Utamu kolea na mkewe ukataka kumtafunaSEHEMU YA KUMI NA MBILI
Sasa Jax hizi karatasi naziona zina jina na picha zisizo zako, lakini pia kuna saini nyingi sana humu, mihuri sijui vikorokoro kibao, halafu naona ni madini aina ya Rubi? Mimi nikadhani dhahabu au Almasi? niliuliza
Kwanza akacheka sana Kisha akafafanua,
Daniel bwana, eti Almasi,
Hiyo hatuiwezi bwana, tungefikia kujadili habari za hiyo kitu, tungeongelea hapa, ok ila umeuliza swali zuri,
Sasa bwana Dani hapa tunaongelea Rubi kwasababu ndiyo aina niliyoagizwa na tajiri ambaye yeye yupo hapa hapa mjini.alifafanua.
Je,Mimi Daniel nawezaje kuijua kuwa hiyo ndiyo Rubi na hii siyo? niliuliza
Kisha akaniashiria tuingie kwenye gari lake huku akifungua mkoba na kutoa vidude fulani vyenye rangi tofauti tofauti,
Hapa nina aina tatu za madini , hizi chenga chenga ni dhahabu, ukisikia dhahabu ghafi ndiyo hii, na hii ni fake yake usione ni kama zinafanana laini Kuna utofauti mkubwa na kizuri zaidi ni kwamba usiwaze kwakuwa utakuwa na Mimi basi Kila kitu kitakaa sawa. alifafanua mshikaji wangu aliyeitwa Justini au Jax.
Je, tunapataje sasa haya madini yaani tunanunua kwa nani? niliuliza
Ewaaaah swali zuri kwanza kuna zaidi ya mikoa minne ambayo Mimi naifahamu, tunaweza kupata lakini ni kwa baadaye, kwasasa Kuna mtu atatuletea mwenyewe, yaani Kuna jamaa mmoja anaitwa Hussein, yupo hapa hapa yeye alisema Mimi nimtafutie soko lilipo, Sasa nikawaza kuliko nimuoneshe tajiri ni vyema nikakutafuta wewe kwanza ili tuwe tunanunua kwa bei kadhaa na tunauza kwa bei hii.
Ni pesa nzuri tutatengeneza Dani, hebu fikiria tupo tu mjini mtu anakuletea madini, Kuna watu wapo machimboni huko wamewekeza hela ndefu na bado hawana uhakika wa kurudisha hata nusu hasara.aliweka kituo.
Dah sawa bwana ila sijajua tunaanza na mtaji wa shilingi ngapi maana haya ni madini kaka, niliuliza.
Siyo hela nyingi kwasababu Gram moja ya Rubi ni .....na Gram moja ya dhahabu ni .........na unaanza kidogo kidogo hata grams hamsini unapeleka kwa tajiri hata kumi tu unapeleka halafuuuu....
Japokuwa sisi tumelenga Rubi lakini lazima tujue bei zote za aina ya madini na pia anaweza kutokea tajiri mwingine wa dhahabu na vitu vingine
alifafanua
Hela ya hizo grams alizonitajia kiukweli nilikuwa nayo, ila uoga na moyo kukataa vilishika nafasi yake, huku tamaa ikiwa kwenye kiwango kikubwa faida ilikuwa inakuja kama mara mbili hivi, hivyo nilishachanganyikiwa.
Sasa Jax tunapaswa
Tuanze na grams ngapi kwanza, na nakutegemea maana kumbuka hii biashara Mimi sijui chochote. niliuliza
Grams hamsini ingekuwa poa ila si vitu vinapatikana kirahisi , halafu tunatakiwa kuishia grams hamsini tuhata kama ukikuta ana kilo moja lakini pia unadhani ni nyanya hizo dani huyo jamaa yangu Hussein aliniambia ndiyo kwanza ana grams thelathini....................
Si mbaya hizo twende tuwachukue,na kwakuwa tunaanza hicho ni kiwango kikubwa sana , nataka niile faida yake kwanza ndipo naweza shawishika zaidi. niliongea huku nikiwa na hamu sana na hiyo biashara.
