N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Ni Krisimasi ya mwaka 1971. Mkulima tajiri wa Iringa akiitwa Said Mwamwindi anamuua kwa risasi Mkuu wa Mkoa RC wa Iringa na Katibu wa Chama Dkt. Wilbert Kleruu.
Kleruu alikuwamo miongoni mwa watawala wasomi wa wakati huo.
Alipendwa na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere, kwa vile alivyobeba falsafa ya Ujamaa na utekelezaji wake usiolegalega wa "Operesheni Tanzania" ya kuunda vijiji. Wengine waliita "Sogesa".
Akiwa RC wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Kleruu anaonesha kivitendo kwamba operesheni Tanzania haishindikani. Peke yake hadi mwishoni mwa miaka ya 1970's alifanikiwa kuunda vijiji kwa akali 750 katika jumla ya vijiji 2,000. Uone jinsi ambavyo alikuwa timamu katika zoezi hilo la "Sogesa".
Hii inatajwa kuwa sababu iliyopelekea Serikali inayoongozwa na MJKN kuona umuhimu wa kumpeleka Iringa ili 'akadili' kiulaloulalo na wakulima matajiri "makabaila" akina Mwamwindi na wenziwe. Hawa walikuwa na Mamia kwa maelfu ya ekari za mashamba ya mahindi kule Isimani, Iringa (Jimboni kwa mzee Lukuvi).
Kwa kutumia mbinu zake Kleruu alifanikiwa kuunda baadhi ya vijiji maarufu Iringa, kikiwamo kijiji cha Ujamaa cha Mkungugu, Sawala, Ilula nakadhalika.
Hata hivyo, pamoja na jitihada zote za Kleruu kuunda vijiji, wakulima matajiri pale Iringa waliendelea kutokubaliana na mpango wa sogesa.
Siku tatu (3) kabla ya umauti wake, RC Kleruu aliitisha kikao na hawa "makabaila" yaani wakulima wa kati na wakubwa. Akina Mwamwindi sasa! "Makabaila" ulikuwa ndio msamiati uliotumika kuwataja majukwaani aina hii ya wakulima.
Mkutano huu RC Kleruu aliuitishia Iringa Mjini. Yaani Iringa taoo/town! Ukipenda!
Ajenda ya mkutano ni: achaneni na mashamba hayo makubwa, jiungeni kwenye ujamaa villages. Mtoto wa Hayati Kleruu anasema "mkutano huo ulikuwa na vuta 'nkuvute za kutosha.
Wakulima hawa makabaila walikataa kuachia mashamba yao. Na kinara miongoni mwao kwenye mgomo huu kwa RC alikuwa huyo jamaa Mwamwindi. Mpango hapa ilikuwa ni kugawa mashamba yao kwa vijiji ambavyo vishaundwa. Jamaa wakagoma.
Siku ya Krismasi mnamo mwaka 1971, RC Kleruu aliendesha motokali yake akielekea kijiji cha ujamaa cha Ndolela. Akiwa hapo kijijini, alishirikiana na wanakijiji wapatao tisini (90), kulima na kupanda mahindi.
RC Kleruu aliendesha Motokaa yake aina ya Peugeot 404 (hiyo pichani), hakuwa na ulinzi wowote wala hakuwa na dereva.
Baada ya kufanya kazi kwa siku nzima, ingali akiwa na njaa na uchovu tele. Kleruu na wale wanakijiji 90 wakasema "kesho nayo ni siku!"
Siku hii walipanda mahindi kwenye shamba la ekari sitini (60).
Wakati akirejea Iringa mjini akitokea Ndolela village. RC Kleruu akasimama. Inaelezwa alisimama karibu na makazi ya Mkulima Kabaila Mwamwindi.
Mwamwindi alikuwa kwenye trekta lake akilima. RC Kleruu akamuamuru ashuke. Na inaelezwa palikuwa na majibizano makali baina ya hawa wawili.
Akitoa ushahidi wake Mahakamani, Mwamwindi aliieleza mahakama kwamba wakati wakiendelea kujibizana, RC Kleruu alikuwa akimbonyabonya tumbo lake kwa mkongojo akisema:
"humu ndimo umefukia mirija yako!?"
Akiwa amegadhabika kwa kitendo hicho, Mwamwindi aliingia ndani ya nyumba yake. RC Kleruu alimfuata.
Mwamwindi alichukua bunduki yake. Haijatajwa ni aina gani. Akammiminia risasi RC Kleruu ambae alifariki eneo la tukio.
Mwamwindi aliuchukua mwili wa RC Kleruu akaupakia kwenye Peugeot (pujhoo!), kisha akaiendesha ile Peugeot kuelekea Kituo cha Polisi.
Pale kituoni, alijitambulisha kwa Koplo wa zamu, kisha akamwambia "kachukueni mbwa wenu kwenye gari".
Habari za kifo cha RC Kleruu zilienea kwa haraka sana.
Inadaiwa kwamba wakulima wenzake na Mwamwindi, walichanga kiasi cha USD 2,500 ili wamtafutie mwenzao Wakili kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo tambo zao za kikabaila hazikufua dafu kwani mzee Omary Chunga ambae ni miongoni mwao anasimulia akisema: 150 katika idadi yao walikamatwa wakafungwa vitambaa usoni wakalundikwa kwenye ndege na kupelekwa kwenye magereza tofauti kote nchini.
Walikaa kifungoni kwa miezi 18 kabla Mwalimu JKN hajawaachia.
Mwamwindi alishtakiwa na kuhukumiwa kifo. Adhabu ambayo ilisainiwa mara moja ikiwa ni moja ya hukumu mbili za kifo ambazo MJKN alisaini katika kipindi chote cha uongozi wake cha miaka 25.
CREDIT: Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere By: I.G., Shivji et. al. PP. 189,190.
MY TAKE:
Vijana tupende kujisomea. Kuna maarifa tele katika maandishi.