Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

Africa haya ni ya kawaida sana
The same style used to kill
in mysterious circumstances, of Kenya’s then foreign minister Robert Ouko.

His body was discovered by a schoolboy on his walkabout, and when the police arrived it was discovered that not only was the body badly burned but it had bullet holes.

A rumour was put out by someone (silly, obviously) suggesting the minister had committed suicide, in which case he would have shot himself and then set himself on fire, or lit the fire and then shot himself.

Noma sana! Umenikumbusha mbali sana.
.
David Balali
 
Ni mauaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Juni 30 mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (conspiracy theory) kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba kweli aliuawa na polisi.

Katika mfululizo wa makala hii, Mwandishi Wetu atakuletea simulizi ya nini hasa kilisababisha mauaji yake, nani walimfyatulia risasi zaidi ya 15, maelezo ya maungamo ya wauaji wake yanasemaje na familia ililipwa fidia ya Shilingi ngapi.

Simulizi hii inaegemea ushahidi uliotolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidia iliyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na simulizi zilizogubika mauaji hayo.

Maneno yalisemwa mengi, mojawapo ni hisia kuwa huenda aliuawa kwa sababu ya urafiki wake wa karibu na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi 1995, lakini kwa kesi ilivyokuwa mahakamani haikuwa sahihi.

Kwa kuwa Kombe alikuwa amepigwa risasi na polisi, licha ya kuripotiwa kuinua mikono yake juu kama ishara ya kujisalimisha kwa watu walioamini ni wezi wa gari, kulikuwa na uvumi kwamba mauaji yake yalikuwa yamepangwa.

Ni kutokana na hisia hizo na moto wa kisiasa juu ya mauaji hayo, Rais wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ambayo iliwasilisha ripoti yake 1997 ambayo si wazi, ikisema Serikali haikuwa na mkono katika mauaji hayo.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva aliyekuwa na Jaji Mussa Kipenka wakati huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali, ilihoji mashahidi 52 na mwaka 1997 ilitoa ripoti kwa Mkapa iliyohitimisha kwamba Serikali haikuwa na mkono wowote katika kifo cha Kombe.

Hadi sasa taarifa ya tume hiyo, kama zilivyo baadhi ya tume zilizoundwa kutafuta ukweli wa jambo ambalo linaibua hisia kali, imekuwa ni siri.

Mwaka 1998, Mbunge wa Temeke Jijini Dar es Salaam, Augustino Mrema aliibua hoja bungeni kuwa kifo cha Kombe kilikuwa sehemu ya mpango wa mauaji uliofanywa na Serikali, ingawa hata hivyo alishindwa kuthibitisha madai hayo. Pamoja na taarifa hiyo ya tume na ushahidi uliotolewa mahakamani kuhusiana na mauaji ya Kombe, bado baadhi ya watu hadi sasa wana hisia tofauti juu ya mauaji hayo na katika makala hii tutakuletea mwanzo mwisho nini kilitokea.

Timu ya makachero ilivyoundwa

Usiku wa Juni 30, 1996 na siku iliyofuata, kulizagaa taarifa za kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa Luteni Jenerali Kombe, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa tano wa TISS na taarifa hizo hazikuzagaa kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyo sasa.

Wakati huo wala simu za kiganjani (kitochi) zilikuwa hazijawa nyingi, licha ya kwamba zilianza kuingia nchini mwaka 1994, hivyo taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu na katika mji wa Moshi, watu walikaa katika makundi wakijadili.

Taarifa hizo zilisema polisi walimuua Kombe kwa kummiminia risasi hata baada ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha, na maiti yake ilipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mawenzi.

Polisi wakati huo walikuwa wanaamini wamemuua mtu waliyekuwa wanaamini ni mwizi mashuhuri wa magari na walikuwa wakitamba kufanikiwa kukamata gari Nissan Patrol namba TZG 50 mali ya D.W Ladwa lililoibwa Jijini Dar es Salaam.

Ni hadi mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro alipopokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Iwisi Shoo, akimwambia gari walilolikamata si lenyewe na mtu waliyemuua si mwizi, bali ni Kombe, mkuu wa zamani wa TISS.

Hapo ndipo Polisi wenyewe walijikuta wakipata ganzi baada ya kugundua waliyemuua ni Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alitumikia cheo cha mkurugenzi wa TISS kati ya mwaka 1983 na 1995.

Hapo ndipo mwili wake sasa ukahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC ili kuhifadhiwa ukisubiri taratibu nyingine za kisheria na mazishi.

Lakini ilikuja kubainika kuwa gari la marehemu namba TZD 8592 aina ya Nissan Patrol lilikuwa likifanana na la Ladwa na siku kadhaa nyuma, polisi Jijini Dar es Salaam, walikuwa wamelikamata na kuliachia baada ya kuridhika silo.

Ingawa Kombe na familia yake ni wenyeji wa Kilimanjaro, wana nyumba jijini Dar es Salaam.

Wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa fiche zilizowaambia kuwa mwizi aliyeiba gari hilo alikuwa amelipeleka mkoani Kilimanjaro, hivyo ofisi ya RCO Dar es Salaam ikawatuma Polisi wawili kwenda Kilimanjaro.

Makachero hao kwa mujibu wa hukumu ya rufaa namba 8 ya 1998 iliyotolewa na majaji watatu wa mahakama ya Rufani iliyoketi Jijini Arusha na kutoa hukumu yake Machi 16,1992, ni Sajini Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa.

Hukumu hiyo ilitolewa na majaji Lameck Mfalila, Barnabas Samatta na Kahwa Lugakingira kutokana na hukumu ya kifo iliyotolewa Januari 26,1998 na Jaji Buxton Chipeta dhidi ya askari wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku.

Kulingana na nyaraka za mahakama ya Rufani, Sajin Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa, waliondoka Jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wakiwa na gari lingine la Ladwa likiendeshwa na dereva wake aitwaye Ismail Katembo.

Dereva huyo ndio angetumika pia kulitambua gari la Ladwa lililoibwa na wote watatu waliwasili Moshi Juni 27,1996 na kuripoti Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na RCO ambaye aliamua kuwaongezea nguvu.

Hapo wakaongezewa makachero watatu, koplo Elisante Tarimo aliyekuwa mshtakiwa wa pili, Koplo Chediel Elinisafi aliyekuja kuwa mshtakiwa wa nne na Konstebo Mataba Matiku aliyekuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo.

Makachero hao walipewa bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) namba N.1270 na risasi 30 ambayo ilibebwa na Mataba Matiku wakati Sajenti Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa kila mmoja alikuwa na bastola yenye risasi nane.

Koplo Elisante Tarimo na Chediel Elinisafi wao hawakuwa na silaha yoyote.

Kwa hiyo timu hiyo ya makachero ikaanza msako wa kulitafuta gari mali ya DW Ladwa aina ya Nissan Patrol lenye namba TZG 50 ambalo lilikuwa likifanana na gari la Luteni Jeneral Kombe TZD 8592 lililokamatwa Jijini Dar es Salaam na kuachiwa.

Siku hiyo ya Juni 30, 1996 kwenye saa 10 alasiri wakiwa katika misheni ya kulisaka gari hilo la Ladwa, wakiwa eneo la kijiji cha Shiri Njoro barabara ya Moshi-Arusha wakati huo wakiwlekea barabara hiyo kuu, mbele waliona gari la Kombe.

Dereva Ismail Katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha-Moshi ndio gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Polisi hao waligeuza gari lao na kuanza kulifukuza gari la Kombe ambalo lilikuwa likifanana kwa rangi na lile na DW Ladwa lililokuwa likitafutwa na wakati wakilifukuza walianza kulishambulia kwa risasi kumlazimisha asimame.

Imran Kombe ni nani

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran Kombe, alikuwa mwanajeshi na kachero wa usalama wa Taifa ambapo katika vita Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza brigedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumtoa Nduli Idd Amin.

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ na kwa mujibu wa taarifa za mitandao zinaonyesha Desemba 30, mwaka huo, alipandishwa cheo na kuwa meja jenerali na mwaka uliofuata aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Hungary.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Uslama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na kustaafu. Aliuawa kwa kushambuliwa kwa risasi Juni 30,1996.

Baada ya mauaji hayo, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya kukusudia haijasikilizwa na kutolewa hukumu.

