Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 86



Kwa upande wa Neema aliamini kuwa mwanae angeenda nyumbani kwa siku hiyo na angechukua ushauri aliopewa na mama Pendo wa kumpeleka Salome kwenye maombi,
“Ila mwanangu atachukia akijua nimewaambia watu kuhusu yaliyomkuta, ila sikuwa na jinsi maana Yule mtu alituona”
Akawaza ila uhakika wa Salome kufika siku hiyo hakuwa nao, wanae wale wadogo nao walikuwa wamerudi na wametulia sebleni kwao wakimuangalia mama yao akiwa na mawazo sana, mmoja akamuuliza
“Mama mbona una mawazo hivyo?”
“Nawaza kuhusu dada yenu Salome sijui leo atakuja”
“Si umpigie simu mama”
“Salome hana simu”
“Mbona anayo, huwa tunamuona nayo akiongea na watu na akiitumia”
Neema akashangaa kusikia kuwa mtoto wake ana simu maana yeye aliamini kuwa mwanae hana simu, aliwauliza wanae kwa mshangao.
“Hebu achene maneno yenu, lini mmemuona dada yenu na simu?”
“Kila siku tunamuona nayo mama, tena muda mwingine anakuwaga anaitumia sana. Toka tumehamia huku anayo”
“Mmh sijui alinunuliwa na nani? Au Ashura?”
“Sijui ila mamdogo Ashura toka siku ameanguka wakati tunakula ndio hatujamuona tena”
Neema akazidi kushangaa na kuwauliza vizuri watoto wake,
“Mbona siwaelewi?”
“Dada alituambia tukacheze eti yeye na mamdogo wanacheza michezo ya kutaniana, na tulipoondoka badae akatuita na kutupakiza kwenye gari halafu tukahamia hapa”
“Inamaana hapa hamkuja na Ashura?”
“Hatukuja nae, dada Salome alisema mamdogo kaondokea kule kule. Ila mimi nilifurahi maana ona huku tunaishi kwa amani sana”
Wakatoka nje na kucheza huku wakimuacha Neema kwenye maswali mengi sana, akajiuliza na kama Ashura aliondokea kule kule ni kwanini Salome alimdanganya kuwa aliondokea kwenye nyumba mpya waliyohamia? Na michezo gani hiyo ya kuanguka wakati wa kula? Alijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu, na kubwa zaidi ni kuhusu kumiliki simu kwa Salome. Alijiuliza sana na mwishowe akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Ashura ila namba haikupatikana, alipiga na kupiga lakini aliambiwa haipatikani.
 
SEHEMU YA 87


Sara bado hakuwa na raha kwani alijiona ni mkosaji sana kwa mama yake akawaza namna ya kumuomba msamaha mama yake, muda huu akatoka chumbani ila alimkuta Salome kwenye korido yao halafu Salome akamwambia Sara nifate, Sara hakujiuliza mara mbili zaidi ya kwenda kumfata Salome.
Alimfata taratibu hadi kwenye chumba ambacho Salome alichukua ufunguo juu na kufungua kisha akaingia nae ndani na kufunga mlango kwahiyo ndani wakawa wawili tu, halafu akamwambia Sara huku akimuonyeshea mlango mdogo wa kwenye chumba kingine ndani ya chumba hiko,
“Fungua ule mlango”
Sara alikuwa akishangaa maana hajawahi kuingia kwenye chumba kile na wala hakuelewa kama kuna chumba kidogo ndani yake kama choo. Ila kwa muda huu aliamriwa na Salome kuwa afungue kile kimlango, Sara akakataa,
“Hapana Salome, unataka nifunguie ili iweje? Sijawahi kuingia humu ndani, sijawahi kujua kama chumba hiki kina chumba ndani yake halafu leo unaniambia nifungue hapana sifungui”
“Kama hutaki basi, ila mimi lengo langu ilikuwa ni kukusaidia”
“Kunisaidia kivipi?”
“Wewe kafungue tu halafu utaona nitakusaidiaje”
Sara akaanza kusogea akitaka kufungua, ila gafla akashtuliwa na sauti iliyotokea nyuma yake ilikuwa ni sauti ya mama yake.
“Unafanya nini hapo?”
Sara aligeuka na kumtazama mama yake ambaye alikuwa amemkazia sura vilivyo, ila cha kushangaza alivyoangaza huku na huku hakumuona Salome.
 
