Simulizi: For You

Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Siku hiyo ikakucha, na sasa ikiwa ni asubuhi na mapema, Nora akaamka kutoka usingizini akijihisi uchovu mwingi wa kiakili. Alitulia tu kitandani hapo akiwaza mambo mengi sana kuhusu vitu ambavyo Lexi alimwambia kuhusu baba yake. Aliwaza pia kuhusu mambo ambayo yeye mwenyewe alikuwa amefanya, ikiwa alikuwa akipita kwenye njia sahihi au la, na kama upande ambao alichagua kujiweka ulikuwa ni upande mzuri au mbaya.

Hakujua mambo mengi sana, lakini kama ni jambo moja alilotaka kujua ilikuwa ni habari kumhusu Lexi. Akajinyanyua kutoka kitandani na kuivuta simu yake, kisha akatafuta namba ya Luteni Michael kumuuliza ikiwa Lexi alifikishwa kule alikopelekwa. Lakini akasita kwanza. Akafikiria jambo fulani, kisha akaona aache tu kufanya hivyo. Moyoni mwake alibeba hisia nzito za hatia kutokana na kitendo fulani alichokifanya, na ijapokuwa hakuwa na uhakika kama kilifanikiwa au la, hakutaka kuanza kujichoresha haraka sana kwa sababu ingemletea shida mapema. Na yeye alikuwa na siri pia.

Akaamua tu kuianza siku yake kwa kujisafisha na kupata kiamsha kinywa, kisha ndiyo angetoka na kuelekea kwenye ofisi yake. Akampigia mdogo wake simu kumsalimu huku akinywa chai, na kabla hajamaliza maongezi yao, mlango wa chumba chake ukagongwa. Akatoka kwenda kuangalia ni nani, na hapo mlangoni akamkuta Luteni Michael pamoja na Mario na Hussein. Hakushtuka. Akatoa tabasamu la kirafiki, huku wenyewe wakimwangalia kwa umakini sana.

"Karibuni," Nora akawakaribisha.

"Nora... tunahitaji kuzungumza," Luteni Michael akamwambia.

"Ndiyo, haina shida. Karibuni ndani," Nora akasema.

Mario na Hussein wakatazamana. Luteni Michael akaendelea tu kusimama hapo.

"Kuna tatizo lolote?" Nora akauliza.

"Yule mwanamke ametoroka," Mario akamwambia.

Nora akatazama chini kwa njia ya kawaida tu.

"Hujasikia kuhusu hilo?" Hussein akamuuliza pia.

Nora akatikisa kichwa kukanusha.

"Ametoroka vipi?" akauliza.

"Ameua wanajeshi wanne waliokuwa wanamlinda na kukimbia. Inashangaza sana kwamba ameweza kufanya jambo hilo kwa wepesi wa hali ya juu. Unafikiri aliwezaje kufanya hivyo?" Luteni Michael akauliza.

"Sijui Michael. Lexi... hamkutakiwa kumwekea watu wanne kumlinda. Ana... ana ustadi mkubwa kwenye mambo mengi," Nora akasema.

Wanajeshi wakaangaliana kwa njia yenye utata.

"Kwa hiyo... hawajamkamata bado?" Nora akauliza.

"Nora... sitaki kuku-accuse kwa lolote. Lakini ni muhimu sana ikiwa utasema ukweli. Ni wewe ndiyo ulimsaidia atoroke?" Luteni Michael akamuuliza.

"Mimi? What... ningemsaidia vipi..."

"Kapteni anafikiri ni wewe ndiye uliyefanya huyo mwanamke akaweza kuwatoroka wanajeshi wale. Anataka tukupeleke kwake ili... akuhoji," akasema Luteni Michael.

Nora akashusha pumzi, kisha akasema, "Haina tatizo. Nitaenda pamoja nanyi."

Luteni Michael alimtazama Nora kwa hisia sana.

Mwanamke huyo akarudi ndani na kuchukua vifaa vyake vichache, kisha akaongozana na wanaume hawa watatu mpaka kule alikokuwa Kapteni Erasto. Ilikuwa ni kwenye jengo lile lile, na baada ya kufikishwa kwenye ofisi yake, Nora akaketi na kutazamana na Kapteni Erasto. Mario na Hussein walimsubiria Luteni Michael nje, hivyo ofisini humo kukawa na watu watatu; Kapteni Erasto, Luteni Michael na ACP Nora.

"Nora... nafurahi kwamba umekuja bila kulazimishwa. Step ya kwanza inayoonyesha kwamba unajaribu kuthibitisha hauna hatia. Bila shaka umesikia kuhusu kilichotokea, siyo?" Kapteni Erasto akamuuliza.

"Ndiyo. Nimesikia," Nora akajibu.

"Haijakushangaza hata kidogo?" Kapteni Erasto akamuuliza.

"Kuna mambo mengi sana ambayo yule mwanamke amefanya huwa yananishangaza. Nimemzoea kwa njia hiyo tayari kwa hiyo... wakati huu sijashangaa sana kuhusu hilo," Nora akasema.

"Mambo kama yapi mengine ambayo amefanya yaliyokushangaza?"

"Ni mengi. Sikudhani angeweza kumkalisha chini Luteni, lakini aliweza," Nora akasema.

"Alibahatisha tu kwa sababu niliangukia kichwa," Luteni Michael akajitetea.

Kapteni Erasto akatabasamu.

"Unajaribu kuwa mcheshi wakati unajua tuko chini ya hali gani?" Kapteni Erasto akamuuliza Nora.

"Sielewi Kapteni unamaanisha nini..."

"Unajua ninachomaanisha. Unajua ulichokifanya. Umemsaidia kutoroka kwa sababu zako za kibinafsi, lakini kwa faida gani? Ili awaue wanaume wenye familia zao kwa ajili yako, au?"

"Mimi sijui unacho..."

"Kaa kimya!" Kapteni Erasto akafoka kwa hasira.

Nora akatulia tu. Luteni Michael akaangalia pembeni.

"Najua ni jinsi gani ulivyo na akili. Umeigeuzia hii kwangu kwa sababu mimi ndiyo nilikagua kile chakula na kuruhusu kipite, kwa hiyo hata kama ikichunguzwa huwezi kukutwa na shida, si ndiyo? Ulifanyaje vile? Ulificha vipi kitu kilichomsaidia atoroke mule?" Kapteni Erasto akamuuliza.

"Kapteni... bado sielewi, na sijui unachomaanisha. Sijafanya lolote unalosema," Nora akaendelea kukataa.

Kapteni Erasto akatoka upande wa kiti chake na kumfata Nora alipoketi.

"Najua una kiburi kwa sababu unajiona kuwa immune cause baba yako ni General. Kwamba... hautaguswa, mtoto wa mfalme. Lakini kwa kitendo ulichofanya, unafikiri tukimwambia baba yako atakuacha salama? Au hujui kwamba yeye ndiye aliyekuwa anamhitaji zaidi mwanamke huyo?" Kapteni Erasto akamuuliza.

Luteni Michael akamtazama kimaswali. Nora akaendelea kukaa kwa utulivu tu.

"Huenda hiyo ndiyo sababu ukaona umsaidie mpenzi wako malaya mkubwa wewe! Kwa sababu unajua baba yako anataka kummaliza yeye mwenyewe. Unaweza ukajiona ni kama umeshinda, lakini huo ushindi hautafika mbali. Tutamkamata huyo mshenzi mwenzako na kumnyonyoa kila sehemu ya ngozi yake mbele ya macho yako. Na yote hiyo kwa ajili ya General... how do you like your father princess, huh?" Kapteni Erasto akasema kwa dharau.

Luteni Michael alikuwa anamtazama Kapteni Erasto kwa umakini sana. Mambo mengi aliyosema yalimshangaza mno.

"Umemaliza?" Nora akauliza kiutulivu.

"Hapana darling. Muziki ndiyo umeanza tu. Vifo vya ma-comrade wetu lazima vitalipwa, hata kwa damu zisizo na hatia. Na hiyo itakuwa ni juu yako," Kapteni Erasto akamwambia kwa ukaribu.

Nora akamwangalia kwa hisia kali, kisha akasimama na kutoka ndani ya ofisi hiyo.

"Kapteni... ni nini kinaendelea? Umeniagiza nimfate, nimlete, na sasa anaondoka... kihivyo tu?" Luteni Michael akauliza.

"Unafikiri nitamfanyaje? Nitamfunga? Unajua baba yake hataruhusu hilo... na ndiyo kinachompa kiburi hata kama akifanya nini," Kapteni Erasto akasema kwa kuudhika.

"Kwa hiyo kumbe Lexi alikuwa anapelekwa kwa General. Naweza kuuliza ni kwa nini? Nilifikiri anapelekwa kambi ya mateso ili aseme ukweli," Luteni Michael akauliza.

"Haina haja ya kujiingiza sana kwenye mambo ya General. Wewe na team yako pigeni utafiti wenu mmnase huyo mshenzi. Na... hakikisha macho yenu hamyaondoi kwa huyo mwanamke, Nora. Anajua mambo mengi kuliko anavyojionyesha," Kapteni Erasto akasema.

"Una uhakika ni yeye ndiye ambaye alimsaidia Lexi?"

"Damn! Ndiyo! Ni yeye ndiye amemsaidia Lexi. Aagh, silipendi hilo jina Luteni naomba usilitaje tena ukiwa mbele yangu! Nenda upige kazi mwanaume, acha maswali mengi," Kapteni Erasto akamwamuru.

Luteni Michael kweli bado alikuwa na maswali mengi sana kichwani kwake, lakini akatii na kuondoka hapo upesi sana. Alikuwa anataka kumwahi Nora ili aweze kuongea naye, na kwa tukio zuri akamkuta akiwa pamoja na Mario na Hussein, pamoja na mwanamke mwingine mwanajeshi aliyeitwa Samia wakiwa wanaongea. Akawafuata hapo walipokuwa wamesimama.

"Yaani hata hatulali dada, huyu Lexi atatukondesha sana mwaka huu," Mario akawa anamwambia Nora.

"Kwa hiyo... kweli aliwaua wanajeshi wale wote?" Nora akauliza.

"Ndiyo... ndiyo wanavyosema. Demu yuko vizuri eeh?" akasema Hussein.

"We mjinga kweli yaani watu wamekufa halafu unamsifia muuaji?" Samia akasema.

"Sijamsifia. Ila wewe kweli fikiria. Yaani wanajeshi sita... wenye silaha na mafunzo hao... wametorokwa na mwanamke aliyefungwa pingu. We ungeweza?" Hussein akamuuliza Samia.

"Ndiyo ninge...."

"Vijana, nahitaji kuongea na ACP," Luteni Michael akayakatisha maongezi yao.

Wanajeshi hao watatu wakaondoka hapo na kuwaacha wawili hawa.

"Nora... nini kinaendelea?" Luteni Michael akauliza.

"Nilifikiri Erasto amemaliza kukupigia mstari juu ya hilo," Nora akasema.

"No monkey business. Niambie ukweli. Umefanya kama vile anavyodai?"

"Unataka nikwambie nini Michael? Kile ambacho unataka kusikia siwezi kukisema, na kile ambacho hautaamini ndiyo nitakachokisema. Mimi ninaacha... mwamini mnachotaka kuamini. I don't care anymore," Nora akasema.

"Ni sababu gani inayomfanya baba yako amhitaji sana Lexi? Ni nini kimefichika?"

"Sijui Michael. Sijui. Lakini naweza tu kusema kwamba... lolote ambalo anafikiria juu yake si zuri... lakini niko mbali sana kiuwezo kuweza kufanya lolote..."

"Ungefanya nini Nora? Yule mwanamke ni... mwovu. Ni msaliti, ni mwongo, ni mtu mbaya sana ambaye amesababisha uharibiwe sifa yako. Unawezaje hata kuwaza kufanya lolote kwa ajili yake?"

Nora akatulia kidogo na kuangalia pembeni.

"Nora... ninajua una moyo mzuri. Lakini kuna watu wanatumia hilo kama udhaifu ili kukufanyia ubaya. Usijiruhusu... usijiruhusu uchezewe namna hiyo. Unastahili mambo mengi mazuri kwa kazi zako zote kwa ajili ya masilahi ya nchi hii... siyo hivi. Kashifa zote, kuvunjiwa heshima, kuhukumiwa... kwa ajili ya nini? Kwa nini? Eh? Kwa nini unapitia haya yote kwa ajili ya huyo mwanamke Nora?" Luteni Michael akauliza kwa hisia.

Nora akaangalia tu chini bila kutoa neno lolote. Luteni Michael akashusha pumzi kwa kufadhaika.

"Unajua haya yote hayataishia pazuri. Hawataacha kukusumbua. Wata... watafanya kila kitu..."