Huu ni mzani na hivi ndivyo unavyosoma Mimi nishawahi jaribu kufanya hii kitu sina ugeni nacho,
Wala usiseme Jax Mimi na wewe tulikutana club fulani kwa mara ya kwanza nilikuwa naogopa hata kukusogelea , ulikuwa na mawe kaka na hivi ilikuwaje ukaporomoka maana wewe hujafikisika Bali umeporomoka, niliuliza.
Nilichukua hela ya mkopo Kisha nikamiliki shimo la dhahabu huko mkoani XX , mwanzo nilipata faida sana tu ila baadaye weeeeeeeh
Tena tuache hizi habari, Jana tu nimepita kwenye nyumba niliyouzaga kwa lazima imeniuma sana. na ndiyo maana nimekwambia tunatakiwa kuishia grams hamsini tu hata kama ni zaidi ya hapo,unauza kwanza ndipo unaendelea na mishe zingine. Lakini kumbuka Mimi kwasasa hela Sina na ningekuwa nayo nisingekushirikisha, unaona gari yangu inatoa Moshi hiyo nakosa hata hela nikafanye overall engine , Sina kitu Dani. alifafanua
Kisha tukaagana
Wakati nipo nyumbani niliwaza sana kuhusu mchongo wa ishu ya madini, ni kitu huwa nakisikia kwa watu tu kuwa wanafanya lakini safari hii nikawa nina hamu ya kutaka kujua habari zake ,
Kwanza ngoja nijaribu ila nitakuwa makini kuliko umakini wenyewe, maana haya mambo huwa yana mlolongo mrefu sana, niliwaza huku nikiona ni fursa nzuri kujiongezea kipato.
Siku tatu baadaye rafiki yangu Jastini alinipigia simu kuwa tukutane mahali,
Nikawasha chombo changu Kisha nikamkuta yupo sehemu katulia anakunywa Juisi fulani.
Yaani Jax siamini kama ni wewe ambaye ulikuwa unakesha kwenye mabaa ukilewa sana , Leo hii wewe wa kunywa juisi. niliongea kiutani
Ni vitu vinawezekana hata wewe siku ukiacha pombe , utagundua siyo ajabu kuacha pombe, na hata Mimi nakushauri rafiki yangu wa damu na wa kweli acha pombe, ni kitu ambacho ukitumia wala hupati faida yeyote na ukiacha hupati hasara yeyote chaguo ni lako.
alifafanua
Wewe umeacha au umepumzika?ila hebu tuachane na hayo,
enhee hapa tunamngoja nani Sasa, niliuliza.
Hapa namsubiri jamaa yangu anaitwa Hussein ni afande wa jeshi la polisi aliniambia tukutane saa kumi hii nadhani yupo njiani maana nimetoka kuongea naye muda si mrefu. alinijibu
Afande tena? mimi hao majamaa wamenikalia kushoto kweli yaani , yaani hata nikiwa kwenye sehemu ya starehe akija tu, huwa nahama hiyo sehemu, huwa sitaki kukaribiana nao au kuwa na mazoea nao Sasa kushirikiana kwenye hii ishu tenaaaa.nilinyong'onyea ghafla.
Tatizo lako ndiyo hilo Dani, unapenda sana matabaka, mbona nyumbani kwako Kuna jirani yako ni askari, unataka kusemaje. aliuliza Jax
Yule si jirani tu, tunaonana tunasalimiana imetoka Sina mazoea naye , Wala hata yeye hana time na mimi, tatizo Hawa majamaa wanakuwaga wachunguzi, wapelelezi na uspy mwingi, binafsi huwa sipendi kuwa na ukaribu ila haina shida Kwani tunafanya biashara haramu , si tutafuata sheria? niliweka kituo
Ndiyo hapo Sasa jiulize unakuwa na wasiwasi gani, tufanye kazi bwana acha mawazo potofu. aliongea yule mshikaji wangu huku kwa siku hiyo na Mimi nikiwa nakunywa soda, sikutaka kugusa pombe maana ningepoteza umakini.
Enheeee mtu mwenyewe ndiyo huyu na hii ni pikipiki yake naijua .
Yule Hussein alipaki pikipiki yake Kisha akavua lile kofia lake, lahaulaaa ni yule askari niliyewahi kukutana naye njiani. Tukasalimiana huku nikikosa amani.
Itaendelea....................