Fuatilia hapa Kesho.............
Hii nilipata kuisikia tangu nikiwa shule ya msingi miaka ya 90
 
Haya matukio siri zake huja kuwekwa wazi baada ya miaka mingi kupita. Kuna tukio la Lissu, yuko hai alinusurika kuuwawa kwa kushambuliwa kwa risasi, hivi huyu mwamba hawezi kuandika kitabu kuelezea mkasa ule yeye mwenyewe au hana intelejensia kufuatilia chanzo cha mkasa ule, au ataandikiwa kitabu na wengine miaka mingi ijayo? Aanze kutoa ndondoo kwa waandishi wa vitabu vya mikasa ya kweli umma ujue ilikuaje akashambuliwa vile
 
Kama una soga zilete hapa basi
Sina soga zaidi isispokuwa nilikuwa najaribu tu kulinganisha matukio haya mawili kwa sababu yote yana upekee uliofanana sana.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kumpoteza Mkurugenzi wa TISS, na possibly, mara ya kwanza kumpoteza Mwanajeshi ambaye ni LUTENI GENERAL kwa sababu at any time t, LUTENI GENERAL huwa ni mmoja tu Tanzania nzima
 
Kwa akili zangu kutokea Itamka Ilongero ni kwamba Dereva nae alinyweshwa sumu ili asije kutoboa siri maana ni raia
 
Ni mauaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Juni 30 mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (conspiracy theory) kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba kweli aliuawa na polisi.

Katika mfululizo wa makala hii, Mwandishi Wetu atakuletea simulizi ya nini hasa kilisababisha mauaji yake, nani walimfyatulia risasi zaidi ya 15, maelezo ya maungamo ya wauaji wake yanasemaje na familia ililipwa fidia ya Shilingi ngapi.

Simulizi hii inaegemea ushahidi uliotolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidia iliyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na simulizi zilizogubika mauaji hayo.

Maneno yalisemwa mengi, mojawapo ni hisia kuwa huenda aliuawa kwa sababu ya urafiki wake wa karibu na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi 1995, lakini kwa kesi ilivyokuwa mahakamani haikuwa sahihi.

Kwa kuwa Kombe alikuwa amepigwa risasi na polisi, licha ya kuripotiwa kuinua mikono yake juu kama ishara ya kujisalimisha kwa watu walioamini ni wezi wa gari, kulikuwa na uvumi kwamba mauaji yake yalikuwa yamepangwa.

Ni kutokana na hisia hizo na moto wa kisiasa juu ya mauaji hayo, Rais wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ambayo iliwasilisha ripoti yake 1997 ambayo si wazi, ikisema Serikali haikuwa na mkono katika mauaji hayo.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva aliyekuwa na Jaji Mussa Kipenka wakati huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali, ilihoji mashahidi 52 na mwaka 1997 ilitoa ripoti kwa Mkapa iliyohitimisha kwamba Serikali haikuwa na mkono wowote katika kifo cha Kombe.

Hadi sasa taarifa ya tume hiyo, kama zilivyo baadhi ya tume zilizoundwa kutafuta ukweli wa jambo ambalo linaibua hisia kali, imekuwa ni siri.

Mwaka 1998, Mbunge wa Temeke Jijini Dar es Salaam, Augustino Mrema aliibua hoja bungeni kuwa kifo cha Kombe kilikuwa sehemu ya mpango wa mauaji uliofanywa na Serikali, ingawa hata hivyo alishindwa kuthibitisha madai hayo. Pamoja na taarifa hiyo ya tume na ushahidi uliotolewa mahakamani kuhusiana na mauaji ya Kombe, bado baadhi ya watu hadi sasa wana hisia tofauti juu ya mauaji hayo na katika makala hii tutakuletea mwanzo mwisho nini kilitokea.

Timu ya makachero ilivyoundwa

Usiku wa Juni 30, 1996 na siku iliyofuata, kulizagaa taarifa za kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa Luteni Jenerali Kombe, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa tano wa TISS na taarifa hizo hazikuzagaa kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyo sasa.

Wakati huo wala simu za kiganjani (kitochi) zilikuwa hazijawa nyingi, licha ya kwamba zilianza kuingia nchini mwaka 1994, hivyo taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu na katika mji wa Moshi, watu walikaa katika makundi wakijadili.

Taarifa hizo zilisema polisi walimuua Kombe kwa kummiminia risasi hata baada ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha, na maiti yake ilipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mawenzi.

Polisi wakati huo walikuwa wanaamini wamemuua mtu waliyekuwa wanaamini ni mwizi mashuhuri wa magari na walikuwa wakitamba kufanikiwa kukamata gari Nissan Patrol namba TZG 50 mali ya D.W Ladwa lililoibwa Jijini Dar es Salaam.

Ni hadi mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro alipopokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Iwisi Shoo, akimwambia gari walilolikamata si lenyewe na mtu waliyemuua si mwizi, bali ni Kombe, mkuu wa zamani wa TISS.

Hapo ndipo Polisi wenyewe walijikuta wakipata ganzi baada ya kugundua waliyemuua ni Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alitumikia cheo cha mkurugenzi wa TISS kati ya mwaka 1983 na 1995.

Hapo ndipo mwili wake sasa ukahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC ili kuhifadhiwa ukisubiri taratibu nyingine za kisheria na mazishi.

Lakini ilikuja kubainika kuwa gari la marehemu namba TZD 8592 aina ya Nissan Patrol lilikuwa likifanana na la Ladwa na siku kadhaa nyuma, polisi Jijini Dar es Salaam, walikuwa wamelikamata na kuliachia baada ya kuridhika silo.

Ingawa Kombe na familia yake ni wenyeji wa Kilimanjaro, wana nyumba jijini Dar es Salaam.

Wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa fiche zilizowaambia kuwa mwizi aliyeiba gari hilo alikuwa amelipeleka mkoani Kilimanjaro, hivyo ofisi ya RCO Dar es Salaam ikawatuma Polisi wawili kwenda Kilimanjaro.

Makachero hao kwa mujibu wa hukumu ya rufaa namba 8 ya 1998 iliyotolewa na majaji watatu wa mahakama ya Rufani iliyoketi Jijini Arusha na kutoa hukumu yake Machi 16,1992, ni Sajini Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa.

Hukumu hiyo ilitolewa na majaji Lameck Mfalila, Barnabas Samatta na Kahwa Lugakingira kutokana na hukumu ya kifo iliyotolewa Januari 26,1998 na Jaji Buxton Chipeta dhidi ya askari wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku.

Kulingana na nyaraka za mahakama ya Rufani, Sajin Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa, waliondoka Jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wakiwa na gari lingine la Ladwa likiendeshwa na dereva wake aitwaye Ismail Katembo.

Dereva huyo ndio angetumika pia kulitambua gari la Ladwa lililoibwa na wote watatu waliwasili Moshi Juni 27,1996 na kuripoti Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na RCO ambaye aliamua kuwaongezea nguvu.

Hapo wakaongezewa makachero watatu, koplo Elisante Tarimo aliyekuwa mshtakiwa wa pili, Koplo Chediel Elinisafi aliyekuja kuwa mshtakiwa wa nne na Konstebo Mataba Matiku aliyekuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo.

Makachero hao walipewa bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) namba N.1270 na risasi 30 ambayo ilibebwa na Mataba Matiku wakati Sajenti Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa kila mmoja alikuwa na bastola yenye risasi nane.

Koplo Elisante Tarimo na Chediel Elinisafi wao hawakuwa na silaha yoyote.

Kwa hiyo timu hiyo ya makachero ikaanza msako wa kulitafuta gari mali ya DW Ladwa aina ya Nissan Patrol lenye namba TZG 50 ambalo lilikuwa likifanana na gari la Luteni Jeneral Kombe TZD 8592 lililokamatwa Jijini Dar es Salaam na kuachiwa.

Siku hiyo ya Juni 30, 1996 kwenye saa 10 alasiri wakiwa katika misheni ya kulisaka gari hilo la Ladwa, wakiwa eneo la kijiji cha Shiri Njoro barabara ya Moshi-Arusha wakati huo wakiwlekea barabara hiyo kuu, mbele waliona gari la Kombe.

Dereva Ismail Katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha-Moshi ndio gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Polisi hao waligeuza gari lao na kuanza kulifukuza gari la Kombe ambalo lilikuwa likifanana kwa rangi na lile na DW Ladwa lililokuwa likitafutwa na wakati wakilifukuza walianza kulishambulia kwa risasi kumlazimisha asimame.

Imran Kombe ni nani

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran Kombe, alikuwa mwanajeshi na kachero wa usalama wa Taifa ambapo katika vita Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza brigedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumtoa Nduli Idd Amin.

