Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI

Masaa ni kama yalikuwa hayasogei , nilifarijika baada ya kuona imefika asubuhi huku tukiitwa na yule mtaalamu kwaajili ya kupewa maelezo fulani.akaanza kwa kusalimia mtu mmoja mmoja.

Alituita wanaume ambao hatuna wagonjwa wa kuuguza, Kisha tukamfuata kwenye ule mti walipofungwa kondoo na kugawa majukumu kwa Kila mmoja.

Wapo aliowaambia waingie porini kukata kuni, wengine kuchota maji kwenye mto fulani ambao haukuwa mbali, wengine tukapewa kazi ya kulimalima kuzunguka kwenye kile kilinge na maeneo mengine yaani miliki nzima ya yule mganga.

Zile kazi zilituwia vigumu haswa kwa sisi wageni, baadhi ya wenzetu walikubali na kuendelea na majukumu mengine,
Binafsi Mimi na dogo fulani hivi tulikuwa kwenye wakati mgumu kwasababu, pale tumeenda kufuata huduma tena ya kulipia , iweje tena tufanyishwe kazi?

Lakini hatukuwa na namna ya kufanya tulichukua majembe na kuanza kulima huku mioyo yetu ikiwa haijaridhika kabisa na kazi zile, kwangu Mimi kazi ya kulima haikuwa ngumu kwani ni nature yetu tangu kijijini, Mimi si mtoto wa kishua , nimezaliwa kwenye familia ambayo ni ya chini yaani ikijitutumua kwa kilimo , tena small scale ile jembe la mkono.

Lakini kwa bwana mdogo niliyekuwa naye ambaye kwa umri wake nilishangaa kafuata nini pale , alikuwa analalamika Kila muda kwamba ni manyanyaso tunafanyiwa, lakini tulifanikiwa kuimaliza ile kazi huku tukijumuika kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa kienyeji zaidi.Maisha haya acha tu.

Naam , ilikuwa ni saa mbili usiku mganga aliniita na kusema usiku wa siku hiyo ni zamu yangu kufanyiwa tiba kama ratiba zinavyosema.

Nenda kule upande walipo akina mama , kachote maji kwenye mapipa kisha yasogeze hapa, na pia mengine nenda kaoge vizuri hakikisha unatakata vizuri. na pia vijana wangu
(wasaidizi wake) watakuja kwaajili ya kuchinja na kukutengenezea dawa . alitoa maagizo yule mtaalamu.

Nilioga maeneo fulani ya pori huku nikiwa nageuka mara kwa mara, kwani kuvua nguo huku uko porini,
ambako usalama ni mdogo, linaweza kutokea la kutokea ukajikuta unatimua mbio ukiwa uchi.

Nilishukuru Mungu baada ya kumaliza kuoga , nikarudi nakuta wale vijana wakiwa wameweka mafiga na sufuria kubwa likichemka,huku wakisema nitamke maneno fulani kabla hawajamchinja yule kondoo.
Nikafanya kama nilivyoambiwa.

Mganga alikuwa na chupa mbili zile zenye dawa, akanipa moja niweke mle kwenye sufuria linalochemka, nikafanya vile.

Akanipa pia majani fulani ambayo yalikuwa mabichi, huku akisema nitamke maneno au nitaje majina ya watu ambao nawahisi huwa wananifanyia fitina.

Hapa kwangu ilikuwa ni jambo gumu kuanza kutaja mtu, ikabidi niulize....

Samahani mtaalamu, Mimi nimekuja kwasababu ya kujilinda na wabaya , Sina mtu ambaye nahisi huwa ananifanyia ubaya na kama yupo, naomba unitengeneze ili hao wabaya kama wapo, wasinipate. niliweka kituo.

Ni kweli nilikuwa na mahasidi wengi lakini sikutaka kumdhuru au kumuharibia mtu,Mimi nilitaka Kinga zangu tu.

Sawa kama huna mtu unayemuhisi basi taja maneno ambayo yatakuwa ni silaha ya kumuangamiza yeyote atakayethubutu kukuchezea Kisha hayo majani yatumbukize kwenye chungu yachemke yaunguzwe
alifafanua mtaalamu.