SEHEMU YA 88


Sara akaanza kusogea akitaka kufungua, ila gafla akashtuliwa na sauti iliyotokea nyuma yake ilikuwa ni sauti ya mama yake.
“Unafanya nini hapo?”
Sara aligeuka na kumtazama mama yake ambaye alikuwa amemkazia sura vilivyo, ila cha kushangaza alivyoangaza huku na huku hakumuona Salome.
Sara alishangaa sana kwa kutokumuona Salome hadi mama yake akamuuliza,
“Mbona unashangaa hivyo?”
Akataka kumwambia mama yake kuwa alikuwa na Salome ila akashangaa mdomo unakuwa mzito kupita maelezo, akabaki tu kimya na mara akamuuliza mama yake,
“umeingiaje humu?”
“Badala nikuulize wewe umeingiaje humu eti unaniuliza mimi! Badala uniulize utatokaje humu unauliza nimeingiaje? Hujui kama humu ni ndani kwangu, popote nina uhuru wa kuingia. Haya umeingiaje humu? Na umefuata nini”
Sara alikuwa kimya tu akimuangalia mama yake kwani kiukweli hata yeye mwenyewe hajui humo amefuata nini maana alikuwa akimfuata tu Salome ndiye aliyempeleka humo ingawa hakumuona tena, mama yake alimuangalia tena kwa hasira na kumuuliza,
“Ulikuwa unafata nini humu? Unashida gani humu wewe mtoto lakini? Yani yote uliyonitendea leo unaona hayatoshi zaidi ya kuendelea kunichokonoa chokonoa? Ngoja nisiongee kwanza humu tutoke kwanza”
Rose alimvuta mwanae mkono kisha akafungua mlango tu kawaida kanakwamba haukufungwa na funguo halafu akatoka nae ila Sara alimchoropoka mama yake kwani bado alikuwa akijiuliza kuwa Salome yuko wapi, alienda moja kwa moja kwenye chumba ambacho huwa analala Moza na kufungua mlango ilia one kama Salome yupo ila alifungua mlango na hakumuona yoyote, mama yake alikuwa nyuma yake na kumuuliza,
“Sasa unatafuta nini?”
Sara alitamani kumwambia mama yake kuwa kwenye chumba kile aliingia na Salome na hakumuona tena kwahiyo alitaka kumuangalia kama chumbani kwake yupo, ila mdomo ulikuwa mzito kusema hayo na alishindwa. Mama yake alipoona mwanae anabung’aa bung’aaa akamvuta tena mkono na kupita nae sebleni, halafu akaenda nae kwenye sebule nyingine ambayo wale mapacha hupenda kuitumia. Akakaa nae na kumuuliza,
“Sara, mimi ni mama yako au sio mama yako?”
“Wewe ni mama yangu”
“Kwanini huniheshimu sasa?”
“Mama sio kwamba sikuheshimu ila linapokuja kwa wewe kuhusishwa na habari za kichawi ndio huogopa”
“Una uhakika kama mimi ni mchawi?”
“Mbona Ana ni mchawi mama”
“Kwahiyo kama Ana ni mchawi huo uchawi nimempa mimi?”
“Hapana mama sijamaanisha hivyo”
“Na kama nimempa Ana uchawi basi nyie wote kwenye nyumba hii ni wachawi, unaponaje kuwa mchawi wakati mama yako mzazi ni mchawi? Uchawi unaujua wewe? Kwanza nani aliyekuambia kama mimi ni mchawi?”
“Sijui mama”
“Sara mwanangu, acha fikra mbaya. Wewe ni mwanangu wa kwanza na mambo mengi nafanya kwaajili ya maisha yenu, kumbuka baba yako alikukataa wewe toka upo tumboni mwangu. Je alikukataa kwavile nilikuwa mchawi? Nimehangaika mimi nimeteseka, nikawapata kaka zako nao wakakataliwa na baba yao. Sasa mimi kumpata mtu na kumdhibiti asifurukute kwenye himaya yangu na awajali nyie na kuwapenda na kuwapa chochote mtakacho ni uchawi huo? Kumtafuta mtoto kama Ana ili kuongeza upendo kwa mwanaume niliyempata, ni uchawi huo? Unaacha kujiuliza kwanini huolewi na umri umeenda umekazana kutafuta uchawi wa mama yako. Sitaki yakukute yaliyonikuta mimi, usiamini maneno au vitendo vya kusema mimi ni mchawi ila nafanya vitu kwaajili na maisha yenu yani wewe na wadogo zako. Sina tatizo na Ana, ni wa tofauti na nyie Yule. Sahau katika maisha yako kama utakuja kuolewa, na kaka zako wasahau maishani mwao kama watakuja kuoa, ila Ana ataolewa na ataolewa sababu nataka amtese mume wake. Mimi sio mchawi mwanangu, na sitaki unifatilie tena. Nadhani tumeelewana!”
“Nimekuelewa mama na ninakuahidi sitakufatilia tena, ila kwanini unasema kuwa mimi sitaolewa wala kaka zangu hawataoa?”
“Nitakwambia sababu ila sio leo, nyie mtaishi name miaka yote”
Rose aliondoka na kumuacha mwanae kwenye dimbwi la mawazo, alikosa jibu kuwa kwanini hatoolewa ila aliweza kuolewa kuwa ni kwanini kila mwanaume anayemleta mama yake anampinga mwanaume huyo, yani hapo ndio akaelewa kuwa mama yake hataki yeye aolewe, akasema lazima awataarifu kaka zake kuhusiana na hicho alichoambiwa na mama yao.
Kisha Sara aliinuka pale na kutoka.
 
SEHEMU YA 90



Mr.Patrick hakuonekana kabisa lakini Salome alielewa kitu gani kimempata Mr.Patrick na alihitaji kumsaidia bila yaw engine kuwa na mashaka, akajifanya kumuita mama yao sebleni maana alijua muda huu ni karibia wale mapacha walikuwa wanarudi, ni kweli baada ya kumuita tu wale mapacha nao walikuwa wamerudi, Salome alianza kwa kumuuliza,
“Yuko wapi baba yangu?”
“Sijui”
“Hujui!”
“Ndio nimekwambia sijui, halafu wewe mtoto sitaki maswala ya kunipanda kichwani kwenye nyumba yangu mwenyewe sitaki unipande kichwani”
“Sawa sitakupanda kichwani ila kila mmoja humu ndani ataona baba alipo leo”
“Unamaanisha nini?”
“Si hujataka kusema baba yuko wapi, basi nitamuonyesha kila mmoja alipo baba”
“Hivi wewe msichana una nini na kwanini unajiamini hivyo?”
“Unaogopa kujiamini kwangu eeh! Najiamini sababu najua hakuna wa kunishinda, baba yangu yuko wapi? Nimekuwa mpole sana kwa siku zote hizi ila hujiongezi wala nini. Subiri tena nakwambia kila mmoja nitamuonyesha baba alipo leo”
kisha Salome akaondoka zake na kwenda chumbani kwake, kwakweli Rose alimshangaa sana Salome kuwa anajiamini na nini mpaka anafikia kumwambia yeye maneno yale wakati watu wengi sana wanamuogopaga yeye, ikabidi aonoke aende chumbani kwa binti yake Ana kuzungumza nae basi na yeye akamueleza mama yake vitisho alivyopewa na Salome,
“Hivi anajiamini nini Yule?”
“Hata mimi mwenyewe namshangaa mama sijui anajiamini nini?”
“Tunatakiwa kufanya jambo mapema iwezekanavyo”
“Ndio mama”
“Sasa tutafanya nini?”
“Tumuingize kwenye kile chumba”
“Sawa sawa mwanangu”
Wakaanza kukubaliana pale namna watakavyomtokomeza Salome, bila ya kujua kuwa mbinu nyingi Salome anazijua.
 
