Simulizi: Hiliki Ya Chumbageni

Simulizi: Hiliki Ya Chumbageni

James Hadley Chase

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
1,984
Reaction score
3,695
HILIKI YA CHUMBAGENI
MWANDISHI: JOSEPH SHALUWA



“BABY umeamkaje?”
“Honey mzima?”
“Mpenzi wangu umeshatoka hotelini?”
“Laazizi wangu, jamani nakutumia text zote hizo na hujibu kitu, kuna nini?”
“Bravo unajua ulivyonizoesha mume wangu, mbona unanifanyia ukatili mkubwa namna hii?”
“Baba yangu, nini kimekupata? Nataka kuona japo text moja tu kutoka kwako nijisikie amani. Nashindwa hata kuondoka nyumbani bila kupata ujumbe wako.”
“Bravo sasa unanipa wasiwasi mpenzi wangu, maana meseji zote huku kwangu inaonekana umezisoma, lakini hujibu kitu, kuna nini?”
Alikuwa ni Viola akituma ujumbe kwa Bravo, mume wake kupitia njia ya Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp. Usiku mzima wa siku hiyo hakuweza kulala usingizi mzuri kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya mume wake.
Ni siku ya tano sasa, mume wake yupo safarini Tanga, kikazi. Alitarajia kukaa huko kwa wiki mbili. Ni muda mrefu sana kwa wanandoa hao wabichi, wenye umri mdogo, damu zao zikichemka!
Viola na Bravo ni wanandoa wapya, ndoa yao ikiwa na miezi mitatu tu tangu walipofunga. Ilikuwa ndoa ya kidini, iliyofungwa kanisani. Wakiwa ndiyo kwanza wameoana, walikwenda mapumzikoni kwenye fungate lao, visiwani Zanzibar ambapo walifurahi huko kwa wiki moja.
Baadaye waliamua kwenda jijini Mbeya na kupumzika milimani kabisa, Tukuyu katika hoteli moja ya kifahari. Walifurahia penzi la ndoa yao mpya kwa baridi tamu, iliyowanasisha karibu muda wote waliokuwa mjini Tukuyu.
Siku za mapumziko zilipokatika, walirejea jijini Dar es Salaam na kuanzisha maisha yao mapya ya ndoa. Kabla ya kuoana, Viola alikuwa akiishi nyumbani kwa wazazi wake, Temeke.
Bravo yeye alikuwa akiishi Kijitonyama, wiki mbili kabla ya kufunga ndoa aliamua kupangisha nyumba nzima, eneo jingine kabisa. Aliamua kuhamia Mbezi Beach, katika eneo ambalo hajulikani!
Walipotoka Tukuyu walifikia Mbezi Beach. Wakaingiza zawadi zao za pande zote, maisha yakaanza rasmi. Yalikuwa maisha yenye furaha, kila mmoja akifurahia kuwa na mwenzake. Jambo moja ambalo Viola alishangazwa nalo kutoka kwa Bravo ni utundu mpya baada ya kufunga ndoa yao.
Ni kweli mara kadhaa wakiwa kwenye uchumba walikuwa wakikutana faragha, tena wakati mwingine walilala pamoja hadi asubuhi, lakini Brano hakuwa mjuzi wa kiwango kile alichokutana nacho kwenye ndoa.
“Baby mbona umekuwa tofauti sana baada ya ndoa?” Viola alimwuliza mume wake, wakiwa katikati ya kazi ya wanandoa, hotelini Tukuyu.
“Kwanini mpenzi?”
“Umekuwa mtundu zaidi, unanifanya nijisikie salama zaidi kuwa na wewe. Unanipa vitu adimu laazizi, ambavyo sikuwahi kuvipata kabla,” akasema Viola.
“Kwani kabla ya Send-off yako ulifanyiwa sherehe gani?” Brano akamwuliza.
“Kitchen Party.”
“Ilikuwa kwa ajili ya nini?”
“Kubwa zaidi ni kufundishwa namna ya kuishi na mume, kufundishwa utundu wa jikoni na chumbani!”
“Safi sana, hata mimi ni hivyohivyo, nilipata darasa kutoka kwa wazee wa Kinyiramba. Maanko zangu walinipa mautundu, ndiyo maana unaona nakula ile kitu roho inataka,” akasema Bravo akionyesha mizaha.
Wote wakaishia kucheka!
ITANDELEA....
 
SEHEMU YA 002


ILIPOISHIA...
“Kwani kabla ya Send-off yako ulifanyiwa sherehe gani?” Bravo akamwuliza.
“Kitchen Party.”
“Ilikuwa kwa ajili ya nini?”
“Kubwa zaidi ni kufundishwa namna ya kuishi na mume, kufundishwa utundu wa jikoni na chumbani!”
“Safi sana, hata mimi ni hivyohivyo, nilipata darasa kutoka kwa wazee wa Kinyiramba. Maanko zangu walinipa mautundu, ndiyo maana unaona nakula ile kitu roho inataka,” akasema Bravo akionyesha mizaha.
Wote wakaishia kucheka!
SASA ENDELEA...
KAZI iliyoendelea baada ya pale ilikuwa siyo ya kusimulia. Viola alijiona mwenye bahati ya pekee kuolewa na mwanaume ambaye alikuwa akiyatambua majukumu yake ipasavyo kama Bravo.
Asubuhi hii yupo chumbani kwake akikumbuka namna Bruno anavyomjulia! Anaanza kupata picha kuwa huenda mumewe huko Tanga ameshakutana na wanawake wa Kitanga, wakamfungia kazi kuliko yeye.
Hakuwahi kufika Tanga, lakini stori za watu kuhusu Tanga alisikia sana. Kwamba Tanga ndipo mapenzi yalipozaliwa... Tanga waja leo, kuondoka majaliwa nk. Mambo hayo yalianza kumpa wasiwasi moyoni mwake.
Hakuwahi kumfikiria mume wake vibaya hata mara moja, lakini kitendo cha kutojibu meseji zake zaidi ya tano za mfululizo, tena zinazoonekana kusomwa, kilimchanganya na kupitisha wazo la kuibiwa kichwani mwake.
“Siyo bure, nitakuwa naibiwa lazima... siyo kawaida yake huyu Bravo,” akajisemea kwa sauti, sasa akiamua kumpipigia mume kwa kutumia WhatsApp.
Yes! WhatsApp Call!
Wazo hilo lilionekana kuwa na maana zaidi. Akaingia kwenye sehemu ya kupiga simu, akabonyeha kwenye jina la mumewe, simu ikaanza kuita. Aliiona picha ya mumewe kwenye kioo cha simu yake, wakati akisubiri apokee.
Simu iliita kwa muda mrefu, lakini haikupokelewa. Akarudia tena kupiga kwa mara nyingine, lakini haikupokelewa. Viola alihisi kupata kichaa.
Hakuelewa ni kwa sababu alijikuta akihisi wivu mkali kiasi kile kuliko siku zote.
“Baby leo umejua kunikomesha, haya bwana asante,” akatuma tena ujumbe mwingine kwa WhatsApp.
Hakutaka kuchelewa zaidi, alikuwa ameshavaa. Akachukua begi lake na ufunguo wa gari, akatoka nje. Akaenda kuingia kwenye gari na kwenda zake kazini. Viola alikuwa mhasibu katika kampuni moja maarufu iliyokuwa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
***
Bravo aliamka mapema sana hotelini kwake. Akajiandaa na kutoka kuelekea kwenye chumba cha kupata kifungua kinywa, akastaftahi harakaharaka. Hakuwa na muda wa kupoteza, akatoka nje ambapo alikutana na wenzake.
Tayari Mzee Shabani, dereva aliyekuwa akiwafuata kila siku hotelini hapo alikuwa ameshafika. Wakaingia na kuelekea kwenye semina. Akiwa kwenye gari ndipo aliingia WhatsApp ili kuona watu waliomtafuta. Huko alikutana na meseji za mke wake, Viola kama mvua!
“Masikini amenitafuta muda mrefu sana, ngoja nimpigie!” akajisemea na muda uleule, akampigia kwa simu ya video.
Alitaka kuzungumza na mke, huku akimuona kwenye kioo cha simu yake. Akapiga simu yake, lakini haikupokelewa. Alirudia mara tatu, akakata tamaa.
“Kwahiyo Viola ameamua kunilipizia au?” akawaza, akiwa hana jibu.
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 3
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Masikini amenitafuta muda mrefu sana, ngoja nimpigie!” akajisemea na muda uleule akampigia kwa simu ya video.
Alitaka kuzungumza na mke wake, huku akimuona kwenye kioo cha simu yake. Akapiga simu yake, lakini haikupokelewa. Alirudia mara tatu, akakata tamaa.
“Kwahiyo Viola ameamua kunilipizia au?” akawaza, akiwa hana jibu.
SASA ENDELEA...
ALICHOJUA Bravo ni kwamba mkewe alikuwa ameamua kumlipizia baada ya yeye kutojibu meseji zake za WhatsApp mfululizo. Hakuwa na wazo lolote baya lililoingia akilini mwake. Alimjua vizuri mkewe alivyokuwa na tabia ya kisirani. Akikasirika, amekasirika. Ni mpaka atakapobembelezwa! Vinginevyo ugomvi haushi.
Akaamua kumpigia tena, kwa njia ileile ya WhatsApp video call. Simu iliita kwa muda mrefu, kwenye kioo akiona sura yake mwenyewe. Ilipokatika, akaamua kuachana na kupiga simu, sasa akaamua kumtumia ujumbe.
“Mpenzi wangu Viola najua umechukia kipenzi, simu sikuwa nayo karibu.”
“Baby niliamka nimechelewa, nikawa na haraka ya kujiandaa hivyo sikuwa karibu na simu.”
“Viola mama, nakujua ulivyo, nijibu basi moyo wangu uridhike.”
“V wangu, please baby, muda huu ndiyo nipo kwenye gari tunaelekea kwenye semina, nijibu basi my dear.”
Zilikuwa meseji za mfululizo, lakini bahati mbaya hazikujibiwa. Robo saa baadaye, gari lilikuwa limeshaegesha kwenye maegesho ya ukumbi maarufu wa mikutano jijini Tanga uitwao Tanga Yetu Conference Centre uliokuwa ufukweni mwa bahari.
Bravo alishuka, lakini kichwa chake kikiwa hakipo sawa, mkewe Viola alimchanganya. Alimjua alivyo na hakutaka kumvuruga. Kwa kawaida ugomvi wao huwa hauishi haraka. Akashika tena simu yake na kumtumia ujumbe:
“Viola wangu, najisikia vibaya, nakuomba unijibu tafadhali.”
Kwenye simu yake, ikaonyesha alama mbili za tiki za rangi ya kijani, zikimaamisha kuwa ujumbe wake ulifika na ulisomwa! Aliendelea kuikodolea macho ili kuona kama angekutana na neno ‘My Love is typing’ lakini hakuona neno hilo wala dalili zake.
Sekunde chache tu, akasikia mlio wa simu, alipotupa macho yake kwenye kioo cha simu, akamuona Viola wake akipiga kupitia simu ya video.
Haraka akapokea!
Alikuwa ameshatafuta kona na kusimama ili azungumze na mkewe kwa nafasi na mapozi.
“Viola ndiyo nini hivyo mama?” akasema Bravo akimwangalia mkewe kupitia kwenye kioo cha simu.
“Nani amemuanza mwenzake?” Viola akamjibu.
“Kwahiyo uliamua kunilipizia?” akauliza Bravo.
“Siyo hivyo Bravo bwana, nilikutumia meseji kibao hukujibu, nikajaribu kukupigia ukagoma kupokea, basi nikaamua kuingia kwenye gari kuja zangu kazini, si unaona bado nipo kwenye gari, ila ndiyo nimefika muda huu,” akasema Viola, sasa akionyesha mandhari ndani ya gari lake.
Bravo akacheka!
“Unanicheka?”
“Hapana mpenzi, nikucheke wewe, miye nimefurahi zangu tu mama!”
“Nikajua tayari watoto wa Kitanga wameshanizidi ujanja.
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 4

NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Kwahiyo uliamua kunilipizia?” akauliza Bravo.
“Siyo hivyo Bravo bwana, nilikutumia meseji kibao hukujibu, nikajaribu kukupigia ukagoma kupokea, basi nikaamua kuingia kwenye gari kuja zangu kazini, si unaona bado nipo kwenye gari, ila ndiyo nimefika muda huu,” akasema Viola, sasa akionyesha mandhari ndani ya gari lake.
Bravo akacheka!
“Unanicheka?”
“Hapana mpenzi, nikucheke wewe, miye nimefurahi zangu tu mama!”
“Nikajua tayari watoto wa Kitanga wameshanizidi ujanja.
SASA ENDELEA...

“Watoto gani gani wanaoweza kukushinda wewe Viola wangu?”
“Wewe sema tu hivyo, lakini nimesikia kuwa watoto wa Kitanga ni hatari, ukiingia hutoki.”

“Ni kweli hata mimi nimesikia hivyo na kidogo hata baadhi ya wenzangu wasio na msimamo naona wamejichanganya na kutekwa na watoto wa Kitanga, lakini si unanijua vizuri mpenzi wangu? Nikusaliti wewe, nimekosa nini miye jamani!”
“Haya bwana, lakini lazima nikueleze ukweli. Moyo wangu ulinienda mbio hatari. Mwenzako sitaki kusikia habari za kushea kabisa!”

“Wivu tu, haya niambie lakini za tangu tulipoachana jana usiku mama?”
“Ninalo basi mpenzi wangu zaidi ya kukumisi? Yaani hapa ni kama naumwa. Na hivyo ulivyonizoesha Bravo wewe! Naona siku zilizobaki kama mwaka!”
“Usijali siyo siku nyingi... nikuambie kitu V wangu?” akasema Bravo.
“Niambie kipenzi cha miye!”

