SURA YA 21
Upande wa huku hospitalini yule baba aiekuja na kijana huyu hospitalini , alikuwa katika hali ya wasiwasi sana na hii ni baada ya kumtafuta Hassani kila kona pasipo kumuona , alijikuta akichanganyikiwa na kuogopa kwa wakati mmoja , alihofia Hassani asije akafanya kitendo hatarishi , kwani alikuwa kwenye majonzi.
Mwanadada Lisa alionekana ni mwenye kuguswa sana na tukio lile . hali ile ilimfanya kukosa amani na kujikuta akiomba wenzake ruhusa kwamba anarudi nyumbani walikokuwa wamepanga , kwani walikuwa ndani ya hospitali hii ya Bombo kwa ajili ya mafunzo ya vitendo .
Baada ya kurudi nyumbani alijikuta akikosa raha kabisa , ni kama mtu ambaye alikuwa akikukumbuka matukio ya nyuma ambayo yalimkosesha Amani , baada ya kuona mawazo bado yanamwandama , alitoka ndani na kisha alisogea upande wa barabarani na kuita bodaboda iliompeleka mpaka mtaa wa Raskazoni sehemu ambayo alikuwa akipendelea sana kukaa pindi anapokuwa na mawazo .
Baada ya kushushwa alijikuta akitembea taratibu sana kutafuta sehemu ya kukaa na ile anageuza upande wa kulia alijikuta akimuona yule kijana aliekuwa hospiutalini akilia , Lisa alijikuta akisogelea na kukaa kwenye kile kimbweta alichokuwa amekaa huyu kijana.
“Pole sana”Ni sauti iliosikika kwa mara ya pili kwenye masikio ya kijana Hassani na kujikuta akigeuza macho yake na kumwangalia mtu anaempa pole , maana hakuwa akijua kuwa pembeni yake kulikuwa na mtu aliekuwa amekaa .
Kijana huyu ambae alionekana kuwa na maisha Duni kutokana na maazi yake aliokuwa amevaa , alijikuta akimwangalia mwanadada huyu mwenye uzuri wa ajabu .
Lakini Lissa ni kama alikuwa amefungulia kilio kwa wakati mwingine kwa kijana huyu , kwani alianza kulia tena kwa kwikwi akionyesha alikuwa kwenye machungu makubwa sana.
“Nimemuua baba , sistahili kuonewa huruma”Aliongea kijana huyu jambo ambalo lilimfanya mwanadada huyu kushangaa ni kwanini kijana huyu anatamka neno kama hilo .
“Sio kweli hupaswi kujilaumu , kila kitu hutokea kwasababu ni mipango ya Mungu”Aliongea mwanadada Lisa huku akionekana kumuonea huruma kijana huyu .
“Kifo cha baba nimekisababisha mimi , na wala sio mpango wa Mungu”
“Sio kweli ni mipango ya Mungu usiseme hivyo”
“Kama Mungu amenionyesha hili jambo kabla ya kutokea , huu sio mpango wa Mungu hata kidogo , mimi ndio wa kupaswa kulaumiwa”Aliongea na kisha alinyanyuka na kuondoka .
Hakika maneno haya yalimchanganya sana mwanadada huyu Lisa , hakuelewa ni kwanini kijana huyu anaongea maneno hayo , alitamani sana kujua ni kwasababu ipi kijana huyu alikuwa akisema amemuua baba yake ,jambo ambalo ni mara chache sana kulisikia ,na hata kama ni kweli kwannini kijana huyo alikuwa akili ilihali alimuua baba yake , na hata kama ilikuwa ni nahati mbaya je ilikuwaje , hayo yote yalikuwa ni maswali aliojiuliza Lisa huku akiendelea kuangalia maji ya bahari .
*****
Naam Ndani ya kijiji cha Nkumba wilayani Muheza ndani ya nyumba moja ndogo sana iliokuwa imeezekwa kwa nyasi tofauti na nyumba zote zilizokuwepo ndani ya kijiji hiki , walionekana baadhi ya wanakijiji waliokuwa na hali ya simanzi kwenye nyuso zao , na hii ni mara baada ya kupokea mwili wa Mzee Nyangwe aliekuwa amefariki ndani ya hospitali ya Bombo Tanga .
Licha ya mazingira kuwa finyu ndani ya eneo hilo , lakini watu walionekana kujaa kwelikweli,huku kijana Hassani aliekuwa amejibanza pembeni ya nyumba yao alionekana ni mwenye huzuni kweli , mrafiki zake kutoka shule ya sekondari Nkumba walikuwa wakimpa pole lakini badi hawakuweza kutoa hali ya huzuni aliokuwa nayo kijana huyu .
Baada ya kama masaa manne kupita ndipo mwili wa marehemu ulitolewa nje na Shekhe alianza kuswali dua kwa ajili ya kuombea mwili huo , kitendo ambacho kilifanyika kwa lisaa na baada ya hapo safari ya kuupeleka kwenye nyumba yake ya milele ilianza , vijana walipokezana kubeba mwili huo kwa kujipanga njiani kuelekea lilipo shamba la Mzee Nyangwe sehemu ambayo ndio kaburi lake lilikuwa limechimbwa.
Ni ndani ya masaa kadhaa baada ya kuupeleka mwili wa mzee Nyangwe katika nyumba yake ya ,milele , muda wa saa sita kamili ndani ya nyumba hii ya mzee Nyangwe kulionekana kumepoa kutokana na kwamba maziko yalikuwa yamekwisha kufanyika na hakukuwa na lingine la kufanyika hapo nyumbani , kwani familia mzee nyangwe maisha yake ya hapo kijijini yalikuwa ni ya kimasiikini sana , kiasi kwamba hata kwenye huo msiba hakuna chochote kilichokuwa kimepikwa.
Ni karibu watu watano tu ndio waliiokuwa wamebakia hapo nyumbani mmoja akiwani rafiki yake wa karibu wa Hassani na wengine walikuwa ni family ya mzee Kitasa ambae ni yule aliemsindikiza Hassani Hospitalini.
Wakati hayo yakiendelea mara baada ya dakika chache walionekana vijana kadha wakiingia ndani ya eneo hilo huku wakiwa wameongozana na mwanadada Lisa ambae haikueleweka amefikaje ndani ya kijiji hicho , , watu wengi wa kijiji hicho walimshangaa sana mwanadada huyo , hasa pale alipoeleza kwamba amekuja kwenye msiba wa Mzee Nyangwe Jambo ambalo liliwashangaza wanakijiji hawa , kwani walikuwa wakimjua mzee ?nyangwe hakuwa na ndugu mjini na juu ya yote ni mwanadada huyu kuja akiwa na gari la kifahari . .