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ na kwa mujibu wa taarifa za mitandao zinaonyesha Desemba 30, mwaka huo, alipandishwa cheo na kuwa meja jenerali na mwaka uliofuata aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Hungary.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Uslama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na kustaafu. Aliuawa kwa kushambuliwa kwa risasi Juni 30,1996.

Baada ya mauaji hayo, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya kukusudia haijasikilizwa na kutolewa hukumu.

Fuatilia hapa Kesho.............
Asante sana mkuu, ila pale uluposema story inabase kwenye hukumu Ya kesi, na nikiwaza alielalamikiwa ni serikali, alie hukumu serikali na hukumu haijamtia hatiani serikali... Naona najilisha upepo tu... 😁 😁 😁
 
SIMULIZI YA MAUAJI YA GENERALI IMRAN KOMBE
(PART I)

IMRAN KOMBE NI NANI?

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran kombe , alikuwa mwanajeshi na kachero wa usalama wa taifa ambapo katika vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza bregedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumuondoa Nduli Idd Amin

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ na kwa mujibu wa taarifa za mitandao zinaonyesha Desemba 30, mwaka huo alipandishwa cheo na kuwa meja jenerali na mwaka uliofuata aliongoza ujembe wa Tanzania kwenda Hungary.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na Kustaafu.

Aliuwawa kwa kushambuliwa na risasi mnamo Juni, 1996.

Baada ya mauwaji hayo jeshi la polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya haijasikilizwa na kutolewa hukumu

Ni mauwaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofautyi juu ya nini hasa kiini cha mauwaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuwawa kwa kupigwa risasi June 30 mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (consirancytheory) kwambapengine kuna mkono wa mtu katika mauwaji hayo yaliyotokea katika kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba kwelialiuwawa na Polisi.

Sasa wacha nikuletee simulizi ya nini hasa kilisababbishamauwaji yake, nani walimfyatulia risasi Zaidi ya 15, maelezo ya maungamano ya wauwaji wake yansemaje na familia ililipwa fidia shilingi ngapi.

Simulizi hii inaegemea ushahidi ulitolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidiailiyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serilkali (AG) na Simulizi ziligubika mauwaji hayo.

Hisia zilikuwa nyingi mojawapo ni hisia kuwa huendaaliuwawa kwasababu ya urafiki wake wa karibu nan a Agustono Lyatonga Mrema, Mgombea urais kwa tiketi ya NCCR –Mageuzi 1995, lakini kwa kesi iliyokuwa mhakamani haikuwa sahihi.

Kwakuwa Kombe alikuwa amepigwa risasi na polisi, licha ya kuripoiwa kuinua mikono yake juu kama ishara ya kujisalimisha kwa watu walioamini ni wezi wa gari,kulikuwa na uvumi kwamba mauwaji yake yalikuwa yamepangwa.

Ni kutokana na hisia hizio na moto wa kisiasa juu a mauwaji hayo, Rais wa awamu ya tatu hayati Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo ambayo iliwasilisha taarifa yake 1997 ambayo si wazi, ikisema Serekali ilikuwa na Mkono wake katika mauwaji hayo.

Tume hiyo ilikuwa chini ya mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva aliyekuwa na Jaji Musa Kipenka wakti huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa serekali

Ilihoji mashahidi 54 mwaka 1997 ilitoa ripoti kwa Mkapa iliyohitimisha kwamba Serekali haikuwa na Mkono wowote katika kifocha Kombe.

Hadi sasa taarifa ya tume hiyo, kama ilivyotume baadhi ya tume zilizoundwa kutafuta ukweli wa jambo linaibua hisia kali, imekuwa ni siri.

Mwaka 1998, Mbunge wa Temeke Jijini Dar es Salaam, Agustino Mrema aliibua hoja Bungeni kuwa kifo cha Kombe kilikuwa mpango wa mauwaji uliofanywa na Serekali, Ingawa hata hivyo alishindwa kuthibitishamadai hayo.

Pamoja na taarifa ya Tume na ushahidi uliotolewa mahakakamani kuhusiana na mauwaji ya Kombe, bado baadhi ya watu hadi sasa wana hisia tofauti juu ya mauwaji hayo.

Timu ya makachero ilivyoundwa.

Usiku wa June 30, 1996 na siku iliyofuata, kulizagaa taarifa za uuwawa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa Luteni General Imran Kombe, aliyekuwa mkurugenzi wa tano wa usalama wa Taifa (TISS), taarifa hizo zilisambaa kama moto wa kifuu kaika mji wa Moshi watu wakiwa katika vikundi wakijadili juu ya mauwaji hayo.

Taarifa zilisema Polisi walimuua Kombe kwa kumiminia Risasi hata baada ya kushuka kwenye gari laki huku akiwa amejisalimisha kwa kunyanyua mikono juu ishara ya kujisalimisha, Mwili wake ulipelekwa katiaka chmba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mawenzi.

Polisi wakati huo walikuwa wanaamini wamemuua mtu ambaye waliamini alikuwa mwizi mashuhuri wa magari na walikuwa wakitamba kufanikiwa kukamata gari Nissan Patrol namba TZG 50 maili ya D.W Ladwa lililoibiwa Jijini Dar es Slaam.

Ni hadi mkuu wa polisi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro alipopokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha Iwisi Shoo, akimwambia gari walilolikamata sio lenyewe na mtu waliyemuwa sio mwizi, bali ni Kombe mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa.

Hapo ndipo pilisi wenyewe walijikuta wakipata ganzi baada ya kugundua waliyemuua ni Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alitumikia cheo cha Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS) kati yam waka 1983 na 1985.

Hapo ndipo mwili wake ukahamishiwa katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Kaskazini ya KCMC ili kuifadhiwa kusubiri taratibu zingine za kisheria na mazishi.

Likini ilikuja kujulikana kuwa gari la marehemu lenye namaba TZD 8592 iaina ya Nissan Patrol lilikuwa likifanana na la Ladwa na siku kadhaa nyuma, walikuwa wamelikamata na kuliachia baada ya kuridhika silo lenyewe.

Ingawa Kombe na Familia yake ni wenyeji wa Kilimanjaro, wana makazi yao jijini Dar es Salaam.

Wakati Polisi wanaendelea na Uchunguzi, walipata taarifa fiche zilizowaambia kuwa mwizi aliye iba gari hilo alikuwa amelipeleka gari hilo Mkoani Kilimanjaro, Hivyo Ofisi ya RCO Dar es Salaam ikawatuma polisi wawili kwenda Kilimanjaro.

Makachero hao kwa mujibu wa hukumu namba 8 ya 1998 iliyotolewa na majaji watatu wa mahakama ya Rufani iliyoketi Jijini Arusha na kutoa hukumu yake Machi 16, 1998 ni Sajini Thomas Mensah na Koplo Juma Mswa.

Hukumu hiyo ilitolewa na Majaji Lameck Mfalila, Barnabas Samatta na Kahwa Lugakingira kutokana na hukumu ya kifo ya kifo iliyotolewa na January 26, 1998 na Jaji Buxton Chipeta dhidi ya askari wawili, Koplo Juma Maswa na Konsteble Mataba Matiku.

Kulingana na nyaraka za mahakama ya Rufaa , Sajini Thomas Mensah na Koplo Juma Mswa , Waliondoka jijnini Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wakiwa na gari linguine la Ledwa likiendeshwa na dereva wake aitwaye Ismail Katembo.

Dereva huyo ndio angetumika pia kulitambua gari hilo la Ladwa lililoibiwa, na wote watatu waliwasili Moshi Juni 27, 1996 na kuripoti makao makuu ya polisi Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa nan a RCO ambaye aliamua kumuongezea nguvu.

Hapo wakaongezewa na Makechoro watatu, Koplo Elisante Tarimo aliyekuwa mshitakiwa wa pili, koplo chediel Elinisafi aliyekuja kuwa mshtakiwa wan ne na Konstebo Mataba Matifu alikuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo.

Makachero hao walipewa bunduki aina ya Submachine Gun (SMG) namba N.1270 na risasi 30 ambayo ilibebwa na Mtaba Matiku wakati Sajento Thomas Mensah na Koplo Juma Mswa kila mmoja alikuwa na bastola yenye risasi nane.

Koplo Elisante Tarimo na Chediel Elinisafi wao hawakuwa na silaha yoyote.