"Najua. Najua Michael," Nora akamkatisha.

"Kwa hiyo... uko radhi kupoteza kila kitu... kwa ajili yake?" Luteni Michael akauliza.

"Ningeweza kufikia hatua hiyo... lakini sasa... sijui. Mambo mengi yamebadilika. Nitakuwa tayari tu kwa lolote litakalokuja mbele yangu. Niko tayari," Nora akasema.

Luteni Michael akatikisa kichwa chake kwa huzuni.

"Okay. Kanali ameitwa na General hii asubuhi, nafikiri kuhusiana na hii ishu. Mambo upande wetu yanakwenda kwa kasi sana, Lexi atapatikana muda siyo mrefu. Natumaini utakuwa tayari kwa kitakachotokea baada ya hapo," Luteni Michael akamwambia.

Nora akamtazama machoni kwa hisia, kisha akatikisa kichwa chake kuonyesha amemwelewa. Akamwacha hapo na kuondoka zake akiwa na mambo mengi sana kichwani. Mario na Hussein walimchukua na kumrudisha mpaka hotelini kwake tena. Alikuwa anajihisi vibaya sana, na baada ya kuingia ndani ya chumba chake, akaanza kulia kwa uchungu mwingi. Alijihisi kuwa kwenye njia panda na hakukuwa na wa kumsaidia kujua pa kwenda.

Simu yake iliita sana, akipigiwa na watu wa kazini, lakini hakujisumbua kuigusa tena na kujilaza tu kitandani kwa muda mrefu akihisi hatia na
upweke mwingi.


★★★★


Upande wa Kanali Oswald Deule. Alikuwa amefika kwenye jumba la kifahari la Jenerali Jacob, ambapo aliitwa ili kukutana naye. Kwenye jumba hilo kubwa ndipo biashara na mikutano ya muhimu baina ya Jenerali na watu wake ilifanywa, na mara kwa mara wote walioshiriki kwenye mipango haramu ya Jenerali na Raisi walialikwa hapo ili kufanya mazungumzo au mambo yao ya kisiri, na Kanali Oswald alikuwa ni kati ya watu wachache waliokwenda hapo nyakati ambazo Jenerali angewaita.

Lakini wakati huu Kanali Oswald alijua dhumuni la kuitwa kwake halikuwa zuri, kwa sababu alichomwahidi Jenerali hakikuwa kimetimia. Alijua fika kuwa Jenerali Jacob alikuwa mwanaume makini asiyependa mchezo hata kidogo, hivyo kuwa kwake hapo angehitaji kujinyenyekeza sana ili mambo yasimharibikie. Alikaribishwa na mabaunsa walinzi wa jengo lile waliomwongoza mpaka sehemu ya ndani, kisha wakamwomba awape silaha yake yoyote aliyokuwa nayo kwa kuwa Jenerali hakupenda silaha ndani ya jengo lake. Lilikuwa jengo jeupe, safi na pana sana. Kulikuwa na wanawake wengi waliofanya kazi hapo, waliovalia chupi na sidiria kama wanamitindo, wakitumiwa pia kama watoaji wa burudani; kutia ndani na mapenzi.

Alipofika usawa wa ngazi zilizoelekea juu ya ghorofa la pili, Kanali Oswald akamwona Luteni Jenerali Weisiko pamoja na Jenerali Jacob mwenyewe, wakiwa wamesimama huku wakionekana kuongelea mambo fulani kwa umakini. Walikuwa wamezungukwa na wanawake watano ambao walikuwa nusu uchi kabisa, wakiwashika-shika mwilini na kuchezesha miili yao mbele yao kama kuwapa burudani. Bila hata kumwangalia, Jenerali Jacob akamtolea ishara Kanali Oswald kuwa apande mpaka hapo juu. Wasiwasi ulimjaa mwanaume huyu, lakini akasogea mpaka huko na kuwasalimu wakubwa wake hao.

"Za safari Oswald? Umeona mnyama gani anayekula nyama njiani?" Jenerali Jacob akauliza.

"Aa... safari ilikuwa tulivu. General... najua kwamba nimekosea, na haikuwa kwa... nia mbaya... yaani... tulizungukwa na...."

"Nimekuuliza umeona mnyama gani wakati unakuja?" Jenerali Jacob akamkatisha.

Kanali Oswald akabaki kimya tu.

"Nilitakiwa kufurahia usingizi wangu ili nikiamka asubuhi niifurahie zawadi ambayo uliahidi kuniletea. Nimeufurahia usingizi, lakini mbona zawadi siioni?" akauliza Jenerali Jacob.

"General... kumradhi sana kwa kuwa..."

Jenerali Jacob akanyanyua vidole vyake juu kumkatisha. Weisiko akawaambia wanawake wale waondoke hapo, nao wakatii. Jenerali Jacob akamsogelea karibu Kanali Oswald, ambaye alikuwa anahisi kama anataka kufa vile kwa presha.

"Kwa nini ulinidanganya?" Jenerali Jacob akauliza.

"Siku... sikukudanganya General. Kuna mambo tu yalitokea bila..."

Kanali Oswald akashindwa kuendelea. Aliona jinsi wawili hao walivyomwangalia kwa njia fulani iliyoonyesha walikuwa na lengo fulani baya sana kumwelekea. Lakini mara ghafla Jenerali Jacob akaanza kucheka kwa njia iliyoonyesha hakuwa na ubaya wowote kumwelekea. Kanali Oswald akachanganywa na hili, lakini naye akajifanya kutabasamu.

"Hahahah.... usiniambie hapo ulipo mikojo tayari ilikuwa imeanza kukushuka! Ulikuwa unaogopa sana eeh?" Jacob akamuuliza.

"General..."

"Kanali... usihofu. Mimi tayari nilikuwa najua huyo msichana alitoroka wakati naongea nawe kwenye simu. Najua unafikiri labda nimekasirika sana na nitakufanya jambo fulani baya, lakini hiyo siyo sababu niliyokuitia hapa. Nimekuita hapa ili kukuonyesha jambo lingine. Uko tayari?" Jenerali Jacob akamwambia.

Kanali Oswald akatikisa kichwa kukubali.

Kisha Jenerali Jacob akatabasamu na kuanza kuondoka kuelekea chini ya ngazi zile. Kanali alipomwangalia Weisiko, aliona bado mwanaume huyo alikuwa anamtazama kwa njia isiyo ya kirafiki kabisa, hivyo akajua bado kulikuwa na nuksi. Hawa hawakuwa watu wa kusamehe na kusahau, lakini kama ni kuwaomba msamaha basi angepiga hata magoti ili aupate.

"Unafanya nini Oswald? Nifate," Jenerali Jacob akasema.

"Sawa mkuu," Kanali Oswald akajibu na kuanza kumfata haraka.

Walishuka ngazi pamoja mpaka sehemu ya chini na kuanza kuelekea upande mwingine ndani ya jengo hili. Kanali Oswald hakujua ni wapi au ni nini angeenda kuonyeshwa, hivyo akajikaza tu kiume na kujifariji kwamba mambo yote yangekuwa sawa. Wakafika kwenye mlango mmoja wa chumba ambacho kilikuwa kimejitenga, kisha Jenerali Jacob akaufungua na kuingia ndani. Kanali Oswald akamfuata, na baada ya kuingia aliweza kuona kilikuwa chumba chenye vifaa vingi vilivyotunzwa, kama stoo vile, nacho kilikuwa na giza kiasi.

Jenerali Jacob akasimama usawa wa pazia kubwa jeupe lililokuwa limetundikwa katikati ya chumba na kumgeukia Kanali Oswald.

"Unajua point ya mambo yote tunayofanya ni nini?" Jenerali Jacob akauliza.

"Ni kwa ajili ya taifa General," Kanali Oswald akajibu.

"Oh good. Kwa hiyo kama unajua hilo, inamaanisha unajua pia kwamba hatutakiwi kuruhusu makosa ya aina yoyote kwenye kazi..."

"General..."

"Sijasema kwamba mambo yote yaliyotokea ni makosa yako. Ila unabidi tu uelewe kwamba hawa... Mess Makers wamekuwa... mwiba mkali sana kwangu... na nilipoku-assign uwashughulikie niliamini kabisa kwamba wasingesikika tena..."

"General..."

"...na uliniahidi, uliniahidi... kwamba wasingesikika tena. Huwa sipendi ahadi fake Oswald unajua hilo. Na pia huwa sipendi kuchafua mikono yangu mwenyewe, ndiyo maana nikakuweka unitolee huo uchafu. Nataka tu kujua ni kwa nini umeshindwa kutimiza hiyo ahadi," Jenerali Jacob akasema kwa sauti tulivu.

"General... sijashindwa. Nakuhakikishia Jabari na huyo mwanamke nitawaleta kwako. Hivi tunavyozungumza wanafatiliwa sehemu zote za jiji hili, na hawawezi kufika mbali kwa sababu hawataweza kutoka nje ya mkoa huu. Na hata kama waki...."

"Kanali... haujaona mnyama yoyote anayekula nyama wakati unakuja huku?" Jenerali Jacob akamkatisha na kumuuliza hivyo kwa mara nyingine tena.

Kanali Oswald hakuweza kumwelewa kabisa, lakini alijua bila shaka swali lake lilikuwa na maana fulani. Ikiwa angetoa jibu lisilo sahihi, basi lazima kuna jambo lingetokea. Lakini hakujua ajibu nini, kwa hiyo akaona tu aseme ukweli.

"Hapana General. Sijaona mnyama yoyote anayekula nyama wakati nakuja," Kanali Oswald akajibu.

Jenerali Jacob akacheka sana, kisha akasema, "Basi... wacha nikuonyeshe jambo fulani."

Akalishika pazia lile na kulivuta lote, naye Kanali Oswald akatoa macho kwa mshangao mkubwa. Hapo aliweza kuona ndoo mbili chini, zikidondokewa na damu kutoka kwenye kiwiliwili cha mtu kilichotundikwa juu kama nyama za buchani. Yaani, hakikuwa na kichwa, wala mikono na miguu. Kuanzia shingoni mpaka usawa wa mapaja ndiyo mwili uliokuwepo, na sehemu zake za siri zilikuwa zimekatwa. Hakujua ulikuwa ni mwili wa nani, lakini ilionekana kuwa ni mwanaume kutokana na kutokuwa na matiti makubwa, na uimara wake tumboni.

Lilikuwa ni jambo moja la kikatili sana, naye Kanali Oswald akamtazama Jenerali akiwa anajikaza. Kuona jinsi ambavyo damu bado zilitiririka ilimaanisha jambo hilo lilikuwa limefanyika siku hiyo hiyo na muda mfupi tu uliopita.

"Hivi ndivyo nilivyopigia picha kuuona mwili wa Jabari na binti yake leo. Ingenipa furaha sana kama ningeweza kuikatakata miili yao namna hii... kwa mikono yangu mwenyewe," Jenerali Jacob akasema.

Kanali Oswald akabaki kimya tu.

"Unajua huyu ni nani? Oh, bila shaka huwezi kujua. Lakini kiukweli Oswald... sijaridhika. Nimejitahidi kutoa hasira yangu namna hii lakini... bado sijaridhika. Bado... nahitaji kuitoa hasira nayohisi kutoka kifuani kwangu. Utanisaidia vipi?" Jenerali Jacob akauliza huku anamwangalia Oswald kwa umakini.

"General... nakuahidi... nakuahidi kwa maisha yangu, nitakupa Jabari na Lexi. Nitawa..."

Kabla hajamaliza kuongea, wanaume wawili wenye miili mikubwa wakaingia ndani hapo pamoja na Luteni Jenerali Weisiko, na wanaume hao wakamshika kwa nguvu Kanali Oswald mikononi. Hofu kubwa ilimwingia mwanaume huyu kwa kuwa alitambua sasa kwamba huu ulikuwa ni mwisho wake.

"General, General... tafadhali nisamehe, nisamehe, nisamehe... General niamini... General nita... nitafanya lolote kwa ajili yako... nimefanya mengi sana ajili yako... General tafafhali usinitendee kwa... tafa... tafadhali General..."

Kanali Oswald akawa anamsihi sana Jenerali asimuumize. Alihisi kile ambacho ametoka kuonyeshwa ndiyo ambacho angefanyiwa. Wanaume wale wawili wakaendelea kumshikilia kwa nguvu na kumpigisha magoti chini, naye Weisiko akasimama pembeni yake Jacob akiwa ameshikilia panga lenye makali pande zote mbili.

"Bado naweza kuwa msaada mkubwa kwako General... tafadhali... niruhusu nirekebishe hili... ninakuhakikishia... General nitawaleta kwako please..."

"Acha kulia-lia kama bwege bwana. Tulia... na hii haitauma sana," Luteni Jenerali Weisiko akamwambia huku akimsogelea na panga leke.