Mambo yanaanza kuwa mamboSEHEMU YA KUMI NA MBILI

KumekuchaSEHEMU YA KUMI NA TATU
Karibu sana ndugu , karibu upande huu hiki kiti tulishaandaa kwaajili yako, vipi habari za jazi afande.
Jax alimsalimia jamaa kwa uchangamfu.
Nzuri tu MUNGU anasaidia ni mambo yanaenda ni hofu tu tuliyokuwa nayo wengi kwenye hii tumbua tumbua ya serikali hii , yaani Kila mtu tumbo joto ndugu.
aliongea yule afande Hussein akiwa ananiangalia sana kama ananifananisha na mtu fulani ila hakuwa na uhakika.
Na Mimi nilitengeneza hali ya kujiamini wakati huo sikutaka kuonesha unyonge wowote, lakini nilitulia tu huku nikiwa bize na simu.
Aaaaaaah afande Hussein huyu ni jamaa yangu, tutashirikiana wote kwenye hii biashara yetu kwasababu, ni mtu mwaminifu na hana tabia mbaya nilikwambia tangu mwanzo kwenye simu kuwa ni muaminifu. aliweka kituo Jax
Hii sura siyo ngeni kuna siku tuliwahi kuwa kwenye gari tukitokea kusini huko miezi michache iliyopita, na ni yeye huyu nimemkumbuka
Habari za siku kaka, alinisalimia.
Kwema tu, unasema tulikutana wapi vile maana sikukumbuki vizuri kaka.
nilijifanya kusahau.huku Jax akikatisha yale mazungumzo.
Basi Mimi nafikiria tuanze mazungumzo yetu, kwanza umekuja na mzigo maana hapa hatuhitaji maneno maneno.
aliongea kwa uchangamfu Jax
Mzigo nimekuja nao jamaa yangu Sasa kumbe tungejadili nini,. aliongea yule Hussein kwa mbwembwe huku akitoa kifuko fulani kidogo kwenye begi lake akaonesha Kisha akarudisha na kufunga begi lake huku akimwangalia Jax na kutabasamu.
Safi sana mimi nadhani basi tuingie
Kwenye gari la jamaa yangu huyu tukafanye mahesabu yetu, mzigo si upo (akimaanisha pesa)aliuliza Jax, nikamjibu kwa kuonesha ishara ya dole gumba nilikuwa na kithethe cha kuongea , nilipata hofu kidogo hasa yule Hussein alivyokuwa ananiangalia Kila muda.
Tuliingia kwenye gari huku nikimwambia Jax akae siti za mbele yeye na jamaa yake, licha ya kuwa gari lilikuwa langu, lengo sikutaka yule afande akae siti za nyuma, maana sikujua mawazo yake.
Dani bwana gari yako, mara ukae nyuma yaani huwa simuelewi, ila basi. aliongea Jax kwa kulalamika kidogo.
Hizi ni grams hamsini net, yaani nilipima ujue, Mimi mwenyewe najua vyema hii biashara sema matajiri zangu wamefilisika tu, na Rubi nadhani Ina wateja wachache si kama madini mengine.
aliongea yule afande.
Hamsini wapi hizi arobaoni na nane, haaa Hussein acha hizo bwana,au ulijua sitapima? aliongea Jax kwa kujiamini
Wewe lipa hizo grams zilizopatikana Mimi nadhani labda mzani wangu ni mbovu, na halafu nilipitia kwenye website ya madini, nikagundua Leo Rubi ipo juu kwahiyo lazima twende sawa na wakati lazima bei iongezeke. aliongea yule afande huku akitoa macho lakini alikuwa anageuka kuangalia nyuma Kila wakati.
Hussein tambua tulishakubaliana bei hayo mambo ya mitandaoni usiyafuatishe, wewe dili na faida yako, je inakulipa?
Ukisema uanze kuingiza tamaa mara ooh nimemsikia huyu mara nani utakosa wateja. aliongea Jax mwenye maneno mengi.
Yaani leo nimepatikana sema tu kwakuwa nina uhitaji wa hela, ila nisingeuza kwahiyo bei nakwambia. alilalamika yule afande.
