Elton Tonny
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 396
- 2,976
- Thread starter
- #261
FOR YOU
Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Siku iliyofuata, Nora aliamka asubuhi ya alfajiri sana na kukuta Lexi akiwa bado amelala pembeni yake kwenye kitanda chao. Giza hafifu lenye kupambana na mwanga wa taa za nje ya jengo hili ulifanya amwone usoni vyema, naye akatabasamu kwa hisia sana. Wawili hawa walikuwa wametumia muda wao vizuri siku iliyopita baada ya kushirikiana na watu wa kundi lake Lexi kuipangilia mipango yao ya kuwasaidia wanyonge. Walicheza pamoja michezo fulani ya kompyuta, waliangalia filamu pamoja, na kujiburudisha kwa kupiga vileo mbalimbali ambavyo vilikuwepo hapo; vingi ambavyo Nora hata hakuwahi kunywa. Kwa hiyo walijikuta wakidondokea tu kitandani na usingizi kuwachukua, mpaka muda huu ambao Nora sasa akawa ameamka.
Akamsogelea Lexi karibu zaidi, naye akawa anautazama uso wake kwa upendezi. Alimaanisha alichomwambia aliposema kwamba alipenda sana kumwona anapofurahi, na kumbukumbu za jinsi walivyojifurahisha siku ya jana zilimfanya atamani maisha yao yangeendelea tu kuwa namna hii, bila kuwaza kuhusu mipango ya visasi. Akawa anapitisha kiganja chake kwenye shingo ya Lexi, taratibu sana, kisha akakilaza kichwa chake kwenye kifua chake. Akaendelea kukilaza hapo kwa dakika kadhaa mpaka alipoanza kuhisi kwamba Lexi alikuwa anataka kujigeuza.
Hivyo akajitoa hapo na kumwangalia, naye Lexi akaugeuza uso wake kwa kuutazamisha upande wa uso wa Nora, kisha macho yake yakaanza kufunguka taratibu. Nora, akiwa amelalia ubavu wake karibu na Lexi huku akimtazama kwa ukaribu, akaendelea kumwangalia tu kwa hisia, naye Lexi akayatuliza macho yake kwake. Nora akaanza kupitisha kidole chake usoni kwa Lexi, akifanya kama kumtekenya taratibu.
"Mambo?" Lexi akauliza kwa sauti ya chini.
"Poa," Nora akajibu kwa sauti ya chini pia.
"Umeamka zamani?"
"No, sasa hivi tu..."
"Nina bonge la hangover..."
"Ahahah... pombe za jana usiku hizo..."
"Yeah..."
Lexi akatazama juu, kama vile anatafakari kitu.
"Unawaza nini?" Nora akauliza.
Lexi akamwangalia na kusema, "Natakiwa kunyanyuka niende kumtoa Zelda. Lakini naona uvivu... na hilo baridi."
"Ni muhimu kumtoa kila asubuhi?"
"Yeah..."
"Vipi kuhusu siku ambazo haukuwa huku? Nani angemtoa nje?"
"LaKeisha..."
"Inaonekana kama LaKeisha pekee ndiye anayeweza vitu vingi tofauti na wengine..."
"Ahahah... hapana, kawaida tu. Zelda amemzoea uncle Ken na Keish, tofauti na mimi hakuna mwingine. Kwa hiyo inategemea na ni nani yuko huku hata kama mie sipo... anamtoa," Lexi akaeleza.
Alikuwa akiongea hayo huku ameanza kutembeza kiganja chake juu ya ngozi laini ya mkono wa Nora, na hiyo ikawa inamsisimua mwanamke huyu.
"Okay. Unamdekeza mnyama wako kweli," Nora akatania.
"Ahah... tumetoka mbali..." Lexi akamwambia.
Macho mazuri ya Lexi yalimvutia sana Nora, naye kwa wakati huu alihisi kama vile anaogelea ndani ya macho hayo kwa kuzama sana kuyatazama. Akaifata midomo ya Lexi taratibu na kuibusu, kisha akamwangalia tena. Lexi akatabasamu tu, lakini Nora akaendelea kuibusu kidogo kidogo, na mwishowe ikaanza kuwa denda ya asubuhi.
"Hii itanichangamsha kido...."
Maneno hayo ya Lexi yakakatishwa na busu za Nora, ambaye aliendelea kumbusu kwa njia iliyoonyesha kwamba hamu yake ilipanda sana. Lexi akakishika kichwa cha Nora kwa nyuma, akianza kujibu busu yake kwa upendo mwingi sana, naye Nora akapitisha mguu wake mmoja kupita mwili wa Lexi uliolala chali na kumlalia kwa juu. (.........).
(..........).
(..........).
Baada ya kutumia muda uliokaribia saa zima wakionyeshana mapenzi, wawili hawa wakaendelea kulala pamoja huku wameibana miili yao kwa ukaribu wakitazamana, na wote wakiwa bila nguo kwenye miili yao wakati huu. Nora akawa anatekenya mgongo wa Lexi taratibu, huku Lexi akitembeza kiganja chake kwenye mapaja na kalio la Nora taratibu.
"Lexi..."
"Mm..."
"Nakupenda..."
"Kwa nini unanipenda?"
"Ahh... hukutakiwa kujibu hivyo bwana... that's so non-romantic..."
"Ahahah... nilitakiwa nijibuje?"
"Basi..."
"Ahah... kweli, nataka tu kujua..."
"Nakupenda... kwa sababu tu nimekupenda tayari. Sihitaji orodha ya mambo mengi..."
"Labda na misukosuko niliyokufanya upitie imechangia..."
"Labda..."
