kwenye hospitali moja... wamemtambua kuwa mmoja wa Mess Makers," mwanajeshi huyo akasema.

Kanali Oswald akamsogelea.

"Na nini kingine?" akamuuliza.

"Alikuwa na mwanaume mwingine ambaye alimpeleka hapo, lakini watu wetu walipofika wakakuta wameshaondoka. Ndiyo wako in pursuit sasa kutafuta barabara zote ambazo ni possible gari walilotumia lilipita..."

"Waambie wahakikishe hafiki mbali, tunaingia huko pia. Tutumie location hizo," Kanali Oswald akatoa amri.

Mwanajeshi huyo, ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kitengo cha kupokea na kutuma taarifa muhimu kwa wanajeshi walio kwenye "mission," akatoka upesi na kurudi kwenye vyumba maalumu vya mawasiliano.

Kanali Oswald na Kapteni Erasto wakatoka upesi pia na kuelekea huko ambako Lexi alikuwa akifuatiliwa. Walitumia helicopter ndogo ya kijeshi ili kuwahi, nao wakaendelea kuwasiliana na wanajeshi waliokuwa wametangulia kupata kujua walifikia wapi, na baada ya mwendo wa kama dakika 15 hivi wakawa wamefika sehemu ambayo wanajeshi walilizingira gari lile la Isiminzile!

Eneo hili lilizungukwa na miti mingi kwa pande za pembeni na barabara kuu, hivyo magari ya wanajeshi yaliyokuwepo yalimulika gari hilo lililoonekana kusimama hapo kwa njia fulani ya mtego. Walihitaji kuwa makini sana kwa sababu waliwaelewa sana Mess Makers kwenye masuala ya mabomu, hivyo wakafikiria huenda kama Lexi angekuwa humo basi angekuwa amejitega na bomu kabisa.

Lakini baada ya helicopter ya Kanali na Kapteni kutua, Kanali Oswald aliwaambia wanajeshi kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kukaa kuliangalia gari badala ya kufanya jambo la maana kujua kama mtu wao yuko humo au la. Kapteni Erasto na wanajeshi kadhaa wakaanza kulielekea gari hilo kwa umakini sana, na baada ya kulifikia karibu, wakalikagua pande zote na kipimo maalumu cha kuhisi mabomu na kukosa, kisha wakaanza kufungua milango na kuangalia ndani lakini na penyewe hakukuwa na mtu ndani yake.

Ikaja kwa kushangaza sana kwa sababu haingewezekana gari hilo kujiendesha lenyewe mpaka kufikia hapo. Ikabidi uchunguzi wa kina uanze kufanywa na kufanya Kapteni Erasto kutambua haraka kwamba walikuwa wanapotezewa muda tu ili Lexi aweze kutoroka. Akamwambia Kanali Oswald inaonekana labda wenzake Lexi ambao walitoroka pia siku hiyo, walikuwa wametumia njia hii kuwazubaisha ili mwanamke huyo aweze kuwatoroka. Kanali Oswald akaanza kuuliza wanajeshi wengine ambao walikuwa kwenye barabara zote za jiji kama kuna magari waliyaruhusu yapite bila kuyachunguza, lakini wakakanusha.

Hasira ilimjaa baba huyo ambaye alipiga kelele kwa nguvu kwa kutambua kwamba habari yake ilikuwa imekwisha. Aliwaza sana angemwambia nini Jenerali Jacob ambaye bila shaka angekasirishwa sana na jambo hili. Ilikuwa imefika saa 10 usiku sasa, na haikuonekana tena kama wangeweza kumpata mwanamke huyo na kundi lake lenye akili kupita maelezo.

Kapteni Erasto akamwahidi Kanali kwamba hawataacha kumtafuta Lexi hata kama wasipolala kwa siku zote zitakazofuata. Akatoa amri kwa wanajeshi wengine kuondoka eneo hilo na kuendelea kutafuta sehemu nyingine za jiji hilo.


★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Ahsante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…