SEHEMU YA 91



Muda huu Sara alienda kuwafata kaka zake na akaongea nao namna ambavyo mama yake alimwambia mchana, ila wale mapacha wakapinga vikali kauli ya mama yao,
“Haiwezekani, kwakweli haiwezekani kabisa. Mimi nitaoa labda wewe Doto ndio hutooa”
“Mimi pia nitaoa, labda wewe mwanae wa kwanza ndio hutaolewa. Sisis tusioe kwa misingi gani? Kwanza mchumba wangu yupo tayari, ni kitendo tu cha kumleta nimtambulishe”
“Mmmh msiwe wabishi, mwenzenu mchumba wangu amepotelea humu kwenye nyumba”
“Kivipi?”
Sara aliwaeleza jinsi Ommy alivyopotea kiajabu ajabu, na kuwaambia kuwa kitu hiko amekiona kwenye ndoto.
“Mmh kwa staili hii simleti tena Yule mchumba wangu”
“Mimi nitamleta tu bila kujali chochote, Yule ni mama yetu lakini hatakiwi kuingilia kwenye mahusiano yetu. Kwanza tusioe kwanini? Au wewe usiolewe kwanini? Hebu acha hizo bhana.”
Mmoja akajikuta akikumbushia ishu ya Salome,
“Jamani huyu dogo Salome mnamuelewa kweli?”
“Jamani Yule mtoto kaka zangu ni ana mambo ya ajabu yani ya ajabu sana, nimejaribu hata kulala nae nimchunguze ila cha kushangaza nikilala nae nakuwa kama mzigo yani nikilala sishtuki hadi kunakucha yani hata chooni siendi. Yule dogo mi mwenyewe simuelewi”
“Ila wewe Sara una moyo, hata kulala na mtu asiyeeleweka vile unaweza mmmh! Mtoto haeleweki Yule, sijawahi kumuelewa toka siku ya kwanza amekuja humu ndani”
“Ila kuna kitu nahisi kuhusu huyu dogo”
“Kipi hicho doto?”
Gafla wakasikia sauti ya mama yao akimuita Salome kwa ukali sana, ikabidi nao waende kushuhuia kuwa kuna nini mbona ameitwa hivyo.
Kufika sebleni walimkuta mama yao akiwa na Ana halafu muda kidogo Salome nae alifika ila kabla hakijaongelewa chochote walishangaa kumuona mama yao akimsogelea Salome na kumsukuma kwa nguvu. Rose alijua Salome ataanguka chini ila ilikuwa kinyume maana Salome hakuanguka chini, Rose akamsukuma tena ila Salome alisimama kamavile mlingoti. Muda huu Rose alipotaka kumsukuma tena Salome alishangaa mkono wake ukianza kutetemeka.
 
SEHEMU YA 92



Rose alijua Salome ataanguka chini ila ilikuwa kinyume maana Salome hakuanguka chini, Rose akamsukuma tena ila Salome alisimama kamavile mlingoti. Muda huu Rose alipotaka kumsukuma tena Salome alishangaa mkono wake ukianza kutetemeka. Kila mmoja ndani ya nyumba yake alimshuhudia Rose akitetemeka mkono, Ana akainuka kwani aliona mama yake asije akaumbuka yeye kisha Ana akamsukuma yeye Salome ila kwake ndio ikawa kinyume kabisa kwani mkono wake uliganda kwenye mwili wa Salome, kila mmoja alikuwa akishangaa na kati ya wale mapacha na Sara hakuna aliyeweza kuongea neno lolote.
Mara Salome alianza kuelekea vyumbani ila Ana ambaye mkono wake uliganda kwa Salome alikuwa akimfata nyuma, halafu Rose naye ambaye mkono wake ulikuwa ukitetemeka alikuwa akimfata nyuma pia, kitendo hiko kiliwafanya wale mapacha na Sara wafate nyuma kwani walitaka kujua ni nini kinaendelea au ni kitu gani huyo Salome anataka kufanya.
Salome aliongoza moja kwa moja mpaka chumbani kwa Rose na kufungua mlango, kila mmoja alikuwa akimfata nyuma huku wengine hawaelewi elewi, alikutwa Patrick akiwa amelala chini sakafuni, Salome akamuangalia Rose na kumuamuru,
“Muamshe”
Rose akiwa anatetemeka, alisogea kwa Patrick na kujaribu kumuamsha. Alimuamsha kwa muda akashindwa, akainua kichwa chake na kumtazama Salome kwa uoga kisha akamwambia,
“Nakuomba basi wanangu watoke humu chumbani nimuamshe”
“Unashindwa nini kumuamsha hivyo hivyo?”
“Tafadhali usinidhalilishe, nakuomba watoke kwanza ndio nimuamshe. Nipeni dakika chache tu nitakuwa nimemuamsha”
Salome akatoka nje na wengine wote walimfata nyuma hadi sebleni kwahiyo walimuacha mama yao akiwa chumbani na Patrick.
Kila mmoja alikuwa akimshangaa tu Salome na wala Ana hakuweza kuutoa mkono wake kwenye mwili wa Salome maana uligandia alipotaka kumsukuma, kwahiyo walikuwa wamesimama tu na hakuna yeyote aliyethubutu kukaa wala kusema neno lolote kwa wakati ule kwani wote walijikuta wakimtazama tu Salome.
 
