Simulizi: Harakati za maisha

Dani,Dani!!
Sijui km utachomoka hapo.
 
Ngoja apeleke umbea ujaziwe nzi.
 
Mzee wa Majanga 7 kila siku janga jipya
 
Jack Daniel umetuacha na alosto, njoo utupe vituuuuz!
 
SEHEMU YA AROBAINI

Nilimpigia simu Shabani ili nimweleze changamoto kuhusu chombo chake huku nikipanga nimchane ukweli juu ya biashara ambayo alitaka kuniweka kwenye wakati mgumu, lakini licha ya kumtafuta mara kadhaa simu haikupokelewa.

Niliingalia ile gari mara mbili mbili huku nikicheka peke yangu namna watu wanavyoishi yaani mke kanyang'anywa chombo hivihivi dah ni hatari sana.nilijisemea moyoni.

Mida fulani usiku nikiwa bado nipo nje nikihakikisha usalama, simu iliita huku mpigaji akiwa ni Shabani,

Ee bro naona huniombei mema hata kidogo, unataka kuniingiza kwenye matatizo yako wewe na mkeo ni dhahiri mkeo ataniona kama ni sehemu ya mtu mfitini kwenye ndoa yake, inakuwaje kunipa niuze chombo chenye matatizo?
Niliuliza.

Daniii hujaacha tu mambo yako, yaani umri huu wetu sisi Mimi na wewe tunawezaje kufanya mambo ya hovyo? Mimi hapa nimeona missed calls zako nikaona labda unataka kunipa taarifa nzuri maana nimekuja huku mashambani mazao ni mengi halafu pesa inakaribia kukata hivyo nategemea sana senti utakayopata tukisukuma chombo kumbe bado tu mwanangu,
Kwani wife kaja kukudisturb?
aliuliza.

Hapana, shem hajaja.
Isipokuwa katika tafuta tafuta ya wateja nilimpata dada fulani ambaye alikuja mahali nilipoweka chombo, lakini , gari kaijua na kudai hatoinunua na pia anaonesha ana ukaribu na anafahamiana na mkeo, Sasa huoni unanitafutia lawama watu tuje kuchukiana bila sababu, Mimi naona njoo uuze mwenyewe, peleka hata yards za minada huko ila binafsi Mimi nimeshindwa kaka.
Niliongea kwa sauti ya kumaanisha .

Dah yaani Dani Wala sikujua kama upo hivyo, halafu usichojua ni kwamba hata kama mke wangu akijua gari ipo na wewe hawezi kukusumbua kwa lolote, kwasababu mimi sijaiba wala kuchukua kwa nguvu bali tulikubaliana baada ya kumwambia tu kuwa achague moja , niuze gari au nimpe talaka.
Akachagua niuze gari haswa baada ya kukiri makosa ambayo aliyafanya. Kwahiyo Dani kuwa huru hakuna mtu yeyote atakusumbua. aliongea huku akinitoa wasiwasi.

Pamoja na kunishawishi sana lakini sikuwa tayari kufanya biashara ile kwani niliona itaniletea matatizo baadaye.

Kesho mida ya mchana nikiwa natafuta lunch, nilipokea simu kutoka kwa Lewis, ni yule mchungaji mtoto wa dada yake na Jastini,

Niambie ndugu, naona kimya kidogo nipe habari. nilikuwa makini kumsikiliza.

Kaka, mambo yamekuwa magumu , ni kwamba uncle wangu Jastini amehukumiwa kifungo cha miaka kumi, ni baada ya jamhuri kumtia hatiani kwa kosa la kufanya biashara isiyokuwa na vibali huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria na hata yeye alikiri mbele ya mahakama.na tulipata wasaa wa kuongea naye na tulimueleza namna ulivyompigania , na hata yeye alifurahi kusikia hukumuacha ila ndiyo hivyo, alipangalo MUNGU mwanadamu mwenye mwili wa nyama hawezi kupangua.
aliweka kituo Lewis huku sauti yake ikiwa ya chini na yenye mkwaruzo akionesha amesikitika sana.