"Tafadhali General... kila kitu kilikuwa kinaenda vyema. Angefika kwako kama isingekuwa ya binti yako... General tafadhali usifanye hivi... nimekufanyia mambo mengi sana... siwezi kukuangusha..."

"Subiri," Jenerali Jacob akasema.

Luteni Jenerali Weisiko akatulia kidogo na kumwangalia usoni. Kanali Oswald alikuwa anapumua kwa hofu huku akitokwa na jasho.

"Unamaanisha nini isingekuwa ya binti yangu?" Jenerali Jacob akauliza.

"Aam... ni ACP Nora ndiye aliyefanya mpaka Lexi akatoroka," Kanali Oswald akajibu kwa hofu.

"Kwa nini afanye kitu cha namna hiyo?" Jenerali Jacob akauliza.

"Binti yako alikuwa na urafiki naye... lakini inaonekana pia kwamba anampenda," Oswald akajibu.

"Nini?" Jenerali Jacob akashangaa.

"Unatutania eti?" Weisiko akamuuliza pia.

"Hapana mkuu, hapana. Ni kweli. Kabla ya kuanzisha safari ile... alituomba sana... Nora... alituomba tumruhusu amwone kwa mara ya mwisho... na mimi kwa sababu namheshimu binti yako nikamruhusu General kwa sababu alionyesha uhitaji. Ila akasaliti imani yetu kwake..."

Kabla hajamaliza kuongea, Weisiko akamshika kidevuni kwa nguvu na kumpiga usoni kwa kishikio cha panga lake. Damu zikaanza kumtoka puani Kanali Oswald, akihisi maumivu makali pia.

"General... niruhusu niukatekate ulimi wake sasa hivi huyu mpuuzi," Weisiko akasema huku anamwangalia Kanali Oswald kiukatili.

"Ngoja..."

Jenerali Jacob akasema hivyo na kusogea karibu zaidi na Kanali Oswald.

"Unajua nitakupa kifo kibaya zaidi ya kile unachofikiria nikijua unamsingizia mtoto wangu," Jenerali Jacob akasema kwa uzito.

"Hapana Jenerali... simsingizii. Lexi asingeweza kutoroka kabisa. Ninajua aliweka kitu fulani kwenye chakula alichoomba kumpatia kabla ya safari, na alikificha kwa akili sana... hatukuweza kutambua. General niamini... siwezi nikasema jambo hilo kuhusu mwanao kama... kama sina uhakika. Na najua sipaswi kumfanya lolote kwa sababu ni binti yako, ila ndiyo hivyo ameshatu-cost tayari na sasa inabidi tu tuendelee kuwatafuta wakina..."

"Kaa kimya," Luteni Jenerali Weisiko akamkatisha.

Kanali Oswald akatulia maana alikuwa anaongea haraka-haraka kama cherehani.

"Ulikuwa wapi kuniambia kuhusu hilo muda huo wote?" Jenerali Jacob akauliza.

"Hatukujua... samahani... Lexi alikuwa anamtumia binti yako ili kupata taarifa nyingi na kujua mambo yote kuhusu mipango yetu. Binti yako ni mtu mzuri, kwa hiyo yule mwanamke amemfanyia ulaghai mwingi sana. Hata hii ya kumsaidia atoroke ninajua atakuwa tu amemfanyia ulaghai..." Kanali Oswald akaongea kwa kujifanya anamtetea mtoto wa Jacob.

Jenerali Jacob akavuta pumzi ndefu na kuishusha, akitafakari mambo haya. Kanali Oswald akawa anauangalia kwa hofu mwili ule uliokatwa, kwa kupigia picha kwamba na yeye angefanywa namna hiyo.

"Hata ijapokuwa unachosema kinashangaza, bado ni makosa yako kwamba mpaka sasa haujaweza kuwaleta watu hao kwa General. Ukifikiri hicho kitakuwa ni kisingizio cha kukuacha salama, umekwama ndugu yangu," Luteni Jenerali Weisiko akamwambia.

"Hapana mkubwa... mimi niko loyal kwenu, sikuzote. Sikumshuku binti yako mwanzoni kwa sababu aliaminika... imetokea tu kwamba akausaliti uaminifu huo... haikuwa lengo langu... haikuwa... tafadhali General... nionyeshe msamaha... niko tayari kufanya lolote kwa ajili yako... nitahakikisha..."

"Basi, basi, inatosha. Nyanyuka," Jenerali Jacob akamwambia.

Kanali Oswald akabaki tu kumwangalia.

"Huelewi Kiswahili? Amesema nyanyuka," Luteni Jenerali Weisiko akamwambia kiukali.

Wanaume wale wawili walikuwa wamemwachia Kanali Oswald, hivyo akajinyanyua na kusimama huku bado akiwa mwenye wasiwasi mwingi.

"Sitaki makosa ya aina yoyote yajitokeze tena, unanielewa?" Jenerali Jacob akamwambia.

"Ndiyo... ndiyo General. Sitakuangusha," Kanali Oswald akasema.

"Acha kuogopa. Sikuwa na lengo la kukuua, najua uko loyal sana," Jenerali Jacob akamwambia huku amemshika bega.

Luteni Jenerali Weisiko akacheka kidogo, naye Kanali Oswald akatoa tabasamu la woga-woga.

"Ila, nataka uwe unanijulisha kila kitu kinachoendelea kuanzia sasa, na ninakupa wiki mbili tu washenzi wale uwe umewaleta kwangu, do you understand?" Jenerali Jacob akasema.

"Ondoa shaka General. Nakuahidi nitawaleta kwako mapema kabla ya muda huo," Kanali Oswald akatoa ahadi.

"Acha kujitapa kwa maneno hewa Kanali. Unatoa ahadi halafu hai..."

"Hapana Luteni Jenerali. Zamu hii hata Mungu hataweza kunizuia. Nitahakikisha siwakwazi na ninawaleta kwenu. Nitawaletea wale watu kwenu... kwako General..." Kanali Oswald akaapa.

Jenerali Jacob akatabasamu na kusema, "Vizuri."

Kanali Oswald akashusha pumzi ya utulivu. Alikuwa anahisi kama vile angejiharishia kabisa.

"General... vipi kuhusu hili suala la Nora?" Luteni Jenerali Weisiko akamuuliza.

"Nora... nitadili naye mimi mwenyewe. Kanali hakikisha hakuna mpuuzi yeyote anamgusa binti yangu, unanielewa?" Jenerali Jacob akasema.

"Ndiyo mkuu," Kanali Oswald akajibu.

"Sawa. Unahisi njaa?" Jenerali Jacob akauliza.

"Aaa... ndiyo General... nahisi njaa kiasi," Kanali Oswald akajibu kiwoga-woga.

"Okay. Sahau haya yote, twende tukapate chakula..."

Jenerali Jacob akasema maneno hayo na kuwatolea ishara wanaume wale wawili kuwa walirudishie pazia lile pale juu, kisha akamshika Kanali Oswald begani kirafiki na kuanza kuondoka pamoja naye. Waliongozana mpaka kwenye meza ya chakula huku Jenerali akimwambia Kanali anapaswa kuacha kuogopa kwa kuwa hangemfanyia jambo baya.

Baada ya kuketi kwenye viti pamoja na Weisiko, Jenerali Jacob akaagiza vyakula kwa ajili yao viletwe, na kusema kwa wanawake wale kwamba wamletee chakula "special" Kanali Oswald. Yeye Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko walikuwa wameletewa vyakula vizuri vya aina mbalimbali, kisha Kanali akaletewa sinia pana lililofunikwa kwa juu na kuwekewa mbele yake. Akahisi bila shaka kulikuwa nuksi kwa ndani, naye akamtazama Jenerali kwa wasiwasi.

"Najua wewe uko loyal kwangu, lakini nataka kuona ikiwa utafanya KILA KITU nitakachokuamuru... kama ulivyotoka kusema muda ule," Jenerali Jacob akasema hivyo huku akitabasamu.

Kanali Oswald akameza mate akianza kuingiwa na hofu kwa kufikiri labda alikuwa anapewa nyoka ale. Kisha Jenerali Jacob akamwambia mwanamke aliyemletea sinia hilo alifunue, na baada ya kulifunua, Kanali Oswald akafumba macho na kugeukia pembeni.

"General... General nini hiki?" Kanali Oswald akauliza kwa kufadhaika sana.

"Ndiyo chakula special kwa ajili yako. Sikuwa na jinsi ila kukupa wewe maana ulisema hukuona mnyama yeyote anayekula nyama wakati unakuja. Nataka unithibitishie kwamba na wewe ni mnyama... hahahahah..." Jenerali Jacob akasema hivyo na kuanza kucheka pamoja na Luteni Jenerali Weisiko.

Kanali Oswald akakitazama tena "chakula" hicho. Kilikuwa ni kichwa kilichokatwa cha mwanaume, na mwanaume huyo alikuwa ndiye yule mwanajeshi ambaye aliendesha gari lile lililokuwa likimsafirisha Lexi usiku wa jana. Pembeni ya kichwa hicho kulikuwa na uume wake uliokatwa, na mipira ya uzazi ikiwa imekatwa na kusambaza damu kwenye sinia hilo. Vyote vikiwa vibichi!

"General..."

"Kula. Nataka ule chochote kati ya hivyo, then mambo mengine yatafuata," Jenerali Jacob akasema.

Kanali Oswald alihisi kuchoka. Alijua alipaswa kula la sivyo cha moto angekiona. Akajitoa akili na kujikaza kiume, kisha akachukua kisu kidogo pembeni na uma, naye akaanza kuikata sehemu ndogo ya sikio kwenye kichwa ili ale, lakini Jenerali Jacob akamzuia.

"Nimekwambia chagua kati ya hivyo ule, sijakwambia ukate. Ukichagua kichwa, ujue unakila chote," Jenerali Jacob akasema.

Aisee!

Wanawake waliokuwa pembeni walihisi vibaya sana kumwelekea Kanali Oswald. Walimwonea huruma. Kanali Oswald akabaki tu kuangalia vitu hivyo mbele yake. Alijiuliza hata walimleta mwanaume huyo huku saa ngapi. Akamtazama Weisiko kidogo, naye akamtolea ishara kwa macho yake kuwa achague na ale. Kanali Oswald akafumba macho na kukaza meno yake, kisha akaweka kisu na uma pembeni, halafu akauchukua uume ule na kuudumbukiza mdomoni!

"Usimeze... tafuna!" Jenerali Jacob akasema kiutulivu.

Kanali Oswald akawa ameweka tango hilo dogo mdomoni huku ametoa macho kimshangao. Akaanza kutafuna huku akijikaza asitapike. Kwachu, kwachu, kwachu, akaendelea kutafuna huku watu hapo ndani wakimwangalia kwa umakini. Wanawake kadhaa walikuwa wameziba macho na midomo wasiamini walichoona. Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko wakaendelea kumwangalia mpaka alipomaliza kutafuna na kumeza, kisha akawa anajitahidi asitapike hata kidogo.

Wawili hao wakaanza kumcheka sana.

"Hahahahaa... mnofu tu..." Jenerali Jacob akasema.

"Mnofu tu," Luteni Jenerali Weisiko akamalizia huku akicheka.

Jenerali Jacob akatoa ishara kwa kiganja chake, kisha chupa kubwa ya wine ikaletwa hapo na kuwekwa mezani.

"Hiyo ilikuwa tamu siyo? Shushia na Hennessey hapo kidogo," akasema Jenerali Jacob, naye Luteni Jenerali Weisiko akacheka.

Kanali Oswald akaichukua chupa hiyo na kuanza kupiga fundo nyingi sana, akijihisi vibaya sana mwilini mwake. Majenerali wakawa wanamcheka tu.

"Safi sana Kanali. Sasa nimeamini unaweza kufanya lolote kwa ajili yangu. Hey, toa hilo sinia, mletee chakula kingine kizuri," Jenerali Jacob akasema.

"No... hap.. hapana. Nahisi kushiba... niko sawa General," Kanali Oswald akasema.

Majenerali wakaangaliana na kucheka pamoja kwa sifa.

Kanali Oswald akabaki tu kupumua kiuchovu utafikiri alikuwa amelishwa tembo mzima. Luteni Jenerali Weisiko akamnyooshea dole gumba kumpongeza, naye Kanali Oswald akatabasamu kinyonge na kunyanyua kidole gumba pia. Jenerali Jacob na Weisiko wakaendelea kula huku wakicheka sana kutokana na kitendo ambacho walikuwa wamemfanyia mwanaume huyo.