Nilifanya Kila nilichoambiwa huku nisiloelewa niliuliza, Kisha mganga akaanza mambo yake , nikiwa nakizunguka kile chungu wakati huo moto mkubwa wa Kuni unawaka na Mimi nimevalishwa nguo nyeusi huku mganga akiwa mbele anaimba nyimbo ambazo sikuzijua huku akitaja maneno fulani Kisha akachukua bakuli fulani jeusi na kuniambia nichote kipande cha nyama Kisha nitafune.
Nikafanya vile licha ya zile nyama kuwa hazikuiva Kisha vijana wake wakawa wanatumbukiza mkia fulani kwenye kile chungu na kunirushia mithili ya chetezo ya maaskofu.
Niliungua siku ile hakuna mfano.

Baada ya lile zoezi tukaingia pale kwenye msitu uliofugwa mganga akanichanja chale mbili za kifuani Kisha kuchukua dawa kwenye pembe lililochimbiwa pale na kunipaka kwenye sehemu nilizochanjwa huku nikigundua dawa inawasha vibaya huku akiniambia siku inayofuata naweza kuoga maji kama kawaida kwani zile chale ni zindiko tu

Kisha mganga akaondoka huku akisema nitamke maneno fulani yaani nijikabidhi kwa mizimu ili initambue na kunipokea kwani ndiyo yenye mamlaka ya kunipa ulinzi. Nikafanya vile huku giza la mule na mganga keshaondoka , hakika ilikuwa siku ya aina yake.

Kisha nikarudi na kumkuta mganga akiangalia kioo na kutabasamu huku akidai mizimu imeshanikubali.nikamkeshi kama tulivyokubaliana

Hiyo nyama yako waweza kwenda nayo maana shughuli yako imeisha. Na kama unawapa wenzio iwafae kama mboga sawa, kama unanipa Mimi sawa japo usijilazimishe maana huwa mnasema waganga tuna tamaa . aliongea Kisha nikampa yeye huku nikimwambia awe na amani. Huku nikitazama saa inaniambia saa tano usiku nikiwaza kuondoka.

Mimi nakushauri leo usiondoke kwasababu ndiyo kwanza una chale mbichi usije kutana na wenyewe usiku huu Kisha mkaanza kushindana haitakuwa sawa. alishauri mganga.

Baada ya kusema vile akawa kama kanitisha ikabidi niungane na wenzangu tukipiga stori huku mganga akiondoka na majamaa wawili ambao hao aliondoka nao mbali milimani huko , huku za chini chini nikisikia ni wamiliki wa kampuni fulani kubwa nchini. (Code)

Asubuhi niliondoka huku baada ya kukaribia sehemu inayoshika mtandao, sms nazo zikaanza kuingia , nyingi zilikuwa za kawaida lakini moja ilinistua kidogo Kwani hata namba ilikuwa ngeni huku nikipiga simu mara kadhaa lakini haikupatikana.ilisomeka hivi

"Najaribu kukuchukia lakini siwezi, najilazimisha kukulaumu lakini najikuta nakuonea tu nahitaji unisaidie lakini"

Nikaamua kupotezea kwa kuona pengine ni mtu alikosea namba kwani ile meseji dizaini haikuwa inanihusu.

Masaa machache nilikuwa barabara kuu, nikatembea hadi Morogoro mjini
Nikatafuta local gest nikaoga maji vizuri nikabadilisha nguo kisha nikaianza safari rasmi ya kurudi nyumbani.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Loading.......
 
SEHEMU YA AROBAINI NA TATU

Nilifika katikati ya jiji bado mapema kisha nikatafuta mgahawa ili nile ninachokipenda maana hali ilikuwa si hali, lengo pia nijicheleweshe ili nyumbani nifike mida mibovu.

Nilianza kupiga simu huku
Watu kadhaa jamaa na marafiki wakilaumu kitendo cha Mimi kutokuwa hewani kwa siku mbili huku , Shabani akiwa ndiye aliyelaumu zaidi.

Aisee Dani safari hii umeniweza nikafikia hatua ya kuona labda nina mkosi kutokana na kuwa chombo nilimnyang'anya wife, nikadhani umeamua kunidhulumu japo akili yangu haikuweza kuamini. kwani ulikuwa wapi bro. aliuliza.

