Simulizi: Harakati za maisha

SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA

Fatma aliniomba namba huku akitoa simu yake ili nimtajie, huku dereva wa lile gari akionesha kukerwa namna yule mwanamke anavyowachelewesha.

Nilimtajia namba yangu nyingine kabisa ambayo huwa haipatikani ili tu kumridhisha, ila sikuwa tayari kutoa namba yangu kwake kwani vidonda alivyonisababishia vilikuwa havijakauka bado na mtaalamu aliwahi niambia kuwa ni watu wale ndiyo walisababisha matatizo yangu japo nilikuwa hamsini kwa hamsini kwenye kuamini.

Alisevu namba au hakusevu sikujua, ila tuliachana huku gari lilipotea mbele ya upeo wa macho yangu.

Kazi ziliendelea huku operators wote wakiwa wananipa alama ya dole gumba (heko) Kila wakipita karibu yangu kiukweli nilikuwa nafarijika sana haswa ukizingatia serikali iliyopita ilikuwa siyo ya mchezo, hivyo uoga, tahadhari na umakini vilihitajika
Japo ajali haina Kinga lolote lingeweza kutokea.

Siku nilizopangiwa zilikaribia kuisha huku nikiwa na amani na Imani kwa maboss wangu, nakumbuka ilikuwa ni siku ya alhamisi nikiwa na mshikaji wangu Medi ambaye ndiye niliyezoeana mapema na pia tabia zetu zilikuwa zinaendana Kwa vitu vingi kasoro kitu kimoja tu uongeaji.
Mwenyeji wangu alijua kuchezesha maneno.

Oyaa kaka eeeh , nimekumbuka Kuna harusi ya jamaa yetu ambaye ni diwani wa kata yetu hii hii anabariki ndoa yake siku ya jumamosi na Mimi ni mmoja wa watu muhimu lakini huwezi amini nilisahau kabisa,
Dah, yaani hata kikao Cha mwisho Cha juzi nimekikosa sijui watanifikiriaje masikini. alilalamika mwenyeji wangu.

Sasa kwanini usahau, na pia huwa Kuna kamati ambayo itafanikisha shughuli nzima. Je huwa hampigiani hata simu kukumbushana?
Niliuliza.

Aaaaah unajua Mimi ni wa Dini nyingine hivyo sipo direct sana kwenye vikao na mambo mengine ila nashukuru nimekumbuka na hili ngoja niliweke Frontline kabisa ila na ujio wako ndiyo umenisahaulisha hili jambo na pia nikukaribishe ndugu maana kazi zako si zimepungua? Wakitoka kanisani huko kwenye kufunga ndoa basi tukutane ukumbini.
aliongea Medi huku akicheka kiutani.

Sasa ndugu nakujaje bila kualikwa,
Sifahamiki na yeyote zaidi yako,
Si ndiyo kwenda kutiana aibu huko.niliongea huku nikimtazama Medi atanijibu nini.

Mimi naona ondoa shaka kwasababu upo na mimi kila kitu kitaenda sawa tu wala usijali kaka.
aliongea jamaa yangu ambaye muda wote kachangamka.

**************************************

Siku ya jumamosi kwakuwa hakukuwa na kazi site,niliamka kisha kama kawaida yangu nikawasha PC
yangu ili kujisomea mambo fulani,kiukweli ni utaratibu ambao ninao hadi leo hii,napenda sana kujisomea,siwezi kaa kwenye TV zaidi ya lisaa kuangalia nini ama nini.lah huwa siwezi.

Ila naweza kaa haya zaidi ya masaa matano kwenye PC,na kama kweli zinaharibu macho kama wataalamu wanavyodai basi mimi huenda nikawa the most muathirika.

Sasa endelea..........

Saa nne asubuhi nilitoka nje ili nikapate breakfast sehemu nilipoambiwa nile kwa bili yao ,
Huku siku hiyo nikiiona imepooza sana kweli rural ni rural tu
the most of them huwa wanakula makwao,kiasi cha wafanyabiashara za vyakula kudai biashara ni ngumu.