Jax aliniashiria nitoe mpunga , nikampa Jax akahesabu Kisha akampa jamaa, yule afande Hussein alikuwa ananiangalia sana haswa baada ya kuwa hela nilikuwa nazo Mimi , na ukweli siku hiyo Jax hakuwa na chochote alichochangia.jax akanipa yale madini nikatia kwenye begi langu
Kabla hatujashuka kwenye gari yule afande akamwambia Jax kuwa Mimi ananifahamu na Kuna kitu huwa haridhiki nacho juu ya safari yangu Mimi pamoja na mkewe.
Jax huyu jamaa tuliwahi kuwa wote kwenye gari la abiria,lilipoharibika ndiyo mwanzo wa kumfahamu huyu jamaa,na tulikuja kwa kuungaunga hadi barabara kuu ambapo kumbe mwenzetu alikuwa na gari kaletewa na kwakuwa Mimi nilikuwa na mambo yangu mengine, nikamuomba msaada huyu jamaa amchukue mke wangu.
Hivi wewe Jax mfano , una mkeo anaenda mahali ambako unajua atafika leoleo ,ukamuombea msaada kwa jamaa mwanaume mwenzio,
Kisha baada mida fulani mkeo akakuambia kuwa nimeshafika kumbe ni uongo.akafika kesho yake na hapohapo ukamuuliza akakwambia gari liliharibika njiani.
Haya hiyo si mbaya na ukaamua kumpigia simu mwanaume mwenzio labda akupe ufafanuzi lakini akakupa jibu la mkato lisilotosheleza, wewe utajisikiaje. afande aliweka kituo huku akijenga tabasamu ambalo moja kwa moja lilikuwa la kulazimisha.
Dah huu ni mtihani kidogo afande, kwahiyo jamaa uliyewahi kunisimulia ni huyu ? aliuliza Jax
Yah ni yeye na hakutaka mawasiliano tena na mimi ila hadi leo hii huwa nashindwa kupata majibu halisi kwani nini kilifanyika Kati ya huyu na mke wangu, licha ya kumbana mke wangu kwa muda wa wiki nzima lakini alidai mawazo yangu siyo, swali kwanini mke wangu aniambie Kafika
wakati alilala njiani, je mimi nisingetangulia na kubaini jambo lile kwa maana hiyo ningekuwa mbumbumbu nisiyejua kitu, na mbaya zaidi nilizikuta namba za huyu jamaa yako kwa mke wangu unataka Mimi nimchukuliaje huyu jamaa.walibadilishana ili iweje?
aliongea yule Hussein huku safari hii akiwa anaonesha kukasirika waziwazi.
Jax aligeuka Kisha akaniangalia akiwa kama anaamini vile maneno ya yule afande, Kisha akaniuliza , bila shaka umesikia malalamiko ya Ndugu yetu, vipi mwanangu Dani ilikuwaje. aliuliza Kwa upole Jax nikijua yupo katikati hataki kuharibu kwangu Wala kwa afande.
Kuna mambo ni ya kipuuzi sana, Mimi gari liliharibika nikaona nilale kwenye vijiji vya njiani , shemeji yangu alihangaika kutafuta usafiri mwingine akakosa ndipo alipoenda kulala alipopajua huku tukibadilishana namba kuwa gari likipona nitampigia tuondoke, ubaya wangu upo wapi Jax, kama suala la kusema mkewe alimdanganya hilo mimi halinihusu, na kwanini mkeo asiseme ukweli, huenda mmezoeshana kudanganyana. niliongea kwa jazba huku nikishindwa kujua hali ya kujiamini imetoka wapi.
Jax eeh Mimi naona yaishe ngoja niwahi majukumu mengine, yule afande aliongea kiunyonge huku akiondoka.
Sasa huu muda umeisha wewe huo mzigo kalale nao kesho tutaenda mjini kwa tajiri yangu. aliongea Jax Kisha tukaagana.
Huyu afande anafahamiana na Jax na huyu afande huenda alikuwa ananitafuta siku nyingi akawa hajui napatikana wapi, je kama atatafuta kampani yake na kumbana Jax , hawezi kuwaleta nyumbani?
Tumbo lilikoroga sana.
Itaendelea.........................
Mambo Ni fire
Hapa ndo unapatikana ule usemi Dunia ni ndogo Dunia duara tutakutana katikati milima haikutani binafamu wanakutana 😂SEHEMU YA KUMI NA TATU