Dah poleni sana jamani , Mimi naamini Kila jambo hutokea kwasababu zake, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo . Niliweka kituo huku Lewis akikata simu.

Aiseee kweli haya maisha tutafute taratibu kama utani yaani jamaa kapigwa nyundo hizo zote , kwa maana hiyo Nigga, Mwamba, na , stronger Jax ni Prisoner?
Asalaaaaleeeeh , Dani napaswa kuwa makini pengine naweza kuwa nafuatia kwenye hili sakata, njia pekee ni kurudi kwa yule mganga maana huenda natafutwa sijijui tu. Niliwaza Kisha nikapiga vijiko viwili tu vya Chakula nikakiacha kama kilivyo huku hata gari la Shabani nikiona kama ni mipango ya shetani kuhakikisha naishia pabaya kama ilivyo kwa Jastini.
Nikawa narudi ofisini taratibu nikiwa mwenye mawazo kiasi kwani siku yangu iliharibika.

Nikiwa bize na mambo yangu, alikuja mtu akaniambia boss ananiita ofisini kwake. Nikainuka haraka nikipandisha ngazi kuelekea ilipo ofisi yake na kukutana na wenzangu wawili ambao wote tuna taaluma zinazofanana.

Niliwasalimia Kisha nikakaa huku nikiwa makini kuhakikisha nasikia point kwa point.

Jamani Mimi nimewaiteni nyinyi ndugu zangu au wafanyakazi wenzangu,

Dani unashangaa Nini ,(huku nikijichekesha) kwani Mimi ni mkurugenzi hapa, Mimi ni Mfanyakazi kama wewe hivyo tunatenganishwa na madaraja tuu.
aliongea kirafiki boss wetu huku siku hiyo nikishangaa namna alivyo mpole maana ni mwenye mikwara mno haswa ukizingatia akikukataa yeye tu basi taasisi nzima imekukataa.

Jamani kumekuwa na changamoto kwenye urekebishaji wa mashine mpya haswa vifaa vinavyotoka bara la Asia, nikamaanisha India, Japan, China na kwingineko.
Maopareta wanalalamika vifaa vinatengenezwa lakini siku mbili tu vinaharibika nini tatizo.

Aliuliza huku akituangalia kwa zamu huku akiandika vitu kwa notebook yake.

Lakini Kila mmoja alikuwa kimya sana huku Mimi tumbo likiunguruma kwa mbali sikujua wenzangu japo sura zao zilionesha nao hawakuwa sawa.

Sasa wiki ijayo Kila mmoja ataenda
Sehemu ninapopajua Mimi, nataka kujua uwezo wenu, lazima tufanyiane interview tena maana mambo hayaendi, mfumo wetu wa taifa unaamini sana katika vyeti kuliko utaalamu , kazi zinasimama kwa kujikuta tumejaza watu weeeengi wasio na ujuzi.
Mmependeza sana na suti zenu lakini nataka niakisi uwezo kama kweli mnaijua Hydraulic vizuri , siyo kupiga pasi nguo na kuja kuperuzi ofisini. Sasa nawapa siku tano mkapumzike nyumbani Kisha mtarudi tuje tupange ratiba zenu.
Aliweka kituo huku Kila mtu akiwa kimya

Tuliteremka Kisha wote tukasimama na kuangaliana kwa sekunde kadhaa pale kwenye korido bila kuongea Kisha Kila moja akielekea ofisini kwake.

Nilikuwa na hofu na mawazo mapya kabisa , sikuwaza kuhusu Jax,
Sikuwaza kuhusu gari la Shabani, Bali niliwaza kuhusu hatima ya kazi yangu , kazi iliyobeba mustakabali wa maisha yangu na familia yangu.
Huku nikiona kabisa boss alituita watu watatu lakini ni kama alinilenga
Mimi maana kazi nilizofanya kwa mara ya mwisho dizaini kama nilichemka hivi.