Hassani alijikuta akishangaa sana ujio wa mwanadada huyu , kwani katika kumbukumbu zake ni kwamba mara walipoonana kule Raskazoni hawakuongea chochote Zaidi ya Hassani kunyanyuka na kuondoka .
“Pole sana”
Ni neon ambalo kwa mara ya tatu mwanadada huyu analitamka akimwambia Hassani.
“Asante”Aliongea Hassani huku akimwangalia kwa Mshangao wanadada huyu .
“Karibu sana Dokta kiti”Aliongea Mzee Kitasa kwani alikuwa akimkumbuka mwanadada huyu kama moja ya madaktari waliokuwa wamemfanyia mzee Nyangwe upasuaji jambo ambalo lilimshangaza kidogo Hassani.
Lisa alieleza kwamba amekuja kwa ajili ya msiba , lakini pia alieleza kuwa alikuwa amegunswa na maneno ambayo kijana Hassani alikuwa akiyatamka , alitaka kujua ni kwanini kijana huyo alikuwa akisema kwamba yeye ndie aliemuaa baba yake
Na hapo ndipo alipoweza kusimuliwa kisa ambacho kilimsisimua na kumsahangaza sana mwanadada huyu .
*****
Kwa majina yangu halisi naitwa Hassani Hamisi Nyangwe nimezaliwa hapa hapa kijijini kwetu na kukulia hapa hapa , mpaka kufikia umri huu wa miaka kumi na sita nikiishi na baba yangu Nyangwe , kwani mama yangu alifariki punde tu baada ya kunileta duniani.
Maisha yetu kwa ujumla sio mazuri sana na naweza kusema kwamba kwa hapa kijijini ni familia yetu pekee ambayo ilikuwa ni ya umasikini uliokithiri , lakini licha ya hivyo sikuwahi hata mara moja kujilaumu kuzaliwa katika aina hii ya familia , kwani nilichokuwa nikiamini katika maisha yangu ni kwamba Mungu ndio mpaji wa yote.
Licha ya umasikini wetu nilikuwa nikimpenda sana baba yangu mzee Nyangwe na hata yeye ia alikuwa akinipenda sana , naweza kusema kwamba tokea nifikie umri wa kujielewa Mzee Nyangwe kwangu ndio baba ndio mama kwangu na kwangu nilimchukulia kama zawaidi ambayo Mungu amenipa
Maisha yetu hapa kijijini kwa ujumla wake licha ya kuwa masikini , yalikuwa ni ya furaha sana , kwani mimi na baba tuliishi maisha kama washikaji , na tulikuwa tumezoeana sana kiasi kwamba hata baadhi ya wanakijiji walikuwa wakishangaa namna ambavyo nilikuwa nimemzoea mzee .
Lakini licha ya furaha niliokuwa nayo katika maisha yangu , kuna jambo moja tu ambalo lilikuwa likinisumbua sana katika maisha yangu na hili ni jambo ambalo nilizaliwa nalo , sikuwahi kujua uwezo huu ambao nilizaliwa nao ulikuwa ukimaanisha nini katika maisha yangu na siku niliokuja kuanza kujua nina uwezo huu ni kipindi nikiwana miaka kumi.
Ilikuwa ni siku ya ijumaa jioni baada ya kumaliza kujisomea kwani kipindi hicho nilikuwa darasa la pili, kama ilivyokuwa kawaida baada ya kusoma nilipanda kitandani na kuutafuta usingizi , kitanda ambacho nilikuwa nikilala na baba , kwani nyumba yetu ilikuw ani ya vyumba viwili tu yaani jiko na sehemu ya kupikia .
Basi wakati nikiwa kwenye usingizi ilinijia ndoto nikiwa naenda shule asubuhi siku ya jumatatu , siku ambayo kwenye ndoto niliona ni siku ambayo ilikuwa na mvua, na hata mwendo ambao nilikuwa nikitembea ni wa kukimbia ili kuepuka kuloanisha nguo na madaftari , basi wakati nafika shule ya sekondari Nkumba , shule ambayo ilikuwa imepaka na shule ya msingi Nkumba , nilijikuta nikiteleza na kutumbukia kwenye mtaro ambao ulikuwa ndio kama mpaka kati ya shule ya sekondari na ya msingi Nkumba , na kutokana na kwamba siku hio mvua ilikuwa imenyesha sana na ule mtalo ulikuwa umejaa maji machafu , yalinichafua mwili mzima na kufanya wanafunzi wenzangu ambao walikuwa wamesimama kwenye korido za madarasa kunicheka .
Kabla ya ndoto kuisha nilijikuta nikiamshwa na baba .
“Wewe hassani Amka kumekucha tujiandae twende shambani”
Basi niliamka baada ya baba kuniamsha na niliwasha moto na kuchemsha mihogo ambayo kwa kipindi hicho ndio kilikuwa chakula chetu kikubwa , kwani ni zadi ya miezi tisa mvua hazijawahi kunyesha na hata msimu wa kulima mahindi ulikuwa unakaribia kupita , lakini mvua bado haikuwa hata na dalili.
Basi hatimae tulienda shambani na kulima na kurudi nyumbani muda wa jioni huku tukiwa tumechoka sana .
“Hivi Hassani mvua isponyesha sijui maisha yatakuwaje miezi ijayo , maana sio kwa hili jua”Aliongea mzee huku akirusha Jembe chini .
“Nimeota mvua itanyesha Jumatatu”
“Hio ni ndoto tu , sidhani kama itanyesha” Aliongea baba na mimi nikacheka na kupotezea na hata siku hio ilipita na siku pia ya jumapili ilipita na siku ya jumatatu ikafika , siku ambayo nilichelewa sana kuamka kiasi kwamba baba ndie alieniamsha .
“Wewe Hassani amka mvua imepungua uwahi shuleni utachelewa”Aliongea baba ambae alinifanya nikurupuke na kuanza kujiandaa kuelekea shuleni , huku nikiwa nimechelewa kweli halafu wiki hio iliokuwa inaanza ilikuwa ni zamu ya mwalimu Bony , mwalimu ambae alikuwa akiogopeka sana kwa kuchapa , alikuwa ni mkurya na alikuwa na kajimsemo kake akitaka kukuchapa anakwambia “Okoa muda” na hata kwenye meza yake ofisini alikuwa ameandika hilo neno la “Okoa Muda” sasa shuleni ndio tulikuwa tunamuita kwa jina hilo la Mzee wa kuokoa Muda , na siku ukiona mwalimu huyu anakwambia okoa Muda basi jua tu anamaanisha lala ule zako ambapo ukiamka baada ya kichapo wiki nzima utakuwa unakaa kwa maumivu mengi sana darasani na pengine usije kabisa shuleni.