"Mmmm... sawa..."
"Nataka niwe naamka kila siku nikiwa ndani ya kumbatio la mikono yako..."
"Oh Nora... sikujua unaweza kuwa romantic namna hii..."
"Ahah... unanifanya najihisi tofauti tu yaani. Natamani... tungeendelea tu kukaa hapa hapa, au twende mbali, tuishi kwa kutulia tu... mimi na wewe... mbali na mambo yote yenye kuvunja moyo..."
"I know. Hata mimi natamani hivyo pia..."
"Itawahi kufika hiyo siku kweli?"
"Ndiyo. Itafika tu. Haiko mbali sana..."
Nora akabaki kumtazama tu kwa hisia.
"Nakupenda pia Nora," Lexi akamwambia.
Nora akatabasamu kwa kuhisi raha nyingi sana moyoni. Lexi naye akatabasamu, nao wakaanzisha tena penzi lao kwa mara nyingine. Walipeleka penzi lao taratibu mpaka bafuni na kusafishana miili yao kwa upendo. Walifanya mambo bila papara mpaka walipomaliza kujisafisha na kurudi chumbani kuvaa nguo. Nora akawa amevalia T-shirt nyeupe yenye mikono mirefu na suruali nyeusi yenye kuvutika kutoka kwenye nguo nyingi za Lexi, huku Lexi yeye akivaa T-shirt ya mikono mirefu iliyokuwa na muundo wa ngozi ya chui, suruali nyeupe ya jeans nyepesi, pamoja na koti refu lenye manyoya.
Alipoangalia saa ya ukutani, Lexi akaona ilikuwa inakaribia saa 1 kamili. Akatoa jaketi kubwa jeusi na kuanza kumvalisha Nora, na kwa sababu walikuwa wamekaribiana sana, Nora akapitisha mikono yake kiunoni kwa Lexi na kuanza tena kumbusu mdomoni mwake. Lexi aliona kweli penzi lilikuwa limemkolea mwanamke huyu, naye akarudisha upendo wake kwa busu nzuri, kisha akajitoa kwake taratibu. Nora akaendelea kumshikilia kiunoni, akionyesha kama bado anataka waendelee kupiga busu.
"Easy tigress..." Lexi akamwambia.
"Umenivalisha hivi kama vile unataka tutoke out..." Nora akasema.
"Ndiyo. Twende..."
"Ahah... wapi?"
"Kwa Zelda..."
"Ahahahah... unanitakia kifo..."
"No, hiyo haiwezi kutokea. Twende. Nataka nikutambulishe kwake vizuri..."
"Oh, hapana. Wewe nenda tu. Me nita..."
"Nora, am serious. Nataka Zelda akujue," Lexi akamkatisha.
"Lakini Lexi... hiyo si ni hatari, vipi akiniumiza?"
"Hawezi kukuumiza nikiwepo..."
"Hivyo siyo Torres alivyosema aliponiambia kuhusu kilichompata Azra..."
"Oh, kumbe amekwambia tayari?"
Nora akabaki kimya.
"Ile ilikuwa accident. Zelda hatakiwi kumwona mtu mwingine kwanza kabla yangu, au Keish, au uncle Kendrick. Alianza kumwona Azra siku hiyo kwa hiyo alifikiri ni adui..." Lexi akaeleza.
"Well... me sielewi sana lakini haijalishi. Siwezi kwenda Lexi... naogopa..."
"Nakuhakikishia hatakuumiza. Okay? Just trust me, Nora. Niamini," Lexi akamwambia kwa uhakika.
Ingawa aliona jambo hili kuwa la ghafla na lenye kuogopesha, Nora akakubali kwenda na Lexi kumfungulia Zelda.
Walitoka pamoja mpaka nje na kuelekea kwenye nyumba ile ndogo ambayo Zelda alikuwa humo. Bado Nora alihisi hofu kwa kadiri fulani, naye akaukaza mkono wake kwake mpaka wanafika sehemu ya mlango mpana wa chuma wa nyumba hiyo ndogo. Lexi akawa anatabasamu tu huku akimwangalia kwa hisia, naye Nora akavuta pumzi na kuishusha kujituliza.
"Uko tayari?" Lexi akauliza.
"Hapana..."
"Ahahah... usijali. Kumbuka haya mambo mawili. Nitakapofungua mlango, usipige hatua kurudi nyuma atakapokuona, na usiache kumwangalia machoni... no matter what," Lexi akamwambia.
"Lexi, naomba tu tusifanye hivi. Sijui sana kama nitaweza..."
"Najua utaweza Nora. Nakujua. I believe in you," Lexi akamwambia
Nora akautazama mlango huo, naye Lexi akakiachia kiganja chake na kusogea karibu nao. Akabonyeza rimoti ndogo aliyokuwa nayo na mlango huo ukaanza kupanda juu taratibu. Mapigo ya moyo wa Nora yalidunda kwa nguvu kiasi, kukiwa na kitu kilichomfanya ahisi ni kama angetakiwa kukimbia, lakini kufanya jambo hilo sasa ikawa kuchelewa mno. Mlango ukafika mwisho, naye Nora akaona jinsi palivyokuwa na mwonekano wa kawaida ndani hapo, kama vile ubaraza, lakini sehemu ndogo ya pembeni kufikia kona ikiwa kama na uoto au majani mafupi ya kubuni. Hakumwona Zelda, naye Lexi akaanza kuingia huku akimwita mnyama wake na kupiga mluzi.