Nilirudi kisha nikaanza kupiga piga simu huku na huku ili kupoteza muda.baada ya hapo katika pitapita kwenye phonebook yangu nikaiona namba ya mtaalamu ambaye nimeshafika mara mbili kwake ,mwanzo matunda ya alichokifanya sikuwa nayaona kiasi cha kufikiria labda ni walewale na pesa nilipoteza.

Nilipiga simu mara kadhaa lakini haikupokelewa nikaona labda yupo busy na wateja wake kama nilivyojionea mwenyewe.

Hizi chenjichenji nazopata huku huyu mtaalamu hazitaki nini,maana ningempa hata shukurani ,ila siwezi kutuma kabla hajapokea simu.
Nilijisemea .

Wakati nikiwa ndani nilisikia sauti ya Medi ,akiongea huku akicheka kwa nguvu na wahudumu wa pale, nikatoka nje huku nikitabasamu maana ukimuona tu Medi unajikuta unacheka kwa visa vyake.

Vipi mshikaji wangu Dani saa sita hii mchana wa juakali bado umelala?
We naye umezidi kupooza,hii wilaya ina wanawake warembo na wazuri sana lakini hata siku moja sijakusikia
Ukigusia masuala hayo,
Haaaaaa Dani au shemeji yangu alikufanyia mambo nini?
Nilitegemea siku za mapumziko kama hizi basi tule maisha yaani tuuuunywe then jumapili tunalala.
aliongea bila breki huku wale wahudumu wakiniangalia huku wakitabasamu hata sikujua walimaamisha nini.

Huku mikoani bwana , wanawake wengi ni wake za watu, hata ambaye hajaolewa unakuta amilikiwa na mtu,
Sasa hunitakii mema Medi,tena kuna wivu huku hatari ,unataka nife halafu magazeti yaandike taarifa ya aibu.
Tulitaniana na Medi kisha nikavaa huku tukiingia mtaani.mchizi alivyo kila atakayekutana naye njiani anasimamisha gari anamsalimia sijui ndiyo kuonekana muungwana hata sikujua.alikuwa na uchale na Uswahili mwingi design kama umeme ulikuwa mdogo kichwani.huku nikishangaa nani kamuini awe msimamizi wa mambo yangu.

Unajua hapa tuelekee hapo juu kuna ukumbi mkubwa kidogo na ndipo sherehe itakapofanyika.nataka nikakutane na wadau wangu fulani.
aliongea Medi huku akibadili uelekeo na kwenda ukumbi ulipo hapakuwa mbali sana ni dakika zisizozidi kumi kwa gari ukitoka kwenye nyumba nayokaa.

Hivi Medi tangu tujuane kuna vitu vya msingi hatujaviongelea au kuulizana,hivi elimu yako ni level gani kaka.niliuliza.

(Kwanza alicheza huku akipunguza spidi ya gari akisimama sehemu ambapo kulikuwa kunapambwa huku bila kuambiwa nikijua hapa ndipo shughuli nzima itafanyika)

Daniel wewe mpelelezi nini mbona umeuliza hivyo, umeniuliza swali ambalo hakuna yeyote aliwahi kuniuliza zaidi ya sehemu husika kunapotakiwa,any way mimi sijasoma sana ila ni ngumu kukutajia elimu yangu.alijibu huku uso ukibadilika alionesha hajapenda.

Aaaah bila shaka hapa ndipo penyewe mahali shughuli nzima itafanyika,gambe itakuwepo?
au mtatunywesha soda,ila Medi nakuamini kwa uwepo wako sidhani kama kutaharibika neno.
Niliongea kwa kujichekesha huku nikimrudisha kwenye reli maana huenda ningemharibia siku kwa swali dogo na rahisi.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Loading............................
 
Naweka kituo hapa hadi iishe
 
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI

Alishuka kwenye gari akiniacha nikiwa tuli mle ndani huku nikichora mazingira ya mtu mmoja mmoja.
Heka heka zilikuwa nyingi na magari yaliyoingia na kutoka yalikuwa si haba,nikaona wenye harusi yao huenda siyo wanyonge mavumba yapo.