Jioni nilitoka nje nikawasha ngalawa
Yangu na kuingia highway huku nikiwa very stressed hata simu kadhaa za baadhi ya watu sikuwa na nguvu ya kuzipokea.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Itaendelea....................
 
SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA

Ilikuwa ni siku ya kwanza Kati ya zile siku tano tulizopewa na boss ili tujiandae na kazi ambayo tutapewa nikiwa hata sijaijua.

Lakini nikapanga lazima zile siku tano nizitumie kutatua mambo yangu yote ikiwemo kuhakikisha narudi kwa mtaalamu nikajiself defence.

Nilimuaga mke wangu kuwa Kuna mahali naenda kikazi ,sikumwambia kuwa naenda kwa mganga najua asingekubali japo hangekuwa na uwezo wa kunizuia.

Kwahiyo mume wangu safari hii unaenda na usafiri binafsi , hii safari mbona kama nakuwa na mashaka nayo hivi, maana unaweza Kuta mpo wawili kwenye ndoa bila kujua, pengine safari hii ni kwa mwanamke mwenzangu Mimi sijui tu.
aliongea kwa utani wife.

Mimi mwanamke wa nini tena wewe mwenyewe nina mpango wa kukuacha, tulitaniana kisha nikakamata njia ya kuelekea kwa mtaalamu wa kipindi kilichopita.

Mida ya saa kumi na moja jioni nilikuwa nishafika kwenye Kijiji kile huku nikishangaa watu walivyozidi kuongezeka watu walikuwa wengi mno kiasi cha kujikuta tupo foleni , mtu ambaye nilimkuta kwa mara nyingine alikuwa ni jamaa mmoja aliyekuwa anauguza mtoto wake mwenye ukichaa.

Kaka vipi naona umerudi kwa mara nyingine vipi habari za huko mjini, ni mwezi wa pili Sasa tangu ulipotuacha hapa ndugu .vipi familia haijambo lakini.
aliongea yule jamaa huku nikigundua hata mwili kapungua tofauti na nilivyomzoea.


Tunashukuru MUNGU familia iko poa sijui nyinyi hapa na vipi kijana wetu anaendeleaje. Niliuliza.

Wewe acha tu kaka ,
Nahisi Mungu hasikii kilio changu, naona ni dhahiri hata Mimi nitakufa tu huu ni mwezi wa tano Niko hapa Kuna muda kijana anaonesha ana nafuu lakini ndani ya siku chache anakatisha tamaa hii inaniuma sana.

Pengine ndiyo maana wanaume tunakufa mapema ni kwakuwa kwenye vifua vyetu tumebeba mengi ambayo huwezi kumsimulia yeyote huku tukiugua kimya kimya.
Kwanza mtoto wangu aliugua mara tu baada ya kuhitimu chuo kikuu huku tukiwa na mpango wa kumtafutia kazi.lakini ile miezi michache akiwa nyumbani tulibaini mabadiliko ya tabia yake , kwani alikuwa anajiamini kupita kiasi huku akikosa adabu kwa baadhi ya watu.

Kila mtu alijua kijana yupo na makundi ya ajabu ya wavuta bangi lakini kadri siku zinavyokwenda ndipo tuligundua kuwa tayari amekuwa mgonjwa , huyu hapa ni mganga wa nne, lakini natamani kutoka niende kujaribu kwa mtaalamu mwingine tatizo pesa imekata kaka na baadhi ya ndugu wa mke wangu wanadai Mimi nilimroga mtoto wangu ili biashara zangu ziende.
aliongea kwa uchungu sana.

Kwani wewe bro una kazi gani, maana hata kipindi kile hatukufahamiana vizuri.
Niliuliza.

Mimi ni mfanyabiashara niliacha kazi ya upolisi miaka miwili tu tangu niajiriwe, nikajikuta nashawishika na biashara zaidi,nikianza na biashara za vyakula vya mifugo.
Huku nikiwa mshauri wa masuala ya ufugaji pia japo sikuwa mtaalamu sana lakini nilijenga jina na biashara ikawa kubwa zaidi.

