Hizi mambo zipo, Mimi mwenyewe nilibisha sana tu kipindi nikiwa teenager, ila kuna siku nikaamini. Iko hivi,
Mwaka fulani nikiwa mwanafunzi wa darasa la sita, kipindi hicho la sita ni mkubwa tu siyo kama sasa,
Nilikuwa na rafiki yangu ambaye kiumri alinipita parefu, ila ndiyo hivyo akawa rafiki yangu , ng'ombe tunachunga pamoja, na vingine vingi.
Basi kama ilivyo desturi ya watu wa vijijini kuoa mapema , mwaka uleule jamaa akatafuta mchumba na kutangaza ndoa.
Suala lile lilipingwa na watu wengi wakiihusisha ile familia na ushirikina wakidai , ni vema akaahirisha mpango wa kumuoa yule Binti na atafute mwingine lakini jamaa akaona ni Imani tu na dhana mbaya akidai hakuna kitu kinaitwa ushirikina.
Harusi ya kienyeji isiyohusisha masuala ya kanisani, msikitini , sijui ukumbini, ilipitishwa huku kijana na mke wake wakipewa baraka na wazee ili wakaishi vyema kwenye ndoa yao.
Lakini sauti ya wengi ni sauti ya Mungu huenda kulikuwa na ukweli, jamaa yangu yapo aliyoanza kuyaona kwenye ndoa yake, akawa ananiambia kuwa anahisi ni kweli mkewe ni mchawi, lakini Mimi nilibisha sana nikiona labda jamaa maisha ya ndoa yameshamshinda.
Ndoa changa kabisa hata miezi mitatu ilikuwa bado ilianza kuyumba huku wazazi wa binti wakidai kijana kama hamtaki binti yao amuache na siyo kumzushia habari zisizoeleweka.
Basi bwana siku moja tukiwa tunatoka machungani tunarudisha ng'ombe kwa wazazi wa jamaa, ili tuwafungie ndani maana kulishakuchwa, tulipata taarifa kuwa mke wa jamaa yangu kafuatwa na wazazi wake na wameondoka.
Loh, mke anauma jamaa alibadilika muda uleule inaonesha alimpenda sana mkewe juu ya kutambua ushirikina wake, mida hiyohiyo akaniomba nimsindikize hadi kwa wakwe zake ili akawaulize walikuwa na maana gani kumchukua mkewe. Licha ya wazazi kushauri kuwa ni usiku ni vema angesubiri ifike asubuhi lakini jamaa akafosi huku nikimsindikiza kwenda kwa wakwe zake umbali wa zaidi ya kilomita kumi , tukafanikiwa kufika mida ya saa nne usiku.
Tulikaribishwa vizuri , Kisha jamaa yangu akaanza kuhoji kiukali kwanini wamemchukua mkewe, lakini yule Mzee akadai ni vema tulale tu ili mambo yale tuongee asubuhi, lakini jamaa yangu aliishia kutukana kisha akasema hawezi kulala kwa watu , licha ya mkwe yule kusisitiza tulale lakini jamaa yangu aligoma akidai kama hawataki kumpa mkewe yeye anaondoka huku akitukana matusi
Kweli tuliondoka huku jamaa akiwa mnyonge, lakini baada ya kutembea kama 2km tunarudi , ulitokea mwanga mkali mbele yetu mithili ya mwanga wa radi ila ule uliganda,ikabidi tusimame huku jamaa akimtaja Yesu atusaidie licha ya kuwa hakuwa mtu wa kupenda kwenda kanisani akidai ni matapeli tu.lakini muda ule kila mtu alimtaja Mungu
Mwanga uliongezeka huku tukitetemeka , ukaanza kutusogelea kisha ukapaa kwenda juu na kupotelea, tukawa tunarudi nyuma huku tumeshikana mikono kwa uoga hakuna aliyemuongelesha mwenzake kisha tukageuka na kutimua mbio kurudi kwa yule mkwe wa jamaa.
cha kushangaza tukamkuta yupo nje anavuta tumbaku yake ni mida kuelekea saa sita usiku , alipotuona alicheka kisha akaniambia Mimi kuwa nisipende kuongozana na watu wabishi nitakuja kuangamia siku moja huku akilaumu kwanini Mimi kijana mdogo nitembee usiku.kisha akatuonesha chumba fulani tulale.
Tulilala huku nikiwa naogopa sana hata kibatari cha mafuta ya taa tulichopewa hatukuzima kwa kuhofia giza,kabla hakijazima chenyewe kulikucha huku yule Mzee akiwa anatabasamu kila muda , akaja na chupa fulani ina dawa akatuambia tujipake usoni kwani tuliyoyaona si ya kawaida,tunaweza kuwa vipofu tukafanya vile huku nikiamini uchawi upo.
Kama una amini Mungu yupo basi na uchawi upo.
Ipo mifano mingi nimekutana nayo ukubwani ni mingi mno hii Dunia acha tu, wabishi utawasikia wanasema kama uchawi upo wachawi si wangeiba mabenki?
Lakini kumbuka mchawi huiba vitu nadharia kama nyota ya mtu, haiba,kipaji n.k ,yaani pesa zako unatumia kwa fujo bila kujua, ukipata pesa mara mtoto kaumwa, mara hiki ili mradi tu pesa zako zitawanyike.
Unakuta binti ni mrembo anaitaka ndoa lakini haolewi, anaishia kutapeliwa kwa kuzalishwa kisha watu wanapita kushoto.
Au kijana unaoa lakini ndoa inaishia pabaya kama ulikuwa na viasset vyako vinavurugika mtu anadai talaka mnapelekana mahakamani mnagawana mali Kisha unaanza upya.kumbe ni mipango ya watu.
Tatizo vijana wa sasahivi wanajiona ni new generation wanaona mambo mengine ni dhahania tu.
Ngoja ninyamaze Kuna mjuba alikuja PM akadai kwanini napromote uganga akaniita tapeli nataka kuibia watu kumbe Mimi nimeleta simulizi kama sehemu ya burudani na kujifunza , kidogo nisusie simulizi lakini nikaona mtu mmoja hasumbui. Nikashindwa kuwapa msaada hata baadhi ya walio.......
Lakini pia ili mtu arogeke anatakiwa aamini uchawi upo maana kitendo cha kuamini uchawi upo tayari umeingia kwenye mfumo.
Mara nyingi ukiyapuuzia haya ni ngumu kurogeka kwani kama ni ndege umepanda nyingine kabisa uwe stable na durable kwenye Imani moja, kama ni Mungu basi mtegee yeye kama ni side B basi iwe hivyo.
Japo ni vigumu kutenganisha Dunia na uchawi.