Medi alipotea kwenye macho yangu huku dakika zikienda nikajua ,na tabia yake ilivyo basi huko ndani alikoingia sijui kama atatoka mapema,kweli nusu saa ilipita huku nikianza kujiona mjinga kwa kubebwabebwa tu ,yaani mimi nilivyo ni wa kuzurulishwa mitaani? Khaah Medi kaniweza leo.

Baada ya muda fulani alikuja akiwa na watu wawili hivyo mwanamke na mwanaume walioonekana kama timu ya mapambo.

Dada eeeh huyu ni rafiki yangu ni mmoja wa watu muhimu hapa wilayani na amekuja kwa shughuli maalumu.si unajua kaka yangu ni aliyeshika tenda ya kutengeneza kile kipande cha barabara kutoka barabara kuu kuja zilipo ofisi ya DC,
Basi huyu ni mmoja wa watu wetu.
Naomba aheshimiwe na atakaa meza kuu kama ilivyo kwa wengine japo mimi nitakuwa kwenye timu ya vinywaji hivyo sitatulia.alinitambulisha kwa yule mwanamke wa makamo.

Karibu sana,karibu ndugu ,anaitwa nani vile? aliuliza yule dada.

Naitwa Daniel (nikitaja majina mawili)nilisaidia kujibu.

Sawa karibu,na jisikie huru sana naitwa Mama mapambo,ndiyo jina langu maarufu hapa kwa shughuli ya upambaji lakini pia anayeoa ni mdogo wangu wa tumbo moja hivyo kwa leo nipo kwenye nafasi nyingi.aliongea yule mama mwenye tabasamu rafiki.

Yaani dada leo ni Two in one,unacheza huku na huku ila maharusi wakifika lazima utatulia tu.
aliongea Medi ambaye pengine waya wa aibu ulikuwa ..........

Sasa Dani wewe nenda kajiandae,mimi nipo hapa na hata kwangu si mbali hivyo chukua gari nenda nalo kajiandae maana maharusi nadhani wako njiani ,huoni hizo Coaster zilizotangulia.na watu ndiyo wenyewe hao.alishauri Medi.

Nilirudi kisha nikajiandaa huku nikijipongeza kwa kuikumbuka na kuibeba Kaunda suit yangu nyeusi ambayo niliivaa siku moja tu,kifupi ilikuwa ni mpya, nilijicheki kwa mirror ili nione ndevu na nywele zisiwe rough sana maana nipo ugenini kuhudhuria kwenye sherehe za watu ukiwa hueleweki ni noma , heshima huwa inashuka.kila kitu kilikuwa poa . nikachukua perfume fulani niliwahi kununua mkoani Mtwara,huku wife akadai haipendi,alidai eti nikiitumia sinukii vizuri. Licha ya kuwa ilikuwa haina harufu kabisa yaani ni inakufanya tu uwe Smart man lakini siyo kila mtu anajua umepakaa perfume.si mpenzi wa Cheni wala pete ,kwanza huwa siwezi kutembea na kitu kinanitekenya shingoni ,hata saa huwa navaa basi tu.
Nilihakiki code yangu nikaona sijazingua nikatoka huku muhudumu wa pale akishindwa kujizuia hisia zake.

Aisee kiukweli kaka tangu ufike hapa sijawahi kukuona ukiwa hivyo jamani , hongera sana,yaani hadi raha .aliongea kwa sauti fulani tamu ya kike.

Sikumjibu ila nilitabasamu tu kuashiria nimependa pongezi zake.

Saa kumi na moja nilishuka kwenye gari nje ya ukumbi ule nikiambiwa watu wameshakula na kinachoendelea ni taratibu zingine tu.nilimpigia rafiki yangu na mwenyeji wangu Medi simu haikupokelewa lengo niongozane naye ,siyo naingia halafu naanza kupepesa macho nisijue nakaa wapi .
Cha ajabu Medi hakupokea simu nikaamua kuingia ndani ya ule ukumbi ,huku muziki fulani ukiendelea kuwaburudisha watu nikasimama mwisho kabisa kwa majamaa fulani ambao huenda hawakualikwa pale

Sina hili wala lile MC alianza kuongea kwa mbwembwe huku akionesha kazi anaijua

Aaaaaah kabla ya yote niwapongeze wale wote tuliomuunga mkono ndugu yetu na huu ni mfano wa kuigwa ,kwa wale ambao tulikuwa kanisani natumai mmesikia vizuri Padre aliyebariki ndoa hii,na kwa wasiokuwepo nitaongea hakika na mimi najuta kuoa kienyejienyeji.aliongea yule
MC huku akiwavunja mbavu watu.