Basi nilijiandaa harakaharaka na kunywa chai isiokuwa na sukari na kisha ninakimbia kuelekea shuleni huku mvua ikiwa inayesha japo sio sana , niliungana na wanafunzi wenzangu na kuendelea na safari , huku nikiwa nimesahau kabisa ndoto niliokuwa nimeota usiku wa kuamkia jumamosi , basi ile nilivyofika katika mtalo nilijikuta nikteleza na kutumbukia mtaloni na kuchafuka mwili mzima , huku wanafunzi wenzangu wakiwa wanazomea na kucheka , hakika ilikuwa ni aibu sana kwangu , nilijiangalia na kujiona sifai kuendelea kubaki hapo shuleni na kugeuza taratibu kurudi nyumbani kwani nisingeweza kuendelea na masomo kwa namna ambavyo nilikuwa nimechafuka na nilikuwa nikitoa harufu.
Sasa wakati narudi ndio nikaanza kukumbuka ile ndoto niliokuwa nimeota , hakika nilishangaa kabisa , kwani kila kitu kilichokuwa kwenye ile ndoto ndio kilichokuwa kimenitokea nilishangaa lakini mwisho wa siku niliipotezea japo pia nilimwambia baba , lakini hata yeye hakuizingatia sana.
Basi siku zilipita na baada ya wiki nilijikuta nikiota ndoto nyingine na hii ilikuwa ni ndoto ambayo nilimuona baba aking`atwa na nyoka , ndoto hii wakati naona ilikuwa ni siku ya jumaanne kuelekea Jumatano na jambo la kushangaza ni kwamba siku hio hio ya Jumatano wakati narudi shuleni nilipokea taarifa kutoka kwa mke wa mzee Kitasa kwamba baba ameng`atwa na nyoka na amepelekwa hospitali ya Teule , taarifa hio ilinishitia mno na kunishangaza kwa wakati mmoja , kwani nilichokuwa nimeota ndio hiko hiko kilichokuwa kimetokea na nilichokuwa nikitaka kuhakikisha ni sehemu ambayo baba alikutwa na janga hilo , na baada ya siku mbili za kutoka hospitali ya Teule ndio nikamwambia baba anionyeshe mahali ambapo alikutwa na mkasa huo wa kung`atwa na nyoka na sehemu alionipeleka ni pale pale ambapo nilipashuhudia ndotoni na hili swala niliamua kumsimulia na baba akaniambia kwamba .
“Hizo ni ndoto tu Hassani hazina maana yoyote “
“Lakini baba hii ni mara ya pili naota kitu kinatokea kweli bahati mbaya haitokeagi mara mbili”
“Basi tufanye hivi kama itatokea umeota mara ya tatu na ikawa kweli nitakupeka kwa mzee Kigo asome nyota yako huenda ukawa Nabii”Aliongea mzee na mimi nikakubaliana nae.
Basi ilipita mwezi namini nilisahau kabisa lile swala na tulikuwa kwenye mfungo wa Ramadhani mwezi wa tano , kipindi ambacho tulikuwa tukielekea kumaliza muhula wa kwanza shuleni ili tufunge shule .
Basi siku moja niliota nyumba ya Mzee Kesi ikiungua na moto huku yeye na familia yake yote wakiwa ndani , na tena ilikuwa ni muda wa usiku kabisa , Mzee kesi alikuwa ni moja ya watu waliokuwa na pesa hapo kijijini , kwani alikuwa akimiliki ‘Chain Saw’(mashine ya kukatia miti na mbao) na kupitia mashine yake hio alikuwa akijipatia pesa nyingi sana kwa kuuza mbao lakini pia kukodisha , mzee huyu alikuwa na familia ya watu saba , mke wake, yeye mwenyewe , Ratifa ambae alikuwa Sekondari Nkumba , Abasi ambaye alikuwa ni mkubwa kabisa ashamaliza shule ila alikuwa akiishi na wazee wake oamoja na wajukuu zake watatu mmoja akiwa ni mtoto wa Abasi aliezaa na mwanamke ambaye alimkimbia na wengine wawili walikuwa ni watoto wa mtoto mkubwa wa mzee Kesi aliekuwa akifahamika kwa jina la Mwantumu ambae alikuwa jijini Dar es salaam.
Basi siku ile kwangu nilikuwa na wasiwasi sana juu ya ile ndoto na mbaya Zaidi sikuwa nyumbani Nkumba siku hii , kwani tulikuwa tumeenda Magila kupasua mawe mimi na baba na Mzee Kitasa , wakati tupo njiani nilimweleza mzee huyu juu ya ndoto hio lakini hakuwa ni mtu wa kuzingatia namimi nikapotezea .
Nakumbuka siku hii tuliweza kurudi muda wa saa moja kasoro hivi na wakati tunafika Nkumba bahati nzuri niliweza kukutana na Ratifa ambae alikuwa amebeba ndoo ya maji akiwa ametangulizana na mtoto wa Abasi aliekuwa akifahamika kwa jina la Adam aliekuwa anasoma Chekechea akiwa na yeye amebeba maji kwenye kigaloni cha lita tatu .
“Dada Rat nimeota ndoto nyumba yenu inaungua”
“Wewe mtoto hebu acha kutuwangia bhna” Aliongea Ratifa kwa dharau na mimi sikumjali sana nikasepa zangu kwani kipindi hiki nilikuwa mtoto na hata ningemwambia mtu asingeniamini. .
Basi nilikuja kuamshwa na vilio vya watu muda huo ilikuwa ni saa Sita za usiku na hata nilipoangalia pembeni baba sikumuona , nilijikuta nikitoka nje na ile natoka tu niliona wingu la moshi likiwa limetanda uelekeo wa nyumba ya Mzee kesi , lakini ile nashangaa sauti za vilio huku nikisia wamam wanaongea kwa sauti ‘Nyumba ya mzee kesi jamani inaungua na wenyewe wapo ndani”
Kusikia hivyo tu nilijikuta nikipatwa kama mshituko wa moyo huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi sana , nilitoka na kuelekea upande huo , sehemu ambayo ulikuwa ukivuka nyumba nne tu unakuwa umefika na ile nafika ni kama vile nipo ndotoni , kwani vile vile moto ulivyokuwa unawaka ndio nilicyo ota , huku watu wakihangaika kuokoa watu waliondani , na maji kumwagwa , lakini ni kama moto ulikuwa ukizidi .
“Bahati nzuri ni kwamba wazee wa kijiji walifanikiwa kutoboa tundu na kuanza kuitia jina la Mzee Kesi wakimwambia atoke lakini tulichoweza kusikia ni neno moja tu kwa mzee Kesi , kwamba hawezi kutoka ilihali familia yake yote imeshateketea kwa moto , wanakijiji walijaribu kumbembeleza mzee Kesi atoke , lakini halikusaidia kwani hakutoka.