Kwa hiyo timu hiyo ya makachero ikaanza msako wa kulitafuta gari mali ya DW Ladwa aina ya Nissan Patrol lenye usajili TZG 50 ambalo lilikuwa likifanan na gari la lutein Jenerali Imran Kombe TZD 8592 lilokamatwa jijini Dar es Salaam na kuachiwa.

Siku hiyo ya juni 30,1996 kwenye saa 10 alasiri wakiwa katika misheni ya kulisaka gari hilo la Ladwaa, wakiwa eneo la kijiji cha XShiri Njoro barabara ya Moshi – Arusha wakati wakielelekea barabara hiyo kuu, mbele waliona gari ya Kombe.

Dereva wa Ismail katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha – Moshi ndilo gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Polisi hao waligeuza gari na kuanza kulifuta gari la Kombe ambalolilikuwa likifanana rangi na lile la DW Ladwa lilokuwa lilikitafutwa, na wakati wakilifukuza walianza kulishambulia kwa risasi kummlazimisha asimame.

Itaendelea
 
Sehemu ya Pili

Ni mauaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuawa kwa risasi Juni 30, mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (conspiracy theory) kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo yaliyotokea Kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba, ni kweli aliuawa na polisi?

Simulizi hii inaegemea ushahidi uliotolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidia iliyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na simulizi zilizogubika mauaji hayo.

Maneno yalisemwa mengi, mojawapo ni hisia kuwa huenda aliuawa kwa sababu ya urafiki wake wa karibu na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea urais wa NCCR-Mageuzi 1995, lakini kwa kesi ilivyokuwa mahakamani haikuwa sahihi.

Ni kutokana na hisia pengine mauaji yake yalikuwa ya kupangwa, Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ambayo iliwasilisha ripoti yake 1997 ambayo sio wazi, ikisema Serikali haikuwa na mkono katika mauaji hayo.

Katika mfululizo wa makala hii, mwandishi wetu atakuletea simulizi ya nini hasa kilisababisha mauaji yake, nani walimfyatulia risasi zaidi ya 15, maelezo ya maungamo ya wauaji wake yanasemaje na familia ililipwa fidia ya kiasi gani cha fedha.

Katika makala iliyopita, tuliona namna makachero wa Jeshi la Polisi Dar es Salaam walivyosafiri hadi Moshi na kuungana na wenzao na kuanza kutafuta gari aina ya Nissan Patrol namba TZG 50, mali ya DW Ladwa lililokuwa limeibwa Juni 24,1996.

Tuliishia pale ambapo dereva wa gari lililokuwa linatumiwa na makachero, ambalo nalo ni mali ya Ladwa, alipoona gari la Kombe linalofanana na wanalolitafuta likitokea barabara ya Arusha na kusema ndilo gari lililoibwa.

Dereva, Ismail Katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha-Moshi ndio gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Hapa, Kombe hakujua kuwa ndio mwisho wa maisha yake umefika.

Badala ya kusimama, alipowapita, Luteni Jenerali Kombe alikata kushoto na kuendelea kuingia ndani kidogo, hapo polisi nao waligeuza gari lao na kulifukuza gari ambalo waliamini ni mshukiwa hatari anatoroka, huku wakifyatua risasi.

Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na marehemu lilisimama baada ya kugonga kisiki, ambapo risasi zilizofyatulia na mshtakiwa wa tatu, Koplo Juma Mswa na wa tano, Konstebo Mataba Matiku zilimpata Kombe na kumuua papo hapo.

Baada ya mauaji, taarifa ilipelekwa kwa RCO Kilimanjaro na kumjulisha kuwa gari lililokuwa limeibwa limepatikana na mwizi hatari aliyekuwa nalo ameuawa.

Lakini, muda mfupi baada ya RCO kujulishwa hivyo, alipokea taarifa kwa simu kutoka kwa mtu aitwaye Iwisi Shoo akimtaarifu kuwa gari la Ladwa lililokuwa limeibwa Dar es Salaam bado halijapatikana na aliyeuawa si jambazi ni Luteni Jenerali Kombe.

Hapo ndipo askari wote watano na dereva walipokamatwa ambao ni Sajini Mensah na Koplo Mswa na dereva wa kiraia waliyetoka naye Dar es Salaam, Katembo na makachero Tarimo, Elinisafi na Matiku walipotiwa mbaroni.

Ushahidi wa mke

Roseleen Kombe ambaye ni mke wa Luteni Jenerali Kombe ambaye walikuwa pamoja kwenye gari, alitoa ushahidi na kueleza kuwa katika kipindi gari hilo la Ladwa linalofanana kwa rangi na lao lilipoibwa, walikuwa jijini Dar es Salaam.

Ni kutokana na mfanano huo wa rangi, gari lao lilitiliwa shaka na lilikakamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam na baadaye kuthibitika silo na wakakabidhiwa gari lao.

Alisimulia mbele ya Jaji Chipeta kuwa Juni 30, 1996 alirejea Moshi na kumkuta mumewe nyumbani kwao kijiji cha Mailisita na ilipofika saa 10 alasiri, yeye na mumewe waliondoka nyumbani kutumia gari hiyo kuelekea Moshi.

Njiani walikuwa na miadi ya kukutana na mfanyakazi wao mpya, lakini baada ya kusafiri kwa kipindi fulani, aliona gari inayokuja mbele yao ikiwa na watu wanne.

Kabla ya kuwafikia, mumewe ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari, alionyesha indiketa kuwa anaingia kushoto, lakini hawakwenda mbali sana ndipo aliposikia mlipuko wa bunduki na ziliendelea na moja ilimpata mumewe kwenye bega.

Kwa mujibu wa Roseleen, alimsikia mumewe akisema “Jiiii” na akamshauri watoke ndani ya gari na kukimbia, na kwamba yeye alitoka na kuanza kukimbia lakini katikati ya kukimbia, alianguka na kusimama tena kisha kuendelea kukimbia.

Roseleen aliiambia mahakama kuwa aliwasikia watu waliokuwa wakiwashambulia wakisema “Tena wako wawili”, na muda wote huo yeye na mumewe walikuwa wanaamini wamevamiwa na majambazi waliokuwa wanataka kuwapora gari.

Anaeleza kuwa yeye aliendelea kukimbia hadi alipofika kwenye nyumba fulani na kujificha nyuma ya gari lililoegeshwa hapo ambapo alikaa hapo hadi alipojiridhisha kuwa hali imetulia ndipo alipoamua kujitokeza kutoka mafichoni.

Alipotoka mafichoni alisikia watu wakisema “majambazi mengi, upoteze maisha kwa sababu ya gari,” hapo ndipo alibaini mumewe ameuawa.

Uchunguzi wa daktari ulibaini kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na matundu tisa ya risasi, manne yanatokana na risasi zilipoingilia na manne mahali zipotokea na risasi hizo zilimpata marehemu eneo la kifua na tumboni na kumuua papo hapo.

Kulingana na uchunguzi huo, wauaji walimshambulia katika umbali usiozidi mita 30 au chini ya hapo na hiyo pekee ilithibitisha kuwa kulikuwa na lengo la kumuua (intention) na risasi zote zilizoingia kwenye mwili zilitoka kupitia kwenye mifupa.

Pamoja na Roseleen Kombe, lakini upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi zaidi ya 15 ambao baada ya kufunga ushahidi wao, mahakama iliwaona washtakiwa watano walikuwa na kesi ya kujibu, ambapo walipanda kizimbani kujitetea.

Hii ni baada ya mshtakiwa wa sita, Ismail Katembo aliyekuwa dereva akiwaendesha washtakiwa ambao ni askari, kufariki dunia akiwa mahabusu.

Fuatilia hapa SEHEMU YA TATU Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)
 
SEHEMU YA TATU

‘Tuliyalenga matairi ya gari sio Imran Kombe’​

  • Katika simulizi iliyopita, tuliona namna Mkurugenzi wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe alivyomiminiwa risasi 15 na Polisi waliodai wamefananisha gari alilokuwa akiliendesha, na lile lililoibwa jijini Dar es Salaam.
Katika simulizi hiyo pia tuliona namna mkewe, Roseleen Kombe alivyoelezea kwa kina nini kilichowapata yeye na mumewe aliyeuawa siku hiyo Juni 30, 1996 na Mahakama ikawakuta washtakiwa wote watano wakiwa na kesi ya kujibu.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa sita, Sajini Thomson Mensah, Koplo Elisante Tarimo, Koplo Juma Mswa, Chediel Elinisafi na Konstebo Mataba Matiku na raia pekee, Ismail Katembo ambaye alifariki akiwa mahabusu kabla kesi haijasikilizwa.