Nikiwa busy na simu haswa baada ya kuona mtaalamu niliyempigia asubuhi akashindwa kupokea anapiga,huku nikitaka nitoke nje nikamsikilize maana nilikuwa near by exist door mara nikasikia kama natajwa jina.

Kuna ndugu yetu hapa bila shaka ni mgeni lakini ningependa aje akae huku mbele jamani,halafu wanakamati mmesahau majukumu yenu? Hebu ndugu yangu uliyesimama hapo nyuma naomba uje mbele hapa basi usijisikie unyonge Mr.aliweka kituo MC

Moyo ulilipuka kwa uoga huku nikijikaza nikisogea kwenda safu ya mbele,watu wakishangilia huku wakiimba baba, baba ,babaaaa, baba
Huyoooo,amependeza na suti yake.

Duh ile siku sitaisahau ,yaani mtu hujajiandaa halafu unaitwa mbele huku maelfu ya macho yakikutazama.

Hebu kabla hujakaa tusalimiane baaaasi,eeeeh hebu jitambulishe.aliongea MC huku nikijikaza na kujitambulisha vizuri,ukumbi wote ukalipuka kwa shangwe na vigelegele,yule aitwaye mama mapambo akaja na kunikumbatia mbele za watu .
Duh ilikuwa ni aibu kwangu .maana mtu anakukumbatia hujui kitu , pengine ana mume hujui,na huyo mume kama akikumaindi maana wanaume tunajijua wenyewe,wenzetu wanawake (baadhi) wanaweza kufanya jambo hata la hatari lakini wasilione kwa muda huo kutokana na furaha kupitiliza.

Nilikaribishwa nikae,huku mtu wa pembeni nisiye mfahamu akiniita , Mr Dani,mr Dani ,kugeuka hamadi!
alikuwa ni Fatma yule askari.
Yaani niliduwaa ila sikushangaa yeye kuwa pale maana yeye ni mwenyeji zaidi kule.

Akahama alipo na kuja kukaa karibu yangu,ikawa hatuongei ila tukikutanisha macho yetu kila mmoja anatabasamu.

Kweli ukitaka kuanguka ,au kuangusha ufalme wa kidume yeyote basi watumie wanawake warembo.
Nasisitiza wawe warembo.
Utafanikisha zoezi lako.

Sasa endelea............

Wakati wa kuwasilisha zawadi uliwadia kama mtiririko wa ratiba ulivyokuwa huku Dj akiweka wimbo fulani wa vijembe yaani kila aliyekuwepo kama hakutoa basi ndo utafanyaje.

Watu walianza kuinuka huku kila mtu akipigiwa makofi kulingana na alichotoa au alichoahidi,huku Mc akisisitiza kuwa wanaoruhusiwa kuahidi ni wale wanaofahamika tu ila kama ni mgeni na huna kwa wakati huo usiahidi chochote labda kama unajiamini utatoa kweli. Wakati huo mahali nilipokaa mimi nadhani walikaa wenye nafasi nzuri kipesa ,yaani wajuba hawakuwa na wasiwasi hata ,pia mijimama iliyokuwa pale ( malkia wa nguvu) walikuwa na tabasamu za pesa tu , mmmh ubaridi ukaanza kuniingia kila nikikumbuka kilichomo kwenye wallet miguu iliishiwa nguvu hata lile tabasamu kwa Fatma lilipungua.nilikuwa nawaza au nimpigie wife aniongezee pesa?
Lakini mbona sijawahi fanya hivi.
Na nilivyotambulishwa kwa mbwembwe ndiyo nilichoka kabisa

Huku Fatma akiwa kama kagundua kitu toka kwangu,akanisogelea na kuninong'oneza kitu huku nikizidi kuwa muoga.

Jifunze,
Elimika,
Burudika.

Weekend njema wadau wangu.

Itaendelea..................
 
Pomoja sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…