SEHEMU YA 93



Baada ya muda kidogo, mama yao alirudi na Patrick sebleni na muda huu hata Ana akaweza kuutoa mwili wake kwenye mwili wa Salome, basi Salome alienda kumfata Patrick na kumkalisha kwenye kiti kisha akapitisha mkono wake machoni pake na kusema,
“Nataka uone yote na zaidi ya yote amabayo mkeo amekuwa akikutendea kwa miaka yote hii”
Ikawa kama akili ya Patrick imefunguka kiasi hivi kwani alianza kujishangaa na kuhoji kuwa yuko wapi,
“Nikowapi hapa?”
Ni Salome pekee aliyekuwa na ujasiri wa kumjibu,
“Unatakiwa kutulia kwanza maana ndio umetoka kifungoni ni ngumu kujua kwa mara moja ulipo. Tulia kwanza tuliza akili halafu utajua ulipo na kila kitu ingawa kuna baadhi ya vitu utavitambua badae sana”
Patrick alikaa kimya kwani alikuwa kama haelewi elewi vile.
Walitamani kumuhoji Salome lakini hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo, kisha Salome akainuka na kwenda zake ndani kisha akawaacha wote pale sebleni. Yani kama kuna siku ambayo Rose aliwaonea wanae aibu basi ilikuwa ni siku ya leo maana nae hakuweza tena kukaa pale sebleni bali aliondoka na kwenda chumbani kisha Ana nae akafata na kwenda chumbani kwake. Kwahiyo sebleni walibaki wale mapacha, Sara na Patrick. Muda kidogo Patrick alimuangalia Sara na kumuomba jambo,
“Naomba kaniletee simu yangu na funguo za gari chumbani”
Sara hakubisha wala nini, alifanya hivyo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo aligonga na mama yake alimkaribisha kwani alijua ni Ana, akashangaa kumuona ni Sara. Akamuuliza kwa mshangao,
“Vipi tena?”
“Baba kanituma funguo za gari na simu yake”
“Chukua hivyo hapo mezani mpelekee”
Yani siku ya leo hata kuhoji hakuhoji zaidi ya kusema funguo zilipo na simu ya mumewe, simu ambayo mume wake ana kitambo sana hajaishika wala kuwasiliana na watu. Sara alichukua na kwenda kumpelekea baba yake huyo wa kambo. Alipompa tu Patrick alitoka nje na kuondoka zake, tena hakuna aliyemuaga kuwa anaenda wapi.
Wale mapacha waliangaliana na dada yao Sara, halafu Sara akawaambia,
“Yani kwa matukio haya naogopa hata kulala peke yangu”
“Sasa utalala na nani?”
“Sijui yani”
“Basi kalale na Ana au Salome”
“Mmmh hao watu ni bora uniambie nikalale getini na mlinzi, nawaogopa hao watu kama kitu gani”
Mara Salome akatokea, Sara akajikuta tu akimwambia
“Baba kaondoka tena bila kuaga, halafu leo kachukua na simu yake”
“Ungekuwa ni wewe ungeweza kuaga?”
“Kivipi?”
“Unajifanya hujui ambayo baba yangu alikuwa akitendewa kwenye nyumba hii? Sasa anatambua kila kitu, maswala ya kumfanya mwenzenu kama ndondocha mwisho”
Sara aliwaangalia wenzie, halafu Salome alitoka nje kabisa na alionekana akielekea getini ambako alitoka na kuondoka.
Sara aliwauliza wenzie,
“Jamani mnamuelewa huyu mtoto?”
“Simuelewi na sitaki kuongea sana”
“Hata mimi pia simuelewi na naogopa kuongea sana”
Kisha wale mapacha wakaondoka zao na Sara akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 94



Rose alipoona mwanae Ana hajaenda chumbani kwake ikabidi yeye mwenyewe ndio aende chumbani kwa Ana, aliingia na kumuuliza mwanae,
“Hivi wewe umeweza kumuelewa huyu Salome?”
“Mama naomba tuzungumze usiku kwenye muda wetu sio muda huu”
“Hata tukisema tuzungumze usiku hatatusikia kweli?”
“Mama, mimi ndio nimekwambia na bado natafakari maana sipo sawa kabisa. Amewezaje Yule kugandisha mkono wangu mama? Yule msichana ana majini sio bure”
“Ndiomana nakwambia tujadili sasa hivi, unajua ile majuzi nilienda kwa mganga mwingine halafu ndani kwa mganga nilimkuta Moza”
“Moza!”
“Ndio nilimkuta Moza”
“Si amekufa huyo mama”
“Mwanangu hatuna uhakika na kifo cha Moza, kumbuka maiti yake ilitoweka kaburini”
“Ndio ilitoweka ila nikajua utafanya jambo, na imekuwaje hadi Moza awe hajafa kweli?”
“Sijui mwanangu, ila kama ile dawa iliyomuua Moza ilichomwa moto basi tumeisha”
“Unamaana gani mama?”
“Ile dawa mwanangu nilipewa na ilikuwa hairuhusiwi kuonekana na mtu yeyote halafu sitakiwi kuiweka mbali na nyumba yangu ndiomana nikaifukia kwenye ua ili nijue ni ua gani nimeifukia. Ni ya muda mrefu sana ile dawa na ilikuwa hairuhusiwi kuonekana na mtu yeyote wala kuungua na moto ndiomana hata kuunguza mboga humu kwenye nyumba yangu huwa sitaki. Sasa kama imechomwa moto sijui itakuwaje, ndiomana tulitakiwa kumzika nayo Moza”
“Sasa mama kama imechomwa moto imechomwa na nani wakati Moza alikuwa amekufa nayo mkononi”
“Kwamaana hiyo inawezekana ipo mahali eeh! Lakini mbona tuliitafuta bila kuiona popote”
“Mi nadhani mama tufanyie usafi kile chumba cha Moza tuitafute kabla hayajawa majanga”
“Sasa lile shetani linalolala kwenye chumba kile tutalifanya nini?”
“Yani huyo mtu ananiumiza kichwa balaa, ila mama na wewe kwanini dawa ya maana hivyo ukaenda kuifukia kwenye ua? Mbona mimi dawa yangu ile ipo chini ya godoro”
“Ni masharti ya ile dawa, kwanza haikutakiwa kuwekwa ndani ya nyumba ila inatakiwa iwe karibu na nyumba halafu haitakiwi mtu aione.”
“Basi mama nitatumia dawa yangu kufanya kitu ili tuweze kupekua kile chumba cha Moza”
“Sawa mwanangu, ndiomana nilikuwa nakufata tujadili. Sasa wewe unataka tufanye kwenye muda wetu, unadhani mambo yalivyotinga hivi tutakumbuka kujadiliana kweli! Ni ngumu mwanangu”
“Kweli mama ila chanzo cha mambo yote haya ni mwanao Sara, yani simpendi Yule mdada simpendi kabisa”
“Kweli mwanangu ni chanzo cha yote lakini ni mwanangu, kumbuka hilo. Yule ni dada yako mpende tu”
Rose akajiribu pale kumshawishi mwanae ili ajende upendo kwa ndugu yake maana alikuwa anapenda watoto wake wapendane.
 