“Nina bahati sana mimi, katika dunia ya leo, kupata mwanamke wa aina yako, ni bahati ya hali ya juu. Namshukuru sana Mungu kwa kukuleta katika maisha yangu, najiona mwenye bahati sana.”
“Hata mimi pia mume wangu mpenzi.”
“Sasa naomba uniruhusu niingie ukumbini mama.”

“Sitaki!”
Bravo akacheka sana! Kitendo cha mkewe kumwambia hataki, alielewa alichotaka. Alitaka aingie kwenye kikao na simu ikiwa hewani...
“Najua unachotaka mama, lakini siyo sahihi. Isitoshe hata wewe utashindwa kufanya kazi zako vizuri, fanya kazi na mimi nifanye kazi. Nakuahidi lunch nitakupigia tena!”

“Bravo nakupenda sana mpenzi.”
“Nakupenda pia baby.”
Mabusu motomoto yakafuatia, kisha wakakata simu. Kila mmoja upande wake alikuwa na lake, Bravo alifurahi kuona alifanikiwa kumuondoa mkewe kwenye wasiwasi, Viola naye akafurahi kuona kwamba hisia zake hazikuwa sahihi.

Kwamba mumewe alikuwa salama salimini!
Hatajekwa na manyang’au ya mjini!
*
Kwa dakika nzima, Bravo aliendelea kukodolea macho meseji iliyoingia kwenye simu yake kwa njia ya WhatsApp ikitokea katika namba ya simu asiyoifahamu.

Pengine isingekuwa maajabu sana kwake kupokea ujumbe wowote kutoka kwa mtu yeyote, hata yule asiyemtambua, lakini tatizo ilikuwa ni aina ya ujumbe aliopokea!
“Kaka Bravo shikamoo. Pia pole sana kwa kazi, najua ni ngumu na umechoka sana. Kuna kitu nataka kukuambia, naomba usinifikirie vibaya. Mimi nimetokea kukupenda sana tena ghafla.

“Nimevutiwa na upole wako, macho yako na kitambi chako kizuri. Kwa hali yoyote ile, nipo tayari kuwa na wewe. Naomba unipe nafasi, nakuahidi sitaichezea. Kwa ninavyokuona, huenda umeoa, lakini kwangu siyo tatizo.

“Chenye umuhimu ni moyo wangu kutulizwa na penzi lako. Narudia tena, naomba unipe nafasi, sitaichezea. Nakuahidi kukufanyia vitu ambavyo hujawahi kufanyiwa katika maisha yako yote tangu umejiingiza kwenye mapenzi.”

ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 5

NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Nimevutiwa na upole wako, macho yako na kitambi chako kizuri. Kwa hali yoyote ile, nipo tayari kuwa na wewe. Naomba unipe nafasi, nakuahidi sitaichezea. Kwa ninavyokuona, huenda umeoa, lakini kwangu siyo tatizo.
“Chenye umuhimu ni moyo wangu kutulizwa na penzi lako. Narudia tena, naomba unipe nafasi, sitaichezea. Nakuahidi kukufanyia vitu ambavyo hujawahi kufanyiwa katika maisha yako yote tangu umejiingiza kwenye mapenzi.”
SASA ENDELEA...

BRAVO alichanganyikiwa. Pamoja na ujanja wake wote, hakuwahi kutongozwa na mwanamke tangu kuzaliwa kwake. Lilikuwa tukio jipya la kumshangaza. Ni kweli aliwahi kusikia stori kutoka kwa rafiki zake, jinsi ambavyo wasichana waliofyatuka wanavyoweza kujitoa fahamu na kuwatokea wanaume, lakini kwake ilikuwa haijawahi kumtokea.

Aliikodolea macho ile meseji alisijue cha kufanya. Hakujua ni nani aliyemwandikia ujumbe ule. Kwa kuwa ilitumwa kupitia WhatsApp, ilikuwa rahisi tu kujua. Akaamua kwenda kwenye sehemu ya picha ya mtumaji! Huko akakutana na maajabu mengine. Iliwekwa picha yenye alama ya kopa, ikisindikizwa na maneno: “Elewa nakupenda, nipokee moyoni mwako.”
“Kweli nakiri sasa nimekaribishwa Tanga rasmi,” akawaza kichwani mwake.

Lakini hata hivyo wazo la kumsaliti mke wake halikuwepo kabisa. Kwanini amsaliti? Amekosa nini kwa Viola, mwanamke mrembo kiasi kile? Hata hivyo alijikuta akitamani kumjua huyo mwanamke.
Akarudi kwenye sehemuya ujumbe, akaangalia juu ya kioo, akaona maneno yanayosomeka ‘online’ yakimaanisha kuwa alikuwa hewani muda huo.

Akamwandikia: “Asante kwa ujumbe wako, ila ni nani mwenzangu?”
“Utanijua tu Bravo, muhimu ni wewe unipende kwanza. Mengine utayajua tu!” akajibiwa.
“Nawezaje kukupenda wakati hata sikufahamu na sijawahi kukuona? Ok! Labda nimekuona, lakini sikukumbuki ndiyo maana nakuuliza, wewe ni nani mwenzangu?”

“Bravo bana... wewe wasiwasi wako ni nini?”
“Basi kama hutaki kujitambulisha, naomba tukate mawasiliano tangu leo.”
“Hapo sasa unajiondolea uanaume wako bana Bravo. Wewe ni kidume, hupaswi kususa. Nakuhakikishia tu kuwa nakupenda na utanifahamu leo hii. Vuta subira lakini nakuhakikishia leo hii utanifahamu!”

Bravo hakujibu kitu, zaidi aliondoka hewani kwenye mitandao ya internet.
*
Hakuagiza chai, lakini ilikuwa ya kwanza kutua mezani. Bravo hakutaka kuuliza, akachukua kikombe cha chai ile iliyokuwa ikinukia, akakipeleka kinywani mwake. Alikutana na ladha tamu ya chai halisi ya rangi iliyokuwa na viungo mbalimbali, lakini kilichosikika zaidi kikiwa ni hiliki!
“Duh! Sijawahi kuonja chai yenye ladha tamu kama hii,” akawaza moyoni mwake.
Alipiga funda mbili tu za chai ile, tayari sahani ya ubwabwa ilikuwa mezani mwake. Mboga zilikuwa pembeni; mchanganyiko – maharage, samaki wa baharini na mboga ya majani aina ya mchunga.

Binti aliyemtengea chakula, alipomaliza zoezi lake, alisimama mbele yake, akamwambia: “Karibu uonje ladha ya mapishi ya mwanamke anayekupenda. Karibu sana Bravo.”
Ilikuwa sauti tamu, laini iliyotolewa taratibu, akiwa hataki mtu mwingine asikie zaidi ya Bravo.
Bravo akatoa macho!

Hakutegemea kusikia kitu hicho kutoka kwa binti yule mdogo, aliyekuwa mbele ya macho yake.

ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 6

NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Ilikuwa sauti tamu, laini iliyotolewa taratibu, akiwa hataki mtu mwingine asikie zaidi ya Bravo.
Bravo akatoa macho!
Hakutegemea kusikia kitu hicho kutoka kwa binti yule mdogo, aliyekuwa mbele ya macho yake.
SASA ENDELEA...

ALIPEKECHA macho yake kidogo kwa mkono wa kushoto; mkono wa kulia ukiwa na kikombe cha chai. Alihisi kama ameingiwa na mchanga usoni.
Lengo lilikuwa ni kusafisha macho yake ili aweze kumuona vizuri mwanamke yule mrembo aliyekuwa mbele ya macho yake.

Alikiri kweli alikuwa mwanamke mrembo. Siyo mara ya kwanza kumuona, alishamuona mara nyingi kabla. Ni sehemu ambayo mara nyingi huwa anapata chakula cha mchana na wenzake wanaokuwa kwenye semina. Lakini hakuwa amemzingatia hata mara moja.
Leo hii anamuona msichana mpya kabisa mbele yake. Swali likabaki kichwani mwake, je, msichana huyo ndiye yule anayemsumbua kwenye WhatsApp kuwa anampenda?
Akataka kupata uhakika wa hilo, lakini akabaki na swali jingine.

Angewezaje kumwuliza kuhusu jambo hilo?
Kitu kimoja alikiri. Mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa mrembo, lakini kitu kingine alichojiaminisha ni kwamba, kamwe hawezi kuingia mkenge wa kumsaliti mkewe kwa tamaa ya mpito.
“Asante sana,” hatimaye Bravo aliitikia kivivu, akijitahidi kuficha hisia zake.
Kifupi Bravo alinasa!
Alichokuwa akifanya ni kujaribu kushindana na moyo wake!
“Asante kushukuru, furahia chakula cha mchana tafadhali,” akasema binti yule.

Wakati anazungumza kwa lafudhi yake ya Kitanga, Bravo alikuwa ameyatuliza macho yake kwenye midomo yake. Alikuwa na midomo minene, mizuri iliyopambwa na lipstick ya kahawia.
Msichana wa watu hakuwa na muda wa kusimama sana, akageuka na kuanza kupiga hatua za taratibu, akiondoka eneo lile.
“Haya ni majaribu ya aina gani?” akajiuliza kichwani mwake.

Macho ya Bravo yaliganda kwenye makalio ya yule dada aliyekuwa akitembea kama ambaye hakuwa na mpango wa kukanyaga ardhini!
Alitembea kwa kunata.
“Anasema mwanaume anayenipenda kivipi? Au ndiye yule wa WhatsApp?” akawaza Bravo.
“Ok! Tufanye ndiye, kama ndivyo ndiyo nimsaliti mke wangu kibwege? Sidhani... haitakiwi hiyo bwana, lazima nitumie akili na nizuie hisia zangu,” akazidi kuwaza Bravo.

Kimsingi kiakili na kihisia alikuwa ametekwa na yule binti. Akaanza kula chakula chake.
Wali samaki, ulioungwa kwa nazi shatashata! Bravo alijilamba kwa mapishi yale. Mwisho kabisa alichanganyikiwa na utamu wa mboga ya majani aina ya mchunga.
Wakati akiendelea kula, yule binti alifika mezani kwake akiwa amebeba kisosi chenye dagaa wa baharini. Pembeni yake kulikuwa na kipande cha limao, pilipili mbuzi na chumvi kidogo.

“Tafuna kidogo na huu uono!” akasema yule binti.
“Uono?” akauliza Bravo.
“Ndiyo... ni dagaa hawa, aina ya uono, tafunia kidogo na ubwabwa wako, utafurahia ladha yake!” akasema yule binti akitabasamu.
Bravo hakuongea kitu tena.

Yule msichana akaachia tabasamu la mtego, kisha akatamka kwa sauti ya taratibu: “Naitwa Tunu.”
Bravo akatingisha kichwa, kisha akasema: “Nashukuru kukufahamu Tunu, mimi...”
“Tunu akamkatisha: “Najua wewe ni Bravo. Labda nikuambie tu, ni mimi ndiye niliyekuandikia ujumbe WhatsApp.”
Tunu akaondoka zake na kumuacha Bravo amekodoa macho!
Tunu alikuwa “tunu” kwelikweli!

ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 7

NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Yule msichana akaachia tabasamu la mtego, kisha akatamka kwa sauti ya taratibu: “Naitwa Tunu.”
Bravo akatingisha kichwa, kisha akasema: “Nashukuru kukufahamu Tunu, mimi...”
“Tunu akamkatisha: “Najua wewe ni Bravo. Labda nikuambie tu, ni mimi ndiye niliyekuandikia ujumbe WhatsApp.”
Tunu akaondoka zake na kumuacha Bravo amekodoa macho!
Tunu alikuwa “tunu” kwelikweli!
SASA ENDELEA...

JASHO la mahaba lilimtoka Bravo. Mambo yale yalikuwa mapya kabisa kwake. Ni kweli mke wake mpenzi, Viola alikuwa na utundu kwenye mambo ya mapenzi, lakini sasa anakiri kuwa kuna mafundi zaidi ya Viola.
“Yes! Wapo wanaomzidi mke wangu Viola...” akawaza Bravo.
Macho yake bado yalikuwa yanamsindikiza Tunu, ambaye alikuwa hakosei chochote katika kazi aliyojipa mwenyewe, isiyo na mshahara wala marupurupu! Yeye shida yake ilikuwa kumpata Bravo tu, mengine hakuwa na haja nayo kabisa!
Bravo akawa mnyonge.

Ni kweli alikubali kuwa Tunu alikuwa mwanamke mrembo, tena wa kumchanganya moyo wake, lakini hakutaka kuruhusu kabisa Tunu awe sababu ya kumsaliti mke wake.
“...ukisikia bahati mbaya ndiyo kama hizi, lakini unaweza kuhojiwa; ni bahati mbaya gani ambayo unaona dalili zake kama hivi halafu unaingia mkenge? Hapa natakiwa kutumia akili!” akazidi kuwaza.

Ni mawazo kama yalivyo mawazo mengine, lakini moyoni mwake aliona ni kwa namna gani alikuwa akijipiga chenga mwenyewe. Ukweli ni kwamba akili yake haikuwa tayari hata kidogo kuingia katika mtego ule, lakini tatizo ni moyo.
Moyo!
Moyo ulikuwa umeshindwa kuhimili hisia zake. Ingekuwa ni moyo peke yake unafanya kazi bila akili, muda uleule angejilipua na kuingia mzimamzima kwa mtoto Tunu, lakini alijaribu kushindana na akili yake.