Hata hivyo, katika simulizi ya utetezi wa washtakiwa, tutaegemea utetezi wa washtakiwa wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku, ambao walipatikana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa huku watatu wakiachiwa huru.

Polisi hao wawili, mmoja Koplo Juma Mswa alikuwa na bastola na Konstebo Mataba Matiku alikuwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) na kwa uchache, walifyatua risasi zisizopungua 15 kuelekea kwenye gari la Kombe.

Mshtakiwa aeleza alivyofyatua risasi

Katika utetezi wake, koplo Juma Mswa aliyekuwa na namba C7874, alieleza namna yeye na mshtakiwa wa kwanza, Sajini Thomson Mensah walioondoka Dar es Salaam kwenda Moshi kutafuta gari lililoibwa na namna walivyokutana nalo.

Alieleza kuwa Juni 30, 1996 saa 10 alasiri walivyokutana na gari walilokuwa wakilitafuta na namna lilivyochepuka na kuingia kwenye njia inayoelekea kwenye shamba la mahindi, katika Kijiji cha Mailisita kilichopo wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Baada ya gari yao (gari ya Ladwa) waliyokuwa wakiitumia kusimama, mshtakiwa wa kwanza, Sajenti Thomson Mensah aliyekuwa kiongozi wa timu, aliwaamuru kushuka mara moja kutoka katika gari hiyo na kufyatua risasi hewani.

Aliiambia Mahakama kuwa ufyatuaji wao huo wa risasi hewani haukulifanya gari waliloelezwa ndilo walilokuwa wakilitafuta kusimama, hivyo waliamua kulenga magurudumu ingawa ilikuwa vigumu kupata shabaha kutokana na barabara.

Alieleza kuwa Kombe alikuwa na jeraha la risasi begani na majeraha mengine na hii kwa maoni yake inathibitisha kuwa hawakuwa na nia ovu wakati wanalifyatulia risasi gari ambalo alikuwa akiliendesha Kombe, akiwa amempakiza mkewe.

Katika utetezi wake alikiri kuwa marehemu hakuwa na silaha lakini baada ya gari la marehemu kusimama na mlango wa abiria kufunguliwa, alifyatua risasi kwa lengo la kumzuia mshukiwa wa wizi wa gari asitoroke na alimuona akianguka.

Alikanusha kufyatua risasi akimlenga Kombe au gari yake lakini alimuona marehemu akishuka kutoka kwenye gari yake na akakimbia hatua chache kisha akaanguka, akisisitiza kuwa aliposhuka kwenye gari hakujisalimisha.

Alisisitiza kuwa ana uhakika kuwa hakuna risasi hata moja iliyokuwa imetoka katika silaha aliyokuwa amekabidhiwa ambayo ilimgusa marehemu kwa kuwa wakati anafytua risasi, yeye alilenga magurudumu ya gari na sio mtu.

Mshtakiwa wa tano, Mataba Matiku mwenye namba E.3479 alieleza baada ya gari ya Kombe kugonga kisiki, waliamriwa na mshtakiwa wa kwanza (Mensah) washuke chini mara moja na wafyatue risasi hewani ili gari la Kombe lisimame.

“Nilishuka kwenye gari na mshtakiwa wa tatu (Juma Mswa) alinifuata. Nilifyatua risasi moja hewani. Nilipokuwa natega (cock) sijui ni risasi ngapi zilitoka kwenye bunduki. Ninachojua bunduki yangu ilikuwa na matatizo.

“Nilirekebisha ile dosari. Lile gari halikusimama. Tuliendelea kulifukuza na kufyatua risasi kuelekea kwenye magurudumu. Gari lilikuwa na mwendo mkali. Sikuhesabu ni risasi ngapi nilifyatua huku nikikimbia,” alisema na kuongeza;

“Nilipokuwa nalenga magurudumu nilikuwa umbali wa kama mita 25 kutoka lilipo gari tulilokuwa tunalifukuza. Niliamua kulenga maguruduu kulipunguza kasi ili tuweze kumkamata mshukiwa aliyekuwa nalo na kulikamata gari pia”

“Nisingeweza kufanya hivyo kwa njia nyingine kwa sababu nilikuwa kwa miguu. Lakini pia mshtakiwa wa tatu (Juma Mswa) alifyatua risasi tatu hewani. Nilizisikia risasi kutoka nyuma yangu. Ilikuwa kama hatua tano tu nyuma yangu”

“Baadaye hilo gari liligonga kisiki. Niliacha kuendelea kulifyatulia risasi baada ya kusimama. Nikaona mlango wa kushoto ukifunguliwa halafu mtu akashuka na kudondoka chini. Lakini alisimama na kukimbia,”alieleza katika utetezi wake.

“Mshtakiwa wa tatu alifyatua risasi kuelekea kule mbele alikokuwa kama kumpa ishara (marehemu) asimame. Halafu marehemu akadondoka. Hakusimama tena. Sikujua kama risasi yake ililenga shabaha au la. Alikuwa amekufa”

Katika utetezi wake huo, alisema wakati huo alikuwa na uhakika kuwa hakuna risasi hata moja aliyoifyatua kumgusa Kombe kwa kuwa alikuwa amelenga magurudumu ya gari alilokuwa akiliendesha na sio yeye.

Wakati akitoa utetezi huo, Daktari wa Patholojia, Ndetiyo Pallangyo aliyechunguza mwili wa Kombe katika ushahidi wake alisema kwa kuwa vichwa vya risasi havikupatikana katika mwili wake, majeraha yalikuwa ni ya bastola au SMG.

Kwa mujibu wa Dk Pallangyo, kwa nje mwili wa Kombe ulikuwa na majeraha tisa, ambapo manne ni risasi zilipoingilia, na manne ni risasi zilipotokea na kwa ujumla risasi hizo ziliingia kupitia kifuani na tumboni na kuharibu viungo.

Katika simulizi yetu kesho, tutawaletea hukumu ya Jaji Buxton Chipeta aliyesikiliza kesi hiyo na kuwahukumu adhabu ya kifo, na kwa nini aliwatia hatiani na kuwapa adhabu hiyo ambayo ndio pekee kwa anayepatikana na hatia ya mauaji.

Imran Kombe ni nani

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran Kombe, alikuwa Mwanajeshi na Kachero wa Usalama wa Taifa ambapo katika vita vya Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza Brigedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumtoa Nduli Idd Amin.

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na alipandishwa cheo na kuwa Meja Jenerali.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na kustaafu. Juni 30,1996 akauawa kwa risasi.

Moja ya sifa kubwa ya Jenerali Kombe hadi sasa, ni picha zake kutokuwepo katika mitandao ya kijamii kama walivyo waliokuja kurithi mikoba yake baada ya kustaafu na anachukuliwa kama kachero ambaye hakujulikana sana.

Baada ya mauaji hayo, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya kukusudia haijasikilizwa na kutolewa hukumu.

Januari 26,1998 Mahakama Kuu Kanda ya Moshi chini ya Jaji Buxton Chipeta ilitoa hukumu yake ambapo iliwatia hatiani askari wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku na kuwahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

Katika kitabu chake cha mwaka 2000 kilichopewa jina la Genocide and Covert Operations in Afrika 1993-1999, mwandishi Wayne Madsen alidai mwaka 1994, Kombe alifahamu juu ya mipango ya mauaji ya Rais wa Rwanda, Habyarimana.

Kulingana na Madsen, Kombe alifahamu pia mipango ya mauaji ya Rais wa Kenya, Daniel Arap Moi na wa Zaire, Mabutu Sese Seko na anaeleza kuwa Kombe alimdokeza Moi ambaye naye akamuonya Mabutu juu ya uwepo wa mipango hiyo.

SEHEMU YA NNE Soma hapa >> Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)
 
  • Thanks
Reactions: I M
Ni mauaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Juni 30 mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (conspiracy theory) kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba kweli aliuawa na polisi.

Katika mfululizo wa makala hii, Mwandishi Wetu atakuletea simulizi ya nini hasa kilisababisha mauaji yake, nani walimfyatulia risasi zaidi ya 15, maelezo ya maungamo ya wauaji wake yanasemaje na familia ililipwa fidia ya Shilingi ngapi.

Simulizi hii inaegemea ushahidi uliotolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidia iliyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na simulizi zilizogubika mauaji hayo.