Ndipo mnyama huyo akatokea ghafla kutoka pembeni, na hilo likamshtua kiasi Nora, lakini akajitahidi kusimama alipokuwa. Lexi akapiga goti moja chini na kumzibia njia Zelda, akianza kumshika manyoya na kumsalimu kwa kiingereza, na hapo Nora akatambua kuwa mnyama huyo alianza kumwangalia.
Lexi akiwa bado ameishikilia shingo ya Zelda, akasema bila kugeuka, "Usiache kumwangalia machoni."
Nora akaendelea kumtazama Zelda machoni, na alikuwa na macho ya njano na makali kweli. Hakukwepesha hata mara moja, kisha Lexi akanyoosha mkono wake mmoja kwa nyuma kumwelekea Nora, bila kumwangalia, naye akatoa ishara ya "njoo." Nora akameza mate kwa nguvu, kisha akaanza kupiga hatua taratibu kumwelekea Lexi, huku akitetemeka kwa kadiri kubwa. Lexi alipoona Zelda ananyanyua mkia, akatoa ishara kwa Nora kuwa asimame, naye Nora akatii.
"Heey... she's a friend... she's my friend... she wants to say hi... she is a friend... she is a friend..."
Lexi akawa anamsemesha maneno hayo Zelda, na taratibu mkia wake ukashuka. Akamwonyesha Nora ishara ya "njoo" tena, naye Nora akasogea mpaka alipoufikia mkono wa Lexi, akiwa hajaacha kumtazama Zelda machoni.
"Chuchumaa karibu yangu..."
Nora akatii maneno hayo ya Lexi, lakini akapiga magoti kabisa usawa wa Lexi huku bado akiwa anamtazama Zelda, na mnyama huyo akamwangalia Lexi.
Lexi akatabasamu na kusema, "Its working. Mshike manyoya yake shingoni."
Nora akatamani amwangalie Lexi kwa hasira, kwa sababu hiki ni kitu ambacho hakumwambia mapema, na kuwaza kwamba angemshika tu mnyama huyo na kunyofolewa kiganja kukamwogopesha.
"Najua unachowaza Nora. Lakini fanya hivyo. Trust me," Lexi akamwambia huku akiendelea kuchezea manyoya ya Zelda.
Nora akaanza kukinyoosha kiganja chake kumwelekea Zelda, na mnyama huyo akamtazama machoni kwa mara nyingine. Akasita kidogo, lakini Lexi akamwambia asiogope na amalize haraka kabla Zelda hajaboeka, na kwa ujasiri Nora akakigusisha kiganja chake kwenye manyoya laini ya simbamarara huyo. Zelda akaendelea tu kumtazama, naye Nora akazidi kukiingiza kiganja chake kwenye manyoya na kukitembeza taratibu kumtekenya.
"Msemeshe..." Lexi akamwambia.
Nora akatulia kidogo, kisha akasema, "Hi... I'm Nora..."
Lexi akacheka kidogo kwa kufurahishwa na jinsi Nora alivyoonyesha kuogopa sana.
Zelda akapiga hatua kumwelekea Nora, na mwanamke huyu akabaki kumtazama kwa hofu iliyopanda kwa kuwa alimsogelea karibu zaidi na uso wake.
"Tulia... Nora... relax... anakupima..."
Lexi akamwambia hivyo, naye Nora akajitia ujasiri mara mbili zaidi na kuendelea kucheza na manyoya ya shingo ya Zelda, huku bado mapigo ya moyo wake yakitaka kupasua kifua. Zelda akanguruma kidogo karibu kabisa na uso wa Nora, naye Nora akaendelea kujituliza.
"Okay... endelea hivyo hivyo... hivyo hivyo..."
Lexi akawa anasema hayo huku akimwachia Zelda, na ni hapa ndiyo Zelda akalaza kichwa chake shingoni kwa Nora. Mwanamke huyu alihisi msisimko wa hali ya juu sana, msisimko wa hofu, lakini akajitahidi kuendelea kuyachezea manyoya yake, na sasa Zelda akawa anazungusha kichwa chake taratibu pia shingoni kwa Nora, na hii ikawa inamtekenya. Punde si punde, Nora akaanza kuitembeza mikono yake mwilini kwa Zelda, huku Zelda akifanya kama kumsukuma-sukuma kwa kichwa chake, naye Nora akawa anamwangalia Lexi huku akitabasamu kwa kutoamini kabisa kwamba aliweza jambo hili.
Lexi akawa anatabasamu kwa furaha, na sasa mnyama huyo akaanza kumzungukia Nora huku ameubana mwili wake kwake kama paka afanyavyo, naye Nora akawa anacheka huku akijitahidi kuendelea kucheza na manyoya yake laini.
"Ahah... this is wonderful..." Nora akasema kwa hisia.
"Yeah... she likes you. Lakini hiyo ni kwa sababu niko hapa," Lexi akamwambia.
"Ukitoka tu ananisahau?"
"Ahahah... anakurarua..."
Nora akacheka kidogo.
"Race you to the top!" Lexi akasema hivyo haraka.
Kabla Nora hajaelewa hiyo ilimaanisha nini, akashtuka baada ya Zelda kutoka kwa kasi sana kuelekea eneo la nje, huku Lexi akinyanyuka kumkimbiza na kumwambia Nora awahi kwenda ndani. Walikuwa wanafanya kama mashidano ya kukimbizana, na hiyo ingekuwa nafasi ya Nora kurudi ndani upesi. Akatoka hapo na kurudi ndani upesi, akiwaacha wawili wale wanakimbizana pale nje. Alitulia sehemu ya mlangoni akiwaangalia kwa umakini, na kiukweli alihisi kuchangamka sana kwa sababu ya kile alichokuwa ametoka kufanya muda mfupi pamoja na Lexi.
