SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
Nilikuwa mnyonge si kidogo hata hivyo nililazimika kutimiza majukumu yangu kama kawaida kwani sikuwa na namna nyingine.
Tuliendelea kutumiana meseji huku wenzangu wakiwa angalau wana furaha lakini kwangu ilikuwa tofauti ,nilipanga kutofanya makosa yeyote kazini,japo mimi ni binadamu mambo ya hapa na pale hayaepukiki.
Dani eeh usijali mwanangu mbona boss kaongea vitu vya kawaida tu,
Huwezi amini nilivyokuwa nawaza na alivyosema tofauti ,nilikuwa nawaza habari za kwenda saiti,Dah kuishi nje ya Dar kwa kipindi hiki siwezi kabisa .
Ilikuwa ni sms ya mmoja wetu ambao tulitoka kikaangoni.
Huku akionesha kufurahi kubaki mjini.
Siku hiyo hata sikutaka kugusa pombe ,licha ya kuwa nilikuwa na extra money ya udalali ,lakini bado akili haikuwa sawa kabisa ,kumbuka niliweza fikisha siku kibao bila kugusa pombe ya aina yeyote.
Nilitoka job nikanyoosha home tu sikutaka kuchepukia popote,
Ni kipindi ambacho nilikuwa nawahi kiasi cha wife kujisikia vizuri,huku mambo yakiwa shwari.
Siku inayofuata angalau nilikuwa na amani baada ya kusikia boss anasafiri na huenda ikakatika miezi miwili, hakika ilikuwa ni shangwe haswa kwenye kundi letu .
Nilikuwa huru sana kwani hata anayekaimu nafasi yake alikuwa ni mwanetu yaani tulikuwa tunammudu vizuri tu na alikuwa humble sana.
Hakuna unoko Wala kufuatiliana.
Baada mida fulani simu ya Shabani ilingia, ikabidi nimsikilize.
Ee bro nambie, naona simu zako Ukiwa huko zipo bize sana yaani hupatikani kabisa. Niliongea kwa uchangamfu.
Ndiyo hivyo , si unajua mazao hupatikana ndani ndani kidogo ambako sometimes network ni shida?
Ila nipo mjini na vipi tunaonana wapi.
aliuliza.
Hapa bro ni baada ya kazi kuisha nadhani jiandae saa kumi na moja hivi njoo maeneo ya kazini kwangu . Nilimjibu kisha nikaendelea na mishe zangu.
Baada ya muda kufika nilimkuta Shabani akiwa sehemu tuliyopanga kukutana , akiwa mnyonge kidogo licha ya mimi kumchangamkia lakini niligundua Kuna kitu kinamsumbua, akavunja ukimya.
Dani Kuna jambo silielewi Kati ya wewe na mke wangu, hili jambo linaninyima raha kabisa na ...........
Jambo gani bro hebu funguka.
Niliuliza kwa pupa.
Imekuwaje tena ukamuuzia gari yule mwanamke, namuita mwanamke kwasababu alishapoteza sifa za kuwa mke wangu siku nyingi sana.
Yaani baada ya Mimi kukudokeza kidogo matatizo yangu ukaona umtafute muongee vizuri si ndiyo?
Tena napata mashaka kidogo Dani nakufahamu vyema sana kwa kupenda wanawake
Pengine umeamua kumnunulia gari yule mke wangu kwasababu ni juzi tu ulisema tuongozane unipe gari baada ya wewe kusema umeshindwa kupata wateja na una mambo mengi.
Halafu siku hiyohiyo ukaniambia mteja kapatikana na umeuza,
Daniel mdogo wangu kuna kitu nimegundua,nishapata picha,kumbe mke wangu siku zote ananisumbua
Kila nikifanya upelelezi nashindwa kumpata muhusika.
Pesa zangu zimevurugika,mtaji wangu umekatika na sikujua ni nani alimshawishi mke wangu kufanya yale,nasikia amejenga kwa siri, anamiliki biashara nyingine tofauti na ya mazao tuliyozoea ,nikaja kugundua baadaye tena kwa kuchelewa ni baada ya yeye......
Kabla hajamaliza maneno yake nilimkatisha.
Ujue Shabani heshima ni kitu cha bure,yaani ukijiheshimu
Utaheshimiwa.
Najua wazi unampenda mkeo , hivyo jitahidi kubalance mambo yako ili tu usijikute unagombana na Kila mtu, matatizo yako yanaumiza lakini usitafute matatizo kwa wengine acha ujinga bro.
Ni kweli Daniel napenda wanawake lakini sijawahi kumtamani mke wa rafiki yangu hata siku moja , ulinikabidhi chombo niuze, mteja aliyekuwa anahitaji nilishangaa kuona kaja na mkeo, huku mkeo akiwa ndiye mteja mwenyewe.