Nilisafiri kidogo si unajua tena mishe zetu huwezi Kaa town bila kuambiwa nenda sehemu fulani.
nilijibu.

Dah sawa, na Mimi nimerudi toka mkoani na vipi chombo nikuachie uendelee kusaka wateja au nichukue tu maana wewe na safari zako hizoooo....,...kabla hajamalizia sentensi yake nikamjibu.

Sema uko wapi ili tuende nikakukabidhi chombo chako maana , Nina mambo mengi ni kweli nataka hela lakini Niko bize kama vipi njoo sehemu fulani tuongozane.
Nilimwambia huku akidai yupo mbali na mjini hivyo ni kesho tunaweza kuonana.

Nikapita pale gereji nilipoacha chombo nikakuta kipo sehemu salama kama kilivyo, yaani kinavutia sana kiasi Cha kujikuta ama niendelee kutafuta wateja hii si hela naiacha hii......
Halafu umasikini nao mbaya ningekuwa na hela ningechukua na kukaa nayo, ni nzuri kwa kuhonga hii , lakini kwasasa Sina hela ya mchezo kununua vitu ambavyo haviko kwenye ratiba, nilijiwazia

Vipi bro naona chombo unaitazama kana kwamba wewe ndiye mteja, na vipi wateja wapo au miyeyusho, Mimi Kuna jamaa yangu alikuja hapa nilimuonesha sema bei yake yupo chini sana au nikupe namba uongee naye mwenyewe? alisema yule dogo huku akiizunguka ile gari.

Halafu pia yule dada aliyekataa siku ile kununua akidai anaifahamu ,alikuja Jana jioni na kakupigia simu hukupatikana, tena kakutafuta kweli yaani. aliongeza yule dogo.

Sasa kaja kufanya nini na wakati alikataa, au ndiyo kaenda kumwambia mwenye gari na kuamua kumleta hapa, yule demu mjinga Nini kwanza ngoja.... Nilichukua simu mfukoni nikampigia.

Aisee samahani kaka nilikutafuta hukupatikana kwani ulikuwa wapi, na kwasasa uko wapi? aliuliza mara tu baada ya kusalimiana.

Wewe sema shida yako unataka Nini?niliongea kwa mikato huku Nikipanga kumchana ikiwa angenipa taarifa ya kimbea, nilimsikiliza kwa makini.

Iko hivi Mimi Kiukweli nilimsimulia shoga yangu kuwa gari Iko na wewe na inauzwa , hivyo kaniruhusu kuwa kama nafika bei ninunue tu hivyo nipo tayari kuchukua kwani uko wapi.
aliuliza

Mimi nipo mahali gari ilipo na nimepata taarifa zako ndiyo maana nikakutafuta , kama unaweza njoo na hela kabisa., niliongea kwa kujiamini.
Huku akidai anakuja na yupo tayari kuchukua.

Lakini dakika zilienda bila mtu kutokea hata simu yake mara nyingi ilikuwa inatumika, nikaona isije kuwa mtego nikaamua kujificha sehemu ili nione atakuja na nani , hawachelewi kuja na maaskari Hawa,
Lakini kizuri zaidi Documents zote ninazo sidhani kama naweza kutuhumiwa kwa habari za wizi.
Nilijipa moyo.

Saa moja kasoro ndiyo niliona watu wawili wakishuka kwenye bajaj huku bajaji ikiondoka na wao wakaingia mle kwenye gereji .
Nikajisogeza taratibu baada ya kujiridhisha, alikuwa ni yule dada Grace na mke wa Shabani nikashtuka kidogo huku nikijifanya nipo sawa.

Tulisalimiana Kisha mke wa Shabani akanivuta pembeni kidogo tuongee.

Samahani shemu kiukweli nimepata taarifa kuwa gari ipo na wewe na umeambiwa uuze , hivyo nimeamua kuinunua kwa mara nyingine, yeye mume wangu si anataka pesa?
shida yake si pesa tu Niko tayari kununua.aliweka kituo huku nilimsikiliza kwa makini.

Sasa shemu kwani gari zimeisha?
Kama una hela kwanini usinunue kwingine huoni kama utaleta utata zaidi kwenye ndoa yako?
niliuliza.