"Hajakutoa vidole?"
Nora akageuka, kukuta ni Kendrick ndiye aliyesema maneno hayo. Alikuwa amevalia T-shirt nyeusi na suruali ya kulalia, akitazama nje pia kupitia mlango huo wa kioo.
"Zelda... ni moja ya vitu vingi vinavyompa furaha sana kijana wangu. Anapendeza sana kila nikimwona anacheka namna hiyo," Kendrick akasema huku akitabasamu.
Nora akaendelea tu kumwangalia.
"Anastahili sana kuishi maisha yake yote namna hiyo... akiwa na furaha kila saa," Kendrick akasema.
Nora akatazama nje tena, kisha akasema, "Ndiyo."
"Ameanza kuonyesha hekima pana sana akiwa na umri mdogo, na imewasaidia hata hao watu wazima unaowaona humu ndani kufika mbali. Mambo yote aliyopitia, yanatakiwa kuisha akiwa amepata sehemu nzuri ya kupumzikia. Hiyo sehemu anaiona kwako, lakini bado hajataka kukubali kwamba anaistahili kwa sababu anajiona kuwa mtu anayetakiwa kuendelea tu kupambana," Kendrick akamwambia.
Nora akamtazama.
"Amepoteza vitu vingi muhimu kwake. Hataki kupoteza vingine. Anatambua kuwa... ni lazima tu mwisho wa siku haya yote yataishia sehemu isiyotarajiwa, lakini bado ni mtu ambaye hataki kukubali hilo, ingawa analielewa vizuri sana..."
Kendrick akasema hayo, kisha akamtazama Nora.
"Msaidie. Niahidi kwamba utaendelea kumsaidia asikate tamaa, kwa sababu kwenye dunia yake ndogo kwa wakati huu... wewe ndiyo wa muhimu zaidi," Kendrick akasema kwa hisia.
Nora akabaki kumtazama tu kwa hisia pia, kisha akaangalia chini na kutikisa kichwa kukubali. Wawili hawa wakatazama tena kule nje, wakimwanagalia Lexi alipoendelea kufurahia wakati wake na Zelda.
★★★★
Kadiri ambavyo siku hii iliendelea kufunguka taratibu, ndivyo shughuli za hapa na pale ndani ya nchi zilivyoendelea kama kawaida. Masaa yalizidi kwenda huku maafisa wa usalama wakiendelea na michakato yao ya kuwasaka wezi hao sugu, bila kuwa na matokeo mazuri yaliyokuja upande wao.
Kanali Oswald Deule hasa ndiye aliyekuwa bado na changamoto ngumu sana mikononi mwake, kwa kuwa sasa zilikuwa zimebaki siku chache tu wiki ya pili iishe bila ya yeye kufanikiwa kuwakamata Mess Makers. Aliwaza sana kuhusu ni nini kingempata kama muda huo ungekwisha bila matokeo mazuri, akielewa wazi kwamba Jenerali Jacob angempa adhabu kali kupita jinsi ambavyo angetazamia. Pamoja na kujitahidi kuwaongoza wanajeshi wake maalumu na timu ya Luteni Michael, hakukuwa na matunda mazuri, na sasa akawa anafikiria kutoroka nchi kabla ya wiki ya pili kuisha la sivyo huenda angeuawa kama vile mwanajeshi yule aliyelazimishwa kula kiungo chake cha mwili alifanywa.
Alikuwa akitafuta njia fulani ambayo isingemshtua Jenerali Jacob kwamba anataka kutoroka, kwa sababu alielewa watu wa Jenerali huyo walikuwa wakimchunga kutokea sehemu asizofahamu. Hakuwa na mtu mwingine aliyemwamini zaidi ya Kapteni Erasto, naye akaona ni vyema akimhusisha katika hali iliyokuwa ikimwandama ili kuona kama angeweza kuwa msaada kwake.
Siku hii alimwita Kapteni Erasto kutoka upande mwingine wa jiji ili waweze kuzungumza kwa faragha, kwa kuwa Kapteni huyo naye alikuwa kwenye jitihada za msako huu. Baada ya Kapteni Erasto kufika kwenye ofisi ya kibinafsi ya Kanali Oswald, akaketi pamoja naye, na kabla hata ya maongezi kuanza tayari aliona kwamba Kanali Oswald alikuwa na wasiwasi mwingi. Akanyanyuka na kuanza kuzunguka huku na huku kama anatafakari jambo fulani, naye Kapteni Erasto akawa bado amechanganywa na jambo hilo.
"Kanali... vipi? Mbona unazunguka-zunguka tu? Kuna tatizo gani?" Kapteni Erasto akauliza.
"Yaani sijui tu nifanyeje Erasto. Mambo kwangu siyo mazuri kabisa," Kanali Oswald akasema kwa sauti yenye hisia.
"Unamaanisha nini?"
"Namaanisha ikiwa sitafanikiwa kuwakamata Mess Makers, basi maisha yangu yatakwisha..."
Kapteni Erasto akashangaa. "Kivipi? Sielewi..." akauliza.
"Nilipewa wiki mbili na Jenerali Jacob kuwashika. Zinaenda kuisha. Erasto... ataniua," Kanali Oswald akasema.
"Kwa nini unasema hivyo? Kwa nini alikupa wiki mbili yaani... kama dili?"
"Hukumbuki nilichokwambia usiku ule tunamsafirisha yule mwanamke kwenda kwa Jenerali?"
"Ndiyo nakumbuka. Kwa hiyo... kumbe alikasirika sana, na ndiyo maana akakupa wiki mbili. Kanali... kila mtu anajua ugumu wa hii kazi, mweleze tu kwamba..."