SEHEMU YA 95


Salome alienda nyumbani kwa mama yake na kumkuta kama kawaida akiwa na wale wadogo zake John na Joseph. Aliwasalimia kisha mama yake akamuomba chumbani kwake ili wakazungumze
“Kwanza imefurahi umerudi nyumbani maana mambo yako siku hizi siyaelewi kabisa. Halafu ngoja nikuulize, hivi una simu”
Salome akacheka,
“Sio unacheka Salome, nijibu una simu?”
“Ndio nina simu”
“Umeitoa wapi?”
“Baba yangu kaninunulia ili niweze kuongea nae”
“Haya, wadogo zako wameniambia Ashura hakuja huku kwenye nyumba mpya, halafu wewe na Ashura kuna mchezo mlikuwa mnacheza kisha Ashura akaanguka. Unajua sijaelewa naomba nieleweshe maana huyo Ashura hata nikimpigia simu zangu hapokei zaidi ya kunitumia ujumbe tu”
“Hivi hat nikikueleza unaweza ukanielewa!”
“Nieleze tu, kwanini nisikuelewe?”
“Acha tu ufahamu unavyofahamu, Yule Ashura si ndugu yako? Uliza kwa ndugu zenu alipo”
“Hivi wewe mtoto unaongelea nini mbona sikuelewi?”
“Huyo mamdogo Ashura yupo kwenye kijiji cha baba yenu amesema anaenda kuangalia kaburi la baba yenu kwahiyo ungeenda na wewe kijijini ili uulize vizuri kuhusu Ashura”
“Tutaenda na wewe?”
“Hapana, mimi nitabaki ila utaenda na wadogo zangu. Mimi nabaki na baba yangu.”
“Haya nitafikiria kwenda”
Salome akainuka, na kumfanya Neema amuulize tena,
“Sasa mbona unaondoka kabla hata sijamaliza maongezi na wewe”
“Subiri nakuja sasa hivi”
Salome aliondoka zake, Neema nae alitoka ila kiukweli hakumuelewa kabisa mwanae na mambo aliyokuwa anayafanya.
Alipokaa muda kidogo mwanae alirudi kisha akampa mama yake tiketi,
“Nimeshakukatia tiketi, wewe na wadogo zangu ya kwenda kutembelea kaburi la babu”
“Kheee kwahiyo ndio unataka tusafiri!”
“Ndio, si mnaenda kukaa wiki tu mnarudi”
“Kwahiyo tiketi umekata ya kuondoka lini?”
“Kuondoka kesho”
“Kheee Salome hebu acha masikhara, tutaondokaje kesho wakati hatujajipanga!”
“Unataka mjipangaje?”
“Sijapanga nguo za watoto, sijawanunulia mama zangu vitenge”
“Ni hayo tu au kuna mengine?”
“Ni hayo ndio”
“Basi nitakusaidia, yani wewe tulia tu nitakusaidia kupanga ila tiketi ni ya kesho”
Neema alimshangaa sana Salome kuwa mtoto wake amebadilika sana na amekuwa na maamuzi ya haraka haraka, akawa anaziangalia tu zile tiketi ambazo alikuwa amekatiwa na Salome.


Usiku kwenye mida ya saa tatu, Neema akiwa amejipumzisha kidogo akamsikia Salome akiingia ndani kwake na kumwambia,
“Mama kila kitu nimekupangia kwahiyo kesho safari”
“Na nguo zangu, na za wadogo zako umepanga?”
“Ndio tayari”
“Ila vitenge bado sijanunua”
“Nilishaenda kununua”
“Kheeee hebu tuvione”
Salome alimtolea Neema vitenge ambavyo aliviangalia na kushangaa tu kuwa Salome amewezaje kwenda mjini kwa muda mfupi vile na kuchagua vitenge bvizuri vile, akainuka na kuangalia mabegi ni kweli yalikuwa yamepangwa vizuri kabisa kwahiyo hakuwa na cha kubisha kuhusu safari ya kesho, swala hilo hata likamsahaulisha kuwa alishauriwa mwanae ampeleke kwenye maombi.
“Nishaongea na dereva tax, kwahiyo atakuja kuwachukua kesho asubuhi”
“Kwahiyo nyumba nani atafunga?”
“Mimi nitafunga, na mkiwa mnarudi mtanikuta maana nitakuwa narudi mara kwa mara”
Neema alimuangalia mwanae Salome hakummaliza maana kwa kawaida Salome wake ni muoga ila leo hii anakubali kuachwa mwenyewe nyumbani na anasema atakuwa anaenda mara kwa mara hata wakirudi watamkuta, alimshangaa kwakweli ila akajisemea labda ndio kukua kumemfanya abadilike.
 
SEHEMU YA 96


Usiku wa manane, Rose alichukuana na mwanae kwenda kufanya msako kwenye chumba cha Moza kutafuta ile dawa iliyomuua Moza maana walihisi bado ipo ndani. Basi walipekua na kupekua lakini hawakufanikiwa kuiona, ndipo walipoanza kupekua nguo moja moja ya Moza ila Ana akamwambia mama yake,
“Mama, tutajichosha bure. Ngoja twende chumbani kwangu nikachukue ile dawa yangu ituonyeshe”
Rose aliafikiana na mwanae na kujilaumu kuwa kwanini walikuwa wakijichelewesha wakati kuna njia rahisi ya kufanya, basi wakatoka mule chumbani kwa Moza na kuelekea chumbani kwa Ana walipofika walishangaa kumuona mtu amekaa kitandani kwa Ana halafu mtu huyo akawaangalia na kuwafanya wagundue kuwa ni Moza.

Rose aliafikiana na mwanae na kujilaumu kuwa kwanini walikuwa wakijichelewesha wakati kuna njia rahisi ya kufanya, basi wakatoka mule chumbani kwa Moza na kuelekea chumbani kwa Ana walipofika walishangaa kumuona mtu amekaa kitandani kwa Ana halafu mtu huyo akawaangalia na kuwafanya wagundue kuwa ni Moza.
Kwa mara ya kwanza Ana alishikwa na uoga ambao hajawahi kuupata kabla, wakafunga mlango haraka haraka na huku wakihema juu juu, hakuna aliyeelewa kwa wakati ule ila wakajikuta tu wanaenda tena chumbani kwa Moza, ila kwa wakati huu napo walimkuta amekaa kitandani, katika siku zote leo mkojo ulimtoka Ana kwa uoga walifunga tena mlango na kukimbilia sebleni huku wakihema juu juu na wakikumbatiana mama na mtoto, kwa wakati huo hakuna uchawi walioweza kuufanya maana uwepo wa Moza uliwachanganya kuwa ni mzimu au ni kitu gani. Hata sebleni hawakuweza kukaa sana kwa uoga wakafungua mlango na kukimbilia nje. Kitendo hiki kilimshtua pia mlinzi aliyekuwa kalala, aliamka na kwenda kuwauliza kuwa tatizo ni nini, Ana alijikuta akiropoka,
“Kuna mzimu ndani”
“Mzimu!”
“Ndio, kuna mzimu wa Moza”
Gafla wakahisi kama eneo hilo linatingishwa yani kama mtu anatingisha ardhi, kisha wote wakazimia. Rose, Ana na mlinzi wao.
 