★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Ilipita wiki nzima Lexi, Kendrick, Mensah, Victor, na Kevin wakiendelea kutafutwa sana na mapolisi na wanajeshi bila mafanikio. Kanali Oswald, akisaidiwa na Kapteni Erasto na timu ya Luteni Michael, walishindwa kuelewa inawezekana vipi watu hao kujificha kwa umakini mkubwa namna hiyo bila kupatikana, kwa sababu walitumia mbinu nyingi sana ili kufanikiwa lakini zikashindikana. Walikuwa pia wamepata picha ya Isiminzile iliyochorwa na wataalamu baada ya kuuliza hospitalini kule ni nani aliyempeleka Lexi usiku ule pale, hivyo na yeye akawa ameongezwa kwenye kundi hilo lililosakwa.

Kanali Oswald alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba huenda wiki ya pili ingekwisha pia bila kwa yeye kufanikiwa kuwapata, na hiyo haingekuwa nzuri kwake maana alikuwa amepewa wiki mbili tu, la sivyo Jenerali Jacob angemfanya jambo baya sana. Hakuweza kujizuia kumchukia sana Nora, kwa sababu alijua ni yeye ndiye aliyefanya mpaka Lexi akatoroka, lakini asingeweza kumgusa mwanamke huyo kwa kuwa baba yake alimlinda. Hivyo hakuwa na njia nyingine ila kuendeleza msako huo bila kupumzika.

Luteni Michael alikuwa akiendeleza msako huo pia huku akimchunga sana Nora. Alijua kwa njia moja au nyingine mwanamke huyu angemwongoza kumpata tena Lexi, hivyo akawa anafatilia kwa siri mambo mengi aliyoyafanya tokea Lexi alipotoroka.

Nora yeye aliendelea na kazi akiwa peke yake, na kwa sababu alionwa kuwa "msaliti," akawa ameondolewa kwenye shughuli za msako huo, lakini hakuruhusiwa kuondoka jijini, na hivyo akaendelea kutumia tu ofisi ile aliyopewa kwa ajili ya mambo mengine ya kipelelezi. Alikuwa amepoteza matumaini ya kumwona Lexi tena kwa sababu alijua asingejitokeza kwake na kujisababishia hatari. Alijua pia kwamba Kanali na Kapteni walikuwa wakifuatilia nyendo zake, lakini hakuwa na jambo lolote la kuficha kwa hiyo kwa kuendelea kufanya hivyo, aliona walikuwa wakijisumbua tu.

Luteni Jenerali Weisiko alikuwa akifanya tafiti za hali ya juu pia kubaini ni sehemu gani ambako Lexi na Kendrick wangekuwa, kwa sababu alielewa wawili hao kuweza kujificha kwa muda huo wote bila kupatikana mpaka sasa ilimaanisha wana nguvu sana. Lakini kihalisi alikuwa pia anaumia kwa sababu ya kumpoteza Azra, au kama alivyomwita, Mary wake. Alitaka sana kuwa naye tena kwa sababu alimpenda kama alivyompenda binti yake, naye angefanya lolote kumtoa huko walipokuwa wamemweka; akifikiri kwamba walikuwa wamemteka hasa kwa sababu ya Lexi kuwa "dada yake."

★★

Basi, asubuhi ya Alhamisi ya wiki hii Nora alipokuwa kwenye chumba chake cha hoteli akijiandaa ili aelekee ofisini, ujumbe fulani ukaingia kwenye simu yake. Alikuwa tu ndiyo amemaliza kuvaa suti yake ya kike na kuichukua simu yake kuuangalia, lakini akashindwa kabisa kuuelewa. Kwanza, ulikuwa ni ujumbe kutoka Tigo Pesa. Na pia, alishangazwa na uhakika wa ujumbe huu. Yaani ilikuwa ni kama umetumwa kwenye laini hususa ya Tigo, lakini yeye hakuwa na laini ya Tigo, bali alitumia mitandao mingine miwili.

Akaketi kwanza akiiangalia kwa umakini SMS hii. Alipata hisia fulani ni kama alikuwa anapewa taarifa isiyo ya moja kwa moja na mtu fulani.

Ujumbe huu ulisomeka hivi: Ndugu Mteja, endelea kufurahia huduma za Tigo Pesa zilizoboreshwa. Piga*150*01# au tumia App ya Tigo Pesa. Pakua kwa Android: hIGEBIE - zz.LII73mwv5z. Karibu sana.

Nora alitafakari sana ujumbe huu kwa sababu akili yake ilimwambia kuwa alikuwa anaambiwa jambo la siri na mtu fulani ili alifanyie kazi. Ni upesi sana aliwaza kwamba huenda huyu alikuwa ni Lexi aliyemtumia ujumbe huu kwa njia ya fumbo ili autatue na kuweza kuuelewa. Akawaza labda alifanya hivi ili asitambulike alipo, hivyo Nora akaweka simu yake kwenye mfuko wake na kuondoka hapo upesi.

Nje ya ghorofa la hoteli alipoishi, alifika usawa wa gari lake na kupiga jicho la wizi upande mwingine wa barabara, na hapo akaliona gari lile lile ambalo, tokea Lexi alipotoroka, aliliona sana nje hapo. Alijua kabisa kuwa bado alikuwa akifuatiliwa, hivyo kama kawaida yake akaingia tu ndani ya gari na kuanza kuelekea ofisini kwake. Aliendelea kuutafakari ujumbe ule aliotumiwa, na mpango ukawa kuutatua vizuri akishafika ndani ya ofisi yake.

Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akawa amefika. Alifunga mlango wa gari lake huku akiliona gari lile likiingia eneo hilo kutokea upande mwingine wa barabara, naye akalipuuzia na kuelekea jengoni mpaka ofisini kwake. Aliletewa makablasha kadhaa ya kazi mbalimbali na msaidizi wake, Halima, naye akayaweka tu pembeni na kumwomba asiruhusu mtu yeyote kuingia ofisini kwake kwa sababu alihitaji muda wa kuwa mwenyewe. Akatii na kuondoka, kisha Nora akachukua simu yake na kuusoma tena ujumbe ule.

Kama kawaida yake katika masuala ya kutatua mafumbo, alianza kupitia kila jambo aliloona hapo na kuandika pembeni mambo aliyofikiria yana maana fulani. Alikuwa makini sana kutambua ni jambo gani lililokuwa la muhimu zaidi kwenye SMS hiyo, naye akafikia mkataa kwamba ilikuwa ni maneno haya: hIGEBIE - zz.LII73mwv5z. Kwa utafiti wake alitambua kwamba sehemu ya maneno hayo ilipaswa kukaa "link" ya Tigo Pesa App, na siyo hayo. Yalikuwa yameandikwa kwa njia ya kificho cha hali ya juu sana, lakini alielewa kwamba aliyemtumia bila shaka alijua alikuwa na uwezo wa kuyatatua mafumbo hayo, naye akaanza kazi.

Nora aliendelea kutafiti, huku akielewa wazi kwamba simu yake huenda ilikuwa imeunganishwa na wakuu wale wa jeshi kwenye vitengo vyao vya uchunguzi wa kimawasiliano katika suala hili hili la kumfatilia, hivyo kama na wao waliupata ujumbe huu na kuhisi kuna nuksi, basi wangekuwa pia wanajaribu kuutatua. Lakini akajipa matumaini kwamba angeweza kuutatua kabla yao. Alikuwa sahihi kabisa kufikiri hivyo kwa sababu Luteni Michael na timu yake waliupata ujumbe huo na kuanza kuushughulikia kwa sababu waliona kuna jambo limefichika. Kila upande ulikuwa makini.



Muda ulizidi kwenda, naye Nora alijitahidi sana kwa uwezo wake wote kutatua fumbo hili, lakini akashindwa. Mpaka inafika saa 7 mchana bado alikuwa akijitahidi kutatua tu fumbo la kwenye maneno hayo, lakini kila jambo alilojaribu halikufanikiwa. Mpaka akahisi hasira sana na kukunjakunja makaratasi yote na kuyarusha chini kwa nguvu. Maneno hayo yalimaanisha nini? Kila alipohisi kukata tamaa, ni kama kuna kitu fulani kikawa kinaendelea kumsukuma asifanye hivyo na kuendelea kuchimba zaidi. Alitaka sana kuuelewa.

"Lexi... tafadhali nieleweshe... unataka kuniambia nini?"

Nora akajisemea maneno hayo huku akiwa anaangalia sana maandishi yale. Akaanza tena kutafuta majibu kwa bidii mpaka inafika saa 9 alasiri, akiwa hajala chochote, hajapokea simu zozote, wala kuonana na yeyote yule. Alianza kuhisi uchovu mwingi wa kiakili, na hisia za kupoteza matumaini zikamjaa sana. Akihisi kushindwa, akayachukua makaratasi yote aliyokuwa ameyaandikia na kuyarusha chini kwa hasira huku anapiga kelele. Msaidizi wake akawahi na kuingia hapo kukuta vitu vingi vimekaa shaghalabaaghala, huku Nora akiwa anazunguka huku na huko na kiganja kukiweka kwenye paji la uso wake.

"Mheshimiwa... kuna tatizo gani?" Halima akamuuliza.

Nora akabaki tu kimya na kukalia meza yake huku ameinamisha kichwa. Halima akaona aanze tu kuyaokota makaratasi yote hapo chini na kuanza kupangilia vitu vizuri. Lakini wakati alipokuwa ameanza kufanya hivi, Nora akatambua jambo fulani. Alikuwa ameitazama karatasi moja ambayo aliiandikia maneno yale kwa kukuza maandishi, lakini ilikuwa imegeuka, kwa hiyo maneno hayo yakawa juu-chini. Msaidizi wake akaifikia karatasi hiyo na kuichukua.

"Halima subiri!"

Nora akamzuia upesi na kumfata. Halima akawa anamwangalia boss wake kwa umakini. Nora akaikwapua karatasi hiyo na kuyaangalia maneno hayo yakiwa yamegeuzwa, na alichokiona kikaanza kupatana na akili.



Geuza simu yako uyaangalie maneno haya msomaji;
(hIGEBIE - zz.LII73mwv5z)




Nora akapata kutambua sasa kwamba fumbo lake hili lilikuwa limegeuzwa. Akayaandika kwa njia ambayo yalisomeka namna hiyo iliyogeuzwa. Kwa hiyo, akapata vitu hivi; hIGEBIE zikawa namba hizi 3183914 na neno hili "zz.LII73mwv5z" likawa kama hivi "2SAmwELII7.22." Alipolitenganisha na kulichambua vizuri neno hili la mwisho, akapata maneno haya "2 Samweli 17:22," kitu kilichomfanya atambue kuwa alipaswa kusoma mistari fulani ya kwenye Biblia yenye jina la kitabu hicho cha Samweli.

Upesi akamwambia Halima ampishe Ili aendelee na kazi, lakini msaidizi wake huyo akatoka ofisini akiwa amechanganywa sana na mwenendo huu wenye kushangaza wa boss wake kwa kuwa alifanya mambo kama ana kichaa vile. Nora sasa akawa na hamu kubwa ya kutaka kujua mistari hiyo ilisema nini, naye akapitia tafsiri mbalimbali za Biblia ili kuyaona maneno ya mistari hiyo. Akaja kupata maneno fulani yaliyoeleweka kwa njia rahisi.

Kitabu hicho, ambacho ni barua ya pili kwa Samweli, sura ya kumi na saba na mstari wa ishirini na mbili, kilikuwa na maneno haya, "Mara moja Daudi na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka na kuvuka Yordani. Wakati wa mapambazuko, hapakuwa na mtu hata mmoja ambaye hakuwa amevuka Yordani."

Nora akayasoma maneno hayo kwa kurudia mara nyingi, kisha akazichukua namba zile "3183914" na kuanza kuzifanyia utafiti pia, akitafuta ulingano wowote unaohusiana nazo kwenye kompyuta yake. Upesi akatambua kwamba zilikuwa ni namba za Latitudo (Latitude), yaani namba zinazoonyesha ENEO kwa kutaja umbali wake kutokea kwenye ikweta kwa vipimo vya digrii (°), naye akaanza kutafuta ni sehemu ipi ambayo zilihusiana nayo hapa nchini. Eneo lenye Latitudo hii -3°18'39.14" lilikuwa ni sehemu iliyoitwa Ngaramtoni, kule Arusha.

Sasa Nora akafurahi kujua kwamba alikuwa amepewa kama anwani ya eneo la kukutana na mtu huyu aliyeamini kabisa kuwa ni Lexi. Lakini bado akawa anajiuliza maneno yale ya kwenye Biblia yalihusiana vipi na eneo hilo la Ngaramtoni. Kwa hiyo akaanza kuyarudia tena huku akifanya utafiti kuhusu eneo hilo. Kwa akili nzuri ya Nora ya kuchanganua mambo, alipata kuelewa sasa fumbo hili lote kwa ujumla.