Maneno yalisemwa mengi, mojawapo ni hisia kuwa huenda aliuawa kwa sababu ya urafiki wake wa karibu na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi 1995, lakini kwa kesi ilivyokuwa mahakamani haikuwa sahihi.

Kwa kuwa Kombe alikuwa amepigwa risasi na polisi, licha ya kuripotiwa kuinua mikono yake juu kama ishara ya kujisalimisha kwa watu walioamini ni wezi wa gari, kulikuwa na uvumi kwamba mauaji yake yalikuwa yamepangwa.

Ni kutokana na hisia hizo na moto wa kisiasa juu ya mauaji hayo, Rais wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ambayo iliwasilisha ripoti yake 1997 ambayo si wazi, ikisema Serikali haikuwa na mkono katika mauaji hayo.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva aliyekuwa na Jaji Mussa Kipenka wakati huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali, ilihoji mashahidi 52 na mwaka 1997 ilitoa ripoti kwa Mkapa iliyohitimisha kwamba Serikali haikuwa na mkono wowote katika kifo cha Kombe.

Hadi sasa taarifa ya tume hiyo, kama zilivyo baadhi ya tume zilizoundwa kutafuta ukweli wa jambo ambalo linaibua hisia kali, imekuwa ni siri.

Mwaka 1998, Mbunge wa Temeke Jijini Dar es Salaam, Augustino Mrema aliibua hoja bungeni kuwa kifo cha Kombe kilikuwa sehemu ya mpango wa mauaji uliofanywa na Serikali, ingawa hata hivyo alishindwa kuthibitisha madai hayo. Pamoja na taarifa hiyo ya tume na ushahidi uliotolewa mahakamani kuhusiana na mauaji ya Kombe, bado baadhi ya watu hadi sasa wana hisia tofauti juu ya mauaji hayo na katika makala hii tutakuletea mwanzo mwisho nini kilitokea.

Timu ya makachero ilivyoundwa

Usiku wa Juni 30, 1996 na siku iliyofuata, kulizagaa taarifa za kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa Luteni Jenerali Kombe, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa tano wa TISS na taarifa hizo hazikuzagaa kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyo sasa.

Wakati huo wala simu za kiganjani (kitochi) zilikuwa hazijawa nyingi, licha ya kwamba zilianza kuingia nchini mwaka 1994, hivyo taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu na katika mji wa Moshi, watu walikaa katika makundi wakijadili.

Taarifa hizo zilisema polisi walimuua Kombe kwa kummiminia risasi hata baada ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha, na maiti yake ilipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mawenzi.

Polisi wakati huo walikuwa wanaamini wamemuua mtu waliyekuwa wanaamini ni mwizi mashuhuri wa magari na walikuwa wakitamba kufanikiwa kukamata gari Nissan Patrol namba TZG 50 mali ya D.W Ladwa lililoibwa Jijini Dar es Salaam.

Ni hadi mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro alipopokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Iwisi Shoo, akimwambia gari walilolikamata si lenyewe na mtu waliyemuua si mwizi, bali ni Kombe, mkuu wa zamani wa TISS.

Hapo ndipo Polisi wenyewe walijikuta wakipata ganzi baada ya kugundua waliyemuua ni Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alitumikia cheo cha mkurugenzi wa TISS kati ya mwaka 1983 na 1995.

Hapo ndipo mwili wake sasa ukahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC ili kuhifadhiwa ukisubiri taratibu nyingine za kisheria na mazishi.

Lakini ilikuja kubainika kuwa gari la marehemu namba TZD 8592 aina ya Nissan Patrol lilikuwa likifanana na la Ladwa na siku kadhaa nyuma, polisi Jijini Dar es Salaam, walikuwa wamelikamata na kuliachia baada ya kuridhika silo.

Ingawa Kombe na familia yake ni wenyeji wa Kilimanjaro, wana nyumba jijini Dar es Salaam.

Wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa fiche zilizowaambia kuwa mwizi aliyeiba gari hilo alikuwa amelipeleka mkoani Kilimanjaro, hivyo ofisi ya RCO Dar es Salaam ikawatuma Polisi wawili kwenda Kilimanjaro.

Makachero hao kwa mujibu wa hukumu ya rufaa namba 8 ya 1998 iliyotolewa na majaji watatu wa mahakama ya Rufani iliyoketi Jijini Arusha na kutoa hukumu yake Machi 16,1992, ni Sajini Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa.

Hukumu hiyo ilitolewa na majaji Lameck Mfalila, Barnabas Samatta na Kahwa Lugakingira kutokana na hukumu ya kifo iliyotolewa Januari 26,1998 na Jaji Buxton Chipeta dhidi ya askari wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku.

Kulingana na nyaraka za mahakama ya Rufani, Sajin Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa, waliondoka Jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wakiwa na gari lingine la Ladwa likiendeshwa na dereva wake aitwaye Ismail Katembo.

Dereva huyo ndio angetumika pia kulitambua gari la Ladwa lililoibwa na wote watatu waliwasili Moshi Juni 27,1996 na kuripoti Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na RCO ambaye aliamua kuwaongezea nguvu.

Hapo wakaongezewa makachero watatu, koplo Elisante Tarimo aliyekuwa mshtakiwa wa pili, Koplo Chediel Elinisafi aliyekuja kuwa mshtakiwa wa nne na Konstebo Mataba Matiku aliyekuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo.

Makachero hao walipewa bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) namba N.1270 na risasi 30 ambayo ilibebwa na Mataba Matiku wakati Sajenti Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa kila mmoja alikuwa na bastola yenye risasi nane.

Koplo Elisante Tarimo na Chediel Elinisafi wao hawakuwa na silaha yoyote.

Kwa hiyo timu hiyo ya makachero ikaanza msako wa kulitafuta gari mali ya DW Ladwa aina ya Nissan Patrol lenye namba TZG 50 ambalo lilikuwa likifanana na gari la Luteni Jeneral Kombe TZD 8592 lililokamatwa Jijini Dar es Salaam na kuachiwa.

Siku hiyo ya Juni 30, 1996 kwenye saa 10 alasiri wakiwa katika misheni ya kulisaka gari hilo la Ladwa, wakiwa eneo la kijiji cha Shiri Njoro barabara ya Moshi-Arusha wakati huo wakiwlekea barabara hiyo kuu, mbele waliona gari la Kombe.

Dereva Ismail Katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha-Moshi ndio gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Polisi hao waligeuza gari lao na kuanza kulifukuza gari la Kombe ambalo lilikuwa likifanana kwa rangi na lile na DW Ladwa lililokuwa likitafutwa na wakati wakilifukuza walianza kulishambulia kwa risasi kumlazimisha asimame.

Imran Kombe ni nani

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran Kombe, alikuwa mwanajeshi na kachero wa usalama wa Taifa ambapo katika vita Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza brigedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumtoa Nduli Idd Amin.

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ na kwa mujibu wa taarifa za mitandao zinaonyesha Desemba 30, mwaka huo, alipandishwa cheo na kuwa meja jenerali na mwaka uliofuata aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Hungary.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Uslama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na kustaafu. Aliuawa kwa kushambuliwa kwa risasi Juni 30,1996.

Baada ya mauaji hayo, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya kukusudia haijasikilizwa na kutolewa hukumu.

Fuatilia hapa Sehemu Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Sehemua Ya Pili)
Ukikubali kuungana na kuwatumikia mashetani, basi utakuwa umekubali kuwa shetani na kuishi kishetani maisha yako yote ya hapa duniani mpaka kufa kwako. Endapo kama hutaki, basi kataa kabisa kujiunga na mashetani tangu hatua za mwanzo kabisa, usikubali kutumika nao.
 
SEHEMU YA NNE
Katika Makala iliyopita, tuliangalia namna askari wawili wa Jeshi la Polisi, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku waliommiminia risasi 15, mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe walivyojitetea kortini.

Katika simulizi hiyo tuliona namna polisi hao waliokuwa na silaha aina ya bastola na bunduki Sub Machine Gun (SMG), walivyoamriwa na kiongozi wa timu, Sajini Thomson Mensah, kushuka kwenye gari na kufyatua risasi kadhaa hewani.

Kila mmoja alieleza namna alivyoshuka kwenye gari na kufyatua risasi hewani na baadaye kuamua kulenga magurudumu ya gari aina ya Nissan Patrol lililokuwa likiendeshwa na marehemu Kombe akiwa na mkewe, Roseleen Kombe.