SEHEMU YA 97


Kulipokucha, wale mapacha waliamka na kujiandaa kutoka kama kawaida na wazo lao walihisi kumkuta mama yao sebleni ila hawakumkuta, muda kidogo Sara nae akatoka na kuwauliza kaka zake,
“Eti mama ameshaondoka?”
“Sijui, sisi wenyewe hatujamkuta hapa sebleni”
“Nimeenda kumuangalia chumbani kwake nimemkosa, sijui atakuwa wapi”
“Sie tunaondoka bhana”
“Nisubirini, yani jumba lote hili mniache peke yangu”
“Mbona zamani ulikuwa unaweza kubaki peke yako!”
“Ushasema zamani, siku hizi mambo yamebadilika. Nisubirini bhana”
Wakamsubiri dada yao ajiandae, alipomaliza akatoka kisha wakatoka nje ili kuondoka ila wakashangaa walipotoka kumuona mama yao, mdogo wao na mlinzi wakiwa chini wamelala maana walipowaamsha waliamka na kushangaa sana, Sara alimuuliza mama yake,
“Imekuwaje mama?”
“Sina jibu kwasasa”
Yule mlinzi aliinuka na kwenda kwenye lindo lake, kisha Rose na Ana waliinuka na kwenda ndani. Ila muda huo Rose aliwaomba wanae wasiondoke wamsubiri kwanza, ikabidi wamsubiri kwani hakuna aliyekuwa anajua kuwa mama yao amepatwa na nini.
Wakati ameenda kujiandaa walienda kumuuliza mlinzi kuwa ni kitu gani kimetokea,
“Hata mimi sielewi”
“Huelewi kivipi?”
“Yani sielewi sijui hata imekuwaje mpaka nimelala pale”
“Kwahiyo hujui ni kitu gani kilitokea?”
“Sijui kweli yani sijui kabisa”
Wakamuacha na kurudi ndani wakimsubiri mama yao na Ana. Baada ya muda kidogo mama yao akatoka, na swali la kwanza alimuuliza Sara,
“Salome mbona sijamuona kaenda wapi?”
“Aliondoka jana na hakurudi tena”
“Aaah sawa, jamani leo mkitoka nawaomba muda wa kurudi msubiri hadi niwapigie simu, asirudi yeyote hapa ndani hadi niwapigie simu. Mimi na Ana kuna mahali tunaenda”
Watoto wake wakatazamana maana hawakuona kama lile jambo lilikuwa na umuhimu kiasi cha wao kurudishwa wasiondoke kwa muda huo na wasubirie maana angeweza hata kuwapigia simu na kuwapa ujumbe huo, baada ya maongezi hayo nyumba nzima wakatoka, kwakweli Rose hakuwa hata na muda wa kuulizia kuhusu Patrick kwani kadri siku zilivyoenda mbele ndivyo akili yake ilivyozidi kuchanganyikiwa.
 
SEHEMU YA 99


Siku ya leo wale mapacha na dada yao walienda sehemu moja ila njiani wakakutana na Salome akidai kuwa anaenda nyumbani,
“Ila hakuna mtu nyumbani”
“Kuna nguo yangu naenda kuichukua”
“Unawezaje kwenda kwenye nyumba ya watu bila ya wenyewe kuwepo?”
“Leo unaniuliza hivyo Sara, hivi siku ile ningeogopa kuja ungepona macho yao hayo?”
“Ila mama amekataza kwenda nyumbani amesema hadi apige simu?”
“Amewakataza ninyi sio mimi”
“Mmmh kasema mtu yeyote”
“Jamani nina uhakika hata nikiwauliza sababu ya kukataza mtashindwa kunijibu, Ngoja niende zangu tu.”
Sara akawa kimya kwa muda basi Salome akawaaga na kuondoka, wakati Salome anaondoka tu kabla hawajaongea chochote alitokea rafiki yake na Sara, kisha aliwasalimia na kuwauliza kuwa Salome ni nani yao,
“Yule aliyeondoka ni nani yenu?”
“Ni ndugu yetu”
“Aaah kumbe siku zile alipona?”
“Siku gani?”
“Siku ile aliyoangukia kaburini”
Wote wakamshangaa kwani hakuna aliyekuwa na wazo kuwa ni Salome ndio aliangukia kaburini,
“Mbona hatukuelewi?”
“Siku ile wakati anazikwa Yule mdada wenu wa kazi basi huyu msichana ndio aliangukia kaburini na akawa kama amepigwa shoti”
“Mmmh au umemfananisha?”
“Hapana sijamfananisha, zile nguo ndio zile zile alikuwa amezivaa siku ile. Halafu nilimshuhudia hadi anapakizwa kwenye gari ili apelekwe hospitali. Nikataka kwenda na mimi ila wakanikatalia. Tena nakumbuka hata dereva aliyembeba ni mtu ambaye anafahamiana na mtu ninayemfahamu, ngoja tukamuulize vizuri ila ni yeye”
“Mmh wewe rafiki yangu wewe Jesca, acha maneno yako”
“Jamani mimi ule umbea mlinifukuzaga kwenu pale nisikanyage nimeshaacha na wala huu ninaoongea sio umbea ni ukweli kabisa. Yule msichana alitumbukia kaburini na akakauka kama amepigwa shoti ya umeme”
Wale mapacha hawakuyaamini maneno ya rafiki wa Sara na kuomba wapelekwe kwa huyo dereva kwa uthibitisho kwani lazima dereva aliyembeba alikuwa anajua, na Yule msichana aliamua kuacha mambo yake aliyokuwa anafanya kwa muda huo na kwenda kumtafuta huyo dereva.
 