Mpaka inafika saa tisa za usiku moto ulikuwa umezima , lakini vilio vilikuwa vya aina yake , sio watoto sio wazee watu walishindwa kujizuia ,kila aliekuwa akiangalia miili iliokuwa imetolewa na kupangwa nje ikiwa imeungua vibaya alijikuta akilia sana , Siku hii pia nililia mno , yaani sana huku nikijiona mkosaji sana .
Tukio hili liliniathiri vibaya sana kisaikolojia kiasi kwamba hata usiku nilikuwa nikiogopa kulala kwa kuhofia kuota jambo baya , na ukiachilia kwamba hiki kipindi bado nilikuwa mtoto ,,Baba nae alijaribu kuniweka sawa , lakini bado niliogopa sana kwa wakati mmoja .
Basi baada ya wiki kupita mzee alinichukua na kunipelka kwa mzee kigo kwa ajili ya nyota yangu kuangaliwa
Mzee kigo alikuwa ni mganga aliekuwa akifahamika sana pale kijijini na kuogopeka sana , alikuwa akifichua wachawi wengi lakini pia kutibu watu wengi wenye shida mbali mbali , na wengi walikuwa wakitoka mpaka mikoani kwa ajili ya kuja kupata huduma kwa mzee Kigo.
Basi nilipokelewa na kuanza kufanyiwa tiba pale , akachukua kioo chake flani hivi alikuwa akikipaka unga flani ambao sikuwa nikiujua halafu anakirusha juu kinatua chini huku anaongea maneno anayoyajua yeye halafu anaangalia tena , na anakirusha tena juu na kinatua chini , , alivyomaliza , alikichukua akaitumbukiza kwenye maji yaliokuwa yamejaa kwenye chungu kikubwa na kisha aliweka unga flani hivi kama majivu na kisha akakitoa kile kioo na kukifuta na kisha akanisogelea na kukiweka kwenye uso wangu , yaani mimi nikiangalia nyuma ya kioo na kisha yeye akiangalia mbele ya kioo.
Baada ya dakika mbili alijikuta akishituka sana na kukidondosha kile kioo na kisha akanza kuniangalia kwa umakini huku akiokota kile kioo na wakati huo baba alikuwa anaangalia tu kinachoendelea .
Baada ya kama dakika kumi hivyo alionekana kumaliza kile alichokuwa anakifanya na kisha alinipa kisu na kuniambia nichukue Jogoo ambae tumekuja nae , maana kwa huyu mzee sheria zake kama unataka kusomewa nyota yako , basi unatakiwa kuja na jogoo mweupe na mchanga wa mlangoni , yaani pale kwenye mlango wa kutokea unachimba chini na unachukua mchanga..
“Tayariii ….. Tayariii …. Hassaniii …” aliongea kwa sauti yake ya kutisha pale na tulikuwa tayari kwa kupokea majibu
SURA YA 22
“Kijana umezaliwa na bahati kubwa sana kwenye maisha yako , Mababu wa ukoo wako wamekupatia uwezo wa kutambua mambo yatakayokuja”
“Unamaanisha nini Mzee Kigo?”Aliuliza baba
“Hassani ni Mlinzi mkuu wa kijiji hiki , mababu wa koo zote hapa Nkumba wamemchagua kama mlinzi , ilikuwa kosa kubwa sana kuruhusu familia ya mzee Kise kuungua na moto , ulitakiwa kuwaokoa, maana ni jukumu la mababu wa koo waliokupatia na hivi sasa wamekasirika na wanapaswa kutulizwa” aliongea Mzee Kigo na kumfanya Mzee wangu kushituka na kujawa na wasiwasi , kwangu mimi sikuwa na imani sana na mambo ya kiganga tofauti na Mzee ambae yeye alikuwa ni muuminni mzuri tu.
“Kwa hio tunafanyaje mzee Kigo”.
“Kafara ya Mbuzi kwa kila koo inatakiwa kufanyika kwa ajili ya kuwatuliza mababu wa koo”.
Basi kama alivyolekeza tuliweza kutoa kafara ya Mbuzi ambayo tunachinja huko juu milimani kabisa kwenye pango moja , pembeni kabisa na kilipo chanzo cha maji ambayo ndio hutumiwa na watu wa kijijini kwetu kwani kulikuwa kumeunganishwa mabomba .
Basi baada ya hapo niliendelea kuota ndoto za kweli tu na katika kuota ndoto hizo , hakuna siku ambayo hata moja niliweza kuzuia ndoto mbaya kutokutokea , yaani nilichoweza mimi ni kuota tu lakini sikuweza kuzuia kile nilichokuwa nikiota kutokutokean kama ni kibaya , licha ya maneno ya Mzee Kigo kwamba ninatakiwa kuzuia.
Basi baada ya miaka kupita , siku ya ijumaa kuelekea jumamosi , mzee wangu muda wa usiku aliweza kuniambia kuwa siku ya kesho wanaelekea Muheza mjini kwa ajili ya kuuza vitunguu na Mzee Kitasa, huku akiniachia kazi ya kwenda kumwagilia pilipili asubuhi na mimi nilikubali na kisha tukala tukalala , basi usiku niliweza kuota ndoto mzee anagongwa na pikipiki Muheza mjini.,ndoto ambayo nilivyokuja kushituka ilikuwa ni saa kumi na moja kama na nusu hivi asubuhi na nilipoangalia pembeni sikumuona mzee ,nilijikuta nikikurupuka na kutoka nje kumwangalia kama mzee yupo lakini sikumuona , nilichokifanya ni kutulia na kusubiria , kwani mzee aliniambia ni asubuhi na huwaga hana ile tabia ya kuondoka pasipo kuniamsha , nilirudi ndani na kusubiri mpaka saa moja na robo ndipo hofu ilipo nijaa na kujua lazima mzee atakuwa amekwisha kwenda Muheza , niliinuka mbio na kwenda nyumbani kwa Mzee kitasa na nilimkuta mke wake akiwa nje anafagia nilimsalimia na kisha kumuuliza kama mzee alikuwa ashaenda mjini na jibu lake ndio liliniacha hoi kwani aliniambia kuwa walikwisha kwenda toka saa kumi na moja .
Nilijihisi kuchangayikiwa na hilo hata kwa mama Jabu aliliona hilo .
“kwani kuna nini Hassani?”
“Baba atakufa , nimeota anakufa” Niliongea na mama Jabu alijikuta akishituka mno kwani pia hata yeye alikuwa akijua uwezo wangu huo wa kuota vitu vinatokea .
“jamani jamani sasa tunafanyaje ?”