"Unajua Jacob siyo mtu wa kusikiliza sababu. Yule anataka matokeo tu. Siku hiyo nimeenda nilikuta wamemkatakata Meshack mwili wake wote, wameuning'iniza, viungo vyake wakaniwekea mezani ili nile!"
Kapteni Erasto akabaki kumwangalia tu usoni.
"Yeye na Weisiko ni wakatili sana. Najua wananiangalia kwa sababu wana watu wengi, ndiyo maana sijui nitafanya nini ikiwa sitafanikisha. Nahitaji msaada wako Erasto," Kanali Oswald akasema.
"Unataka nikusaidie vipi Kanali?"
"Nataka unitafutie njia ya haraka ili nitoroke..."
"Nini?"
"Ndiyo. Macho yao hayapo kwako, kwa hiyo itakuwa rahisi ukinifanyia mpango ili nitoke haraka sana. Tafadhali nisaidie," Kanali Oswald akaomba.
"Kanali... huyu ni General. Kama ulivyosema, ana watu wengi. Tutajua vipi tunayepaswa kumwamini na... yaani haitakuwa rahisi. Ni bora tu ukiongea naye...."
"Haujanielewa Erasto? Yule mwanaume haelewi maneno! Siku hiyo ningekufa kama isingekuwa kumsema binti yake. Walikuwa wameshajiandaa kunichinja kabisa!"
"Aisee!"
"Mwanzoni nilidhani tukijiingiza kwenye mambo yao tutapata faida lakini Erasto... hawa watu siyo. Kuna mambo mengi sana wamefanya. Mambo mabaya kupita jinsi unavyoweza kufikiria. Ndiyo maana wanawaogopa mno Mess Makers maana wanaweza kufichua siri zao. Kunipa wiki mbili halafu nisikamilishe ishu hii itawakasirisha mno, na wataniua tu kama kujifurahisha. Siwezi hata kujilinda maana hata Raisi yuko nao yaani... aah," Kanali Oswald akasema kwa mfadhaiko.
"Raisi Paul? Na yeye kwenye hayo mabaya unayosema, anashirikiana nao?"
"Nisikilize Kapteni. Mimi sijui mambo yote waliyofanya, lakini nahitaji msaada wako kwa hali na mali. Fanya uwezavyo kijana wangu, kwa uangalifu, ili niweze kutoroka moja kwa moja na wasiweze kunifatilia. Utaweza kunisaidia mdogo wangu?" Kanali Oswald akamwomba.
Kapteni Erasto akatafakari kwa kina sana, kisha akamwangalia na kutikisa kichwa kukubali.
"Asante sana kijana wangu. Nakuomba uwe nwangalifu..."
"Usijali Kanali. Nitafanya kila niwezacho kukusaidia. Nikikamilisha njia hiyo nitakujuza ili uondoke haraka," Kapteni Erasto akamwambia.
Kanali Oswald akamshukuru kwa mara nyingine, naye akaanza kuongea naye kuhusiana na mchakato mzima wa kuwatafuta Mess Makers. Kapteni Erasto alimwelezea jinsi ambavyo bado yeye na timu zao walihangaika sana kuwasaka watu wale bila mafanikio yoyote. Wawili hawa hawakuwa wametambua kwamba wakati walipokuwa wakiongea kila kitu ndani hapo, mlangoni alisimama mtu ambaye alisikia maongezi yao yote. Ilikuwa ni Luteni Michael. Alikuwa ameshafika Dar kutokea Tanga, na moja kwa moja alikuwa amekuja huku kwenye ofisi ya Kanali Oswald ili kuzungumza naye kuhusiana na mambo muhimu aliyopata kujua kutoka kwa yule mwanajeshi, Khalid Juma, lakini kabla ya kuyafikisha akawa ameyasikia maongezi ya wawili hawa sasa kuhusiana na Jenerali Jacob.
Mambo mengi yalizidi kumchanganya, kwa kuwa kadiri ambavyo vitu vingi viliendelea kujifunua, hakuelewa ikiwa upande alioutumikia ulikuwa sahihi au la. Ila kutokana tu na mambo aliyosikia, ilikuwa rahisi kuelewa kwamba wakuu wake wengi walikuwa wabinafsi na wenye kuficha siri nyingi mno. Alitaka kujua ni nini hasa kilichokuwa kikiendelea kwenye mchezo huu mtata sana. Akaahirisha kuzifikisha taarifa hizo kwa wakuu hawa, naye akaondoka jengoni hapo na kuelekea kule kwenye jengo la timu yake.
★★★★
Kwenye nyumba ya maficho ya Mess Makers, vijana wote waliokuwa hapo walijulishwa na Kendrick hatimaye kwamba mpango wao mzima ungeanza kazi rasmi siku ya kesho, hivyo walikuwa na muda mchache wa kuhakikisha kila mtu amepangilia mambo yao vizuri na kupitia tena taratibu zao ili kujiweka tayari kwa yale ambayo wangetakiwa kufanya. Kila mtu alikuwa na kazi fulani, isipokuwa Isiminzile, ambaye alitakiwa tu kukaa pembeni kwenye nyumba hii ili kuendelea kuwa salama.
Kendrick alimweka wazi kila mmoja wao kwamba huenda mwisho wa yote haya usingekuwa mzuri, hivyo vijana wake wangetakiwa tu kufanya waliyopaswa kufanya kuhakikisha mipango yao inakwenda vyema kwa asilimia kubwa. Kevin bado alikuwa anatafuta njia ya kuwavurugia mambo kwa hila zake, kwa sababu kutoka ndani ya moyo wake hakupenda kile alichohisi huenda kingewapata baadae kutokana na mpango huo ambao sasa hakuona faida yoyote kuuelekea.