Ngaramtoni huko Arusha ndiyo eneo ambalo aliyemtumia ujumbe huu alitaka wakutane. Maneno ya kwenye Biblia yalikuwa na vipengele alivyounganisha kwa ustadi na kuweza kuelewa mahali HUSUSA ambapo wangekutana. Sehemu fulani ilisema "kuonddoka haraka na kuvuka Yordani." Alijua kwenye Biblia huu ulikuwa mto, lakini kwa Ngaramtoni ilikuwa tofauti. Baada ya utafiti alitambua kwamba kuna sehemu huko Ngaramtoni ambayo ilikuwa na kanisa lililoitwa Vuka Yordani - Grace Evangelical Church of Tanzania. Kwa hiyo aliyetaka wakutane alikuwa anamwambia aende eneo hilo "wakati wa mapambazuko," kama mistari ya kwenye Biblia ilivyosema, ikimaanisha aondoke kesho asubuhi na mapema.

Nora alishusha pumzi kwa kuhisi uchovu mwingi sana. Alikuwa ameweza kulitatua fumbo hili ambalo kiukweli lilihitaji akili ya juu sana. Alijua pia kabisa kwamba huyu alikuwa ni Lexi, kwa sababu njia zake za kufanya mambo sikuzote zilikuwa ni tata sana. Kwa hiyo angehitaji kuondoka kesho mapema sana na kuelekea kule, labda hata aende moja kwa moja mpaka ndani ya kanisa hilo au maeneo ya huko na kusubiri; maadamu tu aende. Lakini alijua kutokana na kufuatiliwa sana isingekuwa rahisi, hivyo akaanza kufikiria ni njia gani angetumia ili kuwaponyoka waliomfatilia.

Kwa upande wake Luteni Michael, alikuwa ametafuta mno chanzo cha ujumbe ule uliokuwa umeingia kwenye simu ya Nora lakini hakufanikiwa kukipata. Yeye pia akawa ametambua kwamba bila shaka ni Lexi ndiye aliyeutuma, na kwa sababu bado hakuwa ameweza kuutatua, kufatilia nyendo za Nora lilikuwa ni jambo la muhimu hata zaidi kwa wakati huu, hivyo macho yake yote yangekuwa kwake, ikionekana Nora ndiyo njia kuu iliyobaki ya kumfikisha kwa Lexi.


★★★★


Nora alimaliza mambo yote yaliyohitajika siku hiyo kazini na kuondoka kwenye mida ya saa 2 usiku. Alihisi njaa sana pia kwa sababu ya kutokula kuanzia asubuhi, hivyo akaona aelekee kwenye hoteli nzuri ili apate chakula hapo. Alikuwa anamuwaza sana Lexi. Akili yake yote ilikuwa kwa Lexi. Alikula taratibu huku akifikiria angefanya nini baada ya kukutana naye tena. Lakini wakati akiwa anaendelea kupata chakula, akasikia sauti nyuma yake ikimwita, naye hakugeuka kwa sababu alimjua vizuri sana mwenye sauti hiyo.

"Hujambo binti yangu?"

Ilikuwa ni baba yake, Jenerali Jacob mwenyewe. Nora akasitisha kula na kuweka sura iliyoonyesha wazi kuwa alikerwa sana na uwepo wa baba yake hapo. Hakugeuka kumwangalia, hivyo Jenerali Jacob akatoka nyuma yake na kuketi kwenye kiti cha pembeni kwenye meza hiyo. Alikuwa amevalia kwa njia ya kawaida sana; shati la mikono mifupi lililofunikwa na jaketi kubwa jeusi kwa juu, kofia iliyofunika vizuri kichwa chake, na suruali ya jeans kama raia wa kawaida tu. Akawa anamwangalia mtoto wake kwa upendo, lakini Nora hakumtazama hata kidogo.

"Hakuna hata shikamoo kwa ajili ya mzee wako?" Jenerali Jacob akauliza.

"Utaipeleka wapi?" Nora akasema na kuendelea kula.

"Ahahah... nimekukumbuka pia," Jenerali Jacob akamwambia.

Nora akaendelea tu kula bila kujisumbua kumtazama, yaani alifanya kama vile hakuwa hapo.

"Vipi kazi lakini?" Jacob akauliza.

Nora akabaki kimya.

"Nasikia umetumiwa sana... maombi ya kupandishwa cheo... lakini yote umeyakataa..."

"We kwani unataka nini?"

"Nataka kukuona unatoka hapa ulipojiweka na kuwa sehemu ambayo inakufaa zaidi..."

"Sihitaji... uniamulie kile ambacho kinanifaa zaidi. Haya ni maisha yangu. Nitayaendesha jinsi ninavyotaka..."

"Oh please. Hii act ya kunichukia utaiacha lini? Pamoja na mambo yote ambayo nimefanya, mimi bado ni baba yako. Nina sehemu muhimu kwenye maisha yako, upende usipende. Nikiona jambo fulani halikufai lazima nikusaidie ili...."

"Kama nilivyokwambia... sihitaji msaada wako. Ulionipa kipindi cha nyuma unatosha. Naomba tu uniache... huo utakuwa msaada tosha kwangu," Nora akasema kwa mkazo.

Akataka kunyanyuka, lakini baba yake akamshika mkono wake kwa nguvu kumzuia.

"Kaa chini bado sijamaliza kuongea na wewe!" Jacob akasema kwa sauti ya chini lakini kiukali.

Nora akauvuta mkono wake kwa nguvu akihisi hasira, naye Jenerali Jacob akamwachia.

"Samahani... samahani. Nahitaji kukwambia tu jambo la muhimu. Nisikilize tafadhali," Jenerali Jacob akasema.

Nora akaangalia pembeni akiwa ameudhika.

"Ona... najua unaniona kama mnyama, na sikulaumu kwa sababu mimi... ndiyo ni mnyama. Lakini kamwe usipuuze ukweli wa kwamba ninakupenda kama baba yako... na ninataka kilicho bora kwa..."

"Kama hicho ndiyo ulikuwa unataka kuniambia, unapoteza muda wako na wangu pia. Nahitaji kurudi kwangu kupumzika, kwa hiyo kama hauna jambo la maana la kusema... sitaki kukuona tena," Nora akasema kwa hisia kali.

Jenerali Jacob akashusha pumzi na kukaa sawa. Kisha akaingiza mkono wake kwenye jaketi na kutoa picha fulani kisha kumpatia. Nora akaichukua na kuitazama, na hapo akaweza kumwona Lexi. Akamtazama baba yake kwa umakini.

"Najua ulikuwa na... summer fling na mtu huyu. Na pia naelewa kwamba ulimsaidia kutoroka kutoka kwa wanajeshi usiku ule. Lakini haujui hii ni mbaya kiasi gani. Umejiweka sehemu mbaya sana binti yangu. Kwa sababu hii kuna watu wengi wanaokuwinda... ninahitaji kukulinda masaa 24 ili usipatwe na jambo lolote baya. Unanielewa? Unaweza kuyaongoza maisha yako ndiyo lakini hapo umeangukia pua vibaya mno. Mimi kama Jenerali, ningetakiwa kukuwajibisha vikali kwa ulichofanya, lakini nimekuonyesha fadhili na kuchukulia kisa hicho chote kama... matokeo tu ya blindfolded love. Kwamba hukuwa kwenye akili timamu kwa yale uliyofanya. Mwanamke huyo ni mtu mbaya sana. Na kuwa kwake huru kunaweza kusababisha maafa ya watu wengi zaidi...."

"Kupitia mikono yako, si ndiyo?" Nora akamkatisha.

"Nini?"

"Fikira ya kwamba mwanamke huyu yuko loose, inakuogopesha sana, si ndiyo? Yaani... uko radhi mpaka kupoteza muda wako kuja kwangu kujifanya baba mwenye upendo sana ili tu upate taarifa yoyote kutoka kwangu... ahahah... sikuwahi kufikiria ungekuja kujigeuza kuwa kituko namna hii," Nora akasema.

"Ninaonekana kuwa kituko wakati huu kwa sababu yako. Isingekuwa ya ushenzi wako na huyo malaya sasa hivi ninge...." Jenerali Jacob akaishia hapo.

"Nini? Ungekuwa unafurahia maisha? Usingekuwa na muda mchafu wa kuja kumwona mtoto wako asiye na umuhimu wowote?" Nora akauliza.

Jenerali Jacob akabaki kumtazama tu.

"Najua usingekuwa hapa kama mwanamke huyu hangekuwa na lolote juu yako. Unajitahidi sana kuficha mabaya uliyofanya... lakini huwezi kuyaficha sikuzote. Kwa njia moja au nyingine, itajulikana tu. Mimi sitajali hata kama maisha yangu yakiharibika. Nimefanya kile ambacho moyo wangu umeniambia ni sahihi, na sijutii. Kwa hiyo fanya lolote unalotaka... mimi sijali," Nora akamwambia.

"Unaongea tu we mtoto," Jenerali Jacob akasema.

"Ndiyo, lazima niongee. Nisipokwambia utajua vipi?" Nora akasema.

Kisha akasimama na kumwangalia usoni.

"Uliacha kuwa baba yangu ulipoamua kutanguliza raha badala ya sisi. Kila jambo ambalo nimefanya, nimelifanya kutoka moyoni mwangu, na sijutii kulifanya hata chembe. Narudia tena, sijutii kwa lolote ambalo nimefanya. Na sihitaji ulinzi wako. Nayafurahia maumivu yangu ya kuangukia pua, kwa hiyo cheza mchezo huu kwa njia yako, na mimi nitacheza kwa njia yangu..."

Nora akasema maneno hayo kisha akaanza kuondoka. Jenerali Jacob alihisi hasira sana, lakini pia maneno ya binti yake yalikuwa yamemchoma sana moyoni. Akanyanyuka na kuweka simu yake sikioni baada ya kupigia mtu fulani huku akielekea nje pia.

★★

Nora alifika hotelini kwake akiwa amevurugwa akili sana na baba yake. Hakupenda kabisa ujio wake ule wa ghafla kwa kuwa alichukizwa sana na mambo mengi ambayo baba yake alikuwa ameitendea familia yao. Baada ya kufika kwenye chumba chake alijilaza kwa dakika chache kitandani, kisha akanyanyuka na kuanza kujipanga kuhusiana na safari ya kuelekea Arusha. Alijua kwamba watu waliomfatilia, aidha wa baba yake, au wa Kanali na Kapteni walikuwa nje wakimchunga, hivyo kutoka kwake hapo kungepaswa kuwa kwa akili sana.

Ikiwa imefika saa 5 usiku sasa, aliamua kuondoka hapo usiku huu huu, kwa sababu angehitaji kuhakikisha anawapiga chenga gizani. Njia ya haraka aliyofikiria ilikuwa ni kutoka kwa njia ya kudanganya mwonekano wake (disguise), yaani ajifanye yeye ni mfanyakazi wa hotelini hapo ili aweze kutoka kiurahisi lakini kwa umakini. Akafanikiwa kumwita mfanyakazi mmoja wa hotelini hapo na kumwahidi kumpatia pesa nyingi sana ili amletee sare za kazi za hoteli hii. Alimwambia hata kama ingehitajika aibe, ingekuwa sawa tu.

Lakini mfanyakazi huyu wa hoteli, ambaye alikuwa mwanamke, alimwambia ingekuwa ngumu sana kwa wakati huo kupata sare za ziada, hivyo akampatia za kwake yeye mwenyewe. Nora alikuwa amemwahidi pesa nyingi, na baada ya kupewa sare hizo, akampatia laki 3 na baadhi ya nguo zake ili avae, kisha akamshukuru sana na kumsihi asimwambie yeyote yule kuhusu hilo.

Baada ya mwanamke huyo kuondoka, Nora akazivaa nguo hizo upesi na kujifunga ushungi kama mwislamu, kisha akachukua nguo zake nyingi na kuziweka kitandani. Akatuma ujumbe kwa Asteria kumtakia usiku mwema na kwamba ndiyo anaingia kulala, ili kwa wale waliokuwa wameunganisha mifumo yao kwa simu yake, ionekane kwamba na huu ulikuwa usiku wa kawaida tu kama zote ambazo wamekuwa wakimfatilia. Alipomaliza, akaiacha simu yake hapo, akabeba pesa zilizobaki na kuweka kwenye pochi yake ndogo, kisha akabeba na nguo zile na kutoka nje ya chumba hicho.