Kwanza ni hiyo bei ya kutupa anayouza, ni gari ambayo naijua ipo vizuri na wewe niuzie kama alivyokuagiza na Grace kaniambia unauza bei fulani na Mimi sihitaji unipunguzie hata mia, nataka Shabani ajue kuwa naweza kuishi mwenyewe, naweza kuishi maisha sawa na yeyote. aliongea kwa hasira sana.

Dah shemu na kwanini mpo hivyo,ni wazi ndoa yenu haiko vizuri,mkiishi kwa mashindano hivi hamuoni mtaibomoa ndoa yenu?
Kwanini msingeenda kwa wasuluhishi ili mkaongee yaishe ni dhahiri hata chombo kisingeuzwa,ili muishi mlee watoto wenu.
niliuliza kinafiki.

Wewe Shemu,funga mdomo wako umeachiwa gari uuze,basi uza gari mimi ni mteja kama wateja wengine,habari za mimi na Shabani achana nazo,kwani kuzaa ndiyo kufanyaje,watoto ni wakubwa wale wanahaki ya kuishi kote kote kama wataishi na mimi sasa kama wataishi na baba yao inshaallah!aliongea kwa jeuri yule mwanamke huku akikosa heshima hata kwangu ila nilivunga lengo niuze gari nipate changu kesho Shabani nimkabidhi mpunga wake.

Biashara ilifanyika nikapokea ile cash nikatia kwenye begi huku manati yangu nikihamishia kiunoni maana.......
Nikatoka huku nikiwaambia wale vijana wa gereji kuwa wao tutazungumza kesho

Nikiwa njiani naelekea nyumbani niligundua kuwa ndoa ya Shabani imevunjika rasmi hata kama yeye hajui ila ni dhahiri hakuna ndoa pale,maana mwanamke anaonesha hela ya mboga,ya nguo na saloon haimpigi chenga na haya ni madhara ya kuwaachia hawa kina Hawa biashara kubwa.

Binafsi tangu nakua enzi hizo niliapa kutokuoa mwanamke msomi na mwenye kazi yake lakini kuna hii changamoto mpya ya biashara ,yaani mwanamke wa kiswahili akiwa na uwezo wa kuizungusha milioni 30 basi dharau zinaanza labda awe si mshamba wa hela au anakupenda tu.nilijiwazia sana.

Nilifika home nikiwa na mwenye mikwara sana huku nikimkataza wife asinipokee begi langu licha ya kuwa ni kawaida yake kufanya vile,nilipitiliza hadi chumbani nikaiweka mizigo yangu huku kile cha juu nilichopata nikijiona kidume kwelikweli kwani ilikuwa rahisi mno,huku nikijiwazia au ile safari ya kwa mtaalamu imezaa matunda?
Yaani majibu yamekuja mapema mno kama ni yeye kweli.

Nikarudi sebuleni huku nikipokea taarifa ya kushtua toka kwa mke wangu kuwa usiku wa jana yake ambapo mimi sikuwepo kuna Jastini alikuja nyumbani na kuniulizia nyakati za usiku mnene.

Nilishtuka sana kwani najua ni siku chache katoka kuhukumiwa iweje aonekane kwangu.huku nikimwambia mke wangu kuwa au kamfananisha?

Sasa mume wangu mimi nimfananishe Jastini?
Ni yeye nakuambia.alifafanua mke wangu.

Jastini ni rafiki yangu ambaye nilipanga nitamtembelea huko jela aliko kwa lengo la kumpa msaada na kumfariji,iweje leo awe mtaani?

Jifunze,
Elimika,
Burudika

Itaendelea....................
 
ivi moneytalk upo kweli
 
Tumehailisha kususia Uzi huu tunaendelea kuusoma ila tupe namba mganga
 
JD unajua kumuacha mtu na hamu zake yaani unapiga viwili unaacha wakati watu tunataka hata 4

Anyways nisamehe bro naelewa una majukumu yako maisha nje ya JF ni mizuka tu ya utamu wa story πŸ˜‚
 
Nilioga maeneo fulani ya pori huku nikiwa nageuka mara kwa mara, kwani kuvua nguo huku uko porini,
ambako usalama ni mdogo, linaweza kutokea la kutokea ukajikuta unatimua mbio ukiwa uchi.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Hapo kwenye kutimua mbio uchi 😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…