★
Basi, ikiwa ni mida fulani ya saa 11 jioni, Lexi na Nora wakawa wameketi kwenye sehemu ile ya nje kutokea dirisha pana la chumba chao, iliyokuwa sehemu nzuri sana ya kupumzikia. Walikuwa wakiongelea mambo mengi yenye kufurahisha pamoja, hasa kuhusu jinsi ambavyo Zelda alijitahidi kumwonyesha urafiki Nora asubuhi hiyo.
"Ahahahah... I swear nilikuwa nayasikia mapigo yako ya moyo yakidunda kama ngoma," Lexi akamwambia kiutani.
"Kiukweli nilikuwa naogopa Lexi... yaani..." Nora akasema.
"Ila si umeona sasa? Anaweza kuzoea mtu akitaka," Lexi akamwambia.
"Yeah. Mwanzo nilidhan labda kuna dawa fulani unatumia ili akuzoee maana siyo rahisi kwa mnyama wa aina yake kuzoea mtu," Nora akasema.
"Aina zao ni adimu sana. Nilipoanza kumfuga nilifanya utafiti kuwahusu nikaelewa vizuri mahitaji yake, vitu wanavyopenda, halafu nikampangia ratiba fulani nzuri ya kulala, kuamka, kula, kucheza, tiba... ili awe na afya nzuri. Ni mkali sana pia, lakini akishamzoea mtu ni nwenye urafiki sana," Lexi akaeleza.
"Inachukua muda mrefu kadiri gani yeye kuzoea mtu?"
"Si..wezi kusema kwa uhakika, maana mimi nimeanza kumfuga tokea akiwa mdogo. Kuna kipindi... tulipokuja huku, Torres alitaka sana kumzoea, na nilijitahidi kumzoesha lakini bado mpaka sasa hajamzoea. Na mambo yetu mengi na nini... inakuwa ngumu kupata muda wa kuendeleza hayo mazoezi kwa hiyo... ndiyo hivyo..."
"Kwa hiyo mtu akimchanganya tu, anamtafuna?"
"Yeah. Bora kama angekuwa dume, angekuwa mzito kiasi lakini ni jike... mkali sana," Lexi akamwambia.
"Mimi imekuwaje akaanza hadi kufanya... purring?"
"Ahahahah... amekupenda tu. Labda kwa sababu we pia ni jike," Lexi akatania.
"Ungekuwa umefanya hivyo na Azra labda angemzoea pia..."
"Yeah ni kweli. Ila muda. Niliporudi huku nilikuwa nimeumizwa kwa risasi kwa hiyo..." Lexi akaishia tu hapo.
Nora akatikisa kichwa kidogo na kutazama pembeni, akionekana kutafakari jambo fulani.
"Unawaza nini?" Lexi akauliza.
Nora akamwangalia, kisha akasema, "Naiwaza kesho. Mambo mengi yatatokea kesho."
"Yeah..."
"Lakini kwa kuwa lengo lenu ni zuri kutokana na mnayofanya na mliyofanya, nafikiri mambo yatajipa tu... Ingawa kuna watu wameumia... na bila shaka wapo watakaoumia," Nora akasema kwa hisia.
"Siyo kwamba kwa sababu lengo letu tokea mwanzo lilikuwa zuri hiyo imaanishe hatujali kuhusu baadhi ya mambo mabaya yaliyotokea kwa kusababishwa na matendo yetu. Kuna mambo tumefanya... kuna vitu nimefanya ambavyo kiukweli... sifurahii," Lexi akasema na kuangalia chini.
Nora akatulia kidogo na kisha kuuliza, "Usiku ule... nilipotekwa... ilikuwa ni wewe uliyewaua wale wanaume, siyo?"
Lexi akamtazama na kutikisa kichwa kukubali. Nora akatazama pembeni.
"Samahani. Najua kile ni kitu ambacho kilikuogopesha sana," Lexi akamwambia.
"I couldn't help but wonder... kwa nini uliamua kuniokoa? Wakati huo hatukuwa na ukaribu kivile na... ingekuwa na faida kwenu kama ningeuawa," Nora akauliza.
"Kilichokuwa kikikaribia kukupata siyo kitu ambacho nilitazamia au kupanga. Na niliingiwa na hasira sana kwa sababu... mtu aliyekufanyia hivyo ni ambaye sikudhani angefanya jambo kama hilo... ndiyo maana niliitoa hasira yangu namna ile," Lexi akasema.
"Unamaanisha Kendrick, siyo?"
"Ndiyo. Naomba radhi kwa ajili yake on that. Ni kwa sababu tu alihuzunishwa na kifo cha Oscar ndiyo maana akatenda bila kufikiri..."
"Mhm... inaonekana nilikuwa mwiba mkali kwenu. Bila shaka wote walitamani yale yaliyonikuta yangefanikiwa. Isingekuwa ya wewe kunisaidia..." Nora akasema maneno hayo kwa hisia sana.
"Usijali tena kuhusiana na hayo. La muhimu sasa ni kwamba uko nasi... na mimi pia," Lexi akamwambia.
"Yeah... sasa ninafurahi sana kuwa upande wako. Nikikaa kuwaza vitu ambavyo baba yangu amefanya, hasira niliyokuwa nayo kumwelekea inazidishwa mara mia," Nora akasema.
"Ulikuwa na hasira nyingi kwa baba yako tokea zamani?"