“naenda ,mjini mama Jabu niazime hela kidogo”
Basi mama Jabu alinipatia elfu moja na miatano ya nauli na kisha nikapanda bodaboda kuwahi mjini kumuokoa baba , safari ambayo kama ningejua nisingeenda , kwani ile nafika uwanja wa jitegemee , sijui ilikuwaje , kuna mtoto alikuwa barabarani na sisi tukawa tupo kwenye spidi kali halafu mbele yetu kulikuwa na gari ya Tanesko inakuja , sasa katika harakari za kumkwepa mtoto yule bodaboda alijikuta akichukua uelekeo wa kwenda hopitali ya Teule na hapo ndipo nipokuja kushitukia baba yupo mbele yetu na pikipiki ilikuwa kwenye spidi kali ,na kilichotokea ni kwamba baba tulimgonga na kumrusha upande mwingine na akaenda kuvaa chuma cha mashine ya kupasulia mbao upande wa kushoto na kujigonga kisha akatumbukia mtaloni huku damu zikiwa zimetapakaa .
****
“Pole sana Hassani , sasa hukujiona kwenye hio ndoto ukiwa kwenye pikipiki?”
“Hapana sikujiona nilchoota ni baba kugongwa na pikipiki tu ila sikujua pikipiki hio ndio itakuwa nitakayopanda” Alijibu Hassani huku mwanadada Lisa akiguswa mno na simulizi hio , licha ya kushangaa uwezo aliokuwa nao Hassani wa kuota mambo yanayotokea kweli , lakini swala la ajali ya baba yake kusababishwa na yeye mwenyewe katika harakati za kumuokoa lilimgusa mno , na aliona ni kweli kijana huyu alikuwa na haki ya kutamka yale maneno ya kwamba amemuua baba yake .
“Mimi naamini kuna kitu cha ziada juu yako , labda hujakitambua bado”
“:Sidhani kama kuna kitu kama hicho ,, hii ni laana kwangu , haiwezekani niote vitu ambavyo ni vya kweli ila nishindwe kuzuia matukio mabaya ninayoota”
“Ushawahi kutoa tukio lolote ambalo sio la kutisha ?”
“Sijawahi kuota “
“Basi kunasababu ya kuwa hivyo Hassani , naamini ni uwezo ambao Mungu kakupatia akiwa na sababu zake”
“Siamini hivyo Sister”
Basi mwandda huyu alitoa rambirambi yake na kisha kuaga huku akiahidi kurudi Nkumba akiwa na jibu juu ya uwezo wa Hassani.
Je simulizi hii inauhusiano gani na Book of all names tuendelea tulipoishia
*****
MIEZI MIWILI BAADA YA MAANDALIZI. ,SIKU MOJA KABLA YA SIKU AMBROSE AKISIMULIWA SIMULIZI YA BOOK OF ALL NAMES
WACO –TEXAS
Ni ndani ya shamba moja kubwa lililokuwa likimilikuwa na bwana mmoja aliekuwa akifahamika kwa jina la Hudson , shamba hili lilionekana kujaa mahindi mengi ambayo yalikuwa akikaribia kuvunwa , kwani yalikuwa kwenye hatua za mwisho , ilikuwa ni muda wa mchana , muda ambao bwana Hudsoni akiwa kwenye banda lake kubwa la Ng`ombe alipokea wageni , mmoja akiwa ni mwanamke rangi ya kiafrika mrembo alievalia suruali ya jeans na tisheti ya Puma , na mwingine alikuwa ni mwanaume pia akiwa ni rangi ya kiafrika alievalia jeans na tisheti nyeupe huku akiwa na koti la suti rangi ya ugoro . .
Mabwana hawa walijitambulisha mmoja akiitwa Linda na huyu mwanaume alijitambulisha kama Zakayo , ujio wa watu hawa ndani ya nyumba ya bwana Hudsoni ilikuwa ni kwa ajili ya kukodi Ghala lake moja la kuhifadhia mahindi kwa muda wa wiki moja , jambo ambalo lilimshangaza bwana Hudson kwa watu hao kuomba Ghala lake ambalo ni mwezi uliopita tu alitoka kulisafisha kwa ajili ya kuweka mahindi mapya na kutoa yale ya zamani .
“Mnahitaji ghala langu kwa madhumbuni yapi?”
“Hilo hatuwezi kuliweka wazi Mr Hudson ila tatalipa pesa nyingi sana Zaidi ya mara mbili ya bei utakayotutajia kukodi eneo hilo kwa wiki moja”
Mzee Hudsoni mwenye umri wa miaka 61 alijikuta akishawishika kwa utayari wa watu hawa kutaka kumlipa mara mbili ya pesa ambayo atawatajia , lakini licha ya kushawishika huko hakuwa tayari kutoa Ghala lake , kwani alikuwa na wasiwasi wa kile watu hao watakifanya pale tu atakapo toa hilo Ghala lake ,na maamuzi alioyafanya ni kutaja bei kubwa Zaidi kuliko s thamani ya Ghala lake na hapo watu wale yaani Zakayo na Linda walitabasamu na kuzidisha mara tatu ya hela aliotaja mzee huyu na kisha wakamwambia watampatiakiasi hicho , jambo ambalo liliibua mshangao na matamanio ya kiasi hicho cha pesa kwa mzee Hudson na moja kwa moja alikubali na kuwapeleka watu hawa kwenye Ghala kwa ajili ya kuangalia lakini pia na kuwaachia mlango .
Lakini licha ya hivyo mzee Hudsoni alitaka malipo yake hapo hapo na ilichukua dakika moja tu malipo yaliweza kufanyika na kuingia kwenye akaunti yake ya benki , kitendo ambacho mzee huyu alitoa macho , kwani hakuwahi kuzania kama anaweza kupata kiasi hiko cha pesa kwa muda mfupi na aliona kwa hela hizo zinamtosha kabisa katika uzee wake na hata asipolima tena .
Basi baada ya Linda na Zakayo kukabidhiwa ufunguo wa ghala hili ambalo lilikuwa na umeme , muda wa saa moja kamili iliingia gari nyingine na hii ilikuwa ikiendeshwa na Erick Peter.
“Kazi nzuri sana mmefanya , lakini ninawasiwasi na mzee Hudsoni asije kuta taarifa”.
“Halafu hilo tumeshau ila nitayaweka sawa na mzee huyu na kutokana na pesa tuliompatia nadhani hatafanya jambo kama hilo”Aliongea Zakayo huku wakisaidiana kutoa baadhi ya vitu kama vile tarakishi , mikoba na mazaga mengine na kuyaingiza kwenye hili Ghala , uzuri ni kwamba hili Ghala lilikuwa limejitenga kwa umbali wa mita kadhaa na nyumba aliokuwa akiishhi Mzee Hudsoni na hata kilichokuwa kinaendelea huku hakuwa ni mwenye kuona .