SEHEMU YA 100



Zamu yao ilifika ya kuingia kwa Yule mganga, waliingia na kumkuta ambapo kabla hawajamueleza matatizo yao Yule mganga aliwaambia,
“Najua kila kitu, yani kitu pekee kinachowasumbua ni Moza”
Walishtuka na kuangaliana sababu huyu mganga amejua kabla hata hawajamueleza, Rose akamuitikia Yule mganga,
“Tawile baba, yani hata hatujui tufanye nini”
“Hapa ndio mwisho wa matatizo, yani mimi ndio kila kitu. Mimi ni tishio la vitu vyote vya ajabu, Yule Moza amerudi kwa lengo moja la kukukomesha wewe. Yule msichana alijua siri zako mapema sana kabla hata hujajua kuwa anafatilia siri zako, na kitendo chake cha kupata ile dawa ndio kila kitu kimekuwa wazi kwake”
“Kwahiyo inamaana Moza ni mzimu?”
“Moza ni zaidi ya mzimu ambao unajua wewe, Moza ana nguvu za ziada kwani ana nguvu za kutoka kwenye mzimu wa bibi yake na ana nguvu za ile dawa yako maana ilichomwa”
Rose alishtuka sana kusikia kuwa dawa yake ilichomwa kwani hapo alihisi kila kitu kimeharibika, kwakweli alihisi nguvu kumuisha akauliza kwa upole,
“Sasa kama ile dawa yangu ilichomwa, aliichoma nani na je nifanye nini?”
“Ile dawa ilichomwa na mume wako”
Rose na Ana walishangaa sana kuwa ile dawa imechomwa na aliyeichoma ni Patrick, kwahiyo walijiuliza kuwa Patrick alipata wapi ujasiri wa kuchoma ile dawa na kwanini alifikia uamuzi wa kuchoma ile dawa,
“Kama nilivyowaambia, Moza anaongozwa na mzimu wa bibi yake na mzimu huo ndio ulimtuma Patrick akachome ile dawa halafu Moza aliongezeka nguvu mara mbili. Nyie mnahisi Moza amekufa ila kiuhalisia Moza hajafa na amerudi kwaajili yenu”
“Sasa tufanyaje?”
“Cha kufanya hapa ni kimoja tu”
“Kipi hiko?”
Akamuangalia Rose na kumwambia,
“Unatakiwa ulale na mlinzi wako”
“Nilale na mlinzi wangu?”
“Ndio, unatakiwa ulale nae”
“Kheee nitawezaje kulala na mlinzi wangu?”
“Nitakupa dawa ya kukusaidia, na ukilala nae kwa hakika kila kitu utaona kimebadilika”
“Jamani mganga sikuelewi, kwanini mlinzi wangu nilale nae?”
“Yule mlinzi alikuwa anampenda sana Moza yani alikuwa na mapenzi ya dhati na Moza. Unatakiwa kulala nae ili kutimiza ile azma ya mapenzi yake kwa Moza kisha ndio tutamuweza Moza. Tena unatakiwa ulale nae kwenye chumba alichokuwa analala Moza”
“Mmh mbona umenipa mtihani mkubwa sana, je litawezekana hilo?”
“Nitakupa dawa na itawezekana”
Rose alijifikiria sana namna ya kulala na mlinzi wake maana siku zote amekuwa akimdharau sasa leo anatakiwa alale nae, kwakweli aliona ni mtihani mkubwa sana ila kwavile alichoshwa na vimbwanga vya hapa na pale akajisemea ni lazima afanye hivyo ili aepukane na vimbwanga vile.
Kwahiyo akakubali kuchukua dawa aliyopewa na mganga, kisha kuuliza kuwa baada ya kulala nae afanyaje.
“Baada ya kulala nae tu, yani kwanza mumeo atarudi na kuwa chini yako halafu Moza atakufa kweli. Nitakupa tu maelekezo ya hii dawa, ukifika getini iweke mdomoni usiongee chochote na mlinzi wako, yani wewe mshike mkono tu hadi chumbani kwa Moza halafu lala nae”
“Hawezi kuniletea shida?”
“Usiongee kitu chochote, na kukataa hawezi hata usijali”
Basi Moza akachukua ile dawa na kuanza safari ya kuondoka akiwa na binti yake Ana, ila muda huu walipata usafiri wa boaboda hadi darajani.
 
SEHEMU YA 101



Salome alifika na kumkuta mlinzi akiwa getini, basi Salome akamuomba kitu Yule mlinzi,
“Kuna mahali nataka nikuagize”
“Mmmh yani niondoke niache lindo langu? Hapana kwakweli”
“Katika maisha yako, umewahi kupewa hela ipi nyingi kwa mkupuo”
“Nimewahi kupewa laki tano”
“Basi mimi nataka nikupe milioni mbili ila tu ukiniahidi kwenda ninapotaka kukuagiza”
Yule mlinzi aliposikia milioni mbili, kwakweli akili yake iliruka kidogo na kusikiliza anapotaka kuagizwa,
“Sio sehemu mbaya, nakuagiza hotelini alipo mzee Patrick uende ukamshawishi hadi urudi nae hapa. Jitahidi kwa ujui wako wote umshawishi arudi”
Yule mlinzi hakuona kama ile ni kazi ngumu, ila alihitaji kupewa hizo hela kabisa na kuuliza tena,
“Na hapa getini atakaa nani?”
“Mimi nitakaa hapa getini kwa siku ya leo na siendi popote, unajua Yule ni baba yangu. Nahitaji aje nyumbani”
Kisha Salome akamkabidhi pesa Yule mlinzi na kumuelekeza mahali alipo mzee Patrick halafu Yule mlinzi akaondoka zake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Yule mlinzi kuondoka kwenye lindo lake hilo wakati mama mwenye nyumba hayupo.
Muda kidogo alirudi Rose na binti yake Ana, ila walimkuta mlinzi yupo getini amesinzia. Rose alikunywa dawa yake na kuanza kumvuta mlinzi mkono ili waelekee nae ndani, ila mlangoni akakutana na Salome. Rose akashtuka kwani hakutegemea kukutana na Salome mlangoni, halafu Salome akamuuliza,
“Vipi huyo mlinzi unampeleka wapi?”
Rose alitamani kumjibu Salome ila akakumbuka masharti aliyopewa na mganga kuwa asiongee kabisa akimeza ile dawa, hakujibu ila akataka kuingia ndani ila Salome akamzuia mlangoni na kumfanya Rose achukie sana akatamani hata mwanae Ana angekuwa karibu apambane na Salome kwani muda huu Ana alikuwa ameachwa getini akisubiria mama yake amalize kwanza shughuli na mlinzi.
Rose akawa anang’ang’aniza aingie ndani,
“Sikupishi hadi uniambie huyo mlinzi unampeleka wapi?”
Rose alipambana na Salome pale mlangoni hadi akajikuta akimwambia,
“Nipishe bwana weee”
Salome alimpisha huku akicheka sana, Rose alikuwa na hasira sana na alijiuliza kama dawa itafanya kazi kama alivyoambiwa na mganga maana kashakosea masharti na kuongea wakati aliambiwa asiongee chochote.
Aliingia na Yule mlinzi kwenye chumba cha Moza na kumuweka kitandani, kisha yeye akainuka na kuanza kuvua nguo zake ila alipomaliza tu kutazama kitandani hakumuona mtu yeyote.
 