"Ndiyo. Kuna wakati sikutaka kabisa hata kuitwa mtoto wake. Usifikiri nilianza kutumia surname ya mama yangu kama kujifurahisha. Yaani nilikuwa sitaki kabisa kubeba jina la huyo mwanaume..."
"Kwa nini? Alikufanyaje?" Lexi akauliza.
"Hasira niliyonayo kumwelekea inatokana na jinsi alivyoitendea familia yetu zamani," akajibu Nora.
"Aliwatendea vibaya?"
"Haikuwa kwa njia ya moja kwa moja kwa sisi watoto wake, ila ni kwa mama yetu. Flora na Aste, wadogo zangu, walikuwa wadogo mno kuelewa mambo mengi ambayo yaliendelea, na ingawa mama alijitahidi kutuficha, nilikuja kuona jinsi huyo mwanaume alivyomtendea mama kama mtumwa wake. Mbele ya watu... alifanya ionekane kama vile sisi ni familia yenye amani na furaha, lakini wakati akiwa na mama angemtukana, angempiga, na kumsimanga sana. Sikuelewa ni kwa nini mama alikazana sana kuendelea kuwa naye, ila baadae nikatambua kwamba alikuwa anaogopa tu kutuacha sisi... kwa sababu nilikuja kumsikia baba akimwambia kwamba kama angejaribu kuondoka, sisi tungepata shida kwa kuwa yeye hakuwa na muda wa kutuangalia sisi, kwamba hiyo ilikuwa ni kazi ya mama yetu pekee. Alisema amemweka ndani kuwa kama mchungaji wa mifugo yake, yaani sisi... na kama angejaribu hata siku moja ku-protest, anajua ni nini kingetokea..."
Lexi akaendelea kumtazama Nora kwa umakini alipoendelea kumsimulia kisa hicho kwa hisia sana.
"Sikuwa na uelewa wa kutosha kujua alimaanisha nini mpaka mama yetu alipokufa. Alijinyonga. Sisi watatu tulijua jinsi alivyokufa, lakini ukweli kuhusu kifo chake ukafichwa, wakasema tu alikuwa mgonjwa, huku baba akiwalisha wadogo zangu uwongo mwingi kwamba mama yao alikuwa hawapendi na ndiyo maana hata hakuwafikiria mpaka kuchukua hatua hiyo. Niliumia sana Lexi. Nili...nilijilaumu kwa kuwa sikuweza..sikuweza kumsaidia wakati huo. Baba alimfanya kuwa kama mfungwa... alimtesa sana... na mama alijitahidi kuyaficha maumivu yake ili sisi tusiyaone. Lakini ilifikia hatua alichoka. Alijua hata kama angekimbia, baba angempata tu, na labda hata kumfanyia ubaya zaidi. Kwa hiyo akaona njia nzuri ya kuyaondoa mateso hayo... ni kuukomesha uhai wake kabisa," Nora akasema huku akidondosha machozi.
Lexi akawa anausugua mgongo wa Nora taratibu, akimwangalia kwa huruma.
"Hhh... kutokea wakati huo... nilimchukia sana baba. Nilikuwa na miaka 15 tu alipoamua kunipeleka nchi za nje kwa sababu nilimwonyesha wazi kwamba nilimchukia. Akanipeleka huko na kuniacha kwa watu nisiowatambua hata kidogo. Lakini unajua nini? Angalau kuanza maisha mapya na kutokumwona kulinisaidia kuendelea kusonga mbele, na nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kusaidia wale walioonewa. Uliponiambia kwa mara ya kwanza kwamba baba alihusika na mauaji ya mamia ya watu kwa sababu za kibinafsi, kuna sehemu fulani ndani ya moyo wangu ilijua kabisa kwamba anaweza kufanya jambo kama hilo. Na inauma hata zaidi kwa kuwa... Ijapokuwa siko kama yeye... bado nabeba damu yake... na hilo linanifanya nijione kuwa mchafu sana Lexi. Yaani ni kama...."
Nora akiwa anaendelea kufunguka, Lexi akakivuta kichwa chake taratibu na kukilaza kifuani kwake, akimbembeleza, huku Nora akiendelea kulia kwa sauti ya chini.
"Hapana Nora. Usihisi kama unatakiwa kubeba mzigo huo wa hatia ya mtu mwingine, hata kama ni baba yako mzazi. Matendo yake naelewa yanakuumiza, lakini hayo ni maamuzi yake mabaya, na siyo ya kwako. Wewe ni mtu mzuri Nora, na wala umwagaji wa damu wa baba yako haukuchafui wewe," Lexi akamtia moyo.
Nora akajitoa kifuani kwa Lexi na kukaa sawa. Lexi akawa anamfuta machozi na kumwangalia machoni kwa hisia.
"Pole sana kwa hayo yote. Naelewa pia kwamba ni ngumu kwako kupigana dhidi ya mtu mwenye uhusiano wa damu pamoja nawe," Lexi akasema.
"Yaani kiukweli Lexi kama ni nafasi nyingine ningepewa ya kuzaliwa, basi ningechagua baba mwingine na siyo huyo," Nora akasema.
"Angalau lakini alionyesha anakujali," Lexi akasema.
"Kivipi?"
"Well... hakukuacha wewe na dada zako mteseke. Alikusomesha, uka..."
"Haijalishi Lexi. Upendo sio material things. Kama alishindwa kumthamini mama yangu, basi hata upendo wake kwetu sisi ilikuwa ni kwa ajili ya kujionyesha tu. Hana mapenzi ya kweli ikiwa anadiriki kuua mzazi au mtoto wa mtu mwingine bila sababu. Na ndiyo maana niko tayari kuwasaidia kumwangusha... hata kama itamaanisha kumwondosha," Nora akasema na kuangalia pembeni.