Ndani ya dakika kadhaa tu , ghala hili liligeuka kama ofisi ya kitehama , kwani kulikuwa na tarakishi moja kubwa na baadhi ya vifaa vingine ambavyo sikujua maana yake , lakini pia kulikuwa na meza na viti , lakini pia kulikuwa na kiti kimoja ambacho kilikuwa wazi , lakini kiti hiki pia kikiwa kimeunganishwa na umeme .
Ilikuwa ni muda wa saa nne kamili za jioni gari nyingine aina ya Range iliingia na kwenda kupaki mbele kabisa ya Ghala hilo . na ndani ya dakika kadhaa tu alionekana Janeth akiwa na mzee mmoja wa kizungu ambae alikuwa amezibwa zura yake huku akiwa na pingu kwenye mikono yake iliofungwa kwa nyuma .
Baada ya madakika sekunde kadhaa mzee alikuwa amekarishwa kwenye kile kiti ambacho kilikuwa wazi lakini kilikuwa kimefungwa na kwa kuunganishiwa umeme .
“Bruno lamberk hatimae upo kwenye mikono yangu”Aliongea mwanadada Janeth na kumvua mzee huyu lile kofia walilokuwa wamemvalisha na hapo mzee huyu aliangalia watu waliokuwa mbele yake kwa mshangao huku akichunguza mandhari ya eneo hilo.
“Janeth unachokitaka kukifanya hutofanikiwa , baba yako alijitahidi sana lakini naamini unajua kilichomkuta watu mnaocheza nao ni watu wa hatari sana na huenda wako njiani kuja eneo hili”Aliongea huyu mzee kwa ujasiri amao ulimpandisha hasira sana Janeth , lakini alijizuia na kutabasamu.
“Tutaona kama utakuwa na ujasiri wa kuongea baada ya kuona kinachoendelea ISLAND X” Aliongea janeth na kisha walifunga karatasi nyeupe mbele ya Bruno na kisha walielekeza Projecta kwenye lile karatasi , huku Linda akimpiga gundi ya mdomo mzee huyu .
Wakati huo hayo nayaendelea Erick Upande wa nje alikuwa akirusha Drones ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kuangalia usalama wa eneo hilo .
Baada tu ya kurudi alisogelea tarakishi ile kubwa na kisha alianza kubonyeza batani kwa spidi na ndani ya dakika chache ule upande kulikokuwa na projecta , projecta mbalimbali kulionekana Picha mbalimbali zikionyesha eneo kubwa la kisiwa.
Na ndani ya madakika kadhaa tu , tu picha ilibadilika na kuonesha eneo la nje la Jumba moja kubwa lililokuwa katikati ya Mikoko likiwa limejengwa kwa ustadi mkubwa sana huku mbele kabisa ya jengoo hilo kukiwa na maandishi makubwa yaliosomeka
ISLAND X –U-97 ECLUSIVE HEADQURTER .
Ni kitendo kilichokuwa kikionesha kama Movie kwani ndani ya madakika kadhaa tu , picha zilionekana zikionesha ndani kabisa ya jumba hili , huku watu eneo hili likiwa na makachero waliokuwa wakilinda kuanzia juu ya paa , pembezoni mwa ukuta ,getini na ndani ya eneo hili .
Baada ya madakika kadhaa tu video ile ilionesha eneo la nje ya kisiwa hiki mita kadhaa kutoka kwenye hili jumba , eneo hili lilikuwa ni sehemu ya Ndege kutua yaani kulikuwa na kiwanja kikubwa cha ndege ambacho kwa haraka haraka kilionekana kutosha ndege kubwa ya abiria kutua kwenye hili eneo .
Zilipita dakika chache tu chopa moja ilifika ndani ya hili eneo huku ikiwa na wanajeshi ambao walishuka na Kamba na kuimarisha ulinzi wa hili eneo , hakika ilikuwa ni jambo la kushangaza na ilikuwa ni kama kwenye Muvi .
Yote haya wakati yanaendelea , Janeth ,Linda , Erick pamoja na Zakayo walikuwa wakifatilia kwa ukaribu kabisa , lakini hilo pia kwa upande wa Bruno pia alikuwa akiangalia kile kilichokuwa kinaendelea huku akionekana ni mwenye kuwa na wasiwasi mkubwa.
Baada ya dakika kadhaa za ulinzi kuimarishwa hatimae ndege moja kubwa ya saizi ya kati ilionekana kutua eneo hili na baada ya kama nusu saa hivi , walionekana wanaume na wanawake waliotoka katika hili ndege wakiwa na mavazi yaliokuwa kama yale ya Majaji wanayovaa , na baada ya watu hawa kutoka , walifuatia watu wanne waliovalia nguo nyeusi wakiwa wamebeba kitu kama jeneza , lakini hili halikuwa jeneza ,ni mfano wake tu lakini likiwa la kioo huku watu wale wakiwa wanabeba kwa umakini mkubwa sana .
Baada ya jeneza hilo kushushwa hatimae alionekana , kijana Ambrose alietoka akiwa amevalia Suti akiwa ndani ya hili eneo na wakati haya yote yanafanyika ilikuwa ni mchana kweupe na jambo hili lilidhihirisha kwamba eneo walilokuwepo hao watu ni bara linguine kutokana na utofauti wa muda..
Basi baada ya ya kijana Ambrose kutoka na kuelekea kwenye Gari hatimae alitoka mtu ambae alimfanya Janeth ageuze Macho na kumwangalia Bruno kwa hasira .
Huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwanaume ambae alikuwa anafanana kwa kila kitu na mwanaume aliekuwa amefungwa kwenye kiti alichokuwa amekalia Bruno , jambo hili lilimfanya mzee huyu afurukute kwenye kiti chake , jambo ambalo lilimfanya Janeth kutabasamu.
“huu ndio mwisho wa U-97 kuwa na nguvu duniani , tunakwenda kusambaratisha kila kitu mlichokiandaa karne na karne wewe pamoja na hao mashetani wenzako”Aliongea janeth akimwagnalia Bruno na kumfanya mwanaume huyu azidi kufurukuta kwani hakuwa na uwezo wa kuongea neno lolote kwani alikuwa amefungwa na gundi mdomoni.
“Operesheni Island X inaanza kuanzia sasa na nataka wote muwe makini , kwani hili ndio jambo ambalo tulikuwa tukilisubiria kwa muda mrefu na hakutakiwa kuwa na makossa ya aina yoyote ile” Aliongea kijana huyu kwa kujiamini huku akiendelea kuchezesha cidole vyake kwenye komputa .
Naam nini kilitokea mpaka kufikia hatua hii ???????.....