Nora alishuka na nguo hizo mpaka kule nje, na mara kwa mara alisemeshwa na watu waliofikiri anafanyia kazi hapo, lakini hakumjibu hata mmoja na kuendelea kusonga tu mbele. Alizibeba usawa wa uso wake, ikionekana kama ni furushi linalopelekwa kutupwa. Baada ya kufika nje ya hoteli aliendelea kuondoka, lakini kwa tukio baya mlinzi mmoja wa nje akamsimamisha. Yaani kutokea aliposimama Nora, watu waliokuwa wakimchunga walikuwa wameegesha magari yao kando tu ya jengo hilo la hoteli.

Mlinzi huyo akamfata Nora na kumuuliza anaenda wapi usiku huo, na kwa haraka Nora akajibu kwamba zamu yake ilikuwa imeisha, lakini kuna mteja hapo kwenye hoteli alikuwa amemwagiza kuzipeleka nguo sehemu fulani ya nje haraka, kwamba kuna mtu alikuwa anazisubiria, kisha angerudi muda siyo mrefu. Hiki kilionekana kuwa kisingizio kisicho na kichwa wala miguu kabisa, lakini mlinzi huyo akakubali na kumwambia awahi upesi sana.

Watu wale waliowekwa kumwangalia Nora hapo walikuwa wakiwatazama wawili hao, bila kumtambua vizuri mwanamke huyo kutokana na njia yake ya kujificha kijanja, kisha akaondoka na kuanza kuelekea upande mwingine wa maeneo hayo. Mmoja wa wanaume wale waliowekwa pale na Kanali Oswald alikuwa anamwambia mwenzake kwamba alihisi huyo mwanamke ana nuksi, lakini mwenzie akasema aache kutamani kila mwanamke anayemwona na akazie fikira kazi yake.

Kwa njia hii Nora akawa amefanikiwa kuwatoroka watu hao, ambao hata kwa kuangalia mahala ambapo simu yake ilikuwa kwa mitambo yao waliendelea kufikiri bado yuko chumbani kwake. Alipotembea mwendo wa zaidi ya dakika 5, akazitupa nguo zake sehemu fulani na kuchukua usafiri wa bodaboda upesi sana ili kuelekea upande tofauti na huo haraka iwezekanavyo. Alimwomba bodaboda ampeleke maeneo yaliyokuwa karibu na stendi ya mabasi ili achukue chumba kwa usiku huo kwenye "lodge" moja, na asubuhi ya kesho angekata tiketi mapema sana ya kuelekea Arusha bila kukawia.

Maisha ya mwanamke huyu yalikuwa yamebadilika kwa uharaka sana kwa sababu ya maamuzi aliyokuwa ameamua kuchukua, yaani, kufuata moyo wake.


★★★★


Siku iliyofuata ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Luteni Michael. Aliwalaumu sana watu wake kwa kumpoteza Nora kizembe. Walimsaka kotekote kwenye maeneo hayo bila mafanikio yoyote.

Baada ya Luteni Michael kuwa wamefanya uchunguzi wa kina, waligundua kwamba Nora alificha mwonekano wake kwa kuvalia kama mfanyakazi wa hapo, hivyo wakambana mfanyakazi yule aliyempatia mavazi yale ya kazi. Lakini yeye alifunguka tu kuhusu kulipwa na mwanamke yule ili afanye yote yale, lakini hakumwambia sababu na sehemu aliyoelekea. Akasema alikuwa na uhitaji wa pesa zile sana ndiyo maana alikubali, hivyo akawaomba sana wasimtendee kwa njia mbaya.

Luteni Michael aliachana naye na kuanza kutumia mbinu mbalimbali ili kujua Nora alielekea wapi. Yaani alihisi ni kama kwenye mchezo huu sikuzote aliyeachwa nyuma ni yeye, wakati yeye ndiye aliyetakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kujua mambo mengi. Taarifa za Nora kuwaponyoka waliokuwa wanamfatilia ziliwafikia Kanali Oswald na Kapteni Erasto pia, ambao hawakufurahishwa na jambo hilo hata kidogo. Lakini Luteni Michael akawaahidi kutoacha mpaka ampate Nora kwa sababu aliamini mwanamke huyo moja kwa moja alikuwa amekwenda sehemu ambayo Lexi alikuwa.


★★★★


Nora hatimaye akawa amefika jijini Arusha. Hii haikuwa mara yake ya kwanza kufika ndani ya jiji hilo, lakini ndiyo ingekuwa mara yake ya kwanza kufika akiwa kama mkimbizi, kwa sababu alijua kuna watu bado walikuwa wanamfatilia. Aliomba sana moyoni mwake kwamba mambo yote aliyofanyia utafiti kuhusu ule ujumbe na kuyabaini yalikuwa sahihi, la sivyo angekata tamaa sana. Hata ijapokuwa kuna sehemu ya moyo wake iliyomhukumu na kumfanya ajione kuwa mjinga kwa mambo haya aliyokuwa akifanya, bado akaamua kufuata moyo wake, na aliamini kabisa moyo wake ungemfikisha kwa Lexi.

Baada ya kuondoka stendi, akiwa na mwonekano tofauti sasa kwa kuvalia baibui nyeusi na ushungi uliofunika vyema kichwa chake, alichukua usafiri ambao ungempeleka mpaka maeneo ya Olmotoni, kisha kutokea hapo angechukua mwingine mpaka Ngaramtoni. Safari ingechukua muda kwa sababu ilikuwa ni kwenye upande mwingine wa jiji hilo, hivyo hakukawia kuondoka hapo upesi.

Maeneo ya Olmotoni baada ya kufika ilikuwa kwenye mida ya saa 11 jioni, naye akatafuta sehemu fulani ili apate chakula kwanza kisha aendelee na safari. Lakini akaona hii huenda ingemfanya akawie, au labda hata kujikamatisha upesi kwa sababu hakuwa na uhakika ikiwa mpaka hapo hakukuwa na mtu aliyemfuatilia. Hivyo akaamua kuelekea upande fulani na kujibanza nyuma ya jengo dogo, kisha akaanza kuangalia kule alikotokea. Alikuwa akitafuta kuona ikiwa kuna mtu au watu wangemfata kwa nyuma, lakini akashukuru Mungu kwa kutoona jambo lolote la namna hiyo.

Maamuzi ya haraka baada ya hapo ikawa ni kuchukua tu usafiri na kuondoka, hiyo ikimaanisha asingekula hata kidogo. Akapanda daladala iliyoelekea kule na kuendelea kuomba kumkuta Lexi huko Ngaramtoni. Alifika huko baada ya dakika kadhaa na kuanza kuelekea kule kulikokuwa na kanisa la Vuka Yordani. Hakuwa na muda wa kuangalia watu wala vitu vya eneo hilo, alikazia fikira kufika pale alipohitaji.

Muda si muda akawa ameliona jengo la kanisa lile, naye akaanza kusogea mpaka eneo lilipokuwepo. Lilikuwa jengo kubwa, na eneo lililozunguka hapo lilikuwa na watu wengi waliofanya shughuli za hapa na pale, kutia ndani masoko madogo madogo na maduka ya bidhaa mbalimbali. Akajiuliza ikiwa alitakiwa kuingia ndani ya kanisa lile, lakini akatulia kwanza kutafakari. Alikumbuka maneno ya andiko lile la Biblia, kwamba "Daudi na watu wote wakaondoka na KUVUKA Yordani," hivyo akafikiria huenda alipaswa "kulivuka" kanisa hilo na siyo kuingia ndani yake.

Nora akaendelea kutembea, akiwa anatazama huku na kule ili kuona kama angemwona mtu aliyemtarajia. Akalipita kanisa hilo na kusimama usawa wa mti fulani mdogo ambao ulikaribiana na barabara ya magari yaliyokuwa yanapita huku na huko. Akaliangalia tena kanisa lile, naye bado akawa hajaona jambo lolote lenye kuvuta uangalifu. Alipopeleka macho yake upande mwingine wa barabara, aliona bango jeupe, likiwa limeandikwa "DAUDI SHOP," na kwa chini mshale ulioelekeza upande wa kushoto ambao ndipo hilo duka ilikuwepo.

Kwa kukumbuka kwamba jina la Daudi lilikuwepo kwenye mistari ile ya Biblia, Nora akatazama upande huo ambapo mshale ulielekeza, na macho yake yakatulia sehemu moja tu. Ilikuwa ni pembezoni mwa jengo kubwa kiasi ambalo ndiyo lilikuwa na duka hilo, na hapo akamwona Lexi akiwa amesimama karibu na ukuta huku anamtazama!



★★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA AROBAINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Wawili hawa waliangaliana sana kwa umbali huo, huku mara kwa mara magari yaliyopita barabarani yakiwazibia utizami huu, lakini bado wakaendelea tu kuangaliana. Nora alihisi faraja kubwa sana moyoni mwake baada ya kumwona Lexi. Mapigo yake ya moyo yalidunda kwa nguvu sana, akihisi ni kama alikuwa amepata ushindi mkubwa mno.

Kutokea alipokuwa amesimama, Lexi akamwonyesha Nora kwa ishara ya kichwa kuwa amfate hapo, naye Nora akaanza kwenda. Alivuka barabara na kuanza kujongea taratibu mpaka sehemu aliyosimama. Lexi alikuwa amevaa sweta zito jeusi lenye sehemu ya kufunika kichwa chake (hood), na suruali ya kardet pamoja na mabuti ya rangi ya kaki; akionekana kama mwanaume. Miwani nyeusi machoni ilisaidia pia kutofanya atambulike kwa urahisi. Nora akamfikia karibu zaidi na kusimama mbele yake, akiwa anamwangalia kwa hisia sana. Kwa ukaribu huo, Lexi akaishusha miwani yake.

"Umenisumbua sana," Nora akasema kwa sauti tulivu.

Lexi akatabasamu na kujinyooshea kidole kwenye shavu lake.

"Bado nina alama ya kofi ulilonipiga, kwa hiyo chukulia na wewe hiyo ilikuwa adhabu yako," Lexi akatania.

"Ahah... unajua nilipaswa kufanya vile ili wasihisi lolote..."

"Yeah... I know..."

Wawili hawa wakaanza kuangaliana kwa hisia tena, kisha Lexi akamkumbatia Nora taratibu. Nora akafumba macho na kuubana vyema mwili wa Lexi pia, akihisi amani sana ndani yake. Alikuwa na mambo mengi aliyotaka sana kuongea naye pia, kwa hiyo kumpata hatimaye kulimfariji sana. Wakaachiana taratibu, naye Lexi akaishika hijab ambayo Nora alikuwa amevaa huku akitabasamu. Nora akacheka kidogo kwa haya.

"Well... niliona ni bora zaidi... kujiweka katika hali ambayo isingefanya nitambulike kirahisi," Nora akasema.

"I know. Hongera kwa ku-solve ile puzzle," Lexi akamwambia.

"Asante. Ilikuwa ngumu kweli nilihitaji muujiza..."

"Ahahah... nilijua ungeweza tu. Okay... twende sasa. Hatuwezi kukaa hapa kwa muda mrefu," Lexi akamwambia na kuvaa miwani yake.

"Tunaenda wapi?" Nora akauliza.

"Sehemu ambayo hawatatupata," Lexi akajibu.

Kisha wakaanza kuondoka hapo huku Lexi akimwongoza kwa kumshika mkono. Walikuwa kama wapendanao fulani hivi, na kwa wengi ambao waliwaangalia hawakuwakazia sana fikira kwa kuwa waliwaona kama marafiki au ndugu wa karibu, ijapokuwa baadhi ya waliokisia kwamba walipendana waliwashangaa kwa kiasi fulani kutokana na wote kuwa wanawake. Lakini Lexi na Nora walipuuzia mambo yote ya pembeni na kukazia tu fikira kule walikokuwa wanakwenda.

Waliifikia pikipiki moja, ambayo ilikuwa ni ya Lexi, naye Nora alipendezwa sana na muundo wake. Ilikuwa nyeusi na yenye sehemu ya kukalia iliyoinuka kutokea katikati, hivyo baada ya Lexi kuvaa 'helmet,' kuvaa 'gloves,' na kupanda, Nora akakaa nyuma yake na kufanya awe kwa juu kiasi. Lexi alikaa kama ameinama kuelekea sehemu za kushikia, na baada ya hapo akaiwasha na kuingia barabarani. Alikuwa amempa Nora helmet nyeusi pia ili avae, na zote zilifunika nyuso zao vizuri.

Njia ya barabara ya lami waliitumia kwa dakika chache, kisha Lexi akaiingiza pikipiki kwenye barabara ya changarawe na kuanza kuelekea eneo lililokuwa na mashamba na miti mingi. Hakukuwa na nyumba nyingi sana huku lakini makazi kwa watu kadhaa yalikuwepo; hasa wakulima na wafugaji. Nora aliweza kuona nguzo kadhaa za umeme pia, ikionyesha ni eneo lililokuwa likifanyiwa maendeleo pia.