Lexi akamwangalia kwa huruma sana.
Nora akashusha pumzi na kumwangalia Lexi, kisha akauliza, "Baada ya kukamilisha kila kitu... utafanya nini?"
"Aam..." Lexi akaishia tu hivyo na kutazama chini.
"Una mpango kwa ajili ya kila kitu halafu hujui utafanya nini baada ya mambo haya?" Nora akauliza kiudadisi.
"Siwezi kusema nina mpango kwa ajili ya kila kitu, maana siwezi kujipangia ikiwa kesho ama kesho kutwa nitakuwa hai au la. Ni kwamba tu... kila jambo tulilofanya mpaka kufikia sasa.... yaani najiuliza itakuwaje kwa wenzangu. Mimi niko tayari ikiwa maisha yangu yatatoweka kwenye pambano hili, lakini siyo kitu ambacho nataka kwa ajili ya wenzangu..." Lexi akamwambia.
"Hapana Lexi, siyo lazima iwe hivyo. Lakini unajua wako pamoja nawe mpaka sasa wakielewa kwamba hilo ni kati ya mambo yanayoweza kuwapata, siyo?"
"Ndiyo... najua lakini..."
"Hili limekuwa suala kubwa zaidi ya nyie wote. Linahusisha watu wengi sana ambao mmewaweka shabaha kuwasaidia. Usiwaze kwamba hautafanikiwa. Utafanikiwa tu. Nina imani na hilo," Nora akasema.
Lexi akashusha pumzi na kutikisa kichwa kuonyesha ameelewa. Nora akavishika viganja vyake na kumwangalia usoni kwa hisia, naye Lexi akatazama chini kwa njia fulani iliyoonyesha huzuni kiasi.
"Kuna jambo fulani nahitaji ujue..." Lexi akasema.
"Ndiyo..." Nora akasema huku ameweka umakini.
Lexi akamtazama na kusema, "Nina mtoto."
Nora akakaza macho kimaswali. "Unamaanisha nini?" akauliza.
"Nimekuja kujua kwamba nina mtoto... wa kike," Lexi akasema.
"Ulijifungua lini?"
"Ahah... hapana. Wakati bado nikiwa kwenye mwili wangu wa kiume niliwahi kutoka na mwanamke fulani... Valentina. Unamkumbuka?"
"Yule wa siku ile supermarket?"
"Ndiyo..."
"Oooh... okay. Yule mtoto wake wa kike ndiyo...."
"Yeah. Alexa ni mtoto wangu..."
"Ulikuwa na miaka mingapi ulipokutana na Valentina?"
"21. Mahusiano yetu mimi na Valentina yalikuwa ndiyo yameanza tu pale nilipohamishwa kwenye mwili wa dada yangu, na muda mfupi baadae familia yangu ikawa imesambaratishwa na Weisiko na Jacob. Hatukupanga kuwa na mtoto, na wakati huo Valentina aliniambia alikuwa kwenye dawa. Inaonekana alikuja kugundua ana ujauzito akifikiri mimi nimeshakufa, kwa hiyo akaamua kuuacha," Lexi akasema.
"Masikini! Kwa hiyo... siku ile mliongea... akasemaje? Ameshamwambia Alexa kuhusu wewe?" Nora akauliza.
"Hapana. Tulipanga kukutana ili tuzungumze vizuri lakini nafasi ikakosekana. Ila nafikiri kufikia sasa atakuwa ameona kwamba niko kwenye kundi linalotangazwa kuwa kundi la kigaidi, na bila shaka anajiuliza imekuwaje. Yaani hata hajui imekuwa vipi mpaka sasa niko hai. Nora... sikutaka maisha yangu yawe hivi. Ile ndiyo ingekuwa nafasi yangu ya kuwa na maisha mazuri... nikiwa na mwanangu. Lakini sasa hivi hata kama nitajaribu kwa njia gani kujisogeza kwake.... mimi sitakuwa mtu mzuri kwenye maisha ya huyo mtoto. Kwanza ataamini vipi kwamba mimi ndiye "baba" yake? Ningekuwa glad kama haya yote yangeisha kwa njia za maigizo halafu nimfate tu binti yangu, nimwambie kwamba nampenda, ingawa sijawahi... aahh..." Lexi akaongea kwa huzuni na kufunika uso kwa kiganja chake.
"Basi Lexi, basi. I'm so sorry kwa hayo yote. Najua inaumiza," Nora akasema huku analaza-laza nywele za Lexi.
"See... sisi wote kuna vitu tunatamani kuenjoy baada ya mambo haya. Lakini hali za maisha zinazotuzunguka zinazidi kufanya iwe ngumu sana. Ahah... kinachobaki inakuwa kutazamia kifo tu," Lexi akasema.
"Kwani Lexi... haikuwezekana kabisa kujua... kujua ni nini kilikupata wewe na pacha wako?" Nora akauliza.
"Hapana. Labda ingekuwa rahisi kama yale yote yasingetupata kwa wakati huo. Ilikuwa ni kama tulirushiwa laana... na huenda kwa wakati huu ungekuwa umekaa na dada yangu halisi na si mimi. Hakuna njia ya kujua ni nini kilitokea, na hakuna njia ya kubadili kilichotokea," Lexi akasema kwa huzuni.
"Mimi nitakwambia..."
Nora akageuka kwa kushtuka baada ya kusikia sauti hiyo kutokea nyuma, naye Lexi akageuka taratibu na kumkuta Isiminzile akiwa amesimama usawa wa milango ya vioo ya dirisha hilo pana.
★★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★★
WHATSAPP +255 787 604 893