Unasahau nilikwambia kuwa Kuna dada anaitwa Grace alishindwa kununua baada ya kugundua ni gari ya mkeo? Atakuwa ni yeye kamshawishi mkeo achukue tu.na nilimshangaa magari yote mjini kwanini ang'ang'anie gari ile sijui kuna hirizi yake.na mimi sikufanya ajizi niliuza kutimiza kazi uliyonipa ,sasa hayo unayotaka kuyaleta nakushangaa ni zaidi ya miaka mitano mkeo sijawahi kumuona hata wewe mwenyewe unasahau tumepoteana kwa muda gani?
Niliongea kwa ukali maana tayari Shabani alitaka kunitafutia kesi na mabalaa mengine.
Ok sawa ,nipe huo mzigo basi.
aliongea kwa sauti ya chini na yenye upole.nilimkabidhi akahakikisha na kujiridhisha kisha akawa ananiangalia bila kusema chochote.
Vipi bro si mzigo umetimia au?
Maana nataka kusepa mimi.
Niliongea huku nikitaka kuinuka maana niligundua tusingeelewana.
Hebu kaa kwanza Danieli mdogo wangu,mimi nimebakiza miaka miwili tu kustaafu kwa mujibu wa sheria kwenye utumishi
Na ndiyo maana unaona najikita zaidi kwenye mambo yangu binafsi.
Lakini naumia kuona mke wangu amebadilika ukubwani.
Yaani miaka yote tumeishi na watoto wetu watatu huku wapo ambao wana kazi zao na maisha yao , kingine tayari tuna wajukuu wawili,lakini mke wangu hakui wala sijui anawaza nini nashindwa kuelewa kifupi hata kitendo cha kumnyang'anya gari nilijua atajisahihisha,lakini ndiyo kwanza kaonesha jeuri ya kununua gari lile lile na hapa ninapoongea nyumbani kwangu kunawaka moto, na hatuelewani hata chakula Sili tena maana sina imani naye, ila nilichomfanya hatokaa asahau
aliongea kwa uchungu Shabani.
Sawa bro mimi naona mnaweza kuyamaliza kwa kuwashirikisha ndugu ,jamaa na marafiki inawezekana kabisa,inabidi ujishushe bro vinginevyo mkiachana mtaanza kugawana mali na kujikuta unazidi kushuka.nilishauri
( Kwanza alicheka)
Dani hujui tu suala lilipofikia wala hahitaji chochote kutoka kwangu na anadai anaweza kuishi bila mimi.
Na haya ndiyo madhara ya utamaduni wa kimagharibi,
Mababu zetu hawakuyaishi haya,
Yaani walizifaidi ndoa vilivyo.na najuta kuoa hawa mahousegirl ,huwezi amini alikuwa mshamba tu huyu,maisha ,biashara kila kitu nilimfunza mimi lakini malipo yake ni haya huwezi amini hata watoto wetu wanamshangaa sana tu
aliongea kwa sauti kiasi cha baadhi ya watu kutuangalia.
Mbona unawatuhumu mahousegirl bro wanakosa gani unajua kilichotokea ni mapungufu ya kibinadamu tu kulingana na kila mtu hisia zinavyomtuma hata angekuwa na masters ngapi sijui angefanya haya kwani ameshaamua kaka.
Niliongea kwa uelewa wangu.
Weweeee kuna muda najuta sana bora ni ningeoa mwanamke msomi unajua hawa wasiokuwa na elimu ndiyo huja kubadilika kama hivi kutokana na ulimbukeni wa maisha?
Wewe Daniel chunguza utaniambia tu hawa waliotoka vijijini hawafai.
Jamaa aliongea kwa Jazba sana.
Kitu ambacho sitaweza,na nisingeweza ni kuoa mwanamke msomi,au mwenye kipato kunizidi, nisingeweza maana ningewezaje kumuongoza,
Woman akishakuwa na uwezo wa kumiliki kila kitu sawa na wewe au more than basi tegemea kuishi na mwanamke siyo mke.hawezi kukuheshimu na hata akifanya hivyo ni kuigiza tu,tambua huna uwezo hata wa kumkoromea au kumtishia chochote.niliongeza.
Daniiii mimi naona cha msingi ni kumuomba Mungu tu ndoa yako iwe imara basi ila kwa upande wangu nimeshaanguka.mwanaume aliongea huku macho yakibadilika.
nilimuonea huruma halafu nikawaza na mimi wife yupo kwenye biashara ,leo kwa Shabani unaweza kuta kesho kwangu eti,
Haaaaaa wewe mimi nitakata mtu kichwa kwanza anawezaje kumiliki kitu kikubwa bila ruhusa yangu.nitazika mtu akiwa hai.
Halafu ngoja lazima nianze kutembelea biashara yake nione inaendaje na nilivyo na machozi ya karibu mbona nitakufa kihoro.
Nilijiwazia.
Lakini kabla hatujaagana mke wa Shabani alikuja pale akiwa na maaskari wawili waliovaa sare,
Sura ya mwanamke yule haikuwa na huruma hata kidogo.
Jifunze,
Elimika,
Burudika.
Itaendelea.............