Kisha ndani ya dakika kadhaa wakafika usawa wa nyumba fulani iliyozungukwa na uzio wenye ulinzi wa chuma za umeme kwa juu. Ilionekana kuwa kubwa kutokea kwa nje; Nora aliona geti jeusi uzioni na bati la rangi nyekundu kule juu ya nyumba hii. Lexi akatoa ishara fulani kwa vidole vyake ambayo ilimchanganya kiasi Nora, na baada ya hapo geti likaanza kujifungua lenyewe. Pikipiki ikaelekea mpaka ndani na kusimama, huku geti likijirudishia lenyewe tena. Walifika mbele kidogo na kusimama sehemu nyingine ambapo kulikuwa na geti tena, nalo likajifungua na wao kupita, kisha likajifunga tena. Wawili hawa wakashuka baada ya Lexi kuisimamisha pikipiki tuli, naye Nora akavua helmet huku akitazama mazingira ya hapo.

Nyumba hii ilikuwa kubwa, pana yaani, iliyojengwa kwa mchanganyiko wa kuta za aina fulani ya shaba, mawe makubwa pembeni, na vioo vizito vilivyoonyesha sehemu fulani ya ndani ya nyumba mwanzoni. Kutokea kule nje kabisa kabla hawajaingia, Nora hakuwa ametambua kwamba ilikuwa ya ghorofa pia, kitu kilichofanya ionekane kuwa kubwa sana ukiwa upande wa ndani.

Sehemu hii waliyokuwa wameegeshea pikipiki, kulikuwa na gari nne; pickup ya Ford Ranger XLT, Toyota Prado Land cruiser TX-L, Toyota Camry, na Ford Edge SEL SUV, zote zikiwa za rangi nyeusi. Pembeni kidogo na magari hayo kulikuwa na gari lingine la kifahari, aina ya BMW i8 2014, naye Nora akamwangalia Lexi na kumwonyeshea kwa kidole huku anatabasamu. Lexi akatabasamu pia na kutikisa kichwa chake kwa shauku.

Ardhi yote ya eneo la hapo ilikuwa imejengewa mawe kwa mpangilio mzuri, na kuelekea sehemu ya kuingilia kwenye nyumba ile zilikuwa ngazi pana za vigae vyeupe. Pembezoni kidogo kabla ya kuzifikia ngazi hizo kulikuwa na jengo dogo jeupe ambalo kwa kukisia Nora aliwaza lingekuwa la vifaa vilivyotunzwa kwa ajili ya magari au mambo mengine, lakini hiyo ndiyo ilikuwa nyumba ya mnyama wa Lexi, yaani Zelda. Kulikuwa na miti pembezoni mwa kuta za uzio ambayo kwa kiasi fulani ilichangia kuficha mwonekano huu wa eneo la ndani mtu akipatazama akiwa huko nje.

Tokea mwanzo, hii ndiyo ilikuwa sehemu ya maficho ya Mess Makers, a.k.a "chini."

Nora alipendezwa na mpangilio mzuri wa nyumba hii, naye Lexi akawa anamtazama tu akiona jinsi mwanamke huyu alivyoangaza huku na kule. Kisha akamwambia amfuate kuelekea kule ndani sasa. Nora alijiuliza Lexi aliweza vipi kujenga nyumba hii yote, na hata kama hakuijenga, aliweza vipi kuwa sehemu kama hii na kushindikana kumkamata kwa wale waliokuwa wanamtafuta. Alijua mengi ya maswali aliyokuwa nayo yangejibiwa tu kwa kuwa sasa walikuwa pamoja, hivyo akaendelea tu kumfuata.

Baada ya kuingia ndani ya nyumba hii, Lexi alimwongoza upande wa mbele zaidi mpaka kwenye mlango fulani wa kioo kinene, kisha wakaingia humo pamoja. Ilikuwa ni sehemu yenye kupendeza, vitu vingi vikiwa vya gharama sana. Kuanzia makanyagio, masofa, mapazia makubwa, meza nene ya kioo, TV pana sana ukutani kama dirisha kubwa, friji, sehemu iliyojengewa kabati za ukutani za kutunzia vyombo na shelf ndefu yenye vinywaji, na mambo MENGI sana yalifanya ionekane kuwa nyumba kwa ajili ya mtu mwenye pesa kupita maelezo. Nora akawaza huenda labda sehemu ya zile trilioni 20 walizoiba ndiyo zilitumika kuijenga.

Kupita hapo kuelekea mbele zaidi ilikuwa ni sehemu pana ambayo Nora angeweza kuona kitanda kikubwa sana kilichofunikwa na mablanketi meupe na matizo, kabati kubwa pia, vifaa vingi vya kutumia kwa ajili ya michezo na mlango mwingine wa kioo ambao bila shaka uliongoza kwenye bafu na choo cha kisasa. Rangi mbalimbali zilipendezesha kuta za ndani pamoja na picha kubwa za kuchorwa. Mambo mengi hapo yalipangiliwa kwa mtindo yenye utofauti ambao ni kama Nora hakuwahi kuona, ijapokuwa aliwahi kuona mambo mengi sana.

"Karibu," Lexi akamwambia Nora.

"Asante," Nora akajibu.

Wakaangaliana sana kwa sekunde chache, kisha Lexi akamwambia aketi ili apumzike. Nora akakaa na kuanza kuuvua ushungi ule kichwani kwake, akiziachia vizuri nywele alizosukwa na Asteria, naye Lexi akafata chakula fulani kizuri sana kilichotengenezwa kwa ustadi, kisha akakiweka mezani na kumletea maji ili amnawishe mikono. Wakati Lexi anamnawisha, akatambua Nora alikuwa anatabasamu sana.

"Vipi?" Lexi akauliza.

"Nothing," Nora akasema.

"Niambie bwana..."

"Ahah... Kuna... sehemu ya kunawia pale... kwa nini umeamua kuninawisha namna hii?" Nora akauliza.

"Ooh... ahahah... nimependa tu. Nataka kuku...fanyia vitu," Lexi akamwambia.

Nora akatabasamu kwa hisia, naye Lexi akatabasamu na kuweka chini chombo chenye maji yale aliyonawia Nora. Kisha akaketi karibu yake na kuanza kumwekea vyakula. Nora alihisi furaha sana, na kihalisi hakujua ni kwa nini ukitegemea na matatizo waliyokuwa nayo. Ilikuwa ni kama Lexi alitaka kumsahaulisha mambo mengine kwanza ili wafurahie kurudiana kwao, hivyo naye akaona aruhusu hilo. Lexi akaendelea kumwekea vyakula mbalimbali na kumsogezea sahani.

"Ahahah... Lexi ume... umenijazia hivyo vyote kweli, si nitapasuka tumbo?" Nora akasema.

"Ndo' nachotaka. Najua una njaa, ko' kula mpaka lipasuke," Lexi akamwambia.

"Unajuaje nina njaa? Je kama nilikuwa nimeshakula?"

"Aa wapi! Nilikuwa nasikia jinsi tumbo lako linavyounguruma kwa nguvu kuliko hata pikipiki," Lexi akamtania.

"Ahahah... haikuwa mimi," Nora akakataa.

"Kweli?"

"Yeah."

"Basi labda nimekosea. Lakini najua haujala, so please... enjoy," Lexi akamwambia.

Nora akakubali, kisha akaanza kula taratibu. Lexi pia alikuwa akila pamoja naye, na Nora angemwangalia sana kwa kujihisi vizuri kuwa karibu yake.

"Unajua akili yako huwa inanishangaza sana," Nora akasema wakiwa bado wanaendelea kula.

"Kwa nini?"

"Uliwezaje... yaani... mara Biblia, mara namba za Latitudo...halafu unageuza kwa juu chini..."

Lexi akawa anacheka.

"Unatoa wapi njia hizo za kufanya mambo?" Nora akauliza.

"Ni utundu mwingi tu. Lakini pia natumia njia za namna hiyo kwa sababu mimi ni mpenzi wa movie," Lexi akasema.

"Mmmm... kwa hiyo unawaiga wakina Dwayne Johnson?"

"Ahahah... akina hao hao..."

"Okay. Kwa hiyo... uko hapa mwenyewe, au?"

"Hapana. Niko na wengine."

"Wako wapi?"

"Mhm... wapo. Unataka kuwasalimia?"

"Ahahahahah... sijui kiukweli maana nafikiri hawajafurahi sana wewe kunileta hapa..."

"Kwa nini unafikiri hivyo?"

Nora akabaki kumwangalia tu machoni.

"Usijali. Wanajua uko hapa. Mtaonana tu. Nilikuwa nataka kwanza upumzike, ule, tuongee..."

Nora akaendelea kumwangalia tu huku akitabasamu kwa mbali. Lexi akachukua nyama ndogo na kumlisha, naye Nora akaila huku anachekea kwa chini.

"Nini?" Lexi akauliza.

Nora akatikisa kichwa kuonyesha hakuna kitu. Lexi akatabasamu na kuendelea kula pia.

"Kwa hiyo wenzako wote wako hapa?" Nora akauliza.

Lexi akatikisa kichwa kukubali.

"Kutia ndani na... Kendrick Jabari?" Nora akauliza tena.

Lexi akamtazama machoni kwa umakini.

"Ndiyo..."

Nora akashtushwa na sauti hiyo na kugeuka nyuma. Kutokea kwenye mlango ule wa kioo wa kuingilia ndani hapo, aliweza kumwona Kendrick mwenyewe akiwa amesimama huku anamwangalia pia.

Nora akasimama kwa kuwa alihisi wasiwasi wa aina fulani hivi, naye Lexi akasimama pia huku akimwangalia. Kendrick akaanza kutembea polepole akiwaelekea wawili hao, na alikuwa amevaa nguo za kawaida tu kwa mtu aliyetulia nyumbani. Akafika mbele yake na kumwangalia Nora usoni kwa umakini sana.

"Nora... mtoto wa Jacob Rweyemamu..." Kendrick akasema kwa uzito.

Nora na Lexi wote walikuwa wanamtazama mwanaume huyu kwa umakini sana.

"Za safari?" Kendrick akamuuliza.

Nora akabaki kimya tu.

Kendrick akatabasamu kidogo, kisha akasema, "Nakuangalia sana na ninayemwona ni baba yako tu. Naweza kusema wewe ni reminder nzuri sana ya mambo yote mabaya ambayo amefanya."

"Uncle..." Lexi akaita kwa sauti ya chini, kama kumzuia.

"Samahani, I can't help it. Nafahamu kwamba wewe ni mtu unayejua mambo mengi, kwa hiyo hakuna haja ya kuanza kurudia mambo yaliyopita. Natumaini yale yote ambayo Lexi anayaona ndani yako ni ya kweli, kwa sababu ukipindisha tu njia yako kutugeuka... nitakuua mimi mwenyewe... kifo kibaya sana," Kendrick akasema kwa uzito.

Nora alikuwa anamwangalia kwa ujasiri, naye Lexi alijisikia vibaya kutokana na jinsi Kendrick alivyomsemesha Nora. Kisha Kendrick akatoa sura ya mkazo na kuachia tabasamu.

"Karibu. Naelewa kuanzia sasa umewekewa target nyuma yako ndiyo maana Lexi ameamua kukulinda. Msaada mdogo uliompatia ili aweze kutoka mikononi mwa baba yako... tunauthamini. Hapa ndiyo sehemu ambayo utakuwa salama, kama tu hautaingiza propaganda za washenzi wenzio..."

"Uncle..." Lexi akaita tena kwa njia ya kuudhika.

"Oh sorry. Force of habit hhmhhm... Lakini Lexi anakuamini, so am down too kwa sababu hiyo. But kumbuka kila kitu nilichosema... I mean it," Kendrick akasema.

Nora akaendelea tu kumtazama mwanaume huyu kwa umakini, kwa sababu hata yeye hakumwamini, hasa ukitegemea alijua kuhusu yeye kutaka kumuua kipindi cha nyuma.

"Hello, hellooow..."

Nora akaangalia mlangoni baada ya kusikia sauti hiyo na kumwona mwanamke fulani akiingia. Alikuwa ni LaKeisha, naye alifuatwa nyuma na Mensah, Kevin, Victor, pamoja na Torres. LaKeisha alikuwa amevaa kiblauzi kilichoishia mbavuni, yaani tumbo lake lilikuwa nje, na kikaptura cha jeans chenye kuishia sehemu ya juu kabisa ya mapaja yake iliyofanya mashavu ya kalio lake yaonekane kidogo. Alikuwa anatembea kwa kunesa na kumpita Kendrick mpaka karibu kabisa na uso wa Nora. Nora akawa anamwangalia kwa kutopendezwa naye.

"Mambo vipi?"