SEHEMU YA 102


Salome alimpisha huku akicheka sana, Rose alikuwa na hasira sana na alijiuliza kama dawa itafanya kazi kama alivyoambiwa na mganga maana kashakosea masharti na kuongea wakati aliambiwa asiongee chochote.
Aliingia na Yule mlinzi kwenye chumba cha Moza na kumuweka kitandani, kisha yeye akainuka na kuanza kuvua nguo zake ila alipomaliza tu kutazama kitandani hakumuona mtu yeyote.
Mlinzi alikuwa ametoweka, kitendo hiki kilimshtua sana Rose na kumfanya achukue nguo zake haraka haraka na kuvaa kisha kukimbia kutoka kwenye kile chumba cha Moza, ila kwenye korido akakutana na Salome yani muda huu hakuweza hata kuongea na Salome zaidi ya kukimbilia nje alipo mtoto wake, Salomealicheka sana kisha akaenda kukaa sebleni na kuwaangoja Rose na mwanae watakavyorudi tena ndani.
Basi Rose alifika alipo mwanae Ana kwenye kile kijumba cha mlinzi, Ana alimuuliza mama yake,
“Tayari mama?”
“Tayari nini mwanangu? Mambo yameharibika”
“Kivipi?”
Mara geti lilifunguliwa halafu wakamuona mlinzi ambaye aliingia na kwenda kufungua geti kubwa na liliingia gari la Patrick. Rose alishtuka sana na kufikicha macho yake kwani alihisi ni kiini macho. Alimshika mwanae mkono na kumpakiza kwenye gari kisha akaondoa gari nje hata mlinzi na Patrick walikuwa wakishangaa ila Patrick alihisi kuwa Rose anamkimbia kwani anajua kuwa anaujua ukweli wa mambo yote sasa.
 
SEHEMU YA 103


Patrick na mlinzi waliingia ndani na kumuta Salome, kwakweli Salome alimpongeza sana Patrick kwani aliona jinsi alivyomfanyia kazi yake kuwa rahisi kwa siku hiyo, kisha akamkaribisha Patrick pale ndani,
“Karibu tena kwenye nyumba yako”
“Ni kweli hii ni nyumba yangu mwanangu, ila sina hamu nayo na siwezi kuishi humu tena”
“Kwanini?”
“Sijisikii tena kuishi na mwanamke shetani kama Rose, nilimuacha mke wangu mpole, mzuri na mcha Mungu Neema, aliyenipenda kwa dhati. Lakini nilimuhisi vibaya kwa makosa ya kusingiziwa, kumbe alisingiziwa kila kitu juu yake. Ashura ni ndugu wa mama yako ila ni mtu mbaya sana”
“Hapana Ashura hakuwa ndugu wa mama”
“Kivipi hakuwa ndugu yake na wakati alikuwa akiishi nae?”
“Niambie kwanza Ashura ni mtu mbaya kivipi na nitakueleza ni namana gani hakuwa na undugu na mama”
Patrick alianza kumueleza kwa kifupi jinsi ilivyofikia hadi kuachana na mama yake,
“Sikia, sikuwa namjua Ashura ila nilikutana nae nyumbani kwa Rose na alitambulishwa kwangu kama msichana wa kazi wa Rose, wakati tunamuongelea mke wangu basi Yule Ashura alidai ya kwamba anamfahamu yani yeye na Neema wamechangia baba. Na akaanza kunieleza kuhusu historia ya Neema, anasema Neema alianza uhuni mapema sana toka yupo darasa la tano na ametoa mimba nyingi sana, ingawa mimi nilimuoa mapema pia ila hakuweza kunizalia sababu kizazi chake hakikuwa na uwezo wa kuzaa maana katoa mimba sana. Ndiomana sikuona umuhimu tena wa kuendelea na Neema wakati ukweli nimeujua. Niliporudi kwa Neema nilikuwa na lengo moja tu la kumuacha kwani mawazo yangu kwa muda huo yalikuwa ni kuanzisha maisha na Rose. Ila Neema aliweza kunishawishi hadi tukashiriki nae tendo la ndoa, na baada ya hapo nikaondoka ila nikapata shinikizo la kumfukuza kwani niliambiwa Neema alikuwa na mahusiano na kijana Fulani pale mtaani, na nikambamba akiongea nae kwakweli nilikuwa na hasira sana nikamfukuza kabisa. Nikashangaa baada ya mwaka mama ananiambia eti kuna mtoto nimezaa na Neema, sikuamini. Kuna moyo mwingine ulikubali lakini niliendelea kujazwa ujinga kuwa haiwezekani lazima mimba ile ilikuwa ya mtu mwingine kwahiyo nisijihusishe na huyo mtoto. Sikutaka kujihusisha kweli, ila niliamini zaidi baada ya kuona Neema akiishi na Ashura, hapo ndio nikajua ni ndugu yake.”
“Pole sana, hizo zote ni mbinu za Rose. Neema hakuwa na undugu wowote na Ashura ila kuna mipango ilipangwa ndiomana ikawa hivyo na utaelewa tu”
“Ila wewe nae unanishangaza, mara nyingine unamuongelea Neema kamavile sio mama yako nan i mtu uliyekuwa nae labda sawa”
“Usijali kuhusu kuongea kwangu, huwa naongea ili mtu anielewe, ila huyu mlinzi amefanya kazi nzuri sana”
Salome akamuita Yule mlinzi na kuwaandalia chakula mezani. Kisha akawakaribisha mezani Patrick na mlinzi wale chakula, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mlinzi kula ndani ya ile nyumba.
 
Back
Top Bottom