Nina zaidi ya miaka 20 kwenye hii biashara lakini tayari mpaka muda huu Mimi ni masikini, kwasababu robo tatu ya pesa yangu imeishia kwa huyu mtoto, nilianza na hospital za Tanzania Kisha India lakini wapi , tukarudi Tanzania na kuamua kutafuta wataalamu Hawa ambao mpaka Sasa sioni dalili ya matumaini.
Jamaa aliongea kwa hisia kali sana.

Pole sana cha muhimu usimkufuru Mungu, unapaswa tu kushukuru kwa Kila hali kudra za mwenyezi MUNGU hazipo karibu.
nilimwambia huku nikigundua uso wake umebadilika.

Wewe acha tu kaka hata shemeji yako, kaamua kuondoka ni baada ya ndugu zake kumlisha maneno kuwa Mimi ndiye namsumbua mtoto wake, hivyo kwasasa nipo mwenyewe huku nikitupiwa lawama ambazo hata sikuwahi kufikiria. Safari hii alilia kabisa huku nikigundua huenda mambo yake anayo muda mrefu na hakuwa na wa kumwambia.

Kesho asubuhi foleni yangu ilifika
Nikaeleza shida yangu ,kisha nikaambiwa shida yangu ndogo tu natakiwa nipate kondoo dume,ambaye hajaota pembe bado.kisha nitarudi.

Niliulizia majirani wakaniambia kuna msukuma ana kondoo wengi sana,yupo kilomita saba tu toka tulipo ,huku wakiniambia nijipange maana tangu agundue kuwa kondoo ni dili basi bei imechangamka.sikujali kuhusu hilo nilichotaka nipate kondoo tu.

Nilifanikiwa,naam nilimpata kondoo saizi niliyoambiwa ,nikamtia kamba,na kumtia nyuma ya Isuzu yangu na kurudi kwa mtaalamu au fundi kama wengi walivyomuita.
Na sijui kama uganga nao ni taaluma.

Baada ya hapo tuliingia ndani ya kilinge huku kondoo akiwa kafungwa kwenye mti fulani ambako kulikuwa na kondoo wengine wanne huku nikijua huenda sipo peke ninayetaka kusafisha nyota.

Mganga akaanza ufafanuzi wake......
Kuna dawa nitakutengenezea wewe si unataka heshima?
aliuliza.

Nikatikisa kichwa kuashiria ndilo hitaji langu kuu.

Eeeh sasa hao watu wako tutawainamisha vichwa vyao viwe chini,watakuonea aibu kukutazama,
Kila watakalopanga kukufanyia vibaya watajikuta wanaghairi na kuinamisha vichwa vyao kama kondoo mdogo,ambaye hata akichinjwa hutoa sauti ndogo sana licha ya maumivu anayopata.

Kazi tutaifanyia hapo msituni nyakati za usiku,ila kuna wenzio wamekutangulia kwa hiyo itabidi uvumilie mpaka kesho kutwa, usiku wa leo ni zamu ya wengine.
Usijali tatizo lako dogo sana,si hautaki usumbufu?
Basi tulia hakuna atakayekupandishia sauti wote watajikuta sauti ndogo vichwa chini.

Sikuwa na jinsi nilikubali kuvumilia huku nikirudi kule kwa wenzangu kupiga stori.

Sema nini msomaji wangu,iko hivi

Maisha yana siri kubwa kati ya nguvu ya Mungu na ushirikina,
Mungu hutambua udhaifu wetu mapema.

Waweza fanikiwa ukijua ni nguvu ya mganga kumbe ni huruma za Mungu yaani unamuasi lakini Mungu hamtupi mja wake.

Nini kitaendelea sehemu ijayo ina majibu.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Loading.................
 
Asante JD nyingine lini 😋😋
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…