Wote walikana kumlenga moja kwa moja Kombe na kusababisha kifo chake Juni 30, 1996 saa 10 alasiri katika kijiji cha Mailisita wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, mauaji ambayo hadi leo bado wananchi wana hisia tofauti.

Washtakiwa katika kesi hii walikuwa sita, Sajini Thomson Mensah, Koplo Elisante Tarimo, Koplo Juma Mswa, Chediel Elinisafi na Konstebo Mataba Matiku na raia pekee, Ismail Katembo ambaye alifariki akiwa mahabusu kabla kesi kusikilizwa.

Tukio hilo liligubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya Luteni Jenerali Imran Kombe.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo na nyingine ni kweli aliuawa na polisi.

Leo tunawaletea simulizi ya namna Jaji Buxton Chipeta wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alivyochambua ushahidi wa upande wa mashtaka na wa polisi hao wawili na kuona kuwa wana hatia na kuwahukumu adhabu ya kunyongwa.

Hukumu ya Jaji Chipeta

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Januari 26,1998, Jaji Chipeta aliyesikiliza kesi hiyo aliwaachia huru askari watatu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yao na kuwatia hatiani askari wawili kati ya hao watano.

Jaji alisema ni ukweli wakati mshtakiwa wa tatu, Koplo Mswa kutoka jijini Dar es Salaam na wa tano, Mataba Matiku kutoka ofisi ya RCO Kilimanjaro, walipoanza kufyatua risasi waliamini mtu aliyekuwa na gari ni mhalifu mwenye silaha.

“Lakini wakati marehemu alipotoka kwenye gari, washtakiwa hawa wawili walijua kuwa hakuwa na silaha. Mbali na hilo, marehemu hakujaribu kukabiliana nao wala kuwafuata. Badala yake alikimbia huku akiyumba.

Wakati huo mshtakiwa wa tatu na wa tano hawakuwa umbali unaozidi mita 30 kulingana na ushahidi wa shahidi wa tatu wa mashtaka na inaweza kuwa ni chini ya umbali huo kulingana na maelezo ya ziada ya mshtakiwa wa tano,”alieleza.

Jaji Chipeta aliendelea kusema kuwa “Kwa hiyo, washtakiwa hawa wawili walikuwa na kila fursa ya kumkamata bila kutumia silaha za kuua. Kulingana na ushahidi na mazingira haya, nimeridhika na ninaona washtakiwa hawa kwa makusudi na bila uhalali walimuua marehemu”

“Pengine walimfyatulia risasi na kumuua marehemu ili kuondokana na jambazi maarufu (kama walivyoshuku). Hii kwa maoni yangu ilikuwa ni kuua kwa nia mbaya,”alisema Jaji na kuwahukumu adhabu ya kifo polisi hao wawili.

Washtakiwa walivyokata rufaa

Washtakiwa hao wawili hawakuridhika na hukumu hiyo na kukata rufaa Mahakama ya Rufani huku mrufani wa kwanza, Juma Mswa akitetewa na wakili Ignas Itemba huku mrufani wa pili, Mataba Matiku alitetewa na wakili Godwin Sandi, wote wa Moshi.

Katika hoja ya kwanza, mtufani Mswa alilalamika kuwa Jaji aliyemuhukumu adhabu ya kifo alikosea kisheria kwa kutojibu swali kuwa wakati anatoka kwenye gari alifanya hivyo kutekeleza amri ya kiongozi wa timu ya mapolisi, Sajin Mensah.

Hivyo Profesa Itemba akasema kwa sababu hiyo, kitendo cha mteja wake kushuka na kufyatua risasi tatu kilikuwa halali kwani alitekeleza amri ya kijeshi.

Akijibu hoja hiyo, wakili mwandamizi wa Serikali, Ama-Isario Munisi, alisema mshtakiwa wa kwanza aliwaamuru washtakiwa wengine watoke kwenye gari na kufyatua risasi hewani, hakuagiza wamfyatulie risasi na kumuua Kombe.

Majaji waliosikiliza rufaa hiyo katika kushughulikia hoja hiyo, walinukuu ushahidi wa mshtakiwa anayetajwa kutoa amri, Mensah aliyesema “Kama mshukiwa anatoroka, hutumii silaha ya moto labda kama naye ana silaha ya moto.

“Ni lazima utafute mbinu nyingine ya kumkamata. Unapomfyatulia risasi unaweza kumuua. Unaweza kufyatua risasi hewani kumuonya.

Huwezi kumpiga mguu kwa risasi kama hana silaha. Unatumia nguvu nyingine kumdhibiti.

“Kwa kuwa walimuona akitoka kwenye gari akiwa hana silaha, haikuwa busara kumshambulia marehemu kwa risasi.

Sio sahihi kusema walitumia nguvu ya wastani ili kumkamata kwa kuwa walimuua mtu asiye na silaha.

Katika ushahidi wake huo, Mensah aliongeza kusema “Baada ya gari (la marehemu Kombe) kusimama, ingekuwa ni rahisi kwa washtakiwa (Mswa na Matiku) kumfukuza marehemu na kumkamata kirahisi kabisa.

Majaji hao walisema kumfukuza na kumkamata marehemu kungekuwa rahisi zaidi kwa sababu tayari alikuwa amejeruhiwa kwa risasi na ndio maana alionekana akikimbia huku akiyumba, hivyo wakaamua kuitupa hoja hiyo.

Katika hoja ya pili ambayo iliibuliwa pia na mrufani wa pili,Mataba Matiku na mrufani wa kwanza, Juma Mswa ilieleza kuwa Mahakama ilikosea iliposema wakati marehemu anatoka ndani ya gari, warufani walifahamu hakuwa na silaha.

Majaji walisema warufani wanakiri kuwa marehemu hakutoa kitisho chochote kwao, kwa hiyo wanakubaliana na Jaji aliyewahukumu kuwa walifahamu au walitakiwa wafahamu kulingana na mazingira, kuwa marehemu hakuwa na silaha.

Katika hoja ya tatu, mrufani Mswa alilalamika kuwa Mahakama ilikosea kumtia hatiani kama msaidizi wa mrufani wa pili katika kufanya mauaji hayo, wakati kulikuwa hakuna ushahidi wowote kuwa wawili hao walikuwa na dhamira moja.

Majaji walikubaliana na hoja hiyo na kusema Jaji aliyewahukumu alikosea kumuhukumu mrufani wa kwanza kama msaidizi wa mauaji wakati tayari alishawaona kuwa kwa makusudi na bila uhalali walisababisha kifo cha Kombe.

Walisema kuna ushahidi uliopokelewa kuwa warufani wote wawili walimfyatulia risasi marehemu na daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu hakuweza kutofautisha ni silaha ipi ilisababisha majeraha yale tisa ya risasi aliyoyabaini.

“Kulikuwa hakuna nafasi kwa mazingira yale kumchukulia mmoja kama ni mhalifu msaidizi na mwingine ndiye muuaji mkuu , kwani hata mwisho wa kesi Jaji aliwatia hatiani wote wawili kwa nia yao ovu ya kumuua marehemu,”walisema majaji.

Kesho tutawaletea simulizi ya hoja za rufaa ya Konstebo Mataba Matiku na namna majaji waliosikiliza rufaa walivyozipima hoja zake hizo.

Usikose sehemu inayofuata ya simulizi hii kesho
 
  • Thanks
Reactions: I M
Ni mauaji yaliyogubikwa na simulizi na hisia tofauti juu ya nini hasa kiini cha mauaji ya mkurugenzi mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe aliyeuawa kwa kupigwa risasi Juni 30 mwaka 1996.

Kumekuwepo na nadharia ya ulaji njama (conspiracy theory) kwamba pengine kuna mkono wa mtu katika mauaji hayo yaliyotokea katika Kijiji cha Mailisita Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na nyingine ni kwamba kweli aliuawa na polisi.

Katika mfululizo wa makala hii, Mwandishi Wetu atakuletea simulizi ya nini hasa kilisababisha mauaji yake, nani walimfyatulia risasi zaidi ya 15, maelezo ya maungamo ya wauaji wake yanasemaje na familia ililipwa fidia ya Shilingi ngapi.

Simulizi hii inaegemea ushahidi uliotolewa mahakamani katika kesi hii na kesi ya madai ya fidia iliyokuwa imefunguliwa na mkewe, Roseleene Kombe dhidi Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na simulizi zilizogubika mauaji hayo.

Maneno yalisemwa mengi, mojawapo ni hisia kuwa huenda aliuawa kwa sababu ya urafiki wake wa karibu na Agustino Lyatonga Mrema, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi 1995, lakini kwa kesi ilivyokuwa mahakamani haikuwa sahihi.

Kwa kuwa Kombe alikuwa amepigwa risasi na polisi, licha ya kuripotiwa kuinua mikono yake juu kama ishara ya kujisalimisha kwa watu walioamini ni wezi wa gari, kulikuwa na uvumi kwamba mauaji yake yalikuwa yamepangwa.

Ni kutokana na hisia hizo na moto wa kisiasa juu ya mauaji hayo, Rais wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Mkapa aliamua kuunda tume ambayo iliwasilisha ripoti yake 1997 ambayo si wazi, ikisema Serikali haikuwa na mkono katika mauaji hayo.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva aliyekuwa na Jaji Mussa Kipenka wakati huo akiwa mwanasheria mwandamizi wa Serikali, ilihoji mashahidi 52 na mwaka 1997 ilitoa ripoti kwa Mkapa iliyohitimisha kwamba Serikali haikuwa na mkono wowote katika kifo cha Kombe.

Hadi sasa taarifa ya tume hiyo, kama zilivyo baadhi ya tume zilizoundwa kutafuta ukweli wa jambo ambalo linaibua hisia kali, imekuwa ni siri.

Mwaka 1998, Mbunge wa Temeke Jijini Dar es Salaam, Augustino Mrema aliibua hoja bungeni kuwa kifo cha Kombe kilikuwa sehemu ya mpango wa mauaji uliofanywa na Serikali, ingawa hata hivyo alishindwa kuthibitisha madai hayo. Pamoja na taarifa hiyo ya tume na ushahidi uliotolewa mahakamani kuhusiana na mauaji ya Kombe, bado baadhi ya watu hadi sasa wana hisia tofauti juu ya mauaji hayo na katika makala hii tutakuletea mwanzo mwisho nini kilitokea.

Timu ya makachero ilivyoundwa

Usiku wa Juni 30, 1996 na siku iliyofuata, kulizagaa taarifa za kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa Luteni Jenerali Kombe, aliyewahi kuwa mkurugenzi wa tano wa TISS na taarifa hizo hazikuzagaa kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyo sasa.

Wakati huo wala simu za kiganjani (kitochi) zilikuwa hazijawa nyingi, licha ya kwamba zilianza kuingia nchini mwaka 1994, hivyo taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu na katika mji wa Moshi, watu walikaa katika makundi wakijadili.

Taarifa hizo zilisema polisi walimuua Kombe kwa kummiminia risasi hata baada ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kujisalimisha, na maiti yake ilipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mawenzi.

Polisi wakati huo walikuwa wanaamini wamemuua mtu waliyekuwa wanaamini ni mwizi mashuhuri wa magari na walikuwa wakitamba kufanikiwa kukamata gari Nissan Patrol namba TZG 50 mali ya D.W Ladwa lililoibwa Jijini Dar es Salaam.

Ni hadi mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa wa Kilimanjaro alipopokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Iwisi Shoo, akimwambia gari walilolikamata si lenyewe na mtu waliyemuua si mwizi, bali ni Kombe, mkuu wa zamani wa TISS.

Hapo ndipo Polisi wenyewe walijikuta wakipata ganzi baada ya kugundua waliyemuua ni Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye alitumikia cheo cha mkurugenzi wa TISS kati ya mwaka 1983 na 1995.

Hapo ndipo mwili wake sasa ukahamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC ili kuhifadhiwa ukisubiri taratibu nyingine za kisheria na mazishi.

Lakini ilikuja kubainika kuwa gari la marehemu namba TZD 8592 aina ya Nissan Patrol lilikuwa likifanana na la Ladwa na siku kadhaa nyuma, polisi Jijini Dar es Salaam, walikuwa wamelikamata na kuliachia baada ya kuridhika silo.

Ingawa Kombe na familia yake ni wenyeji wa Kilimanjaro, wana nyumba jijini Dar es Salaam.

Wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa fiche zilizowaambia kuwa mwizi aliyeiba gari hilo alikuwa amelipeleka mkoani Kilimanjaro, hivyo ofisi ya RCO Dar es Salaam ikawatuma Polisi wawili kwenda Kilimanjaro.

Makachero hao kwa mujibu wa hukumu ya rufaa namba 8 ya 1998 iliyotolewa na majaji watatu wa mahakama ya Rufani iliyoketi Jijini Arusha na kutoa hukumu yake Machi 16,1992, ni Sajini Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa.

Hukumu hiyo ilitolewa na majaji Lameck Mfalila, Barnabas Samatta na Kahwa Lugakingira kutokana na hukumu ya kifo iliyotolewa Januari 26,1998 na Jaji Buxton Chipeta dhidi ya askari wawili, Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku.

Kulingana na nyaraka za mahakama ya Rufani, Sajin Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa, waliondoka Jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Kilimanjaro wakiwa na gari lingine la Ladwa likiendeshwa na dereva wake aitwaye Ismail Katembo.

Dereva huyo ndio angetumika pia kulitambua gari la Ladwa lililoibwa na wote watatu waliwasili Moshi Juni 27,1996 na kuripoti Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na RCO ambaye aliamua kuwaongezea nguvu.

Hapo wakaongezewa makachero watatu, koplo Elisante Tarimo aliyekuwa mshtakiwa wa pili, Koplo Chediel Elinisafi aliyekuja kuwa mshtakiwa wa nne na Konstebo Mataba Matiku aliyekuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo.

Makachero hao walipewa bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) namba N.1270 na risasi 30 ambayo ilibebwa na Mataba Matiku wakati Sajenti Thomson Mensah na Koplo Juma Mswa kila mmoja alikuwa na bastola yenye risasi nane.

Koplo Elisante Tarimo na Chediel Elinisafi wao hawakuwa na silaha yoyote.

Kwa hiyo timu hiyo ya makachero ikaanza msako wa kulitafuta gari mali ya DW Ladwa aina ya Nissan Patrol lenye namba TZG 50 ambalo lilikuwa likifanana na gari la Luteni Jeneral Kombe TZD 8592 lililokamatwa Jijini Dar es Salaam na kuachiwa.

Siku hiyo ya Juni 30, 1996 kwenye saa 10 alasiri wakiwa katika misheni ya kulisaka gari hilo la Ladwa, wakiwa eneo la kijiji cha Shiri Njoro barabara ya Moshi-Arusha wakati huo wakiwlekea barabara hiyo kuu, mbele waliona gari la Kombe.

Dereva Ismail Katembo ambaye sasa ni marehemu alitoa sauti ya mshangao akisema gari lililopo mbele yao likitokea barabara ya Arusha-Moshi ndio gari ambalo wanalitafuta, hivyo akaliwashia taa lisimame, lakini dereva hakusimama.

Polisi hao waligeuza gari lao na kuanza kulifukuza gari la Kombe ambalo lilikuwa likifanana kwa rangi na lile na DW Ladwa lililokuwa likitafutwa na wakati wakilifukuza walianza kulishambulia kwa risasi kumlazimisha asimame.

Imran Kombe ni nani

Luteni Jenerali wa JWTZ Imran Kombe, alikuwa mwanajeshi na kachero wa usalama wa Taifa ambapo katika vita Uganda na Tanzania mwaka 1979, aliongoza brigedi ya 201 wakati Tanzania ilipoivamia Uganda kumtoa Nduli Idd Amin.

Mwaka 1980, ndio alipata wadhifa wa Mnadhimu mkuu wa JWTZ na kwa mujibu wa taarifa za mitandao zinaonyesha Desemba 30, mwaka huo, alipandishwa cheo na kuwa meja jenerali na mwaka uliofuata aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda Hungary.

Mwaka 1983, Kombe aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni Jenerali na kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Uslama wa Taifa (TISS), nafasi aliyoitumikia hadi 1995 na kustaafu. Aliuawa kwa kushambuliwa kwa risasi Juni 30,1996.

Baada ya mauaji hayo, Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni askari watano na raia mmoja, Ismail Katembo ambaye hata hivyo alifariki dunia akiwa gerezani hata kabla ya kesi yao ya mauaji ya kukusudia haijasikilizwa na kutolewa hukumu.

Source: Mwananchi

Fuatilia hapa Sehemu Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Sehemua Ya Pili)
Haya mauaji watu waliusisha na siasa wakati huo Mrema alikuwa moto na huyu IMRAN KOMBE alikuwa karibu na mrema
 
Back
Top Bottom