Mapishi ya Kitanga yakamchanganya hakika. Alikula wali uliokuwa umebaki kidogo na dagaa aina uono aliokuwa amepewa na Tunu. Alijilamba kuliko kawaida. Alipomaliza kula, alikwenda kwenye sehemu ya kunawa mikono, akanawa na kubaki amesimama akiwa hana uelekeo.
Hajui arudi kwenye kiti au aondoke zake. Akiwa katika tafakuri hiyo, Tunu alikuwa ameshafika mbele yake.

“Asante kwa chakula Tunu,” akasema Bravo, akitoa noti ya elfu tano na kumkabidhi.
“Asante nawe kushukuru, naamini umekifurahia chakula!”
“Sana.”

“Ngoja nikueletee chenji yako.”
“Hapana... kwa huduma uliyonipa, chenji wewe kunywa soda tu!” akasema Bravo akijaribu kuficha hisia zake.
“Waooo! Nashukuru sana Bravo. Siku njema.”
“Nawe pia.”

Bravo akaondoka zake.
Kichwani alikuwa na mawazo mengi sana. Alirudi kwenye ukumbi wa semina, akiwa haelewi yupo kwenye hali gani kihisia. Kuna wakati alihisi hasira, chuki, furaha, mapenzi na wakati mwingine alikuwa katikati! Alikuwa na hali zote hizo kwa pamoja.
Ile anaingiza mguu wake wa kwanza katika geti la kuingilia kwenye ukumbi ule, akasikia mlio wa ujumbe wa WhatsApp ukiingia kwenye simu yake. Mara moja akaufungua.

“Naamini nimejitambulisha kwako vizuri Bravo. Nakuomba basi nawe uwe na moyo wa huruma, upokee hili penzi langu kwako. Usiogopeshwe na umri wangu mdogo... najua anachotaka mwanaume, na ninakuhakikishia nitakupa ipasavyo.
“Wewe mwenyewe utajilaumu ni kwa nini ulichelewa kunifahamu. Nategemea jibu zuri kutoka kwako Bravo, nikiamini thamani ya mapenzi yangu iliyojaa moyoni mwangu, hutaiacha hewani. Asante baba kwa kunipa nafasi ya kukuhudumia chakula cha mchana!”

Alikuwa ni Tunu!
Tunu yuleyule, mtoto wa Kitanga.
*
“Baby unafanya nini?”ulikuwa ujumbe wa Viola kupitia WhatsApp, kwenda kwa Bravo.
“Nipo kitandani!”
“Umeshaoga?”
“Tayari honey.”

“Umeshakula?”
“Ndiyo honey, nimekula!”
“Nini?”
“Ugali makange ya kuku.”

“Mh! Umekula chakula kizuri sana, kwanini hukuniita wakati wa kula? Umeanza lini huo uchoyo?” Viola akamtumia ujumbe huo akiambatanisha na emoji inayomwonyesha ana huzuni.
“Sorry kipenzi!” akajibu Bravo.
“Baby naweza kukuomba kitu?” Viola aliandika.
“Ndiyo mpenzi.”
“Nipigie kwa Video Call please.”

“Honey leo nimechoka sana, siwezi kuongea sana, nipe nafasi nilale mpenzi,” ulikuwa ujumbe wa Bravo.
Kwa Viola lilikuwa jibu la ajabu kuliko kawaida. Bravo leo hii anasema amechoka kuongea naye? Moyo wake ulimuuma kuliko kawaida.
“Nimesoma vizuri haya maandishi au macho yangu yana hitilafu?” akauliza Viola akiugulia maumivu makali moyoni mwake.
“Baby ni uchovu tu, hakuna kingine.”

“Sasa nisikilize Bravo, hutaona meseji nyingine kutoka kwangu, nasubiri unipigie kwa Video Call sasa hivi... bye” ujumbe huo kutoka kwa Viola ulisema.
Bravo akachanganyikiwa!
Akiwa katikati ya tafakuri hiyo, ujumbe mwingine wa WhatsApp ukaingia. Aliamini ulitoka kwa mkewe Viola, mara moja akatazama simu yake. Hakuwa Viola, alikuwa ni Tunu.

ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 8

NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Nimesoma vizuri haya maandishi au macho yangu yana hitilafu?” akauliza Viola akiugulia maumivu makali moyoni mwake.
“Baby ni uchovu tu, hakuna kingine.”
“Sasa nisikilize Bravo, hutaona meseji nyingine kutoka kwangu, nasubiri unipigie kwa Video Call sasa hivi... bye” ujumbe huo kutoka kwa Viola ulisema.
Bravo akachanganyikiwa!
Akiwa katikati ya tafakuri hiyo, ujumbe mwingine wa WhatsApp ukaingia. Aliamini ulitoka kwa mkewe Viola, mara moja akatazama simu yake. Hakuwa Viola, alikuwa ni Tunu.
SASA ENDELEA...

BRAVO alivuta pumzi ndefu sana, kisha akazishusha taratibu kabisa! Alitamani kusikia anachosema Tunu. Katika hali ya kushangaza sana, tayari alikuwa ameshaanza kumzoea Tunu ghafla. Kuna wakati aliona kabisa alikuwa akikosa kitu fulani muhimu.

Lakini wakati huohuo alikuwa kwenye mawazo juu ya mke wake Viola. Moyo wake ulimuuma kuona anakosana na mkewe. Ni kawaida kuingia kwenye migongano midogo midogo, lakini safari hii Viola alionekana kukasirika sana.
Kuna nini? Akawaza.
“Lakini na mimi nimekosea,” akajiambia mwenyewe.

Hakuwa na la kufanya zaidi ya kuanza kuusoma ujumbe ule kutoka kwa Tunu. Tunu aliandika maneno matamu sana. Yaliyomsisimua na kuufurahisha moyo wake.
“Najua umechoka sana Bravo, pole sana kwa kazi za kutwa nzima. Nakushauri oga kwa maji ya vuguvugu, jipake sabuni nyingi mwilini, kisha iache itulie kwa dakika moja, halafu usuuze mwili wako. Utajisikia vizuri. Nitafurahi ukiniambia chakula utachohitaji kula kesho. Ulale unono Bravo,” ilikuwa ni meseji ya Tunu.

Kwa mara ya kwanza, Bravo alihisi msisimko kutokana na meseji ya Tunu. Alitamani kumjibu, tena maneno yaliyojaa mahaba mazito, lakini wakati huohuo alitamani kumpigia mkewe Viola ili kuweka mambo sawa.
Aanze na nani?
Hakujua!
Bravo alibaki njia panda!
“Lazima niwe na maamuzi,” akawaza.

“Natakiwa kujua nani zaidi? Halafu najiuliza maswali ya kitoto kabisa... nani zaidi kati ya mke wangu na Tunu? Kwenye nini? Viola ndiyo zaidi kwa hali yoyote ile,” akawaza akijipanga ili kumpigia mke wake.
Ni kweli alitakiwa kuweka mambo sawa kwa mkewe, ambaye ndoa yao ilikuwa changa kabisa. Hakutaka kumpa Tunu nafasi kabisa. Kitendo cha kuacha mpenyo kwake na kumpa nafasi, kungeleta shida katika ndoa yake, jambo ambalo hakuwa tayari kabisa litokee.

Mara moja akaingia kwenye upande wa kupiga simu ya video, akampigia mkewe. Bravo alikuwa kitandani, amelaza kichwa chake juu ya mto. Simu ilikuwa mbele yake, akijitazama mwenyewe kupitia kioo chake, akisubiri kumuona mkewe, wazungumze.
Simu iliita kwa muda mrefu, kisha ikakatika.
Bravo akapiga tena, safari hii iliita mara moja tu, Viola akapokea. Viola alionekana akiwa amekaa kwenye kochi lililokuwa chumbani kwake, uso wake ulikuwa umelowana kwa machozi!

“Viola kwa nini unalia mpenzi?” akasema Bravo akiwa na maumivu moyoni mwake.
Viola hakujibu!
“Si nakuuliza mama? Nini shida?” akauliza tena.
“Kwahiyo unajifanya hujui?” akauliza Viola kwa sauti ya kudeka lakini hasira ikionekana ndani yake.
“Niambie basi mpenzi.”

“Yaani leo hii Bravo unakataa kuongea na mimi, unasema umechoka? Mimi nakuchosha Bravo? Kuongea na mimi kunakuchosha?” akauliza Viola.
“Mama nakuomba usinielewe vibaya. Naomba hayo unisamehe yaishe. Lakini ukweli ni kwamba nimechoka sana mama, si unaona nipo kitandani kabisa!”
“Lakini sijapenda kauli zako Braavo.”
“Najua ndiyo maana nakuomba msamaha mpenzi wangu, sitarudia tena!”
“Kweli?”
“Hakika mpenzi wangu.”

Kidogo Viola akaelewa. Akafuta machozi yake usoni, kisha akamwambia Bravo: “Au upo na mchepuko humo chumbani?”
“Mchepuko utokee wapi mama? Mimi nipo njia kuu na wewe unajua wazi kabisa,” akasema Bravo.
“Nataka kuhakikisha.”
“Kivipi sasa?”

“Sasa kama umemfungia chooni?”
“Kwahiyo ulikusudia kusemaje mama?”
“Nataka uende chooni na hiyo simu, nione kweli kama hakuna mtu!”
Bravo hakujibu kitu zaidi ya kutoa shuka, akainuka pale kitandani na kuanza kutembea kuelekea chooni. Akafungua mlango na kuingia ndani ya choo hicho, akatembeza kamera pande zote za choo hicho. Hapakuwa na mtu!

Viola akacheka sana, akasema: “Masikini pole mpenzi wangu, nimekusumbua bure. Lala mwaya.”
“Usiku mwema nawe.”
“Sitaki.”
“Hutaki nini?”
“Nataka mpaka nikuone umejifunika shuka kabisa.”
Bravo hakuwa na kufanya zaidi ya kupanda kitandani, akajifunika shuka, kisha akamwambia Viola: “Umeridhika?”
“Kabisa kipenzi sasa, zima taa.”

“Mh! Wewe... haya bwana,” akasema Bravo, huku akinyoosha mkono na kushika swichi iliyokuwa inaning’inia pembeni kwa kitanda, kisha akazima taa! Kukawa giza.
“Sasa kata simu ulale!”
Bravo akakata simu kweli. Akiwa anataka kulala, akaona simu ya Tunu. Naye amepiga kwa video.
“Tunu naye... jamani mbona mtaniua nyie viumbe!” akawaza kichwani mwake, akiwa anaikodolea macho ile simu.

ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 9
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Bravo akakata simu kweli. Akiwa anataka kulala, akaona simu ya Tunu. Naye amepiga kwa video.
“Tunu naye... jamani mbona mtaniua nyie viumbe!” akawaza kichwani mwake, akiwa anaikodolea macho ile simu.
SASA ENDELEA...
ILIKUWA ni video call kutoka kwa Tunu, ambaye alionekana wazi alitaka kuzungumza na Bravo huku wanaonana. Bravo alipata wakati mgumu.
Katika maisha yake yote, hakuwahi kuingia kwenye mtego mkali wa kihisia kama huo. Alimpenda sana mke wake Viola. Alitii na kuheshimu hisia zake siku zote. Kauli ya mkewe kuhusiana na penzi lao ilikuwa sawa na sheria.
Ndivyo walivyojiwekea na wote walitii. Waliishi katika ulimwengu wa tofauti kabisa kwenye mapenzi yao shatashata. Viola alimwambia alale kitandani, akalala; akamwambia azime taa, akazima.
Alimwambia akate simu ili alale, akafanya hivyo. Na sasa anapigiwa simu na Tunu, mtoto yule mwenye maneno matamu ya kumtoa nyoka pangoni. Alipata wakati mgumu sana.
Akiwa katika mawazo hayo, simu ilikatika. Bravo akaitupa pembeni, mapigo ya moyo wake yakienda kasi kama mwanariadha aliyemaliza mbio ndefu za Marathon.
“Kwanini majaribu ya aina hii? Au nichepuke mara moja tu kisha nirudi kwa mke wangu?” akawaza Bravo.
Akiendelea kuwaza hivyo, simu ikaanza kuita tena. Akatupa macho yake kwenye kioo cha simu. Alikuwa Tunu.
“Dah! Nimekamatika mimi...” akajisemea moyoni mwake, akiangalia simu ikiendelea kuita.
“Ngoja nimsikilize bwana... Waswahili wanasema, kubali wito kataa neno. Nimsikilize tu, halafu nitapima kama anayosema yana maana au niyapuuze,” akajisemea Bravo.
Alijua nia ya Tunu, alitaka wakati wakizungumza wawe wanaonana. Akanyoosha mkono wake hadi kwenye swichi, akawasha taa, kisha mara moja akapokea simu.
“Bravo baba, pole mwaya...” alikuwa ni Tunu akizungumza kwenye simu, Bravo akimwangalia.
“Asante, habari ya kushinda?”
“Nzuri, shikamoo!”
“Marahaba.”
“...na shikamoo ananipa, duh!” akawaza Bravo.
Bravo alipata wakati mgumu sana kumwangalia Tunu ambaye alikuwa amekaa kwenye kochi wakati akizungumza. Alivaa kanga moja kifuani mwake. Kanga nyepesi ya India!
Alijikuta akibabaika kuzungumza. Alikuwa kimya akimtazama Tunu ambaye uzuri wake uliuvuruga ubonngo wake. Alikaa mkao uliotibua nyongo yake ya mahaba.
“Nakuona mwenyewe umejichokea masikini!” akasema Tunu.
“Ni kweli, nilikuwa busy sana leo.”
“Bravo nimekupigia kwa sababu ya mambo mawili.”
“Niambie Tunu.”
“Kwanza nataka kujua kesho utapenda kula nini?”
“La pili?”
“Nataka ujibu kwanza la kwanza.”
“Ok! Nitakula wali.”
“Mboga?”
“Yoyote utakayopenda wewe.”
“Sawa.”
“Sasa niambie jambo la pili.”
“Bravo nataka uniambie ukweli wa jambo moja. Hivi unajisikiaje mimi kukueleza ukweli wa moyo wangu?” akauliza Tunu kwa sauti laini, akirembua macho yake.
“Kiukweli umenipa wakati mgumu sana.”
“Najua huwa siyo rahisi mwanamke kumtongoza mwanaume. Ni ngumu sana, hata kwangu ilikuwa ngumu, lakini naomba unielewe. Nimesukumwa na mapenzi yangu ya dhati kwako.
“Sijawahi kumtongoza mwanaume hata siku moja, lakini kwako nimelazimika, maana kila dalili nilikuonyesha lakini sikuona kama uliligundua hilo. Naomba uwe muelewa na katika hili, angalia zaidi moyo wangu... unateketea Bravo,” akasema Tunu, macho yake yakianza kulengwa na machozi.
“Kwani unataka nini kwangu Tunu, hebu kuwa wazi.”
“Najua unachomaanisha Bravo. Nafahamu fika kuwa utakuwa umeoa, maana hata kidoleni mwako naona pete ya ndoa. Ninachotaka kwako ni mapenzi. Nataka penzi lako Bravo, lakini pia nataka wewe unipende.
“Kwangu ni fahari sana kupendwa na wewe. Hilo tu, naomba usiniangushe tafadhali. Kitu ninachokuhakikishia, hutajuta kuwa nami, zaidi utajilaumu kwa kuchelewa kunijua!” akasema Tunu kwa kujiamini.
“Unataka lini?”
“Hata sasa hivi,” akasema Tunu, kisha akasimama na kuanza kujionyesha mwili wake wote kupitia simu.
Bravo alichanganyikiwa!
“Sasa hivi haiwezekani, tufanye kesho.”
“Sawa. Lakini una hakika upo serious Bravo?”
“Katika hili sina utani, namaanisha.”
“Sijui nieleze ni kwa kiasi gani umenifurahisha leo. Asante sana mpenzi. Narudia tena kukuambia, hutajuta Bravo. Ulale salama baba. Sasa na mimi nina amani moyoni mwangu,” akasema
Tunu kwa hisia, kisha akakata simu.
Bravo alibaki ameganda anaitazama ile simu. Alijaribu kuvuta picha, akimrudisha Tunu mbele ya macho yake, lakini hilo halikuwezekana. Tunu alimchanganya vya kutosha!
“Nimechoka na haya mateso, mwishowe naweza nikaonekana siyo mzima bure. Acha nione kuna nini, halafu kwa nini anajisifia sana. Hebu ngoja nijionee,” akawaza Bravo, kisha akazima taa na kulala.
Kwa Bravo, kesho ilikuwa mbali sana!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 10
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Bravo alibaki ameganda anaitazama ile simu. Alijaribu kuvuta picha, akimrudisha Tunu mbele ya macho yake, lakini hilo halikuwezekana. Tunu alimchanganya vya kutosha!
“Nimechoka na haya mateso, mwishowe naweza nikaonekana siyo mzima bure. Acha nione kuna nini, halafu kwa nini anajisifia sana. Hebu ngoja nijionee,” akawaza Bravo, kisha akazima taa na kulala.
Kwa Bravo, kesho ilikuwa mbali sana!
SASA ENDELEA...
KUPATA usingizi kilikuwa kibarua kingine, picha ya Tunu ilimsumbua usiku mzima. Muda wote alikuwa akiifikiria kesho namna itakavyokuwa. Kwa namna Tunu alivyokuwa akizungumza ni wazi kuwa alikuwa mtaalamu kwelikweli!
Alikuwa na shauku ya kuona utaalamu huo ambao alikuwa akijisifia kila wakati. Alitaka kuelewa sababu ya mara zote kukazia “hutajutia uamuzi wako, zaidi utajilaumu kwa nini ulichelewa kunifahamu.”
Kauli za Tunu zilimuhamasisha sana. Kwa tabu sana, saa tisa kasoro za usiku, ndipo usingizi ulimpitia. Asubuhi kama kawaida alitakiwa kuamka na kuwahi kwenye semina kama utaratibu ulivyokuwa.
Aliamka saa moja juu ya alama, akaingia bafuni kuoga, kisha akaelekea sehemu maalum ya kupata kifungua kinywa, akahudumiwa.
Saa mbili kamili alikuwa nje ya hoteli aliyofikia, akaingia kwenye gari maalum la wafanyakazi na kupelekwa moja kwa moja kwenye eneo la mkutano. Akiwa kwenye gari ndipo alipopata muda wa kuangalia simu yake.
Kwanza alifungua data za simu yake, akasikia meseji zikiingia kwa fujo kwenye simu yake. Baada ya dakika mbili, akaingia WhatsApp ili kuona meseji zilizoingia. Aliachana na makundi mbalimbali katika mtandao huo wa kijamii, akawa makini na meseji za mtu mmoja mmoja.
Alikutana na meseji za watu watano; rafiki zake Charles, Muddy na Linus, kisha meseji mbili zilitoka kwa Tunu na Viola.
Upinzani mwingine ukaibuka! Aanze kusoma meseji ya nani kati yao? Alitamani kusoma meseji ya mtoto wa Kitanga, lakini pia alitamani kujua mkewe alimwandikia nini!
“Kweli mshika mawili, moja humponyoka! Walitunga huu msemo, waliona mbali sana. Nadhani waliniona hata mimi,” akawaza Bravo.
Akaamua kufanya uamuzi!
Mke kwanza bwana! Akawaza akifungua ujumbe wa mkewe, Viola. Mkewe huyo alikuwa ameamka naye siku hiyo.
Ujumbe wa Viola ulisema: “Morning baby... pole na uchovu. Naamini umeamka salama ukiwa mzima wa afya njema mpenzi. Naomba tu nikupe ratiba yako mpenzi.
“Naomba ukiwa unakula chakula cha mchana, unipigie kwa video call tuzungumze. Ukiwa unatoka kazini, pia unipigie kwa video call, ukifika hotelini pia ufanye hivyo hivyo, hadi muda wa kulala.
“Nataka siku nzima ya leo, kila ratiba yako nione unavyoifanya kupitia video call. Naamini utafanya hivyo. Nakutakia kazi njema. Nakupenda sana mume wangu.”
Bravo alirudia kusoma ile meseji mara mbili. Haikuwa na maneno ya mapenzi zaidi ya “nakupenda sana mume wangu”, mistari mingine yote ilijaa amri.
Bravo hakupenda!
Kwa mara ya kwanza alimkosoa mke wake... akamuona hayupo romantic kwa meseji zake zenye amri.
Hakumjibu!
“Hivi nimeona mke au mtu wa kuniamrisha? Ananipa maelekezo utadhani nipo jeshini?” akawaza Bravo.
“Hebu ngoja nione meseji ya Tunu,” akawaza akifungua meseji ya Tunu.
Tunu alifunguka kimahaba!
Meseji ya Tunu ilisomeka: “Shikamoo Bravo. Naamini umeamka salama mpenzi. Usisahau mchana nitakutayarishia chakula kizuri sana kama ulivyochagua mwenyewe jana.
“Uwahi kuja kula mpenzi, halafu usisahau ahadi yetu ya leo jioni. Najiona mwenye bahati sana kuwa mikononi mwa mwanaume makini kama wewe. Mwaaaaa... kazi njema laazizi.”
Bravo alirudia kusoma ile meseji mara mbilimbili, maandishi yale yaliuburudisha moyo wake. Ni kweli sasa alishaanza kujilaumu kwa kuchelewa kwake kumjua Tunu.
“Nimeamka salama mpenzi wangu Tunu, asante sana kwa ujumbe mzuri kabisa. Mchana nitakuja kula na jioni tutakuwa pamoja, usiwe na shaka kabisa na hilo,” Bravo akamjibu Tunu haraka.
“Usijali Bravo, nipo kwa ajili yako. Napenda kujua mahali tutakapokutana!” ilikuwa meseji kutoka kwa Tunu.
“Nitakuelekeza uje hotelini kwangu nilipofikia.”
“Hapana, sitaki hotelini.”
“Kumbe unataka wapi tena Tunu wangu?”
“Nataka nyumbani.”
“Nyumbani kivipi sasa Tunu? Unamaanisha kwenu?”
“Hapana, kwangu. Ninacho chumba chagu maeneo ya Chuda. Tafadhali naomba usikatae, uje kwangu! Nitakuandalia vitu vizuri sana, mwenyewe utapenda!”
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 11
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Bravo alirudia kusoma ile meseji mara mbili. Haikuwa na maneno ya mapenzi zaidi ya “nakupenda sana mume wangu”, mistari mingine yote ilijaa amri.
Bravo hakupenda!
SASA ENDELEA...
ALIJISIKIA vibaya sana kuona mkewe mpenzi akiwa ana swaga nzuri za mapenzi. Siyo kwamba mkewe alibadilika kwa kiasi hicho, ila aliona tofauti baada ya kuanza kuwasiliana na Tunu, mtoto wa Kitanga.
Kwa mara ya kwanza alimkosoa mke wake... akamuona hayupo romantic kwa meseji zake zenye amri.
Hakumjibu!
“Hivi nimeona mke au mtu wa kuniamrisha? Ananipa maelekezo utadhani nipo jeshini?” akawaza Bravo.
“Hebu ngoja nione meseji ya Tunu,” akawaza akifungua meseji ya Tunu.
Tunu alifunguka kimahaba!
Meseji ya Tunu ilisomeka: “Shikamoo Bravo. Naamini umeamka salama mpenzi. Usisahau mchana nitakutayarishia chakula kizuri sana kama ulivyochagua mwenyewe jana.
“Uwahi kuja kula mpenzi, halafu usisahau ahadi yetu ya leo jioni. Najiona mwenye bahati sana kuwa mikononi mwa mwanaume makini kama wewe. Mwaaaaa... kazi njema laazizi.”
Bravo alirudia kusoma ile meseji mara mbilimbili, maandishi yale yaliuburudisha moyo wake. Ni kweli sasa alishaanza kujilaumu kwa kuchelewa kwake kumjua Tunu.
“Nimeamka salama mpenzi wangu Tunu, asante sana kwa ujumbe mzuri kabisa. Mchana nitakuja kula na jioni tutakuwa pamoja, usiwe na shaka kabisa na hilo,” Bravo akamjibu Tunu haraka.
“Usijali Bravo, nipo kwa ajili yako. Napenda kujua mahali tutakapokutana!” ilikuwa meseji kutoka kwa Tunu.
“Nitakuelekeza uje hotelini kwangu nilipofikia.”
“Hapana, sitaki hotelini.”
“Kumbe unataka wapi tena Tunu wangu?”
“Nataka nyumbani.”
“Nyumbani kivipi sasa Tunu? Unamaanisha kwenu?”
“Hapana, kwangu. Ninacho chumba chagu maeneo ya Chuda. Tafadhali naomba usikate, uje kwangu! Nitakuandalia vitu vizuri sana, mwenyewe utapenda!”
“Kweli?”
“Nakuhakikishia Bravo wangu, hutajuta!”
Bravo alichanganyikiwa hakika. Alishindwa kuelewa ni kwanini kila mara Tunu alipenda kumwambia kuwa hatajutia. Alitamani sana kufahamu hicho anachoringia Tunu.
Ni kweli alikuwa na kazi ngumu ya kuwaridhisha wanawake wote wawili kwa wakati mmoja, lakini Bravo alishaamua kumridhisha mmoja tu, ambaye ni Tunu. Sasa aliweka nia kwamba, hatawasiliana na mkewe kwa siku nzima ili apate wasanii wa kujinafasi na Tunu wake.
Akaamua kuzima simu.
***
Bravo alizima simu yake baada ya kuwasiliana na Tunu na kumweleza kuhusu jambo hilo. Alishamwelekeza mpaka nyumbani kwake, mchana alipokwenda kupata chakula.
Jioni alipotoka kwenye semina, alikwenda hotelini, akajitayarisha kisha mishale ya saa 2 usiku, akakodi taksi iliyompeleka mpaka Chuda. Alipofika sehemu aliyoelekezwa, Bravo aliwasha simu na kuwasiliana na Tunu ambaye hakuwa mbali na eneo hilo.
Akamchukua na kwenda naye nyumbani kwake. Hata hivyo kimsingi haikuwa nyumba, bali chumba kimoja. Ni chumba kimoja, lakini umaridadi wake ulikuwa siyo wa kawaida.
Kilikuwa ni chumba kilichotunzwa vizuri, kisafi, kinachovutia. Picha linaanza; ile ameingia ndani ya chumba hicho, macho yake yakatua mezani ambapo kulikuwa na chakula kilichofunikwa na kawa yenye maandishi yaliyosomeka: Karibu mpenzi ujilie vyako, ufurahi moyoni.