LaKeisha akamuuliza hivyo, akiwa kama anataka kumbusu mdomoni kibabe. Lexi akawa anamwangalia tu, naye Nora alikerwa naye haraka sana, lakini akabaki kimya tu.

"Unanukia kama pussy iliyowekewa vanilla," LaKeisha akasema kwa kejeli.

Mensah na Victor wakachekea kwa chini, naye Torres akatabasamu.

"Keish that's enough... leave her alone (Keish.. inatosha.. mwache)," Lexi akamwambia.

"Oh what, si ndo' namkaribisha? Nataka kuona what this bitch is made of... ndo' part ya kujuana," LaKeisha akasema huku anazungusha uso wake karibu kabisa na wa Nora.

"Mwache bwana. Atakugonga huyo, we msumbue sasa," Victor akamwambia LaKeisha.

"Nitapenda sana hivyo. Maana huyu ndiyo alisababisha Kev akakamatwa, Oscar akaenda, na Lexi nusu afe, kwo' kuziruka naye itanipa furaha sana. Sijui ametumia juju gani kumroga mpaka kamleta hapa. Si ungetumia hiyo hiyo juju kumleta na baba yako huku? Huna idea ni jinsi gani tungekushukuru sana kutupa chance ya kumchinja mbele yako," LaKeisha akasema.

Nora akamwangalia kwa hasira sana.

"LaKeish!" Lexi akamwambia kiukali kidogo.

"Kama unataka kuziruka nami, twende pale nje," Nora akamwambia kwa ujasiri.

Wanawake hawa wakawa wanatazamana kwa hisia kali. Kendrick akatabasamu kidogo.

"Hiyo itakuwa show kali sana. Lakini huu siyo muda wa kuanza kurushiana vyupi warembo..." Kendrick akasema.

Wanaume wote hapo wakacheka, naye LaKeisha akatabasamu.

"Noraaa... jisikie uko nyumbani. Lexi atakuonyesha mandhari ya hapa. Utaipenda," Kendrick akasema, kisha akaanza kuondoka hapo.

LaKeisha bado alikuwa karibu na uso wa Nora akimwangalia kibabe, hivyo Lexi akaja katikati yao na kuwatenganisha. Torres akatoka alipokuwa amesimama na kumsogelea Nora huku akiwa anatabasamu.

"ACP Nora! Habari? Naitwa Torres. Nafurahi sana kukutana nawe. Nakujua tokea Marekani. ila sidhani kama unanikumbuka maana... anyway, karibu sana. Umefanya addition nzuri kwenye timu yetu, najua utakuwa msaada mkubwa. Napenda sana akili yako ya kuchanganua na kuchanganua...."

Nora akamtazama Lexi kimaswali kiasi kwa kushangazwa na jinsi ambavyo Torres alimwongelesha kirafiki sana, naye Lexi akatabasamu kidogo.

"....nilipenda sana aisee, yaani pini ukaificha kwenye nyama ili Lexi atoroke! I mean, who does that with the Captain and Colonel around? Jasiri sana dada! Halafu hata wakati ule ulipofanikiwa kupiga trace za Kevin, which I gotta say was absolute genius, kiukweli kuanzia hapo ndiyo, ndiyo, ndiyo nilijua...."

"Basi inatosha mwishowe ukate ulimi! Amekuelewa," Kevin akamkatisha.

Torres akabaki kutabasamu tu kwa shauku, naye Nora akabasamu kwa mbali.

"Aam Nora... huyu ni Torres. Huyo ni Victor, Mensah, Kevin, na LaKeisha," Lexi akawatambulisha.

Wengine wakamsalimu vizuri, isipokuwa Kevin na LaKeisha.

"Mimi tayari ananijua, alihakikisha nakamatwa na wenzake. Niaje?" Kevin akasema.

Nora hakumjibu, bali akawa anamwangalia tu LaKeisha.

LaKeisha akamshusha na kumpandisha, kisha akaelekea upande wenye friji na kutoa chupa kubwa ya wine.

"Tunajua umechoka, kwa hiyo pumzika kidogo. Lexi atakupa drill nzima. Ngoja tuone kama utaweza kweli kazi," Victor akasema.

Nora akamwangalia Lexi kimaswali, akijiuliza ni kazi gani hiyo.

"Kwa nini unachukua wine yangu, za kwako zimeisha?" Lexi akamuuliza LaKeisha.

LaKeisha akamfata Lexi na kumpiga kidogo kwa kiganja shavuni, kisha akasema, "Finders keepers."

Mwanamke huyu akamwangalia Nora kikejeli, kisha akamshika mkono Torres na kuanza kumvuta ili waondoke. Torres akampungia mkono Nora kumuaga huku akivutwa kwa lazima, naye Nora akampa tabasamu la mbali. Victor, Mensah na Kevin wakaondoka pia, wakiwaacha Nora na Lexi hapo. Nora akashusha pumzi kutuliza hisia zake na kumwangalia Lexi.

"Samahani kuhusu hao. Wana njia fulani ya kukera sana," Lexi akasema.

Nora akaendelea tu kumtazama.

"Are you okay?" Lexi akamuuliza.

Nora akatikisa kichwa kukubali.

"Usim-mind sana LaKeisha, ndo' alivyo," Lexi akasema.

"Nilikuwa natamani nimpige kichwa cha pua!" Nora akasema.

"Ahahah... yeah najua. Mtapatana sana nyie wawili," Lexi akasema.

Nora akatabasamu kidogo.

"Ungependa kujimwagia?" Lexi akauliza.

"Ndiyo, ningependa," Nora akajibu.

"Okay. Come on..."

Lexi akamwongoza kuelekea upande ule wenye kitanda, kisha akamwelekeza bafu na kusema angekuta mambo yote anayohitaji humo, pia kwamba akimaliza kujisafisha atamkuta tu hapo, hivyo ajisikie huru. Nora akakubali na kuelekea ndani kule kuweza kuoga. Alihitaji sana pumziko kwa sababu alijua mambo mengi sana yenye kutatiza yangefuata baada ya wakati huu ulioonekana kuwa mzuri mno.

Nora aliwaza kule alikotoka hali ilikuwa vipi sasa hivi, na ingewachukua muda mrefu kiasi gani wanajeshi na mapolisi kujua alikokuwa. Lakini alimtumaini sana Lexi, akijua kwamba ijapokuwa wengine walimwona Lexi kuwa mbaya, kuna sababu fulani iliyomchochea kufanya mambo aliyofanya, na hasa kwa kuwa ilimhusu na baba yake pia, Jenerali Jacob. Alitaka kujua ukweli wote kutoka kwa Lexi ili aweze kuona kama kweli kuwa upande wake lilikuwa jambo sahihi, na siyo tu kwa sababu alifuata moyo wake.

Kufikia wakati alipokuwa amemaliza kujimwagia maji, giza lilikuwa limeingia, naye akatoka akiwa amevalia taulo yenye muundo kama wa koti refu, aliyoifunga kwa mikanda yake kiunoni, na kichwani kwake alijifuta maji kwa taulo nyingine ndogo. Nywele zake za kusukwa alizibana kwa nyuma, zikiwa laini zaidi kutokana na kulowana. Alikuta nguo fulani kitandani, T-shirt ya kike nyeusi yenye mikono mirefu na suruali nyeupe ya jeans, bila shaka Lexi akiwa ameziweka hapo kwa ajili yake.

Akatazama upande ule wa "sebule" na kumwona Lexi akiwa anasoma mambo fulani kwenye simu, naye akatabasamu kidogo. Lexi akageukia upande wa Nora na kumwona hapo, naye akatabasamu pia na kusimama, kisha akamwonyesha kwa ishara ya nyusi kumuuliza 'vipi?' Nora akafanya kwa ishara ya kichwa kuwa amfate, naye Lexi akatii na kwenda. Alipofika karibu yake, akaanza kumwangalia kwa hisia sana, akipenda mwonekano wake akiwa na nywele zilizolowana.

"Mbona unaniangalia hivyo?" Nora akauliza.

"Aam... nothing," Lexi akasema.

Nora akacheka kidogo.

"Ungependa nikupishe?" Lexi akauliza.

"Uende wapi?"

"Namaanisha... ikiwa unahitaji kuvaa ili... naweza tu kutoka.... kama utaona siyo sahihi mimi kuwa hapa..."

"Kwa nini isiwe sahihi?" Nora akauliza kichokozi.

Lexi akatabasamu na kuuliza, "Ungependa nikae?"

Nora akamsogelea karibu na kusema, "Ningependa kujua ukweli Lexi. Kila kitu."

Lexi akamtazama machoni kwa umakini, kisha akasema, "Nilikuwa nimepanga kukwambia kesho, ili upumzike kwa leo."

"Hapana. Just tell me everything now. Ninahitaji sana kuelewa kila kitu Lexi... please," Nora akamwomba.

Lexi alipokuwa anatafakari cha kusema, mlango wa kuingilia ndani hapo ukagongwa, naye akageuka na kumwona mtu kwa nje. Akamwambia Nora avae kwanza, kisha amfate, nao wangeongea baadae. Akatoka hapo na kumwacha Nora akiwa anamtazama sana, kisha mwanamke huyu akaanza kujitengeneza vizuri na kuvaa nguo zile alizopewa. Akatoka upande huo wa chumba na kuelekea mpaka Lexi alipokuwa, akimkuta na mwanaume mwingine ambaye hakuwa mgeni kabisa kwa Nora.

"Nora... huyu ni Isiminzile. Isiminzile, huyu ndiyo Nora," Lexi akawatambulisha.

"Habari yako dada?" Isiminzile akamsalimu Nora huku akimpa mkono.

Nora akampa mkono pia na kusema, "Ni nzuri tu. Nakufahamu Isiminzile. Nafurahi kukutana nawe."

Isiminzile akaweka uso wenye maswali kiasi.

"Unamfahamu?" Lexi akauliza.

"Ndiyo. Haikuchukua muda mrefu kwa akina Michael kupata utambulisho wake kuwa alikusaidia ule usiku, kwa hiyo na yeye anafatiliwa..."

"Oooh sawa..." Lexi akasema.

"Anajulikana kama mchumba wako pia," Nora akasema.

Lexi akacheka.

"Ahahah... yeah tulifekisha hilo siku hiyo. Nafurahi kukutana nawe pia Nora," Isiminzile akamwambia.

"Isiminzile nilisoma naye chuo. Ilikuwa kama muujiza tu tukakutana usiku huo," Lexi akasema.

"Chuo... wapi... Ghana au?" Nora akauliza.

"Hapana, huku huku. Enzi zile za Demba Group," Isiminzile akasema.

"Okay..." Nora akasema.

"Yeah, kwa hiyo sasa hivi inabidi akae nasi maana...."

"Lexi!" LaKeisha akaingia ghafla na kumkatisha.

"What's up?" Lexi akauliza.

"Let's go, there's trouble (twende kuna shida)," LaKeisha akasema na kuondoka upesi.

Wengine wakamwangalia Lexi kimaswali.

"Aam... nisubirieni, nakuja," Lexi akasema na kuondoka pia.

Lexi akawaacha wawili hao wakiwa wanajiuliza tatizo lingekuwa ni nini. Akaenda mpaka kule chini, naye akawakuta wenzake wote wakiwa hapo tayari, usawa wa kompyuta za Torres. Aliposogea karibu na kuuliza shida ni nini, akaonyeshwa kwenye kompyuta hizo jambo fulani lililomshtua.

Zilikuwa ni video zilizoonyesha kamera za nje ya uzio wa nyumba yao (CCTV camera), na hapo aliweza kuona magari matano meusi, ya aina moja, na watu fulani walioshikilia mabunduki, wakionekana kama majasusi fulani hivi. Walikuwa wanazunguka-zunguka hapo, na mmoja wao akasogea karibu na usawa wa geti na kubonyeza kifaa kama kengele, lakini kinachopaswa kutumiwa kwa ajili ya kuongea. Yaani kama mtu anataka kuingia, basi anabonyeza halafu anaongea, na walio ndani wanamjibu. Mwanaume aliyekibonyeza akaanza kuongea, akisema wao ni shirika la ulinzi na walikuwa hapo kufanya uchunguzi, hivyo wenyeji wafungue geti kuwaruhusu waingie ndani ya dakika tano.

Iliwashangaza sana Mess Makers kuhusu ni jinsi gani watu hao walikuwa wamefika hapo muda huo, tena wakiwa tayari kabisa kimapambano. LaKeisha na Kevin wakaanza kusema bila shaka ni Nora ndiye aliyewaleta, na ilikuwa ni upuuzi kwa Lexi kufikiri kwamba wangemwamini mwanamke huyo. Lexi akaangaliana na Kendrick kwa umakini sana, kwa njia iliyoonyesha walikuwa wanajiuliza wangefanya nini.



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom