SEHEMU YA 18
Ulikuwa usiku wa pili kwa Noela kulala peke yake bila uwepo wa mumewe,lilikuwa jambo gumu sana na alikuwa hajazoea hata kwa mbali,nyumba nzima alikuwa yeye na Oscar aliyekuwa ameajiriwa rasmi kuwa msimamizi wa mifugo yote pale nyumbani katika chakula,usafi na hata katika magonjwa ya hapa na pale.
Majira ya saa tano usiku usingizi ulikuwa umemkosa kabisa Noela aliyekuwa amelala kuanzia majira ya saa mbili usiku.
"sijui kama nitakuwa jasiri lakini ngoja nijaribu kwa leo siwezi kuvumilia zaidi" Noela alikuwa akijiongelea mwenyewe kwa sauti ya chini huku akiwa amekaa kitako kitandani kwake akiwa na khanga moja huku kichwani akiwa amevaa mfuko mweusi wa plastiki kuzuia nywele zake kuvurugika kichwani.
Kwa mkono wake wa kulia aliichukua simu yake ya mkono na kuiweka vyema katika kiganja chake.
"nitume meseji au nipige!!..." alijiuliza Noela.
"mh! Nikipiga kweli nitaweza kuongea mie...tangu utotoni naogopa mie hadi leo miaka 25 hapana ngoja nijaribu" alijipatia jibu mwenyewe.
Akiwa bado anatafakari joto lile kali mbele yake alishtukia mikono laini ya Noela ikizunguka katika mgongo wake na kumng'an'gania kwa nguvu kabisa. Oscar hakujua lengo la Noela alidhani ni uoga wa giza lakini haikuwa hivyo Noela alizidi kumkumbatia kwa nguvu zote,akiwa anakifahamu vyema chumba chake alimzungusha taratibu hadi usawa wa kitanda na kisha akamwangusha pale na yeye kutua juu yake.
"Os..ah! Os...Mchungaji please..." alianza kulalamika Noela juu ya Oscar,ndoto zilizokuwa zinamsumbua kila siku sasa haikuwa ndoto tena Noela alikuwa mbele ya Oscar,uwepo wake pale kitandani ulimchanganya kabisa,japo Oscar alikuwa anatapatapa kujiondoa mikononi mwake lakini kwa nguvu zote alijitahidi kumdhibiti katika himaya yake.
"Noela niachie,niachie jamani kaka atanifikiriaje akinikuta humu unadhani,niache da Noela nikafate mshumaa niwashe giza liondoke" alijitetea Oscar.
"Timoth hayupo jamani tafadhali usiondoke..usiondoke mchungaji" alijibu Noela huku akionekana kutojitambua hata kidogo.
Akili ya Oscar ilifanya kazi haraka akaitambua hatari iliyokuwa mbele yake,hatari hiyo ilikuwa ni kama nusu kifo kama Timoth angerejea muda huo na kumkuta ndani ya chumba chake anachokitumia na mkewe tena alikuwa amevuka mipaka na alikuwa kitandani mbaya zaidi alikuwa na mwanamke mwenye pete ya ndoa katika kidole chake cha shahada.
***
Hadi kufikia kutoa kiapo cha kulipa kisasi kwa mchungaji wa kanisa kwa kitendo kibaya anachoendelea kumfanyia rafiki yake mpendwa (Timoth) Deo alikuwa anajua wapi pa kuanzia na aliamini lazima atafanikiwa.
Deo aliwahi kumsikia Adelah ambaye ni muimba kwaya kanisani lakini pia ni rafiki mkubwa wa mkewe,katika maongezi yao siku moja aliwahi kumsikia akitoa habari fulani ambayo ilikuwa ya kustaajabisha lakini waliichukulia kama tetesi,eti kwamba mke wa mchungaji Marko ametulia baada ya kuolewa na Mchungaji lakini kabla ya hapo alikuwa ni kiruka njia sana."hapo hapo ndio nitaanzia kama kweli ni kiruka njia basi kazi itakuwa nyepesi sana" Deo alifikiria wakati akijiandaa kuanza rasmi kutimiza ahadi aliyokuwa amempa rafiki yake (Timoth) ahadi ya kumlipia kisasi kwa uovu ambao mchungaji anautenda kwa mke wake (Noela)