Akiwa bado ametaharuki, macho yake yakahamia kwenye kitanda ambacho kilitandikwa na shuka jeupe lililodariziwa maneno yaliyosomeka: Raha yako iko kwangu.
Bravo alikiri alikuwa ameingia kwenye ulimwengu mpya kabisa wa mapenzi. Akiwa bado anatafakari cha kuzungumza, akakutana na sauti laini ya Tunu ikimwambia: “Honey utakula kwanza ndiyo ule au ule kwanza halafu ndiyo utakula?”
Bravo alichanganyikiwa!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 12
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Bravo alikiri alikuwa ameingia kwenye ulimwengu mpya kabisa wa mapenzi. Akiwa bado anatafakari cha kuzungumza, akakutana na sauti laini ya Tunu ikimwambia: “Honey utakula kwanza ndiyo ule au ule kwanza halafu ndiyo utakula?”
Bravo alichanganyikiwa!
SASA ENDELEA...
BRAVO alitoa maksi nyingine kwa Tunu. Licha ya uzuri wa chumba, mpangilio uliomvutia, alichanganywa sana na lugha tamu ya mahaba. Alikutana na mwanamke anayejua kuchezea lugha. Kuambiwa atakula kwanza ndiyo ale au ale kwanza halafu ndiyo atakula kulimchanganya kwa hakika.
Sekunde chache baadaye alielewa alichomaanisha Tunu. Msichana yule alimaanisha mahaba. Alitamka chakula akimaanisha mlo, lakini pia chakula kwa maana ile nyingine.
“Tunu...” akaita Bravo.
“Yes honey.”
“Sijakuelewa mama, hebu nifafanulie basi mwenzako, mimi mtoto wa Bara, haya mambo ya Pwani nitayajuaje jamani?” akasema Bravo lakini kichwani mwake akijua maana.
“Honey wewe sema, utakula kwanza ndiyo ule, au ule kwanza halafu ndiyo utakula?” akasema Tunu kwa sauti iliyojaa mahaba.
“Nadhani nile kwanza halafu ndiyo nitakula!”
“Sawa... nenda basi kitandani...” akasema Tunu kwa sauti yake ileile iliyojaa mahaba.
Kama kondoo anayekwenda kuchinjwa, Bravo alijongea hadi kitandani, akaketi akisubiri amri kutoka kwa Tunu.
“Nisubiri...” akasema Tunu kwa sauti ndogo.
Tunu alitoka nje, aliporejea alikuwa na mabeseni mawili makubwa. Akayaweka chini, moja akamimina maji nusu, jingine likawa tupu. Alikuwa na ndoo ndogo iliyokuwa na maji na kopo lake.
Binti huyo mrembo akasimama kisha akasogea pembeni, akasaula gauni lake aina ya kijora, kisha akavaa kanga moja kifuani mwake. Akamfuata Bravo pale kitandani alipokuwa amekaa. Akaanza kumvua soksi zake.
Bravo hakushangaa.
Alipoanza kumtoa shati, Bravo akashtuka kidogo na kumkataza Tunu. Lilikuwa jambo jipya kabisa kwake.
“Shiiiiiiiii.... niache tafadhali,” akasema Tunu ambaye ndani ya dakika moja alifanikiwa kukamilisha zoezi zima.
“Shuka chini,” Tunu akamuamrisha.
Bravo alikuwa kama mtumwa anayesikika kila maelekezo kutoka kwa bosi wake. Tunu akamwelekeza Bravo akae kwenye beseni moja, lililokuwa na maji kidogo.
“Mimi nikae hapo, si nitavunja?” Bravo akahamaki.
“Kaa bwana wewe,” akasema Tunu.
Bravo akaketi kwa woga, lakini Tunu akamwambia atulie na asiwe na wasiwasi. Miguu yake aliinua na kuiweka kwenye beseni la upande wa pili lililokuwa halina maji.
Akiwa pale kwenye beseni, Tunu akaanza kumwogesha Bravo kama mtoto mdogo. Maji ya vuguvugu yaliyonakshiwa na hiliki yalianza kumiminika mwilini kwa Bravo. Alihisi msisimko wa aina yake.
Akamsugua mwili mzima na dodoki laini kisha akamsuuza na maji safi. Zoezi lililofuata baada ya hapo ilikuwa ni kumsugua miguu yake kwa jiwe maalumu. Bravo alihisi kama anatekenywa, lakini ukweli ni kwamba alikuwa akisuguliwa miguu.
Alihisi msisimko wa aina yake. Alifanyia kitu ambacho mke wake Viola hakuwahi kumfanyia tangu amemfahamu! Aliinuliwa pale kwenye beseni na kukaushwa kwa taulo kisha akapakwa mafuta ya nazi na kuwa laini kabisa.
Baada ya hapo, Tunu alikwenda kumwaga maji nje, aliporudi naye akaingia bafuni kuoga. Baada ya kuoga alimfuata Brano na kumwonyesha ni kwa nini alimwambia atajuta kuchelewa kumfahamu!
Ile picha linaanza, kijasho jembamba kilikuwa kinamtoka Bravo wa watu! Hakuzoea mambo hayo! Maandalizi kabla ya mechi yalimtisha, maana hayakuwa ya kitoto.
Wote wakiwa tayari kulianzisha, simu ya Bravo ikaita. Tunu akainuka na kumletea...
“Baby kwani ni nani anapiga?” Bravo akauliza.
“Mkeo.”
“Achana naye. Wewe njoo tule raha zetu,” akasema Bravo akihisi anacheleweshwa kuingia kwenye ulimwengu mwingine usiokuwa na shida za duniani.
Kazi iliyoendelea hapo, ilikuwa haielezeki. Kweli Bravo akajuta kuchelewa kumfahamu Tunu!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 13
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
Wote wakiwa tayari kulianzisha, simu ya Bravo ikaita. Tunu akainuka na kumletea...
“Baby kwani ni nani anapiga?” Bravo akauliza.
“Mkeo.”
“Achana naye. Wewe njoo tule raha zetu,” akasema Bravo akihisi anacheleweshwa kuingia kwenye ulimwengu mwingine usiokuwa na shida za duniani.
SASA ENDELEA...
LILIKUWA kosa la kiufundi, ambalo Bravo hakulipenda kwa hakika. Baada ya kuingia chumbani kwa Tunu, aliamua kuwasha simu kwa muda ili amtumie meseji rafiki yake, kumtaarifu kuwa siku hiyo aende kula peke yake kwa sababu alipewa ofa na “mwenyeji wake”.
Alifanya hivyo na baada ya hapo akasahau kuzima simu. Hakutaka kuwasiliana na mtu yeyote, hasa Viola.
Yes! Viola mke wake.
Hakutaka kuona simu, meseji, wala video call! Kwa wakati huu, Viola hakuwa na thamani tena. Bali Tunu, binti mbichi mwenye umri wa miaka 20 tu, alimwingiza katika ulimwengu mwingine kabisa.
“Baby hebu lete hiyo simu,” akasema Bravo, Tunu akatii.
Bravo akaizimia mbali, kisha akairusha kwenye kochi.
“Watu wengine wanataka kutuharibia starehe zetu, njoo mpenzi wangu!” akasema Bravo.
Kazi iliyoendelea hapo, ilikuwa haielezeki. Kweli Bravo akajuta kuchelewa kumfahamu Tunu! Aliendeshwa kama gari bovu! Hakuwahi kuelewa kama duniani kuna mambo mazuri kiasi hicho katika ulimwengu wa mapenzi.
Ni ngumu kueleza yaliyotokea, lakini kwa Bravo kama alikuwa akifanyishwa mazoezi, maana hakuna kiungo ambacho hakikufanya kazi katika zoezi zima lile.
Bravo alimwangushia mabusu motomoto akiwa haamini alichofanyiwa. Kwa furaha ya mahaba, Bravo alimwaga machozi.
“Tunu mpenzi wangu...” akaita Bravo akitweta.
“Abee mpenzi.”
“Asante sana mama kwa haya yote uliyonifanyia. Kwakweli nakiri, na utu uzima huu, sijawahi kukutana na kitu hiki nilichokikuta kwako!”
“Kweli baba?”
“Kabisa.”
“Bravo hii ni rasharasha, mvua inakuja baba. Mbona mwenyewe utafurahi!” akasema Tunu kwa sauti ya mahaba iliyojaa lafudhi ya Kitanga, akitamka maneno sanifu ya Kiswahili.
“Samahani kwa swali nitakalokuuliza.”
“Uliza tu.”
“Haya mambo umejifunzia wapi? Una wanaume wangapi na nani anakulipia hiki chumba hapa?” Bravo akajikuta anauliza maswali matatu, badala ya moja aliloahidi kuuliza.
“Bravo mimi mtoto wa Kitanga asili, mtoto wa Usambaani, nimechezwa ngoma, nimefundwa nikafundika. Najua maana ya kumfanya mwanaume ajisikie mwenye bahati anapokutana na mwanamke.
“Laazizi wangu, huwezi kuamini mimi kwa sasa nina mwanaume mmoja tu; chumba nalipa mwenyewe, ninacholipwa kwenye biashara ya chakula ndicho ninachotumia na kinanitosha,” akasema Tunu.
Majibu yote ni kama Bravo hakuyasikia, yeye alisikia lile la kuwa na mwanaume mmoja tu. Akatoa macho: “Huyo mwanaume achana naye mara moja, mimi nipo tayari kwa kila kitu. Nitakupa chochote.”
Bravo alijaa!
“Mbona atakoma safari hii! Hapa ameingia penyewe,” akawaza kichwani mwake Tunu.
“Kwa hiyo baby unataka nikuache?”
“Uniache mimi? Acha hizo bwana Tunu.”
“Sasa si umesema niachane na mwanaume niliyenaye?”
“Ndiyo!”
“Sina mwanaume mwingine zaidi yako. Ni wewe peke yako laazizi wa moyo wangu,” akasema Tunu.
Bravo kijasho kikamchuruzika. Alikuwa na kijasho cha awali kilichosababishwa na yale mambo, lakini cha safari hii kilisababishwa na jibu zuri, lililompa faraja ya moyo wake.
Bravo alijihisi mwanaume kwelikweli!
“Asante mpenzi wangu, umenipa maneno mazuri sana leo.”
“Usijali malkia wangu, moyo wangu nimeukabidhi kwako. Utakula vyenye ladha zote kutoka kwangu. Karibu Tanga kipenzi,” akasema Tunu, sasa akichukua taulo jepesi, dogo na kuanza kumkausha Bravo jasho.
“Twende bafuni,” akasema Tunu.
Bravo akaitikia kwa kichwa. Alishuka pale kitandani akiwa kama alivyokuwa wakati wa kazi ileeee! Hakuruhusiwa hata kujifunga taulo. Alielekezwa bafuni, wakaingia wote na Tunu. Kulikuwa na bomba la mvua, lakini Tunu hakutaka watumie hilo.
Kulikuwa na maji special!
Alikuwa na maji kwenye ndoo kubwa, tayari yalikuwa ya moto. Akachanganya katika ndoo mbili ndogo, akampa moja Bravo, yeye akaweka yake pembeni.
“Endelea kuoga mpenzi,” akasema Tunu.
“Na wewe?”
“Wewe oga laazizi wangu,” akasisitiza, Tunu akibetua midogo yake na kusinzisha macho yake.
Bravo aseme nini!
Akaoga!
Alipotoka bafuni, akakutana na maajabu mengine. Kwanza kitandani kulibadishwa shuka. Lilitandikwa jingine jeupe lililodariziwa vizuri. Lilikuwa na maandishi yanayosomeka: “Raundi ya pili.”
Chini kulitandikwa mkeka, kisha ukafunikiwa na kitenge kizito, halafu kukawa na kipande cha mti ambacho hakukielewa. Kilikuwa kipande cha mti wa manjano na jiwe. Bravo akataka kuuliza kitu, lakini akasita.
Tunu akampokea kwa kumfuta kwa taulo, kisha kama kawaida, akampa mafuta ya nazi, akamkalisha kwenye kochi. Yeye akaingia bafuni kuoga. Aliporudi, akamshika mkono Bravo na kumtaka alale pale chini kwenye kitenge.
Bravo akiwa haelewi kitakachoendelea, Tunu akaanza kusaka kile kipande cha mti wa manjano kwa jiwe. Kilikuwa kitu kigeni kwa Bravo, ambaye alikuwa kimya akisubiria chochote kitakachotokea.
Hakuwa na hiyari na chochote tena.
“Bravo huu unaitwa msio, ulishawahi kusigwa,” Tunu alimuuliza Bravo huku akimalizia kusaga ili apate unga wake.
“Nitajuaje mimi mtu wa bara?” Bravo akasema.
“Haya lala nikusige,” Tunu alisema.
Kwa Bravo yalikuwa mashokolomageni!
Mbona pambe!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI - 14
ILIPOISHIA...
“Bravo huu unaitwa msio, ulishawahi kusigwa,” Tunu alimuuliza Bravo huku akimalizia kusaga ili apate unga wake.
“Nitajuaje mimi mtu wa bara?” Bravo akasema.
“Haya lala nikusige,” Tunu alisema.
Kwa Bravo yalikuwa mashokolomageni!
Mbona pambe!
SASA ENDELEA...
KILA kitu kilikuwa kipya kabisa kwa Bravo. Alikubali kufundishwa na Tunu. Alihiyari pasi na shaka yoyote kuwa Tunu ndiye aliyekuwa dereva wake katika mambo yote na yeye alikuwa abiria.
Kama kondoo anayepelekwa machinjioni, Bravo alijilaza pale kwenye kitenge, kisha mikono laini ya Tunu ikaanza kutembea mwilini mwake!
Msisimko!
Ilikuwa hatari. Katika historia yake, Bravo alikuwa hajawahi kusigwa achilia mbali kufanyiwa massage! Yalikuwa mambo mageni kabisa kwake.
Labda nisiwaache mbali wasomaji wangu; kusiga maana yake ni kukanda mwili. Ila sasa kuna tofauti kubwa sana kati ya kukandwa mwili kisasa kwa kutumia mafuta maalum ya madukani na kusigwa kienyeji!
Tunu alikuwa akifanya kazi yake kwa umakini wa hali ya juu. Ndani ya nusu saa viungo vyote vya Bravo vilikuwa laini.
“Hivi mimi nilichelewea wapi kumjua huyu mtoto? Mbona ataniua kwa raha mimi jamani?” akawaza Bravo, akiinuka pale chini, akisubiri maelekezo mengine.
“Unajisikiaje baby?” Tunu akamwuliza.
“Siwezi kuelezea, ila ukweli ni kwamba najisikia raha ambayo siwezi kuielezea,” akasema Bravo akiwa ameyatuliza macho yake usoni mwa Tunu.
Tunu alikuwa anamwangalia akitabasamu, vijishimo mashavuni mwake vikatokeza na kuzidisha uzuri wake aliojaaliwa.
“Haya sasa tunarudi tena bafuni!”
“Tena?”
“Ndiyo.”
Safari hii mtoto wa watu alikalishwa juu ya kigoda, kisha akaanza kuogeshwa kama mtoto mdogo. Kuna wakati Bravo alijikuta akitaka mambo kutokana na namna alivyokuwa akisisimka, lakini Tunu akamwambia awe mpole kwanza.
Zoezi hilo lilipokamilika, Tunu akamkausha kwa taulo, kisha akamshika mkono hadi kitandani! Hayo mengine niliwaachia wenyewe! Kwa hiyo niseme tu kazi iliyofanyika haikuwa ya kawaida.
***
Viola alichanganyikiwa. Kitendo cha mume wake kutokupatikana kwa muda mrefu kilimchanganya sana. Lakini alikuja kuchanganyikiwa zaidi pale ambapo alipatikana, lakini akampigia, hakupokea kisha baadaye ikazimwa tena.
Alihisi kuna jambo zito limemtokea mume wake. Hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba mume wake alikuwa akirina asali kwenye mzinga. Alihisi alikuwa amepatwa na tatizo.