SURA YA 23
BAADA YA MIEZI MIWILI YA DAMIANI KUINGIA NCHINI MAREKANI , LAKINI PIA KUANZIA SIKU AMBAYO PROFESA MIKE ALAN ANAPOKEA MAAGIZO YA KUMUANDAA AMBROSE
FRORIDA –MAREKANI
Ni siku kadhaa tokea Rania kurudi nchi Australia akitokea Tanzania , sehemu ambayo alienda kwa ajili ya kumtambulisha Erick kwa baba yake , zoezi ambalo halikufanikiwa kutokana na hali ya Peter kupoteza kumbukumbu na kutomkumbuka kabisa Rania .
Siku hii ya Jumatano saa tisa za alasiri ndani ya shule ya North Broward ndani kabisa ya eneo la mgahawa wa shule hii sehemu ambayo wazazi wa watoto mara nyingi hufikia ,wanapokuja kuwatembelea watoto wao walionekana wanaume wawili , mmoja akiwa ni kijana wa makamo alkekuwa amevaa nguo zilizompendezesha na mwingine alikuwa ni mwanaume wa miaka kati ya therathi na tano kwenda juu aliekuwa amevalia suti ya rangi ya zambarau , hawa hawakuwa wengine bali walikuwa ni Erick akiwa pamoja na Joseph...
“Mzee hakikisha akili yako inakuwa na utulivu kama unataka kumuokoa mwanao katika hatari ambayo ipo mbele yake”Aliongea kijana Erick akiwa katika hali ya kirafiki kabisa akimweleza mzee huyu ambae alionekana kuwa katika hali ya wasiwasi mno.
“Nimekuelewa”Aliongea Peter au Joseph akionekana ni mwenye kuvuta pumzi akijiweka sawa , kwani alionekana kutokuwa sawa kabisa.
Baada kama nusu saa hivi ya kukaa pale huku wakiwa wanapata kahawa mara alikuja mwanamama wa kizungu aliekuwa amevalia tisheti yenye nembo ya shule hio.
“Nipo hapa kwa ajili ya kuonana na mwanangu , anafahamika kwa jina la Ambrose Joseph”Aliongea mzee huyu mara baada ya mwanamama kujitambulisha kama Matron.,.
“Okey na huyu mwingine ni nani kwa Ambrose?”
“Huyu ni kaka yake” aliongea mzee huyu na kumfanya Erick kutabasabu .
“Okey ngoja nifanye mawasiliano na uongozi ili mpate utaratibu maalumu wa kuonana nae” Aliongea huyu mzungu kwa Lugha ya kingereza na kisha aliondoka na hazikupita dakika tano alirudi akiwa ameongozana na mwalimu mwingine , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwalimu Nick Jonas , mwalimu aliekuw andani ya shule hio kwa ajili ya kazi maalumu , kazi ya kumfanya Ambrose kupenda mambo ya kale.
Baada ya mwalimu huyu kufika mbele ya meza hii ya mzee Peter alimwamuru yule mama kumuacha sasa aendeelee kuanzia hapo jambo ambalo kidogo lilimshangaza Peter kwani aliekuwa akitarajia kuonana nae hakua huyo kijana bali alikuwa ni mtoto wake Ambrose .
“Naitwa Nick Jonas ni mwalimu na mlezi wa Ambrose “
“Naitwa joseph ni baba wa mtoto Ambrose , nipo hapa kwa ajili ya kuonana na mwanangu”
“Nafurahi sana kuonana na wew Mr Joseph” Aliongea mwalimu Nick huku akiweka tabasamu ambalo kwa Erick aliona taasamu hilo ni la kinafiki huku akiwa amenyoosha mkono kumpatia Joseph.
“Nafurahi pia , lakini sipo hapa kwa ajili ya kuonana na wewe Mr Nick nipo kwa ajili ya kuonana na mwanangu”Jibu hili ni kama lilimfikirisha kidogo Mwalimu Nick na kisha akatabasamu.
“Ambrose hayupo hapa bali yupo katika safari ya kimasomo itakayo chukua muda wa miezi miwili , nipo hapa kw ajili ya kukufahamisha hilo lakini pia kukutoa wasiwasi kuwa mtoto wako yupo kwenye mikono salama”.
Mzee huyu alimwangalia Erick kwanza na kisha Erick alimwangalia Peter na kisha na kumpa ishara ya kukubali.
“Basi sawa mwalimu , nitafika hapa baada ya miezi miwili kwa ajili ya kuonana na Ambrose”..
Basi wawili hawa baada ya kupata jibu hilo kutoka kwa Mwalimu Nick walitoka na kuingia kwenye gari yao huku Joseph akionesha waswasi wa waziwazi .
“Mr Erick kipi kinafuata mpaka hapa naamini mtoto wangu hayupo salama kabisa”
“Punguza wasiwasi mzee , kila kitu kitakuwa katika mpangilio wake kama tu utafata kile ninachokuambia , mwanao yupo kwenye mikono hatarishi na hakuna serikali yoyote duniani itakayokusaidia Zaidi yangu , unachotakiwa ni kufata kile ninachokuambia”
“Kwa hayo nishakubali , ninachotaka ni kujua mpango wako kama unamafanikio yoyote ya kumpata mwanangu”.
Aliongea mzee huyu akiwa ni mwenye wasiwasi , lakini kwa Erick hakuonekana mwenye wasiwasi /tena alichukua simu yake na kisha aliangalia ujumbe ulioingia ambao juu kabisa ya kioo hiko cha simu kuna jina lililokuwa likisomeka
STUPID BOSS.
“UNA MIEZI MIWILI TU KULIJUA SOMO LA SIRI”yalikuwa ni maandishi yaliokuwa yameandikwa kwa maneno ya kodi lakini yalioeleweka kwenye kichwa cha Erick , kwani alijua kuwa yalikuwa yakimaanisha kuwa alikuwa na ana miezi miwili tu iliobaki kukamilisha misheni ya kujua simulizi ya Book of all names
Baada ya Erick kusoma ujumbe huu aliweka simu yake mfukoni na kisha akamgeukia mzee Joseph .
“Sikia mpango uliopo hapa ni kuonana na Ambrose na kumshawishi juu ya hatari iliopo mbele yake, lakini ili niweze kumshawishi nitahitaji msaada wako katika hilo”
Aliongea kijana huyu pasipo wasiwasi huku akitoa simu yake na kupiga jina ambalo limesomeka kwene kioo chake kama Damiani.
“Nataka kwenda kuonana na Ambrose kwani kwasasa haifahamiki sehemu alipo na ili kufanikisha hilo nataka kwenda kama Profesa Mike nataka kutumia
Advanced full body mask technology(A-FBM).
****
Hakuna kitu ambacho kilimpagawisha kijana Ambrose kama pale alipopata taarifa kutoka kwa mwalimu Nick kwamba anakwenda kuambiwa siri juu ya ufunguo ambao utamfanya kuwa na uwezo wa kufanya kila kitu ndani ya ya dunia , hakika hili lilikuwa ni jambo kubwa nyuma ya juhudi zake za kujituma katika kuijua historia ya kale , kwani aliaminni njia moja tu ya kutimiza malengo yake ni kuhakikisha anashikilia ufunguo uliokuwa unafungua kila mlango wa mafanikio ndani ya dunia hii , na ili kutimiza ile ndoto yake ya kuweka kumbukumbu ambayo itakuja kukumbukwa na vizazi na vizazi.
Ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku ambayo kijana /ambrose alikuja kutolewa ndani ya shule hii ya North Broward na maafisa usalama wa UMOJA NAMBA TISINI NA SABA , Ambrose baada ya kuambiwa na mwalimu Nick kwamba watu hao watamfikisha kwa mtu ambae anasiri juu ya ufunguo unaoweza kushikilia kila kitu katika dunia hii hakuwa na wasiwasi Zaidi ya kufatishana na wanasalama hao.
Ni ndani ya dakika chache tu kijana huyu alikuwa ndani ya uwanja wa ndegea wa Frorida International Ariport , sehemu ambayo alipitishwa na wanausalama hawa pasipo hata kufata sheria za hapo uwanjani kwani alikuwa amepitishwa kupitia mlango wa VIP , yaani mlango ambao ulikuwa ukitumiwa na viongozi kupita kama vile maraisi .
Ilikuwa ni ndege moja kubwa ya wastani ya kampuni ya Boeng iliokuwa ndani ya eneo hili la uwanja wa ndege ambayo ilikuwa ni Dhahiri kabisa , kijana Ambrose ndio aliokuwa akitarajia kupanda kuelekea mahali ambapo alikuwa anamamini anakwenda kuonana na mtu ambaye atampatia siri ya namna ya kupata ufunguo utakao fungua kila mlango ndani ya dunia hii.
Naam baada ya madakika kadhaa ndege aliokuwa amepanda kijana Ambrose ilikuja kusimama ndani ya kisiwa kimoja kilichokuwa kinamaandishi yaliokuwa yanasomeka kwa jina la ISLAND Y WORLD TOP SECRET ARCHIVES
Hiki ni kisiwa ambacho hakikueleweka uelekeo wake , japo ni kisiwa ambacho kilikuwa ndani ya nchi ya Marekani , lakini jimbo halikufahamika , na hio yote ilikuwa ni kuhakikisha ulinzi wa eneo hili , kwani pia licha ya kwamba eneo hili halikuwa likifahamika lakini pia kulikuwa na ulinzi wa hali ya juu sana , kwani kulikuwa na makachero wengi waliokuwa wamevalia suti nyeusi wakiwa na siraha.
Baada ya kijana huyu kushuka na kuja kupokelewa na wanaume wawili , na wanawake wawili ambao walijitambulisha kwa kijana huyo kama wafanyakazi wa sehemu hio ambao ilitumiaka kama sehemu ya siri sana duniani kwa ajili ya kutunza kumbukumbu.
Kijana huyu alishangazwa na mandhari ya hili eneo , lilikuwa ni jumba kubwa la kifahari lililokuwa limeunganishwa na maktaba kubwa ambayo ilikuwa na mavitabu na nyaraka mbalimbali za mambo ya kale na sasa.
Kijana huyu alijikuta akistaajabu mno , kwani vitu vingi viliandikwa kwa lugha asiokuwa akiielewa , wakati kijana huyu akiendelea kushangaa mara alitokea mzee mmoja wa kizungu , huyu mzee alionekana kuwa umri umeenda sana , kwani hata tembea yake na ngozi yake vilithibitisha hili.
“Karibu sana Ambrose ndani ya sehemu hii muhimu sana ndani ya dunia hii ,Niite Mr Kolfan the Great Grandfather, mimi ndio muongozaji mkuu wa makataba hii” Aliongea mzee huyu kwa sauti yake iliokuwa imenyongea sana na Ambrose alikubali utambulisho huo.
“Nafurahi sana kukufahamu Mr Kolfan”
“ Karibu sana , lakini pia hongera kwa kuteuliwa katika kuifahamu siri kuu ya ulimwengu”sifa hizi zilimfanya kijana huyu mwili kumsisimka mno na aliamini kitu ambacho anakwenda kukijua muda mfupi ni kitu kikubwa sana katika maisha yake na ni mwanzo wa yeye kuanza kuwa na nguvu duniani.
“Asante sana “ waliongea huku wakiwa wanatembea , huku mzee huyu akiwa anamuonesha mambo mbalimbali yanayopatikana kwenye maktaba hio .
“Kila kitabu na nyaraka unaziziona hapa , ni taarifa za siri sana ambazo ni watu wachache sana wanazifahamu , na wewe katika maandalizi yako ya kuifahamu siri kuu ya ulimwengu huu inakubidi upitie baadhi ya nyaraka , lakini katika miezi yako ya maandalizi unatakiwa kujua sababu kuu ya kuundwa kwa UMOJA NAMBA TISINI NA SABA .
“UMOJA NAMBA TISINI NA SABA ??”
“Ndio unaonekana kushangaa juu ya jina hilo , lakini hilo ndio jina linalotambulisha jumuiya ya siri yanye nguvu duniani, nguvu yao ndani ya jumuia hii inashikiliwa na siri kuu ya ulimwengu , siri ambayo muda si mrefu unakwenda kuijua na kukufanya mtu mwenye nguvu sana ndani ya U-97 na duniani”
Kila neno lililokuwa linatoka kwa Mr Kolfani lilikuwa ni dhahabu kwenye masikio ya kijana huyu , na kwa jinsi alivyokuwa na hali ya udadisi katika maisha yake , aliamini ndani ya miezi hio miwili ya kuwa ndani ya Maktaba ya siri duniani atakuwa amejua mambo mengi sana..
Baada ya masaa mengi kupita hatimae Mr Kolfan alimkabidhi mzee huyu kitabu kimoja cha kale sana chenye maandishi makubwa juu yaliosomeka
U-97 THE REAL HISTORY –DR ROSELF J .PECKER.
“Hiko ndio kitabu ambacho kitakufanya ujue namna U-97 ilivyoanzishwa”Aliongea babu huyu na kumfanya Ambrose kupandwa na shauku ya kujua kile kilichokuwa kimeandikwa katika hiko kitabu.
Nini kimeandikwa katika hiko kitabu … see next chapter. On next seaso
ITAENDELEA IJUMAA
LIPIA 1500 NIKUTUMIE HII SIMULIZI YOTE , LIPA NAMBA 0687151346 AIRTEL/0623367345HALOTEL/0657195492TIGO JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI WATSAPP 0687151346
UNAWEZA PIA KUJIUNGA KWENYE GRUPU LANGU LA WATSAPP KWA SHILINGI 2000 NA KUPATA OFA YA SIMULIZI YA NILIMDHANIA KAHANA KUMBE BIKRA