James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,984
- 3,695
- Thread starter
- #21
HILIKI YA CHUMBAGENI – 20
NA JOSEPH SHALUWA
ILIPOISHIA...
“Najua siwezi kukulipa kwa wema wako, lakini kwa sababu umekiri mwenyewe kuwa unafurahishwa na mapenzi yangu, basi leo itakuwa mara kumi zaidi ya awali,” Tunu alisema kwa sauti ya chini, akionekana kuhema kwa tabu.
“Nimekwisha mimi... hivi nitaweza kurudi nyumbani kwangu kweli?” akawaza Bravo kichwani mwake.
Semina ilikuwa imeshaisha jijini Tanga, siku hiyo baadhi ya wafanyakazi walikuwa wameshaanza kuondoka kurejea kwenye vituo vyao vya kazi. Wengine walitarajiwa kuondoka siku iliyofuata!
Lakini siyo Bravo!
Bravo hakujua wala hakupanga siku ya kuondoka Tanga!
SASA ENDELEA...
ULIKUWA mperampera wa aina yake. Alivyokuwa akifikiria Bravo awali, ilikuwa tofauti kabisa. Tunu alikuwa mtaalamu kuliko kawaida.
Aliyoonyeshwa kwenye mechi ya utangulizi, kumbe ilikuwa rasharasha tu. Sasa Tunu akamwonyesha kwa undani ufundi wote aliofundwa unyagoni! Bravo alikiri kwamba, alikutana na kisima cha mahaba, ambacho hakikukauka mahaba ya kila namna.
Baada ya kazi nzito iliyofanyika ndani ya kuta nne za bafu lile ambalo lilifanyiwa usafi wa kina, kiasi kwamba mtu angeweza kula mle bafuni, walioga kwa pamoja.
Bravo aliogeshwa kama mtoto mdogo. Alisuguliwa mwili mzima na dodoki laini, kisha akamwagiwa maji yaliyosuuza mapovu yote, hadi akawa safi kabisa. Akakaushwa kwa taulo laini, kisha akafunguliwa mlango arudi chumbani.
Bravo akatoka chumbani, Tunu akaendelea kuoga, dakika chache baadaye akatoka na kumfuata Bravo. Akaanza kumpaka mafuta mwilini. Ni hapo aligundua kuwa, mpenzi wake alikuwa na kucha ndefu kwenye vidole vya miguuni na mikononi.
Akachukua mashine ya kukatia kucha, akaanza kumkata kwanza kucha za vidole vya miguuni, alipomaliza akahamia kwenye vidole vya mikononi. Baada ya zoezi lile, akachukua chupa ndogo iliyokuwa na spiriti, akaweka kwenye kitambaa, akampata kwenye vidole vyote.
Baada ya hapo, akachukua chupa ya mafuta ya maji ya nazi, akampaka kwenye vidole vile, akarudisha mahali pake. Bravo alikuwa mgeni wa kila kitu.
“Baby hayo ni mafuta gani?”
“Mafuta ya nazi.”
“Yanasaidia nini?”
“Haya ni mafuta halisi, siyo ya kiwandani. Yanalainisha ngozi na kuondoa sugu, ndiyo maana nimekupaka baada ya kukupaka spirit. Sitaki uwe na ngozi iliyokomaa mpenzi wangu,” akasema Tunu akiachia tabasamu pana usoni mwake, lililosababisha vishimo mashavuni mwake vionekane.
“Tunu nimefanya uteuzi leo hii,” hatimaye Bravo akasema alilalama kwa mahaba.
“Uteuzi wa nini tena mpenzi?”
“Nimekuteua wewe kuwa nahodha wa penzi langu kuanzia leo hii. Kwa mambo unayonifanyia, mama nimekubali wewe ndiye uwe mwamuzi wa mwisho wa kila kitu kwenye idara ya mapenzi, maishani mwangu. Sema lolote, nitafuata,” akasema Bravo akitweta.
Tunu alitabasamu.
Moyoni akajisemea: “Na bado... hapa ni Tanga Bravo.”
Lakini hata hivyo, moyoni Tunu alianza kumpenda Bravo zaidi ya ilivyokuwa awali. Mwanzo alichukulia kawaida, lakini kwa namna siku zinavyozidi kwenda na namna Bravo anavyompa umuhimu, ndivyo naye mapenzi yalivyozidi kuongezeka moyoni mwake.
“Bravo naomba nikuambie ukweli baba.”
“Ukweli gani tena malkia?”
“Kadiri siku zinavyosonga ndivyo ninavyozidi kukupenda mpenzi. Naomba usiniache baba. Najua una mke, lakini naomba unipe nafasi yangu mpenzi,” akasema Tunu kwa sauti ya kudeka.
“Unapozungumza mambo ya maana, acha kabisa kumtaja mke wangu. Achana naye, ana mapungufu mengi, lakini nimemvumilia kwa muda mrefu. Nimekuwa na wewe kwa muda mfupi tu, lakini najiona kabisa nimekuwa mwanaume kamili, nimekuwa mpya kabisa mimi,” akasema Bravo.
“Nafurahi kusikia hivyo mpenzi.”
Walimaliza siku nzima wakiwa ndani, wakifurahia ulimwengu wa mapenzi. Mchana Tunu alitoka na kwenda kununua chakula hotelini, wakala pamoja chumbani. Bravo hakusita kumweleza ukweli kuwa, chakula kile hakina ladha kama mapishi yake.
“Kama utakuwepo usiku, nitakupikia mpenzi wangu,” akasema Tunu.
“Siyo kuwepo tu mpenzi, mimi leo nalala hapa hapa kwako,” akasema Bravo akitabasamu.
“Kweli?”
“Ndiyo.”
“Haya sema mwenyewe, unataka kula nini?”
“Kiukweli nina hamu sana na ubwabwa wa nazi,” akasema Bravo akijiramba.
“Hilo limepita, mboga?”
“Nataka mchicha wa kuchanganywa na nyama.”
“Usijali baba, hayo yote utayapata, andaa njaa yako mpenzi.”
Bravo akacheka!
Jioni, mishale ya saa 10, Tunu alitoka na kwenda sokoni. Akamwacha Bravo akiwa peke yake mle chumbani. Alikagua chumba cha Tunu, akajiridhisha kuwa, mwanamke yule alikuwa mwenye kupanga utaratibu wa mambo yake sawasawa!
Tunu aliporudi, alibadili nguo, akavaa dera na kwenda kukaa jikoni kukaangiza chakula. Saa 2: 00 usiku walikuwa chini kwenye mkeka uliotandikwa juu ya zulia, wakipata chakula.
Bravo alitaka wali nyama kwa mchicha, lakini mezani kulikuwa na zaidi ya mboga nne. Dagaa uono wa kukaanga, majani ya maboga yaliyoungwa kwa nazi, matembele na bamia na nyanya chungu (ngogwe) zilizopikwa kwa pamoja.
Bravo alizidi kujionea maajabu. Walipomaliza kula, Tunu aliweka bilauri la juisi ya ubuyu iliyochanganywa na hiliki na amdalasini. Bravo akazidi kuchanganyikiwa!
“Hivi ni kwa nini sikukuona mapema, nikakuoa wewe? Ulikuwa wapi siku zote wewe mwanamke?” Bravo akasema akirudisha glasi ya juisi mkekani.
ITANDELEA....