“Haiwezekani nampigia asipokee simu yangu, halafu baadaye anazima kabisa, huenda kuna tatizo mahali,” akawaza mwenyewe akiwa amejilaza kwenye kochi.
Alirudia kupiga mara kwa mara, lakini simu iliendelea kuwa haipatikani. Lilikuwa jambo lililomchanganya sana. Bahati mbaya hakuwa na namba ya mtu yeyote aliyekuwa kwenye semina na Bravo.
Mshale wa dakika ukazidi kusogea, mara saa tano kamili ikafika! Hapo akaamua kumpigia kwa mara nyingine. Alijiambia kuwa ilikuwa mara ya mwisho kweli. Kwamba baada ya hapo, angeingia chumbani na kulala.
Simu iliita!
“Opffff...” Viola akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu.
Hakuamini macho yake!
***
Baada ya kazi nzito kukamilika, Bravo alikuwa mwepesi kuliko spochi. Alimwangalia Tunu kwa jicho la shukrani, kisha akamwambia: “Wewe mtu utakuja kuniua.”
“Kwa nini baba?” akauliza Tunu.
“Nimekukubali kweli wewe mtoto wa Kitanga.”
“Bravo baba, wewe ni wangu, mimi ni wako. Hapo nimekupa sehemu tu ya raha zilizopo kwangu. Bado kabisa. Muda mwingine uutaelewa namaanisha nini,” alizungumza Tunu kwa sauti yake laini, akiwa amelegeza macho yake.
“Naomba uniruhusu niondoke, acha nikapumzike mapema leo ili kesho niwahi kwenye semina.”
“Sawa mpenzi.”
Bravo akajitayarisha haraka haraka, kuangalia saa iliyokuwa ukutani ilikuwa tayari saa nne na dakika zake usiku. Alitakiwa kuondoka haraka sana pale Chuda, nyumbani kwa Tunu.
Alipata mtihani mwingine mkubwa. Alifahamu dhahiri kuwa alitakiwa kumpatia fedha kidogo kama shukrani kwa ukarimu aliotendewa! Lakini hakuelewa alipaswa kutoa kiasi gani.
Alifungua pochi yake iliyokuwa imenona, kwa harakaharaka akahesabu noti kumi za elfu kumi kumi! Zilikuwa laki moja na kumkabidhi Tunu.
“Za nini?” Tunu akauliza akiwa ameshazichukua.
“Fanya matumizi yako ya hapa na pale!”
“Baby ndiyo zote hizi?”
“Ndiyo usijali. Kwa sababu umenifurahisha, lazima na mimi nikufurahishe!” akasema Bravo akiachia tabasamu mwanana.
Ilikuwa tofauti kabisa kwa Tunu. Yeye alichomoa noti tatu tu, kiasi cha Tsh 30,000 kisha akamrudishia nyingine Bravo.
“Hizi zinanitosha baby, hizi chukua tu,” akasema Tunu akimpa zile fedha Bravo ambaye hakupokea.
Ilikuwa kama ndoto!
Mwanamke anakataa pesa! Bravo akajiuliza kichwani mwake. Ilikuwa mara yake ya kwanza maishani mwake kukutana na mwanamke wa aina ya Tunu.
“Hapana siwezi kuzichukua, naomba zikusaidie tafadhali mpenzi,” akasema Bravo.
“Hapana Bravo. Mimi sijiuzi, nikichukua hiyo pesa ni kama umeninunua. Hii 30 yenyewe nachukua kukuridhisha tu. Wewe ni wangu, isitoshe una familia, hutakiwi kutumia fedha hovyo.
“Nikiwa na shida na pesa nitakuambia, lakini kwa sasa kwa kweli sina kazi nazo. Naomba tu uzichukue!” akasema Tunu.
“Mh! Hata Viola hayupo hivi... mwanamke anakurudishia pesa? Mwanamke wa nje anajali familia yangu? Basi kama ni hivyo ni afadhali ingewakuwa huyu ndiyo mke, halafu Viola ndiyo awe nyumba ndogo.... haya mambo ni mageni kabisa kwangu,” akawaza Bravo akichukua zile noti.
Tunu akamvuta Bravo kifuani mwake, akamkumbatia kwa nguvu!
Alijuta kumfahamu Tunu!
ITAENDELEA...
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 15
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Hapana siwezi kuzichukua, naomba zikusaidie tafadhali mpenzi,” akasema Bravo.
“Hapana Bravo. Mimi sijiuzi, nikichukua hiyo pesa ni kama umeninunua. Hii 30 yenyewe nachukua kukuridhisha tu. Wewe ni wangu, isitoshe una familia, hutakiwi kutumia fedha hovyo.
“Nikiwa na shida na pesa nitakuambia, lakini kwa sasa kwa kweli sina kazi nazo. Naomba tu uzichukue!” akasema Tunu.
“Mh! Hata Viola hayupo hivi... mwanamke anakurudishia pesa? Mwanamke wa nje anajali familia yangu? Basi kama ni hivyo ni afadhali ingewakuwa huyu ndiyo mke, halafu Viola ndiyo awe nyumba ndogo.... haya mambo ni mageni kabisa kwangu,” akawaza Bravo akichukua zile noti.
Tunu akamvuta Bravo kifuani mwake, akamkumbatia kwa nguvu!
Alijuta kumfahamu Tunu!
SASA ENDELEA...
WALIGANDANA kwa dakika tatu nzima, hakuna aliyechoka kati yao. Muda ulizidi kwenda, hapakuwa na dalili za kuachiana. Lakini Bravo akakumbuka kwamba alitakiwa kuwasiliana na Viola.
Hata kama alikutana na mambo tofauti kwa Tunu, lakini bado nafasi ya mkewe ilikuwa palepale. Alimuachia Tunu, kisha akamwambia: “Nakupenda sana mama, naomba uniruhusu niondoke mpenzi.”
“Sawa baba, nakutakia usiku mwema, uote ndoto njema, niutawale usiku wako kipenzi changu!”
“Asante sana mama.”
Bravo akawasha simu yake, kisha akampigia dereva aliyemfikisha pale kwa Tunu. Akamsubiri kwa dakika tano tu akawa amefika, maana hakuwa mbali sana na eneo la Chuda. Alikuwa Mabanda ya Papa.
Bravo akaondoka!
***
Alipofika hotelini, alijitupa kitandani kwa uchovu mwingi. Bado alikuwa akimtafakari Tunu, mtoto wa Kitanga na mambo yake ya Pwani ambayo yalikaribia kuutibua ubongo wake.
“Kweli sasa nimeamini kuna watu wameumbwa kwa ajili ya mapenzi... Tunu ameumbwa kwa ajili hiyo. Ameumbwa kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume... tena mwanaume mwenyewe naamini ni mimi.
“Kwa umri wake, najua atakuwa hajachezewa sana na manyang’au ya mjini. Bado atakuwa na mengi mazuri ya kuufurahisha moyo wangu. Lazima Tunu aingie kwenye maisha yangu,” akawaza Bravo akiwa kitandani ametulia.
Hakuwa na haja ya kuoga, kila kitu kilifanywa na Tunu chumbani kwake. Akiwa bado anaendelea kuwaza, simu ikaita.
Alipoangalia kwenye kioo, akakutana na jina la Tunu.
“Waoooo! Raha ya moyo wangu ananipigia...” akawaza Bravo akikaa vema kitandani ili aweze kuzungumza na daktari wa moyo wake...
“Halooo baby.”
“Haloooo honey, naamini umefika salama kipenzi changu!” ilikuwa sauti laini, tamu, isiyochosha ya Tunu.
“Ndiyo mpenzi, nipo kitandani hapa.”
“Nimekupigia kwanza kujua kama umefika salama, pili kukushukuru kwa kunipa raha na tatu kunipa hela. Asante sana mpenzi wangu. Wewe ni mwanaume wa tofauti sana. Unajua kila kitu. Unajali, unanipenda kwa dhati na unajua mapenzi, utafikiri ulikwenda jando la Kisambaa!” akasema Tunu kwa sauti yake ileile.
Bravo akadata!
Sifa zote hizo! Kiukweli Bravo hakuwahi kufisiwa na mwanamke kwa kiwango hicho. Akakumbuka hata anavyompatia fedha mkewe, hakuwa akimshukuru kwa kiwango hicho. Sasa akakiri kweli alikutana na mwanamke wa kumfanya awe mwanaume kamili!
“Asante mpenzi, umenifanya nijihisi kidume cha nguvu!”
“Siyo kukufanya, wewe ni kidume cha nguvu Bravo... bahati mbaya umeoa, lakini siyo neno, nitatumia nafasi hiyohiyo ndogo uliyoniachia mpenzi wangu!” akasema Tunu.
“Kuoa? Sahau kabisa mambo ya mke Tunu. Wewe una nafasi yako. Tena nataka kukuhakikishia kuwa, wewe una nafasi kubwa zaidi ya mke wangu Viola, nafasi yako ni kubwa sana. Tofauti ni kwamba, Viola naishi naye, wewe hautuishi pamoja.
“Lakini pia siyo neno, nitajua cha kufanya. Napanga mikakati rasmi ya kukufanya uwe na nafasi kubwa kwa vitendo siyo maneno maneno, mimi sitaki kuwa mtu wa maneno maneno,” akasema Bravo.
“Unamaanisha nini?”
“Subiri vitendo, hebu nitajie majina yako kamili,” akasema Bravo.
Tunu alishindwa kuelewa sababu ya kuambiwa vile na Bravo, lakini hakuwa na pingamizi zaidi ya kujibu: “Baby kwani mara hii umesahau kuwa naitwa Tunu?”
“Najua ni Tunu, lakini nahitaji majina yako kamili.”
“Tunu Abdallah.”
“La ukoo?... mama majina huwa ni matatu, la kwanza, ubini na ukoo.”
“Hapo sawa, ngoja sasa nikutajie kikamilifu. Naitwa Tunu Abdallah Mdoe.”
“Basi subiri utekelezaji wangu,” akasema Bravo.
“Mpenzi najua umechoka, sasa nakutakia usiku mwema. Ulale salama baba, uniote kipenzi cha miye!” akasema Tunu.
“Nawe pia Tunu.”
Wakakata simu zao.
Ile amekata tu, simu ikaita tena. Alipoangalia, akakutana na mkewe Viola....
“Ah! Limeshaanza! Kwani linataka nini? Linataka kunivurugia furaha yangu hili limwanamke,” akawaza Bravo akiangalia ile simu.
Iliita mpaka ikakatika, wakati akijishauri kupokea. Kwake ilikuwa ahueni, simu ilivyokatika. Baada ya muda, simu ikaanza kuita tena... akaamua kupokea.
“Haloo!”
“Mume wangu jamani Bravo, ndiyo nini kunifanyia hivyo?” akauliza Viola.
“Nimekufanyia nini kwani?”
“Mbona hupatikani kwa muda mrefu, isitoshe nilikuambia ningekupigia.”
“Kazi nyingi Viola.”
“Na kwa nini ukazima simu?”
“Nimekuambia kazi nyingi, nini usichoelewa?” Bravo akajibu kwa ukali.
“Sasa huo ukali wote unatokea wapi Bravo? Nimekuuliza jambo la kawaida tu, tena linalotuhusu wote, iweje sasa unanijia juu?”
“Kama huna cha kuongea, usiwe unanipigia simu, sawa? Mimi nimechoka na kazi, nahitaji kupumzika sasa,” akasema Bravo kisha akakata simu.
Akaizima kabisa!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 16
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Sasa huo ukali wote unatokea wapi Bravo? Nimekuuliza jambo la kawaida tu, tena linalotuhusu wote, iweje sasa unanijia juu?”
“Kama huna cha kuongea, usiwe unanipigia simu, sawa? Mimi nimechoka na kazi, nahitaji kupumzika sasa,” akasema Bravo kisha akakata simu.
Akaizima kabisa!
SASA ENDELEA...
BRAVO alikuwa amechafukwa hasa! Alishaonja asali na sasa alitaka kuendelea kuifaidi. Yeyote mbele yake, tofauti na Tunu, hakuwa na maana moyoni mwake. Viola alikuwa akimpigia kelele masikioni mwake.
Hakutaka usumbufu. Kwa hasira Bravo alitupa simu mezani, kisha akavuta shuka na kulala. Kichwani mwake kulijaa mawazo ya Tunu.
Alijaribu kuvuta kumbukumbu namna tukio zima lilivyokuwa, ndani ya saa tatu alizokaa na Tunu chumbani kwake, zilimfanya ajione alichelewa sana kumjua mwanamke huyo ambaye alimwingiza katika ulimwengu wa mapenzi upya kabisa.
“Ni kweli nimenasa! Mtu mzima lazima ukubali ukweli. Tunu ameniweza na kwa kweli nikimsikia Viola, nahisi kinyaa... mwanamke hajui mapenzi, hakuna anachojua kwenye ndoa yake, zaidi ya kunichunga na kutaka WhatsApp Call kila wakati.
“Ni hayo tu ndiyo anayojua... mengine aka! Kupika hajui, mapenzi hajui, yeye makelele tu. Mtoto mdogo amemtoa kwenye reli,” akawaza Bravo akiwa kitandani.
Alitumia muda mwingi kumfikiria Tunu wake, Viola alimuweka kando. Mawazo ya Tunu yakawa kama sehemu ya bembelezo, lililomfanya aweze kupata usingizi mwororo kabisa!
***
Viola alijaribu kupiga simu ya Braavo kwa mara ya sita sasa, haikupatikana! Alijiuliza ni kosa gani alilolifanya kwa mume wake, kiasi cha kumjibu majibu ya ovyo kiasi kile hakuona.
Alijaribu kuvuta kumbukumbu vizuri, labda kuna mahali alikosea, lakini hakuona kosa lake. Akazidi kushangaa.
“Nimefanya nini mimi? Halafu kwa nini mume wangu amebadilika ghafla kiasi hicho?” akajiuliza Viola bila kupata majibu.
Alilia sana!
Alilia hadi macho yakawa mekundu, uso wake ukavimba. Muda wote alikuwa akijaribu kumpigia Bravo, hakupatikana. Tayari mambo yalishabadilika. Ni vile tu hakujua, lakini ukweli ni kwamba mumewe alikuwa ameshatekwa na mtoto wa Kisambaa!
“Au amedhulumiwa pesa zake? Nini kimempata mume wangu?” akajiuliza Viola bila kupata majibu.
Kwa tabu sana, alifanikiwa kupata usingizi saa nane za usiku. Muda wote kabla hajapitiwa na usingizi alikuwa na kazi ya kuendelea kumtafuta mume wake.
Alishtuka usingizini saa moja na dakik zake asubuhi. Tayari alikuwa ameshachelewa kazini, lakini pia afya yake haikuwa nzuri. Mwili mzima ulikuwa ukimuuma. Akahairisha suala la kwenda kazini. Akahamia katika kibarua alichokuwa akikifanya usiku uliopita!
Alianza kumtafuta tena Bravo.
Alimpigia mara moja tu, akapokea...
“Za asubuhi mume wangu?” akasalimia Viola.
“Salama, umeamkaje?”
“Mimi mzima kiasi, lakini sijisikii vizuri.”
“Nini tatizo?”
“Mwili hauna nguvu, sina hamu ya kula na nahisi uchovu. Nadhani ni homa,” akasema Viola.
“Pole sana, nakushauri nenda hospitalini ukapime!”
“Nitafanya hivyo.”
“Haya siku njema.”
“Poa, nawe pia.”
Viola aliamua kujishusha kwa mumewe, hakutaka kumuuliza chochote kuhusu ugomvi wao wa usiku uliopita. Hilo lilisaidia kuweka masikilizano hadi mwisho. Alisubiri kuona matokeo yake kwa siku nzima ya siku hiyo.
Alijizoazoa pale kitandani, kisha akaenda bafuni, akaoga. Akavaa mara moja, kisha akaingia kwenye gari lake, akaelekea Hospitali ya Kairuki, Mikocheni. Alitaka kujua tatizo la afya yake kuyumba ghafla.
***
Siku mpya ya Bravo iliwadia. Siku njema kwelikweli. Siku iliyokuwa na ratiba nyingi kuliko kawaida. Pamoja na uwingi na unyeti wa ratiba zake, alidhamiria kuzimaliza zote.
Asubuhi alipata chai na slesi mbili za mkate, akitunza njaa yake mpaka saa 7 mchana, alipokwenda kibandani kwa Tunu kupata msosi wa nguvu. Kweli alikutana na maandalizi ya aina yake.
Alitengewa ugali wa dona, nyama ya mbuzi ya kukaanga maarufu kama stimu, matembele, mlenda, kachumbari na pilipili kidogo. Akiwa bado anashangaa, kabla hajaanza kula, glasi ya mtindi ilishuka mezani.
“Karibu kaka Bravo,” Tunu alimkaribisha akizuga kwa kumuita kaka, ili kuwaficha watu wengine.
Pamoja na kificho hicho, macho yao yalishindwa kuficha mzigo mzito wa mapenzi uliokuwa umejaa mioyoni mwao. Wote wakajikuta wameachia tabasamu mwanana. Tunu akamnawisha mikono Bravo. Akaanza kushambulia chakula.
Alikula kwa kujinafasi. Dakika ishirini zilikatika akiwa mezani. Alipomaliza, akatoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi Tunu. Tunu akamkonyeza airudishe! Bravo akazidi kuchanganyikiwa na ukarimu ule. Hakuwa na namna, akaondoka na kumwacha Tunu akiwa kazini kwake.
Kazi ambayo hakuipenda!
Hakuwa na imani kuwa kwa kuwepo kwake pale, angekuwa anafaidi mambo mazuri kutoka kwake yeye peke yake. Hilo lilimpa tabu na kumwongezea wivu moyoni.
Hakuwa na ratiba ya kurudi tena kwenye semina. Aliishia Barabara ya 12, ambapo aliuliza madalali.
“Unahitaji nini bro? Chumba, nyumba, kiwanja au shamba? Hapa kila kitu kipo,” Dalali Hassan Nyumbanyingi akamwambia Bravo baada ya kufika kijiweni kwake.
“Bwana mimi nahitaji kiwanja kizuri, nusu eka. Kisiwe na longolongo!” akasema Bravo.
“Utashindwa wewe kaka. Viwanja vipo, ni wewe tu uamue unataka mjini, nje kidogo ya mji au nje kabisa ya mji. Chaguo ni lako!” akasema Nyumbanyingi.
Unashangaa nini?
Ni kiwanja cha Tunu kinatafutwa!
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 17
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Utashindwa wewe kaka. Viwanja vipo, ni wewe tu uamue unataka mjini, nje kidogo ya mji au nje kabisa ya mji. Chaguo ni lako!” akasema Nyumbanyingi.
Unashangaa nini?
Ni kiwanja cha Tunu kinatafutwa!
SASA ENDELEA...
“WAPI naweza kupata kiwanja kizuri katika eneo ambalo tayari limepangwa?” Bravo akamwambia Nyumbanyingi.
“Kange ni pazuri sana, kule kumekucha!”
“Siyo nje sana ya mji?”
“Hapana, ndipo stendi kubwa ya mabasi ya mikoani ilipohamishiwa. Ni eneo la washua, linakufaa sana!” akasema Nyumbanyingi.
“Tunaweza kwenda kupaona?”
“Hakuna shida, muhimu utoe mguu tu, tutakwenda.”
“Mguu ndiyo nini?” akauliza Bravo akitabasamu.
“Ni tozo ya kunitoa kijiweni kaka. Ishirini inatosha.”
“Hiyo haina shida.”
“Halafu ukilipia kiwanja unanipa asilimia kumi.”
“Haina shida, muhimu nikipende tu.”
“Basi twende zetu!”
Bravo akakodi Bajaj iliyowapeleka mpaka Kange ambapo alionyeshwa viwanja tofauti zaidi ya vitatu, akaridhika na kimoja kilichokuwa pembeni kabisa, eneo lenye miti mingi.
“Napenda sana hewa nzuri, hapa pananifaa,” akasema Bravo.
“Sasa tunafanyaje? Uko tayari tayari nimuite mhusika?” akauliza Dalali Nyumbanyingi.
“Mimi nipo tayari,” akasema Bravo.
“Subiri.”
Kweli Dalali Nyumbanyingi akainua simu na kuzungumza na mtu aliyesema ni mmiliki wa kiwanja hicho. Mwisho wa mazungumzo yao kwenye simu, ilionekana walikubaliana kuwa angefika eneo hilo baada ya muda mfupi.
“Amesema atafika hapa baada ya nusu saa!” akasema Dalali Nyumbanyingi.
“Amesema hayupo mbali sana?”
“Hapana, yupo mjini.”
“Poa, basi tutafute mahali tumsubiri, akifika atakupigia,” akasema Bravo.
“Poa.”
Jirani na eneo lile kulikuwa na mgahawa, wakaingia hapo kumsubiri mmiliki wa kiwanja kile. Wakati haya yanafanyika, Tunu hakuwa na habari kabisa!
***
Vipimo vya maabara vilitoka, Viola hakuwa akiugua chochote. Alikuwa mzima wa afya. Daktari alimwambia hapakuwa na sababu ya kupewa dawa kwa sababu hawakugundua chochote kwenye damu yake.
“Lakini sijisikii vizuri daktari,” akasema Viola.
“Unalala vya kutosha kweli?”
“Hapana, nina siku ya tatu sasa sijalala vizuri.”
“Unakula vizuri?”
“Kwa kweli kwa siku mbili hizi sizingatii sana.”
“Unaonekana una tatizo jingine nje ya maradhi ya kawaida. Nahisi una mawazo sana, nini kinakusumbua?” daktari akamwuliza akimwangalia usoni.
“Ni kweli daktari, nina matatizo ya kifamilia, yaninyima amani, nashindwa kulala!” akasema Viola.
“Pole sana, lakini hupaswi kuwa hivyo. Jitahidi kulala kadiri uwezavyo kupumzisha kichwa chako. Lala mapema, kula kwa mpangilio, utakuwa sawa kabisa, lakini usinywe dawa yoyote, huna tatizo.”
Viola alirudi nyumbani akiwa amepata ushauri wa daktari. Kweli aliamua kutulia, alijiamuru kuacha kumfuatilia zaidi mumewe. Aliamua kumpa muda. Lakini ili kutafuta faraja ya moyo wake, aliona ni bora ampigie shosti wake, Mariam ili amuombe ushauri.
Mariam ni msichana ambaye alikuwa akifanya naye kazi ofisi moja. Mara moja akampigia na kumweleza kuhusu mkasa mzima wa mume wake. Hakutaka kumficha chochote, aliamua kuwa huru kwake ili aweze kumpa ushauri utakaofaa.
“Kwani hiyo tabia alikuwa nayo siku nyingi?” akauliza Mariam.
“Hapana, ana kama siku tatu sasa. Kifupi ni tabia mpya, ambayo ameanza baada ya kwenda Tanga kikazi!” akasema Viola.
“Basi kwa vyovyote vile, kuna kitu kipya anafanya Tanga. Kipo kitu kilichombadilisha, ndiyo maana amekubadilikia,” akasema Mariam.
“Kweli?”
“Naamini hivyo. Unadhani kwa nini abadilike ghafla? Na ninavyoijua Tanga, kama ni kweli amenasa mahali, kunahitajika nguvu kubwa sana kumrudisha!”
“Sasa unanishauri nifanye nini shosti wangu?” Viola akauliza kwa shauku.
“Tuliza moyo wako shoga yangu, kwa sasa tulia, ukija kesho kazini tutayajenga vizuri mama. Wewe pumzika tu!” akasema Mariam.
“Haya asante sana shoga yangu, maana haya mambo ni mazito kwangu wala si madogo!”
“Usijali, nipo kukusaidia best.”
Wakakata simu zao.
Viola alishusha pumzi.
Alipata ahueni kubwa baada ya kuzungumza na Mariam, ambaye alimpa mwanga wa mahali pa kuanzia. Aliamua kujiongeza mwenyewe, akaamua kutomtafuta kabisa mume wake, Bravo hadi atakapoamua mwenyewe kumpigia...
“Nitafanya hivyo kama sehemu ya kumpima alivyo kwa sasa,” akajisemea moyoni mwake.
Viola alishikilia msimamo huo.
***
Mzee Shekoloa, mmiliki wa kiwanja kile alifika eneo lile na kuwasiliana na Dalali Nyumbanyingi. Bila kupoteza muda, wakakubaliana bei. Bahati nzuri, bei haikuwa kubwa, hivyo hawakuvutana sana.
“Sasa unalipia leoleo au?” akauliza Mzee Shekoloa.
“Hapana baba, ni kesho. Ningeweza kulipa leo, lakini mtu ninayemchukulia sijampanga. Nitakuja naye kesho!” akasema Bravo.
“Kwa hiyo hiyo kesho unakuja na hela kabisa?”
“Hapana.... nitakuja tuandikishiane hapa, kisha ama nitakupa cheki au tuongozane benki nikakuhamishie kwenye akaunti yako au hata ukitaka keshi, lakini benki,” akasema Bravo.
“Sawa, hakuna shida! Kesho saa ngapi sasa?”
“Saa nne asubuhi tukutane hapa. Mzee lakini nitapenda tuandikishiane ofisini kwa mtendaji au serikali ya mtaa!” akasema Bravo.
“Huo ndiyo utaratibu kijana wangu, naujua wala usiwe na shaka na hilo kabisa,” akasema Mzee Shekoloa.
***
“Hivi baby unajua sababu za kutaka majina yako yote matatu?” Bravo alikuwa anaongea na Tunu kwenye simu, muda mfupi baada ya kuachana na Dalali Nyumbanyingi, Barabara ya 12.
“Hapana mpenzi wangu.”
“Utajua kesho... naomba kesho uombe ruhusa, kuna mahali tunakwenda saa 3 asubuhi!”
“Kuna nini?”
“Utajua kesho hiyohiyo! Wewe jiandae tu.”
“Mh!” Tunu akaguna.
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 18
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Kuna nini?”
“Utajua kesho hiyohiyo! Wewe jiandae tu.”
“Mh!” Tunu akaguna.
SASA ENDELEA...
SIKU iliyofuata Viola aliamka mapema sana kuliko kawaida. Akafanya usafi pale nyumbani, akayapanga makochi ya sebuleni katika mtindo mwingine, akabadilisha na vitambaa na mito midogo ya kwenye makochi.
Aliporidhika, akahamia chumbani kwake. Akafanya usafi wa nguvu, kisha akabadilisha kila kilichokuwa mle ndani. Kitanda akakiweka sehemu nyingine. Kochi moja lililokuwa mle chumbani pia akalibadilisha mwelekeo.
Baada ya hayo akaingia bafuni akaoga, alijiremba tofauti na siku zote, akawa na mwonekano wa binti mdogo wa miaka 19. Alionekana mbichi kabisa! Viola alikuwa na umri wa miaka 28. Akaingia kwenye gari, akawasha moto kwenda ofisini kwake.
Njiani alimkumbuka mume wake, lakini alisita kumtafuta. Aliamua kufuata maelekezo aliyojipa mwenyewe. Aliamua kuwa mtulivu kabisa, kuacha kila kitu kiende chenyewe.
Alitaka kujua mwisho wa mume wake ungekuwa nini. Aliendesha gari akiwa mwenye mawazo mengi, hadi alipofika ofisini. Alipoegesha tu gari, akakumbuka jambo moja la muhimu sana.
Muda wa mumewe kukaa Tanga ulikuwa umekwisha, tangu jana yake. Kwa maneno mengine, tayari alikuwa ana siku moja zaidi jijini Tanga, tofauti na alivyomuaga.
Akapatwa na wasiwasi!
“Semina ilikuwa inaishia jana, kwa hiyo anatakiwa leo awe njiani kuja Dar, sasa mbona kimya tena? Mbaya zaidi hanijulishi chochote? huyu mwanaume wangu amekuwaje siku hizi jamani?” akawaza Viola akifungua mlango wa gari lake ili atoke.
Kabla hajaanza kupandisha ngazi za kuelekea Mapokezi, akaona gari la shoga yake, Mariam likiingia sehemu ya maegesho. Akasimama. Kweli alikuwa ni Mariam akiingia ofisini.
Akapata matumani mapya ya nini afanye kupitia kwa rafiki yake huyo ambaye alimwamini sana. Mariam alishuka garini, akafunga milango na kumfuata Viola.
“Vipi shoga, za tangu jana?” Mariam akasalimia.
“Salama, kwema? Vipi shemeji na watoto wangu nyumbani?” Viola akasema.
“Wazima wote!”
“Hata mimi naona wazima, nakuona shoga ulivyo mwepesiiii, ona mimi nilivyo utadhani sijaolewa... stress zimenijaa hadi miguuni!” akasema Viola kwa utani lakini akiwa amekunja uso wake kuonyesha kuwa alichokuwa akisema alikuwa akimaanisha.
“Viola na kupendeza kote huko shoga!”
“Hakuna kitu mama, acha tu nakula msoto wa aina yake.”
“Shosti wangu ndivyo maisha yalivyo, wakati fulani nyumba ina raha, wakati mwingine karaha. Ni kawaida, ni vipindi vya mpito tu. Ndiyo maana mimi nimeweza kukaa na mume wangu mpaka leo, ni usugu wangu ndiyo umesababisha,” akasema Mariam.
“Basi shoga tuondoke, nataka nikakupe chai leo!” akasema Viola.
“Poa, twende zetu.”
Wakaondoka kuelekea kwenye mgahawa wa ofisini kwao. Walipofika waliagiza chai ya maziwa, mayai ya kukaangaa na juice ya mchangayiko wa maembe na parachichi. Wakiwa wanakunywa chai, Viola akaanzisha mazungumzo kuhusu mume wake. Hakuna alichomficha, alimweleza kila kitu ili aweze kumsaidia kikamilifu.
“Ni mapema kusema kuwa mumeo atakuwa amepata mwanamke mwingine Tanga, lakini nasema kwa uhakika kuwa staili yako inaweza kuwa imechangia kumbadilisha mume wako!” akasema Mariam.
“Kwa nini unasema hivyo?” Viola akasema kwa kung’aka kidogo.
“Unamchunga sana... mwanaume hachungwi kama ng’ombe... dawa ya mwanaume ni mapenzi motomoto. Ukiweza kumpa mashamsham ya kutosha, lazima atulie na atakuwa anafanya vile unavyomwelekeza!” akasema Mariam.
“Angalia Mariam, hivi ninavyokuambia ameshamaliza muda wa semina Tanga tangu jana, alitakiwa leo ndiyo aje nyumbani. Hajasema kuwa yupo njiani, huoni hiyo ni dalili mbaya?”
“Kwani siku imeisha?”
“Hapana.”
“Umewasiliana naye akasema haji?”
“Hapana.”
“Sasa usihukumu na wala huna sababu ya kumtafuta. Mwache kama yeye ataona sababu ya kukutafuta atafanya hivyo yeye. Kwa sasa unatakiwa kufanya mambo machache tu; kwanza mwache awe huru.
“Usimfuatilie kabisa, halafu pili onyesha kuwa umebadilika kwa maneno na matendo. Mwache huru, usionyeshe kuwa humwamini. Mfanye awe mfalme wako, mfanyie kila kitu.
“Lakini kubwa, ongeza utundu chumbani. Sijui shoga, lakini kiuno chako sina hakika kama umepaka grisi. Lazima kiuno kiwe chepesi kama feni. Mwanaume anatakiwa akiwa na wewe, ajiulize ni kwa nini atafute mwanamke mwingine nje. Hakikisha unakuwa fundi kwenye eneo hilo,” akasema Mariam.
“Kiukweli shosti eneo hilo mimi ni mtupu kabisa,” akasema Viola.
“Kesho nitakuletea CD itakayokusaidia, ina mafundisho yote muhimu ya chumbani. Imeandaliwa na kungwi mmoja anaitwa Anti Zuh. Ni hatari. Ukiujua utundu wa Anti Zuh, ukautumia vizuri, basi mumeo atatulia kwako jumla,” akasema Mariam.
“Naitaka hiyo CD ya Anti Zuh.”
“Ni hapo kesho basi.”
“Poa shoga yangu, umenisaidia sana mama. Asante sana!”
“Usijali, halafu kingine fanya usafi wa nguvu nyumba yako, badilisha mwonekano na mpangilio wa vitu kabla hajarudi safari!”
“Nimefanya zoezi hilo, asubuhi ya leo.”
ITANDELEA....
 
HILIKI YA CHUMBAGENI – 19
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Naitaka hiyo CD ya Anti Zuh.”
“Ni hapo kesho basi.”
“Poa shoga yangu, umenisaidia sana mama. Asante sana!”
“Usijali, halafu kingine fanya usafi wa nguvu nyumba yako, badilisha mwonekano na mpangilio wa vitu kabla hajarudi safari!”
“Nimefanya zoezi hilo, asubuhi ya leo.”
SASA ENDELEA...
MARIAM alimeza funda kubwa la mate, kisha akatingisha kichwa kuashiria alikuwa amekubaliana na kile alichoongea Viola.
Mariam akasema: “Basi umefanya vizuri shoga... hebu tumalizie hizi juice twende kazini, maana muda wenyewe huu umeshakwenda,” akasema Mariam, akichukua glasi yake ya juice mezani.
Viola naye akachukua yake!
***
Saa 4 juu la alama, Bravo na Tunu waliingia Kange kwenye eneo ambalo Bravo alitaka kumnunulia Tunu. Alimkuta Mzee Shekoloa na Dalali Nyumbanyingi wakiwasubiri.
“Mpenzi wangu nisipoteze muda, huyu hapa anaitwa Mzee Shekoloa, ndiye mmiliki wa hili eneo hapa,” akamwonyesha eneo lenyewe.
“Huyu ni dalali, anaitwa Nyumbanyingi, ndiye amenileta hapa. Nimekuleta hapa kwa sababu nataka kulipia hiki kiwanja na ninafurahi kukujulisha kuwa ni kiwanja chako!” akasema Bravo.
“Bravo unasemaje?” Tunu akasema kwa sauti ya juu.
“Ndiyo hivyo mpenzi wangu!” akasema Bravo.
Tunu alijirusha juu ya kifua cha Bravo. Bila kuchelewa Bravo akaiweka mikono yake kwa nyuma, makalio ya Tunu yakatua mikononi mwake, akawa anabembea kifuani mwa Bravo.
Tunu hakuwa na nguvu za kuzungumza, furaha aliyokuwa nayo haikuweza kuelezeka! Bila hiyari yake, akajikuta akimwaga machozi machoni mwake!
“Usilie honey, nakupenda...” akasema Bravo.
Mzee Shekoloa na Dalali Nyumbanyingi wakabaki wanashangaa!
Walishuhudia sinema ya bure!
“Tunu nikikuambia nakupenda elewa. Mimi sijakutamani, ninakupenda na ninazo sababu za kukupenda. Sijawahi kukutana na mwanamke anayenipenda na kunionyesha mambo nisiyojayua kabisa ya huu ulimwengu.
“Nakuhakikishia nakupenda sana, nashindwa kujua nifanye nini ili kudhihirisha mapenzi yangu kwako, lakini elewa kuwa ninakupenda na nitafanya kila nitakachoweza ili kudhibitisha mapenzi yangu ya dhati kwako,” akasema Bravo.
“Naamini mpenzi wangu, wala huna haja ya kutamka mengi, najua unanipenda baba, nimeona mwenyewe!” akasema Tunu akiendelea kulia.
Bravo alikuwa fundi. Alikuwa na uwezo wa kumbembeleza na kumfuta machozi yake, lakini aliamua kuacha makusudi ili kuwaumiza Mzee Shekoloa na Dalali Nyumbanyingi.
Kwake, macho ya Tunu yalizidi kumhamasisha. Alimpenda hasa na alikuwa na uhakika na hilo, maana moyo wake ulimwambia hayo kwa herufi kubwa! Aliporidhika, sasa akaamua kumtuliza mpenzi wake...
“Haya ni madogo mama, yajayo yanafurahisha. Ni suala la kusubiri tu, lakini nakuhakikishia mpenzi wangu, utafurahi,” akasema Bravo akimfuta machozi na kitambaa chake.
Alivyowaza ndivyo ilivyokuwa, zoezi hilo lilifanikisha kumtuliza Tunu ambaye alikuwa amechizika na alichokuwa anakishuhudia mbele ya macho yake.
“Sasa unaniruhusu nilipie malkia wangu? Umekipenda kiwanja?” akauliza Bravo.
“Kizuri baba, nipo tayari.”
“Sasa mzee wangu Shekoloa, tukamilishe kazi yetu,” akasema Bravo.
“Sawa.”
Wakatoka pamoja hadi zilipokuwa ofisi za serikali ya mtaa. Wakaandikishiana mauziano ya kiwanja kile, kisha Bravo akamwandikia Mzee Shekoloa hundi na kumkabidhi.
Gharama zote za mashahidi na dalali, Bravo alilipa. Kila kitu kiliandikwa kwa jina la Tunu Abdallah Mdoe. Bravo akawa anamrudisha Tunu nyumbani kwake. Njia nzima, Tunu alikuwa akimshukuru Bravo kwa wema wake.
“Bravo umekuja kuyabadilisha maisha yangu, sina cha kukupa mpenzi wangu, zaidi nakushukuru!” akasema Tunu.
“Ati huna cha kunipa?”
“Ndiyo... kwa kweli sina cha kukupa kwa haya uliyonifanyia.”
“Cha kunipa unacho na bahati nzuri umeshanipa, ndiyo matokeo ya haya unayoyaona. Acha ufaidi uwezo wako wa kujua kumpenda mwanaume na kumwonyesha mapenzi yasiyofananishwa na chochote!” akasema Bravo.
“Asante sana mpenzi. Unanifanya nijisikie vizuri, nijione mwenye thamani kabisa, asante sana baba,” akasema Tunu.
Walipofika Chuda, nyumbani kwa Tunu, Bravo akamtaka Tunu ashuke, Tunu akakataa. Ni jambo lililomshangaza sana Bravo.
“Kwa nini sasa hutaki kushuka?” Bravo akauliza kwa hamaki.
“Sitashuka bila wewe.”
Bravo hakujiuliza mara mbili, alijua alichotakiwa kufanya. Alichomoa fedha na kumlipa dereva, akashuka na kuingia chumbani kwa Tunu. Ile wameingia tu, Tunu akaanza fujo...
Akamvamia Bravo na kumchojoa kila kitu, kisha naye akafanya hivyo.
“Twende bafuni,” akasema Tunu akitweta.
Alionekana dhahiri kuwa hakuwa kwenye hali ya kawaida, joto kali la mahaba lilikuwa limempanda. Kama kondoo anayepelekwa machinjioni, Bravo akaongoza njia bila ubishi.
“Najua siwezi kukulipa kwa wema wako, lakini kwa sababu umekiri mwenyewe kuwa unafurahishwa na mapenzi yangu, basi leo itakuwa mara kumi zaidi ya awali,” Tunu alisema kwa sauti ya chini, akionekana kuhema kwa tabu.
“Nimekwisha mimi... hivi nitaweza kurudi nyumbani kwangu kweli?” akawaza Bravo kichwani mwake.
Semina ilikuwa imeshaisha jijini Tanga, siku hiyo baadhi ya wafanyakazi walikuwa wameshaanza kuondoka kurejea kwenye vituo vyao vya kazi. Wengine walitarajiwa kuondoka siku iliyofuata!
Lakini siyo Bravo!
Bravo hakujua wala hakupanga siku yaa kuondoka Tanga!
ITANDELEA....